ZENA (In love with my boss)
MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 01
MAWASILIANO: www.tupohapa.com
ANZA NAYO......
Niite Zena, binti wa tatu kuzaliwa kwenye familia ya watoto watano, familia ambayo ilijaaliwa watoto wakiume wawili na wa kike watatu.
Katika watoto wa kike mimi ndio nilikuwa mkubwa kuzaliwa, lakini kwa ujumla mimi ni mtoto wa tatu kwani kaka zangu walitangulia kuzaliwa kabla yangu.
Nimezaliwa mkoani Arusha mkoa ulio na kila aina ya wauni, mkoa ambao lugha zao kama ni mgeni unatoka patupu 🤣.
Nikiwa nawaongelea wauni wa Arusha naomba na mimi niwepo jamani, Kwanza kabisa nikubali kuwa nimekuwa binti mkorofi sana, mara nyingi niliigiza kama mtoto wa kiume na ata mavazi nilipendelea kuvaa mavazi ya kiume.
Mama na baba yangu, wamekuwa watu wa kunipigia sana kelele, upande wa baba yangu amenipiga sana ili niweze kubadilika lakini nimeshindwa, kama mtu anafanikiwa kuona mwili wangu vizuri lazima astuke kutokana na makovu mengi zana ambayo nilikuwa nayo mwilini.
Zena Mimi sikuwai kuingia kwenye mahusiano ata mara moja, mara nyingi nilijiona kama mwanaume ingawa nilikuwa na mwili mzuri sana wa kike ambao mtu akinuangalia lazima aniangalie kwa kurudia.
Ukirudi usoni pia ndio kabisa, me ni murembo hatari, ukija kwenye mashavu lazima ukutane na dimpoz za ommy dimpoz, walah sijisifiii mimi ni mzuri ila ndo hivyo bhana nimechagua maisha ya kiume.
Kwenye maisha yangu bangi ni kitu cha kawaida tu, shughuli ya ukishandu naiweza sana tu na nafanya kuliko kawaida, sio kwenye ukishandundu tu, mimi ata kuvamia na kuvunja naweza.
Achaneni na maelezo sasa njooni uku mkaone ni jinsi Gani tomboy mimi nimekuja kuangukia kwenye penzi zito la boss wangu.
ANZA NAYO.......
Ikiwa ni siku ya weekend yaani siku ya mapumziko kwa wale Ambao wanakazi zao za kueleweka, lakini ukija kwa upande wetu sisi watafuta hela ambao atujui nani alipoteza kwetu ni kazi juu ya kazi.
Kama kawaida, nikatoka nyumbani kwa kutoloka na kuingia zangu mtaani, safari yangu ilikuja kuishia kwenye kitengo chetu ambapo hapo mtaani kilijulikana kama DAM CHAFU ROHO MBAYA.
"ZEY niaje ??"
Alinisalimia mmoja wa wauni pale tu aliponiona, niligeuka na kumpa tano kisha nikamuuliza.
"Dawa napata au ?"
“Dawa kama kawaida zey, sema leo nina kadili Fulani hivi, kwa haraka haraka naona uwezi kufeli”
Haraka haraka nikakaa Pembeni yake, kwa wakati huo akili yangu ilikuwa inawaza mchongo wa Pesa tu na sio kitu kingine, baada ya Kukaa kwa Sauti ya upole nikamuuliza.
“Dili gani tena ilo ? Sema Liwe la Pesa usije Niletea madili ya ushubwada sitakuelewa”
Basi kijana wa watu akaanza kunipa maelezo pale, baada ya kumaliza nilijikuta nikifurahi sana, lilikuwa Dili moja kubwa sana, Dili ambalo nikiipata tu Pesa hiyo nabadilisha Maisha yangu na familia kiujumla.
******
Majila ya saa 7 usiku mimi na kikundi changu cha watu watano, tulionekana nje ya jumba moja kali sana la kifahari, Jumba ambalo ukiangalia tu nje unajua kabisa wanaoishi umu ni watu na Pesa zao.
Tukiwa tumeficha sura zetu kwa mask, tulianza kuingia mdogo mdogo, muda huo tulipulizia dawa ya usingizi kila kona, kwa upande wetu tulitumia vifaa maalumu kwaajili ya kuzuia dawa isiweze kutuzuru.
Tulifanikiwa kuingia ndani kabisa ya Nyumba na dawa ya usingizi iLifanya kazi vizuri kabisa kwani wamiliki walilala fofofo Utazani wamepoteza maisha.
Lengo letu lilikuwa ni kuingia kwenye chumba ambacho Tajiri wa nyumba hiyo alikuwa akiifadhia mali Zake, kwa kuwa tulikuwa na ramani nzima tuliweza kuingia pasi na vikwazo.
Nyieeeh kuna watu wana Mali bhana, kwanza nilikuwa najuaga watu wenye Mali uwa uwa wanapeleka Bank kumbe sio wote, Tajiri huyu alikuwa akiifadhi kwenye chumba iko maalumu ambacho bila password uwezi kuingia.
Tulienda tukiwa tumeshajiandaa, tulikuwa na mbegi mmoja mkubwa sana na tulitumia kujaza Pesa, baada ya kumaliza kwa haraka tukaanza Kutoka.
Kwa upande Wangu nilibahatika kuona cheni nzuri ya Dhahabu hivyo nilirudi na kutaka kuichukua.
“Zey tusepe wewe”
Alizungumza mmoja kati ya wezi wenzangu.
“Nakuja”
Nilijibu na kuendelea kuvuta cheni hiyo ambayo ilikuwa imebanwa na kabati.
Katika moja na mbili bhana wenzangu wakatoka nje na Mimi Mlango ukajifunga na kufungua kwake ni nje tena kwa kutumia code nika…..
ITAENDELEA…..
ZENA (in love with my boss)
MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 02
MAWASILIANO: www.tupohapa.com
SONGA NAYO…..
Nilitamani kupiga kelele ili kuwastua lakini nilishindwa kutokana na kuofia kusikika na wahusika halafu nikakamatwa, nilitulia na kujipa moyo na kuamini kuwa wenzangu watakuja kunifungulia.
Waswahili usema kuwa siku za mwizi ni 40 nafikili zangu zimefikia 40, niliona kabisa ninavyokamatwa na kuingia sehemu mbaya.
Mwisho nilipata wazo la kipuuzi sana la kujifungia kwenye moja ya makabati uku nikijiambia kuwa nitatoka asubuhi pale tu wahusika watakapokuja kuingia kwenye chumba iko.
Ila ni Kama akili yangu ilifika mwisho hivi, Yaani nawezaje kutoka na wasinione jamani, baada ya kuwaza kwa muda mrefu, nilijikuta tu ikipitiwa na usingizi, my zangu usingizi hauna bondia.
*******
Hatimaye siku Tatu zilipita nikiwa nimekwama kwenye chumba iko, niliteseka na joto, njaa na kitu cha maji, imani yangu ya kuwa kunamtu anaweza Akaja kufungua ilinisaliti bhana na kunifanya niteseke ndani ya siku tatu.
Nikiwa sina nguvu kabisa, natetemeka kwaajili ya njaa na Kiu, nilisogelea mlango na kuanza kugonga kwa nguvu sana, kwa Wakati huo nilikubali kuwa liwalo na liwe tu Ila sio kufa kizembe kwenye nyumba ambayo sitambuliki.
Baada ya muda mlango wa chumba iko uliweza kufunguliwa na uso kwa uso nikakutana na mmiliki wa nyumba hiyo, alikuwa ni mbaba wa makamo, sura yake tu iliniigopesha maana alikuwa na sura personal kabisa 😂🙌.
“Who are you ?? And how did you get in here ??”
Mbaba Huyo aliniuliza uku akizungusha Shingo yake kwa kuangalia uku na uku.
“Maji”
Nilizungumza kwa sauti ya kukata tamaaa kabisa.
Mbaba huyo Aliweza you kugundua kuwa kuna uhalifu umefanyika Alichofanya ni kupiga alam yake maalumu ambayo alifunga nyumbani kwake kwaajili ya ulinzi.
Police awakuchukua ata nusu saa Wakawa wameshafika kwenye eneo la tukio, nilibebwa Kama mualifu na kufikishwa kwenye kituo cha police, kwa wakati huo sikuwa na nguvu ata kidogo, njaa na kiu viliendelea kunitesa, nilijaribu kuomba chakula na maji lakini sikusikilizwa ata kidogo.
Niseme kuwa niliyakanyaga kwani mbaba ambaye tulimuibia ni mtu kubwa sana kwenye kitengo cha usalama hivyo nilishikiliwa vilivyo.
Mwanamke ni mwanamke bhana, Mwili Wangu ulishindwa kabisa kuvumilia njaa na Kiu ya hali ya juu ambayo nilikuwa nayo na mwisho nilijikuta nikipoteza fahamu.
Walijaribu kuniamsha lakini ilishindikana, Mapigo ya Moyo Wangu yalisikika kwa mbali sana hivyo haraka nikawaishwa hospital.
Nilipatiwa Huduma ya kwanza pale na kutundikiwa ndripu ambalo lilisaidia sana kwenye kurudisha hali yangu kwenye Usawa.
Baada ya muda nilipatiwa chakula, nyie nilikula utazani nimeambiwa sitakula tena, nilikula haraka haraka Kana kwamba nilikuwa kwenye mashindano.
Baada ya kushiba na kukaa Sawa, nilichukuliwa na kurudishwa kituoni kwaajili ya maijiano kwani hospital sikuonekana kuwa na ugonjwa wowote ule.
“Binti Pesa zimeibiwa lini na mlikuwa wangapi ??”
Aliniuliza mkuu wa Askari kitengo cha upelelezi.
“Mmmmh “
Niliguna na kubaki nikiwatolea macho uku nikijifanya kutokuelewa kile wanaachoniuliza, baada ya kuona kuwa nipo Kimya Askari huyo akaniuliza Tena.
“Ulikuwa na kina Nani ??”
“Aba, ababa, baa….”
😹Aahaha Ila Mimi jamani, niliamua kujifanya bubu tu maana kuwataja wenzangu ni mbaya kabisa, police huyo alishusha Pumzi ndefu Kisha akatoka nje na kuniacha kwenyewe.
Nilibaki nikitabasamu na kuamini kuwa nimewaweza na Hakuna ukweli wowote ule ambao wataupata kutoka kwangu.
Baada ya muda police Yule alirudi na police mwenzie ambaye pia ni bubu, walahi waliniweza, kwa upande Wangu sijui ata kuongea na bubu halafu wananiletea bubu wakiamini kuwa tunaweza kuelewana 😂🙌.
Niliamua kuwa jeuri tu, sikuzungumza kwa maneno wala kwa Vitendo nilibaki kimya tu.
*******
Siku ya kwanza ilipita nikiwa nimelala maabusu, muda wote niliwaza ni jinsi gani naweza kutoka kwenye Matatizo mazito kiasi iki, akili
Yangu ilihisi kuchanganyikiwa, Pesa ambazo waliondoka nazo wenzangu Zilikuwa ni nyingi mno na kufanya kesi yangu kuwa na uzito wa hali ya juu.
Majila ya saa 3 asubuhi nikaingizwa Tena kwenye chumba cha maojiano na safari hii alikuwepo na muhusika mkuu, Yaani mbaba Yule ambaye tumamuibia.
“Binti unijui sikujui hivyo basi usinifosi kufanya mambo ambayo sitaki kabisa kufanya kwako, wewe ni Binti mdogo sana nikikupa adhabu ata moja Nina uhakika kuwa story yako ya maisha itafutika.
“Aba, abaabaa, aaaah “
Niliendelea kuigiza Kama bubu uku nikiamini kuwa ndio njia Pekee
Ambayo itanisaidia kuwa salama, bwana bwana, kuna watu awataniwi ata kidogo, nilijikuta nikichezea Kichwa kimoja cha pua kilichosababisha nianze kutokwa na Damu puani.
“Mr Mbilinyi, aaaah uko ni kuumiza” alizungumza Askari Yule ambaye alijulikana kama Vero.
“Vero huyu sio bubu aliomba chakula nyumbani Kabla ya kufika hapa kituoni “
Alizungumza mr mbilinyi na kushika shingo yangu, woiiiiih huyu baba ni muuwaji sio bure, Yaani Alinikaba pasi na kuwa na Huruma ata kidogo, alinikaba pasi na kujali kuwa Mimi ni Mtoto wa kike.
Mkabo ulikuwa ni wa kutoana roho, nilikosa ata pumzi, nilijikuta nikianza Kurusha rusha miguu yangu uku na uku.
“ZENA utakufa kizembe “
Nafsi yangu iliamua kuzungumza nami na kwa jazba nikalopoka.
“Nasema….”
EEEH MUNGU ZENA MIMI SIJUI NINI KITANIKUTA.
ITAENDELEA…
ZENA (in love with my boss)
MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 03
MAWASILIANO: www.tupohapa.com
SONGA NAYO…..
"Nasema"
Kitendo cha mimi kuzungumza ni kama kiliniponya hivi maana mbaba yule aliniachia kwa kunisukuma kwa nguvu sana.
Zena mimi nilikihoa kama sina akili nzuri, baada ya kutulia nilirudishwa kwenye kiti na kuulizwa maswali kibabe sana.
"Unauitwa nani ??"
Nilitamani nisijibu lakini nilikumbuka kifinyo nikajikuta mwenyewe nikijibu.
"Naitwa Zena"
"Zena maandazi au vitumbua ??"
"Naitwa Zena Mariki "
"Unakaa wapi na nani na unajishughulisha na kazi gani ??"
Basi niliandikisha jina langu pale pamoja na kila kitu ambacho kinanihusu.
"Zena ulifikaje kwenye nyumba ya Mr mbilinyi"
Nilijikuta nikiwa mpole sana, nilitamani nisiseme kitu lakini nilifikilia jinsi ambavyo waliniacha mwenyewe Pasi na kuja kunifata, yaani awakunitafuta ata kidogo wameniacha niteketee mwenyewe.
"Nitasema kila kitu, nitaongea ukweli mtupu, kiukweli sisi tumepewa kazi na mdogo wako wewe, namaanisha sudy mbilinyi. Sudy ndio mtu pekee ambaye alitutajia pass code za mlango ule lakini pia na ramani nzima ya nyumba yako"
Nilitoa maelezo yote ambayo nilikuwa nikiyajua' baada ya Mahojiano kuisha nilichukuliwa moja kwa moja na kwenda kutupiwa kwenye maabusu, niliwaza na kuwazua uku nikijiuliza nini mwisho wangu je maelezo yangu yatasaidia au laaaaah.
Baada ya kama lisaa limoja kupita familia yangu iliweza kuwasili, alikuja mama, baba pamoja na kaka yangu mkubwa.
"Mama"
Nilimuita mama angu kwa sauti yenye kilio ndani yake.
Nyie mie muhuni lakini hii kesi ilinipa uwoga sana, kesi ilinipa wasiwasi wa hali ya juu, kiasi cha pesa ambacho kilikuwa kimeibiwa kilikuwa kikubwa mno siwezi ata kukitaja kwakweli.
"Koma wewe na ufunge mdomo wako kama bakuli iliyokosa mfuniko "
Imagine nimemuita mama lakini nimepokea jibu moja matata kutoka kwa baba angu, baba angu ni mtu ambaye apendi utani na wala ujinga kwenye mambo ya serious.
Baada ya kufata taratibu zote, niliweza kupata nafasi ya kuzungumza na familia yangu, kwa wakati huo sikuwa na ujanja niliamua kufunguka ukweli wote kutoka kwa familia yangu ili waweze kujua jinsi ya kunisaidia.
Kwanza kwenye maongezi tu niliweza kupokea mabao kadhaa kutoka kwa baba yangu, muda wote huo mama yangu alikuwa kimya akiniangalia kwa macho ya huruma sana.
"Baba nisaidie nitoke hapa "
Nilizungumza kwa sauti ya utaratibu sana.
"Zena kaa kimya, kaa kimya nimesema kaa kimya, yaani niambie hizo milioni 100 sijui mia 200 tunazitoa wapi ? Eeeh niambie kama umeficha mahali tuchukue tujue tunakusaidiaje "
"Baba sina ata pesa, story niliyowapatia ndio ukweli ukweli mtupu "
Baba yangu alishindwa kabisa kuniamini alibaki akiniangalia kwa macho makali sana.
*******
Baada ya miezi mitatu kupita, sudy mbilinyi aliweza kupatikana, lakini pia sio sudy tu ata wale ambao nilikuwa nao siku ya tukio waliweza kupatikana.
Nisiwe muongo jera ilijua kuninyoosha zena mimi, nilipauka mno, ngozi ilinyauka utazani ni Mboga za maboga zilizopigwa na Jua kwa muda Mrefu.
Yote kwa yote nashukuru Mungu kuwa upatikanaji wa wenzangu ulisaidia mimi kutoka gerezani na kuwa raia wa kawaida .
Naweza kusema kuwa gerezani kulijua kunibadilisha tabia, nilijikuta Nikiwa na heshima ya hali ya juu, Baadhi ya Majilani walinicheka na kunikebehi lakini Niliona kuwa Nastahili yote kutokana na maisha ambayo Niliyaishi hapo mwanzo.
*******
Ikiwa ni siku ya Jumanne, niliamka asubuhi na Mapema na kufanya shughuli za hapa na pale kwaajili
Ya kuweka mazingira ya Nyumbani vizuri .
“Aaah gerezani pamejua kukunyoosha Bwana”
Alizungumza baba yangu ambaye alinikuta sebuleni nikifuta futa vumbi.
Niliishia kumuangalia tu, nisiwe muongo, familia yangu ndio Chanzo kikuu cha Mimi kutoka gerezani, waliangaika uku na uku kuhakikisha kuwa napata kufika uraiani kwa Mara nyingine, baba yangu ananisema tu lakini Alikuwa Akikosa usingizi kabisa.
Nikiwa nimeganda namuangalia baba yangu, gafla baba akanigeukia na kuniambia.
“Achana na hizo kazi Saa hizi, shangazi yako mama manka anakuja na mnaenda wote Dar “
Nika…..
ITAENDELEA….
ZENA (in love with my boss)
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote