MTOTO WA DADA
Ni story inayokukutanisha na msichana wa makamo mwenye umri wa miaka 20, ambaye anaishi na mama yake mzazi tu kwenye nyumba ya urithi ambayo baba yake mzazi aliiacha.
Maisha ya binti huyo aliyejulikana kama Zainabu yakiwa yanaendelea kwa amani na raha zote akiwa na mama yake, gafla kisanga kinaanza pale tu mjomba wake yaani kaka wa mama yake anapotoka kijijini na kuja kuishi kwa dada yake.
Mwanaume huyo wa makamo ambaye anarafudhi ya kisukuma, anaingia jijini dar es salaam na kukataa kurudi usukumani na kuanza kufanya mambo kwa mtoto wa dada...
Je ni mambo gani ? Tukutane ndani ndani uku.
USIKUBALI KUPITWA NA MTOTO WA DADA...
MTOTO WA DADA
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 01
Ni story inayokukutanisha na msichana wa makamo mwenye umri wa miaka 20, ambaye anaishi na mama yake mzazi tu kwenye nyumba ya urithi ambayo baba yake mzazi aliiacha.
Maisha ya binti huyo aliyejulikana kama Zainabu yakiwa yanaendelea kwa amani na raha zote akiwa na mama yake, gafla kisanga kinaanza pale tu mjomba wake yaani kaka wa mama yake anapotoka kijijini na kuja kuishi kwa dada yake.
Mwanaume huyo wa makamo ambaye anarafudhi ya kisukuma, anaingia jijini dar es salaam na kukataa kurudi usukumani na kuanza kufanya mambo kwa mtoto wa dada...
Je ni mambo gani ? Tukutane ndani ndani uku.
SONGA NAYO......
My zangu my zangu, aaah walahi kuna watu wamebarikiwa jamani na nasema haya ni kwaajili ya binti zainabu, zainabu ni binti ambaye amepata bahati ya kupendwa na mama yake lakini pia na mjomba wake ambaye alizoeleka kama MASANJA.
Masanja na Kabula ni mtu na dada yake ambao wamezaliwa baba mmoja mama mmoja, baada ya kabula kuolewa uko usukumani, aliama na kuamishia maisha yake jijini dar es salaam.
Kabula na mume wake walifanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike ambaye walimpa jina la Zainabu, baada ya zainabu kuwa binti wa miaka 18 Baba yake alifariki na kumuacha zainabu akiendelea kulelewa na mama yake ambaye ni kabula.
Maisha yaliendelea uku mama na mwana wakiendelea kuishi kwa amani na furaha ya hali ya juu, maisha ya uswazi yamemfanya zainabu kuwa binti mmoja hivi mcharuko sana, yaani binti ambaye vigodoro avimpiti, masherehe aliyoalikwa lazima atokee ukiona ajatokea ujue anaumwa.
Baada ya zaibu kufikia miaka 20 mjomba wa zainabu ambaye ni masanja, alitoka usukumani na kuja mjini kwa dada yake kwa lengo la kutafuta maisha kwani maisha ya kijijini yalimshinda kutokana na upatikanaji wa pesa kuwa mgumu.
Naweza kusema kuwa masanja ni mwanaume na nusu walahi, masanja amekuwa mtu wa maana sana kwenye maisha ya Zanabu lakini pia kwenye maisha ya kabula ambaye ni dada yake.
******
Ikiwa ni siku ya weekend, Zainabu aliamka asubuhi na mapema na kuanza kufanya shughuli zake za nyumbani kama ilivyo ada. Zainabu akiwa Bize na usafi muda huo huo alikuja masanja ambaye ndio kwanza alitoka kuamka, masanja alizunguka uku na uku mwisho alisimama karibu na shimo la choo na kuzungumza.
"Mtoto wa dada kama leo ujaota unakabwa basi umeota unazikwa "
"Mjomba nawe umeanza mambo yako, hizo ndoto labda umeota mwenyewe lakini sio mimi, na kwanini niote ndoto mbaya kama hivyo"
"Sasa kama ujaota ndoto mbaya ni nini kimekufanya asubuhi hii ya saa 12 uwe hapa nje unaangaika na uwanja na si kawaida yako mtoto wa dada, mimi nimezoea uwa unaamka saa 3 uko na majukumu yako uwa unatekeleza muda huo unaoamka "
Zainabu alimuangalia mjomba wake kwa muda kisha akatabasamu na kuzungumza.
"Karibu naolewa mjomba kwahiyo nipo kwenye mazoezi ya kuwa mke bora "
"Ahhahah, mayooo atakaye kuoa wewe aandike amekula hasara yaani anaoa pambo la ndani na si mke "
"Mjomba, maneno yako hayo oooh ujue maneno yanaumba, ata hivyo umenikela sana, nilikuwa nimepanga leo nikupeleke Beach ukainjoy lakini umeshanikela "
"Weeh unasema kweli ? Yaani nilikuwa natamanigi kweli kutembelea maji ya buluu ya uku dalisilamu lakini sikuwa najua njia" alizungumza masanja uku akijichekesha.
"Ndio ushaharibu sikupeleki tena "
"Aaaah usifanye hivyo mtoto wa dada, unajua mjomba nae ni mama eti"
"Kwahiyo mjomba nikikuita mama utaitika ??"
"Kwa leo naitika kabisa kwanini nisiitike, tena wacha nikusaidie kufagia uwanja ili ufanye shughuli zingine tuwai "
"Ebu niache mie, unataka dada ako aje hapa nionekane nimekupa mikazi " alijibu zainabu uku akiendelea kufagia sehemu ndogo ya uwanja ambayo ilibakia.
Majila ya saa 8 mchana alionekana Zainabu akiwa amevaa mvazi yake ya watoto wa 2000, mavazi fulani hivi na kile kishape weeeh alijua kunoga bhana.
Muda huo masanja alikaa sebuleni akimsubili zainabu ili waweze kutoka kwani aliamini kuwa atatoka na zainabu ili kwenda beach.
"Mama jamani tafuta njia ya kumtoa kaka ako hapo sebuleni me nipite niondoke " alizungumza zainabu kwa kulalama akionesha wazi kuwa ataki kutoka na mjomba wake.
"Kwani si ni wewe ndio ulimwambia unataka kutoka nae ? Umelikologa lazima ulinywe kaka angu ameshapigilia suti zake kali kabisa.halafu unataka kumuacha " alijibu mama zainabu na kuachia kicheko cha uchokozi.
"Mama suti gani kali zile, aaah Angevaa kawaida labda ningeenda nae lakini vile suti za kijani shati jekundu kweli mama jamani, angalia na vile viatu vyake kama mzee wa zamani aliyefilisika "
"Ahahahahah muache kaka angu bhana "
Zainabu alichoka ata kusubili, muda uliendelea kwenda na mama yake alikataa kabisa kumsaidia, safari ya zainabu haikuwa ya peke yake bali ilikuwa ni yeye na rafiki zake hivyo walikuwa wakimpigia simu mfululizo kwani alikua akiwachelewesha.
Zainabu baada ya kuona kuwa anachelewa alijitokeza sebuleni, masanja baada ya kumuona mpwa wake aliinuka kwa furaha akijua kuwa safari imeshanukia.
"Mjomba yale manukato ulijipulizia kweli jamani ??" Zanabu alimuuliza mjomba wake.
"Manukato gani jamani ??"
"Nimekuwekea manukato hapo juu ya meza yako ya chumbani kajipulizie haraka tuondoke"
Masanja wa watu pasi na kujua au kuuliza mara mbilimbili, kwa furaha na shauku akaingia chumbani kwake.
Kwa upande wa zainabu alitoka nje mbio mbio na alikuta gari ya rafiki zake ikimsubili, haraka akapanda na wakaondosha gari.
Safari yao ilikuwa ya amani na furaha sana utani kama wote, si unajua tena watoto wa afu mbili wakikutana, yaani watoto wa afu mbili wakikutana tena na mabebi zao story za umo wanajua wenyewe sitaki kuwasemea mie.
Wakiwa bize wanacheza ndani ya Gari baada ya muendeshaji kuwawashia mziki walishtuka sana baada ya kusikia gari ikipigwa kwa nguvu Sana kwa upande wa nyuma.
Kwa wasiwasi na woga walipaki pembeni na kuangalia ni kitu gani kinagonga gari yao.
"Aaah kwakweli nyie amuna masikio kusikia kwa haraka, hivi mnajua nimegonga kwa muda murefu, nawaambia naanguka, nawaambia msiendeshe kwa nguvu mikono imeanza kuteleza amusikii kabisa "
yalikuwa ni malalamiko ya mjomba ambaye alikuwa amepanda nyuma ya gari ilo, yaani sio kwamba alikuwa amekaa kwenye buti hapana, mjomba masanja bhana alikuwa amesimama nyuma ya gari naweza kuchukulia mfano wa wale vijana wanaochezaga barabarani na viatu vya mataili wanavyodandiaga magari ya watu.
Zainabu alijikuta akikosa nguvu kabisa, alishusha pumzi nzito na kuuliza kwa hasira.
"Mjomba ulitaka kujiua au ??"
"Nataka kujiua wapi nawe, watu mmeniacha uko nashukuru Mungu kuruka na kukimbia najua hivyo nikawai na kudandia hapa"
"Shukuru Mungu hatujaingia kwenye barabara kubwa la sivyo tungekuwa tunazungumza habari zingine hapa " alizungumza zainabu kwa hasira kisha akawageukia rafiki zake.
"Naombeni twendeni na mjomba wangu maana mbinu za kumkimbia zimegonga mwamba" alizungumza zainabu kinyonge na kukaa kimya akisubili majibu kutoka kwa rafiki zake.
JE MJOMBA WATAENDA NAE AU NDIO WATAMUACHA ?.
MTOTO WA DADA
SEHEMU YA: 02
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
Zainabu na rafiki zake awakuwa na chaguo zaidi ya kumchukua mjomba na safari ya kwenda beach ikaendelea.
Ila watoto wa afu mbili sijui pesa uwa wanatoa wapi jamani, yaani mimi wa 199..... uko naangaika ata Mia ya Big G sina halafu kuna hawa watoto wa afu mbili wanafanya wanachokitaka haijalishi inakosti kiasi gani cha pesa.
Walifika beach cha kwanza kabisa walibadilisha mavazi yao na kuvaa swimming costume, mavazi haya wakikuvali watoto wa afu mbili lazima ugeuke uwaangalie mara mbili mbili, msimuliaji wenu niliganda nikiwashangaa mpaka nikajikuta namuangusha mmama wa watu mwenye deli la ice cream na kusababisha ice cream zote kumwagika nikapata deni la kulipa kwaajili tu ya kuwashangaa watoto wa afu mbili kwenye mavazi ya kuogelea.
"Mjomba sasa kwakuwa umekuja na suti zako kama unaenda harusini hautaweza kuingia kwenye maji kuogelea zaidi uzunguke zunguke hapa hapa usije ukaenda mbali" alizungumza zainabu ambaye alikuwa na haraka ya kuwafata rafiki zake ambao walishamuacha.
"Mtoto wa dada unaniambia kama unaongea na tutoto tudogo, ata hivyo nina ngili mimi siruhusiwi kuchezea maji ila nafurahi nimekuja kwenye maji ya buluu ya dasilamu "
Muda wote huo zainabu ameonekana kuwa na aibu sana kwani watu wamekuwa wakimuangalia sana kutokana na mavazi ya mjomba wake, ila kwakuwa mimi msimuliaji wenu ni mmbea mmbea nilihisi kuwa ankoli ni siponsa bhana.
Zainabu baada ya kuweka mambo sawa alishika njia na kuwawai rafiki zake ambao walikuwa tayali wameshaanza kuogelea.
"Baby, mjomba ako awezi kuleta jau kweli, maana naona kama anakuwinda sana naogopa ata kukukisi ujue " alizungumza boyfriend wa zainabu ambaye alijulikana kama Peter.
"Tena akikuona nahisi anaweza akakung'oa shingo walahi, kama jana tulikuwa tunaangalia movie ya kizungu, kama unavyojua wazungu mambo ya kukisi ni kawaida sana, sasa mjomba kila sehemu ya kiss alikuwa anaweka mikono yake machoni ili asiweze kuona "
"Ahhaah kweli mmoja wako wa kuja "
Story na kuogelea kuliendelea na kila mtu alionekana kufurahi sana.
Kwa upande wa mjomba alizunguka uku na uku, na kwakuwa ilikuwa ni weekend watu walikuwa wengi mno, mjomba masanja alizunguka na kuzunguka na kujikuta akisahau sehemu ambayo aliambiwa akae.
Mjomba alizunguka vya kutosha, yaani kila alipotembea aliona ni kama kunafanana, mjomba alizunguka na kuchoka mwisho alisogea kwenye mziki na kuomba kutangazwa.
"Naomba nitangaze nimepotea, namtaka mtoto wa dada " alizungumza mjomba akimwambia dee J ambaye alikuwa akiweka ngoma juu ya ngoma.
Dee j alimuangalia mjomba masanja kwa muda kisha akaanguka kicheko kutokana na muonekano wa mavazi ambayo alikuwa amevaa.
"Umesema anaitwa mtoto wa dada ??"
"Ndio ni mtoto wa dada angu, we tangaza sema mtoto wa dada, mjomba wako anakutafuta, sema mjomba wako aliyevaa suti za bei kali za kijani"
Dee j wa watu walijikuta akicheka mno maana daaah mjomba anajiachia kana kwamba yeye ndio aliwapeleka wenzie pale kumbe yeye ndio alipelekwa.
Dee J alifanya jukumu lake na hatimaye zainabu aliweza kumfikia mjomba wake.
"Yaani mjomba sijui una shida gani wewe mbona una usumbufu sana " zainabu alilalamika uku akishika mkono wa mjomba wake na kutoka nae eneo lile.
"Usumbufu gani ? Me niko natembea naona kila sehemu panafanana ulitaka niende wapi, ata hivyo wasiwasi wangu ni juu yako niliogopa kuwa utakuja kupotea "
"Kwahiyo mjomba mimi na wewe nani anapotea uku ??"
"Shika adabu yako wewe "
Ila zainabu na mjomba wake ni kama Zimwi na kibarabara, kuna namna fulani ni kama wote wamekutana wakiwa wanachekesha sana.
Zainabu alimtembeza mjomba wake kwa mwendo wa haraka sana uku akionesha kuwa na hasira ya hali ya juu, katika Vuta vuta na mwendo wa haraka ambao zainabu alikuwa akimpeleka mjomba wake gafla mjomba masanja alianguka chini kama mzigo na kubilingita kwenye michanga meupe ya beach na kumfanya kuwa kama kinyago.
"Oooh mjomba, mjomba samahani sana nisamehe mjomba angu " zainabu aliongea kwa sauti ya wasiwasi na kumsogelea mjomba wake uku akitaka kumsaidia kuinuka.
"Mtoto wa dada, na huo umbau mbau unafikili unaweza kuniokota hapa" alilalama mjomba uku akijiinua mchangani.
"We nawe mjomba utaki kusaidika kabisa, ona sasa umechafuka "
"Si ni wewe umetaka nichafuke ? Unajua hii suti nilivaa siku ya harusi ya dada angu yaani mama ako, nakumbuka nilipendeza ukumbi mzima watu walikuwa wakiniangalia mimi halafu wewe unataka kuniharibia "
"Na suti yako ya mwaka 47 π" alizungumza zainabu kwa sauti ya chini uku akiepuka mjomba wake asiweze kumsikia.
Mjomba aliinuka na kujikung'uta michanga ambayo ilimvaa na alipomaliza, kwa hasira alimsogelea zainabu, zainabu aliogopa sana akiamini kuwa mjomba wake anaenda kumpiga mbele za watu lakini haikuwa hivyo mjomba alimshika mkono zainabu kwa nguvu kabisa na kusema.
"Wacha mtu na afya zangu nikushika kimbaumbau "
Zainabu alijikuta akianza kucheka tu, waliongozana moja kwa moja mpaka kwenye meza ambayo wakina zainabu walikuwa wameshailipia.
"Mjomba utulie sasa, si tunaenda kubadili nguo ili tuje kupata chakula " alizungumza zainabu na hakutaka kusubili jibu akaondoka kubadili mavazi yake.
Baada ya muda kidogo zainabu alirudi akiwa na rafiki zake na walishabadilisha mavazi, safari hii walahi naomba kusema kuwa watoto wa afu mbili wana pepo yao, woiiiih kwa upande wa zainabu alinipigia kigauni kimoja matata sana kila nikiangalia msomaji wenu nikabaki najisemea kuwa lazima zainabu awe wangu.
Waliungana kwenye meza moja ya chakula na hapo chakula kikaletwa, si unajua yale mambo ya kisinia ? Yaani kisinia kimejaa kila aina ya zagazaga, mimi pale walahi na umbea wangu nilikuwa naona nyama tu.
Mjomba alijikuta akitoa macho kama mjusi kafili aliyebanwa na mlango, ila mjomba anauchizi wake binafsi yaani kushangaa tu akaona haitoshi akajikuta akilopoka.
"Kudaaaaa, aaah kudadeki "
Mshangao wa mjomna ilimfanya kila mtu acheke, yaani mjomba ni comedy kabisa ni vile cheka tu hawajamuona bado ila wakimuona ni moja kwa moja stejini..
"Ankol, ukisikia kisinia ndio hiki sasa " alizungumza Amina shoga uyoga wa Zainabu.
"Aaah we nawe unaniona mimi Kolo si ndio ?, hapa kuna sinia wakati ni mbao" alijibu mjomba.
Jibu la mjomba lilimchekesha kila mtu, ila kwa upande wangu naona kuwa mjomba yuko sahihi, si unajua sasa hivi wameboresha mambo, vyakula vingi wanaweka kwenye yale mambao ambayo wameyachonga kama masahani so mjomba yuko sahihi.
"Mambo ya vyukuuu mweeeh " alizungumza mjomba uku akinyoosha mkono na kutaka kuchukua paja la kuku ambalo lilikuwa karibu yake.
"Mjomba, wee mjomba ebu acha kwanza wenzio tunataka kupiga picha " zainabu alimzuia mjomba ake.
"Watoto wa dasilamu mmekosa maadili kabisa, yaani mnakuja ugenini mnatengewa chakula mnataka kupiga picha badala ya kula "
"Siku ukianza kuwa mtu wa social media ndio utaelewa mjomba "
"Mtoto wa dada uwe na heshima sasa sawa, uwe na heshima narudia ooooh mimi nakuwaje social media na mama angu amenipa jina la masanja ??"
Walahi siku hiyo mjomba alijua kuwachekesha watoto wa afu mbili na kwa namna moja au nyingine walijikuta wakiinjoy sana uwepo wa mjomba.
Hatimaye giza iliingia, kwa upande wa mjomba aliamini kuwa ni muda wa kurudi nyumbani, lakini kwa upande wa watoto wa afumbili huo muda ndio ulikuwa wa kujirusha kwani kulikuwa na upande wa disco vumbi.
Kwakuwa zainabu hakutaka kumpa wasiwasi mjomba wake alimsogelea na kuanza kumuelewesha kuwa wanacheza mziki kidogo kisha wanaondoka nyumbani.
Mjomba alikuwa muelewa sana na kwa upendo ambao alikuwa nao juu ya mpwa wake zainabu hakuona shida wakuwasubili wamalize starehe zao ndio waondoke.
Peter ambaye ni mchumba wa zainabu kwa wakati huo alikuwa ameshalewa vya kutosha, hakujali kuwa kulikuwa na mjomba wala nini alichojali yeye ni kuonesha mapenzi yake ya dhati juu ya zainabu, muda wote alimkumbatia na kumkisi vile alivyotaka.
Ukiachana na ushamba wa mjomba, mjomba masanja aliweza kuelewa kuwa Peter na zainabu ni wapenzi hivyo hakuona shida aliwaacha wainjoy tu mahusiano yao.
Miziki ya pale kwakweli haikuweza kumvutia mjomba ata kidogo na kwa sababu hiyo mjomba akawa mpenzi mtazamaji tu na mlinda viatu.
Katika moja na mbili mjomba alijikuta akishindwa kabisa kukaa chini na akaanza kuzunguka kidogo kwenye eneo ilo ilo, baada ya muda mjomba alishika njia na kwenda chooni kwani alikuwa tayali anapajua.
Katika pitapita za uku na uku, mjomba akishtuka sana pale alipomuona Peter akiwa na Amina rafiki kipenzi kabisa wa zainabu, Peter na Amina walikuwa bize wakikisiana jambo ambalo lilimshtua sana mjomba.
JE MJOMBA ATACHUKUA MAAMUZI GANI ? BAKI NA MIMI....
MTOTO WA DADA
MTUNZI: PATRICIA ANTONY
SEHEMU YA: 03
Majila ya saa 5 usiku, walikusanyana kwaajili ya kuondoka, muda wote huo mjomba alikuwa kimya sana lakini alionekana kumuangalia Peter kwa hasira mno.
Kwakuwa mjomba ndio alikuwa mkubwa hivyo alikaa mbele na dereva ambaye ni Peter, kabla ya safari kuanza mjomba alishindwa kabisa kumvumilia Peter hivyo kwa hasira akamwambia.
"Kijana njoo nje tuongee "
Kwa pamoja Peter na mjomba masanja wakashuka na kwenda kuongea pembeni kabisa kwani hakutaka watu wengine kuweza kusikia maongezi yao.
"Nambie mjomba wangu na nusu " alizungumza Peter uku akijichekesha.
"Haina haja ya kunichangamkia, Peter mimi ni mtu mzima, nayajua mapenzi, najua nini maana ya kupendana ila naomba nikuambie ukweli kuwa wewe haupendi mpwa wangu, namaanisha kuwa wewe upo kwaajili ya kumchezea binti yangu, na sitaruhusu ilo liendelee "
"Aaah mjomba unaanza kuleta jau ujue, nampenda sana zainabu wangu, kila ninapoenda nae namtambulisha kwakila mtu washkaji zangu wote wanamjua "
"Usiongee na mimi kama unaongea na tutoto twenzio kijana sawa ? Zainabu ni mpwa wangu mimi, naomba nikuambie mwanzo mwisho leo kukuona wewe na mtoto wa dada sawa ? Baki na Amina " alizungumza mjomba kwa hasira na sauti ya kusisitiza kisha akatangulia ndani ya Gari pasi na kusubili jibu.
Peter alibaki akijiuma uma tu na kujiuliza maswali kwamba mjomba amejuaje kuhusu mahusiano yake na Amina.
Safari ya kurudi nyumbani ilianza, safari hii mjomba alikuwa kimya sana tofauti na mchana ambapo mjomba alikuwa amechangamka sana.
Walifanikiwa kufika nyumbani, si unajua tena wapenzi lazima waagane, basi Peter alishuka garini kwaajili ya kumuaga mpenzi wake.
"Mjomba alikuwa anakuambia nini wakati ule ??" Zainabu alimuuliza mpenzi wake.
"Aaah mjomba kanichimba mkwala wa maana, kaniambia kuwa nisije nikaachana na wewe, yaani nisije nikazitesa hisia zako ata mara moja "
Peter aliamua tu kumdanganya zainabu wa watu, uongo ambao ulimfanya zainabu afurahi sana na kuona kuwa mjomba wake anajali sana kuhusu yeye, na ukirudi kwenye ukweli ni kweli kuwa mjomba anamjali sana mtoto wa dada.
*******
Siku iliyofuata kama kawaida, mjomba aliamka mapema kabisa na kuanza kufanya usafi wa hapa na pale, kama kufagia uwanja na kusafisha choo, lakini kusombelea maji ambayo yalikuwa yakipatikana mbali kidogo na nyumbani.
Majila ya saa 4 ndio kabinti ka afu mbili kana amka sasa, yaani ndio kanatoka kitandani, kuna watu wanajua kulala bhana na zainabu ni mmoja wapo.
"Mjomba angu mzuri mzuri pole na uchovu " alizungumza zainabu baada ya kumkuta mjomba wake sebuleni alidema dema kwaajili ya usingizi.
"Mtoto wa dada, unaamka saa hizi mwenyewe kama katoto ka malkia vile kumbe ni katoto ka....."
Kabla mjomba ajamaliza kuzungumza mama wa zainabu alitokea na kuuliza.
"Mtoto wa nani ??"
"Si mtoto wa kabula au ??"
Kwa pamoja wakacheka, mama zainabu alimsogelea binti yake na kumkumbatia kisha akamuuliza kama anajisikia poa.
"Yaani umu ndani ni kama anaishia zainabu tu, mimi pia nilienda kwenye maji ya buluu lakini sijaulizwa kama najisikia vibaya au laaah " mjomba alilalamika uku akiangalia chini kwa aibu.
"We mwenyewe tu hauna uhakika na maneno yako, kinachokuangalisha chini ni nini sasa " alizungumza mama zainabu.
"Usimfokee mjomba wangu handsome " alijibu zainabu na kumsogelea mjomba wake na kutaka kumshika mashavu kama mtoto mdogo lakini mjomba akakwepa.
"Shika adabu yako na adabu ikushike, unataka kufanya nini ?" Alifoka mjomba.
"We nawe upendeki walahi, yaani nataka kukupeti peti unaanza kunifokea "
"Dada, dada, mwambie mtoto wako me sizoeleki, mwambie kabla sijaanza kumrukisha kichura chura "
"Ili nalo kama toto, kwahiyo hapo unaona hajakusikia au ??"
Ila hii familia bhana, wanaongea wenyewe tu watatu ndani kwao lakini hadi mmbea mimi niliyekuwa nje nasikia kelele zao, yaani wanaongea kwa sauti utazani wanashindana.
"Tuacheni utani sasa, Zainabu kule kwenye hardware utakuwa unaenda na mjomba ili akajifunze funze na awe anakusaidia kazi za pale " alizungumza mama wa zainabu.
Mama zainabu ni mwanamke mpambanaji sana ambapo alikuwa akimiliki hardware moja lakini pia alikuwa akimiliki Kilinge cha genge kubwa tu pale magomeni hivyo mara nyingi alishinda sokoni na binti yake alishinda kwenye duka lao la hardware.
Kwakuwa zainabu alikuwa akiboweka sana kukaa dukani peke yake, alijikuta akifurahi sana, na ata upande wa mjomba alijikuta akifurahi kwani aliamini kuwa ataanza kuingiza pesa kwani dada yake alimwambia kuwa atakuwa anamlipa kila mwisho wa mwezi.
Majila ya saa 11 jioni, mjomba akiwa amekaa na zainabu, kila mtu alikuwa kimya lakini mjomba alionekana akiwaza mbali sana na hapo zainabu akamuuliza.
"Unawaza nini mjomba?"
Kwa mara ya kwanza mjomba hakuweza kabisa kusikia swali la Zainabu kutokana na kuzama katika dimbwi zito kabisa la mawazo, lakini zainabu hakuchoka kabisa kuuliza hivyo alivyouliza kwa mara ya pili mjomba aliweza kusikia na kujibu.
"Yaani hapa nawaza, nikianza kulipwa, mshahara wangu wa kwanza kabisa nanunua kiwanja na mimi niwe na kwangu, yaani sitaki tena maisha ya kijijini"
"Ahahaahaha, hahaha, mjomba usinichekeshe bhana, aaah kwamba mama atakuwa anakulipa milioni ngapi kila mwezi πππΏ mjomba uku sio usukumani ujue ooh au unafikili kiwanja ni mia saba "
Kitendo cha Zainabu kumcheka mjomba, mjomba aliinuka na hapo zainabu akaogopa na kuanza kukimbia mjomba pia hakuona hajizi kumkimbiza mjomba wake.
Mtu na mjomba wake walianza kukimbizana uku na uku, walikuwa na furaha isiyokifani, wakiwa wanaendelea kukimbizana, Amina ambaye ni rafiki wa zainabu aliweza kuwasili kwenye eneo ilo na kufanya mjomba na mjomba wake kuacha kukimbizana.
"Karibu Amina " zainabu alimkaribisha Amina baada ya kuacha kukimbizana na mjomba wake.
"Asante naona wenyewe mtu na mjomba wake mnainjoy "
"Eeeeeh mwaya mjomba ananichangamsha kidogo si unajua tena mjomba pia ni mama "
"Shika adabu yako, nani mama "
Mjomba alianza kupaniki baada ya kumsikia zainabu akisema kuwa mjomba ni mama, zainabu aliangua kicheko kisha yeye na shoga ake wakaingia ndani.
Zainabu na Amina wakiwa chumbani wanapiga umbea wa hapa na pale, Amina alikuwa akimuangalia zainabu kwa jicho fulani hivi, jicho ambalo mimi kama mtu mzima niliona kuwa hakuna kheri kabisa, ni kama Amina alikuwa na jambo lake.
Kwa muda huo zainabu alikuwa bize akijiachia na kujielezea juu ya upendo wake kwa Peter.
"Amina uwezi amini najua Peter si mwanaume wangu wa kwanza lakini naomba nimpe maua yake, yule mkaka ata leo akisema kuwa ananioa siwezi kukataa kuolewa ata kidogo "
"Mmmmh we nawe acha kukurupuka, mchunguze huyo Peter vizuri ndio ufanye maamuzi, kumbuka kuwa wanaume ambao wanapesa wanakuwaga na wanawake wengi sana sana na wanawapata kupitia pesa zao " alizungumza Amina uku akimng'ong'a shoga ake.
"Aaah Amina bhana, mahusiano ya sasa hivi utakiwi kuangalia mtu anafanya nini, kwa upande wangu naangalia nafasi yangu, naangalia jinsi ambavyo ananijali na kuniweka kwenye nafasi nzuri, siwezi kujua kuwa Peter kichwani kwake anawaza nini ila kwa upande wangu niseme nampenda sana na ninamuombea kila siku, naombea mahusiano yetu ili yaweze kuwa na matokeo mazuri"
Maongezi kati ya Amina na zainabu yalinoga sana, lakini kwa upande wa pili, mjomba masanja alikuwa amesimama kwenye dilisha la Zainabu akisikiliza maongezi yale.
Ila mjomba ni mmbea sana jamani, yaani amekaa bize kabisa anasikiliza maongezi ya mabinti wadogo kabisa, mabinti wa afu mbili kweli.
Mjomba akiwa bize na kuchungulia, sijui mama zainabu alitokea pande gani, alimsogelea kaka yake polepole na kwenda kumvuta shati pale dirishani.
"Hii tabia ujaacha tu ?" Mama zainabu alimuuliza kaka yake baada ya kumsogeza pembeni kidogo na eneo la dirishani.
"Tabia gani nawe ? We unajua nilikuwa nafanya nini pale" mjomba alianza kujitetea.
"Unachungulia nini chumbani kwa mtoto wangu, masanja mbona ubadiliki wewe, nakumbuka baba alishawai kukuchoma mikono kwaajili ya hii tabia yako ya kuchungulia madirishani "
Kwa namna moja au nyingine masanja alishindwa kabisa kujitetea mbele ya dada yake akajikuta akifokewa kama mtoto mdogo na akalazimika kukaa kimya tu maana asingeeleweka kabisa.
Majila ya saa 1 usiku Amina aliaga na zainabu hakuwa na hiyana alichofanya ni kumsindikiza shoga yake kidogo tu kwani hakuwa akikaa mbali.
Baada ya zainabu kuagana shoga yake alishika njia na kurudi nyumbani kwao, Amina akiwa bize njiani anaongea na simu uku akielekea nyumbani kwao, alishtuka sana baada ya kusikia akiitiliwa na mtu na sauti haikuwa ngeni kabisa kwani ilikuwa ni ya masanja.
"Eeeeh mjomba mbona uku gafla na nilikuacha nyumbani ?" Amina alimuuliza masanja baada ya kusimama.
"Nina mazungumzo kidogo na wewe ndio maana nimekuja uku "
"Mazungumzo gani tena mjomba, na kama ulikuwa na mazungumzo na mimi si ungeniambia tangu nipo nyumbani jamani "
"Ni mazungumzo ambayo sikutaka watu wengine Wasikie ndio maana "
"Haya nakusikiliza"
"Najua kama wewe na Mtoto wa dada ni marafiki wakubwa sana, najua kuwa urafiki wenu umeanza tangu mkiwa watoto, lakini naona kabisa urafiki wenu unaenda kufa kwa jambo dogo sana "
"Mmmh mjomba bhana, urafiki kati yangu na Zainabu ni wa kudumu, nampenda zainabu na zainabu ananipenda mimi "
"Unampenda zainabu si ndio ? Na unajua kuwa ana mahusiano na Peter??"
"Najua ndio mjomba, na nawaombea wafike mbali "
"Kama ni kweli hayo usemayo basi acha kumzunguka mtoto wa dada, najua zainabu ajui kama wewe una mahusiano na Peter ila mimi najua kama wewe una mahusiano na Peter "
Maneno ya mjomba yalimshtua sana Zainabu ambaye alibaki akitoa macho na kuangalia uku na uku, kilipita kimya kifupi kisha zainabu akazungumza.
"Hakuna kitu kinaendelea kati yangu na Peter mjomba tuheshimiane "
"Nakuheshimu sana na ndio maana sikutaka kukuanika mbele ya mtoto wa dada, nataka ujue kuwa unachofanya ni ukosefu, ninyi ni mabinti wadogo sana na huo unaoufanya wewe ni uchafu tu "
"Uchafu labda uko kijijini kwenu, halafu sikia, kaa mbali na mimi mjomba sawa, punguza mazoea broh" alijibu zainabu kwa dharau sana na kuondoka.
Mjomba alishusha pumzi ndefu kisha akashika njia kurudi nyumbani.
"Mjomba ulikuwa wapi tena, mama amekutafuta mno" alizungumza zainabu ambaye alisimama kwenye kizingiti cha mlango "
"Nilikuwa nanyoosha miguu kwani ni dhambi ??" Aliuliza mjomba uku akionekana kutokuwa sawa kabisa.
"Mmmh haya, nilikuwa nakutafuta kwani chakula kiko tayali "
Kwa pamoja familia hiyo ya watu watatu, iliungana mezani na kuanza kupata chakula, walahi hii familia inastahili kila lililojema, kwani wanapendana na kujaliana kuliko kitu chochote.
******
Siku iliyofuata asubuhi na mapemaa, mjomba na mpwa wake walijiandaa na kuingia kariakoo, sehemu ambayo mama zainabu alikuwa amefungu hardware yake.
"Karibu sana mjomba " alizungumza zainabu akimkaribisha mjomba wake ambaye ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika kwenye ofisi hiyo.
"We nawe uache kunikaribisha hovyo hovyo, unataka kila mtu ajue kuwa mimi ni mgeni au ??"
"Basi nawe"
Siku hiyo zainabu aliinjoy sana akiwa pale ofisini, siku hiyo watu walikuwa wakicheka sana kwani mjomba alikuwa nje akipiga debe kwaajili ya biashara hiyo, ila upigaji wake debe ndio uliwafurahisha watu.
****
Zilipita siku tatu uku mjomba akiwa ameshazoea kazi yake, na kwa namna moja au nyingine uwepo wa mjomba na uchangamfu wake uliwaongezea sana wateja walahi.
Majila ya saa 3 usiku, familia nzima ikiwa imemaliza kula, mama wa zainabu alitoa box la simu na kumkabizi kaka yake na kumwambia.
"Hii ni zawadi yangu ya kwanza kwako kutokana na uchapakazi wako"
Mjomba masanja aka....
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote