UNEXPECTED PREGNANCY WITH BILLIONAIRE
(Ujauzito Wangu Na Billionaire)
Husqer Baltazar
EP 1.
Beathaaa wee bea, ujue teacher wa history anatuita, atupe hints za mtihani huenda zikatoka hizo twende...
Akhaaa Sara my dear we nenda tu, ata sitaisoma kabisa, wazazi wangu hawawezi lipa fees, nije kusengenya watu waliokufa, kwenye madafutal na mitihani, siwezi Somo linasemgenya wafu, na UONGO mwingi, kututafutie kesi na Mungu tu, huo uogo, umesababisha mpaka saivi, tunaishi Kwa kufa, kisa Eva kudanganywa, Sasa na Mimi niludie ujinga ule ule wa Eva, ety sisi tulikuwa nyani!!, my dear siwezi kubali kuchomwa moto mbinguni, kisa UONGO wa history, nahisi kabisa ni shetani aliejigeuza kuwa somo, ilimladi tu na sisi tupate dhambi kama yeye, thubutu siwezi soma history abadani asrani niache nisome mtihani wa kesho kutwa mie...
Bea ujue acha masharaha, hii ni nector, inakubidi upate alama ata kidogo, utafeli form 4 ujue dear..
Sara we nenda, Mimi history itanipotezea muda tu, nitajaza ninachokijua Mimi, niache basi jamani mbona kama, nawewe umetumwa na shetani jamani khaaa..
Heee yamekuwa hayo, mama acha Mimi shetani niende, afadhali tu umeondoka dah...
Mwenzenu kidato Cha nne tu lakini history imenishinda, siipendi kutoka moyoni na kesho ni naanza nector mtoto wa mama bea sijui itakuwaje ...
Nilikuwa Sehemu tulivu Kwa nje karibu na fens ya shule, wakati najibuzana na Sara, kumbe nyuma yangu alikuwepo mkaka mkubwa kamaliza chuo, shule yetu ilikuwa pia na chuo Cha biashara , na huyu sikuwa namtambua, kutokana na wingi wa watu shuleni, huwezi watambua wote, hasa Kwa sisi oleve ni ngumu kuwajua wanachuo, alikuja karibu yangu, nakunisemesha Kwa nini sitaki kusoma history , sikumjibu niliona ananisumbua tu, alionekama kama anawashaa na nikama hakuwa sawa, aliniomba nimsaidie maji ya kunywa, nilikuwa nayo kwenye chupa Kwa Hali alivyokuwa nayo ilibidi nimpe, alikuwa ananukia kitajili sio pw...
Nilimpa ata kushika ikawa tabu ikabidi nimnyweshe, wakati namnywesha alinisogelea karibu sana, ghafra akaanza kunikiss mdomoni ,nikama mtu aliyelukwa na akili ghafra,nilishtuka nikawa namsukuma lakini haikusaidia kitu,alikuwa na nguvu sana, alinivua nguo nakufanya uchafu wake 😭, huku amenibana sauti ni sitoe, nilipambana lakini sikufanikiwa mpaka akamaliza, nilikuwa nimeshazimia, nilishtuka nikiwa ndani ya gari, nikamuona doctor ananihudumia wakike na huyo kaka alienifanyia ubakaji akiwepo..
Niliamka nikiwa na maumivu makali, kwani hii ndio ilikuwa mala yangu ya kwanza, na nimefanyiwa bila kupenda,nilikuwa na hasira nikiwaza kesho Nina mtihani tena nector 😭, yule kaka aliniomba msamaa mno, lakini sikutaka ata kumsikiliza,
Nilichomwa sindano ya maumivu akajitambulisha Kua anaitwa Briton, Mimi sikutaka hata kujitambulisha japo aliniuliza alichofanya aliangalia jina langu kwenye madaftari nakuniambia, beatha Mimi naondoka Leo ila Kwa lolote nipigie simu no zangu nimekuandikia kwenye daftari,Niko tayari kulipia Kwa hili, niliwekewa dawa ndio maana imetokea, naomba unielewe najua kesho ni mtihani wako, naomba usiwaze juu ya hili, nitaliweka sawa Kila kitu, hakuna kitakachohalibika niamini..
Ivi we kaka, unaekewa kweli ulichonifanyia, ama unaongea tu kwasababu sio wewe? ..
Nakuelewa b plz nisamee, sio kusudio langu, naomba unielewe uingie ikajisomee plz, na doctor atakuja asubuhi kukuchoma sindano Ili usipate maumivu ufanye mtihani wako vzr, na nitakutafuta mwalm, awe anakuangalia na kukuelekeza Kwa kipindi hiki Cha mitihani, baada ya mitihani nitakuja tuweke sawa hili lililotokea, na Kila kitu nitalipia nakuahidi..
Sikumjibu kitu nilikuwa nahasira na majuto, bola ningeondoka na Sara, nitamwambia nini Mimi mama bea akija kujua 😭, Briton alinipa pesa, nilizikataa akaziweka kwenye beg langu, Kisha akawasha gari kunisogeza karibu na bweni langu, Ili nisipate tabu na aangalie usalama, niliachwa karibu kabisa na bweni Kisha wanaondoka na doctor.
Itaendelea..
UNEXPECTED PREGNANCY WITH BILLIONEA
Husqer Baltazar
EP 2 .
Niliingia bwenini na kulala, ilikuwa saa kumi na mbili, watu wameenda kula, waingie prepo, niliwaza sana kilichonitokea niliogopa hata kusimulia mtu yeyote, nilifanya mitihani yangu yote, nikamaliza lakini Kwa shida sana na mawazo, sikufanya graduation kutokana na mawazo nilivyokuwa nayo, nilimwambia mama sitofanya, hivyo wasijuandae alinielewa, walinitumia nauli, nilikuwa pia na pesa za Briton, zilikuwa nyingi na Toka anipe, Leo ndio nikazihesabu zilikuwa ml 2 , mmh huyu mtu pesa zote hizi inamaana alinichukulia Mimi kama kahaba wake eee😭, nililia Kwa sababu aliahidi atakuja nikimaliza mitihani, lakini sijamuona naleo ni siku ya tatu Toka mitihani iishe watu wanajiandaa na graduation yeye hajatokea, niliamua kupiga simu, lakini hakupatikana siku mbili mfululizo, nilikata shauli na kuondoka kwenda kwetu, nilipanda gari kutoka dar kwenda mwanza, niliondoka na gari za jioni Ili nifike asubuhi..
Ilipita miezi minne mitatu, Toka nimalize shule,nilianza kuhisi mabadiliko sana mwilini, mama aligundua hili, aliamua kunipima 😭 nilikuwa na mimba ,kibaya zaidi hata matokeo yangu hayakuwa mazuli nilipata 4 , wazazi walichukia Kwa hasira walinifukuza nyumbani, niende Kwa mwenye mimba..
Kwetu tuko wawili tu Mimi na kaka angu Joshua, anaeishi Moshi, amekwisha ajiliwa ni doctor,nililia nakuomba msamaa, nikaomba niwaelezee lakini hakuna alitaka kusikia maelezo yangu hata mmoja, nilitoka na zile pesa alizonipa Briton ,nilimpigia tena simu bado jibu ni lile lile haipatikani..
Niliamua kumpigia kaka nae aliniwakia mno, nakunishauli niende Kwa bibi, niliona ni bola nikaitafute maisha kuliko kwenda kumsumbua bibi yangu na umri wake, niliipigia mahesabu pesa nilivyokuwa nayo, nikaona inanitosha kuanza maisha..
Nilipanda gari kwenda arusha...
**BAADA YA MIAKA SITA.**
"Watu watakuheshimu zaidi endapo utathiubitishia ulimwengukuwa upo kwenye mahusiano,
Mtangaze mpenzi wako siku ya kesho..
"Niamini Mimi hata maadui zako watakuheshimu" secretary Jo alizingumza Kwa ushawishi...
"Sivutiwi na mahusiano Kwa Sasa, Nina mtu ninaemtafuta ingawa Sasa ni miaka 6 Sasa imepita " Briton (CEO wa kampuni ya *Gold clothing and a jewelrs* inayojihusisha na utengenezani wa nguo za madini na dhahabu pamoja na vito vya madini)alizungumza...
"Nia miaka 6 Sasa imepita hajakutafuta, na umemtafuta hujampata, ni vyema umove on, Kuna uvumi umezagaaa kuwa huenda wewe ni shoga au rungu lako halisimami" secretary Jo akiongea Kwa sauti ya chini..
" Ni wazi kabisa Hawa wao hawana uhakika na mashaka Yao, wachukulie hatua wote unaowasikia wakiniita Mimi shoga,kama utawakalia kimya, basi watahisi wewe ndio mwanamke wangu" Briton aliongea..
Ukweli ni kwamba secretary Jo ana chukizwa na namna boss wake ansvyokaaa peke yake Kwa muda mrefu bila mahusiano , na hii ndio sababu ameongeza maneno yauongo kuhusu uvumi Ili kumshawishi boss wake lakini pia ni rafiki yake watoka kitambo...
Shughuli za hapa na pale ziliendelea katika kampuni ya Gold clothing & jewelrs , Briton alipita huku na Kule, kukagua namna wafanyakazi wake wanavyotenda kazi...
Wakati Yuko bize kukagua,simu yake iliita na hakuwa mwingine, Bali ni baba yake mzazi Mzee Easton, ndio Mzee shikamoo..
Mzee Easton; marhaba swala lako limefikia wapi? Mrithi unapaswa kuwa na mke ndani ya wiki hii unapaswa Kuoa, vinginevyo kampuni yangu na Yako, itaenda mikononi mwa mdogo wako wa kambo, na hilo usijekunilaumu kuwa sikukupa kipaumbele, juhudi zako zitaenda bule, kama hautokuwa na cheti Cha ndoa, hatutapata kibali Cha kufungua mgodi, Ili tupewe idhini lazima CEO awe ameoa, na tuna siku 7 tu kama huwezi kuchagua mama ako amekutafutia Kwa wakati huu nafkiri unapaswa kukubali..
Briton; Mzee huyo sio mama angu, ni mke wako na hizo siku ulizonipa zinatosha, nitafanyia kazi sitakuangusha..
Mzee Easton; ok sawa Mimi nimeshakualifu kazi kwako bwana, Kisha akakata simu Kwa hasira , pembeni yake alikuwepo bi wema mkewe, " mme Briton kamkubali? , huyu mtoto jeuri sana amekataa na barua Imetupa siku 7 tu, biwema akajibu," usijali mme wangu, sam na Briton wote ni wanao sam amekwishaoa, hivyo kama Briton atashindwa, tunae Sam nae ni mwanao mme wangu, bi wema aliongea kama kulalamika ,na kumpigia debe mwanae wakumzaa ashike nafasi ya CEO...
Briton alikuwa na mawazo sana, alimpigia rafiki yake mwingine, anaeishi Arusha nae ni mmmiliki wa hospital ya *Sunsweet* anaitwa stv..
Aisee stv nahitaji msaada wako mwanangu,
Stv; upi?
Briton; Kuna proposal niliomba, imeshakaguliwa na Kila kitu Kiko sawa, ila shart Natakiwa niwe na mke wa ndoa, na nimepewa siku Saba tu Toka Leo, nisipokizi vigezo Mzee stampa dogo kampuni zote, yangu na yake Kwa sababu tuliziunganisha, na hawezi kubali kupoteza hili Dili, na beatha mpaka dk hii sijui Yuko wapi, na siwezi Kuoa mtu tofauti na beatha, ni wewe pekee unatambua nini kilitokea, bro kichwa kinaniuma sana..
Stv; dah hapo mtihani mwanangu, nashauli tutafute mwanamke wa kumlipa Kwa mkataba, Dili likitiki unavunja mkataba nae, angalau ndoa ya mwaka mmoja tu, hata msijuane awe wa mbali na dar, serikali wao watataka tu cheti Cha ndoa, wakati huo ukimtafuta taratibu beatha..
Briton; aiseee umenipawazi zuli sana Sasa naomba unisaidie Kwa huko huko, Mimi kesho nakuja tusaidiane bro..
Stv; usijal karibu sana bro .. " shukrani kesho saa 3 nitakuwa Arusha"
Itaendelea..🔥
UNEXPECTED PREGNANCY WITH BILLIONEA
Husqer Baltazar
EP 3.
Upande ya beatha, alikuwa na rafiki yake Sara, Kwa Sasa Sara ni mwalimu , na beatha ni fundi cherehani hakufanikiwa kuendelea, hivyo, aliamua kuendeleza kipaji chake na rafiki yake alimshika mkono Kwa Kila hata, Leo beatha alikuwa kazini akishona, Sara akampigia simu, " Bea mtoto Hali yake sio nzuli tuko njiani nampeleka hosptal, njoo sunsweet hosptal..
Nilikulupuka na hizo hizo, mwenzenu tumbo la uzazi lilicheza, mwanangu nilimzaa na sikoseli, ni Kila wakati anapata shida ya damu sijui karithi wapi jamani dah😭, niliwakuta wameshaanza matibabu..
Nikiwa kwenye Benchi nasubili kutoa damu pia, alipita doctor. nikahisi kama namjua, na ndie alikuwa anamhudumia mwanangu thomas, nilijua atakuwa kanisahau hata sikutaka kuumiza akili yangu..
Ilifika muda wangu nikaingia, alivyoniona alishituka akatizama jina beathaa!, "huyu mtoto ni wako? Nilijibu ndio " ni mtoto wako na braiton naona kafanana na braiton na Kwa hii age nafikili sijakosea ee?..
Doctor naomba usianze kunitia hasira Sasa hivi kama unamtibu mtoto wangu mtibu sitaki makumbusho ya kale na vitu vya ajabu, "beatha mtoto atakuwa sawa anasikoceli kama baba ake akifikisha miaka 18 itaisha", kumbe ndo mana ata akili yake fantu kaja kumrithisha mwanangu matatizo yake Yani huyu paka la bluee wako aiseeeee..
"Beatha mbona ni kama bado unamchukia jamaa? Unajua anavyohangaika kukutafuta, hajaoa mpaka dk hii anakutafuta alikuwa no mbona hukumpigia? ..
Ivi unaelewa unachokiongea wewe, unajua nimepitia mangapi Kwa ujinga wa uyo ndugu Yako? Nimefukuzwa kwetu Kwa sababu yake, nimepiga simu kama naalika msiba Kila siku haipatikani, akaona anipe namba ya gari, kama kakosa kizazi ndo akakumbuka Kuna beatha, mnikome tena ningejua nitakutana na wewe, ningempekeka mwanangu ata aghakhan, nachukia huyo ndugu Yako kaharibu maisha yangu afu uko hapa kuigiza ng'o ng'o ng'o ng'o ng'oooooo, usinihalibie mwaka saivi nakustahi kwasababu mtoto wangu Yuko kwako, siku nyingine usiludie kuniambia habari za huyo mtu hata Kwa bahati mbaya usirogwe..
Nikiongea nikiwa nimefura nakutoka nje, stv alishindwa kuvumilia akampigia picha thom nakumtumia braiton Kisha akampigia..
Braiton; nambie bro umeshapata mtu tayari?,
Stv; bro angalia whatsup Yako now nimekutumia picha huwezi amini hapa nimekutana na beatha Sasa hivi Yuko hapa hospital bro..
Briton; stv naomba usinidanganye bro, kwenye hili plz, picha badae naomba niongee nae plz, " ungetizama picha Briton unamtoto amekufanana Kila kitu bro Yani ni wewe mtupu na anasikoceli kama ilivyokuwa kwako..
Briton aliingia kucheki picha, hakuamini alitamani kupaaa afike muda huo huo, bro ni mwanangu plz nipe niongee nao, na niangalizie mwanangu na mke wangu, nakuja Sasa hivi siwezi tena kusubili kesho siwezi..
" Bado Kuna utata bro, beatha anahasira na wewe, anadai hukuwahi kupatikana ulimdanganya, kafukuzwa kwao, kateseka in short jiandae kisaikorojia, kuja kumuelewesha, hasira yake Iko juu mno..
Bro usijali nitahakikisha nafanikiwa, huenda alinitafuta kipindi sijaludi nchini, na sikumuaga, hakikisha hakupotei Niko njiani naelekea uwanja wa ndege, siwezi tena kusubili na Gali itanicherewesha kufika..
" Ok bro karibu,
Huku nje nilimpa Sara ukweli, kuwa nimekutana na yule doctor anaejuana na baba thom," heee bea! Itakuwaje akija na kutaka kuwachukua?" Hivi Sara unaongea pumba Gani izo ivi siku zote hizo alikuwa wapi ety Leo ndo ajitokeze, Yani uyu ni shetani, aliekimbia majukumu yake motoni, Sasa anataka kuniletea ushetani wake Mimi tena Kwa njia yake hio hio ya UONGO ...
Itaendelea..🔥
UNEXPECTED PREGNANCY WITH BILLIONEA
Husqer Baltazar
EP 4.
Sara; ila Mimi nashauli unisikilize, huenda kulitokea tatizo, ujue kuwa single mother sio kitu rahisi dear, mtoto anawahitaji nyote niwazo tu usije kunikasilikia bule manake wewe na kisrani ni mapacha,tena wamfuko mmoja...
Nakuelewa, lakini siwezi Kwa alichonifanyia sitamani hataa kuniona sura yake tena, lakini unajua anaweza akataka kuchukua mtoto na anavyoonekana pesa kwake sio tatizo Sara naomba tutoloke na mtoto nimeanza kuogopa dear..
" Mmh kumbuka bado mtoto Hali yake sio nzuli, tusubili akiamka akawa sawa," huyu mtu inaonekana wanajuana sana anaweza mpigia simu akaja wakataka kunichukulia mtoto wangu Sara napata mashaka mno..
" Sizani kama atafanyia hivyo lakini tafadhali ni bola, na uzuli wamefunga shule, itabidi tuondoke Kwa muda kwanza, tufatilie kimya kimya lengo lake ni nini kwako, sawa dear ..
Niliitea ofcn Kwa doctor, niliingia nikapewa kalatasi za kusaini..
Stv; shem Saini apo Ili wasijekuwaomba tena kutoa damu na mmeshatoa, naweza nikawa sipo, doctor tujeshimiane Mimi sio shem wako, nilisaini huku namjibu, kingine kama huyo ndugu Yako, mpaka Leo hii Yuko single Mimi siwezi kumtaka, haiwezekani wengine wote hawajamtaka Mimi sio fara Kuna shida mahali Kwa huyo nduguyo, Kwa nini wengine hawamtaki? Mimi ndio niingize matatizo moyoni mwangu, apa tu aliyonipa yashahalibu mfumo mzima wa maisha yangu, mpaka mwili wangu, afu bado nineng'eneke tena Kwa huyo huyo, shetani alokimbia majukumu yake motoni siweziiii...
" Ha ha ha ha shem unafurahisha, sio kwamba hawamtaki,ila yeye hawataki, Kwa sababu tayali anawewe ndani yake" paka wa blue wewe shukuru, unamtibu mwanangu najizuia tu ila tunakoelekea, nitakushuahia maneno magumu unichukie mpaka kiama, nimesha Saini makalatasi Yako, naweza kwenda?..
"Ndio shem na dogo ameshaamka, mnaweza kwenda kumuona, lakini Leo sitawaruhu itabidi mlale hapa" wewe usinitibue zaidi dripu ya damu imeshaisha hapa tunalala kutafuta nini kama sio kumbipu Israel aanze kutufikiria na hatuna mpango wakwenda mbinguni saiv, aisee naomba uturihusu, Mimi na Israel mtoa roho, tunaugomvi Toka niingie reba, akiona sura yangu tena hapa usiku, atahisi nimechoka kuishi, na usijisahau ninamtoto ananitegemea..
Hapa kwenyewe nimejikaza, Kila nikigeuka nahisi kama Israel ananizoom, bado na hizo harufu za madawa na magonjwa yaliyopi hapa mchanganyiko, aiseee siwezi kusubili kukuche, ukizingua najiluhusu ata Kwa vita nitatoka, Sasa utachagua amani ama vita..
" Shem nimepata dah Kwa heshima Yako, nitakulihusu ila Kwa shart la kwenda na doctor, ambae nitakupa atakuwa anamfanyia checkup, Kila ijumaa, ni damu yetu hivyo siwezi kumwacha mpaka azidiwe ndo umlete na atakuwa anatumia dawa na Kuna matunda na vyakula, nakuandikia utakuwa ukimpatia, hivyo hio itamsaidia sana kutokumsogekea Israel mala Kwa mala, kama utazingatia nitakachokuekekeza na vyakula matunda na dawa, hutakanyaga tena hosptal muda sana, chukua na no yangu Kwa lolote hata kama ni usiku wa manane piga nitafika mala moja"...
Sawa ila no sikupi najua utagawa na hizo zilizopo hapo usifikili ni zangu, vingine vyote nipe maelekezo tu nitafanya ila no big nooooo..
" Ha ha ha ha shem bwana sawa nenda kamcheki mtoto, nakuandalia dawa na maelekezo"
Nilitoka nikamwambia Sara, twende mwanao kashaamka tukamuone wanatuandalia kibali tuludi home,tukiingia nakumkutwa mwanangu, anaendelea vizuli japo mwili kaukau, hata nimlishe vipi hanenepi, ashukuru alichukua uzuli wa baba yake, angechukua macho yangu haya makubwa Kaa bundi sijui ingekuwaje, anasura ya kike ila sio yangu, rangi pia baba ake ni mweupe, mimi ni chocolate glas, mtelezo langi yangu huwezi pata hata kipele mwilini mwangu, ni kiooo mwili mzima..
Macho ya Thom wangu madogo kama mbegu za bamia, nywere nzuri na nyusi nyingii, mdomo pink, in short tu katoto kangu kazuri bana😀, japo baba ake sikumuona vzr, ila nakumbuka hasa harufu yake na macho..
Tulipiga story tukisubili ruhusa lakini wapi, naona wengine wanapewa ruhusa sisi tupo tu mmmh nikaona apa asinitanie, nikatimba ofcn, nimefika nakuta anaongea na simu, kuniona akakata, " shem karibu" ivi unanitafuta ugomvi ama nini? Saa ngap saivi wengine unawaruhusu ni sisi tu tumebaki, " hapana sio hivyo nilikuwa naandaa dawa na maelekezo Kaa nikupatie" nilikaa akaanza kunielekeza Sasa nikaona analidia ludia maelekezo, doctor nimeshaelewa nipe niende, " aah shem subili niwapeke" nilikataa nikamwambia anipe tu no ya huyo doctor, nitamuelejeza mwenyewe ikifika hio ijumaa..
Alionekana kuchoka na Mimi nilikuwa nimekunja sura Ili asiniletee utani, nilishaona Kuna jambo ananizungushia, niliondoka haraka, nikawambia tuondoke nahisi Kuna kitu kinakuja..
Tuliita uba, tukaondoka kumbe doctor alichukua gari yake akatufatilia, mpaka nyumbani, tumefika nyumbani kaka angu Joshua, akapiga cm, beatha uko wapi? Niko hapa Arusha Nina gari private bibi Hali yake ni mbaya sana, anakuhitaji wewe na mtoto, na wazee nimeshaongea nao, nakupitia saivi tuondoke nielekeze bibi anakulilia Kila siku huko dogo..
Kaka ujue hapa nimetoka hosptal, thom Hali yake sio hata ndani hatujaingia, ndo tumeshuka kwenye uba, dah, nilimuelekeza kaka ninapoishi alielwewa kwani ilikuwa ni barabarani nilimweleza rafiki yangu alielewa, akaniambia nijiandae yeye atupangie nguo, kweli tulijiandaa haraka haraka...
Kaka Joshua alifika akatuchukua, tukaondoka, usiku huo huo, upande wa stv, Briton alifika, bro mke wangu Yuko wapi?,
Relax briton, nimeshindwa kumzuia hazuiliki angeleta vangi hapa na unatambua sio vyema kuwapigia kelele wagonjwa, hakuwa tayari kunielewa, lakini nimemfatilia mpaka anapoishi hivyo tunaweza kwenda asubuni..
Bro hauko serious kabisa Yani nilale bila kuwaona tena, na wako hapa hapa hapana, naomba tu unifanyie hisani Sasa hivi twende, siwezi hata kupumzika bro..
" Ok twende, naona wote mna maamuzi yasiyopigwa, sijui itakuwaje mkijakupishana maamuzi,waliondoka na kuja mpaka geto, waligonga, Sara alisikia lakini Kwa sababu ilikuwa bado mapema, hakutia shaka akahisi huenda ni sisi, Kuna kitu tumesahau, alienda kufungua mlango na kushangaa, baada ya Kumuona mtu waliyepotezana Kwa muda mrefu sana, alikuwa kama akimfananisha kwani walitengana akiwa darasa la nne, hivyo hakuna na uhakika kama ndie ama sie..
Itaendelea..🔥
UNEXPECTED PREGNANCY WITH BILLIONEA
Husqer Baltazar
EP 5.
Ka stv!!!, saraaaani wewe , stv alimkumbatia mdogo wake Sara huku machozi yakiwatoka kama mvua, Sara na stv wameshea baba mama tofauti, mama Sara alishindwa uke wenza, akamwachia bimkubwa hakutaka wawasiliane Wala kujuana, kwani hawakuachana vizuli,Sara mdogo wangu za miaka na hapa vipi..
Ka stv, ndo naishi hapa, wewe kulikoni hapa nani amekuelekeza? Briton alitamani hata ammeze alijua kakosea tayari, na vijicho vyake Kaa mbegu za bamia vilianza kutia machozi, KARIBUNI mbona mwenzio kama hayuko sawa kaka Kuna tatizo KARIBUNI ndani..
Briton alijikaza na kuongea " kwahiyo umenileta Kwa mdogo wako ama mbona sikuelewi bro" huku machozi yameshindwa kuhimili vijicho vyake yakatoka kama mvua,sio hivyo bro ni hapa nilimuona akija mpaka hapa..
Kaka stv Kuna tatizo?, Nani mlimuona? , "Sara naomba msaada wako huenda ukawa unajua kitu Kuna dada mmoja anaitwa beatha na anakitoto Cha miaka 6 kinaitwa Thomas unaweza kujisaidia kujua wanapoishi kama unawafahamu,Sara alishituka aakamuuliza kaka ake kwanini unawatafuta, muda huo Sasa akamcheki Briton vizuli picha ya thom ikajionesha, akajua huyu ni baba thom, stv na Briton wote wakauliza Kwa pamoja unawajua? Plz tusaidie, Briton mpaka akapiga magoti na machozi..
Sara ni mtu mwenye huruma sana alimchunguza Kwa muda mfupi Briton skagundua Hana madhara kwangu, hakuwa na budi kunichoma rafiki yake, na kuwaeleza ukweli wote mpaka maisha yangu, Ili jinga liliongea, bila kubakisha chochote kisa huruma...
Briton alichoka nilipitia mengi sana, alimshukuru Sara nakuomba asimjulishe chochote, mpaka anipate Ili nisijetoloka, aliamua kuondoka huo huo usiku anifate mwanza, lakini Sara na stv walimzuia Kwa Hali aliyokuwanayo, haitakuwa sawa kwake kusafili usiku akiwa na Hali hio, na ni usiku ni vyema aondoke asubuhi Kwa ndege, na stv alimuahidi kumsindikiza na kumsaidia..
Stv hujui tu familia yangu Iko barabarani bro mtoto mwenyewe ndo katika hosptal hawajapumzika, na huko wanakoitwa hatujui kama ni sarama bro, hata huo usingizi nautoa wapi, nguvu za kupumzika sijamuona beatha nazitoa wapi, anateseka peke yake, na Mimi nipo bro naumia😭..
Sara aligundua, Briton ananipenda na Hana shida, hii chuki yangu ndo shetani mwenyewe na sio Briton, alijiapiza ndani yake kumsaidia Briton kuwa na Mimi..
Walipambana kumshawishi Briton, mpaka akawaelewa, waliagana nakukubaliana hili la Briton likiisha watakaa mtu na dada ake wayajenge pia..
Huku kwetu kulikucha, tulifika nyumbani saa 12 asubuhi tukatia timu mwanza, tulifika nakupokerewa vizuli mno sikutegemea, Kwa jinsi walivyonifikuza nyumbani Leo wananipokea Kwa machozi ya furaha na mtoto wanamgombania, nilifurahi mno jamani miaka 6 sijaonana na wazazi, japo mama nilikuwa naongea nae lakini hamu ya kumuona na kuongea ni tofauti kabisa..
Nilipokelewa na kuchinjiwa ng'ombe ukaribusho wa mjukuu na watoto nyie aaahh, bibi tulimkuta kadhoofu sana, alifurahi mno kutuona tuligongea, tulikula kama hatutokula tena, kaka angu bado hajaoa jamani apa mjukuu ni mmoja acha atambe mwanangu na Ile afya yake alizingatiwa kama yai vile akikohoa tu, Kila mtu kamwahi nini sio mjomba sio Babu , sio bibi Yani hizi laha zilikuwa za kwangu last born😭 , nilijikuta nalia, Yani wote wanamjali tu Thom Mimi ata hawanijali kweli jamani 😭😭😭😭😭, nililia Kwa sauti ndo wakaniuliza tena ata hawakunifata nikaongea sauti kulia...
Mwanangu alinikimbilia kujua nalilia nini na wengine ndo wakaja ety nimekuwaje😭, Yani nyie wote mnamjali Thom tu Mimi hakuna anaenijali, mnaona nalia atakunijali hamna mnaniuliza mkiwa uko uko tom kaja ndo nanyie ndo mnakuja, saweni tu huku navuta mdomo na mchozi ...
Joshuka; ha ha ha ha ha ha ha ha kumekucha na maakucha yake hivi huyu mtoto wenu atakujaa kujua kweli Sasa jitu Zima linamuonea wivu mtoto heee jamani 😀😀😀😀...
Mama Bea; jamani Bea binti yangu mi nilijua ukizaa utakuwa mwanangu uache madeko kumbe ata haijasaidia..
Thom; aah bibi nyie wanawake ndo mlivyo nilikuona ata wewe muda ule tumefika, ulikuwa unamdekea Babu, unalia unajisogeza Kwa babu akukumbatie, 😀 ata shuleni naonaga vidada vinalia Lia ovyo na kudeka, nilikuwa najiuliza mama mbona anadeka sana kumbe ni bibi kamuambukiza Mimi nitakuwa nimerithi Kwa babu au baba, make singa utoto wakulia Lia ovyo..
Ha ha ha ha ha Aya Sasa kumeanza kuchangamka umu ndani, anko kweli aisee we dume la ukweli mwanangu, kumbe na bibi Yako umemuona alivyonamadeko eee ha ha ha ha ha..
Babu Thom; mjukuu wangu ni jembe kweli apa sijala hasara nimepata faida mala mia mjukuu wangu ni mwerevu nimempenda..
Yani niliona wananizingua zaidi nikaongeza kulia, ilibidi thom na baba, wanimbembeleze mpaka nikanyamaza,nakusinzia kabisa..
Ha ha ha ha ivi anko mnaishije uko Kwa Hali hii Yani badala wewe akumbembeleze wewe ndo unambembekeza mama Ako hii Kali ya mwaka Mungu anisaidie nisije nikaoa last born, siwezi hii kazi. Ha ha ha ha..
Anko shiiiiiiu🤫🤫, nyamaza basi ataamka ujue, akiamka utambembekeza mwenyewe mpaka alale, watu ilibidi tu wacheke, Joshua alishindwa kuvumilia, akaamua akavunje mbavu nje Kwa uhuru..
Arusha Briton na stv waliamka alfajili, wakapanda ndege mpaka mwanza, walifika mapema, nakuelekezwa na Sara mpaka kwetu, na waliunganishwa na Joshua Ili awapokee,
Sara; haloow kaka Joshua wageni wamefika tunafanyaje? Nashauli ukawapokee wanaweza kupotea ..
Joshua; ha ha ha sawa ila inabidi tuwambie wazee huo ugeni sio mdogo ata kama hawapatani hayo hayatuhusu, " mmh ila ni kweli hakikisha Bea hajui ataninunia mwaka mzima uyo" afu umenikumbusha ivi Sara 😀 mnaishije na huyu last born wa mama beatha jamani, kafika Leo tu katuonesha maajabu analia bila sababu kweli thom, ndo wakumbembekeza mama ake? ..
Kaka Joshua nawewe apo kigeni kipi mbona mi nishazoea, anadeka Bea we acha tu,
Joshua;aisee poleni Yani Mimi nilitegemea Bea akizaa ataacha kudeka jamani mdogo wangu Sasa huyo mwanaume wake ataweza kweli hii kasheshe...
Sara; anaonekana kumpenda kupitiliza bila shaka anaweza, anaonekana kuweza, fanya basi ukapokee wataanza kutafuta wenyewe Yani mwanaume ni anshamu ya kumuona Bea sio kidogo ni alitaka kuondoka Toka usiku, tumehangaika sana kumuelewesha ..
Joshua ; pia dogo ngoja niwawahi , mama Bea ,mamaa, jamani nini Joshua mbona tunaumizana masikio, kijana wangu..
Njoo tutete apa Kuna jambo, mama alitoka wakasogea nje Kisha Joshua akamueleza, Kuna ugeni alimpa maelezo yote aliyopewa na Sara, Joshua mwanangu hili inabidi tuongee na baba pia ni jambo la heli kama Yuko tayali kuichukua familia yake tushukuru Mungu kwakweli , kwangu Leo imekuwa siku ya baraka kubwa sana, nilikuwa namuwazia binti yangu itakuwaje na jinsi alivyo kuwa single mother Mungu amesikia kilio changu, sikutaka mwanangu azae na wanaume tofauti, hakika hili tutaongea na beatha mpaka ataelewa, ila kwanza tuongee na kijana tumjue tusijekumpa mtoto wetu, mtu asiefaa, ngoja niongee na baba Ako Kisha nikupe jibu kama uwafate uwalete nyumbani ama laa, subili jibu...
Itaendelea...🔥
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote