SIO KILA ANAEJIUZA AMEPENDA
siku moja kuna kijana alinunua dada poa, kwa maana hawa mabinti wanaojiuza, akaenda nae nyumban kwake na walipofika wakafanya yao baada ya hapo yule binti kwa unyonge akataka malipo yake ila yule kaka akamuahidi atamtumia maana alichukua namba zake ..
Kiukweli hakuwa na nia ya kumlipa mpaka yule binti alipomtumia sms inayosema "hata kama haujapata naomba unitumie hata elfu moja nikale tu..
Maneno yale yalimuuma sana yule kijana, na kuamua kumtafuta na kutaka kujua kuwa anaishi wapi, alifika anapoishi akakuta anaishi na bibi yake mzee sana, na hajiwez kwa lolote lile, roho ilimuuma na kuamua kumsaidia yule binti, maana aliamin kuwa hakuwa anajiuza kwa sababu anapenda ila ni shida alizokuwa nazo...
Baadae anakuja kuona uzuri wa yule binti, kimuonekano na kitabia mpaka akahisi huyo ndio yule mwanamke ambae alikuwa anamuota kila siku, je unataka kujua hatma yao usikose simulizi hii ya SUREYAH (changudoa mpaka mke mwema)...
SUREIYAH (changudoa mpaka mke mwema)1
HUSQER BALTAZAR
Wakati ambapo binaadamu tutaacha kuwahukumu watu wengine basi dunia itakuwa sehemu ya amani sana, maana sio kila mtu anapenda kufanya kazi au biashara za kujidhalilisha….
Siku moja usiku kwenye majira ya kama saa nne usiku, sudeys alikuwa anatoka kazin, alikuwa kachoka sana, na siku hio aliacha gari lake kwenye matengenezo na akawa anarudi nyumban kwa miguu taratibu, maana sehemu ambapo aliacha gari mpaka sehemu alipo hakukuwa na umbali sana…
Akiwa anatembea kwa mwendo wa kichovu sana, akiwa ameshikilia simu yake mkono mmoja, na mkono mwingine alikuwa ameshikilia jaketi lake la suti, mara akatokea binti mbele yake, na kwa makadirio alikuwa anaonekana kama anamiaka kumi na tisa au ishirini, binti Yule alimsalimia sudeys kisha akasema “ samahan kaka naomba unisaidie shilling elfu tano….
Kiukweli alikuwa amevaa nguo fupi sana, ila ni kama alikuwa anajionea aibu hata yeye mwenyewe, alikuwa ni mweupe ila ngozi yake ilifubaa, na alikuwa anaonekana kama ana maisha magumu, ila sudeys hakuliangalia hilo, akacheka kwa dharau na kupania kumkomesha, maana alimuona kama Malaya tu, na ndio kawaida yao kuja kuomba omba pesa, hivyo akamjibu “ unaona je kama nikienda kukupa hio elfu tano nyumban kwangu, alisema vile makusudi ili akamshughulikie, na cha ajabu Yule bint hata hakukataa, akakubali, na wakaanza kuongozana mpaka kwenye nyumba ya sudeys….
“ karibu sana nyumban mrembo, ila si unajua dunian hakuna kitu cha bure mamaa, sawa mimi nitakupa hio elfu tano lakin lazima na wewe unipe kitu cha kunilipa, akasema sudeys…
Yule bint aliangalia chini kwa karibu dakika moja na kwa kwa sauti ya chini sana, yenye aibu na kukata tamaa akajibu “ ndio maana nimekuja nyumban kwako, najua hakuna kitu cha bure…
Sudeys alifurah sana na kuona nyama imejileta yenyewe, sasa ni jukum lake kujihudumia tu, basi akaingia chumban kwake kisha akatoka na vipimo, maana hawa wadada wa hivi wanakuwaga na maradhi sana, kisha wakapima na kujikuta wote ni wazima, na sudeys akaanza mambo yake pale pale, akaanza kumshika shika tu Yule bint, ila bint hakuwa anaonekana kama ana hisia kabisa, ila kwakuwa sudeys alikuwa na muda kidogo hajakutana na mwanamke, hivyo hata kama Yule bint hakuwa anatoa ushirikiano kabisa, ila alikuwa anasisimka…
Mwisho akamlaza na kuanza kujilia vyake, alikuwa na upwiru wa dunia ya mwisho, alimkula mtoto wa watu kwa karibu masaa matatu, baada ya kumaliza Yule bint akasema “ umeshamaliza unachokitaka, sasa naomba hio elfu tano…
“ sasa hivi njin usiku sana, hata kama nikisema nikupe sasa hivi hakuna kitu utaifanyia zaidi ya usafiri tu, hivyo kama hautajali naomba usubiri kupambazuka, maana mimi nimechoka sana hivyo siwez kukusindikiza…
Mwanzo Yule bint alikataa, ila sudeys akalazimisha sana, mwisho akakubali, ila alikuwa anaonekana kama mtu mwenye wasiwasi sana, ila sudeys hakujali, na usiku mzima Yule bint hakulala, na kuna muda sudeys alikuwa akiamka anamuona kama anafuta machozi hivi, ila hakumjali akajua lazima atakuwa na mambo yake tu…
Basi kama tunavyojua kuwa kukuzidi kuwa giza basi ndio kunakaribia kukucha, sasa hata kwa upande wa sudeys pamoja na mwanamke wake wa mchongo nao ikawa hivyo hivyo, kwa maana kukakucha, sudeys alivyo mkorofi akamuamsha bint wa watu na cha asubuh , ingawa bint hakuwa anataka ila alimpa tu kwa maana hakuwa na namna, kisha sudeys akaenda kuoga na baada ya kuoga akatoka na kumkuta sureiya ameshajiandaa kana kwamba anataka kuondoka, kisha akasema “ naomba basi hio hela….
“ niachie namba yako na nitakutumia, akasema sudeys ila ukweli ni kwamba alikuwa anataka kumkomesha tu huyu dada, na hakuwa na lengo hata la kumlipa, Yule bint akakubali kumpa namba kisha akasema unaweza kunibip au kutuma sms ili na mimi niwe na namba yako, na kama hautajal naomba unisave sureiyah………….
Basi kweli sudeys alimpigia simu sureyah na sureyah akaondoka zake, na kumuacha sudeys akiwa anaendelea na shughuli zake, kiukweli sudeys hakuwa na mpango hata wa kumlipa, kwa maana kwa maisha aliokuwa nayo asingeweza kukosa elfu tano au zadi ndani…
Baada ya masaa kama mawili sudeys akapokea sms kutoka kwa sureiyah ikasema “ mbona hutumi hio hela, kama huna naomba nisaidie hata shilling elfu moja nikale….
Hii sms ilimshangaza sana sudeys na akajisikia vibaya, alikuwa anataka kumrusha ila maskin ya mungu kumbe sureyah wa watu alikuwa anatafuta pesa ya kula…
Baada ya sureyah kutuma ile sms sudeys akaacha kila anachokifanya kisha akampigia sureiyah, kweli baada ya kupiga simu, simu iliita kwa sekunde kadhaa na kupokelewa, baada byua salamu sudeys akataka kujua suereiyah anaishi wapi, na sureiyah kuwa anahiyana akamuelekeza mpaka anapoishi…
Baada ya dakika kadhaa sudeys akafika kwenye nyumba ambayo sureyah alikuwa anaishi, ilikuwa ni nyumba mbovu sana, kwa maana kwanza haikiuwa imeisha na inaonekana ni kama walikuwa wamepewa hifadhi tu, maana hata juu iliezekwa na turubai…
Sudeys alijisikia viobaya sana na akaul;iza “ ndio huwa una ishi hapa?....
Sureyah kwa sauti ya unyonge akasema “ ndio nakaa hapa na bibi yangu…
Basi sudeys akaenda kuleta mahityaji yote ya msingi ambayo yaliukuwa yanahitajika pale, kwa maana alinunua mchele, unga wa ugali, dagaa, akajaza gesi maana walikuwa nalo, akanunua mafuta, sukari unga wa ngano kisha akamuachia sureyah laki moja kisha akasema “ naomba usifanye tena biashara ambazo huwa unafanya na ukiwa na shida yoyote ile nambie nitakupa pesa…
Basi sudeys akaondoka zake, na kuanzia siku ile sureyah na bibi yake likawa kama jukumu lake, yaan mambo ya misosi ikawa haikosekani, hakuwa anaenda kuwatembelea kila siku ila alikuwa anaenda mara nyingi sana kukaa nao na kuwafariji, na hakuwah hata mara moja kumtaka sureyah kimwili tena kwa maana alikuwa anamuheshimu kama mdogo wake waliozaliwa nae tumbo moja….
Siku moja sudeys alikuwa anaenda kuwatembelea sureyah na bibi yake, ,mara akamuona sureyah anapandishwa kwenye gari na mtu, sureyah wakat huo hakuwa amemuona, akamtumia sms na kusema “ usitake kunambie bado unajiuza mpaka sasa hibvi licha ya mimi kufanya kila kitu…
Sureyah hakujibu ile sms na badala yake akakaa kimya, ni kama ka wivu kakaanza kumuingia sudeys kwa, kwa maana akajikuta anaanza kumtumia sms kwa fujo mara ampigie, sureyah akazima na simu kabisa, na kwenye majira ya kama saa tatu usiku sureyeh akarudi pale ambapo alikuwa anaishi na bibi yake, akashangaa anamkuta sudeys amekaa na bibi yake na wakat huo sudeys alikuwa anamslisha bibi yake na sureyeh…
Basi sudeys akamlisha Yule bibi kisha akatoka na sureyah nje, alikuwa anaonekana kama ana hasira sana, na akamuuliza, “ embu nambie ilikuwaje mpaka ukaamua kwenda kujiuza na wakat unaona kabisa napambana sana kukupa kila unachokitaka…
“ hauwezi kunipa kila ninachokita sudeys, hauwezi, wewe umenisaidia sana kuhakikisha chakula hakikosekani ninapoishi, ila haujawah kujiuliza kuhusu dawa za bibi yangu, bibi yangu anatakiwa pesa ya dawa kila baada ya wiki mbili, unafikiri mimi natowa wapi pesa zake za dawa, akasema sureyeh …
“ lakin si iungeniambia kuliko kwenda kujiuza, au unasikia raha kuutumia mwili wako na kujiwekea nuksi ya kila mwanaume si ndio, akaongea sudeys kwa sauti ya ukali…
“ naona haya naona aibu sana kukuomba kila kitu sudeys, mimi ni binaadamu na nimeumbiwa haya, naona umetusaidia sana nikawa naogopa kukuomba kila siku, unaniona kama nina moyo mgumu kiasi chote hicho, mimi sina moyo mgumu, sina uwezo wa kukuomba kila siku sudeys naona aibu maana umeshanisaidia sana, akawa analalamika sureyah na sudeys akamsogelea kisha akamkumbatia na kusema “ hupaswi kuniogopa, haujui ni kiasi gani huwa najisikia vibaya kila nikijua kuwa umeenda kujiuza, hivyo ukiwa na shida yoyote ile naomba usisite kunambia mamaa, maana hukuniomba ila nimetaka mwenyewe kukusaidia mamaa, nakuomba tena usije ukaenda kujiuza maana nimeshaamua kuwa wewe ndio uwe jukum langu, na nitapambana kuhakikisha unapata kila unachokitaka tena kwa wakaty kila ukiwa na mimi, akasema sudeys kisha akamkiss sureyeh kwenye paji la uso na kumtakia usiku mwema kisha akaondoka zake….
Lakin busu la siudeys ni kama lilibadilisha muelekeo wa mapigo ya moyo ya sureyah na kumfanya sureyeh ahisi msisimko mkubwa sana ambao hajawah kuupata kabla…
NAKUJA………………….
SUREYAH (changudoa mpaka mke mwema) 2
Basi siku hio sureyah alilala kwa tabu sana, yaan kila dakika alikuwa analikumbuka lile busu ambalo sudeys alimpiga kwenye paji la uso wake, akawa anajikuta anapapasa komwe lake kila wakat huku anatabasamu…
Mawazo yake usiku kucha yalikuwa ni juu ya sudeys alikuwa anataman sudeys angeendelea kukaa pemben yake na kumpiga mabusu mpaka asubuh, ila hakujua hata atawezaje kukaa nae na wakat alikuwa asnamchukulia kama mdogo wake tu, licha ya kuwa mara ya kwanza alishawah kulala nae….
Basi siku hio ikapita na hatimae majogoo ya siku mpya yakaanzakuwika, sureyah alishtuka mara baada ya kuona kumepambazuka na wakat hata lepe la usingizi halijagusa macho yake, akajinyoosha nyoosha na kuachia tabasamu mururu kisha akaniambia “ ohhh sudeys sijui kwanini nakufikiria kiasi hichi, kisha akaamka na kuanza majukum yake…
Basi akamuandalia chai bibi yake, kisha akamuogesha maana hawezi kujifanyia chochote kile, na baada ya hapo , akamalizia baadhi ya majukum, ila kila ambapo alikuwa anakaa pekee yake alikuwa analifikiria lile busu la sudeys, alikuwa anataman sana sudeys awe anambusu vile kila wakati, alijikuta kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake akitaman kuwa na mahusiano na hata ikiwezekana aolewe kabisa, na mtu ambae alikuwa anatamani kuolewa nae alikuwa ni sudeys, ila aliamin huenda sudeys hampendi na anamchukulia kama mdogo wake tu…
Basi muda ukawa unazidi kwenda, na siku hio sureyah hakutoka kabisa, maana kama ni dawa bibi yake alikuwa nazo, na kama chakula kilikuwepo cha kutosha, sasa hakuona sababu ya kwenda kubadilishana mwili wake na kitu chochote kile kingine, basi siku nzima alikaa akimfikiria sudeys tu…
Alikuwa na simu ila aliogopa sana kumpigia, ila muda ulizidi kwenda akawa anajikuta uvumilivu unaanza kumshinda na tamaa yake ya kuonana na sudeys ikawa inazidi kuwa kubwa na kila wakat akawa anataman kuina sura yake hata kwa kidogo tu, basi akaingia ndani na kuanza kujiandaa, akaanza kutafuta nguo ambazo zingeweza kumfanya awe mzuri kidogo, ingawa hakuw na nguo yoyotr ile ya maana, kisha aka[paka na wanja wake kidogo ambao uliyapamba vyema macho yake na kuyapa mvuto wa kipekee sana….
Kisha alikuwa na pafymu yake akajipulizia kidogo ili nay eye awe ananukia, akamsogelea bibi yake akamkiss kwenye mikono yake kisha akamuaga na kumuambia kuwa atarudi baada ya muda mfupi, na ilikuwa ni kawaida kwake kuondoka na bibi yake hakuwa na uwezo wa kukataa, basi sureyah akaanza safari mpaka nyumban kwa sudeys…
Alifika na kukuta mlango umerudishiwa , akaugonga kwa dakika kadhaa mara akashangaa kuna mwanamke anatoka, alikuwa amevaa kawaida sana, ila sureyah akajikuta anapatwa na wivu wa ajabu, akawa anataka hata kuondoka, mara akaja sudeys akiwa na taulo kiuno huku akisema ‘ zamda unaondoka saa ngapi na wewe, maana leo umelazimisha mpaka ukashinda hapa siku nzima…
“ naona umepata mwanamke mpya chotara, yaan huyu akipakwa mafuta vizuri ni mzungu kabisa, ila wewe nae umezidi kuhangaika na kukitembeza sijui lini utacha umalaya….
Sio siri yale maneno yalimuuma sana, ila akajikaza, nikajua labda Yule mwanamke ni mwanamke wake, sureyah akaingia ndani kwake kwa unyonge mkubwa sana, kisha taratibu akaenda kukaa kwenye kiti, Yule mwanamke alikuwa anajiandaa kuondoka, kwa maana baada ya sureyah kufika pale alikaa muda mchache sana kisha akaondoka zake, alikuwa nasikia wivu wa ajabu, alikuwa anaumia sana mpaka akawa anajishangaa kwa nini alikuwa anaumia kiasi kile…..
Sudeys akatoka alikuwa kana kwamba anataka kwenda sehemu, ni kama alishasahau kama amemuacha sureyah pale ukumbini, alipomuona akashtuka kisha akasem “ nilishasahau kabisa kama ulikuwa hapa, kliukweli nilikuwa natakiwa kwenda kwenye shughuli kazin, kama hautajali tunaweza kwenda wote, maana sina mwenza wa kuongozana nae…
“ sina nguo ya kuvaa, akajibu sureyah…
“ ahhhh nilisahau, unaweza ukaingia bafuni ukaoga, kisha naenda kukutafutia nguo na utaenda saloon kupigwa makeup kidogo, au tunaweza kutoka kwa pamoja hapa, na tukapitia moja kwa moja kwenye duka la dawa na saloon, akasema sudeys na sureyah akafanya kama sudeys anavyotaka….
Basi akaingia bafuni na kujimwagia maji, na baada ya dakika chache akatoka na mara baada ya kutoka wakaanza kuongozana na sudeys, siku hio gari la sudeys lilikuwa sawa, maana lilisharudi kutoka kwenye matengenezo, basi wakapanda gari, na kuanza kuelekea kwenye duka la nguo, sureyah akaanza kujaribisha nguo, na kwa namna umbo lake lilivyokuwa yaan kila nguo ilikuwa inampendeza sana, na baada ya hapo akaenda saloon…
Yaan ametoka kupambwa sudeys ni kama alipigwa na bumbuwazi kwa namna alivyokuwa mzuri, sureyah alikuwa amevaa gauni lenye rangi nyeupe na maroon, akavaa viatu vyake vyeupe ns pochi ya marron, sudeys slipigwa na butwaa akawa anamuangalia kwa jicho kavu la matamanio makubwa sana, sureyah akatoka na kumfata sudeys na hapo ndipo uvumilivu ukamshinda akajikuta anamsifia na kusema “ hakika wewe ni mrembo sana, sijawah kufikiria kama unaweza kuwa mrembo kwa kiasi chote hichi, sureyah hakuwa na jibu zaidi ya kutabasamu tu….
Basi bana wakaenda walipopanga kwenda ila wakati wote sudeys alikuwa anamchunga sana sureyah na mwanaume yoyoyte Yule ambae atamtazama alikuwa anamchukua suyreyah kila wakati na kumuweka pemben yake, alijikuta ana wasiwasi mkubwa sana wa kumpoteza, sasa kama tunavyojua mambo ya sherehe, huwez kukaa na mtu mmoja kwa muda mrefu na ndivyo hivyo hivyo ilikuwa kwa sureyah, hakuwa anaweza kukaa muda mrefu,ndio hivyo hivyo ikawa kwa sudeys kuna muda alikuwa anasalimiana na watu, mara akasikia sauti ya sureyah ikisema “ niache niache..
Alitoka huko alipo akakuta kuna mwanaume analazimisha kumshika shika, aiseee alimvamia na kuanza kumshushia mangumi mfululizo bila huruma, yule mwanaume akaanza kutoa maneno machafu na kusema “ huyu ni changudoa ni chakula cha kila mtu, sasa kwa kuwa umekuwa nae haimaanishi kama atabadilika tabia na atabaki kuwa changudoa tu..
Sudeys akapoa kisha akamuangalia sureyah kwa hasira na kumshika mkono na kuanza kumkokota kwa lengo la kutaka kurudi nae nyumban……
NAKUJA
SUREYAH (changudoa mpaka mke mwema) 3
HUSQER BALTAZAR
Walipofika kwenye gari sudeys alikuwa na hasira sana akamgeukia sureyah na kusema “ nakuhitaji kwa usiku wa leo unadhani naweza kukulipa bei gani…
Hii kauli ilimfanya sureyah ajisikia vibaya sana, kisha akamjuangalia na kusema “ ni kweli unataka kuninunua na kwanini una hasira kiasi kile, mbona kama naona kama una wivu juu yangu, kama unanipenda nambie tu..
“ nani? Mimi ! yaan nikae naacha kazi zangu nampenda Malaya, nikae namuonea wivu Malaya, nma wakati kuna wanawake wengi sana wazuri tu, ambao wanakila sifa za kuwa wanawake bora na wanamaadili yakueleweka na sio wewe, ambae unajiona mzuri kumbe ni wakawaida tu, na kuamua kutumia uzuri wako kama njia za kukupatia kipato, na ndio maana marafiki zangu wameoa wanawake wa kawaida, ndio naanza kuelewa, yaan kuoa mwanamke mzuri ni sawa na kupanda shamba la miwa kwenye uwanja wa shule…
Yale maneno yualizidi kumkerasana sureyah, akamuangalia sudeys kisha akaanza kufungua mlamgo na kutaka kuondoka..
“ una enda wapi? Akauliza sudeys kwa sauti ya ukali..
“ siwez kukaa na mwanaume kama wewe hapa, Naomba uniache niende nyumban pekee yangu, akasema sureyah akiwa anafungua mlangfo wa gari na akiwa tayari kwa kushuka, akashangaa sudeys anamshika mkono kisha akamuambia “ kwa hio unataka kwenda kuendelea kyufanya umalaya wako si ndio…
“ nji kweli naenda kyfanya umalaya, hivyo naomba niache na maisha yangu, maana siwez kuendelea kuvumilia kukuona unanidhalilisha kiasi hichi, ni kweli mimi nimeshawah kujiuza, ila hilo halimaanishi kwa mba nilikuwa nafanya vile kwa kupenda, wewe mwenyewe unayajua maisha yangu, sina elimu, sina mtaji ulitegemea nitaishije na sina mtu ambae anaweza kuynihudumia hata kwa kidogo, naomba niache nikaendelee na maisha yangu, ingawa nilikuwa nateseka na naumia kufanya hizi biashafra ila angalau nilikuwa naamani kuliko kukaa na mtu kila wakati ananidhalilisha tu…
Akashangaa anavutwa ndani ya gari, kisha sudeys akaanza kulazimisha kumkiss, kwa kuwa sureyah nae alikuwa na hisia na sudeys basi akajikuta anampa ushirikiano wa kytosha, wakaanza kukiss pale na mwisho wakazama kule….
Kila mmoja alifurahia utundu wa mwenzake, ila sudeys ni kama alipatwa na pepo na wivu, kwa maana alijikuta anaumia sana baada ya ile shoo na kumuuliza sureyah kuwa “ kwa hio na hao wanaume wengine huwa unawapaga kama ulivyonipa mimi..
Sureyah akamuangalia kisha akasema “ mimi nakupenda sudeys, nataman kufanya jambo lolote lile kuhakikisha hautoki kwenye upande wangu..
“ unaulizwa swali lingine na unajibu swali lingine kabisa, nimekuuliza kwa hio unawapaga wanaume wengine kama ulivyonipa mimi? Hayo maswala ya kunipenda yametoka wapi hapo? Akauliza sudeys na sureyah akamuangalia bila kumjibu, sudeys akaanza kujiongelesha na kusema “ ndio kawaida ya Malaya hii, yaan hawanaga aibu kabisa, yaan badala ya kusubiri watongozwe wanaanza kujitongozesha wenyewe…
Sureyah alijisikia vibaya sana, akamuangalia sudeys kisha akasema “ mimi naondoka siwez kukaa hapa na kuangalia unaendelea kunidhalilisha hata mara moja…
Sudeys akacheka kile kicheko cha uchungu kisha akasema “ najua unaniaga hapa kumbe umeshaona sms ya mteja, hivyo unatafuta namna ya kuachana na mimi vizuri, ila mbona nimekupa vizuri tu wewe mwanamke, au ndio kunguru hafugiki nijue kabisa….
Sureyah hata hakuymjibu akashuka na kuanza kuodnoka zake, na sudeys klwa hasira akawasha gario na kumuacha sureyah pekee yake, aiseee sureyah alijisikia vibaya, akakaa sehemu akaanza kulia, alilia sana, kisha akaanza zake safari ya klurudi nyumban pole pole..
Ingawa sudeys alijifanya ni baba mahasira, ila hata gari lenyewe hakuwa analiendesha kwa amani, kwa maaana alikuwa anawaza, itakuwaje kama sureyah kapata mteja, akajikuta anashindwa kuendelea na safari, na akaanza kurudi nyuma, alijikuta anawivu wa ajabu sana na sureyah, alipokuwa anarudi nyuma ndio akamuona sureyah amevua viagtu maana vilikuwa ni vizrefu na anatembea akiwa amevishikilai viatu vyake mkononi, taratibu akawa anatembea zake peku peku…
Sudeys alimuona akajisikia vibaya, alijua sababu ya yote ni wivu wake, akampigia simu mtu akamuomba alete taksi maeneo yale, maana alijua kwa hasira ambazo alikuwa nazo sureyah asingeweza kupanda kwenye gari lake, na kweli baada ya muda taksi ikafika, alikuwa ni rafiuki yake sudeys na sureyah alishawah kumuona hivo walikuwa wanafahamiana, sudeys akaomba afanye vyovyote vile, ila ahakikishe sureyah anaenda nyumban na usafir na sio anatembea vile kidhalili, basi Yule kijana alikuwa anaitwa swaleh, hakukataa na kwenda mpaka usawa wa sureyah kisha akasimamisha gari na kushusha kioo cha gari kisha akasema “ ohhh sureyah naweza kukusogeza kidogo…
Ilikuwa ni usiku, hivyo sureyah hakukataa, taratibu akaachia tabasamu na kusema “ asante sana, kisha akaenda kwenye gari na kupanda, hapo sudeys akapata amani kidogo ya moyo, basi sureyah akapelekwa mpaka nyumban na wakati wote huo sudeys alikuwa nyuma anafuatilia, na sureyah alipofika sehemu aliokuwa anaishi akapata amani kidogo na kuanza safari ya kurudi kwake..
Amefika nyumban kwake, akawa anaona hapakaliki kabisa, na muda wote alikuwa anajikuta anakumbuka shoo ya sureyah, akawa anajiambia kuwa “ namtaka huyu bint nataka kumuoa nahisi kama nampenda sana, eee mungu wangu naomba nionyeshe njia sahihi naomba umbadilishe kwaajili yangu, baada ya hizo dua zake, akaona akaoge kisha ajilaze, ila usingizi ni kama uliweka mgomo baridi,m maana alikosa hata lepe na usingizi na kujikuta anafikiria kila alichofanya na sureyah siku hio, akajikuta anamkumbuka sana, akajikuta anataman sana kuwa karibu nae, akawa anajikuta anataman sana kumuona maana aliamin ilia pate usingizi ni lazima amuone sureyah wake……
Akakurupuka wakati ule ule na kuanza safari ya kuelekea anapoishi sureyah, alifika na akawa anahisi lazima atakuwa amelala, ila haikuwa hivyo, akawa anaona mwanga hafifu ndani, kwa maana ulikuwa ni mwanga wa mshumaa au kibatari, akajaribu kuchungulia akamuona sureyah amekaa pemben analia, alijisikia vibaya sana, akahisi labda anaumia kwa alicho mfanyia, akajikuta anaanza kujuta, na namna zureyah alivyokuwa na majuto na maumivu hiki kitu hakikumuacha salama kabisa sudeys, na kama tunavyojua ukimpenda mtu hadi maumivu yake unakuwa unayahisi, na hivyo hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa sudeys, akawa anaumia kwa namna sureyah anavyolia…
Basi siku hio sureyah hakulala kabisa, na sudeys nae akalala pal,e nje, maana aliogopa kumsumbua sureyah wake, na kuamua kumuangalia mpaka akaja kupitiwa na usingizi pale nje…
Asubuh sureyah akaamka ili kuendelea na majukum ya usafi, anashangaa anamuona sudeys amelala pemben ya mlango wao, akaanza kumuangalia kana kwamba anamkagua kisha akamsogelea nakutaka kumbusu, maana akimuona sudeys hata kama ana hasira kiasi gani basi zote zitakata na zitaisha kabisa. Sasa sudeys akaanza kuhisi lile joto la mtu kukaa karibu yake, akakurupuka huku akisema “ sureyah…
NAKUJA……………
SUREYAH (Changudoa mpaka mke mwema) 4
HUSQER BALTAZAR
“ mbona umelala hapa nje? Na ulikuja saa ngapi? Akauliza sureyah..
“ am hamna nimekuja wakati huu iola jana usiku nilikesha kuangalia movie hivyo nilikuwa nasinzia sinzia tu, akasema sudeys ..
“ sawa karibu ndani. Akasema sureryah kwa sauti ya upole, sudeys akamuangalia kisha akatabasamu……
“ mbona unatabasamu, karibu ndani, akaendelea kusisitiza sureyah…
Kwa upole sudeys akasema “ nakupenda mamaa…
Sureyah ni kama hakuwa anamsikia vizuri, akauliza kwa mshangao “ nini!...
“ amna ila nahisi utakuwa umenisikia vizuri sana, mimi naku.., kabla sudeys hajamaliza kitu ambacho alikuwa anataka kukisema mara wakasikia mtyu ndani anakoroma, na hakukuwa na mtu zaidi ya bibi yake sureyah, hivyo wote wakatimka na kwenda kuangalia kuna nini, ndipo wakamkuta anamalizia kukata roho…
Sureyah kiukweli hakuelewa kabisa kinachoendelea, hakuamin kama bibi yake a,mefariki akaamin labda amezidiwa, akaanza kupiga kelele za kutaka msaada kwamba sudeys anatakiwa amsaidie kumpeleka bibi yake hospital…
Sudeys akamsogelea kisha akamkumbatia na kumuambia bibi yako ameshafariki, hatuwezi kumpeleka hospital maana zinatakiwa ziandaliwe taratibu za mazishi yake mamaa…
“ hapana, hapana.. hapanaaa, akaanza kupiga kelele sureyah akiwa kama amechanganyikiwa hivi yaan, kisha akaanza kusema “ bibi yangu hawez kufa, bibi yangu hawez kufa sudeys, bibi yangu ananipenda sana na haeez kufa na kuniacha pekee yangu, akaendelea kupiga kelele za uchungu, ila sudeys akawa anamtuliza, ila sureyah alikurupuka na kuamka kisha akamfata na kumuambia “ ndio ameshakufa hivyo, nani ambae atabalki na mimi, nani ambae atakaa na mimi bibi, kwanini bibi umeniacha, mimi sina ndugu umeniacha bibi yangu, nimefanyaq kila kitu kwaajili ya maisha yako, nimeuza mwili wangu, nimetukanwa ili ubaki na mimi, maana sina mtu mwingine ambae anaweza kuwa upande wangu, sina ndugu mimi, na wewe ndio umeniacha, sasa mimi nitakaa na nani….
“ utakaa na mimi sureyah usilie sana utamkufuru mungu mamaa, akasema sudeys kwa sauti ya upole …
Sureyah hata hakuwa anamuelewa na kitu pekee ambacho alikuwa anafanya ni kulia tu, alilia kwa uchungu sana mpaka akaanza kukusanya watu eneo lile, basi watu wakajaa na taratibu za mazishi zikaanza, haikuwa rahisi kwa sureyah ila mwisho hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na ukweli tu, kuwa hayupo tena na bibi yake, sudeys akasimamia taratibu zote za mazishi, na mwisho mwili wa bibi yake sureyah ukapumzishwa kwenye makazi yake yamilele…
Basi baada ya mazishi sudeys akamchukua sureyah na kwenda kuishi nae, sureyah alikuwa ni mtu ambae amekata nta,ma asana, alikuwa anajifungia ndani na kulia tu, hakuwa anafanya kazi nyingine yoyote zaidi ya kulia, mpaka akapungua maana hakuwa hata anaweza kula, na kila kitu ambacho alikuwa anakifanya alikuwa anakifanya akiwa na bibi yake, hivyo kikawa kinamkumbusha kuhusu bibi yake tu……….
Sudeys alifanya kazi kubwa sana kumuweka sureyah sawa, maana aliona atazidi kumkosa kutokana na msongo wa mawazo ambao alikuwa nao kutokana na kumpoteza bibi yake maana alikuwa na huzuni kupitiliza….
Basi sudeys Akaanza kumuonesha ule upendo wa kweli ambao alihisi kwamba sureyah hakuwah kuupataga kabla…
Siku moja sureyah kama kawaida yake alikuwa ni mtu wa kujifungia ndani tu, kwa maana hakuwa anatoka kabisa hata nje maana aliona kama dunia inamchanganya na kuna muda kama inamuonea vile….
NAKUJA…
SUREYAH (changudoa mpaka mke mwema) 5
HUSQER BALTAZAR
Basi ilikuwa ni birthday yake, hapo sureyah kajifungia ndani, na kwa namna ambavyo alikuwa kama kavurugwa hata hakuwah kutoka nje kuangalia ni kitu gani kilikuwa kinaendelea, sudeys akaandaa kila kitu kisha akazima taa za nyumba nzima na kuanza kumuita sureyah kana kwamba alikuwa anamtafuta, sasa baada ya sureyah kusikia anaitwa akawa anataka kutoka, sasa ile anatika nje, akashangaa anaona nyumba nzima ni giza, mara taa ikawashwa akashangaa anamuona sudeys akiwa amepiga magoti huku kashikilia pete mkononi kitu ambacho sureyah hakuwah kufanyiwa kuanzia anazaliwa kisha kwa upole sudeys akasema “ will you marry me….
Ni kama sureyah alishikwa na bumbuwazi kubwa sana, maana hakutegemea, na alikuwa na huzuni pamoja na majonzi makubwa sana ambayo yalimsahaulisha kabisa kama anatakiwa kuishi licha ya kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea kwenye maisha yake lakin alitakiwa kukubali kuwa sisi ni binaadamu na wote tutakufa muda ukifika, hivyo anapaswa kuamini na kuchukulia kama moja ya mitihani na safar ya kila mtu, maana hata na yeye atapita tu…..
Alishindwa hata kujibu, badala yake aliutoa mkono wake kwa maana alikuwa tayari kuvalishwa ile pete huku akiwa analia, na sudeys hata hakutaka kupoteza muda na badala yake akamvisha petye kisha akasimama na kumkumbatia, na kulikuwa na watu pale, kwa maana ya ndugu wa sudeys wakaanza kupiga makofi kisha sudeys akamnong’oneza sureyah na kusema “ happy birthday mrembo wangu….
Yaan hata sureyah mwenyewe hakuwa anakumbuka kabisa siku yake ya kuzaliwa, alijikuta anamkumbatia sudeys kwa nguvu kisha akasema “ asante sana kwa kuja kwenye maisha yangu sudeys, asante sdana, hakika wewe ni zaidi ya zawadi kwangu, na wewe ndio maana halisi ya Baraka ya misha yangu…
Basi sudeys akamchukua sureyah na kumpeleka kwenye chumba chake kisha akasema “ leo ni siku ambayo nakuchumbia na zaidi sana ni siku yako ya birtyhday hivyo naomba basi uvae na upendeze kwaajilio yangu…
“ lakin sudeys nimeisha sana, na sina uhakika kama kuna nguo yoyote ile ambayo inaweza kunikaa vizuri kwa hali hii ambayo ninayo….
“ embu acha kuongea kama mtu ambae amekata tamaa bana mamaa, mimi nakupenda hivyo hivyo, na nataka kila mtu ajue kuwa nimeoa chombo, yaan wewe hata kama ukonde ubaki mifupa mitupu bado utaendelea kuwa mwanamke mrembo ambae sijawah kumuona hata mara moja kwenye maisha yangu……
Sureyah akatabasamu maana hakuwah kuambiwa hata maneno matamu vile kabla, hivyo akakubali sudeys akatoka kisha yeye akaanza kuvaa, na baada ya hapo akashangaa mlango unagongwa na alipoenda kufungua akakutana na mdada mrembo akamuambia “ nimeagizwa nije kukupodoa, sureyah akatabasamu kisha akamkatribisha ndani….
Basi baada ya muda sureyah alikuwa tayar amependeza mno, na chumba cha sudeys kilikuwa kama ghorofani hivi, hivyo Yule aliempodoa akaondoka zake na sureyah taratibu akaanza kutoka kuelekea kulipokuwa na hio ghafla ndogo ya siku yake yakuzaliwa pamoja na siku ya kuvalishwa pete ya uchumba…
Mwanga hafifu ambao ulikuwa unamulika sebule ambapo sureyah alikuwa anaenda ulimfanya sureayah aonekane mrembo zaidi, maana kila aliekuwa pale alishindwa kudhibito macho yake na wakaanza kumtazama, na sudeys nae hakuwa amemuona ila akashangaa watu wote ambao wapo eneo lile wamegeuka na kushangaa kitu ikabidi nay eye ageuke, yaan hata yeye ni kama alipigwa na bumbuwazi, akajikuta anatabasamu na macho yake yalikuwa yanaburudika kumuangalia sureyah huku moyo wake ukipata msisimko wa kipekee sana…..
Taratibu akajikuta anamsogelea sureyah kisha alipofika kwenye usawa wake akamnong’oneza na kusema “ hakika umependeza sana, yaan mpoaka nataman nikufiche watu wasiendelee kukuangalia hivi mamaa, umependeza mno kipenzi changu…..
Sureyah akatabasamu kisha kwa sauti ya upole akasema “ asante sana sudeys wangu….
NAKUJA………
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote