SIMULIZI: SHADIA (LAANA INAYOTEMBEA)
MTUNZI: SUMAIYA MWENDO TUPO HAPA. COM
SEHEMU YA: 61
Baada ya kuona ukimya wa Shadia bado haujavunjika, Yasri aliamua kuingia bafuni kuoga. Maji baridi yaliyoteremka mwilini mwake yalikuwa kama dawa kwa mawazo yaliyokuwa yakimkosesha amani. Aliwaza, ' Kwa nini Dia amekasirika? Au kuna kitu nimekosea kwake'
Alipotoka bafuni, macho yake yaligongana na chakula kilichokuwa mezani. Kwa sekunde chache, alimtazama Shadia ambaye bado alikuwa amelala kitandani, uso wake umejificha
kwenye mto. Hakutaka kumsongelea zaidi kwa wakati huo, kwa hivyo alijikaribisha mezani na kuanza kujihudumia chakula.
Lakini hata aliposhika kijiko na kuanza kula, chakula kilionekana kupoteza ladha. Ukimya wa Shadia ulikuwa mzito sana; ulimzidi nguvu. Yasri alishusha pumzi ndefu, akaacha kula, na kurudi bafuni tena kupiga mswaki. Baada ya hapo, alirudi chumbani.
Aliingia kitandani polepole, akijisogeza karibu na Shadia ambaye bado alikuwa mgumu, akionyesha wazi kwamba hakutaka ukaribu. Yasri hakukubali umbali kati yao. Aliinua mkono wake na kumvutia Shadia karibu naye kwa nguvu, akamkumbatia kwa mapenzi makubwa.
Shadia alijaribu kujitoa, lakini mkono wa Yasri ulikuwa thabiti. "Dia, kwa nini hutaki kuongea na mimi?" Yasri aliuliza kwa sauti ya chini iliyojaa mahaba, huku akiweka uso wake karibu na wake.
Shadia hakujibu. Yasri alinyanyua uso wake kidogo na kumtazama kwa jicho lenye huruma. "Dia, nakuuliza kwa nini hutaki kuongea?" aliuliza tena, lakini bado hakupata jibu.
Yasri aliweka uso wake karibu zaidi na wa Shadia, akimgeuza kidogo na kumlalia juu yake kwa upole. Macho yao yalikutana kwa sekunde moja iliyozungumza zaidi ya maneno. Yasri alinyanyua kidogo mdomo wake na kujiandaa
kumbusu, lakini Shadia alifurukuta kwa upole, akionyesha kutotaka.
Kama mwanamume mwenye subira lakini pia anayejua kuonyesha upendo wake, Yasri alimwangalia Shadia kwa tabasamu la kejeli. “Sawa basi,” alisema kwa sauti ya kicheko cha upole. “Dia, una machaguo mawili. Uongee sasa hivi, au...” alisita kwa makusudi huku akisonya kwa mapenzi, “tufanye mapenzi.”
Shadia alikaa kimya, macho yake yakimtazama Yasri kwa aibu iliyochanganyika na hisia za ndani. Yasri alihisi mshipa wa moyo wake ukipiga kwa nguvu alipoinama na kumbusu tena, taratibu, kana kwamba alikuwa akiuliza kwa mdomo badala ya maneno.
Shadia alipumua kwa sauti ndogo na hatimaye alisema kwa sauti ya mahaba, “Nataka... nataka tufanye mapenzi, Yasri. Naku... nakupenda sana.”
Yasri alicheka kwa furaha, kicheko cha mtu aliyepata ushindi wa upendo. Alimwangalia Shadia kwa macho ya upendo na kumuuliza kwa utani, “Kwa hiyo, hiki ndicho kilichokufanya ukae kimya muda wote huu?”
Shadia alitabasamu kwa aibu, na kabla hajajibu, Yasri alimvuta karibu zaidi, akimuonyesha kwamba mapenzi yao yalikuwa na nguvu za kuvunja ukimya wowote.
Yasri alifurahi sana baada ya kusikia maneno ya Shadia, na aliandaa kila kitu kichwani mwake.
Mapenzi yalimjaa, moyo wake ukipiga kwa nguvu kana kwamba ulikuwa ukisherehekea usiku wao wa karibu. Lakini wakati alipomsogelea zaidi, Shadia alimuinua mkono kwa upole na kusema kwa sauti ya taratibu, "Yasri... pole, siwezi leo. Niko hedhi."
Maneno hayo yalimpiga Yasri kama radi. Alisimama ghafla, akimtazama Shadia kwa macho yaliyoshangaa, kisha uso wake ukabadilika haraka na kujaa hasira. "Unasema nini, Dia? Kama ulikuwa kwenye hali hiyo, kwa nini ulianza kuniambia yale maneno yote? Uliniacha nikifikiri kitu kingine kabisa."
Shadia alishusha pumzi, akijaribu kuzuia kicheko kilichotaka kupasuka kutoka kinywani mwake. Alimwangalia Yasri kwa macho ya aibu
na kusema kwa upole, "Samahani, Yasri. Nilikuwa natania tu. Sikujua ungekasirika hivi."
"Kutania?" Yasri alirudia kwa hasira, macho yake yakimtazama kwa karibu. Bila kusema neno zaidi, aliinuka kutoka kitandani, akazima taa, na kuelekea kwenye kochi. Alilala kwa kuguna, akimwacha Shadia akiwa peke yake kitandani.
Shadia alitabasamu gizani, akificha uso wake kwenye mto. Ingawa Yasri alikuwa na hasira, alijua kwamba angejituliza asubuhi. Fikra zake zilijaa furaha na utani wake wa usiku. Alilala kwa amani, akimfikiria Yasri na tabia zake za kushangaza.
Asubuhi ilipoingia, Yasri aliinuka kutoka kochini akiwa bado hajamaliza hasira zake. Lakini alipogeuza kichwa chake, alishtuka kumkuta Shadia amelala pembeni yake, amemkumbatia kwa mkono mmoja. Alitabasamu bila kujua, macho yake yakimtazama kwa upendo.
“Dia...” alijisemea kimoyomoyo, "Huyu mwanamke kweli hana mpango wa kuniacha peke yangu, hata kwenye kochi?"
Shadia alionekana bado yuko usingizini, lakini alijigeuza ghafla kana kwamba alikuwa kitandani. Harakati zake zilimsukuma Yasri pembeni, na kabla hajafikiri, walijikuta wote wakielekea chini kwa kishindo.
"Thud!"
Shadia alifumbua macho haraka, akiona uso wa Yasri uliokuwa karibu kabisa na wake. Yasri alicheka kwa sauti kubwa, macho yake yakijaa furaha. "Dia, kweli umeamua kuniangusha asubuhi yote haya?"
Shadia alicheka pia, akijaribu kuamka kutoka sakafuni. "Samahani, Yasri. Sikujua kwamba nilikuwa nakusukuma. Umeumia?"
“Kwa nini nikuumie wakati umeniangukia mwenyewe? Hebu tuache kujitetea na tuseme ukweli, Dia, ulitaka kuniharibia hata kochi?” alisema kwa utani, kicheko kikitawala chumba chote.
Walibaki wakitazamana kwa sekunde chache kabla ya Yasri kumsogeza karibu zaidi. “Dia, unajua hata nikikasirika vipi, huwezi kuniacha, eh?”
Shadia alitabasamu, akamtazama Yasri kwa macho ya mahaba. "Hata ukikasirika, bado nakupenda. Na sitakuacha hata uweje."
Yasri alitikisa kichwa huku kicheko kikidumu. "Huyu mwanamke, kweli ni zaidi ya nilichotegemea. Ni zaidi ya nilicho omba kwa Mungu"
" Mmh! Acha nikuandalie chochote ili uwahi kazini " Shadia aliinuka ili aelekee jikoni lakini Yasri alimvuta na kumwambia.
" hapana leo ni siku tofauti Dia, tuna safari "
" ya wapi?"
" Mwanza, tunaenda wote Mwanza " alijibu Yasri Shadia akabaki ameshangaa akimtazama.
SEHEMU YA: 62
" Huna haja ya kushangaa kwa sababu tayari nimefanya maandalizi yote, tunafaa kuwahi" Yasri alimaliza kuongea Shadi akajikuta amekaa kitandani, alimtazama Yasri usoni na kumwambia kwa upole.
" ujue Yasri, nahisi kama vile umesahau hili, mama alisema anakuja wiki hii, kama leo tuna safari inabidi nimwambie asubiri mpaka turudi huku" Yasri ndo alikumbuka kuhusu hilo hatimae, akamkubalia Shadia kwa kichwa.
" Nisamehe, nimejikuta nasahau mambo haraka ila inabidi tutenge siku nzuri zaidi kwa ajili yake mama hawezi kuja kuja tu hapa, bila utaratibu mzuri yule ni mama mkwe wangu kumbuka hilo" alisema Yasri kumwambia Shadi ambae wala hakumpinga.
Shadia alikubali kisha akajiandaa chap, lakini hakuona kama ni busara kwake kuondoka bila kumuaga Sima wala Sharon, afadhali katika nyumba hiyo hao wawili walikuwa wakimkubali zaidi na kumuelewa. Alipomuaga Sharon alimtakia kila la kheri na hakuonekana kuwa na furaha sana kiasi kwamba Shadia alihisi kuna kitu hakipo sawa kwake.
" Sharon haupo sawa na mimi leo ee?" Alihoji Shadia Sharon akaendelea na bize zake huku akiukwepa uso wa Shadia
" hapana Shadia nipo sawa na kila kitu mbona" alijibu Sharon Shadia akamsogelea na kumshika mabegani.
" unahisi ni kweli nilihusika na mama kuacha kazi?" Alihoji Shadia Sharon akamtazama na kumjibu.
" hapana najua hili halihusiani na wewe, lakini haina haja ya sisi kuliongelea hili. Jiandae na safari hata hivyo iitakuwa safari yako ya kwanza na kaka na isitoshe hamjawahi hata kwenda fungate" Shadia alimtazama Sharon usoni akabaki bila neno. Shadia aligeuka kuondoka lakini Sharon alimsimamisha na kumwambia.
" Usijisikie vibaya wifi, eti kwa sababu sina raha, ndio sina raha sina raha sio kwa sababu ya kaka Yasri na mama, sina furaha kwa sababu nimempenda kijana ambae sio wa hadhi yangu, kiasi kwamba hatamani kuwa na mimi, sijui tu najaribu kuuzuia moyo wangu lakini ishakuwa ngumu sana" Sharon alijibu Shadia akamuonea huruma na kumsogelea tena.
" unahisi yeye hakupendi?"
" hapana sina hisia hizo"
" basi jitahidi aelewe nia yako"
" lakini wifi, mimi hapa nilijitengenezea picha ambayo, hakuna mvulana wa hadhi ya chini anaweza kunikaribia, wengi wanakaa mbali na mimi, hata kwake sidhani kama atanikaribia, nahisi kama ananiogopa sana"
" basi wewe mkaribie"
" wifi siwezii, mimi ni mwanamke"
" najua lakini hapo ndo mahali ambapo mapenzi yako yapo"
" wifi mimi hapa daa!! Hata sijui niseme nini? Sina uwezo wa kumtongoza mwanaume"
" najua na sijasema umtongoze, kitu pekee unachotakiwa kufanya wewe ni kumkaribia, muonyeshe kwamba haupo kama anavyokudhania, maana mpaka wakati huu umemfanya ajione yeye ni duni sana hana uwezo wa kukumiliki, kwa hiyo jaribu kujenga urafiki nae tu, lakini hakikisha hazigundui hisia zako kwa haraka, urafiki kama kumuomba kitu ambacho unajua yeye ana uwezo nacho, hata kama unacho mwambie tu naomba u isaidie kitu fulani, ntakurudishia muombe mbele za watu wengi, alafu baadae ondoka nacho kwa kusudi, kisha tafuta wakati akiwa mwenyewe ndo umpatie, kwa sababu wakati huo utapata hata
wakati wa kupiga nae story kidogo, siku nyingine hata unampa kitu chako akushikie yaani hivyo mdogo mdogo, na uanze kumpima namna anavyokutendea, kisha utaamua awe mpenzi wako au laa??" Sharon alimtazama Shadia na kujikuta amemkumbatia
" najua sio rahisi wifi, ila kwa niaba ya moyo wangu ntajitahidi sana" alimaliza kuongea kisha akamuachia, Shadia alimtakia kila kheri kisha akaondoka zake, walau Sharon alikuwa na tabasamu usoni mwake.
Shadia alipomaliza hapo alienda kwa Sima kumuaga, Sima alitabasamu na kumwambia amsubirie kwanza kabla hajarudi chumbani. Sima alizunguma nje ya nyumba na kuchuma majani fulani hivi ambayo aliyafahamu yeye
mwenyewe, kisha akarudi ndani na kutwanga ikiwa mbichi akakoroga na kumpatia Shadia.
" kitu gani hiki?"
" kunywa ni dawa"
" ya nini, nisije kunywa sumu"
" we nae bhana kunywa hiyo ni dawa ya mapenzi, itawafanya nyie wawili mambo yenu yawe bulbul " Shadia alimtazama Sima na kumshangaa.
" we Sima wewe, usipeleke mambo haraka"
" lakini tayari ni.haraka ishakuwa kunywa dawa basi kabla kaka Yasri hajafika" Shadia alikunywa akiwa na mashaka na Sima, sawa ilikuwa chungu ila iliwahi kuisha.
" mambo hayo, sasa basi hakikisha unarudi hapa ukiwa mama kijacho" alisema Sima Shadia akamtazama haraka
" wewe mbuzi" " ndo hivyo"
" yaani umenipa dawa ya uzazi, una uhakika gani kama mimi na Yasri tutafanya chochote, uwiiih " Shadi hakutaka tena kubaki hapo aliondoka akiwa ana laani kitu alichofanyiwa na Sima, Sima alibaki jikoni akimcheka.
Shadia alifika tu chumbani kwake akagongana na Yasri ambae alikuwa anatoka ili kumfata.
" kwani huoni??" Shadia alifoka
" naona lakini sikuwa nakuona, ndo maana macho yangu hayapo sawa" Yasri aliongea kimahaba na kumpelekea Shadia kupata aibu.
Baada ya maandalizi ya muda kidogo safari yao ilianza, Ilikuwa mara ya kwanza kwa Shadia kusafiri safari ya umbali mrefu kiasi hicho. Waliondoka na gari kwa sababu haikuwa rahisi kwa Shadia kusafiri na ndege ilhali hana vielelezo vyovyote kwa haraka, maana wakati huo ndo Yasri alimuweka Abdallah ashughurikie.
Kwenye gari Yasri na Shadia walipata wakati mzuri na wa kutosha kuwa pamoja, japo safari ilichukua muda mrefu lakini walifika salama jijini mwanza. Walifikia hotelini chumba kilikuwa tayari kwa ajili yao, na chumba chao kilikuwa karibu san na chumba cha Ahmed. Ambae aliwapokea baada ya kufika akiwa wa kwanza kabla yao.
Shadia aliitikia salamu yake na Ahmed akatabasamu, Yasri alimtazama namna ambavyo Ahmed alikuwa akimwangalia Shadia akaamua kuvunga tu kwa wakati huo.
Baada ya kupata muda kuoga na kujiweka sawa Yasri na Shadia, Shadia alikuwa na uchovu sana kiasi kwamba alimuomba Yasri amvumilie kwanza yeye anataka kulala, hawezi kuungana nae kwenye masuhala yake ya kazi. Yasri alikubali alifanya kumbusu tu na kumsindikiza kitandani alale kwanza, Shadia alilala na Yasri alitoka kwenda kuongea na Ahmed ambae alikuwa anacheza pool, Ahmed alimkaribisha Yasri acheze nae pia Yasri hakuwa na hiyana alikaribia na kuanza kucheza huku wakiutumia muda huo kuzungumza mambo yao.
Wao wakiwa wanacheza pool katika hotel hiyo hiyo, kando kabisa na eneo walilokuwa kuna
mwanamke alikuwa anaongea na simu, akiwa kavaa miwani mieusi pamoja na kofia ambayo iliuficha uso wake usionekane.
" ondoa shaka mama, kikubwa niko hapa hotelini tayari kila kitu kitaenda sawa, nitahakikisha Shadia na Yasri wanarudi kwa njia tofauti tofauti, mbali kabisa na walivyokuja" alimaliza kuongea huyo mwanamke kisha akakata simu.
" madam chumba chako kipo tayari " ilikuwa sauti ya muhudumu ambae alimkabidhi mwanamke huyo funguo. Mwanamke huyo alivua kofia yake pamoja na miwani akaifanya sura yake kuonekana, hakuwa mwingine bali Farhiya. Ambae alichukua funguo na kuwatazana Yasri na Ahmed walivyokuwa
wakicheza pamoja, kisha akaondoka kuelekea chumbani.
SEHEMU YA: 63
Baada ya mchezo wa muda mrefu hatimae Yasri aliingia chumbani akiwa amebeba chakula maalum kwa ajili.ya mke wake mrembo, Shadia alikuwa bado amelala kiasi gani uchovu, ulikuwa mwingi sana kwake.
" ka mbuzi kadogo kavivu bado kamejikunyata kwenye blanket lake, haya haya bibie amka upate chakula chako sawa" alisema Yasri Shadia akamsikia kwa mbali akaamua kujigeuza vzuri ili alale zaidi.
" madam huwezi kulala bila kula, labda uwe nje ya himaya yangu mimi hapa Yasri Saleh, haya
amka amka amka" Yasri alimvuta Shadia ambae aling'ang'ania blanket.
" jamani Yasri ntakula baadae, kwa sasa niache nilale" Shadia alijigeuza tena
" hapana haoa huwezi kulala mpaka ule sawa madam boss" Yasri alimvuta na kumnyanyua mikononi mwake Shadia ilibidi atulie.
" umekuwa mwembamba kama karatasi, haiwezekani uwe mwepesi hivi" alisema Yasri Shadia akamshangaa
" kiaje nimekuwa mwepesi, kwani kuna vitu sijala.muda mrefu?" Shadia alihoji
" ndio na vitu vyenyewe, ni bao langu maalum" Shadia alipata aibu
" Yasri nahisi njaa" aliuficha uso wake kwenye kifua cha Yasri ambae alienda nae hadi mezani wakaanza kula. Wakati wanakula Shadia
alitumia muda mrefu sana kumtazama Yasri, akakumbuka tu ni namna ganj alipata tabu kutambua uzuri wa huyu kijana aliekaa karibu nae, hapo mwanzo alimuona kama jambazi tu kutokana na muonekano wake wa awali, lakini.kwa ndani kumbe Yasri ana moyo mlaini sana na mzuri kweli kweli.
Aliikumbuka ile ndoto aliyowahi kuiota hapo zamani alipokuwa ndani ya chumba chake cha mwanga hafifu, alidhani ni ndoto tu za Alinacha kumbe ni kweli Mungu alipanga aje akutane na mwanaume shujaa kama Yasri ambae amempenda sana pamoja na kumlinda bila malipo yoyote yale.
" hapana Yasri mimi sio laaana, bali mimi ni nuru"
" ndio wewe ni nuru" Yasri alijibu moja kwa moja bila hata kuuliza Shadia kawaza nini?
Aliendelea kumlisha chakula chake huku akimbembeleza na kumdekeza kama mtoto mdogo. Baada ya chakula Yasri alimwambia Shadia hawatakuwa na muda mwingi sana mwanza kwa hiyo anatamani wakaogelee.
" Yasri mi sijui kuogelea na sijawahi"
" utajua kupitia mimi kwa hiyo twende" " Yasri lakini ni usiku sasa"
" mambo mazuri kwa watu wanaopendana huwa yanatokea zaidi usiku" Shadia alikubali hata hivyo hakuwa na haki ya kupinga hilo.
Waliongozana moja kwa moja hadi kwenye bwawa la kuogelea. Kwenye eneo hilo walikuwa wao wawili tu bila uwepo wa mtu mwingine, Yasri alimtoa Shadia nguo ya juu na
akabaki na bikini kitu ambacho kilimpa wasiwasi zaidi.
" Yasri mtu akija huku?"
" mtu huyo na mimi hakuna mtu yoyote mwingine ambae atakuja huku" alijibu Yasri na kumsukuma Shadi kwenye maji, Shadia alikuwa muoga kiasi kwamba alitamani kufa maana hakujua afanye nini wala nini? Hadi wakati ambao Yasri alijitipia ndani ya maji na kumshika Shadia akaanza kuogelea nae.
" Yasri naogopa kunywa vibaba"
" zoea kidogo tu jamani, usiwe hivyo " alisema Yasri na wakarndelea kuogelea, japo mwanzo Shadia alikuwa na uwoga lakini baada ya muda alizoea kidogo aliyazoea maji, ila hakujua
kuogelea isipokuwa tu ali enjoy sana kuwa na Yasri hapo.
Wao wakiwa bize wanaogelea wakiamini hakuna mtu hata mmoja aliekuwa akiwaona, Ahmed alikuwa amesimama kwa mbali akiwatazama hao wawili huku akinywa kahawa taratibu, macho yake yalikuwa kwa Shadi alitamani sana kumpata huyo mwanamke mrembo, lakini hakuwa na haki hiyo
" hapana nitajaribu bahati yangu" alijisemea kisha akaenda kulala.
Baada ya kuogelea kwa muda mrefu sana hatimae Yasri na Shadia walirudi chumbani ambapo, Yasri alidai ana hamu sana na Shadia, hata hivyo Shadia alihisi aibu kidogo kwa sababu walikuwa hawajafanya chochote.
" najua haupo kwenye siku zako, huwezi kuniongopea leo" Shadia alitabasamu na kumwambia.
" napata wapi ujasiri wa kukukataa my Mr " Shadia alimkumbatia Yasri na Yasri qkaanza kumbusu kwa hamu sana. Na taratibu mno kiasi kwamba Shadia alijihisi utulivu mkubwa ndani ya busu lake, hakuishia hapo alimvuta karibu yake zaidi na zaidi huku akipapasa sehemu zaie nyeti kama makalio yake pamoja na matiti, haswa nywele zake zilipata kazi sana siku hiyo.
Shadia alikuwa msikivu akimfata Yasri ambavyo alikuwa akimpeleka na yeye anaenda hakuwa mjuzi sana wa mamno wakati huo. Kila kitu kilifata hatua zake, hadi wakati ambao wote walikuwa wamemaliza na wameridhika na tendo mahususi kwa niaba yao.
Majira ya asubuhi Shadia alichelewa sana kuamka, alizoea kuamka mapema na kumuandalia Yasri kiamsha kinywa lakini siku hiyo mambo yalikuwa kinyume, aliamka na kusikia harufu nzuri ya supu ikinukia kwenye pua zake.
Shadia alisafirisha macho yake hadi pale ambapo harufu ilitokea kwa wingi, ndo akagundua kwamba Yasri alikuwa kamwandalia supu asubuhi asubuhi. Shadia alitabasamu na kuinuka kitandani kisha akatembea kuisogelea meza.
" My Special woman, good morning " Shadia alitabasamu baada ya kuokota kikaratasi kidogo kilichokuwa mezani na supu, alikunja na kumfikiria Yasri namna gani alikuwa mzuri na
maalum kwake. Akiwa bado anamuwaza Yasri, aliona karatasi nyingine kando yake.
" Sorry imebidi niondoke mapema sana kwa sababu ya kazi, kila kitu nimekuandalia hapo, na kama kuna kitu utakosa basi mjulishe muhudumu yoyote au usisite kunipigia simu" Shadia alisoma ujumbe huo akiwa na hisia mchanganyiko hakuelewa ikiwa alifaa kufurahia au la?.
Alioga kisha akarejea chumbani na kupata supu kama ambavyo Yasri alimtaka afanye, baada ya hapo alitoka ndani ya chumba. Akiwa anatembea mdogo mdogo aligongana na msichana ambae kidogo mavazi yake yalitia shaka, sura yake haikuwa ngeni kwa Shadia
" lakini yeye ni nani sasa?" Alijiuliza Shadia na mwisho alipotezea na kuendelea na safari yake,
bila kujua mtu huyo aliepishna nae alikuwa Farhiya.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote