Siku zote mapenzi huwa ni hisia na kila ndege hutua kwenye mti aupendao.
Romeo kijana mtanashati anakutana na Mariam binti Machachari , mariamu anatokea kumzomea sana Romeo na kufika hatua ya kwenda kwake mara kwa mara na watu wote mtaani walijua Mariam na Romeo wana uhusiano na Mariam alithibitisha hivyo kwa baadhi ya watu. Mariamu anafanya awezavyo ili awe na mahusiano na Romeo na kweli alifanikiwa kulala nae mara kadhaa lakini Romeo hakuweka moyoni alichukuliwa kama rafiki wa kusaidiana kwa kila jambo .
Romeo anapigana kauli na mabinti watatu ambao ni jirani zake kwa kufungulia mziki kwa sauti kubwa, Romeo anawafuata kuwaambia lakini wanamtukana na kuzidi kufungulia sauti kubwa Romeo anapiha simu polisi Roxana, Vanessa na Tecla wanakuja kukamatwa na kulazwa ndani.
Baada ya siku mbili wazazi wa Roxana wanaenda kituoni kumtoa binti yao kumba Romeo na baba yake Roxana wanafahamiana Roxana anatolewa na kurudi nyumbani . Taratibu Romeo akaanza kuvutiwa na roxa akaona kwani shida nini akaomba msamaha kwa kilichotokea kisha akaomba urafiki baada ya hapo akaandaa mazingira ya Roxana kumpenda lakini kila alivyokuwa anatengeneza mariam alijaribu kuharibu . Badae akaamua kuwa rafiki kwa Roxana na kuanza kujifunza kumpenda mariamu . Lakini moyo uligoma kabisa roxa alichukua nafasi kubwa sana kwenye moyo wake na wakati huo roxa alianza kumpenda ila hakujua itakuwaje ili wawe pamoja.
Anitha mpenzi wa zamani wa Romeo anakuja na kuchafua hali ya hewa Mariam anaamua kuachia ngazi na Roxana anakaa pembeni akiangalia mchezo unavyoenda . Badae Roxana anaona hawezi kuficha hisia zake kwa Romeo na Romeo ilikuwa hivyo hivyo lakini Anitha alikuwa mkali sana aligongana na Roxana kila siku . Tecla na Vanessa wanamshauri Roxana atafute mwanaume wa kuwa nae nae anafanya hivyo. Romeo anaumia kumuona Roxana akiwa na mwanaume mwingine na wakati huo Roxana havutiwi kabisa na mpenzi mpya sababu hayupo romantinc kabisa
ROXANA ( NI WEWE TU)❤️🔥1
MTUNZI SMILE SHINE
Ulikuwa ni Mtaa wa kilima hewa Ni mtaa uliochangamka sana hasa nyakati za jioni kila mtu alikuwa bize wakifanya biashara kando kando ya barabara pia kulikuwa na migahawa mingi sana ya chakula na kila mfanya biashara alikuwa akipenda kazi yake alifanya kila wawezavyo kuhakikisha anavutia wateja ili siku nyingine waweze kurudi.
Kijana Romeo alikuwa mgeni maeneo hayo baada ya kuhamia kikazi kutoka mkoa wa Kilimanjaro , Romeo alikuwa muajiriwa wa jeshi la polisi. Mara nyingi baada ya kutoka kazini alienda mitaani kutembea na kutafuta chakula migahawa kwakuwa hakuna mtu aliyefahamika nae alikuwa akienda kula na kurudi nyumbani kwake.
Siku moja Romeo alienda kwenye mgahawa mmoja kwaajili ya kujipatia chakula Cha jioni. Wakati anakula alitokea dada mmoja ambaye alionekana kuongea sana pia alionekana kuongea na kila mtu pale ndani ya mgahawa.
Yule msichana alipomuona Romeo alienda na kukaa kwenye meza aliyokuwa kakaa kisha akamsalimia
" Mambo
" Safi. Alijibu Romeo huku akimuangalia
" Wewe Ni mgeni hapa? Yule dada aliuliza
" Kwani naonekana Kama mgeni?
" Ndio kwasababu siku fahamu , ungekuwa mwenyeji lazima ningekuwa nakufahamua au mwenzangu unanifahamu?
Romeo alitingisha kichwa Kisha akasema
" Hapana, Mimi Ni mgeni hapa hakuna ninaemfahamu.
" Sasa ulitaka kukataa, mimi nafahamu watu wote wanaoishi mtaa huu na mitaa ya jirani pia wageni nawatambua kama nilivyo kutambua wewe, naitwa mariamu Al maarufu Mamu sijui mwenzangu unaitwa nani?
" Nashukuru kukufahamu mariamu, Mimi naitwa Romeo
" Nimefurahi kukufahamu , pia Leo imekuwa Kama bahati kuonana na wewe acha nikupe mualiko. Romeo alimshangaa Mariam maana ilikuwa Ni Mara ya kwanza kukutana lakini alikuwa mchangamfu Sana. Mariam alitoa kadi na kumpatia
" Kadi ya birthday yangu. Itafanyika mwezi ujao natoa kadi mapema kwasababu ya michango tafadhali naomba uhudhulie kama ukipata muda .
" Sawa
" Kwa Leo langu Ni Hilo tu Ila naimani tutaendelea kuonana na kufahamiana zaidi.
Baada ya hapo mariamu aliondoka na kwenda kuendelea kusambaza kadi za mualiko , Romeo akaendelea kula chakula chake alipomaliza aliondoka.
Kesho yake baada ya kutoka kazini Romeo alikuwa kapumzika ndani kwake akiangalia movie, Mara akasikia mlango una gongwa.
" Ni Nani huyo ? Alijiuliza maana hakutegemea kupata mgeni kwani hakuwa na mazowea na mtu yoyote. Alinyanyuka na kwenda kifungua mlango , alishituka baada ya kumuona mariamu akiwa kasimama mbele ya mlango wake huku akitabasamu.
" Wewe umejuaje Kama naishi hapa?
" Sasa Hilo Ni swali gani ? Mwenzio Mimi najua kila mtu anapoishi. Romeo akawa kasimama mlangoni anamuangalia
" Leo nimetembea Sana unaweza ukanipisha niingie angalau nipumzike kidogo unywe na maji ya kunywa. Romeo alimpisha akaingia ndani na kwenda kukaa kwenye Kochi huku akiendelea kukagua ndani .
" Unaishi mwenyewe hapa ndani?
" Ndio
" Hongera umejitahidi. Mamu alikuwa muongeaji Sana aliuliza maswali mengi na Romeo alikuwa akijibu. Lakini haikuwa kero kwa Romeo alikuwa anafurahia maana aliona kama anamchangamsha.
Walikubaliana kuwa marafiki na mamu alikuwa akimtembelea mara kwa mara wakiwa wanapiga story na kuangalia movies pamoja na walipochukua walitoka pamoja kwenda kuangalia mazingira huko nje.
Siku moja Mamu alienda nyumbani kwa Romeo.
" Natumai Leo utakuwa na nafasi nimekuja kukuchukua nikakutembeze ili ujue mitaa inayotuzunguka . Kwakuwa Romeo hakuwa na kazi ya kufanya aliamua kukubali. Walitoka na kuzunguka maeneo mengi , alipitishwa kila aina ya vichochoro . Baada ya kumaliza matembezi Romeo alimuomba Mamu waende mgahawani wakapate chakula Kisha yeye aende nyumbani kupumzika. Walipomaliza kula waliachana Romeo alishuka njia ya Kurudi nyumbani kwake na Mariam alikuwa akiendelea kupiga soga pale mgahawani.
" Tunakuomba Mariam umejiopolea .
" Macho yameshaanza kuwatoka sasa nimuone mtu anammendea atajuta kuishia huu mtaa maana wasichana wa huu mtaa nawajua na Shobo zao.
Romeo alipofika karibu na nyumbani kwake alisikia mziki ukidunda kwa sauti ya juu na mama mmoja akawa analalamika
" Kumekucha muda wa kupumzika wengine ndio wanaanza heka heka zao hebu kuweni na huruma mtupumzishe jamani .
Romeo alimsalimia yule mama kisha akampita akaingia ndani kwake. Alikaa ndani kwake lakini hakuwa na utulivu kutokana na ule mdundo wa muziki ilimbidi atoke alimkuta yule mama akiwa bado kasimama nje huku akiwa kashika kiuno.
" Samahani kwani hapa Kuna sherehe?
" Sherehe wapi baba hawa mabinti hawana adabu tumeongea sana kuhusu kufungulia mziki kwa sauti ya juu lakini hawaelewi sijui hata tufanye nini tunakosa utulivu wengine wamelaza watoto humo ndani .
" Huu mziki Ni mkubwa Sana watu tunashindwa kupumzika .....
Alitoka mama mwingine wa makamo akasema
" Afadhali uongee wewe baba Hawa mabinti hawasikii, hapa hakuna sherehe yoyote Ila uchizi ukiwapanda huwa hakuna kusikilizana redio inaimba na wao wanapiga kelele.
Romeo alisogea karibu na ule mlango aligonga kwa muda bila kufunguliwa ndipo alipoamua kufungua mlango mpaka mwisho nae akasimama Kati Kati ya mlango akiwaangalia wanavyocheza huku na wao wakifuatisha kuimba
Walikuwa ni mabinti watatu walikuwa wamevalia nguo fupi walicheza mziki huku wakiwa wameshika grass za vinywaji mkononi. Vanessa alikuwa wakwanza kumuona Romeo, alimfuata huku Tecla alienda kuzima radio kisha Tecla alimfuata Vanessa pale mlangoni
" Kaka vipi mbona unavamia ndani kwaa watu Tena unaingia ndani bila kupiga hodi? Tecla aliuliza
" Nimepiga Sana hodi lakini hamkuweza kusikia kwasababu ya kelele za muziki.
" Kwahiyo ndio ukaamua kujiingia Kama chooni? Aliuliza Roxana
" Nashangaa je ungetukuta tupo uchi ungefanya Nini?
Mabinti watatu walimchangia kwa kumuuliza maswali mengi na kumsema kuwa Ni kijana asiekuwa na adabu.
" Ok nimekosea , nisameheni Ila naomba mpunguze kelele na sauti ya radio watu tunataka kupumzika. Roxana na wenzake waliangaliana na kuanza kucheka
" Kwani huyu mtu katoka wapi? Tecla aliuliza
" Sijui ndio kwanza tunamuona leo. Wenzake walijibu
" Kaka kila mtu na maisha yake hivyo tusipangiane maisha.
" Roxana alienda washa radio na kuweka sauti ya juu zaidi. Romeo aliona hiyo Ni dharau aliingia na kwenda kuchomoa nyaya Kisha akataka kutoka . Wakina Vanessa walianza kumshambulia kwa maneno ya kashfa.
" Wewe Kaka Kuna Jambo unalitaka kutoka kwetu lakini bahati mbaya hakuba ambae amevutiwa na wewe hapa.
" Nashangaa anavyotushobokea .
Rimeo alichukizwa na maneno ya wake mabinti lakini hakutaka kujibishana nao alitoka huku akiwa anapiga simu sehemu. Wale mabinti watatu walivamia mlango alafu waliendelea kucheza muziki , baada ya dakika 20 mlango uligongwa , safari hii uligongwa kwa fujo. Roxana alizima redio alafu akasema
" Huyu atatuzowea twendeni kukamchambe mpaka apunguze kiherehere. Wote watatu Walienda mlangoni walipofungua walishituka baada ya kuwaona wanaume wawili wakiwa wamevalia sale za Police na Romeo akiwa kasimama nyuma ya wale polisi
ROXANA ( NI WEWE TU) ❤️🔥 2
MTUNZI SMILE SHINE
Wale mabinti watatu walikuwa kwenye mshangao mkubwa maana hawakutegemea kama Romeo angewauzia police.
" Wewe Kaka umeenda kutuletea polisi....
" Nyamaza wewe ,wote tokeni nje haraka. Alisema polisi mmoja
" Kwani tumefanyia nini? Roxana aliuliza.
" Hamjui kosa alilofanya?
" Basi naomba nichukue simu niwapigie wazazi wangu. Alisema Roxana
" Hakuna muda wa kupiga simu Afande wachukue mkawapumzisheni angalau na sisi tupumzike .
" Sawa mkuu.
Roxana na wenzake Walichukuliwa wakapandishwa kwenye gari ya polisi na kwenda kuwekwa mahabusu. Roxana alichukizwa Sana na kile kitendo Cha wao kuwekwa ndani bila kisa.
" Huu ni uonevu kwani tumefanyia nini kibaya mpaka mtuweke ndani?
" Binti tulia. Alisema afande
" Lakini Nina haki ya kuhoji ili nijue kisa langu Ni lipi. Roxana alijaribu kuongea lakini hakuna Askari aliyemsikiliza ikambidi aende kukaa walipokaa wenzake.
" Kwahiyo Yule mpuuzi anatumia cheo chake kwa kuonea watu wasio kuwa na hatia.
"Roxana nyamaza Mimi hapa nilipo nimechanganyikiwa sijui hata tutatokaje hapa ndani.
" Usijali nikifanikwa kuwasiliana na wazazi wangu kesho tutatoka hatuna kosa kubwa la kutufanya tufungiwe humu ndani sehemu yenyewe chafu. Roxana aliamini hivyo kwasababu yeye Ni binti wa pekee wa mfanyabiashara maarufu Sana na kwao kunapesa ya kutosha Ila hakuvutiwa na maisha ya kufungiwa fungiwa alitamani kuwa huru. Baada ya kumaliza chuo aliungana na wenzie wakapangisha apartment wakaishia pamoja huku wakiwa wanafanya kazi kwenye duka lako la mikate, keki na pizza. Wazazi wa Roxana hawakupenda binti yao kuondoka nyumbani hasa baba yake lakini aliweza kuwashawishi na wao walimkubalia na kumpa mtaji kwaajili ya biashara.
Usiku ule ulipita huku wakiwa wanahangaika hawakupata usingizi maana walikuwa wanang'atwa sana na mbu.
Kulipokucha Roxana alijiangalia mwili wake uliojaa vipele kwaajili ya kungatwa na mbu.
" Huu ni upuuzi gani, ona miili yetu ilivyoharibika. Roxana aliongea kwa hasira huku akinyanyuka na kusogelea mlango wa mahabusu na kuugionga kwa nguvu . Askari mmoja alienda na kuuliza
" Unashida gani mpaka ugonge Kama kichaa?
" Naomba simu nataka kuwapa taarifa wazazi wangu kuwa nipo hapa ndugu zetu wanatakiwa kujua kuwa tupo hapa kama ikiwezekana waje kuziweka dhamana.
Yule Askari alisita kidogo Kisha akasema
" Subiri. Akaondoka baada ya dakika chache alikuja Romeo akauliza
" Ni Nani anahitaji simu?
" Mimi. Alijibu Roxana
" Kumbe na wewe una wazazi? Alisema Romeo na Roxana akajibu huku akitoa tabasamu
" Hapana nilishushwa kutoka mbinguni.
Alijibu Roxana kwa dharau, Romeo alimuangalia alafu akatoa tabasamu la kulazimisha.
" Sikujua Kama wewe Ni jeuri kiasi hicho
" Huo Ni mtazamo wako.... Roxana akitaka kuendelea kuongea Vanessa akamshika mkono na kumsihi anyamaze asijibishane nae.
" Roxana shusha jazba tunatakiwa kunyenyekea ili tutoke hapa. Kabla Roxana hajajibu Romeo akafungua mlango wa mahabusu huku akisema
" Nyie wawili tokeni wewe ulieshushwa kutoka mbinguni utaendelea kubaki. Vanessa na Tecla walitoka haraka na Roxana alirudi nyuma huku akimuangalia Romeo kwa hasira.
" Samahani tunaomba umsamehe Roxana alikujibu vibaya kwaajili ya hasira. Vanessa na Tecla walimtetea rafiki yao.
" Na nyie bado mna hamu ya kuendelea kubaki ?
" Hapana. Walijibu haraka.
" Haya tokeni kachukueni vitu vyenu.
Roxana alienda mpaka mwisho wa ukuta akakaa chini , hakuwa na wasiwasi maana alijua taarifa zitawafikia wazazi wake kupitia wakina Vanessa.
Vanessa na Tecla walitoka nje ya kituo Cha polisi wakipiga simu kwa mama yake Roxana. Wakampa taarifa za Roxana kuwa kukamatwa yupo kituoni
Baada ya mama Roxana kupata hizo taarifa alishituka Sana , alimfuata mume wake sebleni akamwambia.
" Baba Roxana mtoto kakamatwa na polisi .....
" Nini, kwasababu gani?
" Sijui tutaenda kujulia huko huko nyanyuka twende.
" Lakini Nina kikao ......
" Mume wangu ahirisha hicho kikao binti yetu Ni muhimu na kumbuka anahitaji msaada wetu .
" Lakini haya yote yanatokea kwasababu yako umemdekeza Sana Roxana , uliruhusu aende kuishi nje ya nyumbani angekuwa hapa Wala isingetokea hii shida.
" Huu sio muda wa kulaumiana mume wangu, mpigie simu mwanasheria mwambie tukutane kituoni.
" Aaaah achana na mwanasheria kutakuwa hakuna tatizo kubwa atakuwa kafanya fujo sehemu au kagombana na wenzie kwa Mambo ya kijinga.
ROXANA (NI WEWE TU)❤️🔥3
MTUNZI SMILE SHINE
Wazazi wa Roxana walifika kituo Cha polisi , Romeo alikuwa maeneo ya mapokezi alipomuina bwana Paul walimsalimia kwa uchangamfu maana Ni mtu wanaemfahamu.
" Karibu Sana mzee.
" Asante.
" Naona leo umetutembelea Kuna tatizo mzee wangu?
" Binti yangu yupo hapa nasikia kakamatwa na kuwekwa ndani tangia Jana jioni.
" Anaitwa Nani ?
" Roxana. Romeo alishituka kidogo na kuuliza.
" Roxana ni binti yako?
" Ndio.
" Sawa haina shida , ilitokea kutokuelewana kidogo tukawa tumewakamata Ila ataachiwa. Afande nenda kamtoe yule binti alieletwa Jana.
" Sawa afande.
Afande akienda kumfungulia muda ule ule Roxana alitoka akiwa kavaa kikatula kifupi kilichoocha mapaja yake wazi na top iliyoachwa tumbo wazi alipo wakina wazazi wake akasnza kushusha top ili kuziba tumbo lake.
Baba yake alimuangalia kwa hasira jinsi alivyokuwa anaenda kuchukua vitu vyake Kisha akasogea pale aliposimama Romeo na baba yake na kusalimia
" Shikamoo baba. Baba yake hakuitikia Ile salamu alimwambia
" Nenda haraka kwenye gari. Roxana aliondoka akaelekea ilipo gari ya baba yake.
" Asante Sana kijana wangu Yani huyu mtoto ananisumbua Sana na haya yote yanasababishwa na mama yake anamdekeza Sana.
" Usijali mzee wangu ni ujana unamsumbua atabadilika.
Romeo aliachana na mr paul.
Roxana alienda nyumbani kwao na wazazi wake baba yake akawa anamsema .
" Wewe mtoto nimekuchoka na hayo Mambo yako ya ajabu , umetaka kuondoka nyumbani ili ukafanye huu upumbavu wako Ina vinguo unavyovaa hivi huoni aibu mbona unataka kuniaibisha.
" Mume wangu Basi muache mtoto haya Ni Mambo madogo yanarekebishika nitaongea nae Kama mama.
" Umeona unavyotetea ujinga.
Baba yake aliondoka kwa hasira na kuwaacha mama na mwanae waongee.
" Ila Roxana mbona hutaki kutusikiliza sisi wazazi wako?
" Haya Mambo ya kunichunga chunga na kuninyima Uhuru ndio siyataki kabisa Mimi nimeshakuwa mkubwa sipendi mnavyonifanya Kama mtoto wa miaka mitano.
Roxana aliongea kwa hasira kisha akaenda chumbani kwake . Kesho yake kulipokucha
Roxana alirudi sehemu aliyokuwa akiishi na wenzake.
Siku iliyofuata Romeo alikuwa anatoka nyumbani kwake akawa anaelekea kwenye vibanda vya mama ntilie kwenda kupata chakula Cha jioni na wakati huo Mariam alimpigia simu kuwa anamsubiri huko. Romeo alipokuwa anapita karibu na mlango wa kina Roxana alishituka baada ya kumwagiwa maji ya ukoko. Aliemwagia alikuwa ni Roxana, Ilionekana kuwa Ni bahati mbaya maana nae Roxana alionekana kushituka mno, Romeo alisimama akawa anamuangalia moja kwa moja Kama vile anatafakari kitu Cha kufanya.
Roxana alitamani kuomba msamaha lakini akaona Kama atajishusha Sana maana Romeo Ni hasimu wake. Wote wakawa wamesimama wanaangaliana ikabidi Roxana aseme.
" Imetokea Kama ajali tu sikukusudia. Alivyosema hivyo akaingia ndani na kubamiza mlango Kisha akaenda kuchungulia dirishani Romeo akawa anajikunguta ikabidi ageuze na Kurudi ndani kwake na kwenda kujisafisha .
Romeo akiwa anaoga mlango wake ulikuwa unagongwa Sana mpaka baadhi ya majirani walitoka kuchungulia wakiwemo wakina Roxana walijua anaegonga mlangoni kwao.
Mara Romeo alitoka bafuni akamkuta mariamu mlangoni.
" muda wote huo nakungoja kumbe ulikuwa bado haujaoga.
" Nilipata ajali kidogo. Walifungua mpango wakaingia ndani .
Mariam alionekana kumtamani sana Romeo na kutamani kuwa mwanaume wake , kuna baadhi ya vitendo alikuwa anafanya kwaajili ya kumfanya Romeo amtamani na kweli adhima yake ilifanikiwa akajikuta amelala na Romeo.
Mariam alifurahi sana alijua kufanya hilo tendo na Romeo ni tiketi tosha ya kuanzisha safari ya mapenzi yao.
Roxana akawauliza wenzake
" Huyu Mariam atakuwa anatembea na huyu polisi?
" Itakuwa maana mariamu Kama unavyomjua kila mwanaume anaemuona anamfaa yeye anapita nae.
" Mmmh haya.
Ukaribu wa Mariam na Romeo ulifanya watu wengi wahisi Kama Ni wapenzi maana kila jioni walikuwa wanatoka pamoja na kwenda sehemu mbali mbali pia watu walipomuuliza mariamu aliwajibu kuwa Ni mwanaume wake Tena aliwatisha wasichana wa huo mtaa.
" Jamani, jamani nawaambia kabisa Romeo Ni mwanaume wangu Sasa nyie jichanganyeni tu nitakuja kumtoa pua mtoto wa mtu.
Siku moja jioni Roxana alikuwa katoka kwenye mizunguko yake akawa anafagia fagia nje ya mlango wao Mara akashangaa kuona miguu ya mtu umesimama mbele yake ikabidi aache kufagia amuangalie.
" Bwana afande mbona mlangoni kwetu Tena au Kuna mtu umekuja kumkamata? Roxana alimuuliza Romeo ikabidi Romeo aachie tabasamu.
" Roxana najua kukutana kwetu kwa Mara ya kwanza hakukuwa kuzuri pia najua unanichukia Sana Ila Mimi sio mtu baya kwako au kwenu nilikuwa naomba tusiwekeane vinyongo sisi ni binadamu, majirani tunatakiwa kusameheana pale tunapokoseana.
" Lakini unakumbuka uliniweka ndani?
" Nakumbuka vizuri Sana ndio maana nipo hapa kwaajili ya kumaliza tofauti zetu.
Roxana alifikiria kidogo Kisha akasema
" Sawa kwakuwa umeomba msamaha Sina budi kukusamehe.
" Nashukuru Sana. Naitwa Romeo. Romeo alijitambulisha huku akimpa mkono Roxana, Roxana aliachia tabasamu Kisha nae akajitambulisha
" Roxana.
" Jina zuri Kama wewe mwenyewe ulivyo, Roxa mbali ya kuwa majirani tunaweza tunaweza kuwa Marafiki?
Roxana alitulia kwa muda huku akimuangalia usoni baada ya dakika kadhaa alisema.
" Bila Shaka unakaribishwa.
" Asante. Basi baada ya kukubaliana kuwa Marafiki Romeo aliomba siku moja watoke pamoja kwaajili ya urafiki wao. Kabla Roxana hajajibu. Maryam alifika na kusimama katikati yao wote wawili walimtolea macho maana ilikuwa ghafla yeye kufika pale.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote