ROWAN (Mine Alone)

book cover og

Utangulizi

ROWAN (mine alone )
Kutana na Binti Vera, Binti Mdogo anayepitia Maisha ya kudhalilika kwaajili ya mapenzi…
Vera ni Binti anayetoka kwenye family yenye Pesa nyingi sana lakini kwenye mapenzi ni Kama alifeli pakubwa sana, ukiachana na mapenzi urafiki pia unamtupa mkono.
Baada ya maangaiko ya hapa na pale Vera anapata rafiki wa kiume ambayo ni Rowan, kukutana na Rowan sio solution kwa Vera kwani anashindwa kumaliza elimu yake ya chuo huu ya skendo kubwa anayopata.
JE NI SKENDO GANI ? Tukutane ndani ndani Uko tukaone mambo ……….💃🏻💃🏻

ROWAN (Mine alone)

MTUNZI: PATRICIA da mtunzi
Sehemu ya: 01
ANZA NAYO....

Niite Vee, jina la kifupisho cha jina langu la Vera, Vera ndio jina langu halisi nililopewa na wazazi wangu, nimezaliwa miaka kadhaa hapo ya 2000.
Mimi ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto watatu uku mimi ndio nikiwa wakike tu.
Niseme kuwa am blessed, yaani ikija kwenye upande wa kubarikiwa mimi nilikuwa nimebarikiwa Aswa, ukianzia kwenye akili kichwani walahi niko vizuri darasani, ukija kwenye umbo Mashallah niko vizuri, ukirudi kwenye sura hapa nisidanganye, sikuwa na sura nzuri sana ila mafuta mazuri na kujing'alisha kulinusaidia sana.
Nimezaliwa kwenye familia yenye pesa sana hivyo ghalama za skin care ni niliweza kuzimudu ipasavyo.
Niwanafunzi wa mwaka wa pili hapa chuoni UDSM, Nina marafiki wa kutosha jamani, yaani mimi kwa marafiki tu niseme kuwa niko vizuri, Vee mimi ni mtu ambaye nina muamimi mtu kirahisi sana, ukija kuchanganya na ucheshi ndio kabisa.
Katika maisha yangu nimepita kwenye mikono ya hovyo sana juu ya mapenzi, naweza kusema kuwa mapenzi sio vitu vyangu kabisa.
Nimebarikiwa kila kona ila sio mapenzi, kwa kumbukumbu yangu ya haraka haraka, nakumbuka nilianza mahusiano nikiwa kidato cha nne.
Mahusiano yangu ya kwanza hayakwenda sawa kutokana na kujifanya mtoto zaidi, nilikua sijui jinsi ya kuwa romantic na ukija kwenye masuala ya sex ndio unanivuluga Kabisa, sio kwamba nilikuwa sijui hapana, kujua najua ila aibu ilikuwa ni ya kiwango cha rami.
Mpaka nakuja kuingia chuoni,nilishaachana na wanaume kama wanne hivi, na wote nimeachana nao kwaajili tu ya kukataa sex, nilikuwa najiona mdogo sana hivyo niliamini kuwa nakosea na hivyo sikudumu kwenye mahusiano.
Nilipoingia chuoni mwaka wa kwanza, niliweza kukutana na kijana Mike, ni kijana ambaye nilimpenda kuliko maelezo.
Ninaposema kuwa nilimpenda Mike muwe mnanielewa jamani, Mike ni mvulana ambaye alikuwa anatoka kwenye maisha duni sana, lakini kutokana na kumpenda kwangu, nilihakikisha kuwa shida ndogo ndogo namsaidia.
Mike ndio mwanaume ambaye nilijipa asilimia Mia moja kuwa atakuja kuwa mume wangu wa ndoa, nilihakikisha kuwa najenga mahusino Imara sana na Mike.
Uaminifu wangu juu ya Mike ulikuwa ni wa hali ya juu ambapo sikuona hasara mimi kumuachia Mike mwili wangu ili achezee vyovyote awezavyo.
Katika moja na mbili, nilikuja kugundua kuwa Mike ni mkaka wa hovyo sana, kwanza uwa ana warekodi video wanawake wote ambao atabahatika kulala nao, lakini cha pili, Mike anatumia uzuri wake kuwadatisha wanawake wenye pesa, ili tu aweze kutumia pesa zao, na naweza nikasema kuwa Mike ni mzuri kitandani walahi na alituweza wanawake wengi.
Katika wanawake ambao Mike amefanikiwa kulala nao na kuwarekod na mimi nimo, na anatumia video yangu kuendelea kunitesa na kula pesa zangu.
Ouk ouk my zangu, tuachane na hizo brabrah za Mike njooni uku niwape fusho la kijana ROWAN.

SONGA NAYO.....

Ikiwa ni siku ya alhamisi, nikiwa darasani na mashoga zangu, tunapiga zetu picha uku na uku, gafla mkaka aliyejulikana kama Rowan alikuja na kusimama pembeni yangu na kuonekana kutaka kuzungumza kitu.
"Vee"
ROWAN aliita jina langu kwa sauti nzito kabisa kisha akakaa kimya akisubili niitike, nilimuangalia kwa muda kisha nikamuuliza.
"Unataka nini nawe, ata hivyo unaniziba si unaona napiga picha "
"ROWAN alivua kot lake ambalo alivaa pasi na kufunga zipu kisha akanipatia na kusema, jistili na hili kwanza"
Ila wanawake jamani, dharau na jeuri zitatuua na kutupeleka pabaya kabisa, nilikataa koti lake kata kata na kwa dharau nikainuka na kutoka eneo ilo.
Kitendo cha mimi kuinuka, kila mtu alibaki akininyooshea vidole na wengine kucheka, mwisho shoga angu akaniuliza.
"Kwani unaganya fashion show ya period mwenzetu au ? Maana inazidi kukuchafua lakini umo tu "
Kwa jazba na wasiwasi mkubwa, nikageuza mkono wangu nyuma na kuangalia, woiiiiih 🥺 nilijua kudhalilika jamani, yaani damu kama zote na vile nilikuwa nimevaa gauni nyeupe ndio kabisa.
Darasa zima lilinicheka isipokuwa ROWAN, yaani imagine, mpaka watu ambao nawaita marafiki wamebaki wakinicheka badala ya kunisaidia.
Kwa aibu nilitoka nje mbio na kukimbilia chooni, nilikaa uko kwa muda, nilivua gauni yangu na kulisafisha lakini alikutakata kabisa bado liliacha alama kubwa sana, na ni kama niliongezea hivi.
"Vee "
Ilisikia sauti nzito ya kiume ikiitilia jina langu kutoka nje ya choo.
"We nani ??" Niliuliza kwa sauti ya wasiwasi sana.
"ROWAN hapa, aaah nimekuletea pad kwaajili ya kujistili, lakini pia na koti ili "
Nyie, Rowan ni heaven sent walahi, yaani sijui nisemeje lakini alinisaidia sana, basi nilisogea mpaka mlangoni nikatoa mkono nje na kuchukua vitu kutoka kwa Rowan mwisho nikajistili na kutoka nje.
"Bado uko hapa ??" Nilimuuliza Rowan ambaye nilimkuta nje ya mlango mkubwa wa chooni.
"Yaaah nataka kujua kama uko sawa, are okay ??"
"Nisiwe muongo siko sawa kabisa "
"Naelewa, nafikili unaitaji kujisafisha zaidi, na sio hapa ni nyumbani "
"Ni kweli "
Rowan alinisindikiza mpaka nje ya chuo kabisa kisha akarudi darasani kuendelea na vipindi.
Kwa upande wangu niliitisha gari na kuondoka kwenda nyumbani.
JE UNATAKA KUJUA NINI KITAENDELEA ? TUKUTANE SEHEMU YA 2.
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 02
SONGA NAYO.....

Nilifika nyumbani nikajisafisha na kutulia zangu, nilijikuta nikijisikia aibu Sana walahi, ila sijui ni mimi tu au kuna wengine, jambo la period kuonekana mbele za watu kwa upande wangu ni aibu kubwa sana.
Kutokana na aibu ambayo nilikuwa nikijihisi, nilijikuta nikibaki tu nyumbani pasi na kwenda chuoni, yaani kitendo cha mimi kunyanyuka Na kwenda chuoni kilikuwa kizito sana.
*****
Hatimaye week nzima ilipita nikiwa bado naogopa kwenda chuoni, ila marafiki walahi ni wanafiki sana, ukiwa nao wanaigiza kukupenda na kukujali lakini ukiwa mbali uwiiiih ni Kama awakujui hivi.
Imagine tangu nimeondoka pale chuoni, hakuna ata rafiki yangu mmoja aliyenipigia simu kunijulia hali au kunipa pole kwaajili ya kile ambacho kilitokea.
Kwa upande wa Rowan amekuwa akipiga simu mfukulizo kwaajili ya kunijulia hali, lakini Rowan akuishia tu kunijulia hali, alinipigia pia kwaajili ya kunipa ujasili ili niweze kurudi chuoni.

***********

Ni siku nyingine tena, nimeamka zangu na naendelea na Mishe zangu za hapa na pale pasi na kuwaza kuwa natakiwa kwenda masomoni.
"Vee kuna mgeni wako nje "
Ilikuwa ni sauti ya mkaka wa getini, yaani mlinzi wa getini kwetu.
"Ni nani jamani ?"
"Aaah sijamuuliza,nikasema ngoja kwanza nimuulize small madam kama anatalajia kupokea mgeni " alizungumza mlinzi wetu na rafudhi yake ya kinyaturu.
"Unajua wewe hauna akili, badala ya kuuliza jina unakuja kwangu direct, me nitajuaje mama namjua au laaah "
"Basi, small madamu, kwahiyo nikamuulize ??"
"Haina haja wacha nikamuone "

Nilijibu na kujiweka sawa kisha nikatoka nje, ila mimi ni mtu ambaye nina uwoga wa hali ya juu, nilifika getini na kuchungulia ni nani kwanza.
"Rowan " nilishtuka baada ya kumuona Rowan akizunguka nje ya geti letu.
Haraka nikafungua geti, na kumkaribisha Rowan.
“Mkaka karibu “
"Asante za hapa ??"
"Aaah hapa ni njema Kwakweli, njema kabisa”
“aaaah pole nimekuja bila taarifa "
" usijali Rowan, karibu ndani "
"Hapana, nimepita kukuona, lakini pia kukuomba twende chuoni"
"Aaah hapana Kwakweli, niko radhi ni postpone for mwaka mzima kuliko kwenda kudhalilika uko chuoni "
"Ahaahahh Vee unajisikia kweli wewe ?, unajua ujasili unaanza na wewe kwanza, halafu iko kitu sio wewe tu, kila mwanamke anaingia mwezini, utasema kuwa unaogopa wanaume, nikutoe ofu, mimi kama Rowan nilishaitisha darasa kwa wanaume na kuongea nao na kila kitu kiko sawa "
Kwa namna moja au nyingine Rowan alijua kunipa moyo jamani, nilimkaribisha mpaka ndani na kumuacha sebuleni akipata ka juice.
Kwa upande wangu, niliingia chumbani kwangu na kwenda kujiandaa ili kuweza kwenda chuoni.
Kwa wakati huo, nilikuwa nikiogopa sana wanaume kutokana na matukio mfululizo ambayo nilipigwa na Mike.
Nilimaliza kujiandaa na hatimaye safari ya kwenda Chuoni Nikiwa na Rowan ikaanza, siku hii ndio nilijua kuwa Rowan ni kijana fulani hivi, Anaongea sana, Mcheshi mno lakini pia ana Huruma ya hali ya juu.
Tulifika chuoni na kwa kuwa muda wa darasani ulikuwa bado, mimi na Rowan tulishika njia na kwenda chini ya mti, sehemu ambayo ilikiwa tulivu sana lakini pia ilikiwa na ka upepo kakutosha.
“Ila Vee umejua kunishangaza Walahi, Yaani Mdomo wote huo, na heka heka uliyonayo kumbe ni muoga kiasi cha kwamba uwezi kujisimamia Mwenyewe ?”
Rowan aliniuliza uku akiniangalia sana usoni na akinicheka chini chini, kwa macho ya Aibu nikamuangalia Rowan Kisha nikajibu.
“Kwa Mimi naona ni kawaida sana aswa kwa Sisi wanawake, unajua Katika dunia yetu hii mwanamke anadhalilika sana kuliko Mwanaume, kwenye kila tukio mwanaume aangaliwi Kama ambavyo tunaangaliwa sisi mwanawake “
“Jifunze kujisimamia na uache kujitetea, simaanishi kwamba uliyosema ni uongo Ila kujitetea sana na kuangalia facts huo ni udhaifu “
Shoga yenu nilipoa hatari, nilibaki sura ndogo kama kidonge cha pilitoni, Rowan akiwa anaendelea kunipa somo, mashoga zangu Wawili walikuja na kuanza kunichangamkia.
“Shoga tulikumisii sana aiseeeh week nzima chuo uonekani “
Alizungumza Shoga Angu chuchu ambaye nilitokea kumpenda sana.
Nilitaka kujibu kitu lakini Rowan alinituliza kisha akawauliza.
“Baada ya kuona kuwa aonekani chuoni ni Hatua gani mlichukua ??”
Swali langu lilionekana kuwa gumu sana jamani, Shoga zangu walibaki wakiangaliana tu, Rowan alipoona kuwa wameamua kuwa Kimya Akaamua kuendelea kuongea.
“Mliona kuwa Yuko kimya lakini na nyie mkakaa kimya, kwa hali ambayo aliondoka nayo Mwenzenu , ninyi mlipaswa kumfata na ata kumpa moyo cha ajabu nyie ndio mmekuwa wa kwanza kabisa kumcheka ikiwa aibu yake, siku moja inaweza kuwa ya kwenu”
Rowan aliongea sana tena kwa Hasira, Sawa Rowan Ali kuwa akifoka lakini aliongea ukweli mtupu.
“Sina nia ya kuwafanya mjisikie vibaya Ila mnatakiwa kujitambua, wanawake manadhalilika kutokana na upuuzi wenu , Aibu ya mwanamke mwenzio unaibebea bango badala ya kuweka uzio “
Rowan Alimaliza kuzungumza kisha huyo akaondoka kwa Mwendo wa haraka pasi na kuaga.

ITAENDELEA…
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 03
SONGA NAYO.....

Nilibaki na mashoga zangu pale waliniomba Msamaha Nani nikawasamehe na story zikaendelea.
Pole pole nikaanza kuzoeana na Rowan, akawa mtu Wangu wa Karibu sana ambaye nilijifunza mambo mengi sana kipitia yeye, nilijikuta nikiwa na amani sana Mbele ya Rowan.
Niwape kastory kafupi kuhusu Rowani, ni kijana ambaye amelelewa na single baba, mama Mzazi wa Rowan alifariki siku ya kwanza tu ambayo Rowan aliona uso wa dunia.
Rowan kwao ni Mtoto wa Mwisho kuzaliwa Yaani nia Kama Mimi tu, tofauti yetu ni kwamba Rowan kwao wako wanne na wote ni wanaume, Rowan Maisha Yake ameishi na wanaume tu uku ndugu wakike ni wale wa kutoka kwa ndugu wengine wengine.
Nilijua yote hapo baada ya kumzoea sana Rowan, nilijikuta nikimuuliza mengi sana kumuhusu lakini pia alinijibu pasi na kuchoka.
Mimi na Rowan tukiwa kwenye restaurant tunapata Chakula, gafla simu yangu iliita na nilipoangalia Namba ilikuwa ngeni kabisa, nilipokea chapu kisha nikasikiliza sauti ili kujua ni Nani.
“WhatsApp kuna ujumbe wako “
Sauti ilikiwa nzito sana walaahi ambapo kwa Namna moja au nyingine nilijikuta nikipata wasiwasi.
Chapu nikawasha data na kuingia mtandaoni.
Woiiiiih, Yaani ile nafungua tu ujumbe, uso kwa uso na video yangu ya utupu, nakumbuka video hiyo nilijirekodi Kipindi ambacho Nilikuwa na mahusiano na Mike na Nilimtumia yeye kwani aliniomba.
Katika vitu Najutia kwenye maisha yangu basi ni hii ya kumpa Mike utu Wangu wote, Yaani Mike nilimfanya Kama Mtoto Wangu wa mwisho kwamba chochote anachotaka natimiza.
Nilishindwa kuangalia kabisa na nikajikuta nikipata wasiwasi wa hali ya juu.

“Uko Sawa ?”
Rowani aliniuliza.

“Oooh yah, yaah am gud, eat eat” nilijibu nikiwa na wenge la kutosha , muda huo huo ujumbe ukaingia kwenye simu yangu na ulisomeka hivi.
“Bwana ako namdai laki mbili yangu, Mpaka kesho Saa mbili asubuhi asiporejesha Naachia video hizi”
Kijasho Chembamba kikaanza kunitililika mfululizo, Tumbo joto mpaka nikajihisi kuvimbiwa niliangalia uku na uku nikihisi uwenda kuna mtu ananiangalia.
Rowan alibaki akiniangalia jinsi ambavyo nilikuwa nikiangaika, Rowan wa watu akatoa reso yake na kunipatia ili niweze kujifuta jasho ambalo lilikuwa likinitililika mfululizo.
"Rowan nafikili tutaonana kesho "
Niliamua kumuaga tu Rowan maana nilikuwa nikihisi kuchanganyikiwa aiseeh, kwakuwa Rowan ni kijana fulani hivi, mtaratibu mtulivu na ana utu uliopitiliza hakuona vyema kuniacha niondoke Mwenyewe tena kwenye hali ya kichanganyikiwa hivyo akanifata nje.

"Vee, Vee, Vee "

Rowan aliniita mfululizo uku akiitaji nimsubili lakini niligoma kabisa, zaidi niliongeza mwendo, ila mwanaume ni mwanaume bwana, Rowan aliweza kunifikia na akiponifikia akanidaka mkono na kuniuliza.
"Kuna taarifa mbaya umepokea au ? Vee hauko sawa shida nini mama !"
Rowan alionekana kujali sana, lakini kwa upande wangu, akili ilishapaniki hivyo niliona kama ananichanganya, kwakuwa ni jambo la aibu niliendelea kukataa na kusema kuwa niko sawa.
"Vee please nini shida mama "
Rowan hakukata tamaa hivyo akaendelea kuniuliza, nilijikuta nikipatwa na hasira sana ambapo niliamua tu kumfokea Rowan.
"Niko sawa nimekuambia shida yako nini kwani "
Baada ya kujibu hivyo, sikutaka tena kusikia maswali yake, nilinyanyua viatu vyangu na kuondoka kwa kukimbia.
Upande wa na Rowan alibaki akishangaa na kujiuliza maswali ambayo majibu mimi ndio nilikuwa nayo.

ITAENDELEA
ROWAN (Mine alone )

MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 04
SONGA NAYO.....

Kwa upande wangu, niliita gari haraka na kuwai nyumbani kwetu, naweza nikasema siku hiyo ilikuwa ni ya mikosi kwangu walahi, ile nafika tu nyumbani, uso kwa uso na baba na mama, lakini pia na kaka zangu, kiufupi Ni familia nzima ambayo niliikuta sebuleni.
"Kulikoni mwenzetu saa hizi ??"
Mama aliniuliza baada ya kuniona pale tu nilipoingia sebuleni.
Nilitamani ata kuwa invisible kwa wakati huo lakini ni kitu ambacho hakikuwezekana kabisa, kwakuwa akili yangu ilipaniki, nilijikuta nikikosa Ata jibu la uongo la kumpatia mama.
Kwa wakati huo mama alikuwa na haki zote za kuniuliza kwani, niliwai sana kurudi nyumbani ikiwa nimetoka nyumbani masaa mawili yaliyopita.
Mama aliniangalia kwa muda kisha akaniuliza tena.
"Umekuwa bubu au ??"
Nilikosa majibu kabisa, nilikuwa nikitetemeka na wasiwasi ilikuwa ni ya kiwango cha juu sana, ilo jasho sasa mpaka nililoana nguo ya juu.
Nilipiga mahesabu yangu ya haraka haraka na mwisho niliamua tu kukimbilia chumbani kwangu, nilifika chumbani na kujifungia mlango, nilipofunga tu niliangusha kilio cha hali ya juu ambapo sikuweza ata kujizuia.
Familia yangu yote ilichanganyikiwa walahi, walibaki wakigonga tu mlangoni mwangu na kuitilia jina langu kwa kupokezana.
Kujali kwao ni kama ndio kulikuwa kunaniongezea maumivu hivi, akili yangu iliwaza na kuwazua sana, nilifikilia na kujiuliza, familia yangu itajisikiaje siku watakapoona video zangu chafu ?
Nyieeeh haya mambo yasikie tu na yasije yakakukuta, unajua mambo ya sex kwenye dunia yetu ni kawaida sana lakini yasiende public, ni watu wachache sana wanaweza kukuelewa, lakini je ubongo wako utakubali kupokea tukio kubwa la kudhalilisha kama ilo ?
Nililia sana na nilipotulia nilipaza sauti yangu na kusema.
"Msijali niko sawa jamani "
"Vera acha ujinga, uko Sawa na unalia ? Ebu fungua mlango"
Kwakuwa familia yangu ilikuwa na wasiwasi, waliendelea kukaa tu mlangoni, kwa upande wangu nilituliza kichwa na nilipopata wazo nikaamua kufungua mlango.
Kitendo cha kufungua mlango, baba yangu alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu na kuanza kunituliza kwa kupiga piga mgongoni.
"Vee nini shida dada ??" Kaka angu mkubwa aliniuliza.
Niliwaangalia kwa muda kisha nikamkumbatia baba kwa nguvu sana, kwa wakati huo, nilishapata uongo wangu kabambe kabisa, ndipo nikaamua kuwadanganya.
"Rafiki yangu kipenzi wa A level amefariki "
"Ni nani ??" Mama aliuliza haraka haraka.
Baba alinishika vizuri na kwa mwendo wa utulivu tukasogea mpaka kwenye kochi kubwa na kuniweka nitulie ili niweze kuzungumza vizuri.
"Nina rafiki yangu ambaye nilisoma nae A level, ni mtu ambaye tulipotezana muda mrefu sana, sasa leo nimeweza kupata namba yake na kumpigia, ajabu simu yake ilipokelewa na mama yake na akaniambia kuwa Irene amefariki week mbili nyuma "
Weeeh uongo wangu si ndio ukatiki sasa 🤣, sio kwa baba wala mama, kaka zangu ndio kabisa, yaani wote walibaki wakinibembeleza pasi na kujua sababu kuu ya mimi kulia 😆.
"Wazazi wangu mnisamehe tu lakini siwezi kuwa na huzuni Peke yangu ikiwa nyie mpo " nilizungumza kimoyo moyo.
Baada ya kubembelezwa sana, nilijikuta nikipitiwa na usingizi hivyo nikaachwa nilale tu kwenye kochi kwani ni kubwa mno.

*******

Nilikuja kustuka jioni ya saa 11, macho mekundu sana na yamevimba, kutokana na kulia sana na kulala.
Nilipokuja kushika simu yangu, nikiweza kukutana na missed call za kutosha kutoka kwa Rowan, naweza kusema kuwa Rowan ni mtu na nusu, yaani licha ya kumpa maneno na kumfokea hajakata tamaa na anataka kujua naendeleaje.
Kwakuwa niliona kuwa ana wasiwasi sana, niliamua kumpa uongo ambao niliwapa wazazi wangu kwa njia ya meseji.
Nilitumia muda huo pia kuwaza ni njia gani naweza kutumia ili kumaliza tatizo kubwa ambalo liko mbele yangu.
Niwaambie kuwa laki mbili kwangu si kubwa, lakini nilikuwa nikijiuliza maswali sana, yaani Mike amekuwa mtu wa kutumia video zangu kwaajili ya kupata pesa na anajua lazima nimpe.
Kwa safari hii, nilikuwa nashindwa kuelewa kama ni Mike tu ameamua kutumia njia nyingine ili kupata pesa kwangu au ni mtu kweli anamdai Mike, lakini kama ni mtu ambaye anamdai Mike, picha zangu ametoa wapi ?.
Nilijikuta nikiwa na maswali mengi ambayo hayana majibu mwisho niliamua kumpigia simu Mike ambapo niliamini kuwa anamajibu sahihi.
Kitendo tu cha kumpigia Mike chapu akapokea, kwa haraka haraka unaweza kusema kuwa alikuwa akisubilia simu yangu, yaani ni kama Mike alikuwa akisubili mimi nimpigie.
"Vee mama nisamehe mim"
Alizungumza mike kwa sauti ya chini sana na yenye wasiwasi sana.
Sikujali kuhusu utulivu wake hivyo nilimuuliza maswali nikiwa nimepaniki sana.
"Huyu mtu anayenitishia na video ni wewe sio ? , Mike unataka nini kwenye maisha yangu ? "
"Aaah Vee please usinifokee, me mwenyewe nimechanganyikiwa kama wewe sawa ? Iko hivi, huyo jamaa aliyekukutafuta, amewatafuta mademu zangu wote, yaani wote ambao nina video zao na kuanza kuwatisha kwakuwa tu ananidai laki mbili "
Alizungumza Mike akijifanya kuwa na yeye amechanyikiwa.
“Mike usinifanye mimi kama mtoto mdogo sawa ? Mimi ni mtu mzima na ninajielewa, huyo mtu amepataje hizo video ikiwa nilishakulipa zaidi ya milioni kwaajili ya wewe kufuta hizo picha na video zote "
"Huu sio muda wa kunilaumu, fanya hivi, njoo geto tuyamalize”
"Unakichaa wewe ??".
"Vee acha kufikilia upuuzi wewe, sina chochote ninachoitaji kwako sawa?, kwanza hautakuwa mwenyewe, jamaa atakuja nimemuita ili anirudishie simu yangu na ikiwezekana nilipe pesa, najua pesa sina ila nitajua nafanyaje, wanawake wenzio pia wanakuja "
Eeeh Mike anajua kupiga sound jamani uwiiiih, kwa maelezo yake, nilijikuta nikikubali tu kwenda uko.
Nilijiandaa na kuvaa nguo zangu za heshima, nikaaga na kuondoka.
Safari yangu ilikuja kuishia kwenye geto la mike ambapo sikukuta ata mtu mmoja kwakweli, Mike alinipokea pale na kuniaminisha kuwa wengine watakuja.
Kwa wakati wote huo, nliamua kuwa bize na simu tu sikutaka ata kupiga story na Mike.
Ila nyie upwiru sio kitu kizuri, nikiwa nimekaa, nilijikuta nikianza kukumbuka mambo ambayo nilishawai kufanya na Mike, tena kwenye chumba iko iko.
Mike alikuwa akiniangalia sana tena kwa Macho ya tamaa, kwakuwa mike anajua udhaifu wangu, hakuchukua muda kunichanganya na hatimaye tukapinduka kwa mara ya pili.
Nyie katika wanawake wapumbavu na mimi naomba mniweke 🥺💔mimi ni mjinga kabisa.
Baada ya kumaliza kupinduka na kila kitu, mike aliinuka na kusogelea laptop yake kisha akawasha, na kusema.
"Waooooh imetoka vizuri sana, imechukua kila angle yaani, daaah na sura yako imetoka karibu kabisa"
Nilistuka sana na hapo nikagundua kuwa nimerekodiwa kwa mara nyingine uwiiih Vee mimi kwisha habari yangu....

ITAENDELEA
ROWAN (Mine alone )


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote