REGINA MCHARUKO

book cover og

Utangulizi

Regina ni msichana wa miaka 20 aliyekulia kijijini. Aliondoka nyumbani kwao na kuelekea mjini, baada ya kutafutiwa kazi za ndani huko mjini. Alipofika mjini, Regina aliishi katika apartment moja pamoja na dada yake, ambaye alikuwa na mtoto mmoja wa kiume. Hali ya maisha mjini ilikuwa tofauti sana na maisha aliyoyazoea kijijini.

Alipoanza maisha ya mjini, Regina alikuwa binti wa aibu na aliyeonekana kuwa na maadili mazuri. Hakupenda wanaume hata kidogo, na mara kwa mara alikabiliwa na majaribu ya wanaume waliomfuata wakimtamani. Regina hakuwa na uvumilivu wa nao hata kidogo, aliwakaripia vikali na kuwadhihaki kila walipojaribu kumtongoza.

Hata hivyo, mabadiliko makubwa yalitokea kwa Regina baada ya muda mfupi. Kutoka binti aliyekuwa na aibu na ambaye hakuwa na hamu na wanaume, na akageuka na kuwa binti anayejulikana kama "Regina mcharuko" aliyeendana na mtindo wa kisasa na asiyejali sheria za kijamii.

Tabia yake ilizidi kuwa mbaya, akawa mcharuko kiasi cha kuanza uhusiano wa kimapenzi na wanaume mbalimbali, hata wale waliokuwa na familia zao. Regina alijikuta akipoteza maadili yake ya awali na kuvunja mipaka aliyokuwa amejiwekea, huku maisha yake yakiwa ya mkanganyiko na yenye vishawishi vingi sana hakuwa na uwoga wala heshima. Unahisi sababu ya Regina kubadilika hivyo ni ipi? Na kwa nini abadilike kiasi hicho? Sina mengi ya kukwambia zaidi na kusisitiza tu kwamba usiache kufatilia hadithi hii tamu sana.

IMULIZI: REGINA MCHARUKO
MTUNZI: SUMAIYA MWENDO
SEHEMU YA: 01
MUHTASARI.........
REGINA ni binti wa miaka 20 ambae alichukiliwa toka kijijini kwao mkoani Iringa, na mwana dada aitwae Janet, na kuja Dar es Salaam kufanya kazi za ndani. Alipofika Dar es Salaam alikuwa binti mstaarabu sana asie na makuu wala majungu, lakini baada ya kufika tu Dar es Salaam na kukaa kwa muda wa miezi mitatu mambo yalibadilika, alipokutana na ma binti wawili wa uswahilini, Sharifa na Morio, Regina akawa hashikiki wala haambiliki kiasi kwamba dada yake, Janet akapanga amrejeshe kijijini kwao. Lakini REGINA akaingia kwenye mahusiano na baba wa miaka 49 mwenye pesa zake. Bila kujali umri wake wala afya yake na hali yake, kumbe tetesi zilikuwa zinasema mengi kuhusu mzee huyo kwamba, wasichana wengi ambao walikuwa na mahusiano nae, ilikuwa desturi kwamba kila wakitoka nae, basi haipiti miezi miwili wasichana hao wanapotea...... je vipi kuhusu Regina?? Atapotea? na mwanaume huyo huwa anawapeleka wapi hao wasichana? Kujua yote hayo baki na mimi mwanzo mwisho wa Hadithi hii, inayokwenda kwa jina la Regina MCHARUKO.

Anza nayo..........
Ndani ya jiji ya Dar es Salaam katika nyumba moja iliyozunguka na fensi ndefu na pana, kulikuwa na apartment nne. Apartment moja aliishi Mwanamke mmoja mrembo mweupe na mnene kiasi, Mwanamke huyu alionekana kuwa bize sana asubuhi tu huku akijiandaa kwa rasha rasha za asubuhi bila kujua afanye nini? Maana alifaa awahi kazini na hakuna kitu ambacho alikuwa kafanya ndanj mpaka wakati huo.

" Benson mwanangu vaa tunachelewa" aliongea na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka minne ambae alitoka kup8ga mswaki na kujitupia kwenye sofa lililokuwepo chumbani. Janet alihisi kuchoka asubuhi tu alimvuta Benson ambae bado alikuwa na usingizi mwingi kisha akaanza kukpaka mafuta na kumvalisha, alizitazama sare za shule za mtoto wake na kugundua zina mikunjo maana hazijanyooshwa vizuri.

" ee Mungu wangu, Maria alisema atanitafutia dada wa kazi lakini mpaka wakati huu sielewi kitu" alimaliza kumvisha mwanae na yeye pia kuvaa na kumwambia Benson atangulie kwemye gari, Benson alitangulia kutoka nje akiwa na usingizi sana yaani, maana ilimlazimu awe anaamka saa kumi na moja ili aondoke na mama yake, kwa sababu hakukuwa na mtu mwingine wa kumuandaa na kumpeleka kituo cha kusubiri gari ya shule isipokuwa mama yake. Kwa uchovu Benson alianza kulia.

" sasa unalia nini?? Aaah'' Janet alifoka maana alihisi kama vile Benson madeko yanazidi.

" sitaki kwenda shule nataka kulala, nina usingizi sana mama, kwa nini kila siku naamka usiku, wakati shule tunaenda jua linawaka kabisa?" Maneno ya mtoto wake yalimuumiza Janet ambae ilibidi aweke hasira zake kando, alilazimika kuamka muda huo ili aepuke foleni Barabarani. Na muda wa kuwasili kazini ndo kama hivyo saa mbili alifaa kuwa tayari ofisini.

" mtoto wangu" alimshika Benson na kumkumbatia, " usijali, mama anaelewa kuwa Ben anateseka, hivi karibuni atakuja dada ambae atakuwa anakupeleka kwa wakati ufaao sawa mwanangu. Mvumilie mama.kwa hizi siku chache tu mtoto wangu nakuomba" Janet alkumbatia Benson na kumbusu, Benson alikuwa na mzazi mmoja tu kwenye Maisha yake nae si mwimgine bali mama.yake, kuhusu baba yake alikufa mapema tu yeye akiwa tumboni, huo ndo ulikuwa ukweli wa Janet maana Baba Benson alikufa kwa ajali ya ghafla wakiwa na miezi sita tu ndoani, hivyo basi siku zote hizo hakutaka kuingia kwenye mahusiano na mtu yeyote kwanza, alimfikiria zaidi mtoto wake. Benson alimkumbatia mama yake na kumtii mara moja. Waliingia kwenye gari na Janet aliwasha gari na safari ikaanza.

Walipofika katika kituo ambacho huwa Benson anasubiri gari aliteremka na kumpeleka mwanae, kwenye duka moja ambalo lipp karibu na hapo babarani.

" mambo muha" alisalimia kwa heshima
" salama tu mama Ben, habari za muamko" Muha alihoji
" ni salama tu, naomba uniangalizie Benson wangu, gari ikifika muhimize awahi kama kawaida sawa?" Alisema Janet kwa adabu Muha akakubali na kumkaribisha Benson kwemye duka lake.

" njoo ndani mtoto" Benson aliingia ndani akafika na kuweka begi lake kando kisha akalala kwenye benchi

" usiwaze kuhusu yeye Mama Benson, hapa yupo salama kabisa" alipomaliza kuongea Muha Janet aliaga na kuondoka zake akimuonea huruma zaidi mwanae, hakika alihitaji mfanya kazi haswaa.

Mpaka majira ya saa nne alikuwa tayari kazini na amesha sahau kuhusu usumbufu wa asubuhi, na alikuwa akiendelea na kazi. Hadi simu yake ilipo ita Janet alipokea simu.
" aa Maria hatimae leo umenipigia simu?" Aliongea Janet
" ndio, Jane alafu sikia, kutafuta mfanyakazi from no where imekuwa mtihani sana, wasichana wa siku hizi hawaaminiki, kwa sasa nimepata msichana mmoja kwa ajili yako lakini na yeye ishi nae kwa adabu ishi nae kama mdogo wako kabisa, akikosea muonye akienda kinyume mkanye, akifanya vyema msifie kwa sababu Regina ana akili za kitoto sana bado, ila ni mchapa kazi mzuri tu" alisema Maria kwenye simu akimwambia Janet ambae alishangaa kwanza.

" we Maria Regina si mtoto wa mama yako mdogo?"
" ndio Jane lakini ndo yeye sasa ambae anaaminika, na wazazi wake wameridhia aje huko kwa sababu wanakuamini mno" aliongea Maria Janet akashusha pumzi akiwa na khofu kidogo

" khofu ya nini wewe? Nimesema ishi nae kama mdogo wako tu maana reginhana shida kabisa, kikubwa umuelewe tu na uuchukulie kawaida utoto wake." Baada ya Maria kusema hivyo Janet alijibu kwamba atatuma nauli sio muda mrefu kwa hiyo Regina ajiandae.

" aanze safari lini?" Maria alihoji
" iwe juma pili, kwa sababu juma pili ndo siku ambayo nakuwa free sana, ili nimfate stendi mimi mwenyewe " alijibu Janet na Maria akasema. " hiyo imeisha jane, ngoja nimpange hapa Regina ajiandae sasa" Janet alikubaliana na Maria na hatimae simu ilikata Janet aliachia tabasamu.

ITAENDELEA............
USIKOSE KUFATILIA HADITHI HII TAMU SANA.



SIMULIZI: REGINA MCHARUKO
MTUNZI: SUMAIYA MWENDO
SEHEMU YA: 02

SONGA NAYO........

Ilikuwa ni siku ya Juma mosi, baada ya Regina kufanya maandalizi yake yote, aliwaaga hadi ndugu zake kwamba anaenda Dar es Salaam kufanya kazi na atarejea akifanikiwa kwa hiyo wamuombee. Baada ya kusema hayo kwa watu wake ambao walikuwa rafiki zake wa karibu walifurahia na kumuaga kwa uzuri. Regina alirejea nyumbani kwao majira ya usiku, wazazi wake walimkalisha chini na kumwambia asipende kutembea usiku kwa sababu Dar es Salaam ni jiji la watu kwa hiyo, awe msikivu huko aendako, walimpa wosia wa kutosha sana mpaka wakati ambao Regina alienda kulala alikuwa ameshiba wosia wa wazee wa busara.

Regina alikuwa msichana mrembo mwenye rangi nyeupe na umbo zuri zuri la kike ambalo lilivuti mno, sema mazingira ya shida yakimfanya asijipende na aonekane wa kawaida mno. Majira ya asubuhi alikusanya nguo zake zilizokuwa na uafadhali kisha safari kuelekea stendi ilianza, na hatimaye aliagwa na Maria ambae alishughurikia na suhala zima la usafiri mpaka nini atakula njiani. Safari ya Regina ambae alikuwa hana hata hamu ya kuwatazama watu wa kwenye gari mara mbili ilianza..

Alipofika Dar es Salaam alishangaa kwanza, yaani watu wamevaa vimini, suruali za kuwabana sana, wengine walitembea vitovu vikiwa wazi. Akili ya Regina ilimtuma moja kwa moja kwamba watu hao hawana adabu wala maadili. Alikuwa tu akiguna kwa kila alichokiona, akiwa ameketi pembeni katika benchi ambalo aliambiwa na konda akae hapo hadi Janet aje kumchukua, Regina alihisi uchovu mno. Waru wa Dar es salaam walikuwa na shida gani? Muda wote walikimbizana huku na kule bila.uangalifu, wanawake kwa wanaume walibishana na kupandishiana sauti.

" Inhii! Yaani watu wa huku. Mwanamke kweli anampandishia mwanaume sauti, ama kweli hana aibu akipigwa je?" Aliwaza hivyo Regina akiwa ametulia.

" Regina " sauti hiyo ilimtoa kwenye utulivu akamtazama mtu ambae alikuwa akimtata sehemu aliyokuwa amekaa. Regina alishika mdomo wake. Mwanamke huyo ambae aliambiwa ndo dada atakae ishi nae alikuja kavaa pensi ambayo ilimbana sana na alikuwa kavaa t-shirt kubwa. Mapaja yake nje nje na kichwani alivaa kepu, na miwani ya urembo. Regina alishindwa hata kuitika akabaki kumtazama tu.

" Regina, mimi ndo dada Jane" Regina aliinuka na kumfata kwa uwoga akiwa kakumbatia shangazi kaja lake. Janet alimpokea begi lake na kumkumbatia Regina alikuwa hajiamini kabisa mbele ya Janet ambae hakujali kuhusu mwonekano wake. Alifurahi kumpata msichana mdogo mdogo kama huyo, alifaa kwa umri wa Benson. Alimpeleka moja kwa koja kwemye gari, Regina akawa anaogopa vitu kama hivi yeye hakuwa amezoea jamani daaah! Kuna watu wana maisha? Aliwaza Regina na wakati huo Janet aliwasha gari yake na safari ikaanza kuelekea nyumbani.

Safari moja kwa moja mpaka kigambo Buyuni, Regina alikuwa amechoka kidogo lakini hakuacha kuangalia mazingira hayo mageni kwake namna yalivyokuwa mazuri, watu walikuwa na hekaheka zao kibao, kwanza mshangao mkubwa zaidi aliupata wakati wanavuka panton wao wakiwa ndani ya gari huku wengine wakiwa pale pale haki mambo ya kizungu yalikuwa Dar. Alijisemea Regina na kukaa kwa utulivu tena.

Walipofika buyuni, tayari walikuwa wamefika, gari ya Janet ilisogea moja kwa moja hadi kwenye jengo.la apartment nne. Geti lilifunguliwa na mlinzi kisha Janet akaweka gari yake kwenye maegesho, Benson alikuja mbio mbio na kumkumbatia mama yake. Alimtazama Regina ambae hakuwa akimjua hivyo basi hakuuliza kwanza.

" mama Hussein asante kwa kumwangalia Benson " alisema Janet akimwambia mama Hussein, huyu yeye alikuwa kapanga katika apartment ya pili inahofatana na apartment ya Janet, alikuwa na mabinti watatu na watoto wa kiume wawili mtoto mmoja wa mwisho alikuwa na umri sawa na Benson. Mume wake alikuwa sheikh, kwa hiyo wao walikuwa waislam sana na muda wote walivaa ma hijabu vichwani mwao, mama Hussein alikuwa mwanamke mstaarabu sana ambae alikuwa bize na mambo yake zaidi katika hilo jengo.

" mmeshinda salama mama Sharifa?" Janet alimuhoji mwanamke aliekuwa ameketi kibarazani kwake akifumuliwa nywele zake na mabinti zake wawili. Sharifa na Morio, hawa walikuwa na umri sawa sawa na Regina. Janet hakuwa kawazoea sana ila aliwafahamu kwa sababu waliishi nyumba moja.

" ndio ni salama, naona una mgeni?" Janet alitabasamu na kuitikia kwa bashasha
" enhe hatimae amewasili, maana nilimsubiri sana" alijibu Janet. Morio na Sharifa walimtazama Regina namna alivhokuwa kavaa, na nywele zake za mbenjuo kichwani, walijikita wanacheka.

Regina aliwatazama na kuwaona wasichana wasio na adabu. Walivaaje vi taiti vifupi mbele ya mama yao, alafu vitovu vyao vilikuwa wazi ni matangazo kwani?

" karibu ndani Regina " Janet alisukuma mlango na kumkaribisha Regina kwa bashasha, huku Benson akimtazama tu. Alivumilia kwanzia huko nje lakini hadi ndani mama yake bado alikuwa hajasema kitu.

" aah! Mama mi nimeshindwa kuvumilia, enhe! Huyu ndio dada?" Janet alicheka
" hee! Ila Benson kwa hiyo muda wote huo ulikuwa unatuchora?"
" sasa mama wewe unakuja kujaje? Na mtu alafu unampa chumba lakini husemi hata ni nani yeye?" Benson alijituliza kwenye sofa na hapo Janet akapata nafasi ya kuwatambulisha.

" Benson huyu ni dada yako kwanzia hivi sasa anaitwa Regina, Regina huyu ndo mtoto wangu wa pekee Benson ambae namuweka chini ya usimamizi.na uangalizi wako pindi nitakapokuwa sipo, naomba unisaidie kumtuza kama mdogo wako bila kumbagua, wala kumnyenyekea sawa" alisema Janet Regina akakubaliana nae.

Maisha ya Regina yalianza hapo hapo, yaani yalianzia siku hiyo hiyo , baada ya kuonyeshwa chumba chake cha kulala na akamwambia, atamnunulia nguo kesho.yake akitoka kazini. Regina alikubali na kutabasamu.

ITAENDELEA..........
UNAHISI NINI.KITAFATA......?
USIKOSE KUFATILIA...


SIMULIZI: REGINA MCHARUKO
MTUNZI: SUMAIYA MWENDO
SEHEMU YA: 03

SONGA NAYO........
Baada ya kuoga na kula chakula cha mchana alilala kwanza ili kujipumzisha na uchovu wa safari, alikuja kuamka usiku kabisa akashangaa, dada Janet licha ya kuvaa nguo ambazo zilimchanganya bado hakuwa na roho mbaya, alimuacha akalala tu. Alimfata Janet jikoni ambae alikuwa anamalizia kupika na kuomba amsaidie chochote kitu ikiwa anahitaji.

" hapana we nenda kaone Tv kwanza, kwa sasa unahitaji kupumzika, mbona kama ni kazi utafanya tu tena kwa sana yaani" Regina alirudi sebureni kukaa akisubiri aitwe. Benson alimfata na kukaa kando yake akaanza kumhoji maswali.

" eti wewe ni dada nani vile?" Regina alicheka na.kumjibu
" naitwa Regina, wewe niite dada Regi sawa" Benson alifirahi
" anha sawa, mi naotwa Benson Rafael, nasoma darasa la kwanza, dada wewe ni mzuri una mwanya, una mashimo" Regina alicheka na kumuuliza.
" unamaanisha ma Dimpos?" Alijishika mashavu yake"

" ndio hayo si ndio mashimo?"
" Ni ma dimpos sio mashimo sawa" alimpapasa nywele zake Benson akafurahi
" wewe ni mvulana lakini mbona ni mzuri sana, au kwa sababu unafanana na mama yako?"Regina alimwambia

" hapana mi nafanana na baba yangu. Mama huwa anasema hivyo"
" basi baba na mama yako wanafanana" alijibu Regina Benson akakosa raha.
" kama ningemuona basi ningepata cha ku comment " alijibu Benson

" ku pomenti ndo nini?" Regina alihoji
" Dada Regi, sio pomenti ni comment, comment ina maanisha maoni, yaani ningetoa maoni"
" Anha! Kumbe hivyo tu" maongezi ya Regina na Benson yalimfanya Janet aone namna walicyo elewana mwanzo tu. Alifurahia hilo hata hivyo mtoto wake hakuwa na tabia ya kubagua watu. Kwa hiyo jambo hilo lilimfurahisha zaidi, baada ya kuwaza hayo alimwambia Regina afate chakula wale yeye pamoja na Benson. Regina alifanya haraka na kufata chakula jikoni kisha akamuita Benson waka kaa mezani pamoja wakaanza kula. Muda wa mchana chakula kilikuwa kitamu, na muda wa usiku chakula ni kitamu zaidi. Aliwaza Regina na kuhisi kama maisha ya mjini yalikuwa mepesi mno.

Majira ya asubuhi Janet aliamka na kuwaamsha wote Benson na Regina, lengo haikuwa Benson aense shule wakati huo hapana, lengo ilikuwa ni Regina ajue ni namna gani Benson anafaa kuandaliwa kabla ya kwenda shule, ahakikishe kanyoosha nguo, alimfundisha namna ya kuwasha pasi ya umeme kupunguza moto na kuonge, namna ya kuchemsha maji kutumia heater, namna ya kutumia jiko na namna ya kutumia vyombo vyote vya ndani vinavyotumia umeme, ilikuwa asubuhi hiyo ambayo Janet binafsi alipanga kuchelewa kazini, kisha akachukua alam na kui seti muda maalum ambao Regina atafaa kuamka na kumuandaa Benson, na muda muafaka wa kumpeleka Benson akasubiri gari. Alimpa maelekezo kwamba hatakiwi kumuacha Benson mwenyewe mpaka gari yake ya shule ifike na aondoke.

Regina alikuwa na kichwa chepesi mno, hivyo alikalili kila kitu vizuri mno na kwa haraka sana yaani. Siku iliyofata Regina alifanya kila kitu mwenyewe bila usaidizi wa Janet, Janet alimtazama tu na kuona kweli Regina ni mwelewa wa haraka mno.

Baada ya yeye kuondoka, Regina alifanya kila kitu kwa uweredi na mwisho alimpeleka Benson kituoni, Benson alikuwa na furaha sasa, hakukuwa na ulazima wa yeye kuamka asubuhi sana aondoke na mama yake kwenda kusubiri gari, mama yake alimwambia asipo muheshimu dada Regi basi mambo yatarudi kama zamani. Benson alitakiwa kumpenda na kumuheshimu dada Regi kwa namna yoyote ile.

Kwa kuwa Regi alikuwa msichana mwema na anaependa watoto, alimchukulia Benson kama mdogo wake kabisa, Benson alikuwa akitoka shule mapema basi anawahi nyumbani na kumwambia Regina mambo mengi ambayo alijifunza shule, Regina hakuwa anaelewa kila kitu anachosema lakini kuna baadhi alijufunza kwake.
Pale nyumbani Regina alimzoea kidogo mama Hussein na watoto wake, lakini walikuwa hawashindi nyumbani kila mara, na waliokuwa wakishinda nyumbani sana ni wakina Sharifa na Morio. Pamoja na mama yao, wao mchana kutwa walikuwa nyumbani usiku kwanzia saa mbili walikuwa na desturi ya kutoka na kwenda dinner, kwa jinsi ambavyo Regina aliamini hivyo.

Siku moja Regi,baada ya kumpeleka Benson akasubiri gari, alirudi nyumbani na kujiandaa kwenda sokoni, alipokuwa njiani hakuwa makini sana Barabarani nusura agongwe na gari. Regina alishtuka na kuushika moyo. Wake kwa khofu.
" Huna akili wewe? Huoni kama hii ni Barabara" alishuka kijana mmoja ambae alikuwa kavaa mavazi ya Askari police na kusogea mkononi mwake alishika pingu. Regina tangu hapo mwanzo huko kijijini kwao alikuwa akisikia kitu kuhusu askari police bali aliwachukia mno. Sababu yake haikujulikana, lakini alijikuta akipoteza khofu aliyokuwa nayo na kugeuka hasira kubwa.

" msichana mdogo kama wewe unatoa wapi mawazo labda?" Askari huyo alipokuwa anaendelea kuongea Regina alijikuta kamzaba kofi kubwa usoni bila kumfikiria. Askari police alikosa la kusema, huyo msichana mdogo amekosa aibu kiasi gani yaani? Amemzaba kofi akiwa kavaa sare, huyo mtoto hakuwa na wasiwasi wowote ee? Regina alipomaliza kumzaba kofi aliondoka zake.

" Aiyaaaaa! We Simon? Unapigwaje kofi na hako ka mwanamke kadogo, tena kofi zito la usoni bila kujali na wewe umetulia tu, hujafanya kitu?. Haya ni maajabu" alisema Askari mwenzie ambae alikuwa akimtazama Askari huyo kwa mshangao. Simon alijituliza akiwa bado anamshangaa Regina ambae alikuwa akiishilia mbele ya upeo wa macho yake.

ITAENDELEA..........
USIKOSE KUFATILIA MKASA HUU.......



SIMULIZI: REGINA MCHARUKO
MTUNZI: SUMAIYA MWENDO
SEHEMU YA: 04

SONGA NAYO........
Baada ya kufika nyumbani Regina ile sare ya Askari police ilikuwa ikimzonga akili yake alijikuta akikasirika mno kila alipoifikiria, alijiuliza tu ni kwa nini alikutana na huyo Askari, aliona kama vile siku yake imeharibika kwa kumuona tu.

" nawachukia ma askari mimi nawachukia mimi nawachukiaa sana" alitupa sahani la udongo chini kwa hasira likapasuka, akiwa amejiandaa kupasua glass Morio aliingia ndani na kumkuta Regina aliwa kavurugwa.

" wewe Regi, una wazimu ee! Unafikiri upo kwenu hapa? Haupo kwenu dada wewe upo kwa watu na umekuja kufanya kazi, ebu acha jazba" Morio alimvuta na kumkalisha kwenye sofa kisha akaanza kumbembeleza. Regina alipata utulivu wakati huo huo baada ya kulia kwa machungu.

" una shida gani kwani?"
" hamna kitu Morio " alijibu Regina kwa sababu hakujisikia kusema kitu. Morio alinyamaza kwa muda na kumbembeleza tu kisha mwisho alimwambia.
" kama ikitokea umeniamini basi utanieleza ni kitu gani ambacho kina kusibu wewe?" Alisema Morio Regina akamkubalia. Kutokea siku hiyo Regina akajikuta tu yupo karibu na Morio pamoja na Sharifa, licha ya hapo mwanzo kujiweka mbali nao kwa sababu ya kuhofia mwonekano wa mavazi yao, wakati huu alijikuta akielewa kwamba, tabia ya mtu si mavazi bali kila mtu ana moyo wake.
Walikuwa wakifanya mambo mengi pamoja na walienda sokoni pamoja, Regi ndo kwanza alikuwa amechipukia, ki ufupi mwili wake ndo kwanzaa ulikuwa umeanza kujaa jaa nyama. Huko nyuma pali ita hips lilikolea na kuujaza upaja wake. Na mavazi ambayo Janet alimnunulia, zilikuwa nguo nzuri mno za kidada, alianza kuvaa na kujikuta ananoga sana. Hakika alikuwa wa kipekee sana alipo ongozana na sharifa pamoja na Morio. Miluzi ilikuwa mingi mno Barabarani kitu ambacho Regina hakupenda hapo mwanzo.

" unadhani utawakataa na kuwakwepa hadi lini? Mwanaume akiamua kukuganda nakwambia hivi huwezi kuchomoa, kwa hiyo nakushauli tu, kuna muda mtu akikuomba namba ili kuepuka kupoteza muda mkubalie tu na umpe namba, kuhusu kumjibu na kuchat nae hiyo ibaki kuwa juu yako wewe mwenyewe ndo ufanye maamuzi" alisema Sharifa baada ya kuona vutana vutana ya Regi na mvulana ambae alikuwa akimsumbua kwa muda mrefu sana.

" yaani mi huyu kaka ananikera jamani mi kila siku namwambia sina simu lakini yeye hata hanielewi" alijibh Regi

" we Regina kweli huna simu na ukubwa wako wote?" Alihoji Morio kwa mshangao mkubwa.

" ndio kwani kuna ulazima wa mfu kuwa na simu, basi mi sijaipata hiyo bahati kwa sababu simu nayo tumia ni simu ya nyumbani, dada Jane alisajili line na kuweka namba zake. Pamoja na za wazazi wangu tu'' alijibu Regina.

" ama kweli wewe ni wa kuja" alisema Sharifa Regina akabaki kimya.

☆☆☆☆☆
Simon alikuwa amemaliza kufua nguo zake akavaa na kuonekana kijana wa kawaida sana, aliingia kwenye gari na kuondoka huku akiongea na simu.
Alipotoka yeye Regina Sharifa na Morio waliingia kupitia geti hilo hilo, Simon aliishi katika moja ya apartment iliyopatikana katika nyumba ambayo aliishi Regina na Regina hakujua kuhusu hilo.
Majira ya usiku kama ilivyokuwa kawaida, Regina akiwa ndani amekaa anatazam tamthilia huku Janet akimsaidiaa Benson kufanya homework zake. Gari iliwashwa nje ya nyumba yao na Morio pamoja na Sharifa walisikika wakimuaga mama yao.

" hivi dada, kwa nini baba yao Morio na Sharifa huwa anaonana nao usiku tu, kwa nini asitenge siku maalum kwa ajili ya kuwatembelea mchana, inatishia amani dunia imechafuka hii" alisema Regina Janet akacheka na kumwambia Regina.

" nyamaza Regi, usiingilie maisha ya watu sawa" Regina alikubaliana nae hata hivyo alikuwa na adabu sana kwa Janet lakini hali ya Hao watu kuondoka usiku kila mara ilimfanya awe na shahuku ya kujua huwa wanaenda kufanya nini? Kama ni baba yao kwa nini asiwe anawafata tu mchana kuwatembelea.

Kesho yake asubuhi Regina aliamka na kufanya majukumu yake kama kawaida, kisha baada ya kumpeleka Benson kituoni akapanda gari ya shule basi Regina alirudi kuendelea na majukumu yake kama kawaida. Alianza kufua nguo ambazo zilikuwa chafu mle ndani. Wakati ana anika kambani alishangaa kuona Sare za police zikiwa zimeanikwa kwenye kamba, ni mtu gani huyu alianika nguo mbaya na chafu kama hizo hapo nyumbani kwao. Regina bila uwoga isipokuwa hasira tu alizishusha hizo nguo na kuzitupilia mbali. Chini kulikuwa na vumbi na nguo zilijaa vumbi. Hakuishia hapo alichukua majia ambayo alikuwa anafulia akataka kumwagia hizo nguo.

" Regina!!!!!" Sauti kubwa ilisikika nyuma yake na Sharifa alitokea akiwa anachuchumia huku kashika gongo mguu wake ukiwa mbovu, na uso wake ukiwa umejaa manundu. Regina alishangaaa na kumtazama kwa umakini. Ilikuwaje akawa hivyo yaani? Yaani ni kama vile kuna mtu alikuwa kampiga sana na alimkwarua sana uso wake na makucha na mguu wake uliteguka.

" unataka kufanya nini? Hizo ni sare za inspector wa police sio matambala ya deki" alisema Sharifa huku akimfata Regina ambae alikuwa amesahau kabisa kuhusu sare hizo na akili yake ilihamia kwenye mwili wa Sharifa.

" upo sahihi, lakini mbona upo hivyo? Ulipata ajali? Nini kilikukuta Sharifa? Masikini uso wako umeumia mno, na mguu wako ulikuwaje?" Alihoji Regina huku akimvuta akiwa na lengo la kumkalisha chini kwanza ili ajue shida yake ilikuwa nini? Sharifa alijiandaa kusema kitu ambacho kilimsibu na Regina akasikiliza kwa makini.

" ukweli ni kwamba, sisi hapa na Morio juwa tukiondoka usiku mama huwa anatutafutia wateja kwa hiyo....." alitaka kuongea hayo maneno lakini mdomo wake ulikuwa mzito sana hata kutamka.

ITAENDELEA...........

URAHISI NINI KIRAFATA ......??
USIKOSE KUFATILIA HADITHI HII.
SIMULIZI: REGINA MCHARUKO
MTUNZI: SUMAIYA MWENDO
SEHEMU YA: 05

SONGA NAYO........
Sharifa alishindwa kusema kitu akabaki kamtaza REGINA ambae alikuwa akimsubiri aongee maana hali yake ilikuwa mbaya sana.
" hapana Regina sitasema kwa sasa kwa sababu sijisikii vizuri, nilipajali mbaya sana katikati ya soko, nashindwa kuelezea hali yangu" alisema Sharifa na Regina hakutaka hata kumlazimisha aongee alimuacha kwanza kisha akawaza tu kuhusu maisha yake na Morio.

Yeye na Morio hawakuwa ndugu kabisa walikutana tu hapo kwa huyo mama ambae aliwachukua sehemu za vijiji tofauti tofauti na kuamua kuanza kuishi nao akiwa ahidi maisha mazuri. Na aliwatangaza kama watoto wake mbele ya kila mtu, lakini kila ifikapo usiku huwa anawatafutia wateja ambao ni wanaume, wanaume ambao huwa wanaenda kulala nao na wanawalipa pesa, ni kweli Biashara hii ilikuwa ngumu sana hapo mwanzo kwa sababu ilibidi walale na wanaume ambao ni wakubwa sana, wengine sawa sawa na baba zao, wengine waliwazidi hadi baba zao. Hali hiyo iliwavuruga sana akili happ mwanzoni lakini baadae walizoea, na hata Madam Suzy ambae ndo alikuwa mama yao huyo anaewalea, alikuwa akiwajali sana kila waliporudi aliwapa chakula kizuri na aliwapa dawa za kuwaondoa maumivu.

Walizoea kujiuza na kupata pesa ndefu sana ambayo, waliigawa sawa sawa na waliwatumia familia zao vijijini, wadogo zao walisoma na wazazi waliwashukuru na kuwabariki zaidi kwamba kazi yao waendelee nayo vyema Mungu awazidishie, wazazi waliamini kwamba watoto wao wanafanya kazi katika kiwanda cha plastic kitu ambacho sio kweli.

Akiwa kwenye mawazo marefu hatimae Morio alifika akiwa kaongozana na kijana mmoja mtanashati sana, aliwasogelea akiwa kashikana nae mkono kisha akawasalimia hao wasichana wawili waliokaa pamoja.

" Mambo Sharifa, pole sana Morio kanambia ulipata ajali sokoni, pole sana" aliongea kijana huyo Sharifa akaitikia

" ndio lakini nitakuwa sawa hivi karibuni" alijibu Sharifa na kumtazama Morio ambae alimwangalia kwa jicho la kificho, akijua wazi kwamba kilichomtokea sio ajali bali ni alipata ajali kazini, baada ya mke wa mbaba ambae alifaa kulala nae usiku wa jana yake alikuwa ameshamfatilia mume wake na kufahamu kuhusu mkutano wake na sharifa , na mwisho alitafuta kikundi cha wanawake watatu wakawa wa nne, ni kama dakika tano tu sharifa aliingia katika chumba cha hotel na mwanaume huyo, wakiwa wanajiandaa kufanya mambo yao, mwanamke huyo akavamiaa akiwa na kundi lake.

Mwenye mke wake alishtuka, na sharifa akaishia kupigwa kwa nguvu na kukwaruza usoni na makucha ya hao wanawake, licha ya kuwa na miili mikubwa walimpiga sana Sharifa na kumpandia juu. Sharifa alipiga kelele akiomba asaidiwe lakini hao wanawake hawakumuonea huruma. Na mwisho walimtegua mguu wake. Kama sio huyo mwanaume kuingia kati na kumuahidi mke wake harudii tena basi wangemuua bila shaka.

Baada ya kuondoka hilo kundi la watu wengi. Hatimae kuna muhudumu aliingia ndani ya chumba na kujua kuna mtu alikuwa kapigwa vibaya hivyo alipelekwa hospital. Na mwishowe mama yake alienda hospital na kukuta kapewa huduma ya awali, alifanya malipo na kumchukua sharifa kisha akarudi nae nyumbani.

" Asante Juma, ila kwa sasa si unaona navyo endelea" alijibu tena sharifa
" na huyu nii..?" Juma alitaka kujua kuhusu Regina
" anaitwa Regina ni mdogo wa dada Janet " alijibu Morio

" ohh! Kweli ee! Regina wewe ni mrembo sana, naitwa Juma " Juma alijitambulisha kwa kumpa mkono Regina alimpa mkono pia lakini aliwahi kuutoa mkono wake kisha akaingia ndani. Hata hivyo Morio alikuwa amefika kwa hiyo angebaki na sharifa.

" huyo msichana anaogopa watu" Juma alimhoji Morio
" ndio haswa wanaume, hapendi kabisa ukaribu na wanaume sijui walimfanyia nini?" Alisema Sharifa huku akiongozana na kina Morio kwenda kwenye apartment yao.

☆☆☆☆

Simon alirudi akiwa amejichokea mwenyewe kwa kesi iliyokuwa mbele yake, yaani kesi iliyomsumbua ilikuwa ngumu kiasi kwamba hakujua ni kiti gani afanye kila alipo waza. Ni asubuhi tu alitoka kufokewa na mkuu wake wa idara kuhusu uzembe unaoendelea na yeye hatoi mrejesho unaoeleweka toka aanze kufanya utafiti.

" huyu mwanaume anaeteka wanawake na kuwapoteza, ana lengo gani na kazi yangu? Naona kabisa nikipoteza kazi yangu kwa kesi moja tu hii ya sasa" alijisemesha mwenyewe bila kuongea na mtu. Akiwa anatembea tembea kuelekea nyumbani kwake ghafla alishangaa kuona sare zake za kazi zikiwa zimèangushwa chini.

" hii Inawezekanaje?" Alijiuliza na kuita kwa sauti.

" nani aliethubutu kutupa sare zangu chini na kuchafua??" Aliongea kwa hasira Simon, Morio sharifa na Juma walikuwa wa kwanza kutoka nje, Regina pia alisikia makelele ya Simon akatoka akiwa na shahuku ya kumjua huyo mwanaume ambae alianika hizo gwanda chafu kwenye kamba ya hapo nyumbani.

" ni nyie mmetupa nguo zangu, nyie wasichana wawili mnaonekana hamna adabu kabisa" alianza kuwafokea Morio na Sharifa kabla hajamuona Regina, Regina alimuona Simon na kujikuta kaikumbatia mikono yake kifuani akimtazama huyo mwanaume hapo mbele yake. Huyo ndo Askari ambae alibaki kidogo amgonge na gari, alafu akaanza kumfokea kwamba hakuwa mwangalifu na yeye ndo aliishia kumzaba kofi la uso.

" sio wao waliotupa nguo hizo" Simon aligeuka na kukutana uso kwa uso na Regina, huyu msichana alionekana mdogo sana lakini mbona alikuwa na sura ya utata.

" anha! Kwa hiyo wewe ndo umetupa nguo zangu chini? Siku ile ulinizaba kibao mbele ya msaidizi wangu, na leo umetupa sare yangu, unalidhalilisha vazi takatifu la serikali" alimsemesha Regina ambae alihisi kichefu chefu

" unaongea bila uwoga eti vazi takatifu? Mfyuuu kwa utakatifu gani? Nyie ma askari mnajifanya wema sana mbele za watu na mnajifanya kama watu wa watu lakini ukweli ni kwamba nyie watu sio wema kiasi hicho. Nyie ni wabaya" Simon aliona kama huyu mjinga anabwabwaja upuuzi tu. Alimkamata Regina na kuingia nae kwenye gari baada ya kumfunga pingu.

" kaka Simon subiri, Regi haelewi mambo hapa" aliongea Morio alijaribu kumtetea lakini haikuwa rahisi hata hivyo Regina hakuwa na adabu hata kidogo kwa Simon. Ndo maana Simon hakutaka masihara nae, alimpeleka moja kwa moja kituoni na kumuweka Regina sero. Regina licha ya kupelekwa kituoni bado hakuongea na Simon kwa adabu.

ITAENDELEA..........
UNAHISI NINI KITAFATA......??
USIKOSE KUFATILIA HADITHI HII.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote