PENZI LA MJEDA NA MCHARUKO 1
HUSQER BALTAZAR
Kwa majina naitwa LOVENESS PAULO, binti mwenye miaka yangu 18 tu, Nilikuwa nasoma chuo, sasa nikiwa chuo mwaka wa pili nikisomea mambo ya pharmacy, ilikuwa jioni muda wakurejea nyumbani ulifika,
nimefika nyumbani kabla sijaingia ndani nasikia mzozano wa baba na mama yangu wa kambo aitwae MAMA ESTA akimwambia baba asinilipie ada kwakuwa Kwa Sasa Kuna uhaba wa pesa haitoshi kulipia watoto wote na mwanae anatakiwa alipiwe ada pia hivyo kwakuwa nimekuwa waniozeshe Ili mahari iwasaidie nilichoka nikatamani kuingilia lakini nikasita nisikie Mzee atajibu nini Cha ajabu Mzee akawa amekubali niliumia sana sikutaka tena kuingia ndani badala yake nikaamua kuondoka wakati natembea tembea nikiwa siko sawa kabisa ghafra gari ikafunga break mbembeni yangu akatoka mkaka SOJA amepanda hewani ni amekunja sura mie hata sikujali Wala kushtuka ndo kwana nimeganda tu akanifikia kwanza nikala banzi sikujibu chochote nikakaa kimya ni machozi tu ndo Yananitoka akabaki ananishangaa akahisi huenda nimeumia akanibeba nakuniingiza kwenye gari anipeleke hosptal tumefika Mimi Niko kimya na hapo nimepelekwa hosptal ya JESHI nafika naona anapewa saluti ata jina sikuwa nimelijua mpaka muda huo nimefika akaomba nitibiwe wakanishughulikua wakasema Hana shida anaonekana ana msongo wa mawazo tu na mshtuko akaomba kuongea na Mimi, akaniuliza Unaitwa nani?
mimi kimya , Yule kijana nikashangaa kakunja sura, mara nikala banzi ikabidi doctor aingie maana alikuwa nje…
akamwambia PETER ambae ndio Yule mjeda kuwa “usimpige huyo sio mtuhumiwa ,hayuko sawa ongea nae taratibu kama uwezi pisha niongeze nae Kisha nitakwambia ,
jamaa akapiga meza Kwa nguvu akajibu CLAM uyu binti anakiburi hujui tu, yaan siwezi kubembeleza Mimi mtu jeuri
aisee nikanyanyuka nikataka niondoke maana niliona badala ya kutibiwa hapa basi nitaambulia kipigo, akanirudisha Kwa nguvu huku macho yamemuiva, kisha akasema “binti usinijaribu nitakuharibu Sasa hivi, sasa ni hivi jibu maswali yangu kabla sijakuchafua unaitwa nani?....Na unashida Gani ?
sasa hapo nikaona makofi yataniua, maana nilijua nikijichanganya kidogo basi nitabutuliwa mpaka basi, basi nikaanza zangu kulia, akataka kunipiga tena…
DOCTOR CLAM akamzuia akamwambia, akae pembeni yeye ataongea na Mimi
DOCTOR akasogea akanimbembeleza akawa ananiambia “Lia kwanza umalize uchungu wote Lia usiogope toa sauti nilikiamsha mpaka,MJEDA P akatoka nje, nililia karibu saa nzima mpaka kichwa kikawa kinaniuma, basin nilipomaliza kulia nikapewa panador kwa ajili ya kutuliza maumivu Kisha akaniuliza unaitwa nani mtoto nzuri?.....
Nikajibu naitwa loveness…
PENZI LA MJEDA NA MCHARUKO 2
HUSQER BALTAZAR
“najua utaniuliza Kwa nini nilikuwa nalia ,Niwie radhi maana Kuna mambo yalinichanganya ila usijali maana niyakifamilia tu,hivyo siwezi kukwambia Kwa Sasa, na usijal kabisa maana Niko sawa na nashukuru sana, naomba uniombee msamaha Kwa uyo gaidi sijafanya makusudi ila sikusikia ata honi yake…..
Niliongea Kwa upole japo Mimi sio mpole kihivyo……
Kiukweli mambo niliyoyasikia nyumbani yalinifanya kuwa mnyonge mno, Kwa wakati huo nilimukumbuka sana marehemu mama yangu ,
DOCTOR CLAM aliniambia “usijali nitaongea nae na ataelewa,Lakini wakati mwingine kuwa makini barabarani ,
Tukiwa bado tunaongea simu yangu iliyokuwa
kwenye kibeg changu iliita ,
kucheki alikuwa kaka angu wa tumbo moja anaitwa WAMBURA Nina kaka mmoja tu wa pekee nilipokea,
Nikamsalimia akaniuliza uko sawa? Mbona umepoa sana?! Sijutaka kumpa mawazo ,
Kwani Hali yake Kwa wakati huo haikuwa sawa nilimwambia asijal Niko sawa naomba nipigie badae Kwa Sasa Niko bze kidogo
Alinielewa akakata ,
Kumbe wakati naongea P akawa anaingia ikabidi ,
CLAM amtoe nje , wakaanza kuongea na kwakweli sikujua waliongea nini ila waliludi akaomba anipeleke kwetu ……
Nikawaza mtu mwenyewe dk mbili nyingi unashangaa umewekwa mambazi nikajiambia hapana nikakataa,
Aiseeeee nashangaa mjeda p kakasirika, yaan alikasilika ghafra mpaka nikajiuliza uyu ni mzima kweli na hii kisirani yake kosa langu hapo nini sasa ,
Doctor CLAM akaniambia nisiogope hakuna tatizo nipelekwe Kwa usalama wangu, na zaidi muda umekwenda sana ,ikabidi tu nikubali ila kishingo upande nawaza huyu Gaidi sijui kama hatanilapua mabanzi njiani , na kwakweli sikuwa na ujanja wowote ule nikasema ngoja niande tu,
Nikatoka chapu nje nae huyo akaja akafungua nikapanda nyuma akasema njoo mbele Kwa hasiraaa ….
Nikatoka nikaenda kukaa mbele, basi safari ikaanza nikawa namwelekeza ila ndo Kwa ustarabu, Ili nisile mabanzi tulivyokaribia sikutaka afike adi kwetu nikamwambia nishushe nishafika ,
Akasogea Sehemu akapack nikashuka nashangaa nayeye anashuka na migwanda yake, nikajisemea khaaa 🙄 uyu vipi tena !!
Nikamuuliza wewe mbona nyuma yangu tena kwemaa, akasema lazima nikukadhii Kwa wazazi wako ,nikaona Sasa uyu Anataka kunizoea uzuri nishafika , nikamwambia ,
We mjeda usinizoee hujanitoa Kwa wazazi wangu na Mimi sio kitoto kidogo usinipande kichwani na nikuambie tu kuwa sikuogopi …..
mkaka mzuri lakini Gaidi hufai ata Kwa kumbembelezea watoto wewe, na hapa unaponiona Nina yangu usitake niyamalizie kwako ohooooo, nikasema kisha nikaanza kwenda kwa maana alikuwa kimya tu anaivisha macho kaa amemwagiwa pilipili…
Ile nimepiga hatua mbili nikashangaa nimevutwa Kwa nguvu aisee mpaka kwenye kifua Cha jamaa ilikuwa ni ghafla na nilikuwa na kifua saa 6, na sijavaa hata brazia, alivyonisogeza tu kifuani chuchu zinamgusa nikama alihama Kwa muda ..
Mwanzo adi mwili wake ulikuwa mwekundu nikaona Kama amepoa ghafra, nikajitoa haraka Kwa uoga kweli Kuna Hali Flan niliihisi mwilini kwangu….
Nikaona hapa usalama ni sifuri wakati P anashangaa Mimi huyo nduki, anakuja kupata akili nishapotea …
Nafika home muda umeenda na Mimi ndo ninaetegemewa kupika Kila siku, Inshort kazi za nyumbani ni mimi, na watoto wa mama wa kambo ni kama mayai ,hawafanyi chochote hata wakubwa wangu, na baba angu alioa wake wawili mama angu alikuwa mke mkubwa, Kisha huyo mama mdogo a.k.a mama wa kambo nitatumia mama mdogo Kwa sababu ndio nilivyokuwa nikimwita…
mama yangu alituzaa wawili Mimi na kaka angu WAMBURA ….
MAMA MDOGO: anawatoto watano wakiume 3 WAKIKE 2 mama angu alikuwa na shida ya uzazi mimi na kaka angu tumepishana miaka 20, Kwa Sasa kaka yangu yeye ana miaka 38,
watoto wa mamdogo wakwanza, JONH anamiaka 35,ameoa na anawatoto watatu,WAPILI NEEMA ana miaka 30 ameolewa na anawatoto watatu pia,mtoto wake wa tatu anaitwa MKAMI ana miaka 28 ameoa na anawatoto wawili,WANNE anaitwa JOSE ana miaka 25 Yuko chuo,mtoto wa tano anaitwa SOPHIA ana miaka 19 Yuko chuo pia….
Nimefika nyumban yaan nafikia kugombezwaa, Kwa nini nimechelewa Bora niozeshwe nisije wahalibikia nyumbani, kiukweli niliumia sana sikuwa najinsi ningesema nijitetee ningeishia kupigwa tu, nikaingia jikoni nikapika nikatenga tukala, wakati naondoa vyombo nikaitwa na Mzee akasema kuwa anamaongezi na Mimi …….
Nikasogea kumsikiliza akaniambia nijiandae Kuna wachumba wanakuja, hivyo yeye kama baba yangu kaona ni bora niolewe nitasomeshwa na mme wangu Kwa sababu hanielewi kabisa, kwanza ninachelewa kurejea nyumbani na ninagombana na mama Kila siku nayeye hapendi kelele ….
Aisee nilijisikia vibaya sana, na sababu anazozitoa hazina kichwa Wala miguu,niliamua kujibu mi siolewi , alinyanyuka akaanza kunipiga, yaan nilipigwa jamani na hivi baba angu ni mkurya ni kipigo Cha hatari na nikafungiwa ndani hakuna kutoka mpaka huyo mme aje , na simu nikanyang'anywa ….
Upande WAPILI P alirudia mpaka kwake akiwa hayuko sawa kabisa, na huyu mjeda p alikuwa na mtoto wa kike wa miaka 6 , na simulizi fupi mpaka akampata huyu mtoto, ni kwamba ,yeye na mama wa mtoto waliachana mwanamke aliolewa na mkubwa wake wa kazi na yeye akahamishwa kwenda mkoa mwingine Ili asisumbue …..
hii ilimuumiza sana, kuanzia hapo akachukia wanawake wote, na akawa ni mtu wa hasira sana, na alimlea mwanae Toka akiwa na mwaka mpaka Sasa Kwa msaaada wa dada ake P, kwani walikuwa ni yatima na dada ake alipata ajali akapata shida kizazi kikatolewa hivyo Hana uwezo wa kuzaa …
P alipandishwa cheo akawa brigadier wa jeshi, yaan alimzidi hata mme wa ex wake mbali sana ,na siku hio ndio alikuwa ametoka kuchukua barua ya kupanda na kuhamishwa kituo Cha kazi , alikuwa na furaha sana lakini mawazo juu ya LOVE hayakumuisha…
Mpaka dada ake anaitwa LILIANI alihisi mdogo ake Leo hayuko sawa, ikabidi amuulize shida nini inaonekana unatatizo ….
P alishtuka akasema hamna shida sister Niko ok, vp mmeshindaje dada ake akaguna akasema salamu umeshanipa na mpaka Barua yako ya kupandishwa kazi na kuhamishwa nishasoma Aya utanificha ama utanambia tatizo ni nini ?, akasema dada yake…..
“Aaah dada ata sijui nikwambieje Mimi mwenyewe sijielewi dada nahisi ni ujinga tu unanisumbua tu, dada yake akamuangalia kwa udadisi huku anatabasamu akamwambia mdogo ake umempenda nani huyo binti mwenye bahati…..
Ghafra P akakunja sura , dada ake akashangaa….
“ kulikoni mbona umebadilika ghafra tena?!
Sister we hujui tu sijui ata kwanini nakiwaza iki kinguchiro Kidogo , kwanza ni kinajeuri na mdomo mchafu sizani kama tutawezana kwanza wanawake sio watu sister ,aliongea huku akinyanyuka…..
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote