PENZI LA LAST BORN
JE WAJUA mwanamke ananguvu kubwa sana ya kurekebisha tabia ya mwanaume wake akiwa na hekima na busara, njoo TUJIFUNZE kwa pamoja namna lulu alivyooambana kumrekebisha mwanaume wake...
Story yetu ipo hivi
Kijana wa kitajiri ambae alikuwa ni mtoto wa mwisho kwenye familia yao anakuja kumpenda mwanamke ambae yuko busy na utafutaji, kitu ambacho kinasababisha huyu kijana kuwa na vurugu sana, sometimes anaenda kumchukua mdada kazin kibabe akimmiss, bint asipojibu sms Wala kupokea simu kwa wakat ni tatizo, muda mwingine anaigiza anaumwa just mwanamke asiende kazin akae nae tu, lakin lulu anaamua kubadilisha mwanaume wake kitabia, unadhan atafanya nn, usikose Kisa hichi Cha penzi la last born
PENZI LA LAST BORN 1
HUSQER BALTAZAR
Kuna vitu huwa vinachekesha kwenye maisha, na kuna aina za watu unaweza ukahisi kama hawapo dunian, mimi nilivyokuwa mdogo nilikuwa naamin kuwa mwanaume akishakuwa mtu mzima anakuwa mgumu na anakuwa na uwezo wa kubeba majukum, ila kuna ma last born, tena hawa ma last born wa kitajiri, yaan unakuta mtu anazeeka na utoto wake …..
Naitwa lulu ndio jina nililopewa na wazaz wangu, ila mtaani wananiitaga dada mjasi, kwa maana hakuna biashara ambayo sifanyi…
Ingawa nina degree ya maswala ya accountant, lakin nina miaka mitatu sasa sijapata ajira, kwa maana nimeweka vyeti vyangu kabatini vinaendelea kujaa vumbi…
Sasa kutokan a na ugumu wa maisha, kwa maana baba yangu alifariki nikiwa kidato cha kwanza, hivyuo mama ametulea kwa tabu sana, nah ii ndio sababu ya mimi kusoma sana, na ingawa nimesoma na nimepata degree ila nimekuja kugundua kuwa, elimu pekee haiwez kukutajirisha, na kuna muda nataman hata kuuza vyeti vyangu, kwa sababu naona kama havina kazi, kwa maana kuanzia nimemaliza chuo sijawah kuona kazi ya vyeti vyangu hata mara moja……
Sasa katika kuhangaika hangaika na maisha, nikapata kazi kwenye hotel moja ipo Zanzibar kama receptioonalist,…
Ingawa sikuwa nimesomea maswala ya hotel management, Ila ujanja ujanja wa mjini na kujuana na watu, kuliweza kunifikisha pale, japo haikuwa rahisi…
Siku moja usiku wa kama saa mbili usiku, nikiwa kwenye majukum yangu, kwa maana niliamia Zanzibar na kumuacha mama na mdogo wangu ambae kwa wakat huo alikuwa kidato cha tatu, dar es salam, maana niliona maisha ya dar kama yamenishinda kwa maana nilikuwa nafanya kazi za sulubu tena kwa mshahara mdogo, ndio nikaomba Baraka kwa mama yangu ili niweze kwen da kufanya kazi Zanzibar, na kwakuwa m ndio nilikuwa tegemeo la pekee kwenye familia yangu, basi mama akakubali……
Sasa siku hio nikiwa naendelea kupokea wageni, nikaona vijana watatu wakiwa wanaingia hotelin, walikuwa wanaonekana kama wametoka kwenye familia inayojiweza sana, kwa maana kwanza walikuja na gari kali na kingine wakaenda kukaa sehemu ya VIP, kwa maana walikuwa ni wateja maalumu, na pia walikuwa wamevaa suti za gharama sana…..
Niliwakaribisha mpaka sehemu ambayo wanatakiwa kukaa, na baada ya hapo nikamuita muhudumu aje awahudumie, kwa maana kazi yangu kwao ilikuwa imeisha, ila mmoja wa wale vijana akasema “ unaona je kama ukituhudumia wewe?....
Nikatabasamu kisha nikasema “ hapa kwenye hotel yetu kila mmoja ana majukum yake, hivyo naomba nikaendelee na majukum yangu, kwa maana nimeshamaliza kazi yangu kwenu….
Nikashangaa wale wanaume wanaangaliana kisha Yule aliongea akasema “ wewe ni mrembo sana na ndio maana wakakuweka mlangon kwaajili ya kupokea wageni, hivyo tunaomba tuendelee kuuona urembo wako kwa kuendelea kutuhudumia…
Nikashindwa nikubali au nikatae, mara akaja meneja wa hotel akasema kuwa niwahudumie hao wanaume watatu, basi sikuwa na jeuri ya kukataa, hivyo nikauliza kuwa wanataka chakula au kinywaji …
Wanaume wawili kati ya wale ambao walkuwa wamekuja pale, wakaagiza chakula na vinywaji ila yule mmoja akasimama na kusema “ nakutaka wewe, kama ni chakula au kinywaji utanambia…
Nilikuwa kama sijamsikia hivi, kwa maana ananitaka mm kwa namna gani, yaan ndio akanikule au, nikawa nawaza…
Basi Yule kijana akasimama na kunisogelea kisha akaniangalia kwa sekunde kadhaa na kusema, “ nambie unataka bei gani kwa mm kulala na wewe siku nzima..
Nikaangalia chini kwa sekunde kadhaa kisha nikasema “ samahan sana kijana ila sipo hapa kwa ajili ya kujiuza, na kama kuna lolote lile naweza kukusaidia ,simulizi hii imeandikwa na husqer baltazar na inauzwa kwenye link pekee kwa offer ya mia tisa ishirini, ukinunua tofauti na kwenye link jua umenunua kwa wezi, naomba kwa pamoja tutokomeze wizi na tuwasupport waandishi halisi, tuendelee…, na kama hamna naomba nikaendelee na majukumu yangu, kisha nikaanza kuondoka maeneo yale, Yule kijana akaja na kunishika mkono kisha akanambia “ nimekuita na sidhan kama nimekuruhusu uondoke, embu naomba mkaniitie meneja, kwa maana huyu mfanyakazi wake hana adabu kabisa, akasema Yule kijana, na kweli kuna mmoja wa wafanyakazi akaenda kumuita meneja wa ile hotel……
“ nimekuja hapa kwaajili napenda huduma za hii hotel ila huyu mfanyakazi wako mpya hana adabu, na nadhan akiendelea kukaa hapa anaweza kufukuza wateja wengi sana, akasema yule kijana na sio siri nilijisikia vibaya sana, kwa maana sikudhan kama nilikuwa nimemfanyia ubaya wowote ule, sasa kwanini anilipe ubaya, basi meneja alikuja na kwakuwa nilikuwa mpya kwenye ile hotel alinifukuza, na haikuwa hasara kabisa kwao kwa maana sikuwa na athar zozote zile pale…
Usiku ule ule nikakusanya kila kilichokuwa changu na kuanza kuondoka, ila wakat natoka Yule kijana akaja akasimama mbele yangu, sikutaka kabisa kuongea nae wala kumuona, akazidi kunisumbua kisha akanambia “ ona sasa, kama ungekubali kulala na mimi, basi sasa hivi tungekuwa tunaongelea habar nyingine kabisa, haya chagua, utakubali kulala na mimi nikurudishe kazin, au ukatae kulala na mimi na maisha yako yaendelee kuwa mabovu, nilimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha nikasema “ kuliko nilale na wewe, ni bora niende kulala kwenye makasino wanaume wote wa pale wanikule kuliko wewe mmoja, maana nahisi unanuksi, na haujawah kujua hata mara moja kwenye maisha yako ubinaadamu ni nini, kaa na madaraka yako ndio, nimefukuzwa kazi, lakin hii haimaanishi kuwa nitakufa, nitaendelea kuishi bila kutegemea huo msaada wako wa kipuuzi, na wewe tuone utapata nini kwa hizo dharau zako, nikasema kisha nikaondoka…..
Wale wanaume wote watatru walikuwa wananiangalia, ila Yule aliekuwa ananiletea nyodo akawa kama anataka kunifata ila wenzie ni kama walikuwa wanamzuia, basi nikaondoka zangu na kwenda nilipokuwa naishi, na kwakuwa zanzibae hayakuwa makazi yangu, na nilikuja tu kwaajili ya kazi, hikaona kesho yake nirudi zangu nyumban, kwa maana angalau dar nilikuwa nimepazoea, naweza kupita huku nikapita kule nikapata kazi…
Basi kesho yake nikarudi zangu dar, ila nilipofika nyumban nikakuta hali ya mama yangu ni mbovu sana, yaan nikamchukua na kumpeleka hospital, nikaambiwa kuwa atatibiwa kama atatolewa laki mbili, na kiukweli kwenye pochi yangu nilikuwa na elfu nane tu, nikatoa ile elfu nane, nikaacha na simu yangu, na kuwaomba waendelee kumtibu mama yangu na mimi nitaleta hizo hela, kisha nikaondoka…
Nilikaa nje ya hospital kwa kama nussu saa nikiwa nawaza ni wapi ambapo nitapata hizo hela, nikiwa nimekaa nikamkumbuka rafiki yangu mmoja anafanyaga kazi za night club, kuna club moja ubungo anafanyaga kazi, nikamfata moja kwa moja mpaka anapoishi, aliponiona alianza kucheka, kwa maana siku ambayo aliniambia kuwa nikafanye nae kazi, niliona kama kachanganyikiwa nikamtukana na kumtukana, alafu siku hio ananiona nyumban kwake….
“ shida nn lulu? Akaniuliza…
“ nina shida ya laki mbili kwaajili ya mama yangu, nikasema ..
Akacheka kisha akasema “ huwezag kufanya kazi zetu, hio laki mbili ungeipata kwa mara moja tuy, kama ukifika pale ukiwa umevaa vizuri na katajiri kamoja kakikutaman unaenda kukachuna zaidi ya hoi, akasema huyo bint, alikuwa ni mdogo ila hayo mambo alikuwa ameshayazoea, alikuwa anaiywa mwajuma..
Nilikubali haraka haraka mpaka yeye mwenyewe akashangaa na kusema kuwa “ ama kweli samba akizeeka anakula majani, kisha akanambia kuwa anataka apumzike maana tyunatakiwa kwenda kazin usiku, basi nikakaa nae pale nikiwa na mawazo balaa, kwa maana sikuwa najua hata hio kazi ambayo alikuwa anaizungumzia, ilikuwa inafanyika vipi….
Ila kama tunavyojua kuwa masaa hayajawah kuchelewa, usiku ulifika na akanipigisha pamba, ilikuwa ngumu sana kwangu kuvaa nguo fupi ila ndio hivyo sikuwa na namna, kisha akaita uba, na ikatupeleka mpaka kwenye hio club,…..
Tulipofika akanikabidhisha kwa meneja wake, kisha nikapewa jukum la kuwaburudisha wateja, kwa maana mtu akiwa pale akitaka nimshike mshike au nimnywishe vinywaji na mambo kama hayo, sikuwa na namna zaidi ya kukubali….
Nikiwa nashangaa shangaa, nikaona kama mtu ananiangalia sana, ila kwakuwa kuna zile taa za rangi sikuwa nimemtambua ni nani, alikuwa na wenzie wawili ambao walikuwa wamezungukwa na wanawake kasoro yeye, mara akaja mtu akaniita na kunambia naitwa na huyo kijana, nilipofika kwa huyo kijana mwenyewe, kiukweli sikuamin macho yangu kwa maana ndio alikuwa Yule kijana ambae alinisababisha nifukuzwe kazi Zanzibar, sasa anafata nn tena pale?....
Hata mimi sielewi, usikose kipande kinachofuata….
PENZI LA LAST BORN 2
HUSQER BALTAZAR
Nilipofik alipo nikaanza kutetemeka kwa maana niliamin kuwa anataka kunifanyia mambo ya ajabu, ila haikuwa hivyo, akanifata kisha akakaa nyuma yangu na kusema “ mwanamke mrembo kama wewe, unaweza vipi kufanya kazi kama hii?...
Sikutaka kumjibu, kwa maana niliona kama haimuhusu, mimi nifanye kazi yoyote ile, yeye inamuhusu nini….
“ najua una shida ya hela wewe, nitakupa laki tano kwa usiku mmoja, nataka kujua unautamu wa aina gani mpaka unakuwa unajiamin sana na wakat pesa unataka….
Niliposikia laki tano nikakubali, ila tatizo ni kuwa, sikuwah kufanya mapenzi hata matra moja na mwanaume, na hata sikuwa na ukaribu na mwanaume kwa kiwango hicho, alafu leo naenda kutolewa bikra kwa sababu ya pesa, ila maisha ni fumbo sana….
Sasa akiwa ananikokota kwenda chgumban , hapo nina wasiwasi balaa, mara simu yangu ikaanza kuita, pale hospital niliacha simu kubwa nikabaki na kivunja chawa, wakat kinaita Yule mwanaume hakutaka nipokee, kwa maana alipania kunila, ila aliekuwa anapiga ni mdogo wangu, ambae kwa wakt huo yeye ndio alikuwa hospital na mama, nikaona usinitanie, nikawa namuomba Yule mwanaume nipokee simu kistaarabu ila hakutaka, nikampush na kutoka nje, kumbe alikuwa ananifata, ila sikuwa najua…
Basi nilipokea simu, na mdogo wangu akasema “ mama anatakiwa kufanyiwa operation ya figo, hivyo inatakiwa million moja na nusu kwaajili ya upasuaji, laa sivyo mama atakufa…..
“ million moja na nusu!, nilisema kwa mshangao, kisha nikaanza kulia na kusema “ tunafanyaje mdogo wangu, kwa maana hapa nilikuwa natafuta laki mbili kwa ajili ya kulazwa kwa mama na bado sijapata, sasa hio million moja na nusu nitaipatia wapi mimi jamani….
Basi sikuwa na namna zaidi ya kulia, nulihisi kukata tamaa, na sikujua ni kwaajili gani mungu ananipa mtihani mkubwa hivi, mara nikashangaa mtu amekaa pemben yangu nay eye analia, ikabidi nigeuke kuangalia ni nani huyo ambae alikuwa analia, nikashangaa ni Yule kijana ambae alikuwa ananilazimisha nikalale nae, yaan nikajikuta namshangaa kwa maana sikuwa najua hata analia nini, alafu kumuona mwanaume kama yeye, tena handsome na anaonekana ni gentlaman kulia kilikuwa ni kitu kikubwa sana, sasa analia nini, nikawa najiuliza, kumbe ni last born bana, na wale aliokuwa anatembea nao ni kaka zake huwa wanamlinda, nilikuja kujua hilo baadae, kwa maana licha ya umri aliokuwa nao, ila familia yake ilikuwa inamchukulia kama mtoto mdogo ambae bado hata hajui njia ya kwao, na ingawa nyumban kwao wote ni watoto wa kiume, ila yeye ndio anaroho ndogo, kwa maana akiangalia hata movie ya kuhuzunisha, anaweza akalia mpaka mkadhan labda kafiwa, tena na mtu wake wa karibu, kumbe ni majonzi ya kwenye movie, hivyo kulia lia ni kawaida yake….
Akanisogelea na kunambia “pole mamaa, sikuwa najua kama ulikuwa unapitia mambo magumu hivi, yaan kuna sisi ambao tunachezea pesa na kuna ambao wanakosa pesa ya matibabu, nitakusaidia, na unisamehe kwa yote ambayo nilikufanyia, akasema Yule mwanaume, na mimi nikawa nimebaki nimetoa macho kama fundi saa, kwa maana ni kama sikuwa naelewa yale maneno yalikuwa yanatoka kwa nani….
“ naitwa Leon, unawez kuniita lio, kama hautajal naweza kukulipia hilo deni lako?, akasema ….
“ alafu ukishanilipia mimi nitakulipa nini, kwa maana sina cha kukulipa, nikasema…
“ nadhan sasa hivi tunatakiwa kujal hali ya mama yetu, na baada ya hapo nitakuambia ninachotaka unilipe, akasema Leon, na kwa wakat huo hakuna kitu nilikuwa nawaza zaidi ya afya ya mama yangu, na kweli nikamuona kama anaandika sms kisha akaituma, na tukakodi taksi mpaka mnazi mmoja ambapo alilazwa mama yangu, na kama utani Leon alilipa bills zote, ila tukiwa pale kila dakika alikuwa anapigiwa simu, nikawa nahisi ni wanawake zake, kwa maana alikuwa anaonekana kama hajatulia hivi, na kingine alikuwa anatoka pemben kuongea na simu, sasa kuna muda alienda uani, tukiwa pale pale hospital na simu yake alikuwa ameniachia mimi, ndio nikagundua kuwa walio kuwa wanapiga simu ni ndg zake, walikuwa wanawasi wasi kana kwamba ni mtoto mdogo kapotea….
Simu yake haina password nikaona sms inasema “ leon kijana wangu naomba unambie nilipo kwa maana mimi na baba yako tumeshindwa kulala kabisa, maana kaka zako wamesema ulikuwa nao, lakin umeondoka na haijulikani umeenda wapi, leon akajibu, mama usiwe na mashaka mimi nipo wapi…
Sms nyingine zilikuwa zinatoka kwa kaka zake, ambao wote walikuwa na wasiwasi wakitaka kujua kuwa leon yuko wapi, nilishangaa sana, kwa maana anaonekana kama ni kijana wa miaka 25 mpaka 30, sasa kwann ndg zake wana wasi wasi kiasi hichi, ambae mm bint mdogo, naweza nikaenda kulala nje na hata mtu asiniulize kuwa nilikuwa wapi, au nillala wapi, sasa inakuwaje huyu anauliziwa kiasi chote hichi….
Nikamjibia kuwa “ nina rafiki yangu mama yake kalazwa so nipo nae hospital, nikawatumia ndg zake wote hio sms, nikiamin kuwa kufanya hivyo kutawafanya wapate amani, kumbe ndio nilikuwa nimezidi kuwavuruga…..
Leon alitoka uwani, akaja kukaa pemben yangu, akawa anajitahidi kunipa moyo, ila kuna muda, akawa anataman yeye ndio abembelezwe, kwa maana mm nina majonzi lakin ananilalia begani kisha ananambia “ nasikia usingizi nibembeleze kidogo, yaan mpaka nikawa nacheka, badala ya mimi kufarijiwa , mimi ndio namfariji…
Sio siri nilikuwa namshangaa sana, kwa maana sijawah kuona mwanaume wa aina hii, kuna muda nikawa nahisi ni shoga, kumbe ni amelelewa kimayai mayai tu…
Mara nikashangaa watu wamevaa vizuri wanaigia hospital kana kwamba kuna mtu wanamtafuta, alikuwa ni mwanaume wa makamo mwenye zaidi ya miaka hamsin na mwanamke amabe hakuwa anaonekana kama amepishana sana na huyo mzee na vijana wawili, mwanzo sikuwatambua kama ndio wale ambao wanatembea na leon…
Leon alipowaona alishtuka na kusema “ nani amewaita hawa jaman tena hapa, nikamuuliza nini…
“ akaniangalia kisha akasema wale ni wazaz wangu, na wanakuja kunifata, sijui ni kwann hawanion kama nimekuwa na mimi nina uhuru wangu, akasema leon …
Kweli walikuja mpaka tylipo, na Yule mama akamkumbatia mwanae na kusema “ twebnde nyumban kwa maana hapa kuna mbu sana watakuletea malaria, na baba yake akawa anasema “ hapa kuna baridi sana, kesho utaanza kuumwa, hapo leon ananiangalia kama nitasema nn, ila kliukweli nilikuwa nashangaa tu sielewi chochote kinachoendelea ndio leon akajitoa mwilin kwa mama yake kisha akasemw “ mama huyu ni mpenzi wangu na mama yake yuko hospital, naomba muondoke kwa maana mnanifanya nijisikie vibaya mnavyonichukulia kama mtoto mdogo, mnajenga taswira gani kwa mwanamke wangu? Naomba ondokeni, na mniache maana nimetaka mwenyewe kuwa hapa, akasema leon kwa sauti ya kufoka…
NAKUJA…..
PENZI LA LAST BORN 3
HUSQER BALTAZAR
“ hamna shida, hamna shida mwanangu mimi nitakaa hapa na wewe mpaka asubuh, akasema mama yake na leon, na kumtaka kaka zake na baba yake kuondoka, nilishangaa sana, yaan mama analala na mwanae hospital na wakat mtoto mwenyewe amekuja kumuangalia mgonjwa na sio kama yeye ndio anaumwa, nilishangaa kwann wanakuwa na wasiwasi kiasi chote hicho, kwa mtoto ambae ni mtu mzima kabisa yaan, tena mtoto wa kiume…..
Basi kulipambazuka na leon akawa anataka kuendelea kukaa na mimi, ila mama yake akawa anataka aende nyumban kwanza na baada ya hapo atarudi, aligoma ila mama yake akasisitiza sana na mwisho akakubali…
Mama yangu alihudumiwa pale na mdogo wangu hakuamin kama nitaweza kupata kiasi chote cha pesa, ila ndio hivyo leon alinisaidia sana, tena wakat ambao sikuwa nategemea kabisa kama naweza kupata kiasi chote hicho cha pesa…
Nikiwa pale hospital Yule shoga yangu mwajuma ambae alikuwa ndio kaniunganisha na kazi ya club akanipigia simu, na kuniuliza kama naweza kwenda tena, ila kabla sijajibu nikashangaa napokonywa simu, kugeuka ni leon alikuwa amekuja hospital tena, akawa anasikiliza ile simu yangu kwa dakika kadhaa, kisha nikashangaa anajibu kuwa, “ hawez kuja tena kwenye kazi ya kishenzi namna hio, sasa hivi ameshapata mwanaume ambae anaweza kutimiza mahitaji yake yote, so hana haja ya kutumia mwili wake, akasema leon, nilitoa macho kwa maana leon hakuwa mtu wangu, na kwa nilivyokuwa namuona nilikuwa namuona kama sio mwanaume wa kuwa na mimi, kwa maana nilihisi kama hatukuwa tunaendana kabisa, ila kiukweli sikutaka kubishana nae…..
Basi tulikaa pale hospital na alikuwa anatoa gharama zote ambazo mama yangu alikuwa akidaiwa pale hospital mpaka siku mama yangu aliporuhusiwa, baada ya mama kuruhusiwa leon alinipigia simu akanambia kuwa anataka kuonana na mimi…
Sikubisha kwa maana kwanza amenisaidia sana, hio nguvu ya kubisha nitaitoa wapi mimi, basi nikatoka na kwenda ambapo alipanga tukaonane nae, na kama kawaida yake kaka zake walikuwa maeneo yale, nikashangaa leon anasema “ najua unajiuliza kuwa nataka unilipe nini kwa nilichokusaidia, naomba nikuombe jambo na sidhan kama unatakiwa kukataa…
“ jambo gani? Nikamuuliza….
“ will you marry me? Nikashangaa leon anasema kisha akapiga goti na kutoa pete akiwa anataka kunivalisha…
Kiukweli sikuwa nampenda so nikawa kama nimepigwa na butwaa, na nikama leon alijua hilo, akaniambia kuwa “ nikuvalishe pete ya uchumba au unilipe pesa zote ambazo nimekupa kwaajili ya kumsaidia mama yako….
Sikuwa na uwezo wa kumlipa ila nikakubalia anivishe ile pete kwa maana kulikuwa na watu maeneo yale na walikuwa wanatushangaa, so sikutaka kuleta drama mbele ya macho ya watu, na baada ya kuvaa pete, leon akasimama na nikamkumbatia na kumuambia “ sijui kama nimevaa hii pete kwa upendo ila nakuahidi kuwa nitakulipa pesa yako soon…
“ na ukifanikiwa kunilipa nakuacha siku hio hio, usidhan kama wewe ni mzuri sana, kuna wanawake wazuri sana maeneo haya kuliko hata wewe, so unatakiwa kunishkuru kwa maana sio rahisi kwa mwanaume millionea kama mimi kutaka kukuchumbia mwanamke low kama wewe, na badala ya kushkuru unaanza kuniletea kiburi chako, akasema leon…
Nikawa najiambia kuwa ni lazima leon atakuwa amenisaidia ili anitese kwa maana nilishawah kumjibu vibaya, sijui nilikuwa nawaza nn, kumbe mwamba alikuwa ameshanielewa, ila alikuwa na ile jeuri ya pesa na kuamin kuwa hakuna mwanamke ambae anaweza kumkataa mwanaume mwenye pesa kaka yeye……
Basi baada ya yeye kunivisha pete ya uchumba ndio nilielewa ni nini maana ya kudate last born, kwa maana siku ile tulikula na leon hakuwa anataka hata nisogee pemben yake, kuna muda nilienda choon nashangaa natoka namkuta amekaa nje ya choo, nikamuuliza shida ni nn, akanambia ety alijua nimekuja kufanya biashara zangu za mwili kwa maana nilikuwa nimechelewa kutoka choo, nikamuambia nimekaa huku hata dakika tano hazijaisha, kwanini unaniwazia hayo mambo mabaya, ila hata hakunijibu akanishika mkono na kuanza kunikokota tukarudi kukaa, ila hakuwa na amani kabisa, kwa maana hakuwa anataka hata mtu aniangalie, na sikuwa najua ni kwanini, kwa maana nikimuuliza ananimbia ety kwa kuwa wanawake wanaojiuza wanakuwaga na alama so watu wakiniangalia tu huenda wakanitaka na siku hio nilikuwa nae, so analinda heshima yake….
Sikutaka kubishana nae kabisa, kwa maana hio jeuri ya kumlipa pesa anayotaka sikuwa nayo, basi akataka nkunirudisha nyumban, ila kwa ninavyojua maisha ya kule kwetu, yaan mtu anipeleke na gari itakuwa matangazo mtaan, nikashangaa anaanza kugomba…
“ yaan hautaki nikupeleke nyumban kwa sababu unajua kuwa kuna sehemu zako unataka kupita si ndio, waambie hao wanaume wako kuwa umeshachumbiwa, nikabaki nimetoa macho tu, na akanishika mkono na kuanza kunikokota kwa lazima kuelekea kwenye gari lake, sikubisha na akawa kila dakika tukiwa kwenye gari ananiashika mkono, ni kama hakuwa anaamin kuwa amenipata, tumefika nyumban akaniacha mlangon kabisa wa nyumba ninayoishi, sasa kuna kijana akapita na kutusalimia, alikuwa anapita zake tu, nikashangaa leon anasema “ usiwe unasalimia salimia watu hovyo wengine ni wake za watu, yaan mpaka nikaanza kuona aibu kwa maana Yule kijana alitugeukia na kutikisa kichwa tu kisha akawa anaendelea na mambo yake…
Mbona ametuangalia kisha akatikisa kichwa, nina uhakika ananionea huruma kuwa nasema kuwa mke wangu ni Malaya, sijui kwann haukuwa unajituliza wewe bint, kwani ungesema kuwa unatulia ungepungukiwa na nini, jifunze kujiheshimu basi hata kidogo, nikawa nashangaa sana kuwa yale maneno yote yanatoka wapi….
Sikutaka kubishana nae, nikamuomba aende na nikamshkuru sana kwa kunifikisha nyumban, basi siku hio nilikuwa nimechoka sana, nikatupa simu huko, na mdogo wangu alikuwa amepika ila hata sikula, akala yeye na mama tu mimi nikalala zangu, aiseee kumbe leon amenipigia simu weee nikawa sipokei, asubuh na mapema nikawa nasikia mlango wa nyumba ambayo tulikuwa tunaishi unagongwa tena kwa fujo, akaenda kufungua mdogo wangu, nikasikia mtu anaingia ndani kwa fujo kisha akasema “ lulu yuko wapi, akaambiwa kuwa amelala, aisee Yule mama akaja mpaka chumba ambachgo nilikuwa nimelala na kuniweka kibao kisha akasema “ yaan wewe umelala kwa amani lakin mwanangu umemlaza macho, hivi unajua ulikuwa unamtesa mtoto wa nani? Akauliza Yule mama mpaka nikawa namshangaa…
Hakutaka hata kunipa nafasi akawa amenishika mkono na kuanza kunikokota, mama yangu alikuwa anaumwa so asingeweza hata kumzuia na mdogo wangu alipojaribu aliwekwa kibao hicho na Yule mwana mama, akanikokota mpaka kwenye gari , tukaenda mpaka kwenye jumba moja kubwa la kifahari, Yule mama akanikokota mpaka kwenye chumba kimoja nikamkuta leon amelegea kana kwamba alikuwa analia usiku kucha, tulivyofungua mlango nikasikia anasema “ kama hamjamleta lulu wangu naomba mtu asiingie hapa…
Nikaita “ leon, aiseee alikurupuka na kuja kunikumbatia kwa nguvu na kuanza kunikiss kwa fujo bila kujal kama mama yake alikuwa pale, kisha akasema “ jana usiku ulikuwa wapi mamaa kwanini haukuwa unapokea simu zangu, nikabaki nimetoa macho kwa maana hata sikuwa nimesikia kama amenipigia, na hata kama amenipigia ndio awe vile kama mgonjwa mahututi, nikaona eheee hapa kazi ninayo….
NAKUJA….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote