PENZI LA KAKA, ni mkasa unao muhusu Joan na suma
Ni ndugu wawili walio ishi kwenye mazingira magumu kwenye utoto wao
Suma akiwa kama kaka alibeba jukumu la kumlea mdogo wake kwa mapenzi yote alihakikisha anafanya kila aina ya kazi
Mpaka pale maisha yao yalipo badilika na kuwa safi , maisha yalikuwa ya furaha na upendo mkubwa
Mambo yalibadilika pale suma alipo anza kupata hisia za mapenzi kwa joan ,mwanzo alijizuia lakini joan alipo anza mahusiano huko nje ,ulizuka ugomvi mkubwa kati yao ,
Suma akaamua kutimkia nje ya nchi ili asiwe karibu na Joan tena kila mtu aishi maisha yake
Joan anakuja kugundua Suma Hakuwa kaka yake wa Damu , nae anaamua kwenda huko kumtafuta suma wake ,,
ilikuwaje mpaka akamlea yeye,
Yote utayajua ndani ya mkasa huu wa mapenzi
PENZI LA KAKA ♥️01
Mie majina yangu naitwa Joan , nimezaliwa hapa Dar es salaam na nimekuwa hapa Dar , Mie bwana siwafahamu kabisa wazazi wangu , nimejitambua yaan ile kupata akili nipo na kaka yangu Kaka yangu kipenzi kabisa Sumaa , Suma ni kaka yangu wa damu ananipenda kuliko yeye anavyo jipenda alinipa kila kitu nilicho hitaji kipindi nina umri mdogo hakutaka nionewe na mtu hakutaka nisimangwe wala mtu aniseme vibaya Siku zote alikuwa ananiambia kuwa mimi nipo sawa kwa chochote sikosei isipo kuwa watu ndio hukosea Kuhusu wazazi wetu kaka alinambia walifariki alianza baba akamuacha mama mjamzito na mama alifariki baada tu ya kunizaa mimi Namuonea huruma sana kaka yangu alipitia mengi sana ili kusimama Maana nakumbuka kipindi najitambua kwa mbaliii , tulikuwa na maisha magumu sana Lakini kaka hakutaka niteseka hata kidogo , kaka amepambana sanaaa sanaa nakumbuka mpaka nafika darasa la tano ndio maisha kwetu yalianza kubadilika Baada ya kaka kuacha ma kazi yale magumu magumu ya kibarua akafungua kijibiashara chake cha uwakali wa kuweka na kutoa pesa akawa anauza uza na bidhaa ndogo ndogo Mungu alituona hapo akatambua jitihada za kaka taratibu duka lilikuwa kubwaaa akafungua na Pay point kubwaa sana ikawa maarufu Hapo alifungua na matawi tofauti ya uwakala Na Jina kubwa la biashara lilikuwa ni Js pay point yaan Joan pamoja na Suma kaka yangu Mpaka namaliza darasa la saba sisi maisha tulikuwa tumetoboa kwa kiasi kikubwa sanaaa Tayari tulikuwa na nyumba kubwa sanaa, gari mbili za kutembelea , kaka alifungua maduka ya nguo kama mawili makubwa tu akaweka watu Nitake nini mie kwa kaka nikoseee?? Nilifaulu vizuri kwenda secondary , shule sikuwa ndezi kabisaaa , kaka akikuwa ananihasa sana nisome mana yeye hakusoma zaidi aliishia darasa la nne akaingia mtaani kupambana na maisha ili kunilea Na mie sikutaka kumuangusha nilikuwa nakimbiza shule ya msingi sikuwahi kushika nafasi ya pili tangu nimeingia Darasa la tatu ni namba mojaa Kaka alikuwa anafurahi sana Baada ya matokeo kutoka nimefanya vizuri akanambia nichague shule yeyote atanipeleka yaan hapo sasa hakuna tena kusomea hizi saint kayumbaa Nilimwambia anipe muda wa kutafuta shule , nilijaribu kuulizia ulizia shule nzuri lakini sikupata Kaka alipo rudi jioni akaja na shule moja ipo Arusha, akanambia hii shule ni nzuri inafundisha sanaa Nilikubali kwenda tena Boarding , nilikuwa natamani sana hao walio kuwa wanasoma shule hizo Hatimae na mimi naenda boarding school?? Sikuwa na la kusema zaidi ya kumshukuru mungu kwa kuiona familia yetuu Kaka alifanya mipango yote na mie nikasajiliwa hapo , siku ya ku report shule kaka alinipeleka Nikapokelewa kwa taratibu zotee kabisa , nikawa mwanafunzi na mie wa shule kubwa nzuri hapo wanasoma watoto wengi kwao zipo pesa za kutoshaaa Kabla ya kuondoka kaka aliniita akanambia joan umekuja huku kusoma mdogo wangu fata kusoma hivi unanielewa ?? Nikamwambia kaka nakuelewa kwa hilo wala sintakuangusha nakuapia hata usiwazee Akanambia marafiki wa kiume sitaki kuwasikia achia mbali kuwaona umenielewa wewee?? Nikasema ndio nimeelewa hata mie siwataki Akanambia naaamini hauwezi kuniangusha Elimu ndio msingi wetu sawa nikasema sawaaa Basi kaka akaondoka nikabaki mimi shulee, nikawa form one , niliisoma Form ine vizuri sana , kila mwisho wa wiki kaka anakuja shule Tunatoka ananipeleka mjini na nunua ninacho taka tunakula mpaka jioni ndio ananirudisha kama kaja jumamos analala Lodge, juma pili tena anakuja kunichukua hivyo hivyoo Kaka alikuwa maarufu shule.gafla kila mtu alikuwa anamjua mana ndie mzazi pekee ambae kila wiki lazima afike shule Walimu walikuwa wananiambia kaka yako anakupenda sanaa mie nacheka , Kwahiyo sikuwa napata ule muda wa kuzurula na marafiki kabisaaa, shule kama mawaida matokeo yote ya form one nilkuwa nacheza na mbili na tatu sikuwahi kuwa wa kwanza au kuvuka namba tatu Kaka hakuwa anapenda kabisaaa , likizo alinitafutia mwalimu wa tuition akawa ananifundisha Ile likizo yote ya form one kwenda form two sikupumzika nikusoma tu kusoma tuu Na mie nilikaza ili nikirudi shule kaka afurahi ... Basi bwana mie nikaingia kidato cha pili , hapo ndio nilikutana shoga angu huyuu alikuwa anaitwa kemmy .. Kemmy alikuwa amehamia shuleni kwetu kidato cha pili ametokea singinda ITAENDELEA...
PENZI LA KAKA ♥️02
khemmy ni mschana alihamia kutoka singida alitukuta tupo kidato cha pili, Mwanzo nilikuwa nalala peke yangu , sa alipo kuja kemmy tukawa tunalala wote , yeye juu mimi chinii, ndo hapo ukaribu wangu na yeye ulianza ... Alikuwa shoga angu sanaa, kaka alipo kuwa anakuja w/end tunatoka nae yeye familia yake ipo mbaliii Kwa vile alikuwa mpoleee kweli kaka akamkubali kuwa rafiki yangu Ila tu akanionya sana nisijichanganye na wanaume hilo ndio lilikuwa onyo lake kubwa kwangu ... Form two ilipita salama kabisa nikaingia form three hapo ushosti na kemmy ulikuwa umezidi kunogaa sanaaa , Likizo ndogo ndogo hzi anakuja nyumbani kwetu haendi singida tunakaa mpaka shule inafunguliwa Kaka alikuwa ananiruhusu wiki moja kwenye likizo ndefu mfano mwezi wa 6 naenda nyumbani kwao kemmy nakaa then narudi Kemmy alikuwa anampenda sanaa kaka suma , mwanzo nilikuwa namuhisi mana kumsifia kila saa kaka ako mzuri yaan suma handsome mara mpenzi wake na suma ni naniii ?? Mimi sijawahi kumuona Suma na mwanamke maisha yangu yotee mpaka nafika hapa leoo sijawahiii kabisaaa Nikawa namwambia suma hana mwanamke anatafuta kwanza maishaa , sasa akaanza kuwa anajipendekeza kwa kaka akija kutuchukua w/end hivi Kemmy ni kujichekesha masaaa yote kujishaua hakuishii yaan anakuwa na kamchecheto flani hiviii mie mpaka ananitia aibuu Suma alikuwa anamkatia juu juu lakini kemmy wapiii , siku moja Ilikuwa likizo ya kumaliza mwaka hapo tunaingia kidato cha nne , Khemmy alikataa kwenda kwao akasema anataka kukaa kwetu Na kwao tulikuwa tumejenga ukaribu sana haikuwa shida akabaki nyumbani , Yaan khemmy bwana , Siku enyewe naamka usiku simuoni kitandani nikashangaa choo kwetu kimo ndani sasa ameenda wapi huyuu Ilibidi niinuke kumtafuta nilikuwa na wasi wasi kidogo nikatoka sebleni nashangaa kusikia watu wanaongea kwenye chumba cha kaka , Kaka yeye chumba chake kilikuwa chini mimi juu nyumba yetu ni ghorofa moja , basi nikaanza kushuka taratibu huku nazidisha umakini kusikia Nikasikia sauti ya kaka anasema Aisee tutabadilikiana sasa hivii mimi sio mstaarabu kiasi hicho embu toka humu!! Sasa nikasema mungu wangu anamwambia nani huyu kaka akasema tena toka Mmh nikasema mungu wee isije kuwa khemmy mbona aibu hii jamani kabla hata sijaipa majibu akili yangu nikasikia sauti ya khemmy anasema yaan suma mbona umenidhalilisha tayari umeshaona utupu wangu tayari umeona au mie nina kasoro?? Heee nikasema makubwa haya jamani yaan huyu bibie ndio amefikia hukuuu?? Mmh kaka akamwambia Kuna sehemu hatujaelewana wewe kwangu ni kama dada tu hakuna zaidi naomba vaa nguo zako nenda na Joan asije akajua hili sijui unanielewa?? Nikahisi kama mlango unafunguliwa nikajibana kwa sec nilivyoona kimya nikawaza itakuwa anavaa huyo atoke nilikimbiaa kurudi chumbani kwangu Nikaka kitandani zilipita dakika zaidi ya 20 ndio Khemmy akaingia , alipo nikuta macho alishtuka nikamuuliza we nae umetoka wapiii akanambia iwe siri yetu sawa nikasema usijali nambie akanambia kuanzia leo mie wifi Yako, kaka yako amekula tunda langu Mmh nikasema wee kweli akasema hakiamungu tenaaa ona akanionesha et ute ute chini duuh nikasema tu Hongera nimefurahi mana sijawahi kumuona kaka na mwanamke yeyote akasema ukimuona nae tu niambie nikasema usijari kabisa Mie nilimpenda khemmy kwanza ni mzuri sana tu kwahiyo sikuona shida kuwa na kaka yangu .. Sasa muda mwingi niliokuwa na khemmy alikuwa anaongelea sana mambo ya wanaume mapenzi mapenzi yaan hizo ndio story zakee hakuna lingine Mie kwenye masomo nilikuwa nakimbiza wa kwanza yeye alikuwa anashika namba 6 huko mpaka kumi yaan kifupi hakuwa makini kwenye masomo kwanza kwao wanapesa sana sikutaka kujifananisha nae Tuliingia kidato cha nne bado khemmy alikuwa ananiambia anamahusiano na kaka yangu na anampenda sana namie sikuwahi kumuambia et ule usiku nilisikia naongezi yao hapana nilikuwa kimya Kaka alikuwa anamkwepa kweli khemmy ilifika hatua akanambia mie marufuku kwenda kwao na khemmy, Hata khemmy alikuwa anamkataza kuja kwetu ikifika likizo kaka anasema tunasafiri kusalimia ndugu lakini sie hatuna ndugu tupo wawili tu Tunaondoka ananipeleka zanzibar huko tuna enjoy huko mpaka likizo inaisha aisee kaka angu alikuwa ananipenda mnoo hakuwa anataka niteseka hata kwa sec , kaka alipunguza zile safari za kuja shule kila W/end na nilihisi ni kwa sababu ya khemmy sikupenda kabisa kwa mbalii khemmy alianza kunitoka rohoni nilimuona kama ni msumbufu kwa kaka yangu sanaa mpaka kaka inabidi anikwepe mimi kwa sababu yake .... Mie nikavunja ungo nikiwa kidato cha nne , nilichelewa sanaaa wa kwanza kumwambia alikuwa shoga angu khemmy akanambia umekuwa dada hongera nikasema asante akawa ananielekeza baadhi ya vitu mana yeye alivunja ungo yupo shule ya msingi kwa maelezo yake.. kwa hiyo ni mzoefu wa hayo mambo, Gafla tu nilitanuka sanaaa nikapendeza yaan shape ilijitokeza hata sijui ilikuwaga wapii...... ITAENDELEA......
PENZI LA KAKA ♥️03
Nilipendezaa mpaka mwenyewe nikajiona nimependeza, rangi ikawa moja kama chungwa , nilikuwa wa kishua gafla yaan mwenyewe nilibaki nashangaa imekuwajee?? Nilianza kusumbuliwa na wanaume, sio wanafunzi wala walimu , kulikuwa havikaliki , shule nilikuwa joan ndio joan mrembo wa shule , et Khemmy akaanza kuwa ananuna vile nilikuwa nasifiwa Wakati mwanzo yeye alikuwa anasifika kwa ule weupe wake na urefu alikuwa anapewa mauwa yake , mie sikuwa na shape hataa nilikuwa kawaida tuu yaaan mwili nilikuwa nao nilikuwa mweupe lakini kawaida Sijui mnaelewa nikisema mambo yalibadilika gaflaa tako nilikuwa nalo lakini la kukalia sasa likaja la kutikisia eeh mungu wee hizo hips nikang'aaa, ngozi ikawa rainiii .. Khemmy akaanambia Joan kuna mwalimu amenituma et anakutaka mmh kwanza nikaguna mie sijawahi kutongozwa lakini sasa hivi sio hao walimu sio wanafunzi nikaamuuliza mwalimu gani akanambia mkuu wa shule Wee nilishtukaa , we khemmy embu acha utani umeanza lini kuongea na mwalimu tena mkuu kabisa akanambia wewee nakuonaga mshamba mshambaa ndo mana mambo yangu sikuambii , nikasema kumbe mwenzangu una mambo mengi akasema ukikua nitakuambia Nikacheka nikamwambia hadi nikue ki vipi sasa ,akanambia embu sema kwanza Unatoka na mwalimu nikasema aah we mie sitaki akanambia yaan nikamwambie unajua mie sisomi wala sijawahi kufel kwanini Nikasema sijui akanambia kwa sababu natoka na George , Nilishangaa nikasema au sijaelewa akanambia na hautaelewa si unajikuta wewe bado mtotoo ,unahangaikaaa kusoma date na Sir mmoja tu tena wa juu sio hawa vibaraka uone maajabu utasahau hata mara mwisho kufunua daftar na namba yako itabaki ile ilee dadaaa... Nilichoka akili mana huyo George ni Second Master.. Nikamwambia wewe Khemmy kwahiyo kaka yangu huwa unamuongopea?? Akanambia kaka yako mzuri sema hana nguvu za kiume bwana ... Hee !!! Hili tena likawa jipya kwangu nikasema unasema nini wewe?? Akanambia yaan kaka yako amejaariwa mashine lakini haisagi wala kukoboa angekuwa mwanaume kamili yule ooh anaonekana mtamu achaaa Hahaah!! Nikamwambia we embu tumia lugha nzuri yule ni kaka yangu bwana usiongee kama unamuongelea mshakaji wako akanambia ndo nakuchana kaka ako mpini wa buree rungu halisimami lilee .. Nilijisikia vibaya nikamwambia lakini wewe si ulinambia kaka yangu amekula tunda lako na kila mara ulinambia upo na bro?? Akanambia nilikuwa natafuta nafasi nilijua ipo siku nitakuwa nae Lakini sasa nikuambie wala nisikufiche shoga angu nimevua nguo mbele ya kaka yako sio mara mojaa lakini hata haishtukii imelegeaaa kama pira khaa , huo u handsome buree bora hata angezaliwa wa kike angeolewa ... Nilitamani nimuweke kibao mshenzi wa tabia huyuu, nikamwambia tu bwana atajua mwenyewe bwanaa .. Niliamua tu niuwe ile mda kwa staili hiyo , tangu hapo sikuwa na raha kabisa yaan nilijikuta siku yangu inakuwa nzitoo Niliumia kichwa sana kuhusu suma au ndo mana sijawahi kumuona na mwanamke?? Na ndio mana siku hizi hataki kuwa karibu na Khemmy yaan anamkwepa kumbe anamuonea aibuu daah Nilijiuliza maswali mengii mpaka nikajikuta nalia kabisa nilimuonea huruma kaka angu na alivyo mzurii aisee suma hakuna mwanamke anamuona harafu anakaa kimyaa yaan bila kusema lolotee?? Aah wapi utakiri hata moyoni lazimaa amejaaliwa kila kitu kaka angu ni Mtanashati wa haja , hata nimuelezee vipi siwezi mfiti elewa ni zaidi ya Gentlemen .... Maisha na khemmy yakaendelea yakawaida lakini story zilibadilika siku hizi ananiahadithia kuhusu bwana zake tuu yaan hapo nikasema aisee mie kweli huyu binti nilikuwa simjui W/end akanambia Joan mie nataka kwenda kutembea dada angu amekuja twende wotee , Kaka alishanikataza kutoka kabisaa lakini kwa vile haji shule nikaona wacha niende mana dada yake Khemmy nilikua namjua vizuri tu Tukajiandaa vizuri mwenzangu, khemmy akanambia nakulipia usafiri we hata usijali nikasema sawa, Tukatoka Safari mpaka kwenye hotel moja ipo nje nje kidogo ya jijii ni mbali pia na shulee mpaka nikamwambia Khemmy tunaweza kuchelewa kurudi shule mana ni mbali akanambia hata usijali kila kitu mie nitashugulikia nikasema hayaa Tukaingia kwenye hiyo hotel tukapandisha mpaka kwenye moja ya chumba , sikuwa na shaka mana najua dada ake tu hakuna shida Akabisha hodi mlango ukafunguliwa ila sikuona aliefungua Khemmy akanambia ingia tu mie nikaingia Hee nyuma ya mlango si ndio namuona Headmaster , mungu wangu moyo ulifanya paaa!!! ITAENDELEA...
PENZI LA KAKA ♥️04
Moyo ukashtuka baada ya kumuona mkuu wa shule tena lipo tumbo wazii lina cheka cheka chini lina pensi tu khaa !! Nilimgeukia khemmy hii ninii?? Namuuliza moyoni hapo mdomo haufunguki khemmy akawa anacheka cheka na yeye Li mwalimu likanambia njoo mrembo uketi njoo ,,, jamani mwili ulikuwa unatetemeka kweli Nikamwamkia shikamoo akasema aah hapa sio pa shikamoo bwana ha.ha ha .. Et linacheka yaan kama li jingaaa tu vilee , khemmy akamwambia sasa boss mie ndo huyoo malizana nae hivyoo we ongea nae taratibu tu ... Hapo anaongea huku anainuka kutoka , jamani khemmy mbona sikuwahi kumuona hivii mbona nilimchukua ni mschana mpole sana , hata nilipo sikia anamahusiano na kaka yangu nilifurahi Kumbe kuna rangi yake halisi alikuwa anaificha yaan kuna upande wake mwingine sikuwahi kuujuaa ?? Daah !! Niliumia sanaa Niliinuka kabla hata hajafungua mlango , nikamwambia Khemmy please usinifanyie hivii nakuombaa , Headmaster akanishika mkono akanambia keti tuzungumze nitakupa pesa nzuri nipe tu kwa usiku wa leo basi kama hutaki mahusiano na mimi " Khaa!!! Huyu baba hivi anajisikiaa kwelii, nilimtazama nikamwambia sikia wewe mimi sio maraya sawa huyo alienileta hapa anaweza kukuhudumia tu , Akanambia unanijibu hivyo wewe kama nani?? Nikamwambia kama Joan enhee ulitaka nikujibu vipiii..?? Khemmy akanambia we joan embu jiheshimu unamjibu hivyo mkuu wako , nikamwambia mkuu kwako sio kwangu tena mnikomee mbwa wawili nyiee!! Nilijibu huku natokaa ,Headmaster akanambia we mtoto et mie nani nikasema huna adabu huna tofauti na mbwa, akacheka kile kicheko cha uchungu akanambia utaijutia hii siku ya leo yaan unaharibu maisha yako ya yote kwa dakika chache sanaa , polee sanaa ... Sikujali hata anaongea nini lakini nilielewa sana anataka kunifelisha mana huyo mjinga mwenzie si ndio alikuwa ananiambia nikimkubali nifaulu bila hata kusoma na yeye huwa hasomi lakini hashiki mkia hata kidogoo Mie aiamini akili yangu sana tu , sikutishika na maneno yake ,, bahati nzuri nilikuwa nimebeba akiba , nikachukua usari mpaka shule Mie nilifika kabla ya khemmy , nikaingia moja kwa moja bweni , yaan nilikuwa na hasira sana khemmy alinikosea sikutaka hata kuwa karibu nae Nikamfata mschana mwingine huwa analala peke yake , nikamuomba kuhamia kwenye kitanda chake akasema sawa, nilitoa vitu vyangu mpaka khemmy akanakuja nishahama Halafu alikuja usiku kabisaa, akanambia Joan naomba tuongee huku mie nikainuka kumfata huko nje Akanambia yaan wewe mie nimekusogezea mpira miguuni mwako we umesusa wakati ulikuwa unashinda kwa shuti moja tu !! Nikamwambia sijakuelewa nenda moja kwa moja, akanambia Unajua Teacher anakupenda sana joan mkubali utafaidi mengi mie nimekufanyia hivyo sababu nakupenda dear sio kwa ubaya" Nikamwambia sikia Khemmy kuanzia leo sitaki hizo story zako sawa, halafu mimii naijua akili yangu sio kama wewe mjinga Akacheka akanambia haya tutaona sasaa , mie hata sikumjibu kitu nilimpita tu nikarudi zangu kulala ... Asubuhi nilikuwa nipo nafua nikaja kuitwa kuwa kaka angu amekuja , na vile nilikuwa nimemiss nilifurahi kweli amekuja ,, yaan tangu Khemmy anipe story zake , sijamuona na nimezidi sana kumpenda kaka yangu sijui ndio kumuonea huruma hata sijuii ... Nikatoka mbio mpaka kule alipo kuwa kweli nilimkuta kaka angu kipenzi amesimama pembeni ya gari yake alipo niona tu alini hug hiyo ni kawaida sana kwake akanambia nilikumiss sana ujue we katoto, nikacheka akanambia ulikuwa unafanya ninii nikamwambia nilikuwa nafua tu akanambia jana ulikuwa wapi mpaka hukufua nikamwambia nilikuwa nimelala tu akanambia kwelii nikasema Yeah , Akanambia ninakuamini huniongipei mie nikacheka tu , akanambia unacheka kama mazuri eeh , nikazidi kucheka Akanambia nimekuomba tutoke mara moja lakini ni mimi na wewe tu yaan wawili nikasema sawa kaka Moyoni nikawaza hata khemmy najuta kumsogeza karibu yako kaka mana anakucheka kwa madhaifu yako, kidogo chozi linitoke ila nikajikaza .. Akasema nitamuwahisha kuja kufua saw nikasema sawa , Alinipeleka sehemu moja hivii kama hoteli hata sijui ila sehemu ya kula na michezo kibao , Akaniagizia chakula kizuri tu Akanambia joan mdogo wangu ,nikasema abee Hapo alikuwa makini kidogo nikaogopa anataka kusema nini Akanambia unaniona mimi mdogo wangu, mimi sijasomaa kabisa , unalitambua hili si ndio , nikasema ndio natambua kaka Akanambia nguvu zote nimeegemeza kwako natamani uje kuwa mwanamke mwenye heshima sana mtu akilitaja jina lako basi alitaje kwa heshima na adabu zotee Nikamwambia Asante kaka nitafanya kila kitu ili ndoto zako zitimie kupitia mimi !! Akanambia okay , sintakuuliza jana ulikuwa wapi kama hautahitaji kunambia wala sintakulazimisha lakini naomba sana sana sana Joan acha kuzunguka Wewe ni mrembo sana , na kipindi hichi utapitia majaribu mengi sana Kila mtu atasema anakupenda kila mtu ataonesha anakupenda , kila mtu atakusifia wewe ni mzuri lakini hakuna atakae kuwa anamaanisha Kwenye hii dunia mimi pekee ndie ninae ujua uzuri wako, mimi pejee ndie najua nakupenda kiasi gani Joani kwenye hii dunia hakuna mtu atakupenda kama mimi ninavyo kupenda!" Mmh yakanishukaa kaaka alikuwa Serious , akanambia jana nilikuja kukutembelea na kukupata ulitoka naomba uzingatie masomo joan ,Joan tafadhali """ Nikamwambia kaka nimekuelewa naomba sana unisamehe hili halitajirudi akasema tu sawa , basi tulikula tukawa tunapiga story zetu za hapa na pale huku na kulee , akamaliza miladi yake inaendeleaje , biashara imekuwa akanambia kila kituu Nikamuuliza sasa kaka wewe umeshapata maisha unaoa lini akanambia mpaka wewe upate maisha ujitambue hiyo siku nitaoa , nikacheka nikamwambia mie kaka natamani tuwe na familia kubwaa sie tupo wawili tu hatuna ndugu hata akanambia lakini sie ni bora kuliko hizo familia Joan eeh , nikasema kwelii sie tunapendana sana mie nina bahati kaka angu mzuri.ananipenda sanaa mpaka najionea wivuu, akacheka akanikumbatiaa ITAENDELEA .
PENZI LA KAKA ♥️005
Basi akanirudisha shule , baada ya kula na shopping kama zotee , nikatulia zangu kaka akaondoka zake Sasa nilikuwa nipo natizama baadhi ya vitu kaka alivyoninunulia nipo naangalia zangu akapita khemmy akanitazama akacheka akanambia nilikuwa na kaka ako leo alikuja , mie sikumjibu mana ashakuwa mnafiki sana kwangu huyuu Akanambia mkiwa mnanunua vitu embu jaribuni na nguvu za kiume kutafuta na wewe za kike mana wote nyie mahanisij afu mkiambiwa ukweli mnajinunisha !! Daah !!! Nilimtazamaaa jicho la hasiraa , huku najutaa yaan natamani siku zirudi nyuma huyu nisimkaribishe kabisa kwenye familia yangu , ... Kila mtu anamuhadithia kuhusu kaka angu et hanithi jamani, na vile kaka angu ni maarufu hapo shule kwa kuwa anakuja mara kwa mara na ile mwonekani wake aah Nilitamani hata kumwambia kaka lakini naanzia wapiii?? Siku zilienda tukafanya mtihani wa moko kata , nilisoma kwa bidii sana sana kama kawaida yangu lakini matokeo yalikuja nimeshika nafasi ya 20 Sio mimi tu kila mtu alishangaa kila mtu Kaka ndio kabisaa alifunga safari kuja tena walikuja na rafiki yake mmoja huyo tangu nakuwa namuona yupo karibu na kaka yangu yaan yeye anatujua sie kindaki ndakii .. Kaka akanambia Joan naomba uniambie unashida ganiii tafadhali niambie ukweli kwanini umefeli kiasi hikii , jibu la kumpa mie sina nina uhakika kabisa kwenye majibu yangu nilifanya vizuri sasa imekuwje Nilibaki nimeinamisha uso chini jibu la haraka sinaa Yule rafiki yake kaka anaitwa fredy akanambia Joan umeanza mahusiano?? Moyo ukafanya paaa !! Huenda na kaka ndio anafikiria hivyoo , Nilisema hapana kaka hapanaa mie sina mahusiano yeyote yale , kaka akaniuliza kwa ukari sasa mbona umefelii yaan kutoka wa kwanza mpaka 20 tena huku mwisho unaenda kumalizaaa?? Kaka alikuwa na hasira nilipiga magoti ,nilijua nimemkosea sana nikamwambia kaka Nisamehe wakati huu nitafanya vizuri Nilimuomba mnoo mpaka fredy nae alianza kuongea na kaka anisamehe , kaka akasema sawa ila niahidi hauta jiingiza tena kwenye mahusiano mpaka muda utakapo fika nikasema nakuahidi kaka yangu ..... Niliongeza bidii mno kwenye masomo sikutaka kucheza hata kidogo nilikua bize na kitabu , sikutaka shoga wala rafiki Mkuu wa shule alikuwa ananifata mara kwa maraa nimkubalie ombi lake atanipa ufaulu la sivyo nitafeli Niliamini yeye sio Necta kwahiyo hawezi kuamua kuhusu mayokeo yangu , isipo kuwa kitabu na akili yangu tu Tulifanya mtihani wa moko mkoa ,aisee matokeo yanatoka ni mtu wa 35 kati ya wanafunzi 36 , nilichokaaaa hata mguu nilishindwa kusogezaa Halafu khemmy et amekuwa wa kwanzaa , yaan kivipiii?? Hapo ndio maneno ya Headmaster yakaanza kujirudia tena kichwani upyaa kama ndio naambiwa leo , nililia mbele ya matokeo hapo kila mtu ananitazama sikujalii nililiaa Yule dada nilihamia sehemu yake ndio akawa ana kazi ya kunibembeleza ... Kaka alikuja baada tu ya kupata matokeo yangu , walikuja wote na fredy , nilikuwa bweni nimekuja kuitwa nilitoka mbioooo moyo unaniuma maneno ya kaka kuwa kwenye hii dunia yeye tu ndio ananipenda sasa niliyaelewa Nilifika alipo naliaaa akanikumbatia bila hata kuongea kitu , baada ya muda akanambia panda kwenye garii nikapanda Akanambia kuna mtu anakutesa?? Nikasema ndio kaka akanambia ni boyfriend nikasema hapana kaka akanambia ni nani ,nikasema Headmaster akanambia embu nambie vizuri!! Nilimuelezea kuanzia ile siku Khemmy amenambia ujinga mpaka ile siku aliyonipeleka kule kuonana na huyo mwalimu halafu yeye akaniunganisha Nilimuelezea mpaka meneno ya mwalimu atanipa ufaulu kama nitakubalii, na hili la Khemmy kuwa wa kwanza ndo nimethibisha hanaa akili hizo ... Kaka alianza kutetemeka mwiliii , macho yakawa mekunduu, ohoo hata sijamaliza kuzungumza mana nilikuwa naongea huku naliaa tena kwa kwikwiii Tena najiona kabisa nafeli kidato cha nne na jitihada zote zilee.. Kaka akanambia nakuja tulia humu humuuu , akashuka kwenye garii , freddy akafata nyuma akanambia usishuke hata iweje , nikawa sielewi bado Hazikupita hata dakika tano nikaanza kuona watu wanakimbizana ofisini kwa mkuu wa shule nikaangalia hee namuona kaka yangu anamtoa mkuku mkukuuu kamkabaa koo huku anampa vichwaa Nilishtuka mpaka tumbo liliniumaa , Headmaster anatoka damu , nilipiga kelele kwa kuita jina la kaka Sumaa!!!! ITAENDELEA...
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote