Ninah

book cover og

Utangulizi

NINAH

NI story kali inayomuhusi Binti Ninah, Binti ambaye hakuwai kujua mapenzi ya baba baada ya baba yake kufariki yeye akiwa na umri Mdogo.
Katika vitu ambavyo Nina alifaidi ni uwepo wa mama yake ingawa umasikini uliamua kuwatenganisha.
NINAH Anakutana na dhoruba, maangaiko na kila aina ya shida kwenye maisha yake.
JE NINA ATATOBOA ?, ATATOBOA KWA NJIA GANI ? TUKUTANE NDANI NDANI UKU TUKAPATE UONDO…..

NINAH
MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 01
ANZA NAYO.........

Niite NINAH binti pekee kwa wazazi wangu, mimi nimelelewa na single mama, sio kwamba baba yangu alikataa kulea ujauzito hapana, yaani baba angu alifariki pale tu nilipofikisha umri wa miaka 2.
Naweza kusema mama yangu ni super woman wa maana jamani, amepambana kwa kila hali kuhakikisha kuwa napata mahitaji yote muhimu, mama Ninah yuko tayali kutembea peku kwenye jua kali lakini mimi nivae viatu, alikuwa tayali kulala njaa lakini mimi nishibe, alikuwa tayali kuvaa nguo chakavu lakini Mimi nistilike.
Niseme kuwa nimeishi nikiwa naangalia ni jinsi gani mama angu anaangaika na kuteseka, mwanzo sikuwa naelewa kutokana na utoto lakini kila siku zilivyozidi kwenda, nilikuja kugundua kuwa mama angu anateseka sana kwaajili yangu.
Kauli mbiu ya mama yangu ilikuwa ni Ninah Soma Soma, Ninah hakikisha kuwa umuachi elimu akaenda zake, Zatima hakikisha kuwa unakuwa na testimony nzuri kuhusu elimu yako.
Kwa upande wangu naomba nijipe maua yangu bhana, nilikuwa msichana fulani hivi, muelewa, msikivu na mwenye utu na utulivu wa hali ya juu.
Ninah mimi nilijua kushika maneno ya mama yangu, niliweka akili yangu yote kwenye masomo, nilijiepusha na mahusiano muda wote kutokana na mafunzo ambayo nilipatiwa na Mama yangu.
Katika masomo yangu nilifika kidato cha nne na niliweza kufaulu vizuri Sana, nilipata max za juu ambazo ziliniruhusu mimi kuendelea na elimu ya advance level.
Ufaulu wangu ilikuwa ni furaha kubwa sana kwangu na kwa mama yangu, lakini pia at the same time ukageuka na kuwa maumivu pale tu nilipojua kuwa sitaweza kuendelea na shule kutokana na mama yangu kukosa pesa.
Kwa kipindi hiko, nikipambana na mama yangu kila kona kuhakikisha tunapata pesa za kuniendeleza mimi na shule lakini haikuwa rahisi, na hii ikanikatisha tamaa, niliona wazi kuwa ndoto zangu za mimi kuwa Ness mkubwa zimeshakufa mapema sana.
Niliamua kukata tamaa kabisa na kuendelea tu na maisha mengine, kwa kipindi hiko sikujali uzuri wangu ata kidogo na niliangalia sana maisha, nilimsaidia Mama angu kuuza mboga mboga mitaani ili tuweze kupata pesa ya kula lakini pia pesa ya kodi.

SONGA NAYO......

Hatimaye mwaka mzima ulipita Ninah mimi nikiendelea kupigwa na jua kwa kuzungumka mtaani na mboga mboga, kwa wakati huo, wanafunzi wenzangu walikuwa wameshaingia kidato cha sita na mimi niko tu mtaani.
Ukija kwa Mashost wenzangu wa mtaani, walifanya kila aina ya starehe, walipendeza na kila kitu, kuna muda nilitamani kuwa kama Wao uku nikiamini kuwa wanamaisha mazuri sana kuliko mimi.
Swala la kuwa kama wao pia lilishindikana kutokana na mama Ninah kuwa mkali na kunisimamia katika nyenendo zangu zote.
Kama kawaida, mimi na mama yangu uwa tunaingia mtaani pamoja na kurudi nyumbani pamoja, Mama yangu akuwai kuniacha mtaani mwenyewe, yaani ananilinda kila kona.
Mimi na mama Ninah tukiwa mtaani, niliamua kumuuliza mamaangu maswali ya kizushi tu.
"Hivi mama utakuwa unatembea na mimi hivi mpaka lini ?"
"Ninah usianze kabisa, kutembea na wewe ukiwa unamaanisha nini na unajua kabisa tupo kwenye biashara ??"
"Mama ujanielewa, namaajisha hii kuongozana kila kona kama kuku na vifaranga vyake "
"Haya mimi ni kuku na wewe kifaranga, binti nafikili umenielewa "
"Mmmh lakini me nimeshakuwa mtu mzima, saa hizi wewe ungepita Julia me ningepita kushoto kila mtu angepata wateja wake "
"Kifaranga tulia kunguru ni wengi mjini "
Eeeh mama alinipa jibu moja la mwana ukome nikajikuta nikitulia tu maana sikuwa na namna kwa wakati huo.

"Zena, Zena Zena "

Ilisikika sauti nzito kabisa ya kiume ikiitilia jina la mama yangu, basi mimi na mama tukageuka na kuangalia kwa makini ni nani anamuita mama kwa jina lake ikiwa mtaa mzima walimjua kwa jina la mama Ninah.
Kitendo cha kugeuka tu, tuliweza kukutana na mbaba fulani hivi, umri umeenda kiasi lakini pia ni kama pesa ili mstili hivi, hivyo akaonekana kuwa ni mbaba wa kisasa sana.
Mama angu akifurahi sana na kwa furaha aliyonayo, akatupa beseni la mboga na kumkimbilia mwanaume huyo.
Walahi nilipigwa na butwaa, yaani mama yangu anavyojali biashara yake, halafu leo hii anaitupa chini kwaajili tu ya mubaba ambaye sikuwa ATA nikimjua.
Kwa furaha wawili hao wakakumbatiana na kuanza kusalimiana.

"Aaah Zenah sikuwai kufikilia kama kuna siku nitakuja kukuona aiseeeh, yaani daaah, kweli milima haikutani lakini binadamu tunakutana"
"Weeeh mtu jamani, ndio umebadilika hivyo ??" Mama yangu alimuuliza mbaba huyo kuonesha kuwa wanajuana sana.
Kwa upande wangu nikabaki kuwa mpenzi mtazamaji tu 🤣🙌🏻 nikibaki nikiwaangalia na kusikiliza maongezi yao.
"Anyway, nafikili tuna mengi sana ya kuongea kwakweli, na kama unamuda naona tufanye leo maana kesho na weza kurudi dar majila ya jioni " alizungumza mbaba huyo.
"Eeeh kumbe na Moro ulishatokaga kabisa ??"
"Yaaah nimetoka kitambo sana aiseeh "
"Na huyu anayefanana na wewe ndio mjomba nini ?"
Aliuliza mubaba huyo uku akinioneshea kidole.
"Eeh ndo huyo mmoja kama yai mwaya "
"Zena usinambie kuwa uko na mtoto mmoja tu "
"Eeeh ndo huyo Mungu aliyenijaalia "

Story zilizidi kunoga kati yao na wakanisahau kabisa, nilichoka hatari, kiu cha maji kilishika nafasi yake na njaa ndio kabisa, nilikuwa natamani Ata kuzimia.
Baada ya makubaliano yao, mimi na mama yangu , tukaongozana na baba huyo mpaka alikopaki gari yake na safari ya kwenda nyumbani kwetu ikaanza..
Tulifika nyumbani na moja kwa moja tukaingia ndani, nyumbani kwetu hakukuwa na sebule wala nini, yaani tulikuwa tunachumba kimoja tu, ambapo umo umo ni jiko, umo umo ni chumba cha kulala lakini pia ni sebule.
"Karibu sana Benson chato "
Mama alimkaribisha mgeni wake kwa kutaja majina ya kwenye cheti cha kuzaliwa.
"Ahahaha Zena niache bhana, sasa hivi jina la Benson nishalisahau, kila kona ni baba Eddy "
"Eeeh aacha weeeh, haya na wewe una watoto wangapi ??"
"Aaaah ninao wanne, watatu wa kijume, wakubwa sana, maana mkubwa ameajiliwa, wa pili yuko chuo mwaka wa tatu, na watatu yupo kidato cha sita sasa na wanne ndio wakike sasa, binti angu kipenzi anaitwa Mia now anamiaka 8 tu, kapo darasa la 3"
"Eeeh hongera bhana "
"Asante ila umenishangaza sana, yaani miaka yote hiyo bado unamtoto mmoja, tena umri wake kwa haraka haraka ni sawa na mwanangu eddy huyu wa tatu "
"Aaah mambo tu ya kidunia, maisha yapo kasi sana na hatimaye nimezeeka ".
"Zena bhana, umezeeka wapi wewe, sema ujaacha kujiweka nyuma nyuma, unajua ni kitambo sana lakini nakumbuka kila kitu, hivi Daniel mliishia wapi jamani ? Mshikaji wangu bado namkumbuka sana "
Mama aliangalia chini kwa muda kisha akajibu.
"Aaah ndio Baba mzazi wa Ninah, lakini Mipango ya Mungu bhana alifariki Ninah akiwa na miaka miwili ".
"Weeeeh Daniel !, aaah unatania bhana, daaah mshkaji wangu daah "
Basi huzuni ikaanza kutawala, kuna muda nilihisi kuboweka lakini umbea ulinifanya niendelee kusikiliza.
Kwa haraka haraka, mama na huyu mubaba sijui ndio baba eddy, ni watu ambao walisomaga wote miaka hiyo uko nyuma, lakini ndo hivyo, baba eddy katoboa, halafu mama Ninah yuko mbwimbwa yaani katobolewa 😆.
Mama yangu alimsimulia vingi sana baba yule mpaka kuhusu elimu yangu.
"Nafikili nitachukua majukumu ya rafiki yangu juu ya Ninah "
Alizungumza baba eddy na kunifanya nikae vizuri ili nimuelewe ni nini anaongelea.
"Sijakuelewa " mama pia aliamua kuuliza.
"Namaanisha kuwa naitaji kumsomesha Ninah, umri wake bado mdogo na ajachelewa kuendelea na masomo"
Nyieeeeh, nilishindwa kuzuia furaha yangu na kujikuta nikipiga kelele kwa nguvu sana na kuwashtua wote.

"Aaah Benson unanitania ??"
Mama alishindwa kabisa kuamini, hivyo akabaki akimuuliza maswali mfululizo.
Baada ya kila kitu, mama na baba eddy walikubaliana kuwa baba eddy atanisomesha nikiwa hapo hapo na mama yangu, nilifurahi sana kwakweli.
Baada ya maongezi kuisha baba eddy aliaga na kuaidi kuwa atarudi siku inayofuata kabla ajarudi mjini dar es Salam.
HUU NI MWANZO TU TUKUTANE KWENYE SEHEMU YA 2......
NINAH

MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 02
SONGA NAYO……….

Aaaah furaha ambayo nilikuwa nayo naweza kusema kuwa haikuwa ikielezeka , mama angu mwaya, mtu na dini yake, alipiga goti na kumshukuru Mungu kwa kila alichotutendea ikiwa sisi tulishakata tamaa.
Majila ya usiku, Mimi na mama yangu tukiwa tuna pata chakula, mama hakuonekana kuwa Sawa kabisa hivyo nikamuuliza.
“Mama Ninah unawaza nini ??”
“Aaaaaah mambo ni mengi ya kuwaza, nawaza mambo ya muhimu juu yako”
“Mama nawe, kila kitu Kipo Sawa kwa sasa Yaani soon Nina naenda Kuanza masomo, tena amekuja Wakati Mzuri sana, wakati ambao masomo ya mwaka Mpya Ndio kwanza yameanza”
Mama alinikata jicho moja Matata nikajikuta nikijishtukia na kusogea pembeni maana ashindwi kunipiga mbao.
Katika vitu ambavyo mama yangu Avipendi basi ni mdomo mrefu, Nikisema mdomo mrefu namaanisha kuongea sana, na ukija upande Wangu walahi me naongea mno.
“Unabwabwaja tu wala ufikilii, kitu ambacho ujui ni kwamba, niliwai kutelekezwa na Mjomba angu kwa stahili hiyo, Ali ahidi kunisomesha lakini alivyoenda mjini tu akanisahau, hapa nawaza yasije yakakukuta yaliyonikuta Mimi “
“Ila mama Jamani, kwani wewe haumuamini rafiki yako ??”
“We kichwa box wewe nitakuja kukupasua iko kichwa chako, Yaani ni mgumu kuelewa, hapa akija naongea nae ukasome uko uko “
“Mmmmh mama na wewe unabaki na Nani ??”
“Ninah Kwani Mimi na wewe Nani amemzaa mwenzie ??”
“Eeeh basi “

********

Siku iliyofuata,majila ya saa 2 asubuhi baba eddy aliwasili nyumbani Kama ambavyo aliaidi, kwa Namna moja au nyingine niliona kuwa baba Eddy ni mtu ambaye anaenda sambamba na ahadi zake.
Walizungumza Mawili Matatu na mama yangu na mwisho baba Eddy akakubali kwenda na Mimi Dar es salaam, nyie nilifurahi zaidi, Kwanza na zile Sifa zake ambazo nazisikia uwiiiih nilijikuta nikiona kama nachelewa hivi.
“Saa 10 nitakuja kukufata so jiandae Ninah “
Baba Eddy alinipa maagizo kisha akaondoka.
Eeeeeh Ila ushamba ni Mzigo Jamani, niliiingia mtaani na kuanza kuwatafuta Marafiki zangu, kila niliyeonana nae sikuacha kumwambia kuwa naenda Dar 😂.
Majila ya saa 10 baba Eddy akafika nyumbani na kunikuta Nikiwa namsubilia, nilikuwa nishajiandaa nawaka hatari, sio kwamba nawaka nimependeza hapa Mafuta ya nazi yalikuwa yanafanya kazi yake 😂.
Nilimuaga mama angu nikiwa na huzuni sana maana nilikuwa nalia Kama Mtoto mdogo, kwa upande wa mama yeye Aliamua kujikaza tu ingawa Alikuwa na maumivu makali sana.
Ila Kumbe Dar na Moro sio mbali kabisa, Yaani ndani ya masaaa manne tu tulikuwa tayali tushafika kwenye jiji la kelele, nilibaki nikishangaa uku na uku, mama hakuacha kupiga simu na kuuliza Kama tumefika.

Kwa uwezo wa Mungu tukafanikiwa kufika nyumbani kwa Baba Eddy au unaweza kumuita Mr Benson, nyumba yake ilikuwa kubwa sana na ilikuwa ni ya ghorofa mbili.
“Karibu sana Ninah jisiikie upo nyumbani “
Baba Eddy alinikaribishaa tukiwa ndani ya Gari, Yaani bado hatujashuka.
“Asante baba Eddy “

“Ahahaaah Ninah Bhana, hiyo baba Eddy ni mama yako tu Ndio anaruhusiwa kuniita na Watu wengine lakini wewe utapaswa kuniita baba Kuanzia sasa “
Nilijikuta nikiona aibu, nikainamisha shingo yangu na kwa sauti ya chini nikajibu.
“Sawa baba “
Basi tukashuka kwenye gari na kuingia ndani, nyie kuna Watu wanaaishi maisha luxury sana walahi, hiyo sebule ni hatari, nilijikuta nikiganda na kuanza kutembeza macho yangu tu ambayo yalizunguka uku na uku yakisoma mazingira ya sebule hiyo.
“Baba….”

Ilikuwa ni sauti ya binti mdogo ambaye kwa haraka nilijua kabisa huyu Ndio Mia Kutokana na maelezo ya baba yake.
Kwa haraka nilijua kuwa familia ilimmisi sana baba Yao, maana wote walijawa na nyuso za tabasamu pale tu walipomuona baba Yao.
Mwanamke mwenye asili ya uarabu, aliinuka kwenye kochi na kumsogelea baba Eddy, walikumbatiana kwa kunguvu na kukisiana midomo kwa midomo.
Kwa upande Wangu niliamua kufumba macho tu kwakweli maana mambo hayo ni mageni kwangu.
“Linda, Linda “
baba Eddy Aliita Jina ilo kwa kupaza sauti, na baada ya muda mfupi akaja mdada ambaye alivalia sale za jikoni.

“Abeeh baba “
Aliitika Linda.

“Msaidie mwenzio mizigo na Utaenda nae chumbani kwako, hakikisha anakoga Kuanzia sasa ni roommate wako “
Mke wa baba Eddy aligeuka na kuniangalia kwa dharau sana, lakini niliamua tu kutulia uku nikiamini kuwa ni akili
Yangu tu Ndio ina mawazo ya hovyo.
Linda alinipeleka chumbani kwake, niliweza kuoga na kubadili mavazi kisha sote tukaungana kwenye meza ya chakula.
Tukiwa tunaendelea kula, baba Eddy alianza utambulisho pale, ndipo nikajua kuwa Linda ni mdada wa kazi za ndani, lakini pia baba Eddy alitumia wakati huo kunikaribisha rasmi kwenye familia yake uku akiwapa kastory kafupi kuhusu urafiki wake na mama yangu.

“Karibu sana Ninah na ujisikie upo nyumbani, hii ni familia yako Mpya “
Alizungumza mke wa baba Eddy akiwa na tabasamu pana usoni kwake.
Ila nyie twende mbele turudi nyuma baba Eddy anavijana wazuri sana aswaaah huyu mkubwa woiiiih, nilijikuta nikimuangalia kwa muda mrefu mpaka najishtukia.
Ngoja niwatambulishe familia yangu Mpya sasa, kuna baba Eddy, mama Eddy, then kuna kaka mkubwa ambaye Aliitwa Enock, wa pili aliitwa Dinoh, watatu Ndio huyu Eddy na wa mwisho Ndio kabinti Mia.
Kwa Mara ya kwanza Ninah Mimi nikalala kwenye nyumba ya kitajiri, nyumba full kiyoyozi, kitanda kikubwa hatari, usingizi ulionekana kuwa wa shida sana kwa upande Wangu, shoga yenu nilishazoea kulala Na mama yangu tu.
********

Asubuhi na mapema niliamka na kuanza kumsaidia Linda kazi za pale home maana kila kitu anafanya mwenyewe.
Nikiwa nafuta vumbi pale sebuleni, niliweza kumuona Enock akishuka chini, ni wazi kuwa alikuwa akielekea kazini kwani alivalia mavazi ya kiofisi.
“Shikamoo kaka Enock “
Nilimsalimia Tena kwa kukunja goti kidogo, Enock aliniangalia kwa muda kisha akanifokea kwa kusema.
“Niondolee uchuro mie “
Nika……
ITAENDELEA……..
NINAH

MTUNZI: PATRICIA DA MTUNZI
SEHEMU YA: 03
SONGA NAYO……….

Nikajikuta nikikosa ata nguvu ya kuendelea kumuangalia, nilishusha uso wangu chini na kumuacha tu aondoke maaana ni Kama ameamka na kisilani.
“Huyo Ndio Enoch bhana, mkaka mzuri lakini mateNdo sasa mmmmh”
Alizungumza Linda ambaye alikuwa Nyuma yangu, nilitamani kumuuliza vimaswali lakini moyo ulisita kabia nikajikuta nikitabasamu tu kisha nikaendelea na kazi zangu.
Baada ya muda, Niliweza kumuonaa baba eddy akiwa na mkewe lakini pia aliongozana na watoto zake Wawili ambao ni eddy na Mia uku Wote wakionekana kutoka.
“Shikamoo mama, shikamoo baba “
Niliwasalimia kwa heshima Zote uku Nikipiga goti kidogo si unajua tena kujikosha kwamba ni Binti Mwema sana.
“Si tunaingia kwenye majukumu, lakini pia nitatumia week hii kukutafutia shule “
Alizungumza baba kisha yeye na familia yake wakaondoka.
Siku hiyo nilikuwa mpweke sana, muda mwingi nilibaki nikimkumbuka mama Angu mwaya, kilichoniwazisha zaidi ni pale kukumbuka kuwa atakuwa anazunguka Mtaani peke yake uku akichomwa na Jua Kali.
Nikiwa nimekaa zangu tu kwenye bustani nzuri ya maua ambayo ilikuwa ndani ya jumba ilo la kifahari, gafla akaja Dinoh mtoto wa pili wa baba eddy, Dinah alisimama Kando yangu kwa muda kisha akazungumza.
" upweke kwenye makazi mapya ni kitu cha kawaida sana, lakini pia hakikisha kuwa upweke auchukui fikra zako zote na kukufanya ukakosa amani unayostahili "
Niliinua macho yangu na kumtazama Dinoh, ila huyu baba jamani ako na watoto ma handsome sana si anataka tu kuvuluga akili yangu umu ndani.
"Unajisikiaje ?" Dinoh aliniuliza kisha akakaa pembeni yangu.
"Aaaah niko vizuri nasoma mazingira ya jiji la dasilamu bhana "
Dinoh aliniangalia kisha akacheka na kusema.
"Mazingira gani unayasoma kwa stahili hiyo ? 🤣 binti upo ndani na unasema unasoma mazingira ya dar acha kunichekesha basi "
Kwa namna moja au nyingine naweza kusema kuwa dinoh ni mtu tofauti sana, yaani alitofautiana na wenzie, kwanza ni mcheshi sana, mtulivu, lakini pia ana utu wa hali ya juu.
Ingawa ilikuwa ni mara ya kwanza kupiga story na dinoh lakini nilijikuta nikiinjoy sana, yaani Dinoh anajua jinsi ya kuishi na watu lakini pia kumfanya mtu ajisikie vizuri.
Majila ya jioni familia nzima ilikuwa imesharudi nyumbani, kwa upande wangu, Nilijikuta nikishindwa kabisa kuwazoea hivyo mara nyingi nilikaa jikoni nikimsaidia Linda kazi.
Ukiachana na utu wa dinoh umu ndani unakutana na utu wa Linda na baba eddy, hawa wengine naomba niseme kuwa ni pasua kichwa, eddy na Enock ni watu ambao sio rahisi kabisa kuwazoea.
Ukirudi kwenye upande wa mama yao, niseme kuwa sijawai kujua kuwa ni mtu wa aina gani, akili yangu ilishindwa kabisa kumjua kwani ni mtu anayebadilika badilika sana.

******

Baada ya week mbili hatimaye niliweza kupata shule, na niliweza kupelekwa shule Moja na eddy, maandalizi ya mimi kuanza shule yalifanyika haraka sana nilijikuta nikifurahi mno.
Hatimaye siku ya mimi kuanza masomo iliwadia, niliamka mapema sana na kuvalia sale zangu Mpya za shule, raha ambayo nilikuwa nikijisikia ilikuwa aielezeki Jamani, kuna muda nilikuwa naona kama nachelewa hivi kufika shuleni.
School bus iliweza kuwasili kisha mimi na eddy tukapanda na kuanza safari ya kuelekea masomoni.

"Hizi sale zimenipendeza sana si ndio ??"
Nilimuuliza Eddy ambaye nilikuwa nimekaa nae siti ya pamoja.
"Usinipigie kelele, kwani ni mara yako ya kwanza kuvaa sale za shule ? Au ndio ulimbukeni wa kusoma shule za pesa ndefu "
Kheeeeeh jamani kuuliza tu ndio napewa majibu kama hayo, sasa ulimbukeni wangu ni nini hapo 🥹.
Nilijikuta nikikosa nguvu kabisa, nikajikuta nikiwa mtulivu sana ili tu kuepusha kumkela Eddy ambaye hakuonesha kabisa kifurahia mimi kusoma nae shule Moja.
Siku ya kwanza shuleni ilikuwa ngumu Sana walahi , kwanza wanafunzi niliokutana nao wote ni maisha ya juu, ukiachana na maisha ya juu ni watu ambao wanajisikia sana, imagine unamsalimia mtu anakuuliza unasoma kwa scholarship au wazazi wako wanakulipia ?? .

Nilimaliza siku nzima nikiwa mwenyewe, sikuwa nimepata ata rafiki tu wa kuzunguka nae, mazingira ya shule pia sikuwa nikiyajua hivyo mara nyingi nilimfata Eddy na kumuuliza lakini sikufanikiwa kupata majibu mazuri kabisa na ndio iliniongezea upweke.
Majila ya jioni sote tulirudi nyumbani, ile nafika tu, nikakutana uso kwa uso na Enock ambaye alinishika mkono wangu kwa nguvu na kunivutia mpaka chumbani kwake.
"Yalaaaaah unaniumiza bwana"

nililalamika kutokana na jinsi ambavyo alikuwa akiunyonga mkono wangu.
"Ata ukiumia unathamani gani ?, anyway nguo zangu ni chafu sana na kesho naitaji kusafiri nazani itapendeza kama utafua saa hizi kabla ujafanya kitu kingine "
Kwanza nilishtuka sana, yaani Ninah mimi nianze kumfulia nguo libaba kabisa ili lijitu lizima linajua kipi kibaya na kipi kizuri.
Nilijikuta nikichukia sana walahi, nilimuangalia kwa muda na mwisho nikatabasamu na kumuuliza .
"Unachoongea unamaanisha ??"

"Mimi na wewe tunautani tangu lini ??"
Nilitamani kukataa, lakini pia nilitamani kumpa maneno Hayo ambayo nilitaka yamuumize tu, mwisho nikakumbuka kuwa niko nyumbani kwao na niko napata msaada tu.
Kwa sura ya upole na sauti ya utilivu nikamuuliza.
"Nguo ziko wapi ??"
Enock alisogelea tenga la nguo zake ambapo kulikuwa na nguo nyingi sana,niliziangalia kwa muda na kujiuliza kimoyomoyo.
"Hizi nguo amevaa mwezi mzima au ??".

Nilikosa ata hayo majibu maana nguo zilikuwa nyingi sana, nilichukua nguo na kutoka nje nikiwa na hasira sana, nilienda moja kwa moja mpaka sehemu ya kufua na kuanza kufua uku nikiwa nimevalia sale zangu za shule.
Mungu mkubwa bwana na mwanamke ni mwanamke, uzuri mama yangu alinilea vyema sana, mama alinifundisha kila aina ya kazi hivyo nilifua na kumaliza kwa wakati kabisa.
Majila ya usiku familia nzima ikiwa imeshamaliza kupata chakula, watu wote walikaa sebuleni wakiangalia movie, isipokuwa mimi tu ambaye nilikuwa niko chumbani nikijisomea.
Nikiwa bize najisomea gafla niliweza kusikia jina langu likiitwa kwa nguvu sana mpaka nikaogopa.

Kwa wasiwasi niliitika na kwa mwendo wa haraka nikafika sebuleni ambapo nilipofika tu kila mtu akanikazia macho kana kwamba ndio mara ya kwanza wananiona.
Mama Eddy aliinuka kwenye kochi lake na kujisogelea kisha akaniuliza.
"Iliingia chumbani kwa enock leo ??"
"Ndio mama "
Nilijibu pasi na kuwa na wasiwasi wa aina yeyote ile.
"Na ulifata nini kwenye chumba cha mtoto wa kiume ? Yaani nani amekuruhusu uingie ??"
Nilitaka kusema ukweli lakini Enock akinipatia ishara ya kunitishia na kunifanya kishindwe kujibu na kujikuta nikikaa kimya tu.
"Hauna ata majibu ya kunipatia si ndio ? Haya naomba pesa ambazo umechukua chumbani kwa enock"
"Pesa! "
Nilijikuta nikishtuka sana walahi, kwanza sijui walikuwa wanaongelea pesa gani na sikujua ni nini kinaendelea aswaah.
Kitendo cha mimi kushtuka na kuonesha kuwa sijui kitu kiliniponza sana, nilijikuta nikichezea kibao kimoja cha mama wa kambo kutoka kwa mama eddy.
Nika.....

ITAENDELEA......


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote