NILAN (Mimi Sio Kichaa)

book cover og

Utangulizi

Rubina binti anaeishi kijijini na bibi yake maisha yao yalikuwa ya kubangaiza,ilitokea kama bahati kuna mama akienda kumuomba amuajili kama mfanyakazi wa kumuhudumia mgonjwa.
Kwakuwa rubina alikuwa na shida alikubali kwenda kufanya kazi.
Alipofika mjini alipelekwa kwenye jumba la kifahari na kukutana na mtu ambae atatakiwa kumuhudumia , anakutana na Nilan kijana mwenye matatizo ya akili kwa mara ya kwanza rubina alikuwa na hofu alihisi hatutaweza kumuhudumia kichaa lakini kutokana na shida za kwao alikata moyo.
Mwanzo alifanya kazi kwa tabu sana lakini badae alizowea na kuona ni kazi ya kawaida.
Siku moja rubina alipata taarifa ya msiba wa bibi yake ilikuwa ni huzuni sana kwake hata Nilan akihutubia sana hakutaka kukaa nae mbali. Rubina alilala alipokuja kuamka alimkuta Nilan bado kakaa pembeni yake safari hii Nilan alionekana kuwa na akili timamu mpaka Rubina akashangaza, Nilani anajitambulisha kwa Rubina kuwa yeye sio kichaa .anamtaka aifiche hiyo siri maana hakuna anayejua kuwa Nilani ni mzima.
Nilani alijifanya kichaa kwajili ya kumpelekea baba yake mzazi mzee Mbwilo. Nilan anaomba msaada kwa Rubina anataka aanzishe uhusiano wa mapenzi na baba yake. Rubina anakataa lakini badae anakubali . Kwenye mitego ya kumtega mzee Mbwilo Nilan nae anajikuta anampenda rubina na kumuonea wivu.
Hapo sasa baba na mwana nani atapata rubina na Nilan kwanini anampeleleza baba yake ?

MIMI SIO KICHAA 1
MTUNZI SMILE SHINE
katika Kijiji Cha Makumbusho ulikuwa Ni msimu wa jua Kali Sana lililo kusababisha ukame na joto na kufanya watu washindwe kukaa ndani walitafuta vimvuli vya miti ili kupata upepo. Kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa imezungushiwa uzio wa makuti pia kulikuwa na miti baadhi ya vimvuli na matunda. chini ya mti wa muembe alikuwa anakaa binti Rubina na bibi yake anaejulikana pale kijijini kwa jina la bi Amina . Walikuwa wanapunga upepo mwanana uliyokuja na hewa safi.
" Hili jua mwaka huu kiboko mbona tutaiva kwa joto. Rubina aliongea huku akijipepea kwa kutumia kanga .
" Ndio tukae chini ya miti mpaka huko ndani kupoe.
" Mimi mambo ya kukaa nje sipendi .
" Sasa unataka kujificha ndani kwa sababu gani mjukuu wangu itakosa wachumba shauri yako.
" Bibi miaka 18 unafikiria niolewe?
" Kwanimiaka 18 ni mtoto wewe? Mwenzio mimi niliolewa na miaka 14.
" Duuu watu wa zamani mlikuwa mnapenda sana kuolewa, mimi nitaolewa nikiwa na miaka 20 kwenda mbele kwa sasa sitaki kabisa kusikia habari hizo.
" Hilo ni chaguo lako hakuna atakae kulazimisha.

Rubina na Bibi yake waliendelea kupiga story baada ya muda wakaona gari imesimama karibu na nyumba yao.
" Bibi Ile gari vipi mbona imekuja kusimama kwetu?
" Rubina bwana wote tupo hapa alafu unauliza Mimi nitajuaje?
" Labda huenda Ni wageni wako
" Hapana sina wageni wakuja na magari huenda wamesimama tu Wana Mambo yao.
Wote walikuwa makini kuangalia Lile gari mara wakamuona mama Tabu akiwa na mama mmoja ambae alionekana Ni mgeni machoni kwao .
" Hodi bi Amina. Mama Tabu alibisha hodi bi Amina akamuitikia
" Karibu mwali wangu naona leo umeamua kuja kututembelea . Walifika mpaka pale walipokaa wakamsalimia bi Amina , Rubina aliwasalimia kwa heshima kisha akaenda ndani kumchukua viti.
" Rubina nawe ungeleta kiti kimoja kwaajili ya mgeni Mimi ningekaa kwenye mkeka .
" Hata wewe Ni mgeni kaa tu . Wageni walikaa kwenye viti Rubina akarudi kukaa kwenye mkeka na mama tabu akaanza kueleza kilicho wapeleka
" Bi Amina huyu hapa ni shoga yangu anaitwa Najma Ni Kama ndugu yangu, rafiki yangu Yani ukimuona yeye umeniona Mimi , shida zake Ni shida zangu.
" Ahaaa karibu Sana mama jisikie upo nyumbani.
" Asante mama .
Mama tabu akaendelea kwa kusema
" Sasa bi Amina huyu shoga yangu ana shida na tumeona shida yake wewe ndio unaweza kuitatua .
" Shida gani hiyo wanangu?
" Najma anamatatizo kidogo mtoto wa marehemu dada yake anaumwa Sasa alikuwa anatafuta binti wa kwenda kumuangalia, kumsaidia shida ndogondogo nikaona ngoja nije niongee na wewe Kama utaridhia Rubina afanye hiyo kazi. Rubina na Bibi yake waliangaliana Najma akawatoa wasiwasi kwa kusema
" Sio kazi kubwa maana ni kijana mkubwa. Kazi yake itakuwa ni kumuangalia tu kuhakikisha anakula,kumfulia pamoja na kusafisha chumba chake na pia atalipwa pesa nzuri.
Rubina na bibi yake waliangaliana tena , bi amina akauliza
" Rubina vipi utaiweza hiyo kazi?
" Nitaweza Bibi. Alijibu Rubina aliona Bora akubali kwaajili ya kumsaidia Bibi yake maana maisha yao yalikuwa ya kubangaiza .
" Mama tabu, rubina kakubali na Mimi nawapeni mjukuu wangu kwasababu nakufahamu wewe pia Nina Imani hakuna kitu kibaya kitakachotokea mjukuu wangu.
" Usiwe na wasiwasi mama mjukuu wako ataenda kuishi vizuri na atapata kila kitu.
" Sawa Sasa hiyo safari Ni lini?
" Ni kesho acha leo ajiandae na kuweka mambo yake sawa kesho mapema tutakuja kumchukua . Alisema Najim
" Sawa . Walimaliza maongezi yao Najma alifungua pochi yake na kutoa hela kidogo akampatia bi amina .
" Hii mtanunulia hata sukari .
" Asante Sana mwanangu Mungu akubariki.
" Amin atubariki sote. Rubina mama ujiandae kesho nakupitia tunaondoka .
" Sawa.
" Haya kwaherini .

Mama Tabu na Najma walipoondoka rubina na Bibi yake wakaendelea na maongezi
" Mjukuu wangu umeridhika kwenda kufanya kazi?
" Ndio Bibi nahisi hii Ni baraka imetushukia huenda nikienda huko Mambo yatakaa sawa .
" Sawa lakini Kama utaona Mambo magumu urudi nyumbani .
" Sawa Bibi lakini Nina Imani hayatakuwa magumu.

Kesho yake mapema Sana Najma alienda kumchukua rubina safari ya kuelekea mjini ikaanza .

Baada ya masaa nne wakawa wamefika mjini katika jumba Moja kubwa la kifahari. Rubina alipokelewa mzigo wake .
" Usiogope Rubina hapa ndipo utakapofanya kazi jisikie upo nyumbani.
" Sawa. Alijibu Rubina huku akiwa anashangaa
Alikuja kijana mmoja akasalimia
" Shikamoo mama mdogo.
" Marahaba hujambo
" Sijambo. Yule kijana alitupia jicho kwa Rubina akamsalimia
" Mambo.
" Safi
" Odo huyu ndio dada wa kumuhudumia Nilan?
"Ndio anaitwa Rubina.
" Karibu sana Rubina jisikie upo nyumbani.
" Asante.
Walikaa kidogo akaja baba mmoja wa makamo ambae Ni mmiliki wa hiyo nyumba na baba wa hiyo familia Mr Mbwilo . Rubina alisimama na kusalimia kwa heshima huku akibonyeza chini kama vile anataka kupiga magoti.
" Shikamoo
" Marahaba karibu ukae binti. Rubina alirudi kukaa kwenye sofa
" Vipi shemeji . Mr Mbwilo alisalimia Najma
" Safi shem habari za hapa!
" Salama
" Sasa huyu Ni Rubina ndio Dada atakaemsaidia Nilan maana naona anapata tabu na anahitaji mtu wa kumuangalia na kuhakikisha anakula na kupata huduma zote.
" Safi Sana umefanya jambo la maana anaonekana ataiweza hiyo kazi Ni binti mwenye heshima Sana , binti kijana wangu Ni mgonjwa wa akili Yani Kama kichaa flani lakini hana madhara kama ukimuhudumia vizuri nitakupa pesa nzuri.

Rubina alishituka aliposikia mtu anaetaka kumuhudumia Ni kichaa
" Mungu wangu Mimi na kichaa tuta wezana kweli? Akiwa anafikiria alishituliwa na swali alipoulizwa na mzee Mbwilo
" Tumeelewana?
" Ndio nitamuhudumia vizuri.
" Kazi yako itakuwa Ni kumuhudumia yeye tu kukiwa na shida utanijulisha Mimi au wadogo zake zahir na Razaki.
" Sawa . Tahya alijibu huku akimuangalia najma usoni.
" Mimi sitakuwepo hapa ndio maana boss wako hajanitaja Ila nitakuachia namba zangu za simu kukiwa na lolote utanipigia sawa mamy?
" Sawa .
"Haya nyanyuka twende ukamuone mgonjwa wako alafu nitakuonyeshe chumba chako Cha kulala.
" Sawa.

Walinyanyuka wakaenda kwenye chumba ambacho atakuwa analala .
" Hiki Ni chumba ambacho utakimiliki wewe Yani utalala hapa. Rubina alishangaa jinsi chumba kilivyokuwa kizuri kitanda kikubwa pia kulikuwa na TV ndogo.
" Umekipenda chumba chako?
" Nikizuri mno mpaka naogopa kukilalia hicho kitanda . Najma alicheka
" Jamani Rubina acha kunifurahusha Sasa unaogopa Nini?
" Kama Cha malkia.
" Ni Mambo ya kawaida bwana Sasa twende ukamuone Nilan Walitoka kwenye kile chumba na kwenda chumbani kwa Nilan ambacho hakikuwa mbali na chumba atakachokuwa analala yani ni mlango wa pili vyumba vyao vilifuatana. walipoingia chumbani kwa Nilan , Rubina alishangaa kuona chumba kipo rafu vitu vimetupwa ovyo vingine vimepasuliwa alipotupa jicho kumuangalia huyo Nilan alijikuta anakunja uso Nilan alikuwa anakula maembe alijipatia karibia uso wote, Nilan alipowaona akaanza kuchekacheka huku anawazomea alafu akacheka Sana na kusema
" Mmekuja kula maembe yangu nimemaliza yote aoooo nimewazidi ujanja nimekula haraka haraka.
Najma akamgeukia Rubina akamwambia
" Huyu ndio Nilan ndio mtu unatakiwa kumuhudumia anahitaji sana msaada kutoka kwako.

MIMI SIO KICHAA 2

MTUNZI SMILE SHINE

Rubina alikuwa kazubaa anamuangalia huyo mtu ambae anatakiwa kumuhudumia na jinsi alivyokuwa anafanya vituko.
Rubina alizubaa akawa anamuangalia Nilan moja kwa moja mpaka Najma alivyomuita ndio rubina akashituka.
" Mmmm mama ulikuwa unasema?
" Naona upo mbali kimawazo Unawaza Nini?
" Hamna siwazi kitu, nimemuonea huruma mkaka mzuri kuwa hivi.
" Mmh ndio dunia , vipi utaweza hii kazi ya kumuhudumia?
" ndio nitaweza nitamuhudumia vizuri sana lakini hawezi kunipiga?
" Huwa apigi mtu wala kufanya fujo kuwa na amani.
" Sawa.

Najma alimsogelea nilan akamshika kichwani na kumwambia
" Umemuona yule? Nilan alimuangalia Rubina huku anacheka cheka alafu akaitikia kwa kichwa akimaanisha ndio
" Basi yule atakuwa rafiki yako utacheza nae atakupa chakula lakini usinisumbue sawa mwanangu? Nilan alitabasamu huku akimuangalia Rubina kama vile anamuonea aibu huku akichezea vidole vyake vya mikono
" Mama yangu yule amekuja yule ni mama yangu njoo, njoo. Nilan alimuita rubina
" Haya mbona makubwa nimeshakuwa mama Mara hii. Rubina alijisemea.
" Anaitwa Rubina usimsumbue yeye Ni rafiki mzuri kwako atakupa kila unachotaka
" Atanipa pili ya kijiti na chokoleti.
" Ndio atakupa.

Najma alimuangalia Rubina alafu akasema
" Rubina chochote atakachotaka nenda kachukue umpe maana vitu anavyopenda huwa havikosekani hapa ndani.
" Sawa.
" Sitaki kusikia hilo jina baya yule Ni mamaaa, nimesema yeye ni mama yangu mimi.
Nilan alikuwa mkali hakutaka kusikia kabisa jina la Rubina zaidi ya kumuita mama.
" Sawa ni mama yako.
" Haya . Alijibu Nilan huku akiwa kafurahi
Najma alisimama akamwambia Rubina
" Nenda ukapumzike kwanza badae utaanza majukumu yako
" Hapana sijachoka naweza nikaanza Sasa hivi maana hiki chumba kipo rafu Sana .
" Sawa Basi ngoja nikuache Kama utahitaji maelekezo mengine muone dada wa kazi huko nje ( Vick) .
" Sawa.
Rubina aliangalia kila Kona ya kile chumba akawa anapiga mahesabu aanzie wapi kufanya usafi maana kila sehemu kulikuwa rafu nguo zilizagaa chumba kizima , viombo vichafu vilivyokuwa vimevunda kwa chakula .
Akiwa bado anapiga mahesabu kwa kuanzia Nilan alimshitua
" Weeee .......
Rubina alishituka akataka kukimbia , Nilan alicheka mpaka akawa anagaragara sakafuni
" Jamani huyu kichaa atakuja kunitoa roho, hivi hawezi kunipiga kweli? Rubina aliingiwa na uwoga alisimama mlangoni akawa anamuangalia anavyocheka alipotukuta alienda kupanda kitandani akalala na kujifunika shuka mpaka usoni.
" Afadhali alale ngoja nianze kuokota hivi vitu vilivyozagaa na kuweka vizuri .
Nilan alikuwa amejifunza kidogo uso wake akawa anamuangalia anavyohangaika .
Baada ya muda Rubina alihisi kitu alivyogeuka kumuangalia akamuina kasimama anamwaga maji yaliyokuwa kwenye kikombe
" Aaah Sasa ndio nini ? Alienda kumnyanganya kile kikombe logan akawa anachekacheka huku akitaka kumnyang'anya.
" Acha
" Nataka tucheze.
" Tutacheza badae ngoja kwanza tufanye usafi . Rubina a alimshika mkono akamuweka kitandani .
" Sitaki kulala.
" Sawa usilale wewe kaa tu hapa.
Rubina alimalizia kufanya usafi wakati anamalizia kudeki alifika Vick .
" Nimeleta chakula .
" Sawa . Vick alipita na kuweka mezani wakati anaondoka Nilan alidaka na kuvuta nguo yake.
" Acha nguo yangu nitakuzabua vibao. Vicky alimfokea , Nilan akawa anamzomea, Vicky alitishia kumpiga Nilan alikimbia na kwenda kujificha nyuma kwa Rubina.
" Mama anataka kunipiga ,huyu mchokozi.
" Nitakupigia kweli lione.
Alafu Rubina akimaliza kula uje na wewe ule.
" Nitakula nae huku huku .
" Utaweza ?
" Ndio nitaweza. Vick alimuangalia Rubina Kisha akamwambia tena.
" Utaweza kula pamoja na huyu chizi?
" Hakuna shida nitakula nae si kila mmoja na sahani yake.
" Sawa ngoja nikuletee . Vick alitoka Rubina akamalizia kufuta akaingia bafuni akanawa mikono yake vizuri alafu akarudi alimkuta Nilan anakula kile chakula kwa pupa Tena kwa mikono miwili.
" Heeee wewe umenawa wapi?
" Chakula kitamu njoo ulee.
Rubina alienda kumnyang'anya sahani lakini Nilan alikuwa mkali .
" Acha ubwabwa wangu.
Rubina alimuacha aliendelea kusimama hakujua amsaidie je.
" Kula taratibu Basi utapaliwa.
" Haya. Nilan alikuwa anakula kichafu vyakula vilidondoka kutoka mdomoni kabla hajameza aliweka tonge lingine. Vick alifika na sahani ya chakula mkononi
" Ni kweli utaweza kula huku? Rubina a alinyamaza kwa muda ki ukweli alikuwa hawezi Ila kwakuwa ni kazi yake alikubali
" Ndio wewe lete nitakula.
" Aiseee una moyo huoni kinyaa kwa hiyo hali? Rubina hakujibu alichukua sahani akakaa chini na kuanza kula Nilan alifurahi aliendelea kula huku anamuangalia usoni Rubina alikula kwa shida Kuna wakati alishindwa kumeza akaenda kutema chooni na mwisho aliacha kabisa kula . Nilan alipomaliza kula Rubina alianza upya kusafisha maana alimwaga mwaga chakula kila sehemu . Baada ya kusafisha alimbadilisha tishet akakaa pembeni akawa anamuangalia anavyocheza kama mtoto .
" Maskini Kaka wa watu sijui kazaliwa hivi au walimwengu ndio wameshafanya yao?
Rubina alijiongelea mwenyewe Nilan akawa kusikia
" Unasema twende tukatembee , haya nyanyuka twende sasa.
" Hapana sitaki kwenda popote.
" Basi njoo tulale. Alisema Nilan huku akiwa anaenda kuchukua shuka akajilaza sakafuni na kujifunika akaacha uso tu.
" Njoo basi, njoo ukae na mimi.
Rubina alipoona anakazania sana kulala akapata wasiwasi.
" Mmmh mbona ananikazania hivi ukisikia kubakwa ndio huku hata kichaa nae ana hisia. Alinyanyuka taratibu akatoka nje ya kile chumba na kurudishia mlango.

MIMI SIO KICHAA 3

MTUNZI SMILE SHINE

Kadri siku ziliyozidi kwenda Rubina ndivyo alivyozidi kuzowea Ile hali ya Nilan na kufanya kazi za yake vizuri bila uwoga.

Siku moja rubina alipomaliza kazi zake zote alimwambia Nilan
" Nilan unatakuwa kupumzika Sasa.
" Nataka kucheza .
" Tutacheza ukiamka lala kwanza hebu sogea hapa alimvuta Nilan akasogea na kujilaza kwenye mapaja ya Rubina.
Rubina alimbembeleza huku akimshikashika kichwani mpaka Nilan akapitiwa na usingizi alimchungulia alipoona kafumba macho alitabasamu akamtoa mapajani kwake na kumlaza vizuri kitandani Kisha akatoka huku akinyata maana Nilan huwa akisikia sauti ya kitu kidogo huwa anaamka .
Kitendo Cha rubina kutika pake chumbani Nilan aliamka akaa kitandani Kisha akaenda kusimama dirishani akawa anachungulia nje . Akamuona rubina na Vicky wamekaa bustanini wakiwa wanaongea .

Rubina alikuwa na shauku ya kutaka kujua tatizo la Nilan alimuuliza Vicky
" Hivi Nilan alizaliwa akiwa na hali Ile au ni matatizo yaliyomkuta baada ya kuzaliwa?
" Sijui ila nasikia alikuwa mzima hili tatizo limemkutia ukubwani tena nasikia baada ya mama yake mzazi kufariki.
" Maskini itakuwa aliumia sana mpaka ikamsababishia kuwa katika hali kama hii.
" Itakuwa si unajua tena uchungu wa mama .
" Lakini mbona kama ndugu zake hawaonekani kumjali inaweza ikapita hata wiki hawajaenda kumuona chumbani kwake ?.
" Ndivyo walivyo huenda wanamuonea kinyaa lakini hata wewe una moyo kwa jinsi alivyo siwezi kabisa kukaa nae nashangaa wewe unakula nae na Wala hujisikii vibaya
" Nimezowea na namchukulia kawaida tu.
" Na kweli inabidi uzoee maana ndio kazi yako inayokupa kula. Mimi siwezi kukaa nae hata dakika tano .
" Usiseme hivyo Vicky unajua sisi binadamu hatujui mwisho wetu ni upi kama ulivyosema kuwa mwanzo alikuwa mzima hakutegemea
Kama mambo yangegeuka na leo akawa kichaa anafanya mambo ya ajabu bila kufikiria.
" Basi bwana na wewe na huyo Nilan wako unavyo mtetea basi .
" Sio kumtetea anahitaji upendo kutoka kwetu.
" Kumpenda tunampenda lakini kukaa na kula nae hapana .
" Angekuwa ndugu yako ungeweza.
" Mbona ndugu zake hawajaweza na huyo baba yake ndio kabisa wala hajali kuhusu mwanae.... Vicky alitaka kuongea kitu lakini akasita akaangalia huku na huku alipoona hakuna mtu akasogelea rubina na kuongea kwa sauti ya chini.
" Unajua kuna wakati nafikiria huyu baba atakuwa kafanya mwanae chizi kwaajili ya mali .
" Mmmmmh.
" Unaguna , wewe huoni hizi mali zote huyu baba kamfanya mwanae ndondocha hata huko nje watu wanasema hivyo.
" Duuu....

Wakiwa nawaendelea kupiga story baba yake Nilan alirudi kutoka kazini akawakuta Vicky na rubina wakamsalimia
" Rubina huyo mtu wako anafanya Nini?
" Alikuwa amelala .
" Sawa endelea kuwa makini na kazi yako mwezi huku nitakuongezea mshahara.
" Asante baba nashukuru.
Baba Nilan aliingia ndani . Vicky akasema
" Ni haki yako kuongezewa mshahara maana sio kwa ugumu wa kazi Ile .
" Mbona sio ngumu sana ukichukulia kama kazi nyingine unafanya tu
" Hapana ule uchafu siuwezi .
" Haya bwana ngoja nikamiangalie kama kaamka .
Rubina alinyanyuka akawa anaelekea ndani Vick alimuangalia Kisha akaguna
" Mmmh ila hizi shida hazina adabu pale mwenyewe kaona kapata kazi . Kazi yenyewe ya kula tahira sijui kichaa wenye damu yao wamewashinda wanamkata mwenye shida zake mmmmh maisha haya. Acha tu.

Rubina alipofika chumbani kwa Nilan hakumkuta kitandani ila alisikia maji yakiwa yanamwagika bafuni alisogea mpaka kwenye mlango wa bafuni akagonga
" Nilan unafanya Nini huko hebu Toka huko bafuni usichezee maji. Nilan hakusikia aliendelea kujimwagia maji Rubina alishindwa kuingia akihofia huenda akawa Hana nguo akatoka mpaka siting room akamkuta baba Yao anataka kutoka akamwambia
" Samahani baba nilikuwa naomba msaada Nilan yupo bafuni amefungulia maji Yana mwagika nimeshindwa kuingia huenda akawa uchi. Baba Logan alicheka
" Binti unachoogopa Nini Sasa si ukaingie umtoe
" Lakini siwezi kumchungulia mwanaume.
" Sikiliza Rubina a yule Hana madhara nenda kamtoe Mimi sitaweza kukusaidia maana Kuna kazi ya muhimu naenda kuifanya. Baba Nilan aliondoka
" Khaaa huyu mzee Yuko sawa kweli kwahiyo anamdharau Logan kuwa hawezi kufanya chochote hajui hawa vichaa ndio mahodari wa kubaka na wakikushika hawakuachii, hapa niombe tu Mungu. Rubina alirudi chumbani kwa nilan akamkuta katoka bafuni kasimama chumbani huku akiwa kafunga taulo lake vizuri lakini Bado maji yalikuwa yanamwagika bafuni Nilan akiingia bafuni akafunga maji alafu akatembea taratibu kumfuata Nilan pale aliposimama akamshika begani. Nilan aligeuka akamuangalia huku alitabasamu Kisha akasema
" Mama nimeoga. Rubina alitabasamu
" Sawa lakini siku nyingine usioge kama Mimi sipo sawa?
Nilan aliitikia kwa kichwa.
" Mama nataka kulaa
" Haya ngoja nikutolee kwanza nguo uvae alafu naenda kukuchukulia chakula .
" Haya. Rubina a alitoa nguo akaweka kitandani .
" Nguo hizi uvae kama nilivyokuelekeza Mimi naenda kukuchukulia chakula. Nilan hakumjibu zaidi ya kuchekacheka tu.


Kesho yake asubuhi sana watu wote wakiwa Bado wamelala Nilan akianza fujo alipiga kelele zilizomfanya Kila mmoja aamke kwenda kumuangalia
" Mama, Mama namtaka mama yangu namtaka mama . Nilan aliaza kuvunja baadhi ya vitu watu wote walisimama pembeni kumuangalia baba Yao alipotoka alimuangalia Nilan kwa hasira na kufoka kwa sauti Kali
" Nilan acha ujinga . Nilan alitulia akamuangalia huku akiwa kazubaa na shingo yake kaiweka upande . Alafu akaendelea kusema
" Namtaka mama yangu Sara. Safari hii aliongea huku machozi yakitililika mashavuni mwake. Baba yake alimfuata kwa hasira akamnasa kibao Cha nguvu kilichomfanya Nilan akae chini kwa wenge. Kila mtu alishitushwa na kile kibao Rubina alionekana kuumia zaidi maana siku zote huwa anamuonea huruma.
" Pumbavu unanilerea ukichaa wako nyumbani kwangu, Rubina mchukue mpeleke chumbani kwake. Rubina alienda haraka akamshika mkono akamsaidia kunyanyuka pale chini alafu akaenda nae chumbani walipofika mlangoni Nilan alisimama
" Ingia ndani. Rubina aliongea kama mtu anaelia Nilan aligeuka kumuangalia alafu akasema sitaki nataka kaa peke yangu. Rubina alishituka maana Nilan aliongea sauti ya tofauti na alivyomziwea ilikuwa ni sauti ya mtu mwenye akili timamu tena ya kiume pia ya mtu mwenye kujiamini. Rubina akiwa Bado anashangaa Nilan akiingia chumbani kwake akafunga mlango kwa nguvu mpaka Rubina akashituka

MIMI SIO KICHAA 4

MTUNZI SMILE SHINE

Rubina hakujali sana akajua ule ujasiri unatokana na hasira za kupigwa.
Rubina alisogea mlangoni akajatibu kufungua mlango haujufunguka Nilan alikuwa kafungwa na funguo.
" Nilan naomba ufungue mara moja nikwambie kitu.
Chumbani kulikuwa kimnya Nilan hakufungua mlango wala hakuongea kitu.
" Tafadhali Nilan e najua unavyojisikia fungua basi ukae karibu yangu, leo hutaki kukaa karibu na mama, hutaki kucheza na mimi. Au unataka niondoke nikuache?
Bado kulikuwa kimnya , Rubina bado alikuwa kasimama mlangoni akisikilizia.
Mara Vicky alikuja.
" Sasa anahangaika nini na huyo chizi asiejitambua nenda kapumzike zako huko akichokaa kukaa ndani atafungua mlango atatoka.
" Usiseme hivyo Vicky , Nilan anahitaji kufarijiwa ili asijione kama yupo tofauti na wengine jaribu kumchukulia kama unavyowachukulia watu wengine.
" Hayo unaweza wewe yaya wake humu ndani hakuna mwenye muda na huyo kichaa.
" Ndio mimi nipo hapa kwaajili yake na nitafanya kila niwezalo asijisikie vibaya.

Wakiwa bado wanaongea mlango ulifunguliwa na Rubina akaingia ndani.
Akamfuata Nilan kwenye kiti alipokuwa amekaa. Aliushika mkono wa Nilan huku akimuangalia usoni kisha akamuuliza kwa sauti ya chini.
" Unataka nikupe nini?
Nilan alimuangalia na kuanza kucheka alafu akanyanyuka na kwenda kujilaza kitandani.
Rubina walimfuata na kukaa pembeni yake kuna kitu alikuwa anahisi hakiko sawa, alihisi kuwa Nilan anahitaji zaidi mtu wa kuwanae karibu maana pale ndani hakuna mtu anaemtetea kila mmoja anapuuzia na kumchukulia kama kichaa.
Rubina alishituka sana kuona simu chumbani kwa Nilan.
" Nilan nipe hiyo simu ni simu ya nani?
Nilan alipandishwa mabega kama mtoto na kugoma kabisa kutoa ile simu.
Kwa akili za haraka Rubina alijua ile simu niya baba yao maana alishawahi kumuona na simu kama ile.
" Nilani hiyo simu niya baba naomba niirudishe chumbani kwake .
" Sitaki toka hapa.
"Baba akijua umechukua simu yake atakupiga tena.
Rubina alimbembeleza lakini Nilan hakuwa na dalili za kutoa ile simu ndio kwanza aliilalia na kujifanya kapitiwa na usingizi.
" Sitakiwi kusema kama ana simu , kama wakijua watampiga wamuumize.

Siku zilisogea na rubina ndio mtu pekee ambae alikuwa karibu sana na Nilan alikuwa akimjali na kucheza michezo kama watoto kwa Rubina alijionea sawa tu wakawa marafiki wanaelewana sana kuna muda Nilan alikuwa akifanya vituko Rubina alikuwa akimkataza Nilan aliacha mara moja.

Siku moja majira ya saa tano usiku rubina alikurupuka kutoka usingizini akakaa kitandani.
" Mungu wangu hii ndoto unamaana gani mbona inaniogopesha hivi?
Rubina alipotea ile ndoto akafanya maombi alipomaliza akataka kujilaza mara akasikia kama kuna mtu anatembea kwenye korido.
" Ni nani ambae hajala muda huu?
Alihisi huenda anaweza akawa Nilan alinyanyuka pale kitandani akatoka mpaka kwenye korido lakini hakuona mtu.
" Mbona hakuna mtu au maruweruwe bado yananiandama?
Aliamua kwenda jikoni kunywa maji ,alipomaliza kunywa maji alienda chumbani kwa Nilan kuchungulia kama amelala na hiyo ni kawaida yake kufanya hivyo lakini siku hiyo alikuta hakuna mtu kitandani.
" Huyu kaenda wapi tena usiku huu?
Rubina alienda mpaka chooni lakini hakumkuta mtu. Alipatwa na wasiwasi akawa anajiuliza aanzie wapi kumtafuta .
" Hapa hakuna wa kunisaidia na baba hayupo sijui nitamuona wapi.
Alitoka nje ya chumba cha Nilan mara akamuona Nilan anatoka chumbani kwa baba yake huku akiwa kashika kitu mkononi. Nilan alipomuona Rubina alishituka na kuficha kile kitu alichokuwa kashika.
Rubina alimfuata mpaka pale mlangoni.
" Wewe unafanya nini huku chumbani kwa baba? Na huku umeshika nini?
" Niache ukooo.
Rubina alijitahidi sana aone kitu alichoficha Nilan lakini hakufanikiwa.
" Haya twende ukalale.
Alimshika mkono akampeleka chumbani kwake.
" Nilan unajua unanitafuta matatizo kuingia chumbani kwa baba yako unajua mtu mwenyewe hataki maziwa na wewe hivi kwanini hujionei huruma lakini?
" Baba mbaya ananipiga.
" Anakupigia kwasababu husikii.
" Simpendi.
" Yeye ni baba yako unatakiwa kumpenda sawa.
" Sitaki.
"Basi sawa lala hapa.
Alimlaza kichwa chake kwenye mapaja yake huku alimbembeleza alale ili alipitiwa na usingizi aweze kuchukua kile kitu alichokuwa akishikilia mkononi.
Nilan alijilaza kwa amani mapajani kwa Rubina mpaka usingizi ukampitia lakini ilikuwa ngumu sana Rubina kuchukua kile kitu na hakujua ni kitu gani.
Hakuona haja ya kuendelea kusumbua na nae ikiwa mtu kashalala alimlaza vizuri na kumfunika na duvet kisha akaenda chumbani kwake kulala.

Kesho yake mapema aliamka na kuanza kumuhudumia Nilan alikoelekea chai na dawa zake .
" Nilan unatakiwa kunywa chai ili unywe dawa.
Alimuandalia chai Nilan alikunywa mwenyewe kipindi hicho kidogo alikuwa mstaarabu hakuwa akisbaza chakula hovyo.
Alipomaliza kula Rubina alimpa vidonge viwili mkononi pamoja na grass ya maji
" Haya kunywa dawa.
Nilan alinyanyuka akaenda kusimama karibu na kabati la nguo kisha akanywa zile dawa na kusukumwa na yale maji.
" Umeshaanza dawa?
" Ndio aaaaaa. Alisema Nilan huku akiachama mdomo.
" Sasa nenda kaoge nimekuwekea maji kwenye ndoo.
Nilan aliingia bafuni na rubina alisogea karibu na kabati akachungulia nyuma ya kabati.
" Mungu wangu inamaana Nilan huwa haunywi dawa?
" Alisema Rubina kwa mshituko baada ya kuona tembe nyingi za dawa zimetupwa nyuma ya kabati.

MIMI SIO KICHAA 5

MTUNZI SMILE SHINE

rubina akiwa bado anaangalia na kujiuliza inakuwaje dawa ziwe nyingi kiasi kile na hakuwahi kuona na kuna wakati huwa ana hakikisha anakunywa ni siku moja moja ndio anampa ameze mwenyewe.
" Hizi sio za jana wala za leo itakuwa ameanza muda kutupa dawa sasa kwanini hamezi dawa?
Rubina akiinama ili achukue mara akasikia mlango wa bafuni unafunguliwa Nilan alikuwa anatoka bafuni lakini alipomuona Rubina kachuchumaa alisimama kwanza akamuangalia kwa mshituko ile anataka kumfuata mlango ulifunguliwa Najma mama yake mdogo Nilan aliingia. Nilan alipomuona mama yake mdogo alianza kucheka cheka na rubina alitoka pale haraka hakutaka mtu ajue kuwa Nilan haunywi dawa anatupa nyuma ya kabati.
" Vipi nyie mpo sawa?
" Ndio shikamoo mama.
" Marahaba vipi unaendeleaje?
" Naendelea vizuri.
" Rubina naomba unifuate huku nataka kuongea na wewe.
Rubina alishituka maana sio kawaida kwa mama mdogo kutaka kuongea nae Chemba huwa akija walikuwa wakiongea mbele ya Nilan.

Walitoka chumbani kwa Nilan wakaenda kwenye chumba anacholala Rubina.
Najma alikaa pembeni na kumtaka rubina akae pembeni yake. Rubina alikaa na Najma akamshika begani huku akiwa anamuangalia usoni kwa huzuni
" Mama kuna nini?
" Rubina sijui nianzie wapi kuongea.
" Kwani vipi mnataka kunifukuza kazi?
" Hapana ila kuna habari ambazo sio nzuri kwako.
Akili ya rubina alifikiria bibi yake kijijini.
" Bibi yangu yupo sawa?
Najma a alishindwa kuongea machozi yalianza kutoka machoni kwake alijaribu kufuta lakini ilishindikana hofu ilizidi kwa Rubina.
" Niambie mama bibi yangu yupo sawa kweli?
" Pole rubina bibi yako amefariki na muda huu ameshazikwa....
Rubina aliangua kilio kwa sauti kubwa kila mtu aliyekuwepo pale ndani alisikia na kwenda chumbani kwake.

" Basi mwanangu usilie yote ni mipango ya Mungu.
" Kwanini hamkuniambia mapema kuwa bibi yangu kada na mmemzika bila mimi kuwepo kwanini ? Jamani bibi yangu mbona umeniacha ikiwa bado nakuhitaji kimbilio langu liko wapi nitamtegemea nani mimi? Rubina aliomboleza kwa uchungu na kusababisha kila aliyekuwepo pale atokwe na machozi hata Nilan alishindwa kujizuia alimfuata akamkumbatia .
" Nyamaza usilie , wewe odo kwanini umemfokea mwenzio ona sasa analia . Aliongea Nilan huku alimsukuma Najma. Najma alikuwa analia tu hakujali maneno ya Nilan.

Baada ya kulia sana watu walinyamaza na rubina alikuwa katulia huku Nilan akiwa pembeni yake , kuna muda alimbembeleza na kuna muda aliongea maneno ambayo hayakueleweka.
" Mama bibi yangu alikuwa anaumwa?
" Hapana hajaumwa nasikia alienda kuchota maji mtoni bahati mbaya akakamatwa na mamba. Ile siku ya jana watu walimtafuta bila mafanikio, waliitwa wazee wa mila wakafanya mambo yao hapo kwa kuwa muda ulikuwa umeenda watu waliondoka leo asubuhi walirudi mtoni kuangalia ndipo wakata kichwa. Kwahiyo bibi yako kazi kwa kichwa tu.
Taarifa zilizidi kumuumiza rubina akaanza tena kulia.
" Pole Rubina najua unavyojisikia na kuhusu na kuanzia leo wewe ni mwanangu, wewe ni ndugu yangu nitabeba jukumu lako .
" Asante mama.
" Basi pumzika kidogo mwanangu na kushukuru Mungu kwa kila jambo pia usisahau kumuombea bibi huko aendako apikelewe Mungu amsamehe Zambi zake.
" Sawa.

Watu wote walimpa pole na kutoka chumbani wakamuacha chumbani akiwa kajilaza. Kila alipopita taswira ya bibi yake na kukumbuka jinsi walivyokuwa wakiishi pamoja machozi hayakuacha kumtoka . Alilia pale mpaka usingizi ukanipitia.

Rubina alikuja kushtuka giza likiwa limeingia na pembeni yake alikuwa amekaa Nilan akawa anamuangalia.
Rubina alinyanyuka akakaa.
" Nilan mbona upo hapa , umekula?
Nilan hakumjubu alikuwa anamuangalia.
" Twende ukale.
" Usijali kuhusu mimi wewe tulia hapo.
Sauti ya Nilan ilimshitua Rubina, ilikuwa ni sauti ya mwanaume aliyekamilika asiyekuwa na upungufu wowote tena ilikuwa sauti tamu , nzito ya kusisimua.
" Nilan?
" Pole kwa matatizo makubwa yaliyokupata.
" Hapana wewe ni nani?
" Ongea taratibu tafadhali.
Nilan aliendelea kuongea kwa utulivu na umakini mkubwa mpaka rubina akapata hofu.
"Najua una wasiwasi sana kuhusu mimi lakini mimi ndio yule yule kichaa, tahira unaemuhudumia kila siku.
" Lakini leo hufananii na yule Nilani niliwaziwea kumuona kila siku.
" Unamaanisha yule kichaa
" Ndio.
" Ni kweli sababu mimi sio kichaa.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote