NDOA YA BILLIONAIREππ1
MTUNZI SMILE SHINE
Caren na Lina Ni Marafiki wa kubwa Sana tangia walipokuwa Kijijini kwao ni Marafiki waliopenda na mno na kifuatana kila sehemu , yani alipo Caren huwezi kumkosa Lina.
Caren alichukuliwa na mama yake mdogo akaenda mjini na kumuacha Lina mwenyewe pale kijijini , wawili hao walikosa furaha kwa kutengana kwao Ila Caren alimuahidi rafiki yake atakapofika mjini atafanya juu chini Lina nae aende mjini wakaishi pamoja kwani hawezi kukaa mbali nae kwa kipindi kirefu. Lina alikubaliana na rafiki yake hivyobakawa na matumaini ipo siku ataenda mjini kuungana na rafiki yake.
Caren alipofika mjini maisha yalienda vizuri akawa anamsifia mama yake mdogo kazi za nyumbani pindi anapoenda kazini na watoto wake walikuwa wanaenda shule hivyo nyumbani alikuwa anabaki mwenyewe. Kadri muda ulivyozidi kwenda Caren alizidi kunawili akawa mrembo na kumfanya mume wa mama yake mdogo kuanza kummendea. Alijaribu kumshawishi Sana lakini Caren akikataa na kuyishia kumwambia mama yake mdogo.
" Wewe msichana Ni mpbavu Sana Yani unashindwa kujiangalia wewe na maisha yako unajali maisha ya watu wengine. Kama ukinikubali nitakupa chochote unachotaka.
" Sitaki na ukiendelea na hiyo tabia yako nitakwambia mama mdogo.
" Oooh kumbe Sasa ngoja tuone Mimi na wewe nani atasikilizwa na huyo mama yako mdogo.
Baba yake mdogo alianza kumfanyia Visa huku akimsingizia Mambo ya uongo kwa mama yake mdogo.
" Mama Jane huyu mtoto wa dada yako ni Malay Sana kwanza Hana adabu anaingiza wanaume ndani kwangu. Nimechoshwa na tabia zake mbaya sitaki kukuona hapa ndani kwangu.
Mama yake mdogo alimfokea na kumpiga Sana Kisha akamwambia
" Kesho jiandae unarudi Kijijini. Kwanza kafungashe vitu vyako usiku huu huu. Caren alienda kufungasha vitu vyake huku akiwa analia.
Kulipokucha Caren aliamka mapema akaenda kupiga mswaki. Mara alitokea jirani yao wa chumba Cha pili.
" Caren hivi Ni kweli unarudi Kijijini? Caren alishangaa huyu mtu kajulia wapi na Mambo yalitokea usiku kila mtu akiwa kajifungua ndani kwake.
" Umejuaje Kama naenda Kijijini?
" Mmmh hizi nyumba zetu hazina Siri kila kinachoendelea huko kwenu huwa nasikia. Kuna kitu naweza kukusaidia kwaajili ya maisha yako.
" Kitu gani?
" Naweza kukutafutia kazi na ukajikimu kimaisha hapa hapa mjini. Kwakuwa Caren hakutamani Kurudi Kijijini Ilibidi akubali hiyo ofa.
" Sawa lakini nitaishi wapi?
" Hilo sio tatizo nitakutafuta sehemu utakaa mpaka utakapopata mshahara wako unaweza kutafuta sehemu ya kuishi.
" Sawa nitashukuru.
" Sasa Mimi sitaki kesi na huyo mama yako chakufanya kachukue begi lako utoke Mimi utanikuta kituo Cha daladala.
" Sawa.
Caren alipiga mswaki haraka akaingia ndani na kuvaa nguo zake Kisha akabeba begi lake na kuelekea walipo panga wakutane.
Walipokutana yule dada alimpeleka moja kwa moja kwenye hotel aliyokuwa anafanya kazi Kama mpishi. Walienda moja kwa moja mpaka kwa muajili yule dada akaongea nae .
" Dominic nimekuletea mtu uliyekuwa unamtafuta.
" Anavigezo vya kufanya kazi kwenye hoteli yetu?
" Ndio, anaweza kufanya usafi.
" Elimu yake? Yule dada alimuangalia Caren
" Umesoma mpaka darasa la ngapi?
" Darasa la Saba lakini naweza kufanya usafi hata kazi yoyote mtakayonipa.
" Mmmm darasa la Saba hapana. Dominic alisema
" Dominic huyu Ni mdogo wangu tafadhali msaidie. Yule dada alimbembeleza Sana Dominic mpaka akubali. Siku hiyohiyo Caren alianza kazi pia akapata sehemu ya kulala pale pale hotelini.
Caren alijitahidi kufanya kazi kwa bidii mpaka wateja walimpenda. Ilipotimia mwezi mmoja alipokea mshahara wake akaenda kupanga chumba chake. Dani ya miezi sita alisimama kimaisha na ndani kwake alikuwa na kila kitu ndipo alipoamua kwenda kumchukua rafiki yake Kijijini wakaja kuishi pamoja. Siku za mwanzoni Lina alikuwa anakaa tu nyumbani huku Caren aliendelea kumtafutia kazi maana alishajuana na watu wengi. Baada ya muda mchache Lina alipata kazi ya kwenye kampuni inayoshuhurika na mapambo na Mambo yote ya harusi.
Ilikuwa ni majira ya saa moja asubuhi Lina alikuwa kalala kitandani huku aliendelea kuvuta shuka Mara alifika rafiki yake.
" Hivi unalala mpaka saizi Ile kazi ulifanikiwa na baba yako? Caren alikurupuka kutoka usingizini.
" Caren mbona haujaniamsha mapema unajua Leo natakiwa kwenda kupamba kumbi mbili za harusi.
" Usinilaumu huo Ni uzembe wako.
Lina aliamka haraka haraka akaenda bafuni kuogaalipomaliza aliniandaa haraka haraka akatoka Chumbani akiwa anakimbia.
" Ungekunywa chai.
" Sio muhimu kwa Sasa.
Upande wa pili tunakutana na wapenda nao wawili Travis na Adela ambao wapo kwenye harakati za kufunga ndoa siku chache hapo mbele.
Adela alikuwa kakaa mapajani kwa Travis huku akimuangalia usoni
" Siamini Kama wiki ijayo tunafunga ndoa.
" Yani hiyo siku naisubiri kwa hamu Sana maana Ni siku ambayo nilivyokuwa naiota kila ninapolala.
" Ni kweli uchumba miaka minne sio mchezo.
" Lakini kila kitu kipo sawa, shela lako lipo katika Hali nzuri.
" Lazima liwe katika Hali nzuri na lazima nipendeze nataka kila mtu anione mwanamitindo maarufu nilivyopendeza.
" Safi Sana nataka harusi yetu iwe gumzu nchi nzima.
Heka heka na maandalizi ya harusi yakiendelea wazazi wa pande zote mbili walikuwa bize na maandalizi ukizingatia familia zote mbili zilikuwa zinajiweza hivyo shuhuri iliandaliwa kwa mamilioni ya pesa.
Hatimae ilifika siku moja kabla ya harusi na kampuni Yakima Lina ulipata dili ya kuandaa kila kitu kinachohusiana na hiyo sherehe na Lina alikuwa upande wa upambaji wa ukumbi mpaka kanisani.
Ilipofika usiku Adela akiwa anaangalia nguo yake ya harusi huku akitabasamu Mara simu yake iliingiza ujumbe. Alisogea kitandani akachukua simu yake na kusoma ujumbe ulliotoka kwenye kampuni yake ya uwanamitindo.
" Adela kesho mapema unatakiwa kufika ofisini kuchukua tiketi kwaajili ya kwenda Afrika kusini kwaajili ya onyesho litakalo fanyika kesho jioni.
NDOA YA BILLIONAIRE ππ2
MTUNZI SMILE SHINE
Adela alifikiri achague Nini Kati ya ndoa au kazi. Alifikiri Sana huku alizunguka zunguka chumbani kwake hatimae alipata chaguo moja alichagua kazi. Alijibu ujumbe aliyotumiwa Kisha akapanda kitandani akalala.
Kulipokucha Adela alijiandaa akatoka nyumbani kwao bila kuniaga mtu akaelekea ofisini akachukua tiketi Kisha akaelekea uwanja wa ndege kwaajili ya kuondoka kuelekea Africa kusini.
Travis alipoamka Cha kwanza alimtafuta Adela ili kumjulia Hali lakini simu ya Adela haikupatikana. Aliamua kuachana nayo akijua wataonana kanisani.
Baada ya muda kwenda bwana harusi alijiandaa wakaenda kanisani wakaja kumsubiri Bibi harusi afike lakini muda ulienda na kila walipomtafuta haikupatikana na nyumbaninkwao hakuwepo. Watu walizidi kuchanganyikiwa. Travis alipata hofu mpaka akahisi joto ikabidi alegeze tai iliyokuwa imekaa vizuri shingoni kwake.
Wakiwa kwenye sintofahamu alifika Lissa rafiki wa Adela, akamfuata moja kwa moja Travis.
" Travis Nina ujumbe wako kutoka kwa Adela.
" Ujumbe gani, yeye Yuko wapi?
" Hayupo yupo safarini kwenda Afrika kusini kikazi.
" Nini?
" Ndio hivyo. Alijibu Lissa Kisha akaenda kupanda kwenye gari akaondoka.
Wazazi na ndugu walipomuina Travis Kama mtu aliechanganyikiwa walimfuata.
" Travis Kuna Nini?
" Adela kaamua kuchagua kazi na sio Mimi, yupo safarini kuelekea Afrika kusini.
" Mungu wangu Sasa tutafanya Nini, hii mbona fedheha, watu watatuchuka, watapata la kuzungumza na waandishi wa habari walijua itakuwa balaa. Aliongea mama Travis huku machozi yalitoka kutoka.
" Mama tuondokeni hapa kabla mtu yoyote hajajua hili itakuwa Ni aibu na nilazima hii ndoa ifungwe kuficha hii aibu. Waliingia ndani ya chumba kimoja Cha pale kanisani , Travis alishikwa na hasira hakujua afanye Nini, kwa pembeni kulikuwa na kikombe Cha bati Travis alikichukua na kukitupa chini kwa hasira.
Mara mlango ulifunguliwa aliingia Lina kuangalia Nini kimetokea. Alipoona Kuna watu alisalimia.
" Habari...
Kila mtu aligeuka kumuangalia kwa makini kasolo Travis alikuwa kajiinamia.
Mama Travis macho yalimtoka Lisa moja kwa moja .
" Adela unetufanya Nini? Travis kusikia hivyo alinyanyua uso wake kumuangalia nae macho yalimtoka alimuangalia kwa makini zaidi. Aliona kwa mbali Kama haoni vizur alimsogelea mpaka karibu na kuanza kumkagua Kisha akasema
" Wanafanana Ila sio yeye Adela ana alama shingoni, nywele zake ndefu zaidi , macho ya huyu makubwa na yakurembua. Travis aliendelea kumkagua Lina huku Lina akiwa anashangaa hakuelewa chochote.
Oscar Kaka yake Travis akasema
" Kwaajili ya kulinda heshima na kuficha aibu unatakiwa kufunga ndoa na huyu binti.
" Nitawezaje kufunga ndoa na mtu nisiemjua?
" Kumbuka wewe Ni Nani.
" Sawa nitafanya. Travis alimsogekea Lina zaidi akamshika mikono yake Kisha akamwambia
" Tafadhali kubali kuwa Bibi harusi wangu nitakupa chochote utakachotaka. Aliongea Travis kwa sauti ya kumbembeleza.
Lina aliganda Kama sanamu huku akimuangalia Travis usoni akithaminusha utahashati wake alihisi Kama kuvutiwa nae lakini kikubwa kilichomshawishi ilikuwa Ni kupewa chochote atakachotaka .
" Sawa nimekubali kuwa Bibi harusi wako. Jibu la Lina liliwafurahisha watu wote waliokuwepo pale. Muda ule ule Lina alichukuliwa kificho akapekejwa saloon kwaajili ya kufanyiwa maandalizi ili aje kufunga ndoa ilivyomkuta kwa ghafla bila kutegemea.
Travis alikuwa anapiga simu na kusisitiza awe mrembo ili aendane na Adela na kila atakaemuona ahisi kuwa Ni Adela.
Kule saloon Lina aliandaliwa kwa umakini mkubwa na kuvalishwa shela zuri na la gharama pamoja na viatu Kisha wakaenda kanisani Lina na Travis walifungishwa ndoa na hakuna ambae aligundua kuwa yule Bibi harusi alikuwa Ni mtu mwingine.
Baada ya ndoa kupita walienda kwenye jumba Lao la kifahari ambalo lilimuacha mdomo wazi Lina kwani katika maisha yake yote hakuwahi kuona jumba zuri Kama lile.
Walipikelewa a kuinyeshwa chumba Cha kufikia.
" Karibu madam hiki ndio chumba chako. Mfanyakazi alimwambia
" Asante. Mfanyakazi alipotoka Lina alianza kuangalia kile chumba huku akikisifia.
" Mungu wangu kitanda kikubwa hivi nitaweza kulala mwenyewe, chumba Kaka hekalu la kifalme. Akiwa bado yupo kwenye Hali ya kushangaa chumba simu yake iliita Caren alikuwa anampigia.
" Hallow Caren
" Uko wapi mpaka muda huu?
" Caren Leo sitaweza Kurudi nyumbani...
" Unasemaje wewe , uko wapi?
" Naomba kwa siku ya Leo uniache kesho nitakwambia kila kitu wewe tambua nipo sehemu salama. Lina alimaliza kuongea akakata simu.
Alienda kufungua bafuni
" Uwiiiii hivi kweli Mimi naweza kutoka kwenye hili jumba pindi atakaporudi huyo Adela? Alivua nguo yake ya harusi akaingia bafuni kuoga , siku hiyo alichukua muda mwingi Sana kuonga maana alikuwa anajisikia Raha hakuwahi kuoga kwenye bafu la aina Ile.
" Yani huku unaweza kulala hata kula chakula hakutii kinyaa kabisa.
Alipolizika kuoga alitoka bafuni akarudi chumbani akiwa kajifunga taulo, alifika kwenye kioo akashusha taulo likaanguka chini akawa anajiangalia Mara ghafla mlango ulifunguliwa Travis aliingia na kumkuta akiwa Lina akiwa Hana nguo, Lina alishituka akaokota taulo haraka wakati huo Travis alikuwa kageukia pembeni huku akiwa kaziba uso wake kwa kiganja.
NDOA YA BILLIONAIRE ππ 3
MTUNZI SMILE SHINE
Lina alijifunga taulo vizuri Kisha akauliza
" Kwanini uliingia bila kubisha hodi ikiwa unajua kuwa nipo humu ndani?
" Hii Ni nyumba yangu sihitaji ruhusa kuingia pale ninapotaka, na wewe kwanini unakaa uchi kwani wafanyakazi hawajakuletea nguo? Lina hakujibu aliona aibu.
" Umeshavaa?
" Ndio. Travis aligeuka kumuangalia akamuona akiwa kafunga taulo lakini sehemu kubwa ya mapaja ilikuwa wazi Travis akajifanya haoni huku akijisemea
" Hiki Ni Nini Sasa sikutegemea Kama ningemkuta Hana nguo. Travis akajikuta amesahau kilichompeleka Mara kigugumizi kikamshika
" Aaaa.... Eeee nil.. nilikuja kukuangalia Kama utakuwa na shida yoyote.
" Sina shida nipo sawa unaweza kwenda kulala.
Travis aliondoka , Lina akaenda kufunga mlango.
" Eti unakaa uchi huyu jamaa Ni mwendawazimu eee. Alivaa nguo alizoandaliwa akapanda kitandani akalala
Kesho yake asubuhi mlango uligongwa ndipo Lina alikurupuka kitandani na kwenda kufungua Kisha akasimama na kujinyoosha huku akipiga miayo Travis alisimama katikati ya mlango akimuangalia.
" Vipi mbona tunaamshana asubuhi Sana. Travis hakujibu alichungulia saa iliyokuwa ukutani na Lina akageuka kuangalia
" Oooh kumbe Ni saa moja . Mara alikuja mfanya kazi kuwaita kwaajili ya kwenda kupata kifungua kinywa.
Madam nimekuletea nguo ya kubadilisha . Kijakazi alisema huku alimkabidhi gauni la mauwa Kisha akaondoka.
" Mr unaweza kwenda nitakuja huko baada ya dakika chache.
" Nitakupa dakika kumi uwe umefika mezani. Travis aliondoka akamuacha Lina anamshangaa
" Khaaa hivi Hawa watu wanaishije au ndio wale wanaokula kwa kengele ikilia wote mezani .
Baada ya kuvaa nguo aliyokuwa aneangdakiwa na mfanyakazi alishuka mpaka sebleni akamkuta Travis kakaa mezani akiwa anamsubiri , kulikuwa kumeandaliwa vitafunwa vingi Sana.
" Kaa uendelee kupata kifungua kinywa.
Lina alianza kujusevia alikula alichokitaka lakini Travis alikuwa anakunywa maji tu huku akiwa anamuangalia Lina anavyokula.
"Lina nazani unajua kinachoendelea Kati yangu Mimi na wewe.
" Ndio uliniambia kila kitu Jana nipo hapa kushika nafasi ya mwanamke wako Adela.
" Vizuri Sana nimefurahi kuona wewe Ni kuelewa alafu mtu yoyote atakae kuja hapa jitambulishe kuwa wewe Ni Adela.
" Sawa .
" Badae nitakupa kiasi kingine Cha pesa kwaajili ya malipo yako.
" Sawa lakini nilikuwa naomba Leo niende kumuona ndugu yangu atakuwa na wasiwasi juu yangu.
" Hakuna tatizo dereva atakupeleka.
"Sawa.
Travis anaonekana haha Raha hata kidogo , Lina alimuangalia na kujiuliza maswali mengi likiwemo la Adela Yuko wapi mpaka Travis akaamua kufunga ndoa na yeye? Alitamani kumuuliza lakini aliogopa kutokana na Travis alivyokuwa lakini Travis Ni Kama alijua Lina anawaza Nini akajikuta anasema
" Aliondoka siku yetu ya harusi, ilikuwa bahati wewe kuwepo pale umenisaidia Sana maana isingekuwa hivyo Sasa hivi habari zangu zingekuwa zimetapakaa mitaani kila mom ja angeniongekea anavyojua yeye.
" Pole.
" Bado sijapoa Hilo swala limevurudga Sana akili yangu.
Alisema Travis Kisha akanyanyuka na kupandisha chumbani kwake. Lina alimuangalia huku alimuonea huruma.
Lina aliondoka akaenda nyumbani kwa Caren, alimkuta Caren amekaa ndani.
" Wewe unaweza kuniambia ulikuwa wapi na kwanini ulilala huko bila kuniambia?
" Tulia shiga yangu nikwambie unajua nyota ya jaa imekuangukia Mimi Sasa hivi Ni MKE wa mtu nimefunga ndoa Jana Tena nime..... Kabla Lina hajamaliza kuongea Caren aliuangalia mkono wa kushoto wa Lina akaona Kuna Pete ya ndoa Tena Pete ya thamani kubwa Sana.
" Unanitania wewe mpumbavu? Unawezaje kuolewa haraka Mimi sijui Wala familia yako huko Kijijini haijui chochote?
" hebu tulia bwana unajua hii imekuja ghafla Sana kwangu kwani hii ndoa haikuwa yangu nimemshikia tu mtu na nikalipwa kwa hili.
" kwahiyo unataka kuniambia Ni ndoa ya mkataba.
" Mimi sijui Ila kwa Sasa najulikana Kama Adela.
" Mmm uneolewa na Nani Sasa?
" Tajiri mmoja hivi anaitwa Travis.
" Bila shaka ni kibabu.
" Wewe unapta mchana Ni bonge la handsome Mimi mwenyewe natetemeka nilikaa nae karibu maana siendani nae kabisa kilichoniponza Ni hii sura wanadai nimefanaba Sana na huyo mchumba wake.
" Daaa Yani naona Kama mchezo wa kuigiza.
" Ndio hivyo shoga yangu nikirudi tutakuwa watu wengine kabisa .
" Kwahiyo pesa nje nje.
" Ndio hivyo na hapa Nina ukaaji dereva ananingija huko nje.
" Wewe Lina acha kunitania. Lina alitoa pesa mpya mpya akampatia.
" Shika hizi zitakusaidia.
" Aaaaaa wewe hivi Ni kweli hiki ninachokiona ama naota ?
Lina alichota maji kwenye kikombe akamwagia usoni Kisha akasema
" Kana ulikuwa kwenye ndoto amka.
NDOA YA BILLIONAIRE ππ 4
MTUNZI SMILE SHINE
Lina alikuwa huru kufanya Mambo yake hakuna aliemzuia lakini ilikuwa lazima atoke na dereva na Kurudi nyumbani mapema.
Kwakuwa alikuwa na pesa Mara kwa Mara alikuwa anatoka kwenda kukutana na Marafiki zake aliokuwa anafanya nao kazi aliwanunulia chakula , vinywaji na kufurahia maisha. wenzake walijaribu kuhoji pesa amepata wapi lakini hakuwa muwazi kuwaeleza
" Jamani kuleni mshube mkimapiza kila mtu ashike njia yake arudi nyumbani kwao.
Travis alikuwa ametoka alienda kuwatembelea wazazi wake aliporudi alimuuliza muulizia Lina
" MKE wangu Yuko wapi?
" Tangia alipotoka hajarudi .
" Inakuwaje anazurula hivi?
Travis alichukua simu yake na kumpigia
" Wewe uko wapi mpaka saizi?
" Nipo kwa rafiki yangu.
" Naomba urudi nyumbani haraka.
" Sawa.
Lina aliondoka kwa Caren akarudi kwenye jumba la Travis aliwakuta wafanyakazi.
" Habari za saizi
" Salama.
" Mr Travis Yuko wapi? Alivyouliza hivyo wake wafanyakazi waliangaliana , Lina akajishitukia akasahihisha kwa kusema
" Namaanisha mume wangu.
" Yupo dinning.
" Sawa.
Lina aliondoka akaelekea dinning huku nyuma wale wafanyakazi wakawa wanaulizana.
" Hivi huyu Ni yeye kweli?
" Hata Mimi Nina mashaka mbona yupo tofauti au ndoa umebadilisha?
" Hapana huyu sio Adela tuliemzoea .
" Ni kweli sio yeye maana sioni ukaribu wao angekuwa ni Adela saizi angekuwa anadeka huyu hayupo hivyo.
" Sasa yeye Ni Nani?
" Sijui au Adela anapacha wake ?
" Sijui, haya Mambo tuwaachie wenyewe.
Lina alifika na kumsalimia Travis, Travis hakujibu salamu alimuuliza
" Ulikuwa wapi?
" Nilitoka na Marafiki.
" Mbona Kama unataka kuniharibia mipango yangu, umesahau Mimi Ni mtu wa aina gani, itakuwaje Kama Kuna mtu anakufuatilia ?
" Lakini nilienda kwa Marafiki
" Hao sio watu muhimu kwako afadhali ungenianbia umeenda kwa wazazi wako ningekuelewa kuanzia Sasa sitaki kusikia habari za marafiki Wala kutokatoka hapa ndani bila sababu za maana . Kumbuka kwa Sasa wewe sio Lina Ni Adela na Adela alikuwa mtu anaejulikana huoni kana ilionekana watu wahabari wsnaweza kukufuata na kukuhoji maswali utawajibu Nini?
" Nimekuelewa nitatulia mpaka Adela atakaporudi she ashike nafasi yake.
" Jiandae kesho tutawapokea wageni hapa nyumbani
" Sawa.
Lina alienda chumbani kwake huku akijisemea
" Haya Mambo sikuwa nayataja kabisa ona Sasa nihavyofungiwa Kama kuku Yaya Mambo Mimi siyawezi bwana huyo Adela arudi haraka.
Kesho yake mapema baada ya kunywa chai alikuja mtu kwaajili ya kumpamba kwaajili ya kupokea wageni. Lina alipendeza Sana kila aliemuina alijua ni Adela Ila tofauti yao ilikuwa ndogo Lina hakutakiwa kuongea Sana maana hakuna alichokuwa analijua kuhusu Adela hivyo alijitahidi kukwepa watu na kuwa karibu Sana na Travis.
Travis aliniachia alikuwa alimkumbatia na kumbusu Lina alitakuwa kujikaza maana hayo Mambo yalikuwa mageni kwake.
Carlos rafiki wa Travis aliyekuwa kachelewa kwenye ndoa alifika siku ya pili alifurahishwa na uamuzi wa Travis na Adela kufunga ndoa.
" Nimefurahi Sana rafiki kwa uamuzi huu ulioamua nilitamani kuwahi ndoa yenu lakini imekuwa bahati mbaya. Ila natumai bado sijachelewa na nimewapa ofa yangu nimewakodia hotel Paris kwaajili ya fungate yenu na kuhusu gharama za usafiri Ni juu yangu .
Travis alipatiwa na kigugumizi hakutaka maswala ya fungate mpaka Adela atakapokuwa karudi pia hakuwa tayari kumwambia yoyote Siri yake zaidi ya wanafanikiwa na alikuwa na uhakika hakuna ambae angetoa hiyo Siri.
" Vipi Kaja mbona umeduwaa?
" Umenifanyia surprise ya Hali ya juu sikutegemea Kama ungenifanyia haya .
" Mimi na wewe ni Kama Pete na Chanda bro , nataka wewe na shemeji yangu mkafurahie fungate yenu huko .
" Sawa nashukuru Sana ndugu yangu tutakwenda.
Baada ya wageni kuondoka alibaki Collin na Travis walikuwa bado wanaendelea kunywa wine.
" Vipi Kaka kuhusu hiyo fungate? Collin aliuliza
" Tutakwenda.
" Na vipi Adela akirudi?
" Sitaki kumfikiria kwa Sasa natunza heshima yangu. Na kwakuwa sipo sawa kiakili naona hii itakuwa nzuri acha Nika refresh mind Ila huyu Adela sijui nitakuja kumpa adhabu gani amenifanya nipitie magumu Sana kainyakua furaha yangu ambayo nilikuwa nsiota kila siku, Yani ndani ya miaka mitatu ndio she kunikimbia siku ya harusi? Kwahiyo huyo oazi yake Ni muhimu kuliko Mimi?
" Usiyafikirie Sana ukaharibu siku yako. Collin alimtuliza , Travis aliendelea kumimina kinywaji na kunywa mfurulizo.
Usiku kabla yakaenda kulala alienda chumbani kwa Lina akamkuta Lina kavaa pajama akijiandaa kulala. Alikaa kitandani akamuangalia huku akiwa anavuta taswila ya Adela. Lina aliona aibu akaangalia chini na Travis aliachia tabasamu.
" Vipi unataka kulala?
"Ndio.
" Kesho kutwa tunaenda Paris kwaajili ya fungate.
" Fungate?
" Ndio Mimi na wewe tutaenda fungate Paris.
" Fungate huwa wanaenda watu walifunga ndoa kwanini usimsubiri Adela wako ili muende pamoja
" Asante kwa ushauri lakini Mimi sikuja hapa kwaajili ya kushauriwa nimekuja hapa kukupa taarifa jiandae na safari na Kama unataka kulipwa kwenye hili Basi usijali nitakulipa.
Kesho yake wakifanya maandalizi kwaajili ya safari , Lina alienda kumuaga rafiki yake.
" Lina hivi Ni kweli umekubali kwenda huko Tena fungate.
" Ndio si nalipwa , Mimi hapa naangalia pesa tu.
" Una uhakika Ni pesa tu na hauna hisia nae?
" Hahahaha rafiki yangu huwa unafikiria ujinga Yani Mimi na Travis hatufananii hata kidogo Mimi kwake nikama kijakazi tu .
" Sawa Ila Nina wasiwasi...
" Wasiwasi wa Nini Tena?
" Unaenda kwenye nchi za watu na haijui kuongea hata kiingereza.
" Kwani huko nitaenda kuongea na Nani, nilitaka kitu Travis yupo .
" Sawa nakuombea uende salama na urudi salama.
Hilo ndilo uliloliacha rafiki yangu.
Kesho yake waliondoka na ndege ya asubuhi na ilikuwa Mara ya kwanza kwa Lina kupanda ndege hivyo alikuwa na ushamba mwingi Ila Travis alikuwa akimuongoza.
Siku hiyohiyo majira ya saa kumi jioni Adela alikuwa karudi kutoka safari ,alipokelewa na dereva wa kampuni abatofanyia kazi akampelekea mpaka kwao. Alipofika alipokelewa na mama yake ambae alionekana kuwa na hasira Sana.
"Habari mama nilikumiss . Alisema Adela huku akitaka kumkumbatia , mama yake alimkata akasogea pembeni.
" Sasa Nini mama unakataa kumbatio langu?
" Umetoka wapi?
" Bila shaka ujumbe wangu mliupata nilipata safari ya kikazi.
" Hivi una akili kweli wewe unawezaje kuondoka siku ya ndoa yako kwahiyo kazi ilishindwa kuahirishwa na huko kazini kwenu hawakuwa wanajua kuwa unaolewa mpaka wakupangie kazi?
" Mama usiwe na wasiwasi nitaenda kuongea na Travis tutapanga tena siku ya kufunga ndoa .
" Afunge ndoa Mara ngapi? Travis ameowa.
NDOA YA BILLIONAIRE ππ 5
MTUNZI SMILE SHINE
Adela hakuamininkile alichokisikia kwa mama yake.
" Unanitania mama Travis hawezi kufunga ndoa na mwanamke mwingine Mimi ndio mke wake na mwanamke pekee wa maisha yake isitoshe nilimwambia aahirishe mpaka nitakaporudi.
" Kwanini hukusubiri ndoa ipite ndipo na wewe uondoke ?
" Mama kumbuka unaongekea kazi yangu , hii kazi niliipambania Sana na ni ndoto yangu tangia nilipokuwa mtoto umenipa mafanikio mengi siwezi kuiacha kirahisi.
Mama yake alimuangalia Kisha akamtingisha kichwa kwa kumsikitikia maana alikuwa kapoteza na akaambiwa anachukulia utani.
" Nitakwenda Sasa hivi kwa mpenzi wangu tutaongea na kila kitu kitakuwa sawa mama jiandae kwa harusi ya binti yako.
Adela hakuingia hata chumbani kwake aliacha mizigo yake pale sebleni akatoka kwenda kwa Travis.
Alipofika kwa Travis baadhi ya wafanyakazi walishangaa Ila wake waliokuwa karibu na Lina walijua tofauti zao.
Adela alienda moja kwa moja mpaka chumbani kwa Travis lakini hakumkuta mtu alitoka hukuvakipiga simu kwa Travis lakini simu yake haikupatikana. Aliuliza kwa wafanyakazi.
" Travis kaenda wapi?
" Kasafiri.
" Kaenda wapi?
Hakuba alieweza kujibu Hilo swali lakini muda uleule aliingia Colin akajibu.
" Aneenda Paris.
" Kuna Nini Paris?
" Kwenye fungate na mke wake.
" Unasema? Inamaana kaowa kweli?
" Ndio wewe si ulitaka kumdhalilisha nae kaamua kuikwepa hiyo aibu.
" Kamuowa Nani?
" Mwanamke mrembo anaeendaba na wewe hivyo mapenzi yake kahamishia kwake.
Adela alitoa tabasamu la kulazimisha Kisha akasema
" Hicho kitu hakiwezekani hata kidogo Adela nitabaki kuwa Adela najua wapi ninapowezakumshika Travis hakuba mwanamke mwingine anaeweza kujifananisha na Mimi. Alijua Adela Kisha akaondoka kwa hasira.alienda bar kunywa kwanza ili akili yake imkae sawa maana hakuwa sawa.
Lucas mpinzani wa kibiashara wa Travis alijua kuwa Travis alikimbiwa na mpenzi wake siku ya harusi na huo ulikuwa mpango wake aligonga pesa ndefu kwa wakuu wa Adela ili wamuondoe Travis apate pigo litakalomchafua na kumpa stress na ukushusha ufanisi wake wa kazi. Lakini matokeo yalikuja tofauti Travis hakutetereka Kama alivyotaka na ndoa alifunga , aliuliza Sana kichwa kwani alitaka kujua Travis kafunga ndoa na Nani? Na kana Ni mwanamke mwingine mbona hakina tetesi zozote ?
" Hivi huyu mshenzi atakuwa kamuowa Nani?
" Inavyosemekana Ni Adela. Alijibu mpambe wake.
" Sio kweli Adela aliondoka Nina uhakika na Hilo.
Hilo swa la Nani kaolewa na Travis kilimuumiza Sana kichwa Lucas.
" Martin naomba uchunguze hili na uniletee jibu lililokuwa na ukweli , haikuwa rahisi Travis kupangua huu mpango wangu.
Huko Paris Travis na Nina waolikuwa waliokuwa ndani Cha chumbani chso Cha fungate kilichokuwa kumeandaliwa vizuri pia walipatiwa huduma zote na wahudumu waliwajali mnoo.
" Travis Sasa tutalakaje ndani ya chumba kimoja?
" Tutalapa tu kwani unaogopa?
" Hapana Ila naona Kama kutakuwa na ugumu flani itakapofika wakati wa kwenda kuoga kwenye kulala hakuna tatizo Mimi naweza kulala popote hata kujikunja pale kwenye Kochi.
" Kwanini kwenye Kochi wakati kitanda Ni kikubwa?
" Sawa Basi tutalapa hata mzungu wa nne.
" Mzungu wa nne ndio Nini?
" Yani wewe utaweka kichwa huku Mimi nitaweka Kule miguuni.
" Vyovyote utakavyo taka.
Lina alikuwa anaangalia madhali ya chumba Kisha akasogea dirishani akawa anachungulia nje , Travis alianza kuvua shati akabaki kifua wazi,Lina alipogeuka alishituka kumuona Travis kifua wazi . Travis alimuona alivyoshituka lakini Wala hakujali aliendelea na Mambo yake na hakusita kuvua suruali yake akabaki na boksa.lina aligeukia dirishani haraka na kumfanya Travis aachie tabasamu alafuvakaingia bafuni kuoga.
" Hivi huyu mwanaume ana kichaa anawezaje kuvua nguo zake mbele ya mwanamke ? Kumbe mtu unaweza ikawa tajiri lakini kichwani hakuba kitu.
Baada ya Travis kuoga alitoka bafuni akiwa kavalia taulo kiunani na taulo nyingine alishika mkononi kwaajili ya kujifuta maji mwilini. Lina alitamani kutoka kwani hakutaka Tena kuangalia mtu mzima akiwa Hana nguo.
" Inaogopeshs kwakweli kuona mtu mkubwa Hana nguo sijui niekekee wapi nimpishe avue kwanza. Lina alikuwa anawaza hivyo Mara akasikia anaambiwa
" Huendi kuoga?
" Naenda. Alijibu Lina haraka Kisha akachukua nguo zake za kubadili akakimbilia bafuni.
Alitoka bafuni akiwa kavaa nguo zake Safi na Travis tayari alikuwa kavaa tishet yake nyeupeee na kaptura ya kadet yenye rangi ya kijivu. Alikuwa kapendeza Sana Lina alibaki anamuangalia .
" Daaa kumbe hili likaka Ni kizuri hivi sikuwahi kuona huu uzuri wake Sasa huyu Adela alianzaje kuondoka siku ya ndoa yao na kumuacha kijana mtanashati akipitia magumu na mwisho kaangukia kufanya maigizo na mtu kana Mimi. Wakati Lina anawaza hayo yote alikuwa kazubaa anamuangalia mpaka pale Travis alipomshitua.
" Vipi mbona unaniangalia hivyo Kuna tatizo?
" Hapana nilikuwa namuangalia tu.
Mara mlango uligongwa akaingia muhudumu akiwa na chakula , aliwaangalia mezani na kuwakaribisha.
" Karibuni Sana.
" Asante. Travis aliitikia sababu akitumia rugha ngeni .
" Kwahiyo tunakula huku nilijuactutatoka hata huko nje kuangalia mazingira.
" Umezoea Sana kuzurula eee? Travis aliuliza na Lina alinyamaza bila kujibu.
" Zingatia kuwa upo fungate na maana ya fungate Ni kutulia kwenye chumba Cha fungate ......
" Lakini fungate yetu Niya kuiguza haina ukweli wowote.
" Lakini tupo fungate, zingatia neno fungate.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote