Romantinc doctor ni simulizi inayozungumzia mabinti wawili Milanda na Raya. Hawa mabinti wanaishi maisha magumu baada ya kutiwa na wazazi wao Raya anaamua kujiingiza kwenye biashara ya kujiuza na kufanya kazi yoyote ilimradi apate pesa . Milanda ni binti mpole sana na mcha Mungu , siku moja aliamua kwenda club huko Raya anaamua kumuuza kwa kijana tajiri Zanda. Milanda anajitahidi kumtoroka Zanda wakati anakimbia anajikuta anatishiwa nguvu na kuanguka. Kijana mtanashati na muungwana Dave anamuona na kutoa msaada, anamkimbiza hospitali na kuanza kumpatia matibabu, Milanda anaamka na kukutana na tabasamu la Dave. Kuanzia hapo Dave alikuwa akimtembelea Milanda na hatimae wanaanzisha uhusiano. Wawili hao wanatokea kupendana sana , dr Dave alimuonesha upendo wa dhati na kumthamini. Siku moja akimpeleka Milanda kwa kaka yake ili wafahamiane maana Dave alikuwa alimsifia sana mpenzi wake. Kufika kule Milanda anashituka kumuona Zanda. Zanda anamfokea na kumtahadhali Dave aachane nae mara moja kwani Milanda ni kahaba anaejiuza. Dave anakataa ushauri wa kaka yake maana anajua yeye ndio mwanaume wa kwanza kwa milanda. Zanda hakubali anafanya juu chini penzi la wawili hao kusambaratika. Je Zanda atafanikiwa ?
MY ROMANTINC DOCTOR ❤️🩺1
MTUNZI SMILE SHINE
Milanda na Raya ni mabinamu wenye umri Kati ya miaka 19_20, Ni mabinti ambao walilelewa pamoja na wazazi wa milanda baada ya wazazi wa Raya kufariki baba yake milanda aliamua kumchukua mtoto wa dada yake kwaajili ya kumlea, mabinti hao wawili waliishi maisha ya raha na kupatiwa kila walichostahili kupewa ikiwepo elimu bora , Milanda na Raya walikuwa wanapendana sana mpaka watu mtaani waliwaita mapacha.
Baada ya miaka kumi wazazi wa Milanda walifariki kwa ajali ya gari na kuwaacha wenyewe. Ilikuwa ni pigo kubwa Sana kwa Hawa mabinti wawili kila muda walikaa kwa huzuni huku wakiwa wameshika Tama na machozi yakitililika kwani hawakuwa na wakumkimbilia . Baadhi ya Mali za baba yake Milanda zilizurumiwa na Marafiki wenye uchu ambao alikuwa alifanya nao biashara kwasababu walijua hakuna ndugu anaeweza kusimamia Wala kuulizia maana Mali nyingi ndugu walikuwa hawazijui kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri, Mara nyingi ndugu wa baba Milanda (Jonathan) walikuwa hawaridhiki pale waliposaidiwa, walipewa mitaji wakaishia kula na Kurudi kuomba Tena msaada hiyo hali ilimchosha Jonathan akawa hatoi tena msaada kuanzia hapo waliomuona ana roho mbaya , anaringa na Mali zake hivyo wakajitenga.
Mabinti hao walipitia wakati mgumu Sana kwani hawakuwa na na chochote zaidi ya nyumba waliyoachiwa.
Baada ya kula msoto kwa muda mrefu Raya aliamua kutoka majira ya jioni na kuzunguka mitaani kwaajili ya kuomba kazi za kufanya ilimradi wapate chakula lakini hakubahatika kupata hata kazi ya kusuuza viombo kwa mama ntilie.
Kigiza kilianza kuingia akaamua Kurudi nyumbani , alitembea kinyonge sababu alikuwa kachoka . Akiwa anajivuta alisikia honi ya gari, alisogea pembeni akasimama na kugeuka kumuangalia aliempigia honi. Ile gari ilisogea mpaka aliposimama , kioo cha gari kikishuka na kuonekana kaka mmoja mtanashati ambae alionekana kuwa mkubwa kidogo kwa Raya.
"Mambo mtoto mzuri.
" Safi shikamoo. Aliitikia kwa sauti ya chini, yule kaka hakutilia ile salamu .
" Acha hizo unanidalimia unataka kujinyima nini mtoto mzuri?
Raya hakuwa na alisema aliangalia tu chini.
" Mbona umechoka hivyo na midomo imekukauka?
" Njaa inaniuma sijapata chakula tangia asubuhi.
Yule kijana alimkagua kuanzia juu mpaka chini Kisha akamwambia.
" Unaishi wapi?
" Kule mbele. Alijibu Raya huku alionyesha kidole .yule kijana alitoa kiasi Cha pesa Kama elfu 40 akampatia.
" Shika hii.
Raya alipokea harakaharaka na kushukuru maana aliona ni pesa nyingi Sana .
" Unaitwa Nani?
" Naitwa Raya.
" Ok Basi kesho nataka tuonane ili nikupatie pesa nyingine ili ukanunue chakula kingi.
" Sawa.
" Unapafahamu white house hotel.
" Ndio napafahamu.
" Basi njoo pale ,ukifika uende moja kwa moja mpaka mapokezi alafu ulizia zanda.
" Kwahiyo nikiulizia zanda nitakuwa nimekupata?
" Ndio jina langu Ni zanda.
" sawa nitafika hiyo kesho.
Raya alienda kununua chakula kisha akarudi nyumbani .
" Raya ulikuwa wapi mpaka saizi?
"Nilienda kutafuta chakula na Mungu ni mwema nimepata japokuwa ilikuwa kwa kuchelewa, nikiwa nimejikatia tamaa alitokea kaka mmoja anaitwa Zanda akanipatia hii pesa.
" Mungu ashikiliwe sana.
" Njoo tule ndugu yangu.
Walikaa mezani wakawa wanakula huku wanapiga stori raya alikuwa akisimulia jinsi alivyo Kutana na Zanda.
" Jamani huyo kaka ana moyo mzuri sana.
" Ni kweli tena kasema kesho muda ya saa moja niende nikachukua hela nyingine.
" Mmmmh na wewe umekubali kwenda?
" Ndio nitaenda kwasababu tuna shinda .
" Ila kuwa makini maana siku hizi binadamu hawaaminiki.
" Huyu kaka haonyeshi kama ni mtu mwenye roho mbaya .
" Basi sawa.
Walimaliza kula kisha wakaenda kupumzika.
Kesho yake muda ya saa 12 jioni Raya akijiandaa na kwenda white houses hotel, alifika mapokezi na kusalimiana na sasa wa mapokezi.
" Habari
" Salama karibu.
" Asante, samahani nilikuwa namuuliza kaka mmoja anaitwa Zanda.
Kuhudumu wa mapokezi alimuangalia kisha akauliza
" Unamfahamu vizuri huyo Zanda?
" Ndio aliniambia nikija hapa nimuulizie.
Yule mhudumu alisita kidogo kumuelekeza Zanda alipo pia alionekana kutaka kuongea kitu lakini kabla hajafanya hivyo Zanda alitokea.
"Raya umefika hapa muda mrefu?
" Hapana nimefika muda sio mrefu.
" Ok basi zinaweza kwenda. Zanda alishika mkono wakawa wanaelekea kwenye chumba cha hoteli ambacho Zanda alikuwa kalipia, waliingia ndani akafunga mlango Raya akaanza kuwa na wasiwasi.
" Mbona unaonekana kuogopa?
" Nataka kuondoka.
" Usijali utaenda kaa hapa kwanza. Alimkalisha kitandani kisha akatoa kiasi cha pesa na kuweka pembeni yake.
" Sikiliza mtoto mzuri hizo pesa zote ni zako ila na mimi naomba nisaidie kitu kimoja.
" Kitu gani?
" Nahitaji penzi lako.
Raya alishituka mpaka akasimama.
" Aaaaa unaenda wapi sasa hebu kaa tuongee mimi siwezi kujilazimisha Kita ambacho hutaki. Raya alitulia akarudi kukaa na kusema.
" Mimi naogopa.
" Wewe mkubwa hivyo unaogopa nini?
" Sijawahi.....
" Kweli?
" Ndio
Basi usijali kwangu nijambo dogo sana tutamaliza sasa hivi na wala sitakuumiza.
Zanda alimshawishi sana mpaka Raya akakubali na kujikuta anampatia Zanda anachotaka. Mwanzo alisikia maumivu na kumuomba Zanda amuachie lakini Zanda hakusikia malalamiko yake.
Baada ya kumaliza alimpa pole na kumuongeza kiasi cha pesa.
" Pole .
" Asante.
"Sasa naweza kukupeleka nyumbani .
" Sawa.
Raya aliingia bafuni akaiga na kujiweka sawa kisha wakatoka lakini Raya hakuwa anatembea vizuri kutokana na maumivu.
Walipanda kwenye gari safari ya kurudi nyumbani ikaanza. Walifika sehemu Zanda alichukuliwa simu kwaajili ya mawasiliano na kumpa namba zake .
" Hii simu nimekununulia kwasababu nikikutana nikipata kwa urahisi pia ukiwa na shida yoyote nitafute.
" Sawa asante.
Raya alifika nyumbani akiwa na pesa za kutosha pamoja na simu mpya .
" Raya hivi vyote umepewa na huyo mwanamume?
" Ndio.
Milanda alikuwa na wasiwasi akaendelea kuhoji
" Kwanini akupe vitu vyote hivi kuna nini unanificha? Na mbona umerudi ukiwa unachechemea?
" Huku kuchechemea nimejikwaa , na kuhusu kusaidiwa ulitaka nikatae kupokea misaada?
" Sijamaanisha hivyo ila nina wasiwasi.
" Wasiwasi unao wewe ila mimi sina wasiwasi kabisa.
Siku zilienda Raya akawa kasha zoea kutoka na Zanda walizunguka sehemu nyingi za starehe na kufanya starehe za kila aina, maisha ya Raya yalibadilika hakuwa anaambiwa wala kusikia chochote juu ya Zanda.
Siku moja wakiwa club ghafla hakuona Zanda akawa anamtafuta dada mmoja akamuuliza
" Anamtafuta nani?
" Zanda.
" Mbona Zanda amechukua dada poa wawili kaondoka nao sasa hivi. Raya aliwahi kutoka nje mpaka kwenye maegesho ya magari akakuta Zanda bado kusimama akiwa na hao wadada aliokuwa wamevalia nguo zilizoonyesha maungo yao.
" Zanda unafanya nini?
" Kwani vipi?
" Umekuja na mimi alafu unaniacha hapa na....
" Wewe hebu ututokee hapa usitake kutuzibia riziki huyu sio wako ni wa kila mtu ambaye atamtaka sasa hivi ni zamu yetu wewe pita kule subiri muda wako na hakuna atakaye kusumbua
Ulitokea ugomvi wa kumgombania wakaja watu kuamua na kumshika Raya sababu wale dada poa walimchangia. Bila huruma Zanda aliondoka na wale wa dada na kumuacha Raya akiwaangalia.
MY ROMANTINC DOCTOR ❤️ 🩺2
MTUNZI SMILE SHINE
Raya akiwa yupo kwenye simanzi ya kuachwa ndipo alipokuja dada mmoja ambaye nae anafanya biashara ya kujiuza akasema.
" Mdogo wangu huu sio muda wa kugombania mabwana mbona wewe ni mzuri tu ukikaa kwenye mawindoni unapata mtu chapu na utapata wanaume wa maana .
" Mimi sifanyi biashara ya kujiuza Zanda ni mwanaume wangu wale washenzi ndio wamechukua mwanaume wangu.
Yule dada alimuangalia Raya kama vile anamshangaa flani alafu akicheka sana kusikia hivyo.
" Tangia nimefika hapa mjini Sijawahi kumuona Zanda akiwa na wanamke mmoja ninachojua huwa ananunua wanawake kila kukicha anabadilisha. Yule anavutiwa nae au kumtamani huwa anamchukia hilo swala la kupenda mwanamke mmoja ni uongo.
Maneno ya ule dada yalizidi kumuumiza Raya na kujutia kutoa usichana wake kwa mwanaume mshenzi asiyejua thamani ya mtu.
Aliamua kurudi nyumbani kwao huku akiwa na huzuni na siku hiyo hakutaka kuongea chochote na Milanda .
Kesho yake aliamka na kuonekana kuwa mnyonge Milanda akamuuliza.
" Vipi mbona umetoa sana?
" Nafikiria haya maisha.
" Kweli maisha yamekuwa magumu ila nilikuwa nina wazo.
" Wazo gani?
" Tufanye biashara.
" Biashara gani? Una mtaji?
" Hata kuuza maandazi mtaani , hiyo biashara haihitaji mtaji mkubwa.
Raya alimuangalia na kuanza kucheka
" Sasa unacheka nini?
"Acha nicheke ndugu yangu eti mimi Raya nipo mtaani na ndoo ya maandazi napita nikitangaza nauza maandazi, hiyo sitaweza kwakweli bora ufikirie jambo lingine ambalo litatupatia pesa za haraka na nzuri ila sio hizo mia mia tena unaetembea kila nyumba na vumbi kibao miguuni mimi hiyo biashara siwezi kabisa
Raya Alikaa nyumbani kwa wiki moja bila kutoka , lakini uzalendo uliomshinda kutokana na maisha kuzidi kuwa magumu akaamua kutoka akawa anaenda club akipata mwanaume anatoka nae na mara kwa mara alikuwa akikutana na Zanda walikuwa wanapishana ila alipomuhitaji walifanya biashara baada ya hapo kila mmoja alipita njia yake.
Hayo ndio yalikuwa maisha ya Raya aliyo jichagulia.
Siku moja Milanda alimuomba Raya watoke wote maana alichokaa kubaki nyumbani mwenyewe.
" Siku hii ndio nilikuwa nasubiri kwa hamu , sasa naona akili yako imeanza kukomaa.
Waliingia chumbani akachaguliwa nguo za kuvaa na viatu virefu pia akampatia wigi safi.
Milanda alipendeza sana pia nguo aliyokuwa kavaa ilimfanya apendeze zaidi maana ilionyesha umbo lake zuri na miguu yake iliyokauka ilikuwa mwazi kutokana na nguo alivyovaa ilikuwa fupi.
Walitoka na kwenda club kwakuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kwa milanda kufika club alikuwa akishangaa na hakutaka kukaa mbali na Raya.
Zanda aliingia club na jicho lake kikatiba kwa Milanda. Alimuangalia sana na kujikuta anatamani na kuhitaji kuwa nae kwa usiku huo.
Alipiga hatua mpaka walipokuwa wamesimama.
" Mambo zenu warembo.
" Safi. Raya aliitikia
" Naona leo upo na mrembo mpya.
" Ni ndugu yangu. Zanda alikagua kuanzia chini mpaka juu kisha akapiga mruzi kuashiria kama kamkubali.
" Vipi zinaweza kuongea kidogo? Alimwambia Raya kisha wakasogea pembeni
" Mmmmh niambie.
" Hakuhitaji ndugu yako.
" Una kichaa yaani upite na mimi sasa inamtaka ndugu yangu.
Zanda alikuwa anamjua vizuri Raya ni mpenda pesa akatia kiasi cha pesa na kumpatia
" Shika hoi fanya mpango.
Raya alizihesabu alafu akasema ongeza kidogo.
Zanda aliongeza
" Subiri nikaongee nae.
" Ok fanya chap namsubiri huyo mtoto hapa.
Raya alienda kumshawishi Milanda na kumuonyesha zile pesa.
" Hizi zote ni zetu nenda kaongee nae pia kuna kazi ndogo utafanya.
" Kazi gani.
" Utajikita huko ni kazi rahisi.
Milanda alimuamini kwasababu alijua Zanda na Raya ni wapenzi.
Wakiongozana mpaka alipo Zanda, Raya akakabidhi kisha akaenda kuendelea na mambo yake.
Zanda na milanda wakiongozana mpaka hotelini wakaingia chumbani, Zanda alifunga mlango na kuanza kupapasa Milanda akamsukuma
" Wewe unataka nini?
" Kwani hujui ninachotaka au unafikiri tumekuja kuangalia na hapa?
" Kwa hiyo hoi ndio kazi iliyonileta hapa?
" Ndio ndugu yako alikuuza kwangu haya songea hapa tumalizane.
Milanda hakukubaliana na hilo alijitetea na kuleta usumbufu uliomfanya Zanda akasirike na kumnasa kibao shavuni.
" Sitakiwi kumaliza nguvu zangu kuvutana na wewe hizi nguvu natakiwa kuzimaliza kitandani.
" Hebu niache twende ukachukua pesa zako.
" Sihitaji pesa hakutaka wewe
Purukushani iliendelea milanda hakutaka kushindwa alijitahidi kujitetea na kumkwangua kwa kucha zake ndefu karibu na jicho hapo ndipo Zanda akamuachia mitandao akapata mwanya akakimbia . Alikimbia sana huku akiwa haelewi anaelekea wapi. Wasiwasi na mapigo ya moyo wake yakienda mbio alifika sehemu akasimama na kujikuta macho yake yanaanza kuona giza na nguvu zikamuishia akajikuta anaanguka na kupoteza fahamu.
Wakati anaanguka kulikuwa na kaka mmoja ( Dave) alimuona na kwenda haraka kumuangalia. Alipiga magoti na kumuangalia mapigo ya moyo. Alipoona bado ni anapumua na mapigo yake ya moyo wanapiga kwa kasi alimbeba na kupandisha kwenye gari akamuwahisha hospitali.
Alipokelewa na nesi wa zamu.
" Doctor Dave ..... nesi hakumaliza kuongea Dave akamwambi
" Nesi nahitaji misaada haraka .
Kesi alienda kumuangalia kitanda Dave akampata kitandani na kuanza kumpatia matibabu .
MY ROMANTINC DOCTOR 🩺 ❤️ 3
MTUNZI SMILE SHINE
Baada ya kumfanyia vipimo aligundua kuwa mgonjwa alipata tu mshituko na kupelekea kupoteza fahamu.
" Hilo ni tatizo dogo doctor unaweza kwenda kupumzika nyumbani sisi tutamuangalia.
" Usijali nitakuwepo hapa mpaka asubuhi.
" Sawa.
Nesi alitoka na kumuacha Dave akiwa na mgonjwa wake.
Dave Alikaa kwenye kiti mpaka usingizi ukampitia.
Hatimae kulikucha Dave alishituka kutoka usingizini akamuangalia mgonjwa wake akamuona bado Kanumba macho, alitoka wodini akaenda kuzunguka aliporudi alimkuta milanda akiwa kaamka na alikuwa anashangaa mazingira ya pale. Milanda alimuiona Dave anaingia alimuangalia na Dave alipomuona kaamka aliachia tabasamu.
" Vipi unajisikiaje mgonjwa wangu?
" Mgonjwa? Kwani hapa nipo hospitali?
" Ndio jana ilianguka barabarani nikakupa misaada.
Milanda alitulia huku akiwa anavuta kumbukumbu ya kile kilichotokea jana usiku
" Naitwa doctor Dave, ukipenda unaweza kuita Dave.
" Wewe ni doctor?
" Ndio.
Milanda alitaka kunyanyuka pale kitandani , Dave akamsaidia kumnyanyua na kumkalisha vizuri.
" Asante kwa misaada wako
" Usijali, unajisikiaje sasa?
" Nipo sawa najisikia vizuri naweza kutoka hapa?
" Kama upo sawa utaruhusiwa kutoka lakini kama bado unashinda inabidi ubaki hapa uendelee kupata matibabu.
" Tafadhali niruhusu niende nitaenda kujiuguza nyumbani sina pesa za kulipia matibabu.
" Usijali kuhusu hilo nitashuhurikia.
Alisema Dave kisha akasimama na kutoka nje ya wodi, alienda kununua maziwa kwenye mgahawa uliopo karibu na hospitali na kumpelekea.
" Shika maziwa kunywa upashe tumbo. Milanda alipokea na kusema
" Asante.
Alikunywa maziwa kwa uwoga kama kwamba alimuigopa Dave.
" Bado unawasiwasi sana unaweza ukaniambia kwanini ule usiku ulikuwa mtaani na ulikuwa unakimbia nini?
Milanda aliwaza ameambiwa ukweli lakini akaona haifai itamuharibia sifa ikabidi adanganye.
" Nilikuwa natoka kwenye sherehe nikakutana na vibaka wakawa wananikimbiza bahati niliwapoteza ndio nikawa nimefika pale barabarani.
" Oooh pole sana
" Asante.
" Maliza maziwa yako nikufanyiwa vipimo nione kama presha yako ipo sawa.
" Sawa.
Milanda alimaliza kunywa maziwa na Dave akampima mapigo yake ya moyo pamoja na presha.
" Kila kitu kipo sawa unaweza kuruhusiwa.
" Asante doctor
"Kama hautojali naweza kukipeleka nyumbani?
Milanda alisita kujibu lakini badae alikubali
" Sawa.
Milanda alikubali wakaondoka na Dave. Wakiwa njiani milanda aliendelea kumshukuru.
" Nashukuru sana kwa kunisaidia na kujijali sijui ingekuwaje usingetokea ule usiku .
" Kikubwa kushukuru Mungu kuwa upo salama ila usipende kutembea mwenyewe nyakati za usiku ni hatari .
" Sawa.
Hatimae walifika mpaka nyumbani kwa kina Milanda akasimamisha gari mbele ya nyumba yao na Milanda alitoa shukurani.
" Nashukuru kwa wema uliomfanyia dr Dave.
" Usijali , hapa ndipo anapoishi?
" Ndio naishi na ndugu yangu.
" Sawa nimefurahi kupafahamu unapoishi nina imani kuwa leo ndio mwanzo mzuri wa sisi wawili kufahamiana na tutakutana tena.
" Ndio, karibu kwetu.
" Nimesha karibia nitakuja siku nyingine
" Ingiza hata mara moja .
Dave alisita sita lakini Milanda alimuomba sana ikabidi akubali.
Waliingia ndani wakamkuta Raya akiwa anakunywa chai.
" Milanda unajua umenifanya niwe na wasiwasi sana juu yako ulikuwa wapi ?
" Tutaongea. Karibu doctor.
" Asante.
Dave na Milanda walienda kukaa sebleni na Raya aliwafuata .
" Huyu ni dada yangu anaitwa Raya, Raya huyu ni doctor Dave alijisaidia jana usiku baada ya mimi kupata matatizo.
" Matatizo? Matatizo gani? Raya alishangaa maana anachojua yeye kuwa Milanda alimjeruhi Zanda na kukimbia na Zanda alimlaumu sana .
" Alikuwa anakimbia akapata mshituko na kupoteza fahamu. Alijibu Dave
" Oooh pole ndugu yangu sikujua kama ulikuwa kwenye matatizo. Alisema Raya huku akimkumbatia lakini Milanda alimkata jicho.
" Doctor Dave nakushukuru sana kwa kumsaidia ndugu yangu.
" Usijali binadamu tumeumbwa kusaidiana.
" Sio wote wenye moyo kama wako.
Dave alikaa kidogo kisha akaaga.
" Sasa acha niwaache tutaonana wakati mwingine.
" Mbona haraka karibu unywe hata chai.
" Usijali mimi nimeshapata kifungua kinywa nipo sawa.
Milanda alimsindikiza mpaka alipoacha gari yake , Dave alitoa karatasi yenye namba yake ya simu na kumpatia .
" Namba yangu tunaweza kuwasiliana.
" Sawa.
" Haya kwaheri. Dave alipanda kwenye gari akaondoka na Milanda akarudi ndani akiwa na hasira .
" Kumbe siku zote unafanya biashara ya kujiuza na unanidanganya kuwa unatunzwa na Zanda, na imekuwaje ukanikuwadia kwa mwanaume wako?
" Maisha ni magumu ndugu yangu hivyo tunatakiwa kupambana tuwezavyo ilimradi tu tupate pesa.
" Kwa hiyo uliona sawa kuniuza kwa mwanaume wako?
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote