My Perfect Husband

book cover og

Utangulizi

PENZI LA DAKTARI NA MIMI
unaweza Amin nilifall In love na daktar ambae alikuwa ananitibu,yaan nilipoteza fahamu NAKUJA kushtuka nakutana na daktar handsome mpaka nikahisi nimekutana na malaika, licha ya muonekano MZURI LAKIN alikuja kuwa mume Bora sana kwangu, Amin usiamin mapenzi ya kweli yapo, na unaweza kukutana na mwanaume mwenye sifa zote mpaka usiamin kama umekutana na mtu ama jini

MY PERFECT HUSBAND 1
HUSQER BALTAZAR
Maisha ni fumbo kubwa sna, kuna muda tunaumizwa sana na mapenzi mpaka tunaamin kama ma[penzi ya kweli hayapo kabisa, kuna muda unapitia magumu kwenye maisha mpaka unajihisi kama upo pekee yako na hakuna mtu yoyote Yule ambae yuko upande wako, na ambae anataman kabisa kukusikiliza, kuna muda tunafanya makosa kwenye maisha ambayo yanasababisha watu wakutenge na kukuhisi kama ni muovu wa mwisho…

Nilikuwa nimemaliza kidato cha nne mwaka mmoja nyuma, na kwa bahat mbaya sikuwa nimefaulu, na kuanzia nipo secondary nilikuwa na mahusiano na mwanaume mmoja ambae tulikuwa darasa moja, na alikuwa amenipita mwaka mmoja tu, alikuwa amenipita mwaka mmoja tu, na alikuwa ndio mwanaume wangu wa kwanza, na wakat huo nilikuwa na miaka 18 tu….

Alikuwa anaitwa Mussa, na mimi naitwa sanifa, tulifanya mambo mengi ambayo wapenzi wengi walikuwa wanafanya, likiwemo na tendo la ndoa, kama tunavyojua kwenye mapenzi kuna hisia, na kunwa muda ni ngumu sana kuzuia hisia zetu, tukiwa na wanaume tunaowapenda ……

Sikuwa nimepanga kubeba mimba, ila sikuwa najua hjata namna ya kutumia uzaz wa mpango vizuri, na kujikuta nabeba mimba ya mussa, kitu ambacho kilibadilisha maisha yangu kwa kiasi kikubwa sana, nilimuambia mussa kuwa nina mimba yake na alikuwa anaonekana kama hakuwa amejipanga kabisa kuwa baba, na alishtuka mno, kutokana na hofiu na wasiwasi mkubwa niliokuwa nao mimi, alikubaliana na mimi ingawa kishingo upande ili asinifanye nijisikie vibaya, ila kadri muda ulivyokuwa unaenda alikuwa anaonekana kama anataka kunitenga, na alikuwa ananiambia vimaneno vya kunitaka nitoe ile mimba, na sio siri nilikuwa naogopa sana….

Nilikuwa naishi nyumban, na nilikuwa na tumbo dogo,. Ila mimba ilikuwa inanipelekesha sana, maana nikaanza kupata zile homa za asubuh, nilikuwa natapika mno, nas nilikuwa siwez kula vyakula vingi sana, kitu kilichopelekea mama yangu kuhisi kama nilikuwa mjamzito, na hata aliponiouliza nikakataa kabisa, ila aligoma kabisa kukubaliana na mimi, hivyo akanilazimisha na nikaenda kupima, ambapo nilikutwa na ujauzito wa mwezi mmoja na wiki mbili……

Mama yangu alipiga ukunga hospital, ,maana aliona kama nimemdhalilisha sana, alikuwa ananitegemea sana, na aliona kama nimemuabisha sana, akaanza kuniuliza baba wa mtoto, ila sio siri nilikuwa naogopa hata kumtaja, maana nilikuwa nampenda sana Mussa na sikuwa nataka kumsababisha matatizo ypoyote yale, mama a;limuambia kaka yangu mkubwa, na akawa ananipiga sana niseme mwenye mimba ila niligoma kusema…..

Pamoja na kumlinda kote mussa, ila hakuwa anajali kabisa kuhusu ninayopiytia na mara zote alikuwa akinisisitiza nitoe mimba, kitu ambacho sikuwa tayar kabisa kukifanya, maana nilikuwa najua madhara ya kutoa mimba, na nilikuwa najua kuwa inaweza kunipelekea kufa au kupoteza kabisa uwezo wangu wa kuzaa…..

Siku mpoja mama alinifukuza, na kunambia kuwa niende nikamlete baba wa mtoto au nirudi nyumban kwake nikiwa sina mimba, sikuwa na pa kwenda zaidi ya kwa mussa, ambapo wakat huo alikuwa naishi kwa kaka yake ambae alikuwa anafanya kazi mkoa mwingine, hivyo nyuumban alikuwa anabaki pekee yake, na hata mimi kwenda kukaa pale halikuwa kabisa tatizo kwake…

Siku moja nikiwa nimekaa nae, akaniletea dawa flani nikanywa, aiseee tumbo lilikuwa linaniuma balaa, nikaanza kulia na kulalamika, na mussa akawa ananiangalia tu, nikaanmza kuvuja damu sehemu za siri, na zikwa zionatoka kwa mabonge mabonge, nikajua lazima alikuwa amenipa dawa za kutoa mimba, nilikuwa namuwa mpaka nahisi kuchanganyikiwa, mpaka kapoteza fahamu, nimekuja kushtuka kesho yake asubuh, na pemben kuna daktar uchwara akanambia kuwa mimba imeshatoka, sikuwa na mpango wa kuzaa, ila sijui ni kwanini roho ilikuwa inaniuma sana kwa kutolewa mimba…..

Basi mussa akaanza kuniletea masupu niwe na kunywa ili kuryudisha damu iliopotea, ila sikuwa na nguvu kabisa, na kuna muda nilikuwa nahisi maumivu makali sana ya tumbo, siku moja nilitoka na kwenda dispensary kutafuta dawa za kupunguza maumivu, wakat narudi nilipita kwenye mtaa mmoja, haukuwa umechangamka sana, si ndio nikamuona mwanaume wangu akiwa na mwanamke mwingine, kwa namna walivyokuwa, basi usingekataa kuwa walikuwa ni wapenzi, nilijisikia vibaya sana, na kuamua kumfata na kumuuliza kuwa Yule aliesimama nae ni nani?...

Aliponiona akaanza kunitukana, aiseee nilioga mvua ya matusi, na akawa anasema kwanza mimi sina ladha, alikuwa ananivumilia kwa sababu hana cha kufanya tu, ila hajawah kunipenda, na kwa kuwa nimeshamuona na mwanamke mwingine nikae nikijua kuwa hataki kuniona tena nyumban kwake, na niondoke, nilihisi kama kuchanganyikiwa, nikawa natembea nisijue hata nilikuwa naenda wapi, nikashangaa nasikia kizungu zungu na kupoteza fahamu nikiwa barabaran…

Nimekuja kushtuka nipo kwenye chumba cheupe na niloipofungua macho nikakutana na mkaka ni mzuri huyo ananiangalia huku anatabsamu, kwa akili zangu za haraka haraka nikajua nimeshakufa sasa pale nilikuwa mbinguni, nikajikuta nimeropoka, “ sitaki kuamin kama nimeshakufa…

Nikashangaa Yule kaka anacheka kisha akasema “ haujafa ila upo hospital, kisha akaanza kunipima pima pale, na kwanamna alivyokuwa na kmuonekano mzuri, nilikuwa nahisi kama ananidanganya kuwa sijafa, maana nahisi katika maisha yangu, sijawah kuona mwanaume handsome kama huyu aliekuwa ananihudumia, akanipima pale kisha akaja kuniuliza kwanini nilitoa mimba, maana ilikuwa inaenda kuniozesha kizazi……

Nikajikuta naanza kulia, nikalia pale, akaanza kufanya kazi ya kunibembeleza pale, mwisho akanondoka na kuniahidi kuwa atakuja kuniangaliua kujua nina hali gani, na nilipokuwa nimelala pale nikasikia manesi wawili wanasema, “ yaan mkaka kusomea unesi ni kazi sana, yaan mkaka handsome kama huyu alafu anafanya kazi ya nursing, yaan huyu kaka kwa namna ambavyo alikuwa na muonekano mzuri alafu angekuwa docta wa kitu flani, mfano hata docta wa wanawake, nakuapia hii hospital yetu isingeisha wagonjwa, ila maskin ya mungu ni nurse analipwa laki tatu, wakawa wanasema wale manures wengine, hapo wanajua kuwa hakuna anaewazingatia, nikajikuta nimeropoka, “ kama nyie mnaona anafanya kazi ya ajabu mbona na nyinyi mn afanya kazi kama yake, yeye ni nurse nay eye ni nurse, tofauti yenu ni maziwa na ndevu tu, na kama ingekuwa kusomea udaktar nikitu kirahisi, na nyie mngekuwa madaktar sasa hivi, na sio mnamsema mtu mnaefanana nae kila kitu kasoro jinsia, nikasema …..

“ sijui nilikuwa najiamin nini, maana kwanza pale nipo hospityal na nilikuwa na uhakika kuwa siwez hata kulipa gharama zangu za hospital, na kingine sikuwa hata najua naenda wapi, alafu naanza kutukana ma nurse, wale manures wawili wakasunya kisha wakaondoka zao,. Kumbe yyule nurse wa kujme ambae alikuwa ananihudumia akaja na kunambia “ asante sana, kuanzia nimeanza kazi hapa, wewe ndio mwanamke pekee ambae umenitetea, nashkuru sana…

“ hawa wadada wanakutaka hawa, ila nahisi sijui ni umewakataa ndio maana wanatuletea makasirikio yao, nikasema kisha akaanza kucheka…
“ kwanini uliamua kutoa mimba? Akaniuliza, nikajikuta naanza kulia, kisha nikamuambia ni story ndefu sana, maana sio mimi nilietoa mimba ila nilitolewea, alinionea huruma kisha akasema kuwa ameshanisafisha hivyo nitakuwa sawa, na jion ya siku hio niliruhusiwa,ila wakat ambao nilikuwa natoka nikapita kaunta, nikashangaa napewa bill elfu 97, nikaangalia pochi yangu nina elfu tatu tu…..

Nikajikuta nimekaa chini na kuanza kulia, na wakat huo Yule nurse wa kiume ndio alikuwa anaenda zake nyumban, aliponiona alikuja, kisha sijui aliongea nn na wale watu wa kanta, na nikaruhusiwa, nikauliza kuhusu bili akanambioa kuwa ameshalipa, sio siri nilijisikia vibaya sana, maana niliamin kuwa analipwa laki tatu alafu atoe elfu 90 kwenye mshahara wake, niliona kama nimempa wakat mgumu sana, akanishika na nikatoka nae mpaka nje, na nilipofika nje, akasema “ naomba namba zako za simu, na nambie unaitwa nani?....

“ naitwa saufa, nikajibu kisha nikampa namba za simu kama alivyohitaji kisha akanambia “ mimi naitwa Suleyman, nimeshakubip na ukifika unapoishi naomba usisite kunitafuta nijue hali yako, kisha akatoa pesa kama elfu kumi na kunipa, nilijisikia vibaya sana, maana nilihisi kama nimemalizia pesa yake , nikakataa mila akanishika moono na kunikabidhi kisha akasema “ kama hauitaki basi itupe kisha akaondoka zake, yaan aliponigusa, aiseee kaka ananukia huyu sijawah kuona, na anamikono ,milain kama hajawah kufanya kazi toka azaliwe, nikajikuta natabasamu huku namuangalia namna ambavyo anaondoka….
NAKUJA………………………….


MY PERFECT HUSBAND 2
HUSQER BALTAZAR
Sikuwa najua hata naenda wapi, maana nilikuwa najua kuwa siwez kwenda kwa mussa, maana nilikuwa nina uhakika kuwa alikuwa na mwanamke wake, na nilikuwa naogopa pia kwenda kwetu, maana sikujua wangenipokea je, ila mwisho nikakata shauri na kusjiambia kuwa “ ,mama ni mama, so acha niende kwa mama yangu, kama ni kunifukuza ni bora nifukuzwe na yeye kuliko kufukuzwa na mussa…..

Tofauti na nilivyofikiria, ila mama yangu alinipokea kwa furaha sana, alikuwa anaonesha ni kiasi gani alikuwa na wasiwasi kuhusu mimi, akaniingiza ndani na kuniuliza kama niko sawa, nikamsimulia mambo yote ambayo niliyapitia, aiseee mpaka mama yangu akaanza kulia, alilia sana kisha akasems “ nilikufukuza sio kwakuwa sikuwa nakupenda mwanangu, ila ni kwasababu nilikuwa nataman sana ujifunze na pia nilikuwa na hasira sana, ila ndio hivyo mwanangu nilikuwa nawasiwasi sana,. Ila angalau umeachana na huyo mpuuzi wako, na hauna mtoto, hivyo haitakuwa shida maana utakuja kuolewa sasa, maana hautakuwa na dosari yoyote hio…………………………..

Basi mama yangu akaanza kunihudumia kama anamuhudumia mzazi, na suleyman hakuacha kunitafuta kunijua hali, alikuwa ni mwanaume anaejali sana, mpaka nikawa nashangaa yaan, alikuwa ananitumia pesa ndogo ndogo za kuendesha maisha yangu, na akawa anazungumza na mimi karibu kila siku, na kwa akili zangu za haraka haraka nikahisi labdfa amenipenda, sasa kwa namna ambavyo nilikuwa na maumivu ya mapenzi, nilitaka kuishi maisha yangu, maana noimuamina sana mussa, alikuwa ni mwanaume wangu wa kwanza na mwanaume ambae nilikuwa nampenda kupita maelezo, na sijawah kuwaza kama kuna siku hata moja mussa anaweza kuja kuniacha, tena kwenye kipindi cha shida ambayo ameisababisha yeye mwenyewe……

Namshkuru mungu suleyman maana hakuwah kutoka upande wangu hata kwa bahat mbaya, alikuwa ni zaidi ya mwanaume na nusu kwangu, alikuwa ni mwanaume anaeniheshimu sana, pamoja alikuwa na juonekano mzuri na alikuwa ananijali sana ila hakuwah kunitamkia neon lolote lile la kunitaka kimapenzi licha ya kuwa alikuwa ananisaidia sana kwenye mambo mengi….

Tulikuwa marafiki sana, yaan ndani ya muda mfupi tukawa kama watu ambao tunajuana sana, maana nilijikuta najua ratiba zake zote, na namna maisha yake yanavyoenda licha ya kwamba hatukuwa tunakaa sehemu moja, alikuwa ananisisitiza sana kuwa nikiwa na shida yoyote ile nimuambie, nikajikuta naogopa sana, kwa maana hakuwa mpenzi wangu, hivyo kumuomba mahitaji nilikuwa naona kama ni kumchosha na nilishaamin kuwa alikuwa na mshahara mdogo sana…..

Alikuwa ni kijana mwenye muonekano mzuri sana, ila alikuwa ni mtu wa mungu sana, mimi sikuwa ni mtu wa ibada, kwa maana nilikuwa ni wale waislamu wa kulumangia tu, yaan kwakuwa baba na mama ni waislam ndio maana na mimi ni muislam ila suleyman akaanza kunibadilisha, akawa anataka niwe navaa mavazi ya stara sana, na alikuwa anataka nirudi kwenda kusoma dini na niwe mtu wa ibada, maana kila muda wa swala akawa ananipigia niswali, na nisiwe muon go nilikuwa namuitikia tu ila sikuwa naswali hata…

Nahisi alikuwa anajua, akaniunganisha na dada mmoja ambae sikuwa namfahamu, akanambia ni ndugu yake, akawa ananiambia kuwa atakuwa anakuja nyumban kwetu, kweli Yule dada ndani ya muda mchache tukawa marafiki sana, sasa akawa ananisisitiza sana katika kufanya mambo mema, mpaka nikajikuta na mimi naanza kufanya ibada taratibu na kusoma dini mpaka nikazoea…

Mama yangu nae hakuamin, maana ungekutana na mimi mwaka mmoja nyuma ungeona ni kiasi gani ujana ulikuwa unaelekea kuniharibu, na mama yangu alishaongea mpaka akachoka, mwisho akaona aniache tu, ila kuanzia suleyman amekuja kwenye maisha yangu nikajikuta nakuwa mwanamke wa tiofauti sana, kutokana na ukaribu wangu na Yule dada alikuwa anaitwa mauwa nikawa mtu wa tofauti mno, na wakat wote huo suleyman hakuwah kunitongoza kabisa, ila alikuwa ananijal mno, na kwa namna alivyo mzuri, niliamin kama ananionea huruma tu, ndio maana anafanya mambo yote yale kwangu, maana kila nikijaribu kujiweka kwa sulayman nilikuwa najiona kama ka hause girl kasichokuwa na thaman kabisa, maana nilijiona kama siendani nae kabisa, nikawa naufundisha moyo wangu kuwa suleyman ni rafiki tu na hawez kuwa tofauti na hapo….

Muda ukaenda akawa ananambia kuwa anataka niwe na fani yoyote ile, akawa ananiyuliza nataka niwe na fani gani, nikamuambia nataman kujua kupika na kupamba keki, nikashangaa baada ya siku mbili ananiita pale hospital, mana hatukuwa tunakawaida ya kuonana mara kwa mara, maana najua yeye ni mtu ambae yuko busy, na kuanzia tumefahamiana tumeshawah kuonana mara moja tena ni muda kidogo, kitu pekee tulichokuwa tunakifanya ni kuwasiliana tu…..

Nilikuwa nimeshaanza kuvaa stara, aliponiona tu akaanza kutabasamu, nikamsogelea mpaka alipo kisha nikamsalimia, akaitikia salamu kisha tukaenda nyuma ya ile hospital kulikuwa na kama kamgahawa hivi tukakaa, ila muda mwingi akawa ananiangalia tu huku anatabasamu, na hasemi kitu, ikabidi nivunje ukimya…

“ bwana muuguzi mbona unaniangalia hivyo? Nikauliza…
Akacheka kisha akasema “ mimi sio muuguzi bana ni nurse wa kiume, naomba usinipandishe cheo…
“ ohhhh nurse wa kiume, haya nurse wa kiume mbona unaniangalia hivyo? Nikauliza tena…
“ kwani macho yanakatazwa kutazama, macho yanaangalia poote pale ambapo poanayavutia, usikute hata umenivutia hapa navunga vunga tu, akasema suleyman …

“ usiniambie kuwa umeshaanza kunitamani, ila wanaume jamani, nikajikuta nimeropoka, sikujua kama hili jibu lilikuwa jibu baya sana kwa suleyman, maana dakika hio hio akawa anataka kunyanyuka na kusema kuwa “ kuna mgonjwa nimepigiwa simu natakiwa nikamuhudumie, kula unachotaka mimi nitalipa….

“ ndio nimekuja sasa hivi, na uliomba sana kukutana na mimi, kwanini unaondoka tena, hapo sikuwa najua kuwa suleyman amemind jibu langiu, niliamin ni kweli kuna mgonjwa yupo nae, kumbe alikuwa ameshakasirika…
Alikuwa amesimama akitaka kuondoka, mara akakaa na kuniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akaniuliza “ hivi ukiulizwa mimi ni mwanuame wa aina gani na mtu utaweza kumjibu vipi?...

“ kiukweli kwenye maisha yangu sijawah kukutana na mwanaume mkamilifu kama wewe, kwanza unamuonekano mzuri sana, mwanamke yoyote Yule mwenye moyo wa kupenda hawez kulaumiwa kwa kukupenda wewe, na kingine ni mtu wa mungu sana, kitu ambnacho hata mimi sikuwah kukifikiria kabisa, na kingine una jali mno, na nina uhakika kuwa mke wako atakuwa mwanamke wa bahat sana kuwa na mume kama wewe, kwa maana unaukamilifu kwenye mambo mengi sana, na sio mwanaume unaependa ujinga kabisa, nikasema…..

Suleyman akaniangalia kisha akatabasamu na kusema “ haya sasa mfano wewe ukiulizwa kuwa unaweza kuwa huyo mwanamke mwenye bahat ya kuwa na mimi kwa kuangalia tabia zangu na kwa namna unavyoniona….
“ sisi ni marafiki wazuri sana na sijui kama tunaweza kuwa wapenzi, nilijibu kwa maana sikuwa najua kama suleyman ameanza kunipenda na ananipenda, na mambo yote ambayo alikuwa anayafanya alikuwa anayafanya kwaajili ya upendo, sasa mimi nikachukulia kama anaongea tu, aiseee alipiga meza ngumi, uzuri ilikuwa ni meza ya mbao hivyo haikuvunjika kisha akanambia “ ondoka… kwa sauti ya ukali mno, mpaka nikaanza kuogopa maana sijawah kumuona suleyman akiwa na ahjadirsa kiasi kile, nikiwa nimetoa macho tu akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema kwa sauti ya ukali tena na kusema “ naomba uondoke saufa, ondoka please, nikaona isiwe tabu nikaanza zangu kuondoka, ila nilipogeuka kumtazama alikaa kwenye kiti kama mtu mwenye maumivu ya moyo makubwa mno, alikuwa anashika ndevu zake kisha ananiangalia kwa jicho flani hivi la hasira mno, utasema amepandisha mashetani…..
NAKUJA……………………..


MY PERFECT HUSBAND 3
HUSQER BALTAZAR
Nikaondoka na kwenda zangu nyumban, nimefika nikamtumia sms kuwa nimeshafika nyumbnan, maana alikuwa annanisistiza sana kuwa nikitoka niage na nikirudi nimuambie, ila hata hakunijibu, nikamtumia sms nyingine inasema “ kuanzia nimekujua sijawah kukuona ukiwa na hasira kiasi kile, na inaonekana kama mimi ndio nimekukwaza, naomba unambie kosa langu suleyman, maana sio siri sijakuzoea hivyo, na kingine, sisi ni marafiki na nakumbuka mara ya mwisho ulishawah kunambia kuwa marafiki huwa hawafichani kitu, na huwa wanaambiana ukweli pale wanapokoseana, naomba unambia kosa langu, na nakuahidi kubadilika na kuwa kama unavyotaka, maana naamin hauwez kunipeleka kwenye njia isiyofaa…

Nikashangaa simu yangu inaita, alikuwa ni suleyman, akanambia “ ni mambo yang utu saufa, naomba usiwe na wasiwasi mamaa, mimi nina kasoro moja tu ya kuwa na hasira za karibu, ila naamin nikiwa na wewe haskitra zote zitaisha, maana ingawa sisi ni marafiki ila sio siri moyo wangu unakuelewa sana, na maneno yako kwangu ni kama yananguvu za ziada, maana hata kama nikitaka kufanya jambo, ila ukisema acha tu, najikuta nimeshaacha, hjivyo usiwe na mashaka kabisa na mimi, nauwe na amani mamaaaa, alafu nataka nianze kukubadilisha jina, na wewe unibadilishe jina, niwekee hata yale majina ambayo unapenda kuwawekea watu unaowapenda na kuwathamin mamaa….

“ unataka nikusave nini? Nikamuuliza…
“ kwani wewe unapenda nini? Akauliza…
“ kiukweli mimi napenda sana cake, chocolate, na lollipop, nikajibu…
“ nikichagua jina naomba uniahidi kuwa ndio utanisave hivyo, akasema suleyman…

“ wewe ni zaidi ya rafiki kwangu, naombi lako kwangu niamri, so nambie chochote na nitatii, niokajibu…
“ my sweet lollipop, naomba unisave my sweet lolippop, ili kila utakapoona lolippop unikumbuke, akasema suleyman ….

Nikaanza kucheka kisha nikasema “ mbona kama unaanza kunitaka bwana nurse, hilo jina watu wanawasave wapenzi wao…
“ eee hata mimi ni rafiki yako kipenzi, na ukitoa neon rafiki kwenye sentinsi nilioisema nakuwa kipenzi chako, sasa kuna shida gani, alafu ukiniita nurse naomba umalizie na nurse wa kiume, maana najivunia sana kazi yangu, nan ataman watu wote ambao wananijua wajivunie kitu ambacho hata mimi huwa najivunia mno, akasema suleyman …..

“ sawa rafiki kipenzi, ambae unataka nitoe neon rafiki nikuite kipenzi, na kwa sisi kipenzi itakuwa ni kifupi cha rafiki kipenzi, nikasema …
“ embu jipigie makofi kwanza, maana siku hizi umekuwa na akili sana , yaan unaelewa mapema mno, hivi darasan kwenu ulikuwa unakuwaga wa kwanza eeee, akasema suleyman …

“ ndio kipenzi ila wa kwanza kutoka mwisho, nikajibu, aiseee alicheka sana kisha akanambia hauna akili wewe…
“ haya tukubaliane kuanzia leo hakuna maswala ya kuitana rafiki rafiki, tutakuwa tunatumia ufupisho wake ambao ni kipenzi, au mpendwa, au kwa kizungu unaweza kuniita my love, mimi wala sitakuwa na neon, akasema suleyman…

“ sasa siku niwe nimakaa nakaazana nakuita my love my love, kumbe mwanamke wako yuko maeneo hayo, mimi najua nimemaanisha urafiki alafu yeye ahisi nimke mwenzie, najiona namna nitakavyopasuliwa mpaka nisahau njia ya kurudi kwetu, nikasema….

“ na ulivyo na maneno, najua hauwezi kukubali kupasulia hadi usahau njia ya kurudi kwenu, najua hata kama atakuchapa na fimbo ila kwa ninavyokujua unaweza ukamsema mpaka akazimia, uongo au ji kweli? Akauliza suleyman ….

“ sasa wewe ndio rafiki ambae unanijua vizur, aiseee mm sikaagi kinyonge, akininyoosha na mimi namnyoosha, yaan ni mwendo wa kunyooshana tu mpaka tumpate mshindi, nikasema


“ unaona sasa, sasa ngoja nikuambie kitu kimoja my love, akasema suleyman ….
“ my love ni neon ambalo tumeshakubaliana kuwa tuwe tunaitana likiwa na maana ya urafiki, ila sijui hata ni kwanini alipolitamka nilijissikia vizuri sana, na mwili mpaka moyo wangu ukaanza kusisimka, nikajikuta natabasamu mwenyewe, mpaka nikashnindewa hata nimjibu nini…
“ kipenzi mbona upo kimya, akaendelea kusema suleyman ….

“ ohhhh samahan my love, siunajua nimetoka kuamka dakika chache zilizopita hivyo ni akili za usingizi hizi, nikajibu, nikashangaa suleyman kahema kwa nguvu, ule muhemo wake ndio ulikuwa unanivuruga kabisa, akawa amekaa kimya kwa kama dakika moja kisha akaniita “ saufa…

Mie tena nikajibu abeee…
“ hivi unataka mwanaume au mume wa aina gani kwenye maisha yako? Akauliza….
“ kama wewe, nikajikuta nimejibu nikijua nimejibu kiutani maana dakika chache nyuma tulikuwa tunaongea kwa masikhara kumbe mwenzangu yuko kihisi mno, akahema tena kisha akasema “ kama mimi eee, kwa sauti flani ya mwanaume ambae hawez kuzizuia hisia zake, mimi nikawa kimya…
“ nijibu saufa unataka mwanaume kama mimi si ndio?, akaendelea kuuliza….

“ samahan sana suleyman, naona kama jibu langu limebadilisha kabisa hali ya hewa, naomba tu, kabla sijamalizia nilichokuwa nataka kusema nikashangaa suleyman anasema kwa sauti ya utulivu sana, kana kwamba alikuwa ananibembeleza akasema “ nijibu mamaaaa, jibu ni dogo sana, ni ndio au hapana na siitaji maelezo mengi zaidi ya hayo please, nataka nisikie umesema ndio kwa maana umekubali au umesema hapana kwa ishara ya kukataa basi na sio jibu lolote lile lingine…………..

“ ndio suleyman nataman kuwa na mume kama wewe, ila shida wewe ni handsome sana , akiwa handsome hivyo kama wewe,m nahisi nitakuwa nakufa kwa wivu, nikasema …
“ aaaa wewe nawe, kwnain uhandsome ni nini, mwanaume handsome ndio hanaga mapenzi ya kweli, au unataka uwe na mwanaume ambae haiuwezi hata kuongozana nae, kuwa na mtu anaekuvutia bana , yaan wewe uvutiwe na mimi na mimi nivutiwe na wewe au unaonaje , akasema suleyman …

“ mbona unajitolea mifano hai sana, nimeshakuvutia nini? Nikauliza
“ woyooo ameelewa na hii, huyu bint mimi naamin walimu walikuwa wanamkatiaga majibu, maana anaakili sana, ulikuwa unatakiwa uwe wa kwanza kutoka mwanzo na sio wa kwanza kutoka mwisho, mimi suleyman nikiwa na akili zangu timamu naomba niseme kuwa nimevutiwa na ninakupenda na wewe my love, akasema suleyman…

‘ ambapo my love inaamaanisha kuwa rafiki yako kipenzi, nikajibu…
“ ewaaaa nakupenda sana kipenzi, hio rafiki utakuwa unaiweka mwenyewe kimoyo moyo, akasema suleyman, mpaka nikajikuta naanza kucheka….
“ nilikuwaga nakuona kama mtu ambae huna maneno mengi na haupendi maneno mengi, sijawah kufikiria kama unavituko kiasi hichi, yaan unaweza kumpa mwanamke yoyote Yule furaha suleyman, wewe ni mkamilifu mno babaaa…..

Akahema kidogo kisha akasema “ mimi sio mkamilifu kwa mwanamke yoyote saufa, ila kwa mwanamke ninaempenda, nikaanza kuona kama huyu suleyman sio utani kama ninavyofikiria bali anamaanisha anachokisema ……
NAKUJA…………………….



MY PERFECT HUSBAND 4
HUSQER BALTAZAR
“ my love mbona kama upo serious sana, nikasema …
Akahema kwa nguvu na kuanza kuongea sauti kama inashindwa kutoka na akasema “ kwani kuna shida gani nikimaanisha, au una mwanaume wako, au kuna mwanaume unampenda, au kuna mwanaume ambae unataman akuoe, au bado unamkumbuka Yule mwanaume aliekutelekeza wakat wa maumivu yako, maana nyie wanawake hamjawah kujua mnataka nini, na naomba usinijibu chochote na nikutakie usiku mwema, na nikuombe kuwa makin sana, maana sio kila mwanaume ni mwanaume wako, akasema suleyman kisha akakata simu……………………..

Nilianza kumuona kama suleyman ananipenda, ila nilishazoea mwanaume akikutaka anakuwa na hisia na wewe na anaweza hata kukushika au hata kukukumbatia hovy, kitu ambacho sikuwah kukiona kabisa kwa suleyman, basi nilikuwa nahisi kama moyo wangu unaenda mbio sana kila nikimfikiria, nilikuwa nataman niwe naongea nae kila wakat, nilikuwa nataman niwe namsikia kila saa, basi nikwa namfikiria pale mpaka ambapo nilipitiwa na usingizi……

Nimekuja kuamka saa kumi nambili, nikakutana na sms mbili na missied call mbili kutoka kwa suleyman, moja ilikuwa inasema amka uswali kipenzi, sikutaka kuendelea kupoteza muda, basi nikaenda kuswali, maana kwanza muda ulikuwa umeshaenda kwa kiasi flani, na nilipomaliza kuswali nikasema nishike simu niangalie ile sms nyingine ilikuwa inasema nini, alikuwa ameandika kuwa “ kuna muda kwenye maisha unaweza ukawa unapitia mambo yenye kukuumiza kwa sababu Mungu anataka kukupeleka kwenye mambo ambayo yatakufurahisha baadae, Muda mwingine tunakataa tamaa sana, na huenda tukawa tunajiona kama watu wasiokuwa na thaman kabisa, ila haya yote ni kwa sababu tumeacha kumtegemea mungu, maana ni yeye pekee ambae anaweza kutukutanisha na mtu bora zaidi kwenye maisha yetu, sio kila mwanaume anaweza kusema nakupenda moja kwa moja ila kuna baadhi ya watu matendo yao ndio yanaongea vilivyopo kwenye mioyo yao, saufa wewe ni mwanamke wa kipekee sana kwenye maisha yangu, na siku zote nitakupenda na kukulinda kivyovyote vile my love, utajua mwenyewe kama utaona nimemaanisha rafiki yangu kipenzi au kipenzi cha moyo wangu…………

Nikajikuta natabasamu, maana sidhan kama kuna mwanamke anaweza kukataa kuwa na mwanaume kama suleyman, basi imefika kama saa nne akanipigia simu, maana sikuyn hio nilitakiwa kwenda kujifunza namna ya kutengeneza cake, maana nilimuambia kuwa ndio kitu ambacho huwa nataman sana kukifanya, akanambia niende mpaka pale hospital atanipeleka, maana hata sehemu yenyewe yeye ndio alikuwa amenitafutia, na ndio aliniahidi kuwa atanilipia ada, nilikuwa nashangaa sana, maana kwanza nilikuwa nahisi kama anakipato kidogo sana, sasa atawezaje kunisaidia mambo yote hayo…….

Sikutaka kubishana nae, maana niliamin kuwa alikuwa ni mtu mzima, na kiukweli alikuwa anajua anachokifanya, nikajiandaa bibi mimi na kuanza safari ya kwenda mpaka kwenye hospital ambayo suleyman alikuwa anafanya kazi…

Nilipofika nikampigia simu kuwa nipo nje, akanambia kuwa atakuwa hapo muda huo huo, na kweli baada ya dakika chache akatoka, aiseee alikuwa amependeza balaa, na vile anakarangi f;lani hivi, na zile lips zake, na urefu na vimacho vyake, na hicho kifua, nikajikuta namuangalia huku natabasamu, maana alikuwa handsome sana mpaka nikawa najiogopa mimi mwenyewe, na alipiga short kanzu flani hivi nyeupe na raba zake, na akawa ananukia nyie nyie nyie, nilikuwa nahisi kama suleyman sio binaadamu bali ni jinni, hivi kweli wanawake hawamuoni wamtege mpaka apambane kunifanyia kila kitu mimi…..


Basi bana akaja mpaka nilipo kisha akanisalimia na kunambia “ siku hizi unavaa star asana mashallah, mpaka naogopa nitakuja kukupenda…
“ kwani huwa hunipendagi? Nikauliza…

NAKUJA


MY PERFECT HUSBAND 5
HUSQER BALTAZAR
“ eeee mimi nikupende ili uniongezee nini, wewe twende huko unapotakiwa kwenda kabla haujachelewa, akasema na mimi nikajikuta natabasamu, ila lile jibu alilonipa kuwa anipende ili aniongezee nini lilinifanya nijisikie vibaya sana, ila nikavunga, tukiwa bara baran badala ya wanaume kunishangaa mimi, wanawake sasa wakawa wanamshangaa suleyman mpaka nikawa najisikia vibaya……


Basi tukafika mpaka hio sehemu ambayo nilitakiwa kwenda kufundishwa cake, lilikuwa ni ghorofa, juu ndio kuna hioo cake class, akapanda na mimi, yaan kuna muda nilikuwa nahisi kama anataka kunishika mkono ila ni kama alikuwa anajizuia tu, na mimi sikutaka kujirahisisha…

Tumefika nikasajiliwa pale, na ada ikawa ni laki moja na nusu kwa mwezi, na natakiwa angalau nisome miezi sita, hivyo nilitakiwa kulipiwa shilling laki tisa za kitganzania, yaan suleyman akatoa zile pesa pale pale mpaka nikashangaa, nikataka kumuuliza alitolea wapi hizo pesa , ila nikaogopa na kujiambia kuwa huyu ni mwanaume na sitakiwi kumhoji sana……

Basi akaniacha hapo, watu wakaanza kuniuliza kuwa huyo kaka ni nani, nikawa nawaambia kaka yangu, ila nilikuwa nasikia wivu vibaya mno, maana nilikuwa nahisi kama nampenda sana, alafu wanawake wanaanza kumuulizia ulizia, vile vibint vya pale vikawa vinataka baadhi niwaunganishe na suleyman ila nilikuwa najua kabisa kuwa siwez kufanya hivyo hata iweje, yaan mimi na akili zangu timamu nikae nimuunganishe mwanaume ninaempenda na mwanamke mwingine si nitakuwa nimechanganyikiwa…

Basi huwa natoka hapo saa tisa, siku hio suleyman hakuja maana alikuwa anashift ya mchana ambapo atatakiwa kutoka saa kumi na mbili, nikawa narudi nyumban, ila kila wakat alikuwa anataka kujua ratiba zangu zote, alikuwa anataka kujua muda nionaoamka, muda ninao lala, muda ambao nitakuwa nakula, na muda ninaopumzika, yaan hata nikienda dukani alikuwa anataka ajue, na wakat wote huo hajawah kunitongoza hata kwa bahat mbaya yaan,ila ananijal mpaka nikawa najiona kama mke wake tayar….

Sasa nilikuwa na rafiki yangu mmoja, ikabidi nimshirikishe, maana niliona kama sio kitu cha kawaida, yaan mwanaume uwasiliane nae wakat wote huo, na hata mara moja asikutongoze, na wakat anakufanyia kila unachokitaka , nikamuulioza akanambia kuwa huyo mwanaume ananipenda ila ananiheshimu sana, yaan anataman sana niwe ni mtu flani hivi ambae najiheshimu sana na ndio maana anataka kila ninachokifanya akijue, ili aweze kujihakikishia kuwa yeye ni wangu pekee yangu, nilimuelewa na nilitaman kujua nifanye nini ili anieleze hisia zake, akanambia kuwa huyo mwanaume anaweza kunieleza hisia zake kwa vitendo na sio maneno hivyo nisiwe na haraka….

Na kweli niliona ni namna gani suleyman alikuwa ananipenda, yaan ilifikia wakat unakuta miki nnaenda collage nay eye anaenda kazin, sasa unakuta wote tupo busy, alikuwa anaweza akaja mpka nyumban kwetu ili tu anione kisha anaondoka zake, ndio nikaja kugundua kuwa alikuwa ananipenda sana, yaan mpaka raha yaan……

Sasa nilikuwa nashangaa mbona hajawah hata kunigusa, ni kwamba hana hisia, maana hata angeniomba sijui kama ningeweza kumkatalia, basi siku moja usiku kama saa nne hivi alikuja nyumban kwetu, ndio alikuwa ametoka kazin, na mimi sikuwa nimevaa vzur sana maana ilikuwa ni usiku, nikatoka na kagauni na mtandio, sikuwa najua kama kale kagauni kalikuwa kanachora tuchuchu twangu, nimefika namuona suleyman jasho linamtoka, nikajua labda anaumwa nikamuuliza unaumwa, akawa kimya ananiangalia tu, si ndio nikasema nimshike paji la uso kisha nimpime joto, aiseee alinivuta akanishushia busu moja matata, mpaka mapigo yangu ya moyo yakaanza kwenda mbio, na hisia za mapenzi zikanipanda kwa kiasi kikubwa mno, maana mimi mwenyewe toka nilipoachana na yule boya sijawah kulala na mwanaume na unapita mwaka sasa, hivyo alichokuwa anakifanya kilikuwa kinanifanya nijisikie vizuri sana…..

NAKUJA……………………………


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote