My Maid (My Baby Mama)

book cover og

Utangulizi

HOUSEGIRL ALIEPENDWA NA MUME WA BOSS WAKE....
muda mwingine uvivu wa wanawake unaweza ukapelekea mwanaume kusaliti ndoa yake...
Unakuta mwanamke anamtegemea house girl kwa kila kitu, hawez hata kufungua macho kwaajili ya kumuaga mume wake...
Mume wake anakuja kisafiri na kuingia jijini tanga, jiji lenye wanawake wanaojua thaman ya mwanaume, wanaokulisha huku wanakuimbia, anakuja kukutana na usaina, mtoto wa kitanga mwenye madeko yake mjini, anajikuta anapata utulivu sana kwa usaina na kuamua kumuoa kama bi mdogo ingawa kwa siri sana..
Wanakuja kujaliwa mtoto, na kwakuwa faris na mkewe mkubwa hawakuwah kubahatika kupata mtoto, faris anamshawish mkewe wakamiasili mtoto, na wanaenda kumchukua mtoto wa usaina na faris kwa maana faris anamuasili mwanae mwenyewe na kumchukua usaina kama yaya wa mtoto wao ili aendelee kumlea...
Faris anajikuta anashindwa kumchukulia usaina kama yaya kama walivyopanga na mapenzi yake na hisia zake zinashindwa kujificha ingawa mkewe yuko hapo hapo, ingawa ndio hajiwez kwa chochote....
Unadhan siku salha akija kujua usaina na faris ni mke na mume kwa maana usaina ni mke mwenzie, na huyo mtoto ni wa mumewe na usaina na usaina sio yaya kama alivyofikiria itakuwaje..
Na je ni nani atakuwa mshindi wa vita hii ya mapenzi kati ya usaina na salha na nani ataishia na majuto?

MY MAID (MY BABY MAMA) 1

MTUNZI SMILE SHINE

Ikiwa ni asubuhi Kwenye nyumba Moja la kifahari anaonekana Binti mrembo akiwa amelala kitandani " Salha, mke wangu amka basi muda umeenda sana " ilikuwa ni sauti ya kijana mmoja mtanashati aliyeenda kwa Jina la Faris" Unataka Nini Tena kuamshana asubuhi asubuhi ? Salha aliongea kwa sauti iliyojaa uchovu " Mke wangu umesahau kuwa unatakiwa kufanya majukumu yako kama mke ,hukuniandalia chochote sio nguo za kuvaa kazini Wala kifungua kinywa " alilalamika Faris" Nimechoka Faris naomba uniache nipumzike ,nilimwambia Sia akuandalie kifungua kinywa na kuhusu nguo Sia atakuandalia pia, kwasababu ni yeye ndo anaekuandaliga hata hivyo" alijibu salha akarudi kulala, Faris hakutaka waendelee kubisha aliingia bafuni akaoga alivyotoka alikuta nguo kitandani alizichukua akavaa Kisha akamsogelea mkewe pale kitandani" Salha mke wangu naenda kazini huamki hata kuniaga ? Aliuliza Faris" Faris kwanini wewe sio muelewa mume wangu unajua kabisa Jana nimechelewa kurudi nyumbani nilikuwa kwenye sherehe ya shoga angu ,nataka kupumzika nikuage Nini kwani hutarudi hiyo jioni " salha aliendelea kulala " Sawa nimekuelewa mke wangu usikasirike uwe na siku njema " Faris alimkiss salha shavuni akaondoka " Shkamoo kaka Faris " alisalimia Sia ambae ni msaidizi wao wa kazi " Marahaba " aliitikia faris" Kaka Faris nimekuandalia kifungua kinywa mezani " alisema Sia baada ya kumuona Faris anaelekea mlangoni aondoke " Oh Asante sana Sia ila nimechelewa sana kazini Leo Wacha niwahi " alisema Faris na kuelekea kwenye sehemu ya kupaki magari kulikuwa na magari kama matano hivi Faris alichukua gari ya aina ya range na kupanda. mlinzi alifungua geti Faris akatoka na kuelekea Moja kwa Moja kwenye kampuni yake " Habari za asubuhi boss " alisalimia rahma ambae ni secretary wa Faris " Salama tu ,vipi Leo nina ratiba Gani ? Aliuliza Faris" Aah una kikao na Mr Rahim saa 5 asubuhi na ni kuhusu mkataba mpya wa kufanya kazi pamoja na kampuni yake" alisema rahma" Na baada ya hapo nitakuwa na ratiba Gani ?" Hautakuwa na ratiba ya nje ya kampuni zaidi ya hiyo Moja tu Kwa Leo " alijibu Rahma " Andaa mkataba wa makubaliano ya mkataba mpya na Mr Rahim kama nilivyokuelekeza Jana " alisema Faris " Sawa boss nitatekeleza kama ulivyosema "rahma alienda kwenye ofisi yake iliyopo nje ya ofisi ya Faris ambae ni ceo wa kampuni" Kama kawaida yako umekuja kulala Tena ofisini kwangu " Faris alimwambia Anwar ambae ni rafiki yake kipenzi" Nimechoka sana Leo sitamani hata kufanya kazi " alisema Anwar " Umefanya kitu Gani cha kukuchosha na wakati Jana ilikuwa ni weekend ? Aliuliza Faris" Si nilienda kwenye sherehe ya Faisal , umesahau kama Faisal ameoa ? Na nilimuona mke wako kwenye sherehe "" Aaagh mambo mengi si unajua Tena natakiwa kufika Tanga week ijayo kuna vitu naenda kufuatilia " alizuga Faris ila ukweli ni kwamba hakuwa na taarifa kama kutakuwa kuna sherehe ya Faisal na Samia baada ya ndoa Yao na mke wake salha alimdanganya anaenda kwenye sherehe ya rafiki yake " Sawa bhana kama ndo ivyo Mimi ngoja nikaendelee na Kazi " Anwar alinyanyuka na kuelekea ofisini kwake yeye alikuwa ni meneja kwenye hiyo kampuni" Ina maana salha ameanza kunidanganya siku hizi anajua kabisa Faisal na Mimi hatuna maelewano mazuri " Faris alitingisha kichwa chake akaanza kufanya kazi zake Siku ilifanikiwa kuisha salama kabisa mida ya jioni Faris aliondoka kwenye kampuni yake na kuelekea nyumbani kwake hakusahau kumnunilia mke wake zawadi kama kawaida yake " Assalam alaykum " alisalimia Faris " Walykum Salam ,karibu mume wangu "salha alimkaribisha mume wake lakini alikuwa busy kucheza simu yake " Salha mke wangu ina maana hujaiona kama nimebeba mzigo ? Aliuliza Faris" Oh sorry ,kuna kitu huku Instagram kimenivutia sana ,we Sia ,siaa " aliita salha huku anacheka " Abee dada " aliitika sia " Pokea mzigo " alisema salha Kisha akaendelea kucheza simu yake " Sawa dada " " Shkamoo kaka Faris " " Marahaba " Faris aliitikia akampa ule mzigo Sia akaupokea yeye akaelekea chumbani " Natamani abadilike lakini kwasababu nampenda itabidi nizoee hii hali " alijiongelea Faris Kisha akaingia bafuni kuoga na baada ya hapo alienda sitting room " Sia mtengee kaka yako chakula basi kwani mpaka nikwambie si ujiongeze " alifoka salha " Sawa dada nitaandaa meza Sasa ivi " alijibu Sia " Amna sia Wala usihangaike natoka kidogo naenda msikitini nikirudi utanitengea " " Sawa kaka " " Mke wangu natoka kidogo naenda msikitini na wewe uswali usifanye mzaha " alisisitiza Faris " Sawa nimekuelewa nitaswali Sasa ivi " alisema salha lakini hakuacha kucheza simu yake ,Faris alitoka akaelekea msikitini Mida ya saa mbili na nusu usiku Faris alirudi nyumbani ,Sia alimtengea chakula" Kaka karibu chakula" " Asante , salha mke wangu twende tukale pamoja " alisema Faris " Wewe nenda tu ukale mume wangu Mimi nimeshakula " alijibu salha huku yupo busy kuangalia tamthilia kwenye runinga " Okay " Faris alienda kula mwenyewe lakini alianza kukumbuka jinsi ilivyokuwa mpaka kumuoa bibie salha.





MY MAID (MY BABY MAMA) 2

MTUNZI SMILE SHINE

Okay " Faris alienda kula mwenyewe lakini alianza kukumbuka jinsi ilivyokuwa mpaka kumuoa bibie salha Miaka minne iliyopita Faris shawar alikuwa ni kijana wa miaka 23 tu na alikuwa amerudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yake nchini Saud Arabia " Kijana wangu umekuwa Sasa na sisi wazazi wako tunataka tukupe zawadi mbili Moja nitakupa Mimi na nyingine atakupa mama yako " alisema Mzee shawar" Nitafurahi sana baba chochote mtakachonipa nitakipokea kwa mikono miwili " alisema Faris huku anatabasamu.. Baba yake alitoa bahasha Moja na mama yake bi Shamsa alitoa bahasha pia ,Faris alipokea bahasha zote mbili alifungua kwanza aliyopewa na baba yake ilikuwa ni bahasha kubwa Faris alitabasamu baada ya kuona kilichopo kwenye bahasha. baba yake alimfungulia kijana wake Faris kampuni atakayoimiliki yeye mwenyewe" Asante sana baba Allah akuzidishie " alishukuru sana Faris " Hivyo ni vitu vidogo tu kijana wangu ,fungua na hiyo bahasha nyingine " alisema Mzee shawar.Faris alifungua lakini tabasamu lililokuwepo usoni mwake lilififia " Mama ,baba hii ina maana Gani ? Aliuliza Faris huku kashika picha za msichana mrembo mkononi mwake " Unatakiwa kuoa Faris na hakuna msichana atakaekufaa zaidi ya salha Binti Suleiman namjua vizuri ana maadili mazuri na mtoto wa rafiki yangu" alisema bi Shamsa" Baba na mama ninaweza kukataa kumuoa huyu Binti ? Aliuliza Faris kwa upole " Hapana hairuhusiwi kukataa kwani tayari tumesha peleka posa na mahari Imeshalipwa na ndoa ni week ijayo usitake kututia aibu Binti mwenyewe ameshakubali wewe unataka ukatae " alisema Mzee shawar" Nitafanya kama mlivyosema nimekubali kumuoa " alikubali Faris lakini moyoni alikuwa hajalidhia kabisa Wazazi wake walifurahi sana wakaahidi mengi kwa kijana wao kuwa watawajengea na nyumba kubwa ya kuanzia maisha.. Usiku mida ya saa 5 Faris alimpigia simu rafiki yake Faisal " Faisal kuna kitu nataka nikwambie" " Kitu Gani hicho usiku wote huu"" Nitakuja hapo kwenu Sasa ivi " alisema Faris" Okay wewe njoo lakini unajua pa kupita sio mlangoni " " Poa "Faris alitoka nyumbani kwao akaelekea nyumbani kwa kina Faisal hapakuwa mbali sana na nyumbani kwao ,aliruka ukuta akapanda ghorofani kwa kutumia kamba akaingia chumbani kwa Faisal " Oya bro umekuja kweli? Mimi nilijua utani basi hicho kitu kitakuwa kipo serious sana " alisema Faisal" Ndiyo sio utani ,unajua ndo kwanza nimerudi Tanzania Sina hata mwezi lakini baba na mama wanataka nioe na wameshanitafutia mwanamke wa kuoa " alisema Faris akaweka kituo " Hahahah Sasa unaogopa kuoa au kwanza huyo demu mwenyewe yupo je analipa ?" Aliuliza Faisal,Faris alikaa kimya kwa muda akitafakali amueleze vipi Ili Faisal amuelewe " Ila usikasirike bro Mimi mwenyewe nilishtuka sana baada ya kuona picha zake " " Wewe nioneshe Izo picha acha maneno mengi " alisema FaisalFaris alitoa picha kwenye mfuko wake wa suruali akampatia Faisal " Acha utani kaka huyu si salha wangu ,salha Binti Suleiman au naona wenge ? Aliuliza Faisal ." Ni yeye kabisa kaka" Faris alikuja kushtukia ameshikwa shati " Kwahiyo umekuja hapa kunionyesha kuwa wewe ndo sababu ya salha kutaka kuachana na Mimi si ndio " Faisal alikasilika sana " Hapana bro Mimi naanzaje na wakati najua kabisa salha ni shemeji yangu" lakini Faisal hakutaka kumsikiliza Faris akaanza kumpiga ulikuwa ugomvi mkubwa mpaka baba yake na mama yake Faisal pamoja na kaka yake waliamka na kwenda kuamulia ugomvi " Nyie kuna Nini acheni kupigana " alifoka baba yake na Faisal na kaka yake Faisal alienda kuwaachanisha " Nyie si ndo mnajiitaga mapacha nyie imekewaje Leo mnagombana shida Nini ? Aliuliza ramadhan kaka yake na Faisal" Usiniulize Mimi muulize huyu boya " Faisal alitaka Tena kumvamia Faris akazuiwa " Eti Faris shida Nini mpaka mnagombana ? Aliuliza baba yake na Faisal " Uncle Mimi Sina kosa nimerudi nyumbani siku siyo nyingi wazazi wangu wamenitafutia mchumba na kwa bahati mbaya huyo mwanamke alikuwa ni shemeji yangu kwa Faisal Mimi sikuona kama itakuwa sahihi kumuoa ndo mana nipo hapa kumuomba yeye ushauri tunafanya Nini ?" Aliongea Faris " Huyu msichana unaemzungumzia anaitwa nani ? Aliuliza baba yake na Faisal " Anaitwa salha" alijibu Faris" Kama huyo mwanamke ameridhia umuone wewe nenda tu ukamuoe kwa Faisal hakuna muoaji " alisema baba yake Faisal" Baba kwanini unasema hivyo ,Mimi nampenda sana salha" alilalamika Faisal" Huo moyo wako unapenda wanawake wangapi , kuna Layla, swaumu , hamidat , zaituni , Maryam na salha hao kwa ninao wajua tu sijui kama kuna wengine " alisema ramadhan kaka wa Faisal" Umeona kumbe kaka yako anawajua Hadi kwa majina ,Mimi mara kibao nimekuwa nikikuona na wanawake tofauti tofauti muache salha aolewe na Faris ,Faris ni kijana mzuri sijui kwanini alikuwa na urafiki na wewe " alisema baba yake Faisal Kisha akaondoka " Badilika mwanangu kwanini Kila siku wewe tu Kwani huoni Faris mwenzio alivyo kijana mwema Hadi nawaonea wivu wazazi wake " aliongea mama yake na Faisal kwa hasira na yeye akaondoka " Mnanikosea sana"alilalamika Faisal" Faris twende nikupeleke nyumbani achana na huyo mpuuzi" alisema ramadhan alimshika mkono Faris wakatoka nje Walipanda kwenye gari na safari ya kwenda kwa kina Faris ikaanza " Faris wewe ni kama mdogo wangu pia si unalijua Hilo ? Aliuliza ramadhan" Ndiyo kaka najua " " Nakuomba usikatae kumuoa salha ni msichana mzuri licha ya kuwa amelewa kwa kudekezwa sana lakini anatabia nzuri na pia kuhusu salha na Faisal walishaachana na aliyesababisha ni Faisal mwenyewe , salha alimfumania na mwanamke mwingine na badala ya kuomba msamaha akaanza kumtukana salha pamoja na familia yake ukikataa kumuoa salha sio yeye tu atakae pata aibu bali familia yake yote itapata aibu " alisema ramadhan " Kwa kuwa ni wewe umesema hivyo nitajitahidi kusahau yaliyopita kuwa alikuwa shemeji yangu na nitajifunza kumpenda na nitampa furaha ,sipendi kuona mwanamke anateseka " alisema Faris" Asante sana Faris" " Usijali kaka " Faris alishuka kwenye gari na kuingia nyumbani kwao kwa kujificha .. hatimae siku ya ndoa ilifika walifanyiwa sherehe kubwa sana na baada ya hapo maisha ya ndoa yalianza walijikuta wanapendana na kufumba na kufumbua miaka minne ikapita" Yupo hivi kwasababu ya malezi aliyopata kwao sio kosa lake " alijiongelea Faris huku anaendelea kula " Umesemaje mume wangu ? Aliuliza salha " Nilikuwa nasema nakupenda mke wangu " alisema Faris huku anatabasamu" nakupenda pia mume wangu " salha alimtumia Faris mabusu ya hewani Kisha akaendelea kuangalia tamthilia.


MY MAID (MY BABY MAMA) 3

MTUNZI SMILE SHINE

"nakupenda pia mume wangu " salha alimtumia Faris mabusu ya hewani Kisha akaendelea kuangalia tamthiliaFaris alimaliza kula Sia akatoa vyombo , Faris alienda kukaa pembeni ya salha " Mke wangu naweza kukuuliza kitu ? "" Ndiyo wewe uliza tu mume wangu " " Jana ulienda kwenye sherehe ya nani ?" Salha alishtuka kidogo lakini akazuga " Ni rafiki yangu anaitwa sada wewe humjui " alidanganya salha" Niambie ukweli " Faris alianza kukasirika " Basi unakasirika Nini nitakwambia , Mimi nilienda kwenye sherehe ya Faisal na Samia" " Kwanini ulinidanganya ?"" Sikutaka ukasirike ndomana ,Mimi sikutaka kwenda ila yule Samia alinitumia message kama huamini simu yangu hii apa " salha alimpa Faris simu yake Faris aliingia sehemu ya message na kweli alikuta message nyingi za huyo Samia : "Najua bado unamtaka Faisal wangu angalia tu usije ukalia mbele za watu kama hutaki kuaibika usilete pua yako ukumbini"" Kwanini nilie nahisi nitacheka kwa furaha kwani nimeondokana na Hilo jinamizi na nimempata mume anaejua Nini maana ua upendo na kumuheshimu mwanamke na kwa taalifa yako kesho nakuja kwenye hiyo sherehe yenu na zawadi nitakuletea upo" Faris alisoma zile massage akaanza kucheka " Sasa unacheka Nini ? Aliuliza salha " Nimefurahi kuona mke wangu ananipenda " alijibu Faris huku anatabasamu"Kwani nani alikwambia sikupendi ,embu Lete simu yangu " " Twende tukale mke wangu muda umeenda saa nne saizi " alisema Faris " Faris wewe acha nimalizie tamthilia yangu kwanza " salha alimnyanganya faris limoti akawasha Tena tv" Mimi naenda kulala lakini hakikisha hauchelewi kuja kulala sio asubuhi nakuamsha kuswali unaanza kuleta Sababu zako zisizo eleweka " " Kama nipo kwenye siku zangu je ? Alisema salha " Unadhani nashindwa kukukagua " Faris alimsogelea salha walijikuta wanaanza kucheka " Usiku mwema" Faris alimkiss salha shavuni akaelekea chumbani Kesho yake asubuhi Faris alijiandaa na kwenda kazini.. Faris alipokea simu Toka kwa baba yake Mzee shawar " Shkamoo baba " " Marahaba , jioni ukitoka kazini pitia nyumbani kwangu kuna mambo muhimu nataka tuyaongee kama familia " alisema Mzee shawar " Sawa baba nitajitahidi kuwahi " Jioni baada ya Faris kutoka kazini alienda Moja kwa Moja nyumbani kwao akamkuta baba yake na mama yake pamoja na salha alishangaa kwanini salha Yuko pale " Assalam alaykum " alisema Faris " Walykum Salam ,karibu mwanangu " bi Shamsa alimkaribisha mwanae Faris " Asante mama " Faris alienda kukaa pembeni ya salha " Tusicheleweshe muda madhumuni ya hiki kikao ni kutaka kujua mnampango Gani mana salha ameshaenda Kila aina ya hospital Hadi nje ya nchi lakini majibu ndo Yale Yale kuwa Hana uwezo wa kushika mimba " alisema Mzee shawar" Baba ,mtoto ni zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu na natamani sana kuwa na mtoto lakini kumbuka pia watoto ni mtihani tunaweza tukapata mtoto kesho akawa mtenda maovu ,huenda Mwenyezi Mungu katuepushia Hilo " " Kwahiyo mwafaka wako ni upi kama hamuwezi kupata mtoto na kuoa mke wapili hutaki ? Aliuliza Mzee shawar"Sitaki mtoto Wala sitooa mke wa pili mtanisamehe sana sijawahi kwenda kinyume na nyie ila hii itakuwa ni mara ya kwanza " Faris alisimama akaondoka " Baba , mama nipeni muda nitaongea na Faris atakubali kuoa mke wa pili " alisema salha" Hapana Haina haja " alisema bi Shamsa" Kwanini ? Aliuliza Mzee shawar" Ni kweli Faris tumemzaa akiwa peke yake naelewa unachotaka unatamani kuwa na wajukuu na Faris awe na familia kubwa lakini utakuwa unawaumiza wote wawili Faris na salha kwa wakati mmoja kwanini tusiwaache wakaamua kufanya wanachoona kwao ni sawa " alisema bi Shamsa" Sawa fanyeni mnavyotaka " alikubali Mzee shawar" Salha Binti yangu nenda kamuite Faris tulimalize hili " " Sawa mama " salha alitoka nje akamkuta Faris kakaa kwenye ngazi akiwa na mawazo " Faris mume wangu " aliita salha " Kama umekuja kunishawishi Ili nikubali kuoa mke wa pili naomba uondoke" alisema Faris" Mimi nilivyo na wivu nikubali kabisa na kukushawishi uoe mke wapili labda nitakuwa Sina akili " alisema salha " Hahaha " walijikuta wanatabasamu" Baba na mama wanakuita ndani mama amemshawishi baba atuache tufanye tutakachoona kwetu ni sawa " " Kweli ? Aliuliza Faris" Ndiyo , twende " salha alimshika Faris mkono wakaingia ndani" Baba na mama naombeni mnisamehe sikukusudia kuondoka kwa namna Ile zilikuwa ni hasira tu " Faris aliomba msamaha " Usijali naelewa unavyojisikia umekuwa ukitii Kila tunachokwambia tangia ulipokuwa mtoto " alisema Mzee shawar " Baba,mama ..Mimi na mke wangu tumeamua kuasili mtoto " alisema Faris " Sio wazo baya ilimladi mmelidhia wote wawili Mimi Sina neno Tena " alisema Mzee shawar Faris na salha walifurahi sana na baada ya chakula cha usiku walirudi nyumbani kwao " Jumamosi ya weekend hii naenda Tanga mara Moja tunataka kufungua tawi la kampuni yetu huko " alisema Faris" Jamani utakuwa huko kwa muda Gani ? Aliuliza salha " Kama mwezi mmoja hivi au mambo yakiisha mapema itanichukua week tatu tu " " Unavyosema Sasa week tatu tu kama vile ni siku kidogo Mimi nitakuwa peke yangu siku zote hizo jaman "alilalamika salha " Ni kazi tu hata Mimi sitaki kuwa mbali na wewe mke wangu kipenzi " " Sawa ila kuna kitu naona unataka kusahau " alise!a salha " Kitu Gani hicho ? Aliuliza Faris" Umesahau kuwa tunatakiwa kwenda kuasili mtoto " " Oh nilisahau kabisaa, ila subiri nikirudi tutaenda pamoja " " Sawa mume wangu" Siku ya ijumaa usiku fasir alikuwa anajiandaa na safari ya kuelekea Tanga " Sia usisahau kupiga pasi Izo nguo za kaka yako basi " alisema salha " Sawa dada naenda kupiga Sasa ivi " " Ndo usichelewe mana wewe nakujua mara unasahau " alisema salha " Dada nae kwa kutuma kama muhindi na nimeshamwambia mwaka huu ni wa mwisho narudi kwetu " alilalamika Sia, Faris alimsikia akamfuata.


MY MAID (MY BABY MAMA) 4

MTUNZI SMILE SHINE

Faris alimsikia akamfuata " Sia mdogo angu na jua unafanya kazi nyingi sana za kuzidi uwezo wako yote ni makosa yangu" " Sio hivyo kaka " " Subiri nikirudi nitafanya mchakato upate mtu wa kusaidiana nae kazi za hapa nyumbani " alisema Faris" Asanteh sana kaka kwa kunijali kama mdogo wako " " Wewe ni mdogo wangu na sio kama mdogo angu , uwahi kulala sawa ee"alisema Faris Kisha akaondoka Kesho yake asubuhi Faris aliondoka na kuelekea Tanga akiongoza na secretary wake mwingine aliyeenda kwa Jina la hamisi " Sikutegemea kama patakuwa Pako vizuri hivi " alisema Faris baada tu ya kufika eneo watakaloanza ujenzi wa kampuni Yao mpya " Kwani ulikuwa huniamini nilikwambia eneo lipo vizuri " alisema hamisi " Vipi kuhusu ujenzi unaanza lini umeshafanya michakato yote? aliuliza Faris" Kesho mapema sana watafika hapa mafundi ,Tena nimeajiri kabisa kampuni ya ujenzi inayojulikana na sikuokota mafundi mtaani " " Vizuri sana " Faris alikagua kagua lile eneo mwisho waliondoka hamisi alienda nyumbani kwa mama yake aliyekuwa akiishi huko huko Tanga na kwa upande wa Faris alikodi nyumba nzima ambayo angetumia kwa siku atakazokuwa pale " Habari zenú " Faris aliwasalimia mafundi " Salama kabisa bosi" " Aah niiteni tu Faris ,mnaweza kwenda kuanza kazi ila abaki kiongozi wenu nataka kuongea nae mawili matatu " mafundi waliondoka akabaki mmoja " Naitwa luckman Mimi ndo kiongozi wao " alijitambulisha kiongozi wa wale mafundi " Nashkuru sana kukufahamu , nilikuwa nataka kujua kuhusu chakula inakuwaje Mimi ni mgeni hapa sijui nitawaagizia wapi chakula na mwenyeji wangu hajafika mpaka Sasa " alisema Faris" Usijali kuhusu Hilo nitaagiza kuna mtu namfahamu anafanya biashara ya chakula " alisema luckman " Okay vizuri nataka uongee nae nijue ni kiasi Gani kwanzia kifungua kinywa mpaka chakula cha mchana vyote vitakuwa juu yangu " " nitawasiliana nae Sasa ivi" luckman alisogea pembeni kidogo alitoa simu yake akampigia mama yake " Shkamoo mama " " Marahaba" "Mama chakula cha mchana itakuwa kiasi Gani kwa watu kama 25 hivi ? Boss wangu anahitaji kuagiza" Aliuliza luckman" Kwanza huyo bosi wako mwambie atoe pesa ya kuanzia kama anataka chakula kizuri " alisema bi mboni mama wa luckman" Ngoja nimuulize " luckman alimsogelea Faris " Bosi unataka chakula cha kiwango Gani ,Yani kama ni chakula kizuri zaidi unatakiwa kutoa pesa ya kuanzia " alitoa maelezo luckman" Laki tano inaweza kutosha kwa kuanzia tu na nitakuwa namlipa Kila week muulize kama atakubali " alisema Faris " Mama anasema ana laki tano ya kuanzia na atakuwa anakulipa Kila week apo unasemaje ? " " Mwambie ailete hiyo pesa saizi tukafanye manunuzi " " Huyo mtu mwenyewe ni mgeni ngoja niongee nae nione atasemaje " luckman alikata simu akaenda kwa Faris " Amesema pesa ipelekwe saizi akafanye manunuzi " " Tunaweza kwenda wote ? Aliuliza Faris" Ndiyo bosi tunaweza kwenda wote " luckman alipanda kwenye gari la Faris na safari ilianza mpaka kwenye mgahawa mmoja " Mmmh huu mgahawa mbona wa hali ya chini sana chakula chake kitakuwa kinapikwa kwa usafi kweli ? Faris alijiwazia ila hakuonyesha tofauti yoyote " Bosi Faris tumefika unaweza kushuka " alisema luckman" Hapana Mimi sitoshuka chukua pesa hii hapa mkabidhi haraka tuondoke " alisema Faris huku anamkabidhi luckman zile pesa " Sawa bosi " luckman aliingia ndani ya mgahawa akamkuta bi mboni na mdogo wake " Assalam alaykum kaka luckman" alisalimia Binti aliyeenda kwa Jina la Usaina" Walykum Salam ,kumbe na wewe upo hapa" " Ndiyo nasaidia saidia " alijibu Usaina" Enheee amekupa hiyo pesa ? aliuliza bi mboni " Ndiyo hii hapa utaandaa chakula utakachoamua wewe nakuaminia chakula chako mara zote ni kitamu " luckman alimkabidhi mama yake zile pesa akaondoka Luckman na Faris walirudi eneo la ujenzi ....Usaina Amour ni Binti wa miaka 22 tu kwao wamezaliwa watatu yeye na kaka zake wawili luckman na juma ,ni Binti mwenye heshima sana lakini alikuwa muongeaji kupita maelezo na mchapakazi Kila mtu alimpenda sana kuachilia mbali na kuwa na heshima kwa Kila mtu pia alikuwa ni mrembo sana. Bi mboni na Binti yake Usaina walienda sokoni walinunua vitu mbalimbali kwaajili ya kupika na baada ya hapo walianza kuandaa chakula " Mama kwani uyo bosi wa kaka luckman umeshawahi kumuona ?" Aliuliza Usaina huku anakaa chini " Maswali Gani hayo ya kijinga si ulikuwepo hapa wakati naongea na simu na kaka yako amesema kuwa ni mgeni, najua unaniuliza uliza maswali ya kijinga Ili nisikutume " alisema bi mboni" Mama bhana niache nipumzike mguu kwanza unaniuma mwambie juma apeleke icho chakula Mimi siendi Leo nitaenda kesho"alilalamika Usaina " Mwana koma kaka yako juma ana kazi nyingi za kufanya haya nyanyuka haraka uende kwani umeambiwa unaenda kwa mguu si unachukua bodaboda hapo " Usaina alinyanyuka na kuelekea ndani " Unaenda wapi ? Aliuliza bi mboni " Naenda kubadirisha nguo mama ona hii ilivyo chafuka " Usaina alienda kubadirisha nguo alitoka akachukua vyakula vilivyokuwa vimepakiwa vizuri aliita bodaboda akapanda walifika eneo la ujenzi ..Usaina aliangaza huku na huku kumtafuta luckman lakini kwa bahati nzuri alimuona Faris akiwa amevalia overall na mabuti " Wewe mkaka njoo unisaidie kushusha basi umeniona lakini unajifanya kama hujaniona vile " Usaina alimwambia Faris asijue ndiyo bosi mwenyewe " Mimi ? Aliuliza Faris huku anajinyooshea kidole " Ndiyo wewe kwani hapo kuna mtu mwingine zaidi yako " alijibu Usaina , Faris alisogea akaenda kumsaidia kushusha vyakula kwenye bodaboda" Beba vizuri usije ukamwaga Bure nikapata kesi kwa bi mboni " Usaina alimpa vyakula vyote akabeba Faris yeye alikuwa anatembea kama bosi " Wewe Usaina unafanya ujinga Gani ? Luckman alienda kumpokea Faris Ile mizigo " Acha tu hata sio vizito " alijibu Faris huku anatabasamu " Kwani kuna Nini akibeba hivyo vyakula na wakati na yeye ni mfanyakazi hapa " alisema Usaina" Wewe mjinga muombe msamaha " alifoka luckman " Kwanini nimuombe msamaha ? Aliuliza Usaina " Huyu ndo bosi wetu wewe pimbi " alijibu luckman kwa sauti ya chini " Heee " Usaina alishtuka sana akaanza kujichekesha ," samahani kaka bosi ...namaanisha bosi unajua kwa hivyo ulivyovaa nilihisi ni mfanyakazi mwanzake na kaka luckman"" Wala usijali ni vitu vya kawaida tu ,Haina hata haja ya kuomba samahani " alisema Faris" Asante kwa kuwa muelewa " mafundi walikusanyika na wote walipata parcel za chakula pamoja na juice ,ilibaki parcel Moja Usaina alichukua na kumpeleka Faris aliyekuwa ameshabadirisha nguo yupo kwenye gari lake " Samahani bosi nimeona wewe hukuja kujumuika na wengine chakula chako hiki hapa " Usaina alimpa Faris kile chakula " Oh asante " Faris alifunua kile chakula akaanza kula " mashallah ,chakula ni kitamu na kinanukia vizuri " Faris alikisifia chakula " Mama yangu amekuwa akifanya biashara ya mgahawa tangia sisi ni wadogo sana ni mzoefu kwenye mambo hayo na watu wengi wanakisifia chakula chake " alisema UsainaFaris hakujibu chochote aliendelea kula , Faris Huwa sio muongeaji sana na akikutana na mtu mgeni ndo Huwa anazidi kuwa mkimya " Bosi Mimi ngoja nikuache uendelee kufurahia chakula chako " Usaina aliamua kumuaga Faris Kisha akaondoka alienda kwa kaka yake luckman" Ulikuwa unaongea nae Nini naona unajichekesha tu " alisema luckman huku amemkazia jicho Usaina " Kaka si alikisifia tu chakula na Mimi nikamuelezea kwanini ni kitamu na nani anakipika basi na kwanza mtu mwenyewe kapoa kama Nini "alisema Usaina " Haya changanya miguu yako urudi nyumbani haraka sana " " Sawa naondoka " Usaina aliondoka huku kanuna , Faris aliliona lile alimsindkiza Usaina kwa macho mpaka alipopotelea Kesho yake mapema hamisi alimpitia Faris kwenye nyumba aliyofikia" Naona Leo ndo umekumbuka majukumu yako ? Aliuliza Faris " Nisamehe bro Jana nilipata homa kidogo ndomana sikutokea " alijitetea hamisi " Sawa pole" " Asanteh"" Sasa si ungepumzika tu nyumbani nitaenda Tena kusimamia ujenzi " alisema Faris " Ngoja twende wote nikakusaidie" Faris na hamisi waliongozana hadi kwenye eneo la ujenzi na kumkuta usaina " Assalam alaykum " hamisi alimsalimia Usaina " Walykum Salam , za masiku kaka mzuri "" Salama tu naona Kila siku unazidi kuwa mrembo " alisema hamisi " Toka hapa na uongo wako mwenzio nazidi kufubaa na hili jua ukijumlisha na joto la jikoni " alisema Usaina" Hahaha ,sio kweli bhana wewe mashAllah upotofauti na wasichana wengi kwanza unajisitili " " Kweli ee " Usaina aliwapa kifungua kinywa Kisha akaondoka " Ulimjulia wapi Usaina ? Faris alimuuliza hamisi " Najuana na kaka yake luckman siku nyingi sana ndomana namjua na yeye pia " alisema hamisi ..Siku zilikata hatimaye week tatu ziliisha ikabaki week Moja tu ya Faris kuwa pale... ukaribu wa Usaina na Faris uliongezeka walikuwa wanakaa na kupiga story mpaka Usaina anachelewa kurudi nyumbani.
MY MAID (MY BABY MAMA) 5

MTUNZI SMILE SHINE

Siku zilikata hatimaye week tatu ziliisha ikabaki week Moja tu ya Faris kuwa pale.. ukaribu wa Usaina na Faris uliongezeka walikuwa wanakaa na kupiga story mpaka Usaina anachelewa kurudi nyumbani" Malipo ya mama haya hapa " Faris alitoa laki tatu akampati Usaina " Asanteh kaka Faris ngoja Mimi nimuwahi mama " Usaina aliondoka Mida ya jioni Faris alikuwa anaondoka eneo la ujenzi akamuona Usaina amekaa pembezoni mwa jengo lililokuwa likijengwa analia , Faris alisimamisha gari akashuka " Usaina mbona unalia ?na kwanini upo hapa mpaka saizi ?" Aliuliza faris" Kaka faris naogopa kurudi nyumbani sijui mama atanifanya Nini Mimi " Usaina aliongea huku analia " Niambie Sasa shida Nini labda naweza kukusaidia " " Ile pesa uliyonipatia nimpeleke mama nimepolwa njiani hapo tu chini hata sio mbali "" Sasa laki tatu tu ndo ikufanye ulie namna hii panda kwenye gari Mimi nitakupa hiyo pesa " alisema Faris" Kweli kaka Faris? Aliuliza Usaina" Lakini nitakulipa Nini ? Aliuliza Tena Usaina kwa unyonge" Usijali Mimi sitaki malipo yoyote " " Asante sana kaka Faris " Faris na Usaina walienda Moja kwa Moja kwenye ATM Faris alitoa pesa kama laki tano na zote akampatia Usaina" Kaka Faris mbona naona kama ni nyingi" " Laki tatu mpelekee mama na nyingine utakula pipi " aliongea Faris kwa utani huku anatabasamu" Mimi siwezi kuzichukua hiyo nyingine bhana " Usaina alichukua laki tatu tu nyingine akaziacha kwenye gari Faris alishuka kwenye gari akamfuata walisimama kwenye kichochoro cha kuelekea nyumbani kwa kina Usaina " Chukua tafadhali sitojisikia vizuri ukiziacha kama hivi " Faris aliushika mkono wa Usaina akaziweka zile pesa kumbe wakati huo kaka yake juma alikuwa anawaona " Wewe boya kumbe ni wewe ndo unatuharibia mdogo wetu si ndio " juma alisogea pale walipokuwa wamesimama " Kaka juma sio kama unavyofikilia huyu ni bosi wa kaka luckman " " Kwahiyo kama ni bosi wa luckman ndo anaruhusiwa kukugusa sio umesahau kuwa wewe ni Binti uliyelelewa kwenye maadili mazuri ya dini" alifoka juma " Nitajielezea naomba usimfokee Usaina " alisema Faris lakini juma hakumsikiliza " Wakubwaa tokeni uko mje mshuhudie " juma aliwaita wahuni wenzie" Kumbe huyu ndo anamuwinda sista etu" alisema mmoja wa marafiki wa juma " Sasa apa kinachofuata mnakijua " juma aliwapa ishara marafiki zake walimchukua Faris kwa nguvu Hadi nyumbani kwao " Dingi Leo nimekuletea nyama mnasemaga oo Usaina asiolewe bado mdogo na Leo nimemkuta kwenye Chocho huko na hiki kibwana chake " juma alimwambia baba Yao mzee Amour" Usaina unataka kutuaibisha " alifoka Mzee Amour" Hapana baba sio kweli kaka Faris alikuwa anisindikiza tu nyumbani" " Hakuna cha kujitetea hapa mashahidi si hao wapo unataka kubisha nini" alisema juma" Mume wangu namjua Binti yetu vizuri hawezi kufanya ujinga hata siku Moja" bi mboni alimtetea Usaina "Juma kamuite shekhe shabani haraka sana mwambie kuna ndoa huku ya kufungisha msisahau na ubani " alisema Mzee Amour" Mzee samahani sana unawezaje kumuozesha Binti yako kwa namna hii hata hunijui Niko vipi na kingine siwezi kumuoa tayari nina mke na ninampenda sana mke wangu " alisema Faris" Mimi nilijua unao wake wanne kumbe mmoja utaongeza na huyu awe wa pili " alisema Mzee AmourFaris alichoka ,alimuangalia Usaina aliyekuwa analia baada ya kama dakika Tano alifika shekhe shabani na ndoa ilifungwa na baada ya ndoa Faris aliondoka na Usaina Hadi kwenye nyumba aliyofikia " Baba haukufanya sawa kabisa yule ni bosi wangu na ni rafiki wa hamisi na hizi siku tulizokuwa pamoja hawezi kuwa na tabia za namna hiyo " alisema luckman" Mwambie baba yako maana yeye anamsikiliza sana juma na wakati anamjua vizuri juma mambo yake " alilalamika bi mboni " Wote nataka mnyamaze kwanza ndoa imeshapita na kijana amelipa mahali keshi niacheni nipumzike sitaki kelele " Mzee Amour aliingia chumbani akafunga mlango " Sijui Usaina wangu atakuwa bado analia " alisema bi mboni kwa huzuni " Usijali mama hata hivyo Faris ni kijana mzuri hivyo Sina wasiwasi sana ndo Imeshatokea tutafanyaje " luckman alimbembeleza mama yake Kwa upande wa Faris na Usaina Kila mmoja alikuwa amekaa kochi lake na Kila mmoja alionekana kuwa na mawazo sana " Usaina nenda kapumzike tutaongea vizuri kesho " Faris alisimama akaingia chumbani kwake , Usaina aliingia chumbani cha pili yake Simu ya Faris ilianza kuita na mpigaji alikuwa ni hamisi " Hallo " "Vipi kaka upo sawa nimesikia kilichotokea "" Naanzaje kuwa sawa hamisi ,unajua kabisa namchukulia Usaina kama mdogo wangu na isitoshe naanzaje kumwambia salha eti nimeoa kwa kulazimisha atanielewa kweli " " Fanya hivi usimwambie kwanza mpaka utakaporudi nyumbani " " Na kuhusu Usaina itakuwaje yani nashindwa kuelewa kabisa nahisi kuchanganyikiwa "" Ongea na Usaina umsikie atakavyosema " " Sawa nitafanya hivyo" Kesho yake asubuhi Faris aliamka akamkuta Usaina anaswali alimuangalia Kisha akatoka na kuelekea msikitini aliporudi nyumbani alirudi kulala mida ya saa tatu alitoka chumbani akamkuta Usaina amekaa sebleni na nyumba ilikuwa safi na kifungua kinywa pia kilikuwa mezani " Assalam alaykum" Faris alimsalimia Usaina " Walykum Salam " kaka Faris kifungua kinywa kipo tayari " " Asanteh " Faris alikaa kwenye kiti na kuanza kula baada ya kifungua kinywa Faris alimuita Usaina Ili waongee "Usaina unajua hukustahili kupitia haya yote " alisema Faris " Kaka Faris najua unachotaka kusema nimekubali najua unampenda sana mke wako na Mimi siwezi kuingilia upendo wenu , ulisema umebaki na week Moja tu ya kuwa hapa unaonaje ukaniacha hapa nitakaa kwenye hii nyumba kwa muda, mwezi unatosha baada ya hapo unaweza kutuma talaka " aliongea Usaina huku anatabasamu lakini macho yake yalilegwalegwa na machozi " Usaina unajua kama talaka haitolewi kizembe namna hiyo " " Najua lakini hatuna jinsi , usiwe na wasiwasi nitajua Mimi jinsi ya kumalizana na familia yangu "" Sawa kama ndo umeamua hivyo , Mimi natoka kidogo nitarudi muda si mrefu nikuletee zawadi gani ? Aliuliza Faris " Hamna haja ya kuniletea zawadi kaka Faris ukirudi tu wewe ukiwa ni mzima Mimi kwangu ni zawadi tosha " Usaina ailingea kwa kuchangamka " Nitakuletea zawadi yoyote sawa ee " Faris aliondoka na kumuacha Usaina nyumbani


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote