Masha na Dick ni wapenzi walikuwa wanapenda na sana na kusaidiana kwa kila jambo, kwakuwa Masha alikuwa anatoka kwenye familia inayojiweza kidogo aliweza kumaliza shida ndogo ndogo za Dick. Dick anaahidi kumuowa endapo mambo yake yatakuwa sawa.
Dick anafanikiwa kupata kazi nje ya mji wanaoishi kabla hajaondoka aliniahidi Masha mambo mengi ikiwemo kufunga ndoa baada ya miaka miwili, lakini mambo yalibadilika baada ya Dick kukata mawasiliano.
baada ya kufiwa na baba maisha yanabadilika Masha anaamua kwenda kuishi kwa rafiki yake . Huko Masha anapata rafiki wanajeshi ana sana , siku moja Masha anaenda kumtembelea Glory anakutana na picha ya Dick na Glory anamtambulisha kuwa ni mchumba wake na yupo Marekani kwa wakati huo.
Masha anaumia na kutaka kupambanua penzi lake aliamini Dick yupo na Glory kwaajili ya manufaa yake sababu glory anatoka kwenye familia yenye pesa.
GLORY anaamua kumpa kazi kwenye kampuni wanayomiliki na Dick.
Dick anarudi na kukutana na Masha anashitushwa na uwepo wa Masha na kuanza kumfanyia visa na kejer ili aondoke kwenye maisha yao kwakuwa Masha hakuwa na kitu aliamua kuvumilia kila kitu.
Kwa bahati Masha akiwa kazini kwao anakutana na na kijana handsome, tajiri anayemiliki makampuni makubwa .
Amir anatokea kumpenda sana mpaka Masha akajiona alikuwa mjinga kumfanya mwanaume ambae hakumthamini wala kumuonyesha mapenzi kama anayomuonyesha Amir.
Dick alivyoona Masha yupo kwenye huba zito anaanza kuwa na wivu na kutaka kurudiana naye huku akisema yupo kwa glory kwa sababu na sio sababu ya pesa. Je hiyo sababu ni ipi?
Dick atafanikiwa kurubuni Masha ili warudishe? Na vipi kuhusu handsome boy Amir kijana mwenye wivu alipenda kupitiliza atakubali kumpoteza Masha?
MY EX , MY BOSS π
(ALINIACHA SASA ANANIONEA WIVU) 1
MTUNZ SMILE SHINE
Anaitwa Masha binti aliyehitimu chuo kikuu cha biashara lakini hakubahatika kupata kazi mapema ,pia ni binti ambae anatoka kwenye familia inayojiweza kidogo hivyo hakukosa vihela vidogo vidogo kwaajili ya mambo yake kama mtoto wa kike.
Katika familia yake walizaliwa wawili yeye na mdogo wake wa kiume aitwae Munir, wazazi wao walikuwa wakiwapenda na kuwajali sana kifupi familia yao ilikuwa yenye furaha.
Masha tangia alipokuwa chuo alikuwa kwenye mahusiano na kijana mmoja anayefahamika kwa jina la SADICK (Dick). Dick na Masha walikuwa wakipenda na sana na walikuwa wakisaidiana kwenye shida na raha.walipanga mambo mengi sana ya maisha yao ya mbele na hatima ya upendo wao ilikuwa ni kufunga ndoa na kuishi kama mume na mke.
Kuna wakati Masha alifanya matukio magumu kwaajili ya kumsaidia Dick.
Kuna kipindi Dick alipata matatizo kwenye familia yake wakachukua mkopo na huo mkopo Dick ndio alitakiwa kulipa , ilipofika muda wa kurejesha bado alikuwa ana hali ngumu ikabidi Masha atie marejesho ya mwanzo.
" Masha mpenzi wangu najua nakuuliza sana naomba unisamehe kwa hilo.
" Usiseme hivyo matatizo ni yetu sote.
" Ni kweli lakini siwezi kumuachia hili deni natakiwa kutafuta kazi lakini kaishia kwenye kazi za kusaidia fundi nalipwa elfu kumi na hiyo hela yote inaishia kwenye kula tu.
Masha alisikitika na hakuwa na uwezo wa kumsaidia zaidi .
" Nitahangaika kujitafutia kazi angalau yenye malipo mazuri kidogo.
Dick alimuangalia kisha akatoa tabasamu lenye kukata tamaa.
" Wewe mwenyewe huna ajira alafu unanifikiria mimi?
" Ukipata wewe ndio nimepata mimi.
Walikubaliana hivyo na Masha
alianza kumtafutia kazi sehemu . Alifika kwenye ofisi moja akakutana na boss ambae walikuwa wanafahamiana
" Masha kwahiyo umeamua kumtafutia mwanaume wako kazi?
" Ndio john naomba unisaidie.
Yule boss alimuangalia alafu akasema
" Sawa nitakusaidia lakini siku hizi mambo ni kusaidiana Masha .
" Unataka pesa kiasi gani?
" Unafikiri nitakuwa na shida na pesa?
" Kumbe unataka nini?
" Nahitaji penzi lako.
Masha alishituka hakutegemea kama John angetaka rushwa ya ngono.
" John unanichukuliaje?
" Kawaida tu. Kama huwezi basi kazi hakuna.
Masha alijifukitia sana pia akafikiria maisha ya Dick mwisho wa yote aliamua kukubali.
" Sawa nitafanya.
" Safi kesho saa mbili usiku tukutane peace hotel.
Masha aliitikia kwa kichwa kisha akaondoka.
Kesho yake jioni Masha alienda peace hotel akakutana na John wakamalizana na Dick alipata kazi kwenye kampuni ya john.
Dick alifurahi sana na kumshukuru sana mpenzi wake kwa kunipambania lakini Masha hakuwa na amani nafsi yake ilimsuta hakuwa na amani hata kidogo alitamani kumueleza ukweli Dick.
Dick alifanya kazi kwa muda wa miezi sita lakini manyanyaso kwa boss yalizidi na yote john alikuwa akimtaka Masha.
" Hivi una nini wewe ikiwa hata hii kazi alikutafuzia mwanamke wako , unajua ni kiasi gani alikupambania? Alitoa mwili wake kwangu namaanisha nililala nae.
Dick alikunja uso wake huku akiwa kakunja ngumi.
" Unataka kupigana na mimi?
" Usinione nimenyakaza ukaona siwezi kufanya chochote....
" Fanya unachotaka kufanya.
Dick aliona itakuwa kesi na kumsumbua aliamua kuacha kazi na kuondoka.
Dick hakutaka kumwambia chochote Masha japokuwa lilikuwa kinamuumiza sana moyo wake.
Siku moja Dick alimpigia simu Masha akamuomba waonane.
Masha akijiandaa haraka huku akiwa na shauku ya kutaka kujua mpenzi wake kamuitia nini.
Basi aliondoka na kwenda kukutana na. Masha alipomuona mpenzi wake alimkumbatia kwa bashasha na mabusu ya kutosha lakini Dick alikuwa mtu ambaye hana furaha.
" Mpenzi mbona upo hivyo unatatizo gani?
Dick alitulia akaangalia chini. Masha alishika kidevu cha Dick kwa upole kisha Dick akanyanyuka macho kumuangalia.
" Tafadhali baby niambie umepatwa na nini? Ukiwa kwenye hali hiyo ujue unanipa wasiwasi sana .
" Mpenzi nipo kwenye wakati mgumu sana nahitaji misaada wako.
" Niambie baby unataka nini? Masha aliuliza kwa shauku kwani alitaka kujua haraka kinachomsibu mpenzi wake.
Bado sadiki alionekana kusita.
" Kwani unanificha nini Sadick au unataka kuniambia hunitaki tena? Alisema Masha huku machozi yakilenga machoni kwake.
" Hapana baby siwezi kukuacha kwani wewe ni sehemu ya maisha yangu lakini mambo yanaweza kwenda tofauti na tulivyokuwa tumepanga.
" Sitaweza kufunga ndoa mwaka huu kama tulivyokuwa tumepanga.
Masha alishituka.
" Kwanini? Kwanini uhairishe?
" Nimepata kazi nje na hapa natakiwa kuondoka .
" Dick unataka kuniacha mwenyewe hapa?
" Unakwenda lakini nakuahidi nitakayorudi nitakuwa mpenzi .
Masha alishindwa kuongea na wote walikuwa na huzuni sana .
" Nilijua utaumia hivi , hata mimi naumia sana kwenda mbali na wewe lakini sina la kufanya natakiwa nikafanye kazi kwasababu ya maisha yetu , nitaishije na wewe ikiwa sitakuwa na pesa za kukutunza?
" Unauhakika utarudi kwasababu yangu sadick.
" Ndio mpenzi nakuahidi kurudi kwaajili yako mpenzi.
Dick alijaribu kujieleza mpaka Masha akamuelewa tatizo lingine Dick alikuwa hana pesa ya kutosha kwaajili ya safari yake ilimbidi amuombe Masha akuongezee kiasi cha pesa.
Masha alikubali
" Usijali mpenzi kwaajili ya maisha yetu nikakupatia hizo pesa.
Masha alirudi nyumbani kwao jioni alikaa na baba yake.
" Baba inakuwaje kuhusu ile pesa ya mtaji niliyokuomba?
" Ooooh unajua nina mambo mengi nilikuwa nimeshasahau, hivi ulisema unahitaji kiasi gani kwaajili ya hiyo biashara yako?
" Sio pesa nyingi sana baba unaweza ukanipitia milioni tano za kuanzia.
" Ni biashara gani ya milioni 5?
" Nataka kuagiza nguo kutoka china na hii ni mwanzo tu kama mambo yanaenda vizuri utaniongezea baba yangu.
" Sawa . Baba Masha alikubali akasaini check, alisaini check ya milioni 5 kisha akampatia .
" Asante baba. Alishukuru kwa furaha
Kesho yake mapema alienda bank kutoa pesa kisha akaenda nyumbani kwa kina sadick na kumpatia million tatu.
" Baby mbona pesa nyingi sana? Sadick alishangaa ni kwamba hakutegemea kama angependa pesa nyingi kiasi kile.
" Hizi pesa hazina thamani kama ulivyo wewe, alafu wewe ni mume wangu mtarajiwa hivyo sina shaka .
Sadick akimkumbatia na kumshukuru sana.
Baada ya siku chache sadick alijiandaa na safari na Masha ndie alimsindikiza kupanda ndege , waliachana huku kila mmoja machozi yakimtoka na kupeana ahadi kedekede.
" Usijali mpenzi nitatimiza ahadi nilizokuahidi na pesa uliyonipa nitatumia vizuri pia nitazilipa zaidi ya hizi uliyonipa.
" Sawa mpenzi nenda , nenda kawajibike na usisahau kuwa nipo huku kwaajili yako.
" Sawa mpenzi naomba ujitumze
Ukifika muda wa safari Sadick alienda kupanda ndege huku bado Masha akiwa kasimama sehemu anaangalia mpaka alipoona ndege ipo angani akaondoka akarudi nyumbani kwao akiwa na huzuni alihisi kupungukiwa .
Siku zilienda wakawa wanawasiliana vizuri na kupeana matumaini mengi sana.
Siku hazigandi hatimae mwaka mmoja ulipita huku Masha akiwa na biashara zake ndogo ndogo kwani haikufaa tena kukaa nyumbani wakati wazazi wanajua walitoa pesa za mtaji. Japokuwa hakufungua biashara alivyodhamiria lakini haikuwa mbaya kazi yake ya mgahawa ilimlipa kwa kiasi fulani huku akiwa na matumaini mwaka ujao mpenzi wake anarudi waje kufunga ndoa.
Siku zilienda mawasiliano kati ya Masha na Dick yalianza kupungua kutokana na ubize wa Masha kumuuguza baba yake ambae alikuwa akipambana maisha yake baada ya ugonjwa wake wa kansa kufikia hatua ya mwisho kabisa.
Masha na mdogo wake hawakuwa wanajua kama baba yao ni mgonjwa kwa kipindi kirefu kidogo wazazi wao walijaribu kuwaficha.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa mgonjwa mpaka ukapelekwa kufariki.
Msiba ulikuwa pigo kubwa kwa Masha kwasababu yeye ndio alikuwa mtoto kipenzi sana kwa baba yake kama vile watu wasemavyo kuwa mtoto wa kike miwa baba.
Ndugu walikaa kikao na kutaka Masha aondoke pale nyumbani .
" Masha unatakiwa kwenda kwa ndugu yako Tula . Ilikuwa ni kauli ya baba yake mdogo ambae ndio baba mzazi wa huyo Tula.
" Lakini siwezi kwenda mbali na hapa ....
" Masha mwanangu mazingira ya hapa ndani bado yatazidi kujutia unyonge bora uende ukae na ndugu yako maana huko yuko anaishi mwenyewe.
Masha hakuwa na jinsi alikubali kwenda kuishi na Tula .
Baada ya siku hiyo kupita Masha aliondoka na Tula kwenda kuanza maisha mapya
MY EX , MY BOSS π
(ALINIACHA SASA ANANIONEA WIVU)2
MTUNZI SMILE SHINE
Tula alifanya kila njia ili Masha asahau msiba wa baba yake alikuwa akitoka na kwenda kuonana na marafiki zake na kufurahia pamoja , marafiki wa Tula walimzoea Masha na kumfanya kama rafiki.
Glory alikuwa akivutiwa sana na Masha kutokana na uchangamfu wake pia alikuwa muelewa sana wa mambo .
Siku moja glory alimuomba Masha atembelee nyumbani kwake na Masha hakuwa na hayana alifurahia huo mualiko , basi kesho yake Masha akijiandaa akacheka kua usafiri na kufika nyumbani kwa glory kwa kufuata maelekezo.
Hatimae Masha alifika na kupokelewa kwa furaha sana na glory.
" Waoooo karibu sana kipenzi.
" Asante my dear nimeiaribia.
Waliingia ndani huku wakiwa wameshikana mikono.
" Glory hivi hapa unaishi na wazazi?
" Hapana hapa ni kwangu, naishi na mpenzi wangu lakini kwasasa hayupo hivyo nipo pekee yangu.
" Hongera .
" Asante.
Walifika ndani glory akamkaribisha kwenye kochi .
" Haya sasa niambie unataka kupooza koo kwa kinywaji gani?
"Mmm itakuwa poa kama nikipata juice baridiiiiii.
" Sawa nakuja sasa hivi .
Glory alienda jikoni akamuacha Masha pale sebleni.
Masha alitangaza macho kuangalia vitu vilivyopo pale sebleni. Ilikuwa seble iliyopangwa na kuoendeza ilimvitia sana Masha mpaka akasimama kwenda kuangalia mapambo alipofika kabatini alishituka baada ya kuona picha moja ya mwanaume ambae alihisi kumfahamu. Alipomuangalia kwa karibu alihisi mapigo yake ya moyo yanaenda mbio.
" Siamini macho yangu . Masha alinyanyua ile picha na kuiangalia vizuri .
Mara glory alirudi akiwa na trei ya juice akaenda kuiweka mezani kisha akaenda kusimama pembeni . Masha alishituka akageuka kumuangalia, Glory aliachia tabasamu huku akichukua ile picha kutoka kwa Masha.
" Ni mpenzi wangu. Alisema Glory huku akiifuta.
" Hu.... huyu ndio mpenzi wako? Aliuliza Masha huku akiwa na kigugumizi.
" Ndio huyu ndio shemeji yako anaitwa Sadick.
Masha aliposikia jina la Sadick moyo ulipasuka .
" Ni muda sasa yupo mbali nami ila siku sio nyingi atarudi.
" Yuko wapi?
" Alienda Marekani miaka miwili iliyopita .
Kwa maelezo ya glory ilijitosheleza kuamini kuwa huyo mwanaume anaeongelewa ni Sadick mwanaume aliyempenda kwa dhati ya moyo wake
" Masha alijikaza na kutoa tabasamu la uongo lakini moyoni alikuwa ameumia sana maumivu aliyoyahusi ni mithili ya mshale iliochoka moyoni kwake.
Glory alirudisha ile picha sehemu ilipokuwa .
" Hongera sana umekua kuchagua.
" Hahahaha asante sana kipenzi, unajua huyu mwanaume ni kila kitu kwangu.
" Inaonekana unampenda sana.
" Kifupi tunapendana mno.
Wakirudi kukaa glory akamkabidhi grass ya juice wakawa wanakunywa huku Glory akipiga story za hapa na pale lakini maongezi yake yalikuwa hayakai wala hakujielewa anaongea nini akili yake ilikuwa imeshavurugika.
" Glory nimefurahi kufahamu unapoishi ila sina muda zaidi wa kuwepo hapa....
" Usiniambie unataka kuondoka mapema yote hii wakati tulipanga tutashinda wote.
" Acha niende Tula kanitumia msg kuna mtu natakiwa kwenda kuonana nae si unajua nahangaikia kazi.
" Sawa , kwani umepata sehemu ?
" Bado nahangaika.
" Kama itashindikana naweza kukupa nafasi kwenye kampuni ya mpenzi wangu.
" Sawa acha nikaonana na huyu mtu kwanza kama itashindikana nitakuja tuongee vizuri.
" Sawa.
Masha alitoka huku glory akimsindikiza mpaka nje . Usafiri ulifika wakaagana Masha akapanda kwenye bajaji akarudi nyumbani kwa Tula.
Ndio kwanza alimkuta Tula anatoka kazini kwake. Masha alienda kujitupa kwenye kochi huku akiwa katiba uso wake kwa viganja vyake vya mikono.
" Wewe una tatizo gani,? Aliuliza Tula
" Tula roho yangu inauma kama kidonda sijui kwanini aliamua kunitendea hivi kwani nilimkosea nini, mbona nilimpa kila kitu alichotaka, nilimpa upendo wangu wote..... Aliongea Masha akiwa analia. Tula alinyanyuka alipokuwa amekaa na kwenda kukaa karibu na Masha.
" Unaongea kuhusu nini?
" Dick, Tula kumbe ukimnya wa Dick alikuwa amepata mwanamke mwingine
" Amekutafuta atakwambia kuwa ana mwanamke mwingine?
" Hapana sijaambiwa na mtu bali nimeshuhudia kwa macho yangu. Hivi unajua mwanaume wa glory ndio Dick wangu?
Tula alishituka
" Unasemaje? Huyu Dick mwanaume wa Glory ndio alikuwa mwanaume wako wewe?
" Ndio.
Tula alikuja kichwa huku akishusha pumzi ndefu.
"Umemwambia Glory kuwa Dick ni mwanaume wako?
" Hapana hajui chochote.
" Afadhali haujanwambia maana ungeweza kusababisha mzozo mkubwa sana kati yako na yeye glory maana huwa hataki kusikia chochote kuhusu Dick yupo radhi kugombana kwaajili ya kunipambania penzi lake.
" Kwahiyo unataka kusema kuwa mimi ndio sina uchungu na Dick? Kumbuka nimetoka mbali sana na mpenzi wangu na nina amini kuwa Dick bado ananipenda sana .
" Lakini ana mwanamke mwingine tena mwenye kila kitu na glory na familia yake ndio wamempa maisha huyo Dick mpaka kufikia hatua ya kumiliki kampuni.
" Umeona sasa kumbe Dick wangu yupo kwao kwasababu ya pesa tu na sio mapenzi ila kwangu Dick alikuwa kwaajili ya mapenzi na nasema nitafanya juu chini Dick arudi kwangu.
"Unataka kufanya nini Masha?
" Nitafanya jambo la ajabu wala sitatumia nguvu nitatumia akili kubaini kipi kitakuwa na nguvu kati ya mapenzi ya kweli au pesa.
MY EX,MY BOSS π 3
( ALIMUACHA SASA ANANIONEA WIVU)
MTUNZI SMILE SHINE
Masha aliongea huku akiwa anamaanisha anachosema .
" Masha unajua nimetoka mbali na GLORY chonde chonde usije ukanigombanisha na udugu wangu.
" Hili swala halikuhusi Tula niachie mwenyewe. Kwanza ungejaribu kufikiria hili swala kama ungekufika wewe ungejisikiaje?
" Najua inaumiza lakini......
" Basi kama unajua inaumiza usiongeze neno acha nisubiri hiyo siku ya kurudi huyo Sadick.
Alimaliza kuongea akanyanyuka na kwenda chumbani.
Licha ya kuumizwa na swala la Dick kuwa na glory lakini Masha alijaribu sana kuficha hisia zake ndio kwanza alikuwa karibu sana na Glory mara kwa mara alienda nyumbani kwa Glory na kuna wakati alilala hukohuko.
" Glory si unajua ndugu yako sina maisha na kila ninapoona kazi mambo yanakuwa magumu sijui unanisaidiaje kuhusu kunichimeka pale kazini kwa mume wako.
" Kuhusu hilo hakuna shida kabisa na kila siku nimekuwa nikikuomba kuhusu kufanya kazi kwenye ofisi yetu umekuwa mtu wa kukwepa ndio maana na mimi nilikuwa nimetumia.
" Basi yamenifika shingoni nahitaji kazi haraka ili na mimi nianze maisha yangu nimechoka kuzunguka mara leo kwa Tula kesho kwako nataka kutulia kwenye Kiwira changu.
" Hilo limeisha kipenzi.
Tuombe Mungu kukuche salama kesho tutaenda ofisini.
" Asante sana kipenzi.
" Usijali wewe ni ndugu yangu lazima nifanikishe kile ambacho naweza kufanya kwako.
Waliendelea na maongezi baada ya muda kusogea kila mmoja alienda chumbani kwake kupumzika .
Kesho yake mapema waliamka wakiandaa na kwenda kwenye kampuni ya S&G Company.
" Kipenzi hii ndio kampuni yangu na Sadick.
Masha aliachia tabasamu na kumpongeza.
" Hongera sana kipenzi , umejitahidi sana .
" Asante. Msimamo uwepo wako hapa utaongeza kitu kwenye kampuni yetu.
" Bila shaka kipenzi.
Glory alinizungusha kila sehemu na kumtambulisha kwa wafanyakazi wengine kuanzia siku hiyo Masha alitambulika rasmi kama mfanyakazi wa kampuni ya S&G Company kama meneja masoko.
Masha alijitahidi sana kufanya kazi kwa bidii na kwa muda mchache mafanikio yalianza kuonekana kwenye kampuni.
Glory alimjulisha Sadick maendeleo ya kampuni , sadick alifurahi na kumsifia mpenzi wake.
"Sijui nikushukuru vipi mpenzi wangu ila acha niseme asante Mungu kwa kunipatia mke muelewa na mwenye akili kama wewe.
" Asante mpenzi lakini haya yote ni kwaajili ya rafiki yangu ni mchapakazi mno.
" Bado shukurani zote nitatoa kwako sababu bila wewe kumpatia kazi huyo rafiki yako mambo yasingekuwa hivi. Natamani kumuona huyo rafiki yako mwenye akili nyingi.
" Kikubwa ni kumuomba Mungu atupe uzima utakuta na tutaendelea na kazi pamoja ni uhakika tutafika mbali.
" Sawa mpenzi
Baada ya Glory kukata simu alimwambia Masha.
" Shemeji yako anakusalimia sana pia anatamani sana kukuona.
Masha alitabasamu alafu akasema
" Nimezipokea salamu , hata mimi nina shauku kubwa ya kukutana nae na tufanye kazi pamoja.
" Hata nae hiyo ndio shauku yake kubwa.
Kesho yake Masha alipotoka kazini alienda nyumbani kwa Tula.
" Sikutegemea kama ingekuja leo.
" Sina sehemu maalumu ila sio sio nyingi nitakuwa na kwangu.
" Lakini sijasema kwa ubaya.
" Najua hujasema kwa ubaya , nasikia wiki ijayo sadick anarudi.
" Kwahiyo inakuwaje, si urudi nyumbani sasa.
" Hapana nimekuja hapa kuchukua nguo ngamia kabisa nyumbani kwa Glory.
Tula alishituka akajikuta kasimama bila kutegemea
" Unataka kufanya nini Masha?
" Hakuna kibaya dada kuna jambo langu nataka kuliweka sawa baada ya wiki mbili nitaondoka na kwenda kuanza maisha yangu mapya.
" Acha kuleta ujinga kwenye haya maisha , umepata kazi nzuri yenye mshahara mnono bado unataka kuichezea? Achana na mapenzi mbona wanaume na handsome wapo wengi tafuta wa kuendana nae achana kabisa na Dick.
Masha alishusha pumzi alafu akasimama wakawa wanaangaliana .
" Tula sina nia ya kuharibu uhusiano wa glory na Dick ila nataka Dick alipie kwa alichokifanya.
" Itasaidia nini sasa?
" Kwa mtazamo wa watu wengine haitasaidia lakini kwa upande wangu kuna kitu nitapunguza .
Masha aliingia chumbani akachukua baadhi ya nguo zake .
" Masha unajua moyo wangu hauna amani kabisa naomba usiende.
"Tula naomba uniamini hakuna baya kitatokea.
Tula alimruhusu Masha aondoke lakini hakuridhishwa na uondoaji wake.
Siku moja majira ya usiku wakiwa wamekaa nje wanaounga upepo huku wakisindikizwa na vinywaji.
" Unajua kesho shemeji vyako anakuja.
Alisema Glory na kumfanya Masha akae vizuri.
" Wewe unamaana kesho mzee ndani ya nyumba.
" Ndio, yani hapa natamani kesho ifike mapema nimemiss sana mwanaume wangu.
Glory alivyosema hivyo Masha alijihisi wivu ila ndio mali ya watu ilibidi ajikaze tu.
" Sijui niandae nini kwaajili ya mume wangu.
" Usijali kuhusu kupika najua wewe sio mtaalamu wa kupika hiyo nafasi niachie mimi.
" Hapo ndipo ninapokupendea shoga yangu .
" Wewe niambie niandae nini mimi nitaandaa.
" Sina haja ya kusema wewe andaa chakula chochote kitamu.
" Basi hilo limeisha sema kama kuna lingine.
" Hakuna.
Kesho mapema waliamka na kufanya usafi pale ndani na kufanya nyumba ing'ae na kuvutia kwa mapambo.
Muda uliopangwa Glory alienda kumpokea Dick na Masha alikuwa jikoni akimalizia kuandaa chakula.
Alipomaliza kupika alienda kuandaa kila kitu mezani baada ya hapo alienda kuingia bafuni kuoga. Alipomaliza alivalia nguo yake nzuri na kujipamba uso wake na kufanya awe kwenye muonekano mzuri.
Glory na Dick walifika nyumbani wakati huo Masha alikuwa kasimama dirishani anawachungulia. wakaingia ndani na kupitiliza chumbani kwao, walifurahia kukutana tena kwa mara nyingine kisha wakaenda kuoga pamoja baada ya hapo walienda dinning kupata chakula .
" Baby iliniambia rafiki yako yupo hapa na mbona simuoni akija kuungana nasi hapa mezani?
"Ngoja nikamuite.
Glory alipotaka kuamka akamuona Masha anakuja alitabasamu akarudi kukaa.
" Vipi mbona umerudi kukaa?
" Anakuja.
Dick aligeuka shingo yake na kuangalia kule anakotokea Masha alijikuta anashituka na kuangusha kijiko kilichokuwa na chakula.
MY EX,MY BOSS π 3
( ALIMUACHA SASA ANANIONEA WIVU)
MTUNZI SMILE SHINE
Masha aliongea huku akiwa anamaanisha anachosema .
" Masha unajua nimetoka mbali na GLORY chonde chonde usije ukanigombanisha na udugu wangu.
" Hili swala halikuhusi Tula niachie mwenyewe. Kwanza ungejaribu kufikiria hili swala kama ungekufika wewe ungejisikiaje?
" Najua inaumiza lakini......
" Basi kama unajua inaumiza usiongeze neno acha nisubiri hiyo siku ya kurudi huyo Sadick.
Alimaliza kuongea akanyanyuka na kwenda chumbani.
Licha ya kuumizwa na swala la Dick kuwa na glory lakini Masha alijaribu sana kuficha hisia zake ndio kwanza alikuwa karibu sana na Glory mara kwa mara alienda nyumbani kwa Glory na kuna wakati alilala hukohuko.
" Glory si unajua ndugu yako sina maisha na kila ninapoona kazi mambo yanakuwa magumu sijui unanisaidiaje kuhusu kunichimeka pale kazini kwa mume wako.
" Kuhusu hilo hakuna shida kabisa na kila siku nimekuwa nikikuomba kuhusu kufanya kazi kwenye ofisi yetu umekuwa mtu wa kukwepa ndio maana na mimi nilikuwa nimetumia.
" Basi yamenifika shingoni nahitaji kazi haraka ili na mimi nianze maisha yangu nimechoka kuzunguka mara leo kwa Tula kesho kwako nataka kutulia kwenye Kiwira changu.
" Hilo limeisha kipenzi.
Tuombe Mungu kukuche salama kesho tutaenda ofisini.
" Asante sana kipenzi.
" Usijali wewe ni ndugu yangu lazima nifanikishe kile ambacho naweza kufanya kwako.
Waliendelea na maongezi baada ya muda kusogea kila mmoja alienda chumbani kwake kupumzika .
Kesho yake mapema waliamka wakiandaa na kwenda kwenye kampuni ya S&G Company.
" Kipenzi hii ndio kampuni yangu na Sadick.
Masha aliachia tabasamu na kumpongeza.
" Hongera sana kipenzi , umejitahidi sana .
" Asante. Msimamo uwepo wako hapa utaongeza kitu kwenye kampuni yetu.
" Bila shaka kipenzi.
Glory alinizungusha kila sehemu na kumtambulisha kwa wafanyakazi wengine kuanzia siku hiyo Masha alitambulika rasmi kama mfanyakazi wa kampuni ya S&G Company kama meneja masoko.
Masha alijitahidi sana kufanya kazi kwa bidii na kwa muda mchache mafanikio yalianza kuonekana kwenye kampuni.
Glory alimjulisha Sadick maendeleo ya kampuni , sadick alifurahi na kumsifia mpenzi wake.
"Sijui nikushukuru vipi mpenzi wangu ila acha niseme asante Mungu kwa kunipatia mke muelewa na mwenye akili kama wewe.
" Asante mpenzi lakini haya yote ni kwaajili ya rafiki yangu ni mchapakazi mno.
" Bado shukurani zote nitatoa kwako sababu bila wewe kumpatia kazi huyo rafiki yako mambo yasingekuwa hivi. Natamani kumuona huyo rafiki yako mwenye akili nyingi.
" Kikubwa ni kumuomba Mungu atupe uzima utakuta na tutaendelea na kazi pamoja ni uhakika tutafika mbali.
" Sawa mpenzi
Baada ya Glory kukata simu alimwambia Masha.
" Shemeji yako anakusalimia sana pia anatamani sana kukuona.
Masha alitabasamu alafu akasema
" Nimezipokea salamu , hata mimi nina shauku kubwa ya kukutana nae na tufanye kazi pamoja.
" Hata nae hiyo ndio shauku yake kubwa.
Kesho yake Masha alipotoka kazini alienda nyumbani kwa Tula.
" Sikutegemea kama ingekuja leo.
" Sina sehemu maalumu ila sio sio nyingi nitakuwa na kwangu.
" Lakini sijasema kwa ubaya.
" Najua hujasema kwa ubaya , nasikia wiki ijayo sadick anarudi.
" Kwahiyo inakuwaje, si urudi nyumbani sasa.
" Hapana nimekuja hapa kuchukua nguo ngamia kabisa nyumbani kwa Glory.
Tula alishituka akajikuta kasimama bila kutegemea
" Unataka kufanya nini Masha?
" Hakuna kibaya dada kuna jambo langu nataka kuliweka sawa baada ya wiki mbili nitaondoka na kwenda kuanza maisha yangu mapya.
" Acha kuleta ujinga kwenye haya maisha , umepata kazi nzuri yenye mshahara mnono bado unataka kuichezea? Achana na mapenzi mbona wanaume na handsome wapo wengi tafuta wa kuendana nae achana kabisa na Dick.
Masha alishusha pumzi alafu akasimama wakawa wanaangaliana .
" Tula sina nia ya kuharibu uhusiano wa glory na Dick ila nataka Dick alipie kwa alichokifanya.
" Itasaidia nini sasa?
" Kwa mtazamo wa watu wengine haitasaidia lakini kwa upande wangu kuna kitu nitapunguza .
Masha aliingia chumbani akachukua baadhi ya nguo zake .
" Masha unajua moyo wangu hauna amani kabisa naomba usiende.
"Tula naomba uniamini hakuna baya kitatokea.
Tula alimruhusu Masha aondoke lakini hakuridhishwa na uondoaji wake.
Siku moja majira ya usiku wakiwa wamekaa nje wanaounga upepo huku wakisindikizwa na vinywaji.
" Unajua kesho shemeji vyako anakuja.
Alisema Glory na kumfanya Masha akae vizuri.
" Wewe unamaana kesho mzee ndani ya nyumba.
" Ndio, yani hapa natamani kesho ifike mapema nimemiss sana mwanaume wangu.
Glory alivyosema hivyo Masha alijihisi wivu ila ndio mali ya watu ilibidi ajikaze tu.
" Sijui niandae nini kwaajili ya mume wangu.
" Usijali kuhusu kupika najua wewe sio mtaalamu wa kupika hiyo nafasi niachie mimi.
" Hapo ndipo ninapokupendea shoga yangu .
" Wewe niambie niandae nini mimi nitaandaa.
" Sina haja ya kusema wewe andaa chakula chochote kitamu.
" Basi hilo limeisha sema kama kuna lingine.
" Hakuna.
Kesho mapema waliamka na kufanya usafi pale ndani na kufanya nyumba ing'ae na kuvutia kwa mapambo.
Muda uliopangwa Glory alienda kumpokea Dick na Masha alikuwa jikoni akimalizia kuandaa chakula.
Alipomaliza kupika alienda kuandaa kila kitu mezani baada ya hapo alienda kuingia bafuni kuoga. Alipomaliza alivalia nguo yake nzuri na kujipamba uso wake na kufanya awe kwenye muonekano mzuri.
Glory na Dick walifika nyumbani wakati huo Masha alikuwa kasimama dirishani anawachungulia. wakaingia ndani na kupitiliza chumbani kwao, walifurahia kukutana tena kwa mara nyingine kisha wakaenda kuoga pamoja baada ya hapo walienda dinning kupata chakula .
" Baby iliniambia rafiki yako yupo hapa na mbona simuoni akija kuungana nasi hapa mezani?
"Ngoja nikamuite.
Glory alipotaka kuamka akamuona Masha anakuja alitabasamu akarudi kukaa.
" Vipi mbona umerudi kukaa?
" Anakuja.
Dick aligeuka shingo yake na kuangalia kule anakotokea Masha alijikuta anashituka na kuangusha kijiko kilichokuwa na chakula.
MY EX, MY BOSS π 4
( ALINIACHA SASA ANANIONEA WIVU)
MTUNZI SMILE SHINE
Kitendo cha kijiko kuanguka ilimshitua Glory
" Vipi mpenzi?
" Aaaaa.... Eee kijiko kimeniponyoka.
Masha alikuwa katika karibu akachukua kijiko kingine na kumpatia.
" Pole shemeji kijiko kingine hiki hapa.
Dick alizipokea huku akimuangalia usoni na Masha alikuwa anatabasamu. Baada ya Dick kupokea kijiko Masha alivuta kiti alafu akakaa.
" Pole kwa safari na karibu nyumbani nikimaanisha karibu nchini kwetu Tanzania.
" Asante. Alijibu Dick kwa sauti ya chini huku akiwa na hofu.
" Baby huyu nidio yule rafiki yangu niliekuwa nakwambia anaitwa....
Kabla Glory hajataka jina. Masha akamuwahi
" Naitwa Masha.
" Nimefurahi kukufahamu Masha karibu.
" Nimeshakaribia shemeji.
Waliendelea kula huku glory alisifia chakula.
" Mmmh shoga umefanya kifuru gani leo unataka watu tujing'ate.
" Kwanini kipenzi?
" Chakula kimezidi utamu mno yani ukiendelea kunipigia hivi kila siku nitabasila kwa kunenepa.
" Hahahaha shauri yako kama hautajidhibiti utakuwa kama puto kwa kunenepa alafu shemeji akatafuta vi miss huko.
" Eti baby nikinenepa utafanya hivyo?
" Mmmh hapana haiwezekani baby.
" Umeona mpenzi wangu ananipenda vyovyote nitakavyokuwa.
Waliendelea kula lakini Dick hakuwa na furaha hofu ilitawala alijua uwepo wa Masha pale ni hatari unaweza ukaharibu kila kitu.
" Hapana sitaruhusu ndoto zangu ziharibike huyu Masha hatakiwi kuwa kwenye maisha yetu lazima nimzoee hapa ndani kwa gharama yoyote ile.
Baada ya kupata chakula Dick alikuwa wakwanza kunyanyuka akaenda chumbani na baada ya muda glory alinyanyuka akamfuata. Huku nyuma Masha aliachia tabasamu na kusema
" Huu ni mwanzo tu Dick nitahakikisha na kunyima raha na unajutia kunisaliti na kunifanya mjinga pamoja na kunipotezea muda wangu.
Dick alikuwa chumbani akiwa hana raha furaha yake yote ilizimwa na Masha.
" Vipi baby mbona kama haupo sawa au haujapendeza na rafiki yangu?
" Hapana mpenzi wangu kwanini nisipendezwe na mwanamke mchapakazi sema sijisikii vizuri nahitaji kupumzika.
Ilifika usiku Dick hakutaka kwenda kupata chakula cha pamoja alimuomba Glory ampelekee chakula chumbani.
" Mpenzi naomba uniletee chakula huku.
" Jamani mpenzi imeanza lini wewe kuja chakula chumbani?
" Leo nimejisikia hivyo siku nyingine zitaungana pamoja mezani.
" Unajua siwezi kula bila wewe ikiwa upo hapa na itakuwaje kama tutamuacha Masha pekee yake mezani atahisi tunamtenga.
" Ni kwaleo tu mueleze kama ni muelewa atakuelewa.
" Sawa.
Glory walitoka chumbani akaenda sebleni akamkuta Masha ameshalala kwenye meza ya chakula anawasubiri.
" Mbona umekuja mwenyewe shem yuko wapi?
" Utamuweza shemeji yako si amekataa kuja kula huku anataka tukale chumbani.
Masha alitulia kidogo kisha akasema
" Mmmm sio vibaya itakuwa kamiss kuwa na wewe beba chakula nendeni mikale.
" Nisamehe bure rafiki yangu.
" Usijali naelewa .
" Asante kwa kutuelewa.
Glory alibeba chakula akaenda chumbani.
" Shiiit kwahiyo ananikwepa si ndio? Atakuwa anafikiria nini akiniona? Atakuwa anaumia kuniona sababu bado anaupendo na mimi au anaogopa anahisi nipo hapa kwaajili ya kumuharibia?
Baada ya siku mbili kupita majira ya asubuhi wakiwa wanahekaheka ya kujiandaa kwenda kazini . Glory alikuwa anajiandaa kwaajili ya kwenda kwenye biashara zake na Dick walikuwa kasimama mbele ya kioo cha dressing table akiweka tai yake vizuri.
" Baby inabidi mnipumzishe ofisini kwangu alafu nyie ndio muende kazini kwenu.
" Tukupotishe na nani?
" Wewe si utampa lift Masha?
" Hapana kwenye gari yangu hawezi kupanda mwanamke mwingine tofauti na wewe mke wangu.
Glory alikuwa anavaa viatu ilibidi aache kwanza na kumuangalia Dick huku akiwa anacheka.
" Unajua mume wangu unanifurahisha sasa Masha anashinda gani na unajua ni rafiki yangu ?
" Unajua mimi sana?
" Masha hana shida.
" Inawezekana asiwe na shida lakini msimamo wangu ndio huo nenda kawaambie kabisa achukue usafiri mwingine awahi kazini.
Kwakuwa glory anamjua mwanaume wake anasimamia misimamo yake hakuona haja ya kuendelea kutekeleza na maana hakuna kitakacho badilika alitoka na kwenda chumbani kwa Masha.
" Kipenzi umeshamakiza kujiandaa?
" Ndio nilikuwa nataka kutoka nikaeasubiri sebleni .
" Sasa mambo yamebadilika Dick wataelekea kazini sasa hivi hivyo inabidi uchukue usafiri mwingine.
" haina shida acha niondoke tutaonana jioni.
" Sawa uwe na kazi njema
" Nawe pia kipenzi.
Masha aliondoka huku akiwa anajua kuwa Dick anamkwepa.
Masha kiwa kazini anaendelea na kazi alikuja kuitwa na secretary.
" Dada Masha unaitwa na boss ofisini kwake.
Masha aliposikia hivyo moyo wake uliopasuka .
" Sawa naenda.
Baada ya secretary kuondoka nae alinyanyuka na kuelekea ofisini kwa boss wake.
Alibusha hodi akakaribishwa.
Aliingia na kwenda kusimama mbele ya meza na kusalimia huku akitabasamu
" Habari za asubuhi boss.
" Salama karibu ukae.
Masha alivuta kiti akakaa na kumuangalia Dick usoni.
" Habari za miaka mingi mr sadick.
" Masha nimekuita hapa kwaajili ya kuongea na wewe jambo moja na tufanye makubaliano nipo tayari kufanya kila kitu ili uwe mbali na maisha yangu. Sema unataka nikulipe kiasi gani ili ukae mbali na maisha yangu. Aliongea Dick huku akiwa kamkazoa macho bila hata kupepesa.
MY EX,MY BOSS π 5
( ALINIACHA SASA ANANIONEA WIVU)
MTUNZI SMILE SHINE
Masha alimuangalia Dick huku akiwa kakunja sura yake.
" Unasemaje Dick? Hivi unafikiri unaweza kununua kwa pesa penzi langu halinunuliki ulianza sasa acha tumalize pamoja.
" Unamaana gani kusema hivyo?
" Huna usilolijia Dick kumbuka tulipotoka, wewe ndio mwanaume ulietoa usichana wangu, nimefanya mambo mengi kwaajili yako ilifikia hatua niliona mpaka pesa nyumbani nikakupatia, nikidanganya wazazi wangu kuwa nataka kufungua biashara na pesa nikakupatia lakini bado hazikutosha ukaja kunisaliti baada ya kukupa pesa yangu kwaajili ya kuja kuanza kazi.
" Piga gharama ya pesa zako nitakupa pia ukitaka nilipie muda niliokupotezea nitalipa na ukitaka nilipie pia usichana wako nitaulipia.....
Kabla Dick hajamaliza kuongea alishitukia kibao cha nguvu kujitia shavuni kwake.
Dick alijiinamia huku akiwa kashika shavu lake lililokuwa linawaka moto kwa maumivu.
" Shetani mkubwa wewe unafikiri ukiwa na pesa unaweza kufanya chochote unachojisikia?
Dick alisimama kwa hasira huku akiwa kakunja sura yake.
" Toka ofisini kwangu.
Aliongea kwa sauti ya ukali na masha bado alikuwa kasimama
" Nasema toka ofisini kwangu haraka kabla sijafanya jambo baya kwako.
Masha alitoka ilikuepusha Shari alishindwa kabisa kuendelea na kazi alienda kuchukua vitu vyake akaondoka na kwenda kazini kwa Tula.
Tula alipomuona alishituka kwanza sio kawaida Masha kwenda ofisini kwake na tena ule ulikuwa ni muda wa kazi hata kwa Masha alafu uso wa Masha ulikuwa mwekundu kwa kulia.
" Masha umepatwa na nini ndugu yangu?
" Tula sijui ninwambiaje.... Aliongea Masha huku akikaribia kulia
" Umefukuzwa kazi?
" Bora ningefukuzwa kazi nisingekuwa na machungu kiasi hiki, hivi kweli dickz ni wakuniambia maneno mazito kiasi kile eti anataka kunilipa kwaajili ya kila kitu tulichopitia.
" Mmmmh lakini nilikwambia kaa mbali na wale watu ,achana na mambo yaliyopita angalia yanayokuja mbele yako.
" Dick anatakiwa kulipia kwa hili.
" Unataka alipie nini sasa ? Alafu kumbuka glory hana kosa lolote hapo usije ukanisababishia maumivu.
" Najua lakini bado nampenda Sadick yeye ndio mwanaume wangu wa pekee sijawahi kuwa ba mwanaume zaidi yake yeye ndio alinionyesha na kujifunza mapenzi...
" Sasa ndio kaamua kukuacha.
" Kwanini aniache na kujisahau kirahisi hivyo?
" Masha achana na maswali ya kupuuzi naomba urudi nyumbani haraka sitaki matatizo.
Ngoja nikwambie kitu kimoja ambacho hata wewe unalijua lakini inajitoa ufahamu, Dick hakipendi tena.
" Sio kweli.
" Dick angekuwa anakupenda asingekwambia hayo maneno hata kama kakosea angeongea na wewe kistaarabu.
Masha alifikiria akaona maneno ya Tula yana ukweli ndani yake.
" Sawa. Alijibu Masha kisha akawa anaondoka
" Unaenda wapi sasa?
" Nyumbani.
Dick aliporudi nyumbani alimkuta glory anesharudi yupo jikoni anapika. Alimfuata wakasalimiana.
" Vipi baby umeshindaje?
" Nimeshinda salama kabisa hofu yangu ni kwako.
" Mimi ni mzima kama unavyoniona.
" Masha yuko wapi?
" Aaah sijamuona
" Nilijua mtarudi pamoja.
" Nilikwambia siwezi kubeba mwanamke tofauti na wewe kwenye gari yangu.
Masha alirudi usiku aliowakuta Glory akiwa Kampala Dick mapajani akiwaangalia akamsalimia
" Hallow, habari. Alijitahidi kuchangamka lakini moyoni alikuwa na maumivu hasa alipowaona amekaa kimahaba.
" Salama mamy pole na kazi .
" Asante. Nipo ndani .
Masha alipenda ndani Dick alimwambia Glory.
" Hebu nyanyuka mara moja tuongee jambo.
Glory alinyanyuka akakaa.
" Naomba uniambie rafiki yako aondoke hapa ndani sina uhuru wa kuwa na wewe na unajua sijazowea kujibana bana.
" Mpenzi....
" Unataka kunipiga?
" Hapana lakini nitaanza wapi?
" Subiri nakuja.
Dick alinyanyuka akaenda ndani baada ya dakika kadhaa alirudi.
Kampatie hii funguo nimeshamtafutia nyumba ya kuishi.
" Mbona haujanishilikisha?
" Mimi ni mwanaume nimeshafanya maamuzi na kama huwezi kuongea nae nitaongea nae mwenyewe.
Alisema Dick huku akielekea chumbani kwa Masha.
" Dick jamani hebu njoo kwanza tuongee .
Dick hakusikilizwa alifika mbele ya mlango wa chumba cha Masha akagonga.
Baada ya muda mlango ulifunguliwa Masha alipomuona Dick alikunja sura yake.
" Sikiliza unatakiwa kuhama hapa ndani nimeshakutafutia nyumba na funguo hii hapa.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote