ILA MIMBA JAMANI
Yaan Kuna muda ukimuona mjamzito na vituko vyake unaweza Dhani labda anaigiza,kumbe ni kweli mimba inamtuma tofauti...
Kim CEO kwenye kampun kubwa ya mazao nchin ambae alilelewa na bibi yake baada ya wazaz wake kufariki, Kim hakuwa tayari kuwa na mahusiano Wala mtoto na bibi yake mara kadhaa alikuwa akimtafutia WAnawake ili angalau awe na familia ila hakuwa tayari, mpaka alipopewa shart la kuwa kama anataka kuwa mrithi na msimamizi wa mali lazima awe na mtoto, na bibi yake aliamin akimshinikiza awe na mtoto n lazima atakuwa na mwanamke, na badala yake Kim anatafuta mwanamke wa kumzalia ambae anamlipa, na mwanamke huyo anaitwa Farida, Farida atapandikizwa mbegu za Kim na kubeba ujauzito wa kim, na Kim anakuwa Hana muda nae, ila zile tabia za mimba ya farida zinakuwa kero kwa Kim, maana mimba ilikuwa inamtuma Farida kuwa karibu na Kim kitu ambacho Kim mwanzo hakuwa anakifurahia ila miwsho anajikuta anazoea usumbufu wa Farida na usumbufu ule unageuka upendo...
Usikose mkasa huu wa kusisimua wa Mr CEO na mimba yangu
MR CEO NA MIMBA YANGU 1
(he only need a child )
HUSQER BALTAZAR
Alikuwa anaonekana kijana mmoja akiwa anaingia kwenye kampuni moja kubwa ya mazao, ambayo inahusika na kuuza mazao kwa serikali, kampuni hii ilikuwa inaenda kununua mazao kwa wakulima kote nchi na kuiuzia serikali, ni kampuni kubwa sana, katika kam[puni hio kulikuwa na kijana mmoja ambae alitambulika kwa jina la Kim, kim ni mtoto wa pekee kwenye familia ambayo baba na mama yake walikufa kwenye ajali, na kupelekea kubaki na bibi yake, ambae ndio alikuwa anamlea kwa kipindi chote hicho, na kuanzia anakuwa, alifundishwa namna ya kuiendesha kampuni, kwa maana alikuwa ndio mrithi pekee wa kusimamia mali za kampuni yao….
Kim alikuwa kijana mtanashati, ambae muonekano wake ulikuwa ni nd oto za wanawake wote , kwa maana alikuwa mrefu, amejazia flani hivi, na alikuwa na pesa, yaan ukimuangalia tu unaweza ukajikuta umeshiba bila kutaka….
Kim alikuwa na sifa nyingi sana kutokana na utendaji kazi wake, na kila mtu alikuwa akimuongelea kwa mazuri tu, ila alikuwa na kasoro moja tu, ambayo ni kuwa hakuwah kuonekana na mwanamke kuanzia anakuwa mpaka anafikia umri wa miaka 27…..
Kuna baadhi ya watu walikuwa wanahisi labda ni shoga, wengine wakawa wanamzulia kuwa ananyanyasa sana wanawake ndio maana wanawake wanamkimbia, ila hakuna ambae alikuwa na uhakika ni kwanini kim hajihusishi na mahusiano kabisa kwenye maisha yake…
Ule uvumi ulikuwa unamuogopesha sana bibi yake, na kuhisi huenda jina la kampuni yake linaweza kuharibika, hivyo akawa anataman sana kumuona mjukuu wake anaoa, au hata anamtoto, ili nkuwaaminisha watu, kuwa yeye ni mwanaume kamili, ambae anayajua majukum yake, ila alishawah kuongea na kim mara kadhaa, ambapo alikuwa anataman sana kumuona kim na mwanamke ila kim hakuwa na jibu na wala hakuwah kuonesha ushirikiano kwa bibi yake kabisa kuhusu kutafuta mahusiano…………..
Mwisho bibi yake akaja na shauri kuwa, kama anataman kuwa mrithi wa kampuni ni lazima awe na mtoto, na akalipeleka hilo kwa mwanasheria mkuu wa familia, na akawa anatakiwa kwenda kuchukua sahihi za kim ili kukubaliana na moja ya mambo mawili, la kwanza ni kuwa na mwanamke ambae anaweza kumzalia, na lapilli ni kuiachia kampuni…
Basi mwanasheria akakubaliana na babu yake kim na kwenda mpaka ofisin kwa kim na kumuambia masharti ambayo bibi yake ameyasema juu yake, kim akacheka sana kisha akasema “ amesema niwe na mtoto na nisiwe na mke, asijali hilo limepita, kwa maana hata mimi nataman sana kuwa na mtoto, so nitatafuta mwanamke wa kunizalia na baada ya kuzaa ataendelea na maisha yake, kwa maana ni lazima tutafute mrithi kwenye familia yetu, akasema kim kumuambia mwanasheria wa familia….
“ lakin bibi yako hakuwa amemaanisha kuwa uzae tu, bali anataman sana uwe na mke, ambae atawaletea mtoto, akasema mwanasheria, na kim akadakia na kusema “ kwa maelezo yako umesema kuwa bibi yangu anataka mimi niwe na mtoto, na sijaona mahala popote pale ambapo anataka niwe na mke, bali anataka niwe na mtoto, na kuhusu mtoto, msijali baada ya miezi tisa atamuona, na mwambie kuwa nitakuwa tayar kwaajili ya kufanya nae vipimo vya vinasaba ili kuona kama ni wangu au laa, ili aniamin kabisa, akasema kim, jibu ambalo lilimfanya mwanasheria wa familia yao akoser la kusema na kuondoka akiwa haamin kabisa majibu ya kim, kuwa ataweza vipi kuzaa bila kuwa na mwanamke…..
Anaonekana bint mmoja akiwa anajiandaa kama amechanganyikiwa, alikuwa akivaa nguo zake kuu kuu, na alikuwa anaonekana kuchagua nguo yenye afadhali kidogo, kwa maana hakuwa na nguo yoyote ile ya maana, na alipotaka kwenda kupiga mswaki, akaona saa na kukuta anadakika kumi na tano anatakiwa afike sehemu ambayo alikuwa anatakiwa kufanya usaili na alikuwa anadakika kumi na tano kufika kwenye eneo ambalo lilikuwa linahitaji karibu dakika 45 mpaka kufika anapotakiwa kwenda….
Bint Yule alifika kwenye jengo moja kubwa, ambalo nje kulikuwa kuna kama kinyago cha mti wa muhindi na maharage na kulikuwa na picha kadhaa za mazao, ikionesha kuwa lilikuwa ni shirika kubwa sana la mazao, Yule bint akiwa kama mtu mwenye haraka sana akapita kwenye geti kuu, na hata mlinzi wa hapo alipomuita hata hakugeuka nyuma, ila alipofika kwenye lango kuu la kuingilia kwneye kampuni akazuiliwa na mlinzi mwingine na kuulizwa anaenda wapi….
“ naenda kufanya usaili, naomba usinizuie maana nimeshachelewa sana, akawa anasema Yule bint akiwa anajitoa kwa mlinizi ili aende zake kwenye usaili…
“ madam acha vurugu maana usaili umeshapita na umechelewa sana, sasa nomba urudi ulipotoka maana hakuna mtu anaweza kukusaidia hapa, akasema mlinzi na Yule bint akakaa chini na kuanza kulia, yaan kila ambae alikuwa anapita pale alikuwa anamshangaa, kwa maana hakuna ambae alikuwa anajua hata nilikuwa nalia nini….
Mara Yule bint akaanza kusema “ kwanini nina bahati mbaya kiasi hichi mimi, nilikuwa naamin kuwa huu usaili utabadilisha masomo yangu, sijui mdogo wangu atasomaje, na sijui maisha yangu yatakuwaje jaman, ni lini mungu anataniona na mimi lakin…
Sasa wakat analia lia pale chini mara kim na msaidizi wake wakapita, ikabidi waulize Yule bint analia nini, ndio mlizni akawaambia kuwa alikuwa amechelewa kwenye usaili ndio analia…
Kim akasogea mpaka a;lipo Yule bint kisha akasema “ naitwa karim, ila watu wamezoea kuniita ceo kim, naweza kujua una shida gani na unahitaji msaada gani…
Yule bint akatabasamu kisha akasema “ naitwa farida, nilikuwa nina shida sana ya kazi boss, naomba unisaidie…
Kim akamuangalia farida kwa dakika kadhaa kisha akamnong’oneza Yule msaidizi wake kitu kisha akamtaka farida aende nae ofisini kwake, farida ni kama hakuamin kabisa, kwa maana alikuwa anahisi labda ndio kashakosa kazi, ila kitendo cxha boss kuomba aende nae ofisin kwake, akajua wazi kuwa huenda anaenda kufanyishwa usaili pekee yake, akawa anajipongeza kimoyo moyo kwa kujitoa ufahamu, maana huenda angekosa kazi, bila kujua anatakiwa kwenda kufanya kazi gani…
Basi akafika ofisin kwa kim, na wakat wote kim alikuwa kimya, na mpambe wake alitoka na baada ya kama nusu saa alirudi Yule msaidizi wa kim, na kumpa kim taarifa flani hivi basi kim akatabasamu kisha akamgeukia farida na kusema, “ naanza kukupa kwanza mshahara kabla ya kazi, kwa maana nityamgharamikia mdogo wako kila anachokitaka, na kingine nitakutafutia nyumba nzuri na utakuka na kuvza unachotaka..
Sasa farida anachekelea anajiona amepata boss mzuri, na alivyo kiazi hata hakuuliza ni kazi gani, imefika usiku anashangaa mdogo wake anampigia simu na kumshukuru, na kesho yake akaenda kuoneshwa kwenye nyumba, ilikuwa ni ghorofa moja, na kulikuwa kuna bint wa kazi, yaan mpaka farida akawa anajiona kama ameokota pochi ya mzungu…
Basi alikaa kwenye hio nyumba kwa siku kadhaa bila kujua kazi anayotakiwa kufanya, moaka siku hio alipokuja Yule msaidizi wa kim, anaitwa haroon, akamfata farida kisha akamuambia, “ ni muda wako sasa wa kufanya kazi yako…
“ kazi gani? Na usijal nipo tayar kufanya lolote lile, maana mmenionesha ukarimu wa hali ya juu kwake..
“ unatakiwa kumzalia boss kim, akasema Yule msaidizi wa kim, kitu kilichomfanya farida atoe macho kama kinyonga aliekosa muelekeo…
NAKUJA….
MR CEO NA MIMBA YANGU 2
HUSQER BALTAZAR
“ namzaliaje mwanaume mimi, kwanza hata sijawah kulala na mwanaume, alafu anatokea mtu ananiambia kuwa nimzalie, mimi siwez kulala na Yule boss wako mwenye kiburi mimi, siwez kabisa, akawa analalamika farida…
“ hautalala nae kabisa, ila unatakiwa kuzaa nae tu, kwa maana ameshaweka sampo zake maabara, na unatakiwa kwenda kupandikizwa, akasema Yule msaidizi wa kim, kiukweli nilishangaa sana, kwa maana mambo ya kwenda kupandikizwa sampo yalikuwa mapya sana kwangu, na sikuwa nataka kabisa, ila Yule msaidiz wa kim akanambia kama sitokuwa tayar kumzalia basi nirudishe kila alichonipa…
Kurudisha nyumba halikuwa tatizo sana kwa farida, maana angeondoka zake tu, ila tatizo ni kwenye kurudidha pesa ambazo mdogo wake amepewa, maana hata kama farida angefanya kazi kwa miaka mitano kwa kim bila kulipowa ila asingeweza kurudisha pesa zote ambazo amepewa, hivyo kwa shingo upande akakubali kwenda kupandikizwa mimba….
Basi alienda maabara akiwa pamoja na msaidiz wa kim, jambo ambalo lilikuwa linamshangaza sana farida, maana aliamin kuwa kim atakuwa nay eye bega kwa bega kwa kipindi chote hicho maana alikuwa ndio mwenye uhitaji wa mtoto ila haikuwa kama anavyofikiria kabisa, akajikuta anahisi unyonge sana moyoni mwake, maana ndoto zake zilikuwa ni kuzaa akiwa na mwanaume anampenda, na sio kupandikizwa mbegu alafu akapambane nazo mwenyewe hata kama atakuwa anahudumiwa…
Basi baada ya kurudi anapoishi, na hapo alirudishwa na yule msaidizi wa kim, kisha wakaagana na mwisho wakaondoka zao, farida alirudi ndani na kulia sana, akawa anayatafakari sana maisha yake, kwa sababu asingekuwa maskin basi asingetumika kama bidhaa tu, na huenda angepatas mtoto kwa bashasha kubwa ya baba mtoto wake na sio kama ambavyo ilitokea kwake….
Basi bana mimba ikamaliza mwezi, kiukweli hakuwah kuja kutembelewa na kim hata kwa bahat mbaya, au hatya kupigiwa simu, ingawa alikuwa na mfanyakazi na alikuwa anapata kila anachokitaka, ila hakuwa na fueraha kabisa, na muda mwingi akawa anajifungia ndani pekee yake tu, akiwa na unyonge wa hali ya juu…..
Siku moja akiwa zake amekaa anaangalia luninga, mara akajikuta anamkumbuka sana kim, akawa anataman kunusa harufu au hata manukato ya kim, ila hakujua atapata wapi hio nafasi, maana huwa tunajua vituko vya mimba, sasa kwa farida vikamjia kihivyo, akawa anataman sana kusikia harufu ya kim tu, akawa anapotezea ile hali, ila ikawa inamsumbua mpaka akawa anajikuta anashindwa kujizuia, na kuanza kujiandaa kisha akaenda mpaka kwenye kampuni ambayo alikuwa anafanya kazi kim na kutaka kumuona…
“ dada una apportment nae, akauliza mlinzi mara baada ya farida kufika kwenye kampuni…
“ apportment ya nini? Kwanza mnajua mimi ni nani?, akauliza farida kwa sauti kubwa nay a kujiamin sana…
“ hatukufahamu, na hauwez kumuona boss kama hamjakubaliana mapema, hivyo dada kama hautajali naomba uondoke, akasema mlinzi…
Farida asingeweza kabisa kurudi nyumban, maana tamaa yake ya kutaka kusikia harufu ya kim ilikuwa inaongezeka kadri muda unavyozidi kwenda, akaona usinitanie, akamuangalia Yule mlinzi kisha akataka kupita kwa nguvu…
“ dada samahan hauwez kuingia hapa bila kupewa apportment, akaendelea kusema mlinzi…
“ mimi ni mwanamke wa kim, na hapa nilipo nina ujauzito wake, na mwanangu amemkumbuka sana baba yake, nahisi haunielewi, maana kumkera mtoto wa kim alietumboni, ni zaidi hata ya kumkera kim mwenyewe, akasema farida kwa sauti kubwa, na kila ambae alikuwa eneo lile alimsikia vyema kabisa…
Swala la farida kupandikizwa mbegu lilikuwa siri sana, na kila wakati alisisitizwa asiseme, Ila ndfio hivyo ameshapasua jipu, na kila mtu kajua sasa kuwa farida ana mimba ya kim….
Watu wakiwa kwenye mshangao, huku minong’ono ya hapa na pale ikiendelea kuongezeka, mara msaidizi wa kim akapita eneo lile na kumuona farida akiwa anabishana na mlinzi, akasogea mpaka walipo kisha kwa sauti ya mamlaka akauliza “ kuna nini kinaendelea hapa?...
“ yaan sijui hata huyu mlinzi wenu anashida gani, namuambia kuwa mimi nina ujauzito wa kim, ila hataki hata kunielewa, embu waambie hawa kuwa mimi na kim hapa tulipo tunakaribia kupata mtoto, akaendelea kusema farida, akiwa anaongea kana kwamba anaongea kitu cha maana na wakati alikuwa anasisitiziwa kila wakati kuwa inatakiwa kuwa siri…
Yule msaidizi wa kim alibaki katoa macho, ila hakutaka watu wajue mshtuko wake, kisha akamsogelea mlinzi na kumuambia “ huyu mwanamke akija hapa, naomba umruhusu kuingia maana anaukaribu sana na viongozi wa hii kampuni, kisha akanishika mkono na kunipeleka mpaka kwenye ofisi ya kim na kuniuyliza “ umeshindwa kupiga simu, embu nambie una shida gani?...
“ kwani wewe ndio baba wa mwanangu mpaka uniulize shida yangu, sasa ni hivi mtoto amemkumbuka baba yake, ndio maana nikamleta aje aongee na baba yake, sijui kama umenielewa, akasema farida akiwa kama amepanic flani…
Yule msaidizi hakutaka hata kubishana nae, na badala yake akaondoka zake, ila wakat anaondoka akamuambia farida kuwa atulie pale ofisin, maana kim yuko kwenye kikao, hivyo atarudi muda sio mrefu sana…
Farida akatabasamu na kumuitikia tu sawa, na baada ya hapo Yule msaidizi akaondoka zake, na pale ofisin alibaki farida pekee yake, farida akaenda na kukaa kwenye kile kiti ambacho huwa anakaa kim, kisha akatoa udongo wake na kuanza kula huku anajizungusha kwenye kiti, hapo anasikia rahaa balaa…
Baada ya dakika chache kim akaingia ofisin kwake, akamkuta farida anazunguka kwneye kile kiti kana kwamba anafanya mchezo vile, kwa sauti ya ukali kim akasema “ unafanya nini kwenye kiti changu…
Farida akaacha kabisa kucheza na kiti kisha akasimama bila kusema neno lolote lile akaanza kusogea alipo kim, kana kwanba mtoto ambae aliona pipi, akasogea mpaka lilipo kwapa lake na kuanza kumnusa, kitu ambacho kilishangaza sana kim, akataka kumsukuma ila Yule msaidizi wake akampa ishara kuwa amuache, ikabidia atulie lakin alikuwa amekunja sura huyo kama amekula ndimu, farida alinusa harufu ya kwapa la kim kwa takriban dakika moja kisha akasema “ angalau sasa nitalala vizuri….
Uzalendo ukamshinda kim akajikuta anauliza “ kwa hio umekuja kufanya nini hapa…
Farida akacheka kidogo kisha akasema “ mtoto alimiss harufu ya jasho lako, kisha huyo akawa anaondoka zake na kwa namna alivyojibu ni kama ameshapata anachokitaka sasa moyo wake unaaman, kim akabaki kutoa macho, kwa maana hakuwah kuishi na mama mjamzito na hajui vituko vya mimba, akamuangalia Yule msaidizi wake, na msaidizi akatabasamu tu, maana yeye kidogo ana watoto huenda akawa anaelewa alichokuja kufan ya farida pale, kweli ni mimba au anataka tu kumsumbua….
NAKUJA
MR CEO NA MIMBA YANGU 3
he only need a child
HUSQER BALTAZAR
“ embu nambie maana sijamuelewa kabisa huyu bint, ni nini hichi amekuja kufanya hapa? Akauliza kim mara baada ya farida kuondoka…
“ mimba zina mambo mengi boss, hata mimi mke wangu alipokuwa na mimba ya mtoto wangu wa pili, alikuwa nioge, na anataka kunisikia nikiwa nanuka jasho, hivyo inawezekana ni mimba kweli maana unakuta sio yeye ni mimba ndio inamtuma….
“ mungu aepushilie mbali, huyu bint asije kujua hilo, maana anaweza kunifanyia kusudi akajifanya anapenda kusikia harufu ya jasho langu na asitake nioge, akasema kim na Yule msaidizi wake hakuwa na chakufanya zaidi ya kucheka tu, kisha akasema “ miezi tisa ni mimngi, hivyo jiandae kwa chochote, ,maana hichi cha leo ndio kituko cha kwanza, bado vingine na hatujui atataka nini tena…
Mbona kazi rahisi sana hio, kama ni kweli anapenda harufu ya jasho langu, naomba unisaidie kuwaambia wafanya kazi wangu kuwa, watafute mashati matano ambayo hawajayafua nab ado yananukia jasho langu, alafu wa mpelekee Yule bint kichaa ilia ache kunisumbua…
Msaidizi wa kim hakuwa na hiyana, akafanya kama boss wake alivyomuelekeza, akaenda kutafuta mashati matano kweli, na baada ya kazi, akaenda mpaka anapoishi farida na kumkabidhi….
“ ni nini hiki? Akauliza farida mara baada ya kim kufika na kuingia ndani…
“ boss kanambia unapenda harufu ya jasho lake, hivyo kaagiza nikuletee mashati yake ambayo yanajasho lake, akasema Yule msaidizi wa kim, na farida akatabasamu kisha akasema tu asante na baada ya hapo kim akaanza kuondoka zake….
Sasa farida amekaa ananusa yale mashati, akaona hapati ile raha ambayo aliipatya mcahana wakat ambapo alikuw ananusa kwapa la kim, wakat ambapo kim alikuwa amevaa hio nguo...
Ila akajikuta anataman sana kim angekuwa hapo wakati huo walau amkumbatie, kwa maana ni kama alikuwa amelikumbuka sana joto lake…
Ilikuwa tayar saa tano kasoro, na farida hakuwa na namba ya kim, hivyo akampigia Yule msaidizi wake, na baada ya dakika kadhaa simu ikapokelewa na farifa akaanza kulia sasa…
“ vipi unataka nini, na haujui kama mimi nimeoa kwanini unanipigia saa hizi, akasema msaidizi wa kim….
“kama hautaki nikupigie wewe basi nipe namba ya kim, maana mtoto amemmiss sana, akasema farida kwa sauti ya kilio….
“ hivi wewe mwanamke una shida gani lakin? Akualiza Yule msaidizi wa kim, na farida hakuwa anajibu chochote kile zaidi ya kulia tu, mpaka Yule msaidizi wa kim akakata simu…..
Farida basi siku hio alishinda analia mpaka asubuh, na kulivyopambazuka akataka kwenda kazin kwa kim, ni kweli alikuwa anataman hata amkumbatie walau kidogo, ila akasema ngoja ajizuie, maana mwisho atamuona ni mzumbufu, maana hata yeye hakuwa anajua kabisa ile hali ilikuwa inatokana na nini, maana hakuwah kubeba mimba hapo kabla, na hakuwah hata kuwa na mwanaume, yaan anaanza kuwa na mimba kabla ya kuwa na mwanaume ………
NAKUJA……
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote