MAPENZI YA WATOTO WA KAMBI YA JESHI
nikisema hivi namzungumzia yasir, shamte na mimi...
Wazazi wetu wote walikuwa ni wanajeshi hivyo tuliishi na kukuwa kambin..
Tulivyoanza kukuwa shamte na yasir wakaanza kunipenda kisiri siri wakawa wanagombania kuwa karibu yangu, mwisho nikaja kujua..
Nilivyojua nikaona nimchague yasir maana alikuwa anabusara na alikuwa msafi sana..
Maisha yakaja kutitenganisha ambapo shamte na yasir walienda kisoma nje udaktar wanakuja kurudi na kunitafuta na yasir akata tiendeleze mahusiano na kwa namna alivyobadilika nikakubali kumbe sikuwa bado nimekuwa kiakili, maana nilimuona kama amezubaa na kuanza kumtaman shamte ambae alikuwa ni playboy..
Nikaja kuyaharibu mahusiano yangu kwa ujinga wangu...
Ukitaka kujua mkasa huu ulivyo usikose simulizi ya MPENZI WAKO NI MKE WANGU
MPENZI WAKO NI MKE WANGU 1
MTUNZI SMILE SHINE
Sophia na Shamsa walikuwa ni marafiki walioshibana, kwa mara ya kwanza walikutana chuo cha IFM wote wakiwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza walitokea kupendana sana na kuambiana mambo yao mengi sana . Siri ya Sophia ilikuwa ya Shamsa na ya Shamsa ilikuwa ya Sophia kifupi hakuna walichofichana.
Mara kwa mara Sophia alikuwa akisimulia shazma habari zake za utotoni hasa kuhusu vijana wawili ambao alikuwa nao tangia wakiwa chekechea. vijana hao ni Shamte na Nassir.
Shamsa alikuwa alifurahishwa sana na vituko alivyokuwa akisumbuliwa na kutamani kuwaona hao vijana Nassir na Shamte.
Siku moja Sophia alikuwa anatafuta kitu kwenye begi lake alitoa vitu vyote na kuanza kukunguta kitu kimoja kimoja, katika harakati za kung'uta begi ilianguka picha, aliokota ile picha na kuiangalia aliangalia sana ile picha na kujikuta anatabasamu.
" Shamsa njoo uone sasa. Shamsa alienda alipo Sophia na Sophia akampa ile picha . Shamsa aliangalia ile picha kwa makini huku akimuangalia Sophia usoni alafu akasema.
" Huyu binti hapa kati kati ni wewe hawa watoto wa kiume sijui ni wakina nani.
Sophia akitabasamu kisha akachukua ile picha na kuanza kumuelekeza.
"Hapa tulikuwa darasa la sita huyu wa upande wa kulia ni Nassir na huyu wa kushoto ni Shamte.
" Waooo kumbe ndio hao ma handsome unaowataja kila siku.
" Haswaaa huyu ni Shamte na huyu ni Nassir.
" Kwakuwa leo nimeziona sura zao unaweza kuanza kuniambia historia yako na wao.
" Nitakwambia kwasababu sichoki kusimulia historia yangu na hawa vijana. Huko miaka ya nyuma mimi , Shamte na Nassir tulikuwa tunaishi kwenye kambi ya jeshi wazazi wetu walikuwa wanajeshi hivyo basi tulikuwa pamoja na kusoma pamoja tulikuwa marafiki wakubwa sana alipo Shamte ulikuwa hunikosi mimi wala Nassir yani tulifuata na kama kumbikumbi, kuna baadhi ya watu walitimiza Lucky three.
Tulipofika darasa la saba kuna kitu kulijitokeza kati yetu vijana hawa wapuuzi ni kama vile barehe ilianza kuwasumbua wakaanza kunigombania kisiri siri pasipo mimi kujua yani hapo kila mmoja alikuwa anataka niwe mchumba wake tulikuwa tukitoka shule Nassir alibeba begi langu na Shamte alibeba chochote nilichokuwa nimeshika na kama sikuwa na kitu basi wakigombania begi langu mmoja akawa akanishika mkono wa kulia na mwingine mkono wa kushoto , mimi sikuwa na hili wala lile nilikuwa najionea kama mchezo tu .
Siku moja ilikuwa siku ya sikukuu ya christimas karibia watoto wote ya pale kambini zilichukuliwa na kwenda kutembea kwenye michezo ya watoto pamoja na kuona wanyama , tukiwa
Huko Nassir alikuja kunishika mkono na kunivalisha saa Shamte alivyoona vile aliona wivu akaenda kununua miwani ya watoto akaja kunivalisha . Shamte akaanza kusema
" Miwani imekupendeza kuliko saa kwanza saa yenyewe ya bei rahisi.
Nassir alichukua nae akarusha vijembe vyake.
" Acha majivuno kwanza miwani yenyewe rangi yake mbaya , Sophia bora uvue haujapendeza hata kidogo upo kama yale maombi ya kwenye mziki wa Michael Jackoson .
mwisho wa siku walishikana na kudundana bahati walikuja kuamuliwa kabla hawajaumizana lakin baada ya hapo walikuwa wamekasirikana.
" Mmmh ikawaje sasa? Shamsa alinogewa na story.
" Walikuwa wabishana na na kugombana mara kwa mara. Tulipofika form one nilipevuka kiakili nikawa nimewaelewa hawa vijana wawili , ulikuwa ni mtihani mkubwa kwangu lakini ilinibidi nifanye maamuzi. mwisho wa siku moyo wangu iliangukia kwa Nassir tukawa wapenzi tunaandikiana vibarua. Haikuchukua muda Shamte alihamishwa shule akaenda kusoma shule ya bweni hapo kidogo ilikuwa nafuu kwetu lakini mwaka uliofuata baba yake Nassir alihamishiwa kambi wakaondoka familia nzima , pale nikabaki pekee yangu Shamte alikuwa shule tulionana wakati wa likizo na kipindi hicho hakuwa na mpango na mimi tulikuwa marafiki ila sio kama zamani alafu wakati huo alikuwa na msichana palepale kambini , mimi na Nassir tulikuwa tukitumia na vibarua tu badae tulikuja kupotezana kabisa lakini mwaka jana nilipata mawasiliano na Shamte kumbe wapo chuo kimoja huko Uturuki nime wamiss sana natamani kuwaona tena.
" Waooo story nzuri sana . Kwahiyo Nassir akija na kutaka muendelezo mlipoishia utakubali?
" Hahahaha ooooh Mungu wangu! Shamsa kipindi kile tulikuwa hatujitambui wala hatuelewi nini maana ya mapenzi saingine wenzangu huko wamepata waturuki huko.
" Kama mlikuwa mnapendana basi alama ya upendo haiwezi kufutika kati yenu.
Miaka miwili badae Nassir na Shamte walirudi nchini na walikuwa na shauku kubwa ya kukutana na rafiki yao kipenzi Sophia na siku hiyo Sophia alikuwa na furaha sana alimuomba Shamsa amsindikize kwenda kukutana na marafiki zake. Shamsa alikubali wanajiandaa na kuvalia nguo zao nzuri kisha wakaenda kwenye hoteli waliyokuwa wamefikia.
Sophia na Shamsa walipofika walienda moja kwa moja restaurant kisha wakapiga siku kuwataarifu kuwa wameshafika.
Shamte na Nassir walitoka kwenye vyumba vyao na kwenda mpaka restaurant, Sophia alipowaona kwa mbali aliachia tabasamu.
" Shamsa waangalie wale pale wanakuja.
Shamsa aligeuka kuwaangalia huku macho yakimtoka maana walikuwa ni wanaume wa nguvu yani vijana wa maana kabisa .
" Mungu wangu hawa vijana mbona wanavutiwa hivi?
" Ndio wenyewe yule mrefu zaidi ni Shamte na huyu mwingine aliyevalia tisheti nyeupe iliyoshika mwili ni Nassir.
Shamte na Nassir Walifika karibu yao Sophia alisimama na kuwakumbatia kwa furaha .
" Siamini kama nimewaona tena, nimefurahi mno kuwaona.
" Kwa upande wangu ni zaidi yako nilikumiss sana . Alisema Nassir huku akimshuka mashavu.
" Inatosha Nassir nipe nafasi na mimi ya kumkumbatia huyo mrembo nilimmiss sana huyo wildcat. Alisema Shamte na Nassir alisogea pembeni kumpa nafasi. Shamte nae akimkumbatia kisha baada ya hapo walikaa na Sophia akamtambulisha Shamsa.
" Jana huyu ni rafikiye yangu kipenzi , ndugu yangu anaitwa Shamsa.
" Tumefurahi kukufahamu Shamsa kuwa huru unapokuwa na sisi.
" Asante.
Waliendelea kula na kunywa huku wakikumbushiana mambo ya zamani.
" Jamani msiondoke tena kaeni karibu yangu.
" Mimi siwezi labda Nassir.
Alisema Shamte kama utani.
Baada ya kuzungumza kwa muda mrefu Shamsa na Sophia walirudi kwao wanakoishi na Shamte na Nassir walibaki hotelini lakini lengo lao ilikuwa kutafuta nyumba ya kuishi kwenye ule mji sababu walipanga kuishi pale Shamte alipata kazi kwenye hospitali ya jeshi na Nassibu alipata kazi kwenye hospitali ya rufaa.
Mara kwa mara watu hawa walikuwa wakikutana na
Shamsa alijiunga kwenye urafiki wao.
Nassir na Sophia alijikuta wa
wanarudisha mahusiano yao ya zamani ikabidi Shamte nae arushe ndoano kwa Shamsa kwa bahati alikubali kiroho safi na mapenzi motomoto yakaanza.
MPENZI WAKO NI MKE WANGU 2
MTUNZI SMILE SHINE
Siku zilizidi kusonga marafiki hao walikuwa wenye furaha sana na walikuwa wakitoka pamoja kwenda sehemu mbali mbali za starehe.
Taratibu Shamte alianza kumjua makucha yake alishindwa kabisa kujizuia kuwaona wadada wazuri wanapita mbele yake , akiwaangalia na kuwasifia Shamsa alipomlalamikia kuhusu hilo tabia yake aliishia kusema.
" Fahari ya macho haifilisi duka, mimi naangalia tu lakini furaha yangu ni wewe.
Licha ya Shamte kumpa mapenzi na kumuonyesha Shamsa mapenzi ya hali ya juu lakini hakuweza kutulia na mwanamke mmoja mara nyingi alikuwa akitoka na wanawake wengine . Kifupi alikuwa akicheza sana na mioyo ya wanawake, alikuwa anatoa ahadi nyingi nzuri ikiwepo ahadi ya ndoa . Wanawake wengi walimkubalia na alipokuwa nao aliwatumia tu baada ya hapo aliwaacha kwenye mataa .
Siku moja walihudhuria sherehe moja ya uchumba daktari mwenzao alikuwa anamvaliaha mchumba wake pete.
Katika hiyo sherehe Shamte alikuwa hatulii mara nyingi alimtelekeza shamsa na kwenda kusimama na wanawake wengine ile tabia haikumpendeza Shamsa hivyo ilimfanya awe mnyonge, na kujiona hana thamani. Nassir alimkuta akiwa kakaa kinyonge .
" Vipi Shamsa mbona umepooza hivyo shemeji yangu hebu changamkia basi tupo kwenye sherehe hapa.
Shamsa alilazimishwa tabasamu.
" Usijali nipo sawa.
Nassir alimuona Shamte akiwa anazunguka hovyo na kuongea na wanawake na kuna muda alikuwa anabadilisha nao namba za simu. Kwakuwa anamfahamu vizuri rafiki yake aliamua kumfuata na kumvutia pembeni.
" Vipi kaka mbona unanivutia pembeni.
" Shamte hivi utakuwa lini kwanini hubadilika wewe.
" Kwani nimefanya nini kaka?
" Tabia yako ya uhuni utaachwa lini unafikiri yule mtoto wa watu haumii kwa hicho unachomfanyia?
" Aaaaa kwani anajua ninafanya nini?
" Shamte yule sio kipofu wala mjinga anaelewa kila kitu hebu jaribu kumuheshimu binti wa watu mbona yeye ni mstaarabu sana na ameamua kukupa mapenzi yote iweje wewe unamfanyia ujinga?
" Basi kaka yameisha. Hilo limeisha kabisa naenda kwa Shamsa wangu.
" Nenda bwana unajua unamkosesha raha mtoto wa watu kukupenda isiwe adhabu kwake.
" Sawa kaka umeelezwa mbona.
Shamte alienda alipokaa Shamsa akakaa pembeni yake.
" Vipi mpenzi mbona huna raha?
" Nakuwaje na raha ikiwa hutaki kukaa na mimi na unaonekana kufurahia kukaa na wanawake wengine.
Shamte aliachia tabasamu
" Punguza wivu mpenzi wangu wewe pekee ndio una nafasi kwenye moyo wangu hao wengine nawachukulia kama marafiki tu , nakupenda sana wewe.
Shamsa alilidhika na maneno ya Shamte akajiona yeye ndio yeye.
Baada ya kutoka kwenye sherehe waliondoka na kwenda kulala pamoja kwenye nyumba ya Shamte na Nassir.
Wakiwa chumbani Nassir alimwambia Sophia.
" Mpenzi sitamani maisha yetu yawe hivi nataka haraka iwezekanavyo tufunge ndoa.
Sophia alifurahi sana
" Jamani mpenzi hili ndilo lililokuwa wakisubiri kutoka kwako , nitakuwa na amani sasa.
" Kwani sasa huna amani?
" Kusema ukweli sina nahofia usije ukawa unamambo yako ya chinichini kama Shamte.
" Hahaha haiwezekani hata kidogo , Shamte bado hajajua anataka nini ila angefikiria vizuri Shamsa ni mwanamke anaemfaa sana.
" Labda ipo siku atalitambua hilo.
Upande wa kina Shamsa simu ya Shamte ilikuwa ikiita mara kwa mara.
" Shamte ni nani anakupigia usiku huu?
" Itakuwa wagonjwa.
" Wagonjwa muda huu wanataka nini, kwani huko hospitali hakuna na daktari wengine?
" Kwahiyo unanifokea?
Alihoji Shamte baada ya kuona hana jibu.
" Sio nakufokea nina haki ya kujua wewe ni mwanaume wangu.
" Kwahiyo kama mimi ni mwanaume wako ndio unipande kichwani?
Shamte alikuwa mkali aliongea kwa sauti ya juu .
Nassir na Sophia walisikia marumbano yao wakiwa chumbani kwao.
" Hebu sikiliza huko. Alisema Sophia
" Kuna nini?
" Itakuwa wameanza kugombana.
Nassir alinyanyuka kitandani akavaa suruali yake ya track suti .
" Hapa shida itakuwa ni Shamte tu.
Walitoka kwenda kuamua ugomvi.
" Shamte una nini wewe?
" Huyu mwanamke anataka kunipanda kichwani na mimi sio mwanaume wa aina hiyo .
Shamsa alishindwa kujitetea alikuwa akilia, Nassir alijisikia vibaya akamfuata na kumkumbatia huku alimmbembeleza, Sophia alitoka nje na Shamte kwaajili ya kuongea.
" Shamte unajua unakosea sana mwanamke haongeleshwi kwa hasira kiasi hicho.
" Ameyataka mwenyewe ninampatia kila anachotaka licha ya kuwa nina mambo yangu lakini moyo wangu nimempatia yeye nenda kamuulize anakosa nini kwangu kama kitandani namridhisha mpaka anaomba poo .
Huko ndani Nassir aliendelea kumbembeleza huku alimfuta machozi.
" Shemeji mimi nashindwa Shamte ananionea.
" Basi shemeji yangu nitaongea nae na kila kitu kitakuwa sawa.
Baada ya pande zote mbili kuongea waliungana pamoja na kusuruhusha mambo yakawa sawa kila mmoja akamchukua mtu wake wakaenda vyumbani kwao kulala.
MPENZI WAKO NI MKE WANGU 3
MTUNZI SMILE SHINE
Mahusiano ya Shamsa na Shamte yalikuwa na vikwazo vingi , ugomvi kila siku kutokana na tabia za Shamte kujifanya jogoo anataka kupanda kila mtetea unaomvutia, Nassir na Sophia walikuwa anasuruhisha ugomvi wao mara kwa mara na kumpa moyo Shamsa , walikuwa akimsihi kuwa mvumilivu ipo siku mambo yatakuwa sawa sababu Shamte alikuwa anampenda ila ndio haikuwa jambo la mara moja yeye kubadilika.
Mara nyingi Nassir alikuwa karibu nae akimfariji.
Kumbe ukaribu wa Nassir ulianza kujenga kitu kwenye moyo wa Shamsa. Alitamani siku moja apate mwanaume anayejali na kuthamini kama Nassir . Kuna wakati alitamani Nassir ndio angechukua nafasi ya Shamte.
" Hivi nawaza nini ? Nassir ni shemeji yangu. Mungu wangu niondokee haya mawazo yenye utata kwenye akili yangu .
Mara nyingi Shamsa alikuwa akikaa mwenyewe mawazo yake yalikuwa kwa Nassir alijikuta anaandika kwenye diarly yake matukio mengi alivyofanyiwa na Nassir na hiyo diarly alijificha mbali sana rafiki yake Sophia asiweze kuiona maana ikitokea Sophia akiona hawezi kumuelewa kutokana na kile alichokuwa anaandika kwenye ile diarly. Japokuwa hakuandika kwa ubaya ilikuwa ni kujifurahisha tu maana alikuwa anaijua mipaka yake na kuheshimu uhusiano wa rafiki yake.
Siku ya weekend walitoka wakaenda beach kuogelea kila mmoja akiwa na mpenzi wake, Shamte na shamsa walikuwa kwenye maji wanaogelea kuna wakati Shamte alimnyanyua juu wakawa wanacheza kwenye maji.
Sophia alikuwa akimuangalia sana Shamte kuna kitu alikuwa kagundua kutoka kwa mwanaume huyo mtanashati aliekuwa na nguvu na mwenye kifua cha kilichojazia kwa mazoezi.
Sophia aligundua Shamte yupo tofauti sana na Nassir.
" Sasa nimeweza kujua nini sababu ya wanawake wengi kumtaka Shamte pia shoga yangu Shamsa kuna kitu anafaidi ndio maana kila siku aishiwi na wivu na kutoa machozi kwaajili yake.
Akiwa kwenye dimbwi la mawazo alishitukia na Nassir.
" Vipi unataka kwenda kuogelea?
" Ndio twende tukaungana na wenzetu.
" Ila mimi nitakuwa msindikizaji nitaishia kwenye kina kifupi kule mbali siwezi kufika.
" Nakujua vizuri sana , ila unatakiwa ujitunze si unaona Shamte anavyopenda mbali na mpenzi wake.
" Kwahiyo unawatamania?
" Natamani siku moja na sisi tuwe kama wao.
Walinyanyuka pale walipokuwa wamekaa Wakaenda kuogelea lakini akili ya Sophia ilikuwa kwa Shamte bado alikuwa akimchunguza umbo lake kifua chake kilichokuwa kinavutia wanawake wengi, hata muonekano wa Shamte ulikuwa wa kuvutia zaidi alimpita Nassir japokuwa nae alikuwa anamfuto wake.
" Nassir unaweza kujaribu twende kule kwenye maji marefu? Alisema Sophia ili kupata njia ya kuomba aende na shamte
" Hapana kwakweli siwezi naogopa sana maji marefu.
" Jamani , Shamte unaweza kunipeleka kule? Sophia alimgeukia Shamte akamuomba
" Haina shida. mamy ngoja nimpeleke nakuja sasa hivi. Shamte alimuomba Shamsa
" Hakuna tatizo.
Sophia alimshika bega Shamte wakawa wanaongoza na kuelekea sehemu ya maji yenye kina kirefu , kadiri walivyokuwa wakasogea Sophia alikuwa akimng'ang'ania Shamte.
Nassir na Shamsa walikuwa wakiwaangalia na kila mmoja alikuwa na amani .
" Vipi tunaweza kwenda kuwasubiri kule kwenye mchanga?
" Sawa.
Walitoka kwenye maji na kwenda kukaa chini ya mnazi.
" Hatuwezi kukaa kipwekee hivi nisubiri nakuja. Alisema Nassir huku akinyanyuka na kwenda kuchukua ice cream.
Sophia na Shamte Walifika kwenye kina kirefu cha maji. Sophia aliendelea kumshika kwa nguvu akawa kama kamkumbatia huku jicho la Sophia likiwa kwenye kifua cha Shamte.
" Niachie basi utaogeleaje ukiwa umenishika hivyo?
" Shamte usije ukaniachia naogopa kufa kwenye maji. Aliongea Sophia kwa sauti ya kudeka
" Siwezi kukuacha uzame .
" Basi nishikilie vizuri mwenzio.
" Usijali.
Shamte alimshika kama vile alivyotaka Sophia wakaanza kuogelea pamoja .
Upande wa pili Nassir na Shamsa walikuwa wanakula ice cream huku wakipiga story.
" Vipi jamaa kapunguza fujo zake? Nassir aliuliza.
" Mmmh ndio hivyo hivyo inabidi niziwee huenda ipo siku atabadilika.
" Ni kweli kwasababu anaonyesha kukupenda.
" Ni kweli lakini ningenda awe kama wewe yani natamani sana.
" Kwani mimi nipoje shem?
" Upo tofauti sana na yeye . wewe ni mwanaume anaejielewa sana .
" Basi watu huwa hatufanani kwa kila kitu ila naamini ipo siku Shamte anathamini upendo wako na kuamua kuacha mambo yake ya ajabu. Naona penzi lenu litafika mbali .
" na iwe heri na mimi niwe na furaha na mpenzi wangu.
Hatimae muda ulienda marafiki hao waliamua kuondoka wakarudi nyumbani.
Usiku Sophia alikuwa kakaa na kikombe cha kahawa huku akiwa mbali kimawazo , alikuwa akikumbuka jinsi alivyokuwa karibu na Shamte, jinsi alivyokuwa akimkumbatia kama vile anaogopa kumbe ilikuwa makusu alikuwa anaweza sana kuogelea alikuwa anataka kuwa karibu na Shamte kwani kuna hisia flani alikuwa anazipata juu yake.
Shamsa alimfuata alipokaa wakawa wanaongea.
" Umecheza sana kwenye maji mpaka mafua yamekubana.
" Ndio nime enjoy sana kuogelea kwenye kina kirefu Shamte ni hodari sana kwenye kuogelea.
" Ni kweli huwa anapenda sana kuogelea hasa kwenye kina kirefu.
"Hata mimi napenda sana. Shamsa hivi mna mpango gani na Shamte?
" Mpango kuhusu nini?
"Namaanisha hatima ya mapenzi yenu ni ipi?
"Sijajua kwakweli mimi nipo nipo nae tu .
Sophia alicheka.
" Unamaana humpendi au yeye hakupenda?
" Kwa upande wake bado sijamuelewa . Vipi wewe na Nassir?
" Tunampango wa kuchumbiana hivi karibuni.
" Waooo hongera sana umepata mwanaume mwenye msimamo huwa napenda sana maamuzi ya Nassir huwa sio mbabaifu.
Waliongea mawili matatu baada ya hapo kila mmoja alienda chumbani kwake kupumzika.
Kadri siku zilivyokuwa zinaenda ndivyo Sophia alikuwa akimtega Shamte, Shamte alielewa lakini ilikuwa ngumu sana kwake kumsaliti rafiki yake kipenzi Nassir hivyo kuna muda alijifanya haoni na kuja wakati alimlaani shetani.
Siku moja Sophia alimshauri Shamsa awafanyie surprise wapenzi wao waende nyumbani kwao wakaandae chakula kizuri.
" Sophia labda tukafanye kwaajili yako mimi sina imani na yule kichaa wangu naweza kuhangaika kwa juhudi zangu zote kumbe akitoka kazini anaenda kwa Aisha.
" Usifikie hivyo bwana , nitafanya kitu lazima Shamte atarudi mapema.
" Sawa.
Walikubaliana wakaenda nyumbani kwa wapenzi wao jambo la kwanza wakiingia vyumbani na kufanya usafi pamoja na kuviomba vyumba vyao walipomaliza walihamia jikoni kuandaa chakula .
Muda ulienda Shamte na Nassir walirudi nyumbani na kila mmoja alipokelewa na mpenzi wake wakaenda chumbani wakaona baada ya hapo wote walikutana mezani wakawa wanakula. Sophia alionekana kumuangalia sana Shamte , kuna muda Shamte alimuangalia na Sophia walimfanyia jicho na Shamte aliangalia pembeni. Sophia hakuishia hapo alitembezwa vidole vya miguu yake Shamte.
" Eeee Mungu wangu nipe uvumilivu. Mbona huyu Sophia anataka nifanye kitu cha ajabu ikiwa mimi sitaki kumsaliti rafiki yangu.
Sophia hakukoma kumsumbua Shamte alichokaa kuvumilia akaona bora anyanyuke.
" Baby nakuja naenda uwani mara moja.
Shamte aliondoka pale na muda huo huo Sophia alinyanyuka akadai anaenda jikoni kuongeza mboga .
Sophia alienda jikoni akaweka bakuli jikoni kisha akaenda kumtafuta Shamte , alienda mpaka chumbani kwa Shamte akamkuta kasimama dirishani anamchungulia nje. Sophia akinyata na kumkumbatia kwa nyuma kwa akili ya haraka Shamte alijua ni Shamsa alikidhika mikono ya Sophia na kuipapasa.
" Inamaana umenikipia si ndio?
Shamte alishitushwa na sauti ya Sophia akatoa mikono ya Sophia na kusogea pembeni.
MPENZI WAKO NI MKE WANGU 4
MTUNZI SMILE SHINE
Sophia akitabasamu na kumsogelea karibu kabisa na alipokuwa amesimama.
" Unaogopa nini sasa?
" Sophia unafanya nini chumbani kwangu?
" Nipo hapa kwaajili yako Shamte , hivi kwanini unajifanya huelewi kitu wakati wewe ni mtu mzima , au unataka nitamke kwa mdomo kuwa nataka kitu fulani kutoka kwako?
" Sophia unajua nakuheshimu sana acha mara moja hiyo michezo yako.
" Najua unaniheshimu na mimi nakuheshimu pia ila kuna jambo nilikuwa naomba kutoka kwako.
" Jambo gani?
" Shamte nimegundua kuwa wewe ndio ulikuwa mwanaume sahihi kwangu na sio Nassir nilimkosea sana kufanya maamuzi.....
" Unasemaje wewe? Nia yako ni nini kwangu? Hujui kuwa Nassir ni rafiki yangu tena ni zaidi ya rafiki pia mwanamke wangu ni rafiki yako kipenzi.
" Najua humpendi Shamsa.
" Una uhakika gani kuwa simpendi.
" Ungekuwa unampenda usingetoa na wanawake wengine au inamaana kuwa haujapata unachotaka ndio maana bado anahangaika na wanawake huko nje? Shamte mimi naweza kukutuliza , nikakupa unachotaka na ukaridhia kabisa.
" Acha kuichanganya akili yangu nimesema kaa mbali na mimi wewe ni shemeji kwangu na upande mwingine na kuchukulia kama rafiki wa kawaida tu na kama ulikuwa unafikiria simpendi Shamsa basi umekosea, Shamsa ana nafasi kubwa kwangu na huku kutoka na wanawake wengine sio sababu kuwa simpendi.
" Basi Shamsa bado hajajua kushika na kuudhibiti kuwapo faragha ila mimi kwangu haitajutia nitahakikisha unaridhia .
Shamte alimuangalia Sophia bila kujibu kitu.
" Hii sio sehemu sahihi naomba tupange muda tuongee vizuri . Sophia alimsogelea na kumbusu shavuni kisha akarudi nyuma huku akitabasamu alafu akatoka nje ya kile chumba na kumuacha Shamte kasimama kama vile mtu alieganda.
" Sophia anataka kufanya nini jamani mbona anataka kuamsha vita ya pili ya dunia, mtu mwenyewe najijua sipigiwi nacheza sasa inakuwaje nikipigiwa , Sophia, Sophia umedhamiria kufanya nini wewe binti.
Shamte aliwaza akawazua baada ya hapo alirudi kwenda kuungana na wenzie.
Siku zilienda Sophia na Shamte walikuwa wakiwasiliana kwenye simu usiku walitumia na msg za mahaba . Sophia akijua sana kucheza na akili ya Shamte maneno aliyokuwa akiongea au kumuandikia kwenye msg yalikuwa yanaamsha hisia zake.
Mwisho wa siku Shamte alishindwa kuvumilia akiomba wakutane . Kwa upande wa Sophia ilikuwa ni furaha pia kwani alijua alilitaka linaenda kutumia kwani kukutana na Shamte halitaweza kumuacha salama .
Siku hiyo walikutana hotelini wakapata chakula pamoja.
" Niambie mrembo hivi ni kweli unahitaji penzi langu?
" Haswaaa nakuhitaji sana Shamte.
" Vipi kuhusu Nassir?
" Shamte naomba unapokaa na mimi usiwataje hao watu wawili tuongee kuhusu mimi na wewe.
Shamte aliachia tabasamu kisha akasema
" Sawa malkia, sasa unaonaje leo ikawa siku rasmi kwetu?
" Sawa hata mimi nilisubiri sana siku kama hii.
" Basi ngoja nikachukua chumba.
" Sawa.
Shamte alinyanyuka anaelekea mapokezi kuchukua chumba baada ya hapo alirudi kwa Sophia akamchukua wakaongozana mpaka kwenye chumba cha hoteli, huko kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzie hakuna aliyetaka kusubiri kila mmoja alionyesha ujuzi wake.
Siku hiyo wakinogewa na kila mmoja alimsifia mwenzie kwa kuwa hodari.
" Sikujua kama unaweza kiasi hiki, laiti ningejua nisinge ruhusu Nassir akuchukue.
" Hata hivyo bado haujachelewa nafasi unayo.
" Tunafanyaje ikiwa tayari ananipangia kukuposa?
"Mmmmh palipo na nia hawakosi njia kama tukirudhiana basi tutajua nini cha kufanya.
Shamte alicheka kisha akamkumbatia na mechi ikaanza upya.
Ilifika majira ya saa tatu usiku Sophia hakurudi nyumbani na wala hakupatikana kwenye simu na kwa upande wa Shamte ilikuwa hivyo hivyo lakini Shamsa hakujali sana kuhusu Shamte kwasababu ni kawaida yake mara nyingi akiwa kwenye mambo yake huwa hapokei simu na wala hapokei.
Kwa upande wa Nassari ilikuwa ni shida mara kwa mara alimpigia Sophia alipoona hapati alimpigia Shamsa.
" Shamsa hivi huyu mtu yupo hapo?
" Hapana hayupo nyumbani na simu yake hapatikani.
" Unajua anaweza akawa yuko wapi?
" Kwakweli hakuniaga na sio kawaida yake kufanya hivi.
" Hilo ndio linalompa wasiwasi.
" Usijali itakuwa yupo mbali kidogo na simu yake imeisha chaji si unajua yule ni mama wa mishemishe.
" Sawa shemeji. Shamsa alimtoa wasiwasi japokuwa nae alikuwa na wasiwasi.
Muda ulizidi kwenda bado wakawa hawapatikani.
Siku hiyo Shamte na Sophia walilala hotelini kulipokucha Shamte akijiandaa na kuelekea kazini na Sophia alirudi nyumbani akamkuta Shamsa yupo nje anamwagilia mauwa.
" Hallow baby!
" Hi.
" Vipi uko poa? Sophia alionekana kuchangamka kuliko kawaida.
" Niko poa, vipi mwenzetu ulikuwa wapi na ililala wapi?
" Nilikuwa kwa mpenzi wangu.
Shamsa alimuangalia na kumsogelea karibu alimuangalia sehemu za shingoni aliona love bite.
" Sophia ulikuwa kwa mpenzi wako yupi?
" Kwani nina wapenzi wangapi?
" Najua ni mmoja lakini najua hukuwa nae jana alikuwa akitafuta sana mpaka kupelekea kukosa usingizi.
Sophia aliona siri yake imefichua akabaki kutabasamu.
" Sophia unamaana kuna mwanaume mwingine mbali na Nassari?
" Hebu iwe siri yako nitakueleza hili badae maana sasa hivi nimechoka sana ficha ya kuwa mwili wangu umekuwa mwepesi.
Alisema Sophia alafu akaingia ndani. Shamsa alitingisha kichwa kwa kusikitika.
" Anakosa nini kwa Nassir mpaka anaamua kumsaliti?
Shamsa aliachana naye akaendelea kumwagilia mauwa.
Sophia akiwa chumba kwake aliamua kuwasha simu yake na mtu wa kwanza kumtafuta alikuwa Shamte alimtumia msg kumwambia.
" Shamte niruhusu nikuote mpenzi umenipapawisha mpaka hapa nilipo sijielewi najilaumu sana kwa kukosa tangua mwanzo, ila nina imani itanipa nafasi kwenye moyo wako na mimi nifurahi penzi lako kwaajili ya furaha yangu nipo tayari kuwa nafasi ya pili kwako.
Msg ilimfikia Shamte akisoma huku akitabasamu baada ya hapo alijibu.
" Naanzaje kukataa ombi lako tamu yangu, kuna mengi nimeona kwako na sitaki kuyakosa nakupenda na mwenyewe unajua kuwa nakupenda.
Sophia alisoma msg kutoka kwa Shamte akajikuta anapiga kelele za furaha huku akigaragara kitandani.
Shamsa alisikia zile kelele akatoka mbio na kwenda chumbani kwa Sophia akamkuta akigaragara kitandani kwa furaha.
" Una shida gani ?
" Shamsa unajua mwenzio nilikuwa nipo nipo tu sikuwahi kujua kama kuna wanaume wanaja mapenzi mpaka kupelekea akili ya mtu kuhama , hivi kwanini watu mna siri nzito huwa haniambii wenzenu jinsi mnavyofurahia mapenzi pindi anapokuwa faragha na wapenzi wenu?
MPENZI WAKO NI MKE WANGU 5
MTUNZI SMILE SHINE
Shamsa alisimama akawa anamuangalia huku akitingisha kichwa maana Sophia alikuwa kama mtu aliechizika na mapenzi.
" Unajua tangia umekuja sikuelewi kabisa kwanza una furaha kupitiliza ,pili maneno yako siyaelewi kabisa.
" Utanielewa tu my dear kuwa mpole.
" Labda nitakuwa mpole kama utaniambia sababu ya wewe kuchangamka hivyo.
" Haya mambo hayataki haraka kipenzi mbona utaelewa taratibu. Ila tambua kuwa kuna wanaume wameandikiwa wanajua mapenzi wanajua mahaba yani sijui niseme nini.
" Sophia unamsaliti Nassir?
" Hapana ila nilienda kujaribu nje ili nipate radha tofauti na kweli nimeona hiyo radha ya vanilla.
" Hicho unachofanya sio sawa Sophia unafikiri Nassir akijua atajisikiaje wakati unajua anakupenda na kukiamini pia.
" Ajue aambiwe na nani? Kama atajua basi atakuwa kaambiwa na wewe.
" Siwezi kwenda kumwambia huo ujinga ila unatakiwa kujirekebisha.
" Shamsa wewe upo nyuma sana ndio maana Shamte huwa anatoka na wanawake wengine changamka ujue raha zilivyo.
" Siwezi kufanya hivyo......
Wakiwa wanaendelea kuongea mara simu ya Sophia ilianza kuita ,aliangalia na kuona Nassir alikuwa anapiga.
" Sitamani hata kupokea simu yake.
" Kwasababu gani?
" Sitamani kujibu maswali ambayo sina majibu yake.
" Sophia acha ujinga pokea simu unajua mwenzio tangia jana usiku alikuwa na wasiwasi, hakuwa na amani kwaajili yako.
Baada ya kuambiwa hivyo na Shamsa ndipo Sophia akaamua kupokea simu.
" Hallow. Aliongea kama vile analazimishwa.
" Vipi baby upo sawa kweli?
" Yes nipo sawa.
" Mbona jana ulikuwa hupatikani na haukuwepo nyumbani ulikuwa wapi?
" Nilienda kuwasalimu wazazi lakini nimesharudi nipo hapa nyumbani.
" Sawa ila Uliniweka roho juu kwenye simu sikupata.
" Simu haikuwa na chaji.
"Basi kama upo salama ni heri nilitaka kujua hilo na jioni nitapita kuja kukuona.
" Sawa.
Siku zilizidi kwenda mapenzi ya siri kati ya Sophia na Shamte yaliendelea bila Nassir na Shamsa kugundua chochote.
Waliendelea kutoka pamoja kama zamani lakini kuna wakati Sophia alikuwa akihisi wivu aliona kama Shamsa anafaidi sana kuwa na Shamte.
Siku moja walikuwa wametoka pamoja kwaajili ya kupata chakula cha jioni , Shamsa wakati anakula alijimwagia mchuzi kidogo Shamte alichukua kitambaa akawa anamfuta kile kitendo kilimkasirisha Sophia alimuangalua Shamsa kwa hasira, alishindwa kuvumilia kuona vile alinyanyuka akaenda pembeni na kumtumia msg Shamte.
" Inachokifanya sijaipenda kabisa hata kama mnapendana sio umuonyeshe mbele yangu.
Shamte alisoma ule ujumbe kisha akarudisha simu mfukoni na kuendelea kula. Sophia alirudi akakaa lakini hakuwa na furaha kama mwanzo.
Baada ,a kumaliza kupata chakula Shamte alisema kitu.
" Hivi mnaonaje leo tukaenda kulala nyumbani kwetu?
" Hiyo itakuwa nzuri au unasemaje baby. Nassir alisalia bila kujua akili ya Shamte ilikuwa imewaza nini.
Walivyokubaliana waliondoka pale hotelini wakaenda nyumbani kwao na kila mmoja aliingia chumbani na mpenzi wake.
Nassir alimshika Sophia na kumtaka walale lakini Sophia alionekana kuwa hayupo tayari kwa hilo zoezi.
" Leo una nini baby mbona kama unanikataa?
" Leo sijisikii vizuri na sipo tayari kufanya chochote.
Nassir hakutaka kulazimisha alimpa pole kisha akamvuta na kumkumbatia.
Sophia alipoona Nassir kapitiwa na usingizi alitoka pale chumbani akiwa kashika simu yake mkononi akiwa kwenye korido alituma messege kwa Shamte.
" Njoo sebleni.
Alienda kukaa sebleni kukiwa na giza akimsubiri. Baada ya sekunde chache Shamte alitoka akiwa kavaa boksa tu.
" Vipi?
" Nakuhitaji Shamte nimeshindwa kufanya chochote na Nassir kwasababu nakuhitaji wewe.
" Sawa lakini kwa huu muda haifai wanaweza wakatoka.
" Siwezi kujizuia liwalo na liwe.
Sophia akimng'ang'ania Shamte mpaka Shamte akaamua kumpa kile alichohitaji. Walipomaliza Shamte alivaa nguo yake na kutaka kuondoka lakini kabla hajafanya hivyo Sophia alimtaka na kumvutia kwake.
" Unataka nini tena? Shamte aliuliza.
" Shamte nimejitoa kwako kwahiyo kuwa makini na moyo wangu.
Shamte alimpiga busu kwenye paji la uso kisha akatoa mikono ya Sophia mwilini mwake ile anataka kugeuka aondoke taa za sebleni zikawashwa.
Ilikuwa bahati Shamte aliwahi kuinama na kwenda kujificha nyuma ya kochi.
Nassir alijitokeza akamuona Sophia kasimama sebleni
" Baby mbona uko huku unafanya nini huku tena kwenye giza.
" Aaaaa .... Unajua sijisikii vizuri nilikuja kunywa maji na pia sikuwa na usingizi nikaamua kuja kukaa huku. Sophia alijikanyaga kanyaga hakutoa maelezo yaliyonyooka.
" Kwanini hukuniambia mpenzi wangu kuwa unakuja huku .
" Sikutaka kujisumbua najua umechoshwa na wagonjwa huko hospitali.
" Lakini na wewe ni muhimu sana una nafasi yako kwangu utakacho nipo tayari kufanya. Basi acha niwaache TV tuangalie.
Alisema Nassir huku alisogea ilipo TV na ilikuwa akienda huko kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kumuona Shamte.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote