MOYO WANGU UNADUNDA KWAAJILI YAKO ( EVELYN)
Ni simulizi inayowahusu mabinti wawili mapacha Regina na Evelyn
Regina ni kulwa na Evelyn ni doto
Wasichana Hawa wawili walifanana Sana ni vitu vichache tu viliwafanya watofautiane .
Evelyn alichukua akili za baba yao Mr Wilson ambae ni dactari bingwa ila Kwa upande wa Regina yeye hakuwa vizuri kwenye mambo ya masomo na alikuwa mpole , mtaratibu na alikuwa na heshima sana
Kwa upande wa Evelyn yeye ilikuwa ni kinyume na mwenzie alikuwa machepele sana na wakati mwingine hakujali anaongea na nani aliongea anachona yeye kinafaa .
Licha ya kutofautina ki tabia Regina na Evelyn walipendana sana Kila sehemu walienda pamoja na wakati mwingine walivaa nguo za kufanana.
Siku Moja baba Yao aliwaita wanae na kuwaelezea habari njema kuwa kijana wa rafiki yake wa zamani Mr zimbwe anaeitwa Isaac alitakiwa kumuoa Regina
Na kipindi hicho Regina Alizama penzini na kijana aliyeitwa Francis
Kuondokana na ndoa ya bila upendo Regina apanga mpango na pacha wake Evelyn aende kukutana na Isaac Kwa niaba yake
Evelyn kwasababu ya upendo kwa pacha wake alikubali na kwenda kukutana na Isaac kijana mtanashati na ceo wa kampuni ya Double T
akiwa na lengo la kumfanyia vituko Ili akatae kumuoa Regina
Evelyn alijitahidi sana kufanya Kil awezavyo kumkwaza Isaac lakini badala yake Isaac kukasirishwa na tabia yake ajatokea kumpenda Evelyn akijua ndo Regina binti anayetakiwa kufunga nae ndoa .
Upendo aliokuwa akiuonyesha Isaa inabadilisha mawazo ya evelny, Evelny anatokea kuvutiwa na Isaack
Penzi Lilinoga mpaka Evelyn akapata ujauzito wa Isaac .
Je itakuwaje Isaac akijua ukweli kuwa yule aliyekuwa anakutana nae ni Evelyn na sio Regina
Na vipi kwa upande wa wazazi watalipokeaje Hilo suala
MOYO WANGU UNADUNDA KWAAJILI YAKO ( EVELYN)
MTUNZI SMILE SHINE
EP : 1
Katika familia ya bwana Wilson na bibi Neema walibarikiwa kupata watoto mapacha wakike wawili waliofanana sana Regina na Evelyn.
walikuwa ni mabinti wa miaka 23, tofauti Yao ilikuwa Moja Regina alikuwa mnene kidogo kwa mwenzie na mpole tofauti na Evelyn aliyekuwa mcharuko ,mwembamba na wote walibarikiwa kuwa na shepu nzuri
" Regina unalala sana embu amka basi kuna sehemu nataka unipeleke "
Evelyn alimuamsha Regina kwa fujo
" Evelyn jifunze kuwa mstaarabu Yani wewe ndo mwenye shida badala uniombe vizuri unanilazimisha Mimi nimechoka bhana nahitaji kupumzika "
alilalamika Regina Kisha alirudi kulala
" Mamaa we mamaa umemuona Regina alivyo "
Evelyn alimuita mama yake kwa sauti Kali
" Kafanya Nini Tena wewe Kila siku kumshtakia mwenzio na wewe ndo mkorofi lione "
alisema bi Neema hata kabla ya kumsikiliza Evelyn kwani anawajua vizuri watoto wake
" Anhaaa unamtetea sawa naenda kusema kwa Dady"
alitishia Evelyn
" Unamtisha nani embu tupishe hapa "
bi Neema aliamua kuondoka zake baada ya kuona hakuna cha maana alichoitiwa Evelyn alirudi chumbani kwa Regina akiwa anapiga simu sehemu simu ilivyopokelewa tu akaanza kulia
" Dady najua upo busy sana lakini Regina amelala mpaka saizi na hataki kunisindikiza kununua nguo kwaajili ya interview yangu ya kesho kutwa Sasa Mimi nitaenda na nani Dady na nimeshazoea kwenda nae Kila sehemu "
Evelyn aliendelea kujiliza
" Usilie mwanangu kipenzi embu fanya kumuamsha huyo Regina umpe simu niongee nae "
alisema Mr Wilson
" Okay Dady , Regina Dady anataka kuongea na wewe "
Evelyn alimuamsha Regina Kisha akampatia Ile simu
" Shkamoo Dady "
alisalimia Regina kwa sauti ya uchovu sana
" Marahaba unalala Nini mpaka saizi jiandae haraka umsindike mwenzio madukani akanunue nguo kwaajili ya interview yake ya kesho kutwa au hutaki mwenzio apate kazi?"
Aliuliza Mr Wilson
"Sio hivyo Dady nitampeleka Sasa ivi "
Regina alikata simu akampa Evelyn
" Kikowapi nilijua tu Kwa amri Moja tu ya Dady lazima utanipeleka tu "
Evelyn alimzomea Regina akaondoka
" Huyu mpuuzi nguo si kanunua Jana anabahati sijamsemea"
Regina alinyanyuka pale kitandani akaingia bafuni
Evelyn na Regina walitofautia uwezo wa kufaulu darasani , Evelyn alifuata nyayo za baba Yao ambae ni dactari wa mambo ya moyo , Evelyn alikuwa ni mwepesi sana na alikuwa na ufaulu wa juu mara zote na kwa upande wa Regina Kila siku alikuwa mtu wa kufeli alijitahidi hivyo hivyo mpaka kuishia form 6 napo alitoka na 4 hakutaka kujishughurisha Tena na mambo ya elimu aliamua kufuata ndoto zake alifungua salon kubwa na duka la nguo baada ya kupewa mtaji na baba yao Mr Wilson
" Weee Regina tunachelewa bhana unaoga mwaka mzima "
Evelyn alienda kumgongea Regina bafuni
"Nakuja kwani mpaka uniharakishe hivyo lakini "
Regina alitoka bafuni akavaa gauni lake refu mpaka chini alipendeza sana lakini Evelyn alimuangalia kama kaona kituko
"Badilisha bhana nguo Gani Sasa iyoo embu nipishe nikuchagulie mwenyewe"
Evelyn alienda kabatini kwa Regina alimchagulia suruali , kitop na ki shati cha shifon
" Tunaenda wapi kwani ?"
Aliuliza Regina
" Vaa hizi wewe utaona huko mbele ya safari tunapoelekea "
Regina hakuwa mbishi alivaa zile nguo alizopewa na pacha wake
" Wow umetokelezea Yani ungekuwa sio uo mwili wako nakuhakikishia tungetikisa huu mji twende zetu "
walikuwa wamevaa nguo za kufanana ,Evelyn alimshika Regina mkono wakatoka
" Mom sisi tunatoka tutachelewa kidogo kurudi "
Evelyn aliongea kwa mapozi kama kawaida yake
" Loooh mpaka ukamuamsha mwenzio mtoto una balaa wewe huwezi kumuacha mwenzio apumzike , nendeni lakini mkitoka mjue na muda wa kurudi "
alisema bi Neema
" Sawa mama tutawahi kurudi Wala usijali "
alijibu Regina walimkiss mama Yao kwenye mashavu wakaondoka
" Lucas ...Lucas "
Evelyn alimuita Lucas ambae ni dereva wao
" Naam "
" Ulikuwa wapi mpaka Koo langu linakauka kwa kuita ndo unajileta "
Lucas alinyamaza kimya kwani ameshazoea kelele za Evelyn
" Eve embu kuwa mstaarabu hata kidogo hili neno Huwa nakwambia Kila siku lakini Wala hulizingatii hata kidogo "
alisema Regina
" Bibi weee embu niache , Lucas naomba funguo ya gari Leo tunaendesha wenyewe "
alisema Evelyn
" Hii hapa "
Lucas aliwapatia funguo akaenda kukaa na mlinzi Regina na Evelyn Walipanda kwenye gari na kuondoka walifika mpaka kwenye jumba Moja la kifahari
" Nilijua tu huna lolote ulikuwa unataka tu kuja kwa mpenzi wako "
" Leo ni birthday ya mpenzi wangu Adrian naanzaje kukosa siku yake muhimu kama hii ya Leo "
Evelyn alifungua mlango alishuka na kuanza kuingia ndani Regina nae alimfuata nyuma
" Mbona kupo kimya hivi "
aliuliza Regina
" Sijui nahis... ngoja kwanza hizo sauti zinatokea wapi? "
Evelyn alielekea upande wa vyumba alifungua chumba cha Adrian hakuamini macho yake alimkuta Adrian akiwa na mwanamke mwingine kitandani
" Mungu wangu "
Regina alishtuka
" Adrian huu ni ujinga Gani ?"
Aliuliza Evelyn
" Mmm huyu ndo mwanamke wa maisha yangu Evelyn kwako nilikuwa tu napoteza muda kwanza unanuka shida tupu, unaweza kwenda usituharibie starehe zetu "
Adrian aliongea kwa dharau
" Hahahah unanichekesha ujue umesemaje labda sijakusiia vizuri "
Evelyn alianza kuwasogelea pale kitandani alinyanyua chupa ya mvinyo alitaka kumpiga nayo Adrian lakini Regina alimuwahi akamzuia
" Usifanye hivyo eve punguza hasira yeye ndo aliyekupoteza wewe Kwa ujinga wake utapata mwingine aliye Bora kuliko huyu na fikilia mara mbili ukifanya tukio kama Hilo wazazi wetu watajisikiaje ,tuondoke "
Regina alimshika mkono Evelyn wakatoka nje
" Nawezaje kuondoka kirahisi hivi nataka kumpiga hata kibao nitajisikia vizuri "
alisema Evelyn
" Kuna njia Moja tu na utafurahi "
Jioni kulikuwa kuna part kwenye lile jumba Regina na Evelyn walikuwa wanachungulia kwenye ukuta
" Wakati ndo huu twende kama tulivyopanga "
alisema Regina na Evelyn aliitikia kwa kichwa Waliruka ukuta wakaingia ndaniwalisogea mpaka eneo la tukio na muda huo ulikuwa ni muda wa kukata keki Evelyn na Regina walipiga hatua kwa pamoja Regina aliinamisha kichwa cha Adrian kwenye keki
Adrian alichafuka sana na muda huo huo Evelyn alimsukuma yule dada kwenye swimming pool
" Nyie ni kina nani ?"
aliuliza kaka mmoja rafiki wa Adrian
" Ni wakinaniani Tena kama sio wavamizi wa sherehe za watu masikini wakubwaa"
alijibu dada mmoja
" Dada koma nimevurugwa nisije nikahamishia hasira zangu kwako "
aliongea Evelyn huku anamnyooshea kidole yule dada
" Wewe si ni Evelyn "
kuna rafiki wa Adrian alimtambua Evelyn
" Ndiyo Mimi mwingine kopi "
" Piga simu polisi ,nitawapeleka polisi mmekuja kuharibu part yangu sito wasamehe kwa hili "
aliongea Adrian akiwa ameshikwa na wenzie mana alitaka kuwapiga Regina na Evelyn
" Pigeni huko polisi kwani tumewaambia tunaogopa "
Evelyn alimshika Regina mkono wakaondoka na hakuna aliyewagusa Walipanda kwenye gari na kuondoka walifika nyumbani kwao
" Mbona mmenywea hivyo tofauti na mlivyoondoka ?"
Aliuliza bi Neema
" Amna mama tumechoka tu "
Regina alimshika mkono Evelyn wakaenda chumbani
" Hataaa nawajua vizuri sana "
mama Yao alijua kutakuwa na shida maana mara zote wakiwa wanagombana anajua kabisa wako sawa nando upendo wao ulivyo, ila akiona tu wamekuwa karibu sana anajua kabisa kuna shida hapa
" Faith malizia kuandaa chakula nakuja Sasa ivi "
" Sawa mama "
faith alikuwa ni msaidizi wao wa kazi
Bi Neema alienda kusimama mlango wa chumba cha Evelyn akaanza kuwasikiliza
" Nikwambie kitu eve ukitaka kusahau Kila kitu kilichotokea basi ubadilishe mazingira unaonaje tukienda Zanzibar rafiki yangu swaumu yule uk alinipa hizi tiketi kama zawadi mana nilimdanganya Nina mchumba akasema Nika enjoy huko na hoteli ya kufikia pia alilipia"
Regina alitoa hizo ticket akamuonyesha Evelyn
" Hahaha "
Evelyn alianza kucheka
" Sasa unacheka nini ?" Aliuliza Regina
" Ama kweli sisi ni mapacha ukiachana na uwezo wa darasani Kila kitu tunafanana wewe ulimfumamia mpenzi wako na akakuita kibonge hahaha na Mimi Leo nimemfumania wakwangu "
aliongea Evelyn huku Hana mbavu kwa kucheka
" Sasa ndo unikumbushie machungu na Mimi mfyuu"
siku za nyuma Regina alikuwa mnene sana baada ya kuachana na mpenzi wake na kumtolea maneno makali kuwa Hataki wasichana wanene alianza kufanya mazoezi na alibaki na mwili wa wastani sio mnene Wala mwembamba sana ila alimzidi mwili Evelyn kidogo sana
" Ndiyo Ili tuumie wote "
aliongea Evelyn huku anacheka Na Regina alianza kucheka
MOYO WANGU UNADUNDA KWAAJILI YAKO ( EVELYN)
EP :2
"Ndiyo Ili tuumie wote "
aliongea Evelyn huku anacheka Na Regina alianza kucheka
" Hawa watoto mmmh "
bi Neema aliondoka akarudi jikoni Hatimae Siku ya interview ilifika
" leo ndo siku ya interview ?"
Aliuliza Mr Wilson
" Ndiyo Dady ni Leo hapa nakunywa chai haraka niondoke, Dady nataka kwenda na Regina "
Evelyn aliongea kwa sauti ya kudeka
" Regina utampeleka mwenzio akafanye interview"
alisema Mr Wilson
" Lakini Dady yeye ni mtu mzima si aende mwenyewe Mimi Nina kazi zangu za kufanya kwanza Leo natakiwa kwenda kupokea mzigo mpya bandarini"
alilalamika Regina
" Regina mpelekee mwenzio kwa Leo tu "
alisema bi Neema kwani alijua fika kilichomkuta Binti yake siku mbili zilizopita
" Sawa nitaenda nae "
baada ya kifungua kinywa Regina alimpeleka Evelyn mpaka kwenye kampuni aliyotakiwa kufanyiwa interviewKulikuwa kuna watu wengi sana walisubiri sana na hatimaye ilifika zamu ya Evelyn aliingia kwenye chumba cha interview na baada ya muda mfupi alitoka
" Twende nimeshamaliza "
" Majibu yanatoka lini ?" Aliuliza Regina
" Ulivyo na haraka ya hayo majibu utazani ni wewe ndo umefanya hiyo interview " alisema Evelyn
" Usiniambie kama hutaki niliuliza kwa wema tu "
" Ndo umenuna majibu ni baada ya week Moja "
" Sawa kwahiyo tutaenda Zanzibar kesho au hutaki kubadilisha mazingira ?"
Aliuliza Regina
" Nataka sana ,, twende tupitie huko bandarini ukafuatilie huo mzigo wako"
alisema Evelyn Walipanda kwenye gari wakaondoka Jioni waliwaaga wazazi wao kuwa wanaenda Zanzibar kutembea kwa siku Tano na wazazi wao walikubali
kesho yake mapema Walipanda boti ya kwenda Zanzibar na muda wa kama dakika 45 walikuwa wameshaingia bandari ya Zanzibar walifikia kwenye hoteli waliyolipiwa na swaumu rafiki wa Regina walipokelewa vizuri
" Wow nilijiona nimetembea sehemu zote nzuri lakini hapa pamenistajabisha Pako vizuri nimepapenda sana "
aliongea Evelyn huku anaagalia mawimbi ya bahari akiwa ghorofani
" Si nilikwambia Mimi utafurahia "
Regina alienda kusimama pembeni ya Evelyn wakifurahia mandhari nzuri
Regina na Evelyn walitembelea sehemu mbalimbali za vivutio zilizopo Zanzibar na walionekana kufurahia sana
Siku Moja Mida ya jioni Regina alimuomba Evelyn waende beach
" Evelyn twende beach basi tukatembee tembee na kuchezea maji kidogo "
" Mimi nimechoka bhana nenda mwenyewe kwa Leo "
Evelyn aliendelea kucheza game kwenye simu yake
" Okay"
Regina alitoka akaenda beach alikaa pembeni huku akiangalia mawimbi ya bahari na watu waliokuwa wakiogelea Wazo la kwenda kujaribu kuogelea likamjia alisimama na kuingia kwenye maji alienda kwenye maji marefu baada ya muda kidogo maji yalianza kumzidi akaanza kutapatapa ila bahati ilikuwa kwake kuna mkaka alimuona akaenda kumsaidia na kumtoa kwenye maji
" Upo sawa ?"
Aliuliza yule kaka ,Regina aliitikia kwa kichwa huku anahema kwa tabu
" Asante kaka angu sijui ingekuwaje kama usingekuja kuniokoa"
" Usiongee na uvute pumzi kwanza utakuwa sawa "
Regina alifanya kama alivyoambiwa walikaa kimya kwa muda mrefu huku wakiwa wanaangalia jua linavyozama upande wa baharini
" Naitwa Francis sijui mwenzangu unaitwa nani ?"
" Regina ndo Jina langu "
alijibu Regina huku anatabasamu
" Unajina zuri , Zanzibar sio nyumbani ?"
Aliuliza Francis
" Yeah ,umejuaje ?" Aliuliza Regina
" Haha nimehisi tu Kwa rafudhi yako na inaonekana umefikia hapa hotelini"
" Ni kweli nimefika hapa hotelini kwetu ni dar es salaam"
" Hata Mimi pia natokea dar es salaam , tunaweza kuwa marafiki ?"
Aliuliza Francis
" Ndio tunaweza kuwa marafiki "
walipiga story nyingi sana muda ulienda waliamua kubadirishana Namba na baada ya hapo Kila mmoja alienda kwenye chumba chake
" Mmmh ulipotea au mana nimesubiri mpaka nikakata tamaa nilijua utatumia dakika hata kumi tu utarudi"
alisema Evelyn
" Nilipata rafiki wewe si uligoma kwenda na Mimi "
Regina alijilaza kitandani
" Huyo rafiki yako anaitwa nani ?"
Evelyn aliuliza huku anakaa vizuri mana alimuona Regina anatabasamu
" Anaitwa Francis bhna "
"Mmmh haya bhana nataka nimuone huyo shemeji yangu "
aliongea Evelyn kwa utani
" Heee jamani Kawa shemeji tayari , nimekwambia ni rafiki tu Tena kaka wa watu yupo smart atakuwa tu tayari anampenzi "
" Kwahiyo umemuelewa si ndio ?"
Aliuliza Evelyn
" Aagh Mimi sijui bhana niache nipumzike kidogo "
mara Simu ya Regina ilianza kuingiza massage mfululizo kwa upande wa Whatsapp
Evelyn alichukua akaanza kusoma zile message
"Mkaamua kupiga na picha naoana hapa kakutumia "
"Mbona hatukupiga picha hizo picha zimetokea wapi embu tuone "
Regina alichukua simu yake na kuanza kuangalia alijikuta anatabasamu kumbe wakati wapo beach Francis alimpiga Regina picha kibao bila yeye kujua na zote zilitoka vizuri
Siku za kukaa pale hotelini ziliisha wakaondoka na kurudi nyumbani kwao na majibu ya interview ya Evelyn yalikuwa yametoka na alifanikiwa kupata kazi kwenye Ile kampuni ya OKING
" Hongera Sana Binti yangu hatimaye ndoto zako zitaenda kutimia "
alisema Mr Wilson
" Asante sana Dady "
" Hongera ndo ukatulie huko ufanye kazi mana nakujua mambo yako " alisema bi Neema
" Sawa mom nimekusikia nitakuwa nitakuwa Binti mzuri Kila nitakachoambia ni ndio boss "
" Ndo sio Kila kitu unchoambiwa unafanya wewe ni mtu mzima jiongeze "
alisema bi Neema ,
muda wote Regina alikuwa anawaangalia na kutabasamu tu
MOYO WANGU UNADUNDA KWAAJILI YAKO ( EVELYN)
EP : 3&4
Kesho yake asubuhi ya saa 12 Regina alienda kumuamsha Evelyn
" Eve Yani unaujasiri wa kulala mpaka saizi na huko kazi unataka nani aende "
Regina alimtingisha Evelyn
" Regina sijui likoje ndo unaniamshaje hivyo wenzio niache niendelee kulala kidogo "
Evelyn alivuta shuka akajifunika vizuri
" Siku ya kwanza tu kuripoti kazini unataka kuchelewa embu amka "
Evelyn alikurupuka akakaa kitandani
" Saa ngapi saizi ?" Evelyn alimuuliza Regina
" Saa 12 na nusu tangia saa 12 kamili nakuamsha wewe tu "
Evelyn alinyanyuka kwa spidi na kuingia bafuni alipiga mswaki na kuoga haraka alitoka bafuni akakuta Regina amemuandalia nguo
" Asante ndomana nakupendaga "
Evelyn alichukua nguo zake akavaa alichukua viatu na pochi yake alitoka mbio mbio mpka nje alimkuta Lucas anamsubiri kwenye gari alipanda safari ilianza Moja kwa Moja mpaka kwenye kampuni ya OKING
Bahati ilikuwa upande wake aliwahi kufika kabla ya bosi wake kufika
" Oops asanteh mungu "
Evelyn alikuwa anahema juu juu alikuja dada mmoja akamsalimia
" Habari za asubuhi , wewe ndo secretary mpya wa Mr kinyogori ?"
Aliuliza yule dada
" Salama ,ndiyo ni mimi "
" Sawa nifuate "
Evelyn alimfuata yule dada walienda mpaka kwenye ofisi Moja wakaingia
" Mimi naitwa Brandina nitakuwa na wewe kwa miezi mitatu mpaka utakapozoea vizuri kazi yako "
" Anha nashkuru kukufahamu Mimi niite Evelyn, wewe ndo secretary wa zamani wa Mr kinyogori nimesikia unaenda kusoma "
" Yeah naenda kujiendeleza ,tuachane na hayo twende kwenye kazi , hii hapa ni ipad yako nimekuandalia ratiba zote na mambo muhimu yote yanayomuhusu Mr kinyogori "
Brandina alimuelekeza Evelyn mambo mengi ya kufanya na Kila Kona ya Ile kampuni alimtembeza Ili ayajue mazingira vizuri
"Mmmh kamekuja Leo tu lakini kanavyojikuta Sasa na huyo Brandina wote ndo wale wale "
alisema msichana mmoja aliyeitwa Marge
"Umeona ee na Ile nguo ilivyombana anataka kumtega Mr kinyogori siku yake ya kwanza tu kazini umalaya tu unamsumbua mfyuuu "
alisema Doris rafiki na mfanyakazi mwenzie na Marge
"Ukiwa hapa kwenye hii kampuni usisikilize maneno ya watu ukiwa mzuri kuwazidi wao ni kosa ,ukipendeza ni kosa na ukiwa karibu na Mr kinyogori ni kosa kwahiyo Wala usiwajali hapa fanya kazi iliyokuleta maneno Yao yasikuumize "
Brandina alimwambia Evelyn
" Asante kwa maneno yako ya busara lakini hapa kwangu mbona wataongea mpaka midomo ikae upande Wala hawanikeri "
Brandina alicheka kwa maneno ya Evelyn
Baada ya kumtembeza kwenye kampuni waliamua kurudi ofisini
Brandina alipokea simu kutoka kwa ceo Mr kinyogori
" Sawa bosi anakuja Sasa ivi "
" Mr kinyogori anakuita ofisini kwake akikuuliza maswali mjibu kile unachokijua usimuogope"
" Sawa ngoja niende nikamsikilize"
Evelyn alisimama na kuelekea ofisini kwa ceo aligonga mlango akaruhusiwa kuingia
" Habari za mchana bosi "
Evelyn alisalimia kwa heshima
" Safi , karibu ukae "
Mr kinyogori alimuonyesha Evelyn sehemu ya kukaa na Evelyn alitii
" Mmmh Leo ni siku yako ya kwanza kazini najua umetoka chuoni tu na kujiunga na kampuni yetu huna uzoefu mkubwa kwahiyo Brandina atakuwa hapa kwa muda akikusaidia na sio ndo ubweteke no, nataka ujifunze mambo yote muhimu sitaki kupata tabu siku Brandina akiondoka sijui tumeelewana "
alisema Mr kinyogori
" Ndiyo boss nimekusikia na nimekuelewa vizuri tu usiwe na shaka juu ya Hilo "
aliongea Evelyn huku anatabasamu
" Vizuri nimependa kujiamini kwako natarajia ufanyaji kazi mzuri kutoka kwako unaweza kwenda Sasa "
"Asante boss "
Evelyn alifungua mlango na kutoka ofisini kwa Mr kinyogori
" Amekwambia Nini huko ?"
Aliuliza Brandina kama mtu mwenye shauku kubwa ya kutaka kujua
" Ameniambia nijifunze kwa bidii Ili siku ukiondoka asipate tabu kunielekeza na wakati Mimi ndo secretary wake "
" Anha kumbe ndo hivyo tu "
Evelyn aliinyakua simu ya Brandina akakimbia nayo aliangalia wallpaper ya juu aliona ni picha ya Brandina na Mr kinyogori na walionekana kama wapenzi
" Evelyn nipe bhana mbona upo hivyo "
Brandina alichukua simu yake kwa Evelyn
"Mmmh nilijua tu Mimi hua sikosei Niko vizuri sijui kwanini sikuwa mpelelezi "
aliongea Evelyn huku anacheka
" Umejuaje na wafanyakazi wote hakuna hata mmoja anaejua zaidi ya kuhisi tu na hawana ushahidi "
aliuliza Brandina
" Ulivyopokea simu kuongea nae uliongea kwa kasauti flani hivi ka kudeka na saizi nimetoka tu ofisini kwake umenidaka juu juu na niliona macho yako yanaonyesha kabisa una wivu "
Evelyn aliongea kwa sauti ya chini
" Ni kweli sisi ni wapenzi nimekuwa secretary wake kwa miaka mitano Sasa na uchumba wetu unamiaka miwili sitamani hata kuondoka "
Brandina aliongea kwa huzuni
"Kwani si umetaka mwenyewe kwenda kusoma , wewe nenda kasome ukirudi Mr wako unamkuta hapa hapa anakusubiri Mimi nitamlinda maana naona kuna mapaka shume wanammendea "
"Hahaha Evelyn bhana , sawa Mimi nakuamini nimetokea sana kukuamini na nakuchukulia kama mdogo wangu "
Ulipita mwezi mmoja Evelyn alikuwa ameshazoea kazi yake na Brandina alikuwa ameshaondoka
" Wow , upo vizuri umeniandalia ratiba zangu vizuri kabisa kweli nimeamini you are genius"
Mr kinyogori alimsifia Evelyn
" Asanteh boss nitaendelea kufanya kazi kwa bidii "
Regina akiwa kwenye duka lake la nguo alipokea simu kutoka kwa Francis
" Hallo , mrembo uko poa !"
" Niko poa za wewe best ?"
" Mimi nashkuru mzima kiasi "
" Kwanini mzima kiasi na sio sana kwani unaumwa ?"
Aliuliza Regina huku anakaa kwenye kiti
" Naumwa sipo sawa kabisa "
"Basi nenda hospital kwani hakuna mtu karibu hapo unipe simu niongee nae kama umezidiwa sana Ili akupeleke hospital "
" Amna haja nipo njiani naenda kumuona daktari wangu "
" Vizuri ukitoka huko hospital unimbie basi unasumbuliwa na Nini "
" Kinachonisumbua nakijua vizuri sana Regina na dactari wangu ni wewe "
" Mmmh ...."
Regina alikuwa haelewi kinachoendelea na kilichomchanganya zaidi alimuona mtu kama Francis amesimama kwenye lango kuu la duka lake
"Wewe ndo dactari wa moyo wangu utakaponipeleka Mimi naenda tu ukiamua kunipa tiba nikapona au ukiamua kuniacha nife ni uamuzi wako moyo wangu upo mikononi mwako Regina "
Francis aliongea huku anamsogelea Regina na simu yake bado ilikuwa sikioni , Francis alifika mpaka alipokuwa amesimama Regina akamshika mkono uliokuwa na simu aliichukua akaiweka mezani
" Regina wewe ni mtu mzima nadhani umenielewa ninachokimaanisha "
" Francis ndo kwanza tumekutana mwezi mmoja uliopita unajua mengi kuhusu Mimi na Mimi najua mengi kuhusu kwanzia kazi , familia na mengineyo lakini naona ni mapema sana kuwa pamoja na huenda hujanipenda Bali umenitamani tu "
aliongea Regina huku anaangalia chini
" Nope nakuapia Regina nakupenda kweli na sio kukutamani sio lazima unipe jibu Leo chukua muda wako lakini usinifanye ni subiri sana "
francis alinyanyua mkono wa Regina akaukiss kisha akaondoka
" Ooo mungu wangu mbona Francis ananipa wakati mgumu sitakiwi kumuwaza yeye kwa Sasa ngoja niendelee na Kazi zangu "
Jioni Regina na Evelyn wakiwa nyumbani Kila mmoja katoka kwenye kazi zake walikuwa wamekaa chumani Kila mmoja alikuwa busy kuchati
" Unachati na nani ?" Regina alimuuliza Evelyn
" We nae mpana mpka ujue , ni mpuuzi Mmoja tu wa pale ofisini kwetu anajishobokesha , na wewe unachati na nani ?"
Aliuliza Evelyn
" Nachati na Francis sijui hata nimjibu Nini ?"
" Kwani amekutongoza ?"
Evelyn alikuwa amejilaza kitandani alinyanyuka akakaa vizuri
" Ndiyo ila naogopa kumkubalia "
" Kwani wewe humpendi ?"
" Nampenda ila naogopa kuumizwa sitaki tena "
" Acha ujinga wewe kama unampenda unaogopa Nini ?unajitoa tu muhanga unamkubalia apoo , huenda Francis ndo rizki yako na mwanaume Bora ukimkataa leo unaweza kujutia baadae Shauri yako"
aliongea Evelyn huku anacheka
Muda huo huo Francis alianza kupiga baada ya kuona Regina hajibu message zake
" Anapigaa "
Regina aliitupa simu pembeni kama kaona mzimu
" Hii huyu wa wapi , Sasa Hadi kuongea nae unaogopa utazani mtoto wa darasa la pili na huenda wanakushinda "
Evelyn aliichukua Ile simu akapokea
" Regina mama mbona hujibu message zangu na upo online au ndo unachati na mpinzani wangu na anataka kunizidi kete "
aliongea Francis kwa kulalamika
Evelyn alikohoa kidogo
" Bwana Francis ni kweli unampenda Regina ?"
Aliuliza Evelyn
" kumbe ni eve , ndiyo nampenda sana Regina na siwezi kumuumiza najua anawasiwasi kuwa nitakuja kumuacha lakini Mimi siwezi kufanya kitu kama icho labda aje aniache yeye "
" Okay nimekuelewa na hata hivyo Regina pia anakupenda Sana tu ni uoga unamsumbua Sasa ole wako ni sikie umemcheat au umemkosea kwa namna yoyote Ile tutakula sahani Moja Mimi ni mkorofi Regina hakukwambia "
" Wewe Evelyn unaongea ujinga Gani embu nipe simu yangu "
Regina alichukua simu yake akaiweka sikioni alimsikia Francis anacheka
" Mpuuzie huyu akili zake anazijua mwenyewe "
Regina alikuwa anaongea huku anangata kucha
" Masikini weee Yani unaongea na mtu kwenye simu unan'gata kucha je ikiwa ana kwa ana sijui itakuwaje , ngoja niwaache muongee Mimi naendazangu chumani kwangu "
Evelyn alitoka akamuacha Regina anaongea na Francis
Regina na Francis walianza ukurasa wao mpya wa mapenzi ilipita miezi Saba wakiwa kwenye mahusiana na walipendana sana Francis alifikia kumtambulisha Regina kwa ndugu zake na wazazi wake walitokea kumpenda Sana Regina
Siku Moja Mr Wilson aliwaita mabinti zake pamoja na mkewe bi Neema
"Kuna jambo dogo nataka kuwaambia ni jambo la kheri na la furaha "
aliongea Mr Wilson huku anatabasamu
" Ni kuhusu Nini Dady "
alidakia Evelyn
" Sasa si usubiri baba yako amalize kuongea tabia mbaya tu"
bi Neema alifinya sikio la Evelyn
" Mama unaniumiza "
Evelyn alilalamika huku anashika sikio lake lililofinywa
" Ndo ukome "
alisema Regina akamzomea Evelyn
" Acheni ugomvi na mnisikilize Tena hili jambo linakuhusu sana wewe Regina "
aliongea Mr Wilson huku anamuangalia Regina
" Mimi Dady ?"
Regina alijinyooshea kidole
" Ndiyo wewe , mnamkumbuka Uncle zimbwe?"
Aliuliza Mr Wilson
" Ndiyo tunamkumbuka si yule alikuwaga anatuletea toys na chocolate na ndo mmiliki wa hospital ya st Joseph"
alijibu Evelyn
" Ndiyo huyo huyo ,sasa ana kijana wake anitwa Isaac hamjawahi kumuona alikuwa marekani kwa mama yake kwa Sasa amerudi Tanzania na anasimamia kampuni Yao inaitwa DOUBLE T , na Mr zimbwe amependekeza Regina ndo awe mke wa mtoto wake "aliongea Mr Wilson huku anatabasamu ni wazi alifurahia lile suala
" Dady kwanini Mimi na sio Evelyn ?"
" Heee huyu wa wapi umetajwa wewe uko usinirushie mpira "
Evelyn aliongea kwa kupayuka
" Wamemchagua Regina kwasababu anataka mkwe wake awe mama wa nyumbani anataka kupata wajukuu na wewe ndo huna kazi ya kuajiliwa umejiajiri mwenyewe kwa Evelyn haiwezekani "
" Kwani mume wangu ni lazima kijana wake aoe kwenye familia yetu si akamtafutie mke kwenye familia nyingine "
alisema bi Neema
" Umesahau Mr zimbwe alikotutoa bila yeye tusingekuwa na haya maisha huenda tungekuwa shamba huko tunalima "
alisema Mr Wilson
" Lakini Dady Mimi si ... "
Kabla regina hajamaliza alichotaka kuongea Mr Wilson alimkatisha
" Hakuna cha lakini hii ni amri kesho unatakiwa kwenda kuonana na Isaac na akikupenda tu wewe hauna chaguo ni ndoa tu "
alisema Mr Wilson Kisha akondoka
MOYO WANGU UNADUNDA KWAAJILI YAKO ( EVELYN)
EP :5
"Lakini Dady Mimi si ... "
Kabla regina hajamaliza alichotaka kuongea Mr Wilson alimkatisha
" Hakuna cha lakini hii ni amri kesho unatakiwa kwenda kuonana na Isaac na akikupenda tu wewe hauna chaguo ni ndoa tu "
alisema Mr Wilson Kisha akondoka
" mama ongea na Dady Mimi siwezi kwenda kukutana na huyo mwanaume "
Regina alimuomba mama yake
" Regina Mimi Sina cha kufanya kwasababu ni kweli Mr zimbwe ametusaidia sana nenda tu Binti yangu na ndoa sio jambo baya ni jambo la kherii "
bi Neema alinyanyuka akondoka pia na kuelekea chumbani
" Sasa kwanini hujamwambia mama kuwa una mchumba unataka kufanya Siri mpaka lini? "
aliuliza Evelyn
" Unazani baba atajali hata nikimwambia kuna mtu nampenda na yupo tayari kunioa ni lazima atasema tuachane na nikaolewe na huyo mwanaume sijui ndo Isaac"
" Basi usihuzunike sana twende chumbani ukalale tutajua cha kufanya hiyo kesho na nitajaribu kuongea na Dady"
Evelyn alimshika mkono Regina wakaenda chumbani muda wote Regina alionekana kuwa na mawazo sana
" Unawaza Nini Tena si nimeshakwambia nitaongea na Dady kesho kama atanisikikiza "
" Kuna wazo nimepata "
aliongea Regina huku anatabasamu
" Wazo Gani ?"
" Eve nenda wewe ukakutane na Isaac"
Regina aliongea huku ameshika mikono ya Evelyn
" Wewee harafu Ili iweje ?"
Aliuliza Evelyn
" Subiri basi nimalizie yeye si hatujui hata kama ameonyeshwa picha yangu lakini atashindwa kututofautisha kwahiyo ukifika kule mfanyie vituko vya Kila aina hakikisha anakataa kunioa please"
Regina alimuomba sana Evelyn
" Mimi siwezi kufanya hivyo kwanza Niko busy sana siku hizi"
" Umesahau Kila mara ulikuwa ukipata shida ni Mimi ndo nakusaidi unakumbuka nilipigwa na jiwe hapa kichwani kisa kukusaidia wewe na hapa unakumbuka nilikatwa na chupa baada ya wewe na shoga yako kugombania mwanaume "
Regina alikuwa anamuonyesha Evelyn sehemu zote alizoumia kwasababu yake Tena akiwa anamtetea
" Sawa nitaenda kukutana nae acha kunikumbusha huo upuuzi ,mmh Na malipo yangu yatakuwa ni Nini hapo au ndo kujitoa tu sadaka ?"
" Wewe unataka nikupe Nini ? Lakini usichague kitu ambacho Sina uwezo nacho "
alisema Regina
" Okay nataka unipe ruksa ya kuja kuchukua nguo yoyote ninayoitaka dukani kwako na saluni pia nitaenda buree "
" Sawa kama ni hivyo tu hakuna shida "
Regina alikubali kwani aliona bora iwe hivyo kuliko kutengana na Francis na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine
" Sasa itabidi uhakikishe muda wa kukutana iwe ni jioni muda wa Mimi kutoka kazini"
" Asante sana Evelyn "
Regina alienda kumkumbatia Evelyn
Kesho yake mida ya mchana Regina alimtumia Evelyn sehemu watakayokutana na Isaac pamoja na Namba ya simu ya Isaac
" Sehemu ya kukutana ni greenview hotel saa 12 jioni na Namba ya simu ya Isaac ni 0710......."
" Okay Sasa usirudishe hiyo miguu yako nyumbani mpaka nikwambie nimetoka kuonana nae "
" Sasa muda wote huo nitakaa wapi na biashara yangu nafunga saa 11 ?"
Aliuliza Regina
" Akaa jiongeze shoga si uende kwa Francis au mwambie mtoke mpaka ufundishwe"
" Hahaha sawa bhana "
Jioni Evelyn baada ya kutoka kazini alienda kubadirisha nguo dukani kwa Regina Kisha alienda greenview hotel
" Huyu sijui atakuwa kashafika au vipi ?"
Evelyn aliingia ndani ya Ile hoteli
" Samahani dada ulifanya booking ya meza mana meza zote zinawatu "
alisema muhudumu wa pale anaepokea wageni
"Mmmh hata sijui kama kunakufanya booking huyo alieniambia nikutane nae hapa naona bado hajafika "
" Jina lake ni nani ?"
Aliuliza muhudumu
" Isaac zimbwe "
" Oh samahani sana madam unaweza kuingia sikujua kama wewe ndo mgeni wa Mr Isaac nitakupeleka kwenye meza yenu "
yule muhudumu alimuongoza Evelyn mpka kwenye meza
" Yuko wapi Isaac ?"
" Hajafika bado msubiri kidogo tukuletee kinywaji Gani ?"
" Niletee wine "
Baada ya dakika chache muhudumu alirudi akiwa na glass ya wine
" Karibu "
muhudumu aliweka wine kwenye meza Evelyn alikuwa busy anamtumia message Regina
" Oya uyu boya wako hajafika mpaka saizi na Mimi nimechoka sana saa Moja kasoro hii naondoka Sasa ivi "
" Usiondoke subiri kidogo bhana au mtafute si nimekupa Namba yake "
" Afu kweli "
Evelyn aliweka Namba ya Isaac akaanza kuipiga Evelyn alishtuka simu inaita pembeni yake alinyanyua macho yake akamuona mwanaume amevalia suti ya rangi ya maruni ,alikuwa ni bonge Moja la handsome aliachia tabasamu akaikata Ile simu
" Wewe ndo miss Regina ?"
Aliuliza yule mwanaume
" Yeah ndo mimi bila shaka wewe ndo Isaac , karibu ukae "
Isaac alivuta kiti akaakaa Kisha alitoa business card yake na kumpatia Evelyn
" Hii ni business card yangu tuongee haraka nimechoka sana nataka kwenda nyumbani kupumzika " Isaac aliongea kwa dharau
Evelyn aliipokea Ile business card akaiangalia
" Mr Isaac zimbwe ceo wa kampuni ya Double T, ivi unaadabu hata kidogo ?"
Evelyn aliitupa Ile business card chini akaikanyaga na kiatu chake kirefu
Isaac aliiangalia business card yake inavyokanyagwa na Evelyn aliyemfahamu kwa Jina la regina
" Umeniweka hapa kwanzia saa 12 kamili ,umefika hata kuomba samahani umeshindwa na unasema kwamba unaharaka unahisi wewe tu ndo mtu pekee aliyekuwa busy kwenye hii Dunia ,nimeacha kazi zangu kuja hapa sijui unanielewa "
Evelyn aliongea kwa nyodo kama kawaida yake
" Okay tufanye hivi unataka nikulipe kiasi Gani kufidia muda wako "
Isaac aliongea kwa dharau huku anachezea Pete yake
" Kiasi chochote kitatosha "
Evelyn aliongea huku anamkazia macho Isaac
Isaac alimuita secretary wake akampatia cheki
" Hii inaitwa blank check jaza kiasi chochote unachokitaka na Mimi nitakupatia hua sionagi tabu kugawa pesa ndogo ndogo za kunywea maji "
Isaac alimpatia Evelyn Ile check
" Ooh jamani wewe kweli ni tajiri sana "
alisema Evelyn huku anaandika kwenye Ile check
" Mtanashati Na ni ndoto ya Kila mwanamke usisahau Hilo "
Isaac alijisifia mwenyewe
Evelyn alimaliza kuandika kwenye Ile check akasimama akaiweka Ile check mezani alinyanyua Glass ya wine akaimwagia Kisha alimsogelea Isaac akaibandika Ile karatasi kwenye paji lake la USO secretary wa Isaac alitaka kusogea Isaac alimuonyesha ishara asisogee pale
" Nenda kwenu ukapumzike na ujifunze adabu na baada ya kujifunza jinsi ya kuheshimu wengine utanipigia tukutane huenda nikakuonea huruma na kukubali kuolewa na wewe ".
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote