KIJAKAZI WA KUNIZALIA
Kuna watu wamechoshwa na maisha nyie, alafu Kuna sisi ambao umaskin unatusababisha tuingie kwenye mambo ambayo hatujayafikiria , kutokana na Hali ya mama yangu kuwa mbaya ilinibidi nitafute namna ya kumtibu ndipo nilipokutana na hii issue ya kumzalia tajiri Mmoja...
Haikuwa rahisi ila pesa za mahitaji ya mama yangu zilikuwa kubwa sana, kiasi kwamba ilibidi nikubali kumzalia huyo tajiri, aliweka mbegu zake maabara na nikapandikizwa na sikuwah kumuona, alilea mimba bila Mimi kumjua nilikuwa natumiwa pesa tu, kwa uangalizi wa daktar wake ambae alinipa hio dili...
Hatimae miezi tisa ikafika na wakat wa kujifungua ukafika, na kila mtu alijua nitazaa mtoto Mmoja, ila wakat najifingua nikajifungua mapacha, Mimi kama mama niliumia kumuacha mwanangu nikaomba sana nibaki na mtoto Mmoja..
Maisha yalienda mwisho nikaja kukutana na huyo tajiri bila kujua kuwa ndio baba wa wanangu na akatokea kuvutiwa na Mimi jemimah...
Unadhan ni ipi hatma yetu, Melvin loves me bila kujua he is my baby daddy
MELVIN ( MY BABY DADDY)💖 1
Ilikuwa majira ya saa nne asubuhi Jemima alikuwa anamazilia kufanya usafi nje ya nyumba yao Mara ghafla alisikia kishindo kikubwa kilitokea ndani aliacha kufanya kazi aliyokuwa anajifanya akakimbilia ndani. Alipofika sebleni alishituka baada ya kumuona mama Yake ameanguka na akiwa hajitambui alimsogelea karibu na kuanza kumuita
" Mama, mama hebu fumbua macho, umepatwa na Nini? Baada ya kuona mama Yake hajitingishi alipiga kelele majirani wakafika.
" Jamani nisaidieni mama yangu kaanguka. Majirani walifika na kuuliza
"Ilikuwaje mpaka aanguke?aliuliza jirani mmoja
" Sijui nilikuwa nje nikasikia kishindo.
" Basi tumuwahisheni hospital. Walimchukua mama Jemima na kumkimbiza hospital , huko alipokelewa na kuanza kufanyiwa vipimo huku jemima akiwa kakaa nje akisubiri doctor atoke wodini.
Baada ya dakika kadhaa doctor kutoka Jemima akamfuata
" Daktari tafadhali muokoe mama yangu” Jemima aliongea huku akilia .
"Hakuna tunachoweza kufanya , isipokuwa pesa za upasuaji wake na zinatakiwa kulipwa kisha atahudumiwa."
"Dokta hakuna jinsi naweza kuongeza hela kidogo mimi ni mhudumu tu" na sina sehemu ya kwenda kumuomba msaada" alilia kwa sauti.
"Pole sana Jemima, natamani sana ningesaidia" samahani sana" Daktari James alisema na kutoka nje ya wodi.
Jemima alidondoka chini huku akilia kwa uchungu maana hakuwa na jinsi aliona Ni jinsi gani anaenda kumpoteza mama yake kipenzi sababu tu Hana pesa za matibabu
"Nitapata wapi pesa kama hizo? Hakuna familia ya kunisaidia wala marafiki wa kutoa msaada"
alimtazama mama yake aliyepoteza fahamu akiwa amelala kitandani akiwa hajitambui. Jemima alimuangalia na kuzidisha kulia
"Mama, amka uniangalie mwanao nipo kwenye wakati mgumu Sana tafadhali usije ukaniacha Baki na mimi ...
James aliingia ofisini kwake na kukaa kwenye kiti chake kwa uchovu,
Alipumua akikumbuka jinsi Jemima alivyokuwa anatia huruma,
"Natamani sana kusaidia, alinong'ona
akafungua laptop yake iliyokuwa juu ya mezamara simu yake ikaita.
.
Aliangalia aliyekuwa anapiga ikawa ni rafiki yake mkubwa MELVIN Aliachia tabasamu dogo Kisha akapokea
" Hallow Leo naona Kama ajabu kunipigia simu mida hii?" James alisema kwa furaha
"Punguza ujinga James, kwani huwa Kuna mida ambaya natakiwa kupiga simu?
" Kwa hii baridi lazima ungekuwa umelala na kujifunika na blanget. Tuachane na hayo unaweza kuniambia kwanini umepiga simu muda huu?
"Khaaa swali gani Hilo kwani hujui sababu ya Mimi kupiga simu ,kwani juzi tuliongea Nini?
" Aiseee hivi Ni kweli umedhamilia kutafuta mchumba ?
" Achana na maswala aliyoongea mzee kuhusu mchumba Mimi nilikuwa naongelea kuhusu Ile safari tuliyopanga.
" Lakini mzee anataka uchumbie ,. Anataka kuona ulijali wako ulipo anataka mjukuu ...
"Tulia rafiki, unataka kunipa presha na hayo maswala ya mzee ???
"Nani anajali kuhusu wewe, unatakiwa kumrudhisha mzee wako , fanya kile anachotaka . James alicheka , Melvin alipoona James anamcheka aliamua kukata simu
" Melvin anatakiwa kubadilika aache utoto. Nitampata wapi mwanamke wa kumfanya ampende?
Wakati doctor James anafikiria uliingia ujumbe kwenye simu yake , ujumbe ulikuwa inatoka kwa Melvin.
James aliposoma ule ujumbe
Akili yake ilimwelekea Jemima Kisha akatabasamu
"Ndio, Jemima anaweza kufanya hili"
Natumai atakubali" aliongea Kisha akanyanyuka kuelekea wodini.
Alienda hadi wodini na kwa bahati nzuri alimkuta Jemima anataka kuondoka akamuita
"Jemima.
"Dokta, kuna tatizo?" Jemima aliuliza
“Hakuna tatizo Jemima badala yake nina ofa nzuri kwa ajili yako” alisema huku akitabasamu lilimchanganya Jemima.
"Ofa?? Ofa gani??
"Ni ofa ambayo itatoa pesa za kutosha kwa ajili ya upasuaji wa mama yako na chenchi itabaki" James alijibu na Jemima alimtolea macho maana ilikuwa Kama bahati iliyomshukia
"Kweli?
" Ndio
"nipo tayari kufanya lolote kumuokoa mama yangu” alisema Jemima huku akiushika mkono wa doctor James
"Lakini Hilo swala Ni gumu . Alisema doctor James kwa msisitizo huku akiwa kamtolea macho Jemima.
MELVIN ( MY BABY DADY) 💖 2
JEMIMA aliganda kwa muda wakawa wanaangaliana na doctor James.
" Ni ngumu Sana James alisema kwa kumsisitizo zaidi na kufanya Jemima aogope lakini akaona bora aulize kabla ya kukata tamaa.
" Unaweza kuniambia ugumu wake na ni kazi gani?
James alimsogelea karibu Kisha akaongea kwa sauti ya chini.
" Tunahitaji mwanamke wa kupandikiza mbegu za kiume yani wa kutuzalia mtoto. Jemima alishituka Kisha akasema
" Unata.. nifanye hivyo? Jemima alishikwa na kigugumizi
" Ndio. Je utaweza ? Jemima alizubaa huku akiwa anafikiria
" Hii Ni nafasi adimu Sana iliyonishukia Sina sehemu nyingine ya kupata pesa za matibabu ya mama kwanini nikatae hii ofa, acha nifanye kwaajili ya mama yangu kipenzi.
" Kana hutaweza tunaweza kuachana nalo.
" Hapana Nitafanya , nipo tayari. Jemima alikubari haraka haraka kitu ambacho James hakutegemea.
" Ni kweli umekubali na hautakuja kubadili maamuzi yako hapo badae?
" Ndio doctor nitafanya.
" Sawa nitakwenda kumjulisha muhusika. Jemima akaitikia kwa kichwa.
" Madam mama yangu atakuwa salama naahidi kuifanya hiyo kazi Tena kwa moyo mmoja. James alitabasamu Kisha akamshika begani
" Usijali atakuwa sawa.
" Sawa malipo yatakuwa baada ya muda gani?
" Ni baada ya wewe kupandikizwa utawewa pesa na kuhusu huduma utapata huduma zote kikubwa wewe Ni kubeba mimba na kuitunza vizuri
" Sawa doctor.
Baada ya kumaliza maongezi yao Dr James alirudi ofisini kwake na Jemima akaenda alipolala mama yake alimshika usoni na kusema
" Mama naenda kufanya Jambo ambalo sijakushirikisha Ila Sina jinsi natakiwa kufanya tu kwaajili yako mama. Natamani uamke tuongee na kucheka pamoja. Aliongea huku machozi yakitoka.
James alipofika ofisini kwake alimpigia simu Melvin.
" Unaweza ukanipa sababu za wewe kupiga simu?
" Hebu tulia , Kuna Jambo zuri nataka kukwambia.
" Mmmh niambie
" Nimepata mwanamke wa kukubebea ujauzito. Melvin alinyamaza mpaka James akaita
" Hallow Melvin
" Nipo unasema umepata mwanamke na amekubali?
" Ndio kakubali. Melvin alishusha pumzi alafu akaendelea kusema
" Vipi itafanyika lini Sasa?
" Tunatakiwa kufanya vipimo kwanza tujue siku zake za kushika ujauzito.
" Sawa anahitaji kiasi gani Cha pesa?
" Milioni 35
" Haina tatizo nipatie account number Yake ya bank ili niweze kumuingizia hizo pesa. Lakini hakikisha Ni mtu makini sitaki kutapeliwa. Alafu zingatia muonekano wa sura yake sitaki kuharibiwa mbegu yangu.
" Uhakika hawezi kutapeli na kwa urembo Ni mrembo sema Ni maisha yanemfubaza , Pia nadhani ingekuwa vizuri Kama ungekuja kuonana nae.
" Hiyo haina haja ikiwa umelidhika nae wewe basi atafaa .
Baada ya kukubaliana James alikata simu.
Kesho Yake Jemima alipoenda kumtembelea mama yake hospital alikutana na doctor James.
" Afadhali tumekutana mapema , kuhusu Lile swala tuliloongea unatakiwa kwenda kufanyiwa uchunguzi.
" Mimi nipo tayari doctor.
" Sawa nifuate. Jemima na doctor James walifuatana mpaka kwenye chumba kimoja ambako walikutana na doctor mmoja wa kike .
" Karibu Jemima unaweza kupanda kitandani tuanze kukufanyia vipimo. Yule doctor wa kike alisema na James alikuwa kasimama pembeni akiwaangalia.
Jemima alipanda kitandani akafanyiwa vipimo na kuonekana yupo sawa.
" Dr kila kitu kipo sawa na tuna bahat hata yai lake lipokaribu kupevuka.
" Safi Sana. Jemima alinyanyuka pale kitandani na kujiweka sawa.
" Samahani doctor vipi kuhusu mama yangu?
" Kesho mapema Sana atafanyiwa upasuaji maana pesa ninazo baada ya kutoka hapa nifuate ofisini kwangu.
" Sawa. Jemima alilidhishwa na jibu la doctor akatoka na kwenda wodini kwa mama yake baada ya hapo alienda kuonana na Dr James.
" Nimekuja doctor.
Doctor James alifungua drop ya meza yake akatoa mfuko na kuiweka juu ya meza alafu akaisogeza kwa Jemima.
" Hizo Ni pesa za malipo yako, tumeshakata pesa ya matibabu imebaki hiyo milioni kumi.
Jemima alihisi kuchanganyikiwa hakuwahi kushika Wala kumiliki kiasi kikubwa Cha pesa Kama hicho.
" Doctor mbona unanipa wakati sijafanya Hilo zoezi?
" Kwa namna nyingine nakuamini ndio maana nimelipa hizo pesa, nenda kamalize shida zako ndogo ndogo pia kumbuka kuacha akiba.
"Sawa doctor Asante.
Alijibu Jemima huku machozi yakitililika.
" Mbona unalia Sasa?
" Sijui nilishukuru vipi doctor nashukuru Sana, Mungu asimame na wewe.
" Amiiina. Alijibu James huku akitabasamu.
Jemima alichukua ule mfuko na kuufunga vizuri kwenye mtandio aliokuwa kajifunika kichwani Kisha akazikumbatia na kuondoka
Baada ya siku tatu kupita Jemima alienda kufanyiwa upandikizaji wa mbegu. Wakiwa kwenye chumba Cha upandikizaji James alikuwa anavaa gloves kwaajili ya kuanza kazi.
" Jemima unauhakika upo tayari?
" Ndio nipo tayari.
" Sawa acha tuanze kazi
Baada ya kukubaliana Jemima alijilaza kitandani na shughuri ya upandikizaji wa mbegu za Melvin ukaanza. Walipomaliza dr James alibaki na Jemima
" Zoezi letu limekamilika ,Sasa unatakiwa kuwa makini kwenye utunzaji wa hiiyo mimba baada ya wiki mbili tutakufanyi vipimo ili kuangalia Kama imenasa.
" Sawa doctor, Sasa naweza kwenda kumuona mama yangu.
" Ndio unaweza kwenda pia hutakiwi kuwa na mawazo mengi, upate muda mwingi wa kupumzika
" Sawa.
Jemima alitoka akaenda kwenye wodi aliyolazwa mama yake alikuta bado kafumba macho alimshika usoni na kusema
" Mama utaamka lini? Natamani ufumbue macho yako hata Mara moja tu.... Wakati anaongea Dr James akaingia.
" Jemima hutakiwi kulia na kusononeka kila siku, mama yako atapona sema atakuwa kwenye Hali ya Kona kwa muda tu. James alikuwa anajitahidi Sana kumpa moyo Jemima na kumfanya asiwe na huzuni.
Zilipofika wiki mbili jemima alipima na kuonekana ujamzito umeshikilia ilikuwa ni furaha Sana kwa James.
" Jemima tumboni kwako Kuna kiumbe nitakachokuwa kina kuwa kila siku hivyo mwili wako utakuwa na mabadiliko ,utaweza kupata homa za kipindi, kichefu chefu hata kuchoka , tafadhali utakapojisikia vibaya hutakiwi kunywa dawa mpaka unitaarifu.
" Sawa doctor.
Jemima alianza kulea mimba huku alipata matunzo kutoka kwa Dr James na hakumjua mwanaume aliembebea ujauzito lakini hakujali kikubwa alilipwa na mama yake alifanyiwa upasuaji pia alitunzwa na kupewa kila alichotaka maisha yake yalikuwa mazuri kuliko hapo mwanzo
MELVIN ( MY BABY DADDY)💖 3
MTUNZI SMILE SHINE
Hali ya Jemima ilikuwa nzuri alipata kila alichotaka na hakutumia pesa zake zaidi ya alizokuwa alipewa na James Kama pesa ya matumizi . Pia Hali ya mama yake ilikuwa nzuri kiasi alifanyiwa upasuaji akafumbua macho lakini alikuwa hawezi kuongea zaidi ya kuangalia tu.
Doctor James alikuwa akimjali Sana Jemima mpaka ikafikia wakati Jemima akahisi huenda James ndio muhusika wa ule ujauzito, lakini alijiuliza maswali kwanini Kama muhusika Ni James kwanini aamue kumpandikiza na sababu ya kufanya hivyo Ni Nini?
Siku moja Jemima alikuwa anaondoka baada ya kutoka kumuangalia mama yake hospital akakutana na James.
" Jamima unaelekea wapi?
" Naenda nyumbani.
" Acha leo nikupeleke.
" Sawa.
Waliongozana mpaka kilipo gari , James akamfungulia mlango Jemima akapanda na James akaenda kupanda Kisha wakaanza safari .
" Doctor sijui nikushukuru vipi Yani bila wewe nahisi ningempoteza mama yangu.
" Usijal Mungu amependa iwe hivyo.
" Asante Sana.
Jemima alishukuru kwa Mara nyingine Kisha ukimnya ukatawala.
Jemima alivunja ukimnya kwa kuuliza
" Doctor naweza kumjua muhusika wa huu ujauzito?
" Hapana Jemima hataki kufahamika anachotaka Ni mtoto tu.
" Sawa.
Hatimae miezi ilienda na tumbo la Jemima lilizidi kukuwa, siku moja alikuwa amekaa wodini huku akifanya maombi kwaajili ya mama Yake. Mara akaona mama yake katingisha mkono hakuamini alisimama kutoka kwenye kiti alichokuwa amekaa na kusogea karibu na kitanda huku akiwa amemkazia macho mama Yake
" Mama nipo hapa tafadhali ongea kitu. Miezi mingi imekatika ukiwa kimnya hapo hebu amka uongee kitu. Mara aliona vidole vikiendelea kucheza . Jemima hakuamini akaita kwa sauti
" Mama! Mama yake alinyanyua mdomo na kuita jina la Jemima japo ilikuwa kwa shida na sauti ya chini. Jemima alitoka mbio kwenda kumuita doctor.
" Doctor, doctor. Jemima aligongana na Dr James ambae alikuwa anakuja mbio huku baadhi ya wauguzi walimfuata nyuma.
" Daktari mama yangu... Mama yangu.... Jemima alishindwa kumalizia kuongea akaanza kupumua kwa nguvu
" Jitulize Jemima pia jiangalie hiyo Hali yako. Dr James alisema
" Sawa,mama yangu anataka kuongea abachezesha vidole vya mkono na miguu.
" Nini? Doctor alimuacha jamima akaingia wodini,Jemima alimfuata nyuma huku akiwa amelishikilia tumbo lake. Alipiga hatua chache Mara akajikuta hawezi Tena kupiga hatua akapiga kelele za maumivu.
" Aaaaaaaah.
James aligeuka na kumfuata
" Jemima upo sawa? James alimuangalia akaona chupa imepasuka
" Nenda kalete wheelchair haraka. Nesi alikimbia kwenda kuchukua wheel chair wakamkalisha na kumkimbiza leba huku wauguzi wengine waliendelea kumuangalia mama Yake.
Jemima aliingizwa Leba huku akiwa anapiga kelele za kuomba msaada. James alimpigia simu Melvin kwaajili ya kumpa taarifa.
" Melvin,Jemima yupo Lena Sasa.
" Jemima? Jemima Ni Nani?
" Mwanamke aliyekubebea mimba.
" Sikiliza James huyo mwanamke anatakiwa kupata huduma Bora, anatakiwa kujifungua salama la sivyo.....
" La sivyo Nini ?Sasa mbona Kama tunatishan? Melvin alikuwa kashakata simu
" Khaaa anakichaa huyu.
James alienda leba akamkuta Jemima bado analalamika
" Oooh jamani nakufa.
" Usijali Jemima nipo hapa .aliongea James huku akisafisha mikono Yake na kuvaa gloves Kisha akamsogelea karibu na kumuita
"Jemima, Jemima unachotakiwa kufanya Ni kumsukuma kwa nguvu. Jemima aliitikia kwa kichwa huku akitililikwa na jasho jingi
James alimuhesabia mpaka tatu
" Moja,mbili,tatu haya sukuma.. Jemima alijitahidi mwishowe akasema
" Doctor siwezi nimechoka. Wakati huo jasho likimtoka
" Unaweza jaribu Tena nakusaidia. James alimminya tumbo Jemima aliposukuma mtoto alitoka na kuanza kulia .
" Hongera Jemima , Ni msichana. James alisema huku akitabasamu.
Jemima alikuwa kachoka Sana aliachia tabasamu la mbali Kisha akasema
" Naweza kumuona binti yangu? Jemima aliomba kwa unyonge kwani alijua hawezi kuishi na yule mtoto anaenda kuchukuliwa na mzazi wake. James alimpatia mtoto na mtoto alinyamaza kulia. Jemima alimlaza kifuani na kutabasamu .
" Nakupenda mwanangu kipenzi. Aliongea huku machozi yakizidi kumtoka . Jemima alimuangalia James akamuuliza
" Wanakuja kumchukua ? James aliitolikia kwa kichwa huku alimuonea huruma Ila hakuwa na njia ya kumsaidia
Jemima alimuangalia mtoto wake alafu akambusu kwenye paji la uso Kisha akamrudisha kwa Dr James. James alimpokea na alipotaka kuondoka aligeuka kumuangalia Jemima aliyekuwa analia kwa uchungu kila mtu aliyekuwepo pale alimuonea huruma nesi mmoja alianza kumbembeleza na James aliondoka na mtoto. Ghafla Jemima alipiga kelele Kali ziliziwashitua manesi
" Vipi upo sawa? Wakati wakijiuliza Nini sababu ya kupiga kelele Mara nesi mmoja aliona kichwa Cha mtoto, yule nesi alipiga kelele akisema
" Mtoto mwingine.
MELVIN (MY BABY DADDY) 💖 4
Manesi walishituka na kuangalia kweli waliona kichwa Cha mtoto.
" Kweli Kuna mtoto mwingine
" Nini?Jemima nae akauliza kwa mshangao
"Mtoto mwingine?
Nesi mmoja alienda kumuita doctor. Baada ya dakika chache Dr James alifika na kushangaa
" Inawezekana vipi? Alionekana amebeba mtoto mmoja. Ok Jemima Vita pumzi na usukume . Jemima alifanya Kama alivyoelekezwa mtoto alitoka alikuwa mtoto wa kiume
" Hongera Sana Jemima Ni wakiume.
" Naweza kumuona mwanangu? Aliongea jemima huku akionekana kuchoka. Alipewa mtoto akamuangalia Kisha akamrudisha kwa doctor huku akiwa na huzuni
" Tafadhali doctor naomba usimchukue niachie mtoto wangu. Jemima aliomba huku akiwa anatia huruma
" Usijali tulia, huyu siwezi kumchukua mpango wetu ulikuwa mtoto mmoja na tayari tumempa. Huyu Ni wako Mungu amekupatia Kama zawadi. Alisema Dr James na Jemima alitabasamu na kumshukuru
" Asante sana doctor.
Baada ya hapo Jemima aliipoteza fahamu . Ilibidi atolewe leba na kuhamishiwa wodini huko alipata matibabu maana Hali yake kiafya haikuwa nzuri , mwili wake haukuwa na nguvu hivyo muda mwingi akitumia kulala tu, mtoto alihudumiwa na hospital na alikuwa chini ya uwangalizi w Dr James.
Wakati huo mama yake alikuwa alijaribu kukaa na kufanyishwa mazoezi ya kutembea. Baada ya siku kupita mama Jemima alienda kumuangalia binti yake .
" Haya Ni majaribu gani tunapitia ilikuwa Mimi Sasa mwanangu.
" Usilie mama ugonjwa wa Jemima Ni wakawaida atakuwa sawa.
" Kwani tatizo Ni Nini?
" Aliipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua pia Hana nguvu.
" Sasa amepatiwa hiyo damu?
" Ndio.
" Nahitaji kumuona mjukuu wangu Harry.
" Sawa twende huku. Waliongozana na doctor wakaenda kwenye chumba alichohifadhiwa Harry.
Kesho yake Jemima aliamka kutoka kwenye usingizi mzito hakuamini alichokiona mbele yake alikuwa Ni mama yake amekaa akuwa kampakata Harry
" Mama
" Jemima usiamke ngoja nikamuite doctor. Mama Jemima alisimama kabla hajapiga hatua Jemima alimzuia
" Subiri mama ,Mimi nipo sawa. Mama unaweza kunipa mtoto wangu?
" Sawa lakini sidhani Kama utaweza kumpakata .
" Usijali mama nitamlaza karibu yangu.
Mama Jemima alienda kumlaza pembeni yake . Jemima alimuangalia mtoto wake alafu akasema
" nakupenda mwanangu wewe ndio faraja yangu na furaha yangu.
" Ni kweli Ila baba wa huyu mtoto Yuko wapi?
"Mama Ni story ndefu kidogo naomba unipe muda.
Harry alianza kulia ikabidi waache kuongea
" Mtoto wako ananjaa unatakiwa kumnyonyesha . Mana Jemima alisema na Jemima aliamka na kumchukua mtoto na kuanza kumnyonyesha.
Kesho yake waliruhusiwa wakarudi nyumbani. Dr James aliwasindikiza mpaka kwenye lango kuu la kuingilia hospital
" Nawatakia safari njema
" Asante Sana doctor. Jemima alijibu . Dr James alimgeukia mama Jemima
" Mama unatakiwa kutumia dawa zako kwa wakati pia usisahau kufanya mazoezi.
" Sawa doctor nitafuata maagizo pia nashukuru Sana kwa yote uliyonifanyia.
" Usijali Ni kazi yangu. Taxi ilifika walipanda kwenye taxi wakaondoka.
Wakati gari inatoka kwenye geti la hospital walipishana na gari moja ya kifahari alikuwa Ni Melvin aneenda kumchukua binti yake ambae alimsubiri kwa hamu kwa hiyo miezi 9 aliyokuwa tumboni.
Melvin alishuka kwenye gari haraka na kuelekea ofisini kwa Dr James.
Alipikaribua mlango wa ofisini alimuona James anakuja kwa mbele.
" James, binti yangu Yuko wapi?
"Mbona una haraka hivyo?
" Unajua kwanini Nina haraka , mama yangu anashauku Sana ya kumuona mtoto .
" Ok mtoto yupo wodini.
Waliongozana mpaka kwenye wodi waliyomtunza mtoto aliona kitoto kichanga Cha kike kikiwa kimelala kwa utulivu mkubwa, Melvin alijiangalia kile kichanga huku akitabasamu.
" Yeye ni Malaika nitakuita hivyo, nikarembo Sana .
" Ni mrembo Kama mama yake.
" Basi hongera kwa kuhifashi mbegu yangu sehemu nzuri, naweza kumchukua binti yangu?
" Ndio unaweza lakini itakuwaje kuhusu matunzo maana huyu mtoto bado mdogo Sana.
" James hivi wewe ni ngeni kwangu? Hakuna kitu kinashindikana kwangu binti yangu ataishi vizuri Sana.
" Sawa .
Dr James alimruhusu mtoto akachukuliwa Kisha wakaondoka .
Walipokuwa njiani Melvin alikuwa akimuangalia Sana binti yake hukubakijisemea
" Swala la mtoto nimeshskimakuza matumaini sitasumbuliwa Tena na wale wazee.
Kwa upande wa Jemima nao walifika nyumbani Jemima alimpaza mtoto wake kitandani na mama yake akajilaza pembeni nae akakaa kwenye kiti.
" Wewe bado ni mzazi hutakiwi kukaa muda mrefu njoo ujilaze kidogo.
" Nitakuja. Alijibu Jemima alafu akatulia na kuonekana Kama alikuwa anawaza Jambo. Mama yake alihisi mwanae anawaza jinsi ya kuishi na yule mtoto kwani alijua jinsi maisha yao yalivyoyumba
" Mwanangu kwani huyu mtoto baba yake Ni Nani?
Jemima alitulia akifikiria jibu la kumpa mama yake ili aelewe.
" Mana sijui nikueleze vipi ili unielewe.
" Nieleze nitakuekewa tu.
" Simjui baba wa mtoto na Wala sijui binti yangu ataenda kuishije bila Mimi.
" Wewe unanieleza kiti gani, inakuwaje hujui mtu aliekupa mimba na huyo binti unaemzungumzia Ni binti gani?
" Ni story ndefu mama pumzika kwanza .....
" Sitaki kusikia Hilo swala la kupumzika nataka kujua kila kitu Sasa hivi, Yani Mimi kuumwa umeamua kuufanya mwili wako sehemu ya kuingizia kipato inamaana ulikuwa unajiuza ili kujikimu ?
Jemima alimuangalia mama yake ambae aliongea kwa ukali na kuonekana mwenye hasira.
" Mama Mimi sio mtu wa namna hiyo nimefanya haya yote kwaajili ya kupata pesa zako za matibabu....
" Jemima , Jemima pesa za matibabu yangu zilikuwa nyingi Sana inamaana hizo pesa umetoa wewe?
Jemima aliitikia kwa kichwa na kumfanya mama yake azidi kuchoka na akili yake ilimpelekea kuwaza kuwa binti yake atakuwa kafanya Jambo moja baya mno maana kujiuza tu hakuwezi kumpatia pesa zote hizo Tena kwa muda wa miezi michache.
MELVIN MY BABY DADDY 💖 5
Mana Jemima alimkazia macho binti yake wakati huo Jemima machozi yalikuwa yakimtililika.
" Kulia sio jibu binti yangu niambie kabla sijapata tatizo litakalo nifanya nife au niumwe Tena.
Jemima alivyosikia hivyo alifuta machozi na kusema
" Sitaki ifikie huko mama nitakuelezea kila kitu.
Jemima alitaka kuongea lakini aliacha baada ya mlango kugongwa. Jemima alienda kufungua mlango akaingia mama Jennifer jirani yao ambae aliongea na Jemima kwaajili ya kuja kumuhudumia yeye na mama yake.
" Karibu mama Jenny.
" Asante.
Walienda chumbani mama Jenny alikutana na mama Jemima wakasalimiana Kisha akamshika mtoto, baada ya hapo alimlaza mtoto kitandani, jemima alichukua pochi yake iliyokuwa imetundikwa ukutani akatoa kiasi Cha pesa kwaajili ya kununua vitu pamoja na chakula. Mama Jenny alizipokea zile pesa akaenda kuendelea na kazi .
" Mama , mama Jenny atatusaidia mpaka tutakapokuwa sawa.
" Sawa lakini utamlipa Nini?
" Pesa ipo.
" Jemima ujue unanichanganya wewe mtoto.
" Mama ukweli Ni kwamba mimba niliyobeba nilipandikizwa nikalipwa pesa nyingi nikalipia pesa zako za matibabu na nyingine zilibaki. Wakati wa kujifungua nilianza kupata mtoto wa kike. Na huyo ndio kachukuliwa , niliumia Sana baada ya mtoto wangu kuchukuliwa sikuwa najua Kama kujifungua huwa kunauma kiasi kile na mtu anakuwa na mapenzi na mtoto anaemzaa Ila sikuwa na jinsi pesa nimeshamtumia laiti ingekuwa pesa ipo ningerudisha nibaki na mwanangu Ila Mungu hakutaka kuniacha mpweke alinifuata machozi na kujipunguzia machungu kwa kunipa mtoto mwingine. Kwa huruma ya Dr James aliamua kuniachia.
Mama Jemima alimuonea huruma binti yake pia aliumia kwa maneno makali aliyokwambia hakujua Kama Jemima aliamua kufanya yote hayo kwaajili ya kunusuru maisha yake.
" Nisamehe mwanangu na pole kwa kukwambia maneno makali.
" Usijal mama hata ingekuwa mtu mwingine angeweza kuwa kana wewe.
MELVIN kaagizia watu wapeleke vitu vya mtoto nyumbani kwao pia aliandaliwa mtu wa kumtunza mtoto.
Mana yake alishangazwa sana na Yale maandalizi kwani hakuwa anataarifa yoyote, alipouliza aliambiwa Ni maagizo kutoka kwa Melvin. Basi mama yake alitulia aone mwisho wa Hilo Jambo.
Baada ya muda gari ya Melvin ilifika nyumbani kwao na Melvin balushuka akiwa kabeba mtoto mikononi kwake. Mana yake alipimuona alishangaa , alisimama pale alipokuwa kakaa na kumfuata. Alimuangalia mtoto Kisha Melvin alafu akauliza
" Melvin umemtoa wapi mtoto mchanga hivi?
" Mama huyu Ni binti yangu anaitwa Malaika (Angle).
" Nini? Mtoto wako kivipi? umemtoa wapi?
" Hii Ni damu yangu, hebu mshike mjukuu wako.
Mama Melvin alimpokea akawa anamuangalia yule mtoto.
" Mlitaka niwe na mtoto Sasa huyo hapo.
" Mama yake Yuko wapi?
" Sijui
" Khaaaa hujui kivipi?
" Sijawahi kumuona .
" Melvin sipo kwenye utani naomba uongee kitu kilichonyooka. Mama Melvin aliongea kwa ukali na wakati huo baba yake Melvin alifika akamkuta mke wake kashika mtoto.
" Hiki kichanga Cha Nani?
" Muulize mwanao.
Kabla baba Melvin hajauliza Melvin alijielezea.
" Ni mtoto wangu kazaliwa leo na mwanamke ambae nilimlipa akabeba mbegu zangu Sasa mtoto kazaliwa huyu mtoto Ni damu yangu.
" Sasa mbona hatumuoni huyo mama wa mtoto?
" Wakazi gani? Kashanaliza oazi yake kaondoka zake .
" Melvin huyu mtoto Ni mdogo mno hawezi kuishi bila mama namtaka huyo mama hapa . Alisema baba yake.
" Baba mlitaka mjukuu Sasa huyo hapo Sasa huyo msichana wa kazi gani hapa?
" Melvin kuwa na huruma huyu mtoto atahitaji kunyonya na ukaribu wa mama yake.
" Mimi sijui kwa kumpata.
Melvin alipishaba kauli na wazazi wake kila mmoja aliongea lake Mara mtoto akaanza kulia.
" Mnapiga kelele mpaka mtoto wangu analia . Melvin alimchukua mtoto wake akawa anambembekeza lakini mtoto aliendelea kulia, alikuja mlezi aliemuajiri akamchukua akaenda kumpa maziwa.
" Hakikisha mtoto wangu unamlea vizuri sipendi kusikia analialia.
" Sawa boss
" Melvin nataka huyu mtoto apate haki yake ,wewe hukulekewa bila mama namtaka mama wa mtoto aje hapa.
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote