Sherry ni binti wa chuo anae anzisha mahusiano na Arnold ambae ni kaka wa Aliyah kisa tu Arnold ni mwanaume mwenye pesa. Sherry anamtesa Arnold kihisia mpaka inapeleka Arnold kujiua.
Hii inamchukiza sana Aliyah mpaka kuamua kulipiza kisasi kwa Sherry. Anamtumia Mpenzi wa Sherry kulipiza kisasi na anafanikiwa kwa kiasi kikubwa kumliza Sherry kama jinsi alivyotaka.
Lakini katika hatua hizo za kulipiza kisasi Aliyah anajikuta anampenda mpenzi wa Sherry! Unadhani Sherry nae atakubali kumpoteza mpenzi wake kwa Aliyah?
MADAM BOSS (Kisasai Kilicho Jenga Upendo)
By Miss Hamida
*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*
Kuna mda moyo wako hauwezi kupata amani pasipo kulipiza. Unahisi huwenda ukilipiza unaweza kupata amani kwa kumwadhibu mkosaji.
Sana sana kisasi kinatokana na hasira juu ya kitendo ulicho fanyiwa. Na kuna wakati kweli unaona anae adhibiwa anastahili adhabu iyo.
SEHEMU YA : 1
Tuanzie nyuma kidogo kama miaka sita iliyopita. Kipindi icho Aliyah alikua anasoma chuo kimoja kikubwa sana hapa Dar.
Alipenda sana kusomaa maana aliamini kupitia elimu angeweza kutoboa kimaisha. Wakati huo Aliyah alikua akiishi na kaka yake kwa jina la Arnold.
Hawakua na maisha mazuri lakini pia hawakua na maisha magumu! Waliishi kwa amani na upendo huku Arnold akihakikisha kua hakuna kitu ambacho Aliyah alikitaka akakosa.
Kwa bahati mbaya wazazi wao walifariki pindi wakiwa wadogo na kupelekea ndugu hawa kubakia wawili tu.
Arnold alifanya kila kitu kwa ajili ya Aliyah. Na Aliyah alimpenda kweli kaka yake. Alimheshimu na alifanya vitu sahihi ambavyo visinge mchukiza.
Basi kila weekend baada ya masomo Aliyah alirudi nyumbani kwaajili ya mapumziko.
Sasa siku hiyo alipofika nyumbani alikuta hali ya tofauti kidogo. Arnold alikua kapooza kuliko kawaida. Hata hakumchangamkia kama siku nyingine anavyo fanyaga.
“kwani una nini kaka? Unaumwa?”
“Hapana siumwi!” Arnold aligeuka upande wa pili
“Sasa shida nini!”
“Kwanza si umesema jumatatu una mtihani? Sasa kwanini umerudi nyumbani?”
“Si kwasababu ulini ahidi utamalizia ada! Na pasipo ada mimi siwezi fanya mtihani”
“Hakuna shida! Nitaangalia nafanyaje”
Arnold alisimama na kwenda chumbani akamuacha Aliyah peke yake akiwa anamshangaa.
“Au labda ana njaa?? Pengine atakua kalimisi pilau langu”
Aliyah alikwenda jikoni akaanza kukarangiza pilau ili tu kaka yake apate kula. Alipomaliza kupika alitenga chakula sebuleni na kwenda kumuita Arnold.
Alipofika mlangoni kwa kaka yake akaanza kubisha hodi. Alibisha hodi mda mrefu pasipo kufunguliwa. Aliyah akachoka kuendelea kusubiria akafungua mlango na kuingia ndani.
Kumbe Arnold alikua bafuni ndio maana hakumsikia Aliyah alipokua anabisha Hodi. Lakini simu yake ilikua kitandani, na ilikua inaingiza meseji nyingi kama mvua.
Aliyah akatamani kujua, akaichukua na kuifungua. Alikutana na meseji nyingi toka kwa nambaa iliyo seviwa Sherry.
Alianza kuzisoma ndipo akagundua kaka yake alikua kwenye mahusiano na huyo Dada alie itwa Sherry. Na kwa mda huo Sherry alimtumia Arnold meseji akitaka waachane, na hio ndo sababu iliyomfanya Arnold kunyong’onyea.
Wakati Aliyah alipokua anaendelea kupekua simu, Arnold akawa ametoka bafuni. Haraka alimuwai Aliyah na kumnyang’anya simu yake.
“Umeanza lini kugusa vitu vyangu bila ruhusa”
“Huyu Sherry ni nani?”
“Achana na mambo yangu Aliyah”
“Ni mpenzi wako sio?”
“hata nikikuambia haita saidia kitu”
“hakuna ajabu kwa wewe kua na mahusiano na mwanamke lakini kinacho nishangaza ni namna huyu dada anavyo kuendesha! Kila siku anataka hela na wewe una mtumia. Kwa jinsi nilivyo soma meseji zenu nimeona kabisa hakupendi bali anakutumia”
“nyamaza Aliyah hakuna unalo lijua” Arnold alichukia
“Ndo ukweli huo! Alafu mpaka hela yangu ya ada umemtumia yote! Laki tano nzima”
“Aliyah….”
“Kaka huyo dada hakupendi! Anakutumia tu! Achana nae kama anavyo taka”
“Ananipenda! Tumegombana kidogo tu anataka tuachane! Nahisi ni hasira, akikaa sawa tutaendelea na mahusiano”
“Kaka hakupendi..”
“Aliyaaaah……” Arnold alifoka kwa hasira na kumfanya Aliyah aogope
“Sawa! Chakula kipo mezani!”
Aliyah alitoka kwa hasira na kwenda chumbani kwake. Alijifungia na kuanza kulia. Aliumia jinsi alivyo fokewa ukizingatia kakaa yake hakuwai kumfanyia ivo kabla.
Basi Arnold akawa katambua kosa lake! Anampenda mno mdogo wake na hakutaka wagombane. Alimfuata akamuomba msamaha kisha wakaenda kula chakula alicho kiandaa Aliyah.
Baada ya weekend kuisha Aliyah alirudi chuoni akiwa tayari kashalipiwa Ada yote. Alifanya mtihani yote na aliifanya vizuri maana alijiandaa vya kutosha.
Mtihani wa mwisho ulipomalizika ilikua ni siku ya alhamisi. Akapanga arudi nyumbani akapumzike sababu hakua mpenzi wa kukaa sana hostel.
“Unaenda wapi tena??” Najma rafiki wa Aliyah alimuuliza
“nyumbani”
“Sema tu ume mmiss kaka yako ndo maana unaenda”
“Ndio! Alafu toka juzi hajanipigia simu! Moyo wangu hauna amani kabisa Najma!”
“Aliyah kuna wakati unabidi ukubali kuwa kaka yako ni mtu mzima! Kama hajakupigia simu labda yupo bize na kazi”
“Hapana! Sio kawaida yake! Namjua kaka yangu vizuri”
“Sawaa nitaongea nini mimi! Watu wenye kaka zao! Kila siku kaka kaka kaka, sijui sisi marafiki tutaonekana lini”
“Acha maneno yako Najma! Ngoja niende”
Aliyah alitoka mbio mbio akachukua usafiri mpaka nyumbani kwao. Huko palikua kimya kweli, alifungua mlango na kuingia ndani.
Alikutana na chupa nyingi za pombe zikiwa zimetapakaa kila sehemu. Alipozidi kusogea ndipo akamuona kaka yake akiwa kajiegemeza kwenye ukuta akiendelea kunywa pombee.
“Kaka!” Aliita kwa sauti ya huruma
“Umeku…jaaa” Arnold akajifanya kutabasamu
“nini shida? Mbona unakunywa pombe wakati hunywagi??”
“Amna…”
“Ni kwasababu ya Sherry sio?? Sherry ndo anafanya unakunywa pombee”
Arnold badala ya kujibu akaanza kucheka sana kisha akamgeukia Aliyah na kumuambia
“Mapenzi yanauma mdogo wangu! Mwamba kama mimi niwa kuteseka na mapenzi kweli? Kazi hazipandi kwasababu yake! Nimemjua kwa mda mfupi lakini ananichanganya sana kichizi”
“Nimekuambia hakupendi”
“Najua hanipendi lakini mimi nampenda! Kumsahau ndo kitu ambacho siwezi!”
“Jaribu kumsahau! Hakuna haja ya wewe kumuwaza mtu ambae hakupendi! Mbona wanawake wapo wengi utampata atakae kupenda kwa dhati”
“Sitaki mwingine zaidi yake”
“Kaka..”
“Sherry ana mwanaume mwingine! Anampenda kuliko mimi! Anasema eti hajawai kunipenda mbali ya yale yote niliyo mfanyia! Eti alikua ananitumia tu sababu ya hela. Aliyah yule mwanamke nimemfanyia mambo mengi ambayo nilipaswa nikufanyie wewe mdogo wangu. Ulikua unalalamika simu yako ni mbovu, badala ya kukununulia wewe nikaenda mnunulia Sherry! Tena Iphone 16!! Bado kuna out, shopping za mara kwa mara! Unajua kabisa kaka yako sina pesa lakini nikamaliza mshahara wangu wote kwake. Nilipokosa hela nikakopa ili tu nimuonyeshe jinsi gani nampenda! Ila vyote hivyo hakuviona, mpaka hela yako ya ada nilimpa yeye akafanyia birthday na kwendea out na Bwana ake! Yote hayo kanifanyia lakini bado nampenda”
“achana nae! Hakufai!”
“Mimi nampenda Aliyah! Nampenda sana”
Aliyah akashindwa afanye nini tena maana kaka yake alikua mbishi kuelewa. Alinyamaza kwa dakika chache kisha akamnyang’anya ile chupa ya pombe na kuiweka pembeni.
“Nenda kaoge kisha utakuta tayari nimekuandalia supu! Ukishakua sawa ndo tutaweza kuongea”
“Sawa”
Arnold kwa uvivu akajinyanyua toka pale chini na kuelekea chumbani kwake. Huku nyuma Aliyah alianza kwa kufanya usafi.
Alifagia kwanza, akatoa chupa zote za pombe kisha akadeki. Baada ya pale akaenda buchani kununua nyama ya supu maana friji lilikua tupu.
Aliporudi akaanza kuchemsha nyama na kuitia viazi angalau supu iwe nzito. Wakati supu ikiwa inaendelea kuchemka Aliyah alichukua simu yake na kumpigia Najma. Alimuelezea kila kitu maana hakuna mtu mwingine ambae angeweza kumshauri zaidi Yake.
“Woooh! Au uyo dada kamloga nini?”
“sidhani bhana”
“Aliyah ilo linawezekana! Siku hizi watu wapo vizuri”
“Hajalogwa, sema ni vile hajawai penda apo kabla! Huyu Sherry ndie mwanamke wake wa kwanza”
“Kwanza huyo Sherry unamjua yupoje?”
“sijawai muona na sijui ni mrefu ama mfupi”
“Mimi apo cha kukushauri ni ujaribu kuongea na kaka yako! Mshauri na umpe maneno ya busara! Mtie moyo pia maana kuachika sio jambo jepesi! Ukishindwa kabisa itabidi atafutiwe mwana saikolojia”
“Asante best angu”
“Ndo ufanye ivo sasa”
“Sawa Najma”
Aliyah alikata simu, na kuanza kumimina supu kwenye kibakuli maana ilisha kwiva tayari. Alipomaliza alitenga mezani na kwenda kumuita Arnold chumbani.
Aligonga sana ila mlango haukufunguliwa, akaita wee napo hakujibiwa. Akapata hofu, akanyonga kitasa haraka na kuingia ndani.
Alicho kiona huko kilimfanya atamani kulia. Arnold alikua kalala chini huku damu zikimtoka mkononi. Alichana mshipa wa damu mkononi kwa kiwembe lengo likiwa ni kuutoa uhai wake.
Mapenzii na maumivu vilimchosha, ni heri angekufa kuliko kuendelea kuona mwanamke anae mpenda amemuacha.
Nakuja………..
SEHEMU YA : 2
“Kaka..” Aliyah alimtikisa bila mafanikio, tayari Arnold alishapoteza fahamu mda sana.
Alicho fanya ni kumnyanyua kutoka pale chini akajaribu kumvuta mpaka nje ili apate msaada wa kumpeleka hospitali.
Bahati nzuri vijana wasamaria walimbeba wakampakiza kwenye bajaji na safari ya kwenda hospitali ilianza.
Njia nzima Aliyah alikua akilia tu, hakuta tayari kumpoteza kaka yake ikiwa ni familia pekee aliyo bakiwa nayo.
Alimtazama na kuona damu ikizidi kumtoka, bila aibu alivua blauzi yake akaufunga ule mkono. Aliyah akabaki amevaa sidiria pekee yake na hakujali.
Walipofika hospitali watu walimshangaa tu, ili kuondoa aibu yule dereva bajaji alivua t-shirt yake ili Aliyah apate kujisitiri.
“asante sana..” alimshukuru
“hakuna shida sista! Hakikisha bro anapona”
“S
Pale pale walikuja manesi wakiwa na kitanda cha wagonjwa, wakambeba Arnold na kwenda nae ndani huku Aliyah akiwafuata nyuma.
Matibabu yalianza kwa haraka ili kuyaokoa maisha ya Arnold. Maskini Aliyah akabaki akilia tu, alilia mno akiwa nje ya chumba cha matibabu alichokua Arnold.
Alianza kufikiria ikiwa kaka yake angefariki angebaki na nani?? Angeishije ikiwa alikua anamtegemea kwa kila kitu??
“Kaka yangu akifa na mimi nitakufa! Nitajiua na mimi! Sitaweza kuishi mwenyewe! Siweziiii…”
Aliongea peke yake kama chizi, alisimama mara akakaa. Alipoona haitoshi alizunguka huku na kule huku akifikicha vidole vyake.
Alipochoka kabisa alikaa chini kwenye sakafu huku mikono yake ikiwa kichwani.
“Mbona hawatoki?? Eehhh?? Wamekaa sana huko ndani”
Saa yake ya mkononi ilisoma saa tisa na nusu alasiri. Tayari yalipita masaa matatu pasipo kusikia chochote toka kwa madaktari waliokua kule ndani.
Aliyah akiwa anaendelea kusubiria alikuja yule dereva bajaji ambae alimpa Nguo yake avae. Yule kaka alishindwa kuendelea na kazi zake, aliona jinsi gani Aliyah alivyokua anateseka ivyo aliamua kumpa kampani angalau atulie.
“Hujaondoka bado??”
“Hapana! Roho imeniuma! nimeona nirudi tu”
“asante sana”
“usijali tupo pamoja”
Aliyah alipata faraja kua angalau alikua na mtu pembeni wa kumfariji. Basi kwa pamoja wakaendelea kusubiria.
Ilipotimu saa kumi kamili mlango ulifunguliwa na Madaktari wakatoka. Aliyah alisimama haraka akamsogelea Daktari mmoja huku akimshika mkono
“Kaka yangu anaendeleaje?? Eeeh???”
“Tulia kwanza..”
“Nataka kujua hali ya kaka yangu, mimi siwezi kutulia”
“Ok! Kaka yako anaendelea vizuri ingawa tumepata shida kweli kuiunga tena mishipa yake na kuzuia damu isiendelee kutoka sababu alikunywa pombe. Kinacho hitajika sasa ivi ni damu pamoja na dawa! Kwa bahati mbaya benki yetu ya damu imeishiwa damu Group 0! Wewe una damu group gani?”
“Group A”
“tungepata mchangiaji wenye group 0 ingekua vizurii zaidi!”
“Mimi ni Group 0! Naweza kumchangia?” Alisema yule dereva bajaji kwa kujiamini
“Ooh ndio! Lakini kwanza tukupime”
“Hakuna shida”
“Kama hutajali nifuate”
Dokta pamoja na yule dereva bajaji walifuatana nyuma mpaka chumba cha maabara. Alipopimwa hakua na shida yoyote ile na damu yake ilifaa kuchangia.
Aliyah alifurai kweli na alishindwa angemlipa nini yule kaka alie jitambulisha kwa jina la Morris.
“Asante sana! Sijui nikushukuru kwa namna gani kaka yangu”
“amna haja! Duniani ni kusaidiana huwezi jua pengine na mimi nikipata shida unaweza kuja kunisaidia baadae”
“Ni sawa ila umejua kunisaidia! Sijutii kukufahamu”
Aliyah alitabasamu huku akimpisha Morris aendelee kuchangia damu yeye akatoka nje. Alienda kununua dawa zilizo hitajika kwaajili ya kaka yake.
Baada ya pale ndipo akakumbuka kumjulisha Najma juu ya kile kilicho tokea.
“Aliyah nimekupigia sana, nina habari nzuri” Najma hakumpa Aliyah nafasi ya kuongea
“mimi nina habari mbaya”
“nini tena kimetokea??”
“niambie kwanza izo habari nzuri pengine naweza nika enjoy kidogo”
“ok! Majina ya scholarship yametoka! Jina lako lipo Aliyah! Finally utaenda kusoma Canada”
“Kweli??”
“Ndio! Tena la kwanza”
“daaah! Nimefurai kweli, i wish hizi taarifa zingetoka mapema Najma! Apa ninapo ongea na wewe nipo hospitali! Kaka yangu alitaka kujiua! Ameukata mshipa wa damu kwa kiwembe”
“Nini??”
“Ndio”
“Mungu wangu Aliyah nakuja sasa ivi! Ooooh pole rafiki yangu jamani! Uwiiii”
“Njoo usichelewe”
“Nakuja nakuja”
Aliyah alikata simu na kurudi kuendelea kusubiri. Hakukaa mda mrefu nae Najma akawa amefika. Walikumbatiana huku Aliyah akianza upya kulia.
“Oooh imekuaje tena??”
“Yote ni kwasababu ya Sherry! Anataka kujiua sababu ya Sherry”
“Ndo maana nakuambia Aliyah yawezekana pengine kamloga! Kwa jinsi ninavyo mjua kaka yako sio mtu wa kukata tamaa kiasi cha kutaka kujiua”
“Ndo ivi Najma, moyo wangu unauma mno”
“Tulia basi! Eeeh! Embu tulia kidogo”
Wakiwa bado wamekumbatiana Alifika Morris, alikua ameshamaliza kuchangia damu. Aliyah Alimtambulisha Morris kwa Najma! Wakawa wamefahamiana.
Morris hata hakukaa sana, aliaga na kuondoka akimuahidi Aliyah kua angerudi kesho yake. Alipoondoka tu Najma alimgeukia Aliyah akamuuliza
“huyu kaka ulikua unamjua kabla??”
“hapana! Si nishakuambia kwamba alinisaidia kumleta Kakaa hospitali? Kamchangia na damu”
“Maana mhhh jinsi anavyo kutazama”
“Ananitazamaje??”
“Macho flanii iviii…”
“Najma please Stop, najua unapotaka kuelekea ila sipo huko”
“Sema ni kembamba kama kuni za nyongeza”
“Acha bhana usimuongelee vibaya! Kanisaidia ujue”
“Sawa! Nimenyamaza”
Aliyah alitabasamu maana akili za Najma alikua anazielewa vizuri. Basi wakaendelea kukaa pale hospitali mpaka giza lilipo ingia ambapo Najma nae aliaga na kuondoka.
Akawa amebakia Aliyah peke yake akisubiri kaka yake afungue macho. Hakuruhusiwa kuingia wodini ivyo akawa amekaa nje kwenye benchi.
Usingizi ulipomshika alijilaza vizuri na kujikunja akalala. Alilala mda mrefu kweli hadi alipokuja kuamshwa na nesi.
“Dada… dada samahani” nesi alimtikisa Aliyah
“abeee….!”
“Samahani..”
“bila samahani!” Aliyah alinyanyuka na kukaa akimtazama alie muamsha
“nilikua nataka kukuambia kaka yako ameamka”
“kweli?? Kweli kamka?? Kaka yangu kamka”
“Ndio kamka! Na anahitaji kuongea na wewe ila tafadhali utakapo ingia wodini nakuomba uongee nae taratibu sawa? Bado hajapona vizuri”
“Hakuna shida”
Aliyah aliporuhusiwa akaingia wodini. Macho yake yalitua kwa Arnold aliekua anatazama kwa shida. Alikua hana nguvu sababu ya kupoteza damu nyingi.
Aliyah akaanza kulia tena!
“Mbona unalia?? Sijafa!” Arnold alizungumza kwa sauti ya chini akijaribu kutabasamu kwa shida
“Ndio hujafa! Ungekufa na mimi ningekufa”
“usiseme ivo”
“we hukunifikiria mimi hata kidogo?? Eeeh! Ningeishi na nani sasa?”
“umenikasirikia?”
“unataka nifurai?? Tena upone haraka ili niweze kukugombeza vizuri”
Arnold akatabasamu tena, Aliyah akashindwa kuvumilia, alimsogelea na kumkumbatia kwa nguvu! Walibaki vile kwa dakika 3 ndipo akamuachia
“Unajisikiaje?”
“vizuri, japo sio sana! Mwili wangu hauna nguvu hata pumzi navuta kwa shida”
“umemwambia dokta??”
“ndio! Amenambia….. kama hali ikizidi… nitapumulia mashine” Arnold aliongea kwa nukta ili apate nguvu ya kuvuta pumzi
“Please ukipona niahidi kua hutafanya ivi tena!”
“Sitafanya… nakuahidi”
“muone kwanza! Umeniliza kama nini!”
“Am sorry.! Aliyah nikuombe kitu?”
“Ndio kitu gani!”
“Please nahitaji kuongea na Sherry!…. Nisaidie niongee…. Nae”
Aliyah alichoka, yani baada ya kuyahatarisha maisha yake sababu ya Sherry ila bado tu hakuacha kumpenda.
“Unampenda sana huyu mwanamke?”
“ndio! Ipo siku… Aliyah… utajua namaanisha…nini!”
“Sawa nitakusaidia uongee na Sherry! Tutampigia simu”
“Hapana…! Nataka kuonana nae ana kwa ana! Niongee nae nikiwa namtazama machoni! Please”
“mhhhhhh! okay, nampataje huyu Sherry?”
“Anasoma chuo kimoja na wewe ila… kozi tofauti…! Yeye…. Anasomea… accounting..! Jina lake kamili ni Sherry Samson Kaluwa yupo mwaka wa kwanza kama wewe”
“ni mwanachuo? Anae kutesa ivi ni mwanachuo?? Nikajua labda ni mwanamke mwenye kazi yake” Aliyah alishangaa
“We niletee… Sherry! Mwambie yeye ndo…. dawa yangu! Bila yeye…. Siwezi pona”
“kaka”
“nisaidie mdogo wangu!”
“Ok nakwenda kukuletea Sherry”
Nakuja…………
SEHEMU YA 3
Aliyah alinyanyuka akatoka kule wodini akiwa anajiuliza maswali mengi kichwani. Kwani kaka yake alipewa dawa gani mpaka akawa vile?.
Ni mapenzi tu ndo chanzo cha shida zote zile ama kuna kitu kingine ambacho yeye hakijui.
Aliendelea kutembea akiwaza hata alipopishana na Najma hakumuona.
“We Aliyah??? Ina maana hujaniona?”
“oh Najma umefika saa ngapi?”
“sasa ivi! Mimi naingia naona na wewe unatoka! Unaenda wapi hata huangalii unapo enda”
“acha tu Najma! Kaka amepata fahamu”
“kweli? Saa ngapi?”
“asubui hii! Ila cha kushangaza bado anamtaka Sherry! Amenambia nikamletee Sherry”
“Kwaiyo ndo unaenda?”
“ndio sasa nifanye nini? Amesema Ndo dawa yake! Atapona kama atamuona Sherry!”
“Mhhh! Sasa utampatia wapi!”
“chuoni kwetu! Sherry anasoma chuoni kwetu!”
“Weeeee!”
“Twende tusije chelewa”
Najma na Aliyah walitoka mbio mbio kuelekea chuoni kwao. Walipofika wakaenda kwenye darasa ambalo kozi ya accounting walikua wanakipindi asubui ile.
Walikuta baadhi yao walishaingia darasani huku wengine ndo wakiwa wanafika. Aliyah akaulizia Jina la Sherry Samson Kaluwa akaambiwa bado hajafika.
Ivo yeye na Najma wakaendelea kukaa nje ya lile darasa wakiendelea kusubiria. Lakini Dakika Zile zile Sherry alifika.
Kusema kweli Sherry ni mrembo sana, kuanzia rangi yake mpaka shepu yake. Na wanaume wengi walimtaka sababu alivutia mno.
Basi Sherry aliwapita pale nje na kuingia darasani. Kwakua Aliyah hakua anajua Sherry anafananaje ikawa ngumu kumtambua hasa alipo wapita.
Sasa kule ndani Darasani Sherry alipewa taarifa kuwa kuna watu walikua wanamuulizia.
“ni akina nani?”
“Hatuwajui lakini sio wa kozii yetu” rafiki yake alimuambia
“wanataka nini? Na wamenijuaje?”
“kwa hapo sijui! Ila wao wanaonekana wanakujua maana wamelitaja jina lako kamili”
“Kutaja jina kamili sio shida, si unajua jinsi gani watu wananijua sana kisa uzuri wangu?”
“wapo nje lakini kwani hujawaona??”
“Hapana! Embu ngoja nikawasikilize shida yao”
Sherry alitoka tena nje ya darasa na mara hii alimuona Aliyah na Najma. Aliwasogelea akakunja mikono yake na kuwatazama.
“Enhee shida yenu??”
“Shida yetu?? Kwani we ni nani kwani mpaka utuulize ivo?” Najma alikua mkali sababu ya Dharau za Sherry
“Nyie si mnanitafuta??”
“we ndo Sherry…?” Aliyah akaanza kutabasamu
“Ndo mimi! Enhee shida yenu ni ipi?”
“Sherry mimi naitwa Aliyah! Mdogo wake na Arnold”
Jina la Arnold lilipo tajwa Sherry alibinua midomo yake juu kwa dharau.
“Kwaiyo?”
“Anahitaji kukuona! Please naomba ukamuone kaka yangu”
“Ameamua kutuma mdogo wake ili aniombe?? Makubwa” akacheka kweli
“Kaka angu yupo kwenye hali mbaya sana! Amesema akikuona atakua sawa please msaidie”
“Kwanza kaka yako mimi simpendi! Nishamuambia ilo ila yeye ni king’ang’anizi”
“Sasa kama ulikua humpendi kwanini ulikua nae kwenye mahusiano!?”
“Alikua ana honga vizuri sasa mimi nifanye nini? Iyo ndo sababu ya mimi kua nae! Alafu kwanza nilidhani tulikua tuki enjoy tu kumbe mwenzangu alikua akinipenda kweli”
Aliyah aliumizwa mno na yale maneno. Kwajinsi alivyo chukia alitamani hata angepigana na yule dada ila kwakua ana shida nae ilibidi avumilie.
“Ok, ndio humpendi ila please jaribu kumuona! Unajua alitaka kujiua sababu yako! Hali yake ni mbaya mno Sherry, wewe pekee unaweza msaidia akakaa sawa”
Aliyah alidhani labda akisema vile atabadilisha maamuzi ya Sherry ila haikua ivo.
“Sina huo mda! Okay?”
“Sherry Tafadhali”
“Nimeshakataa and please sitaki mnisumbue tena”
Sherry alirudi darasani huku akiwa kakasirika. Alikaa pembeni ya rafiki yake akiendelea kukunja sura.
“Nini shida Sherry!”
“Si huyu Arnold! Kaka ni mpuuzi sana yule! Kaona simtaki ndo kaamua kumtuma mdogo wake”
“Heee! Makubwa”
“Naskia alitaka kujiua kwasababu yangu”
“sherry! unajua ni vibaya ivo?”
“Sabra na wewe ishia hapo hapo! Unajua ni kiasi gani nampenda Clayton! Huyo ndo mwanaume ambae amefanikiwa kuuchanganya ubongo wangu! Huyo Arnold nilikua nae tu kwasababu ya shida ya pesa. Nishalipa Ada! Nimeshalipa hosteli na mama yangu nyumbani anahela ya kula! Unadhani bila ivyo ingekuaje?”
“Sawa ila angalau ungemuona! Sherry usiwe mgumu wa moyo kiasi icho”
“Simpendi kwanza yule kaka! Ni king’ang’a pro max! Simpendi hata jina lake sitaki lisikia! Na kama unataka tuendelee kuwa marafiki naomba acha kulitaja jina la Arnold”
“Sawa” Sabra aliamua kunyamaza kimya maana hakuna ambacho angekisema kingeweza badili mawazo ya Sherry.
Upande wa njee Aliyah bado aliendelea kusubiria. Hakukata tamaa kwaajili tu ya kaka yake.
“Aliyah tuondoke bhana!” Najma alilalamika
“Siwezi! Tusubiri wakitoka darasani nijaribu kumuomba tena Sherry!”
“Achana nae bhana si ameshakataa”
“tatizo Najma naogopa! Itakuaje kama sitakwenda na Sherry?? Jambo baya linaweza kumkuta kaka maana pia anaongea vitu vya ajabu ajabu! Mara hana mda mrefu mara Sherry ndo dawa yake”
“Hakuna kitakacho mkuta bhana tuondoke”
“NO! Najma tafadhali nivumilie eeeh? Nafanya ivi kwaajili ya kaka yangu sio kwamba napenda kunyenyekea binadamu mwenzangu na kuwaomba omba”
“Sawa”
Najma alitulia kidogo na kuendelea kusubiria. Kipindi kilikua cha masaa 2 ivyo kilipokwisha wakatoka. Aliyah alisimama haraka akasogea mlangoni huku macho yake yakimtafuta Sherry.
Alipomuona alimkimbilia na kumshika mkono wake.
“sherry tafadhali! Eeeh! Hata dakika 10 hazitaisha”
“Embu niache we dada”
“Kaka yangu anahitaji kukuona! Sherry…” machozi yalimtoka Aliyah
“Niache huko” Sherry alimsukuma Aliyah, ambae aliteleza na kudondoka chini.
Moyo ulimuuma sana Aliyah! Hakupenda dharau ila tu kwaajili ya kaka yake alikua tayari kuvumilia manyanyaso yote.
Alisimama, akajikung’uta na kumkimbilia Sherry kwa mara nyingine. Alipomfikia akaushika tena mkono wake.
“Upo tayari kumuona kaka yangu anakufa? Mbona unakua na roho ngumu kiasi hiko? Kwani ukienda kumuona utapungukiwa na nini? Kwani ni kitu gani kibaya alicho kutendea hadi unamfanyia ukatili wa namna hii?”
“Tatizo lake ni king’ang’a kama ulivyo wewe! Familia yenu imejaa ving’ang’anizi! Ila ngoja nikupe ujumbe wangu umpelekee….! Mwambie simpendi! Aniache kama nilivyo nina mwanaume wangu tayari! Kama ni kufa afe tu!”
Aliyah taratibu alimuachilia Sherry, akageukia na kurudi alipokua amesimama Najma.
“Si nilikuambia? Hakukua na haja ya kumsubiria Yule mpuuzi! Tuondoke zetu”
Najma aliushika mkono wa Aliyah na wakaondoka kurudi hospitalini. Njia nzima Aliyah alikua kimya akilia. Ahadi aliyo muahidi kaka yake alishindwa kuitimiza. Je angemuelewa kama Sherry alikataa kwenda kumuona.
Alishusha pumzi na kujifuta machozi yake.
Nakuja………..
SEHEMU YA : 4
Walifika hospitalini wakapitiliza moja kwa moja wodini alipo lazwa Arnold. Nje walimkuta Morris, alifika mda mrefu kweli, alipo mkosa Aliyah akaamua kukaa pale nje.
“Aliyah ulikua wapi? Madaktari wamekutafuta sana”
Alisema Morris akiwa amepanick
“Kuna nini? Kaka yupo sawa?”
“yupo sawa sema hali yake ilibadilika! Sasa ivi wamemuwekea mashine ya oksijeni! Aliyah kaka yako anapumulia mashine”
“Nini??”
“ivyo ndo ilivyo kuwa”
Aliyah alihisi ukichaa, alitoka mbio mpaka ndani ya wodi akamuona Arnold kweli akiwa na anapumulia mashine.
Alimsogelea na kuushika mkono wake! Alimpapasa taratibu kichwani machozi yakizidi kumbubujika.
Arnold alipoguswa tu akafungua macho yake. Uso wake ulionyesha nuru kwani alijua lazima Aliyah angerudi na Sherry.
“Yupo….. wapi…. Sherry??”
Swali lilikua gumu kwa Aliyah kujibu. Alijifanya hajasikia alicho ulizwa
“Aliyah……!” Arnold akamuita
“Abe..e!”
“Yupo…. Wapi… Sherry”
“Pumzika kwanza! Tutaongea baadae sawa??”
Arnold akaumia moyo! Akajua tu Sherry alikataa kwenda kumuona. Akajilaumu na kujiona mjinga kwa kujidhuru sababu ya mwanamke ambae hakustahili upendo wake.
Lakini hata angeendelea kujuta tayari alikwisha chelewa. Hali yake ilikua mbaya sababu ya maamuzi yake magumu aliyo yachukua.
Alipo ukata mshipa wa damu, mishipa mingine ilishindwa kupeleka damu kwenye moyo. Ndo maana akawa anapata ugumu kwenye kupumua.
“niambie…. Ukweli…!”
Aliyah alimsikitikia sana kaka yake, alipangusa machozi yake kwa mkono mmoja kisha akamuambia
“Kaka! Sherry sio mwanamke anae kufaa! Hakua anakupenda hata kidogo! Kilicho mleta kwako ni pesa tu na kwakua alizipata basi akaona huna tena thamani! Najua unaumia ila amenambia hakupendi!”
Arnold alitoa chozi la uchungu, akamuangalia mdogo wake kwa macho ya huruma kisha akasema
“Nisamee… kaka … yako maana… nimefanya maamuzi…. Magumu kweli! Ninge kusikiliza… mapema haya yote yasinge tokea!…. Nisamee pia…. Sababu…. Nitakuacha mwenyewe!…….. Natamani…. ningeona mafanikio yako…. Na kizazi chako”
“Usiseme ivo kaka.! Kaka usiseme ivo”
“Nisamee….”
Pale pale mashine ilitoa mlio mkali na mistari iliyokua inapanda na kushuka ikawa flat kuashiria tayari alisha fariki.
Aliyah alihisi mwili wake wote ulikua mzito ghafla! aliona giza kila mahali. Alidondoka chini na kupoteza fahamu.
Kishindo cha Aliyah kudondoka ndicho kilicho washtua Najma pamoja na Morris walio kua nje. Walipo ingia ndani walimkuta Aliyah yupo chini hata hajitambui. Ikabidi waite manesi walio mchukua Aliyah na kumpeleka chumba kingine huku haraka wakimpa huduma ya kwanza.
Alipokuja kuzinduka tu cha kwanza aliulizia kuhusu kaka yake. Alidhani pengine alicho kiona kilikua ni ndoto ila haikua ivo. Arnold alifariki kweli.
“hapana….hapana…..hapana….” Aliyah alianza kupiga kelele akiwa kama mtu alie changanyikiwa yaani.
“Hawezi kufa… Najma kaka yangu hawezi kufa akaniacha peke yangu! Hawezi kufaaaa! Mimi sina ndugu yoyote yule, kaka kwanini umeniacha! Nitakaa na nani mimi! Nitaishije jamaniiiii”
Aliyah kitu pekee alicho kifanya mda huo ni kuzidisha kilio na kupiga kelele nyingi. Alizidisha kilio cha uchungu hadi madaktari wakaona ni bora wampige sindano ya usingizi ili aweze kutulia.
Basi taarifa za kifo cha Arnold kilisambaa kila kona kuanzia kwa rafiki zake mpaka ofisini kwake alipokua anafanyia kazi.
Zilienda hadi zikamfikia Sabra rafiki wa Sherry! Alihuzunika mno na alijua wazi kifo cha Arnold kilisababishwa na Sherry.
Alimfuata mhusika mpaka hosteli, alimkuta ndo ametoka kuoga anapaka mafuta ili aweze kuvaa nguo.
“Sherry umepata habari?”
“Habari gani?”
“Kuhusu Arnold”
“ivi sabra hupendi kuniona na Amani! We furaha yangu inakuchoma choma kwanini?? Si nilikuambia sitaki kabisa kusikia habari za huyo mpuuzi??”
“Huna namna hizi habari lazima uzisikie maana nisipo kuambia mimi lazima tu utazisikia huko nje”
“Ok! Habaari gani? Na ziwe zina maana”
“Arnold amefariki jioni hii”
Mkono wa Sherry ulikua mzito ghafla, akadondosha mafuta chini huku joto lake la mwili likiongezeka
“umeona sasa? Ichi ndo ulichokua unakitaka sio? Kaka wa watu kafariki? Kwani ungeenda kumuona ungepungukiwa na nini?”
“Sabra acha kunitania”
“linapo kuja swala la uhai wa mtu siwezi tania hata kidogo! Arnold amekufa”
“Mungu wangu” Sherry alikaa chini huku moyo ukimuuma sana. Alikumbuka namna ambavyo Aliyah alimuomba akamuone kaka yake lakini aliishia kumletea Dharau
“yote ni kwasababu yako”
“Nini nimefanya mimi!…. Ni nini nimefanya…..”
“Sherry ninae mjua mimi hana roho mbaya kiasi icho! Ila kwa Arnold uligeuka mnyama bila sababu ya msingi na wakati kaka wa watu hakukufanyia kitu kibaya zaidi ya kukupenda! Bila yeye usingeweza kulipia ada, kulipia hosteli wala kumtumia mama yako hela! Amekufanyia vitu ambavyo hata Clayton hawezi kukufanyia! Ila badala ya kumlipa wema ukamlipa mabaya”
“Basi Sabra… inatosha sasa! usiongee tena”
“imekuchoma eeeh! Natumaini huo utakua mwanzo tu”
Sabra alitoka na kumuacha Sherry akiwa amepigwa na bumbuwazi. Alimfikiria Arnold mno mpaka akajikuta afanyi kitu kingine zaidi ya kumuwaza.
Sio icho tu hata usiku hakuweza kufunga jicho maana Arnold alimjia usingizini akimlilia. Roho ikazidi kumuuma Sherry, akaanza hadi kulia na kusononeka kila wakati.
Akaona aende kwenye mazishi ya Arnold, kama hakuweza kuokoa uhai wake basi angalau angeenda kumpumzisha kwenye nyumba yake ya milele.
“Unaenda wapi?” Sabra alimuuliza
“kwenye mazishi ya Arnold! Si anazikwa leo sio?”
“ndio!” Sabra alimtazama Sherry
“acha nikamzike”
“We Sherry unapenda matatizo sio?? Unajipeleka huko ili nini? Unadhani wakikuona huko kwenye mazishi utakua salama?? Na hivi wana hasira na wewe! Usiende tu shoga angu”
“Nisipoenda nahisi nitaendelea kuteseka usingizi! Acha niende Sabra”
“Sawa we nenda”
Sherry akamalizia kujitanda mtandio wake, akachukua pochi yake na kuondoka. Moja kwa moja akaelekea alipokua anaishi Arnold.
Alipofika alikumbuka kipindi alipokua nae kwenye mahusiano alishawai mpelekega pale, walikula na kunywa kisha Arnold akampa simu mpya.
Badala ya kutembea Sherry akabakia akitoa machozi tu! Kwa mbele aliona umati wa watu ukiimba nyimbo za mapambio sababu mwili wa marehemu tayari ulikua umeshafika.
Basi Sherry akajikaza na kuendelea kutembea hadi akafika eneo la msiba. Watu walikua wengi ila sio sana! Alikaa nyuma kabisa kwenye turubai la mwisho huku akijitanda vizuri na mtandio wake ili asijulikane.
Mchungaji alifika na alianza kuendesha ibada! Ibada ikiwa inaendelea Aliyah yeye alikua amekaa chini kabisa kwenye sakafu akilia.
Kama kuna kipindi kigumu alicho kipata Najma ni icho kipindi cha Aliyah kufiwa. Alikua na wakati mgumu sana wa kumtuliza.
Kwa bahati mbaya Aliyah akiwa kwenye majonzi macho yake yalitua kwa Sherry. Mbali na kujificha kwenye mtandio haikumfanya Aliyah asimtambue.
Taratibu Aliyah alinyanyuka pale chini na kufanya watu wamshangae. Kisha kwa haraka alipiga hatua ndefu na kwenda kumvamia Sherry pale alipokua amekaa.
“Umefata nini hapa??? Umekuja kufanya nini hapa si naongea na wewe??”
Sherry alishindwa ajibu nini zaidi ya kuzuia ngumi zilizokua zinarushwa na Aliyah.
“Umekuja kuhakikisha kama Amekufa??? Amekufa sasa! Umefurai?? Ameshakufaaa kaka yangu ameshakufaaa” Aliyah alitamani aendelee kumpiga sema ni vile Najma aliwai akamdaka
“Aliyah nisamee!… nisamee mimi”
“Nikusamee?? Unasemaje wewe??? Nikusameee??? Umesababisha kifo cha kaka yangu alafu unasema nikusamee??? Msamaha wangu ndo utarudisha uhai wake?? Nakuuliza atarudi tena??”
“Aliyah…”
“Umekuja kuhakikisha kama kafa sio maana icho ndicho ulichokua unakitaka”
“moyo unaniuma Aliyah! Najua nilikosea! Nashindwa hata kulala usiku please nisamee”
“na moyo haujakuuma bado! Nakuahidi Sherry! Nakuahidi mbele ya huu umati, lazima nitakuja kulipiza! Kifo cha kaka yangu hakita enda ivi ivi laziima utalipia! Kama ambavyo umeichukua furaha yangu na mimi nitaichukua furaha yako! Kama ambavyo umeinyang’anya furaha yangu na mimi nitakunyang’anya furaha yako na kukuacha na machozi kama mimi”
Maneno yale yalikua mazito na yalisemwa toka moyoni kwa Aliyah. Sherry aliposikia vile akatoka mbio mbio akaondoka.
Nakuja………
SEHEMU YA : 5
Kila mtu anakitu ambacho kinampa furaha ama mtu ambae anampa furaha. Kwa Aliyah furaha yake ilikua ni kaka yake ambae alifariki.
Kwa Sherry furaha yake ilikua ni Clayton. Sasa kama Aliyah aliapa kumnyang’anya furaha yake ina maana atamnyang’anya Clayton???
Sherry hakutaka kuamini, uoga ukamuingia. Alidhani Huwenda Aliyah angemdhuru Clayton wake na kumuacha na kilio.
Kwakua aliogopa sana, baada ya kutoka pale msibani alikwenda ofisini kwa Clayton. Kalikua nika ofisi kadogo tu kalicho husika na masuala ya udobi! Yani kufua na kupiga pasi nguo za watu.
Clayton ndo alikua akimiliki hako ka ofisi. Basi Sherry alipofika alimuona Clayton yupo bize anahangaika kunyoosha nguo za wateja.
Alisogea mpaka alipokua, akapitisha mikono yake na kumkumbatia kwa nyuma kisha akasema
“nimeku miss sana Baby”
Taratibu Clayton aligeuka na kumtazama Sherry kwa macho yaliyo jaa mapenzi. Aisee niseme tu ukweli, Clayton ni mwanaume na nusu! Kuanzia muonekano wake mpaka moyo wake! Alafu alivutia mno ni vile alikosa matunzo! Angepata matunzo japo kidogo tu basi angekua tishio kubwa kwa wadada wa Dar.
“Mbona umevimba mama?? Nini shida”
Sauti ya Clayton ikausuuza moyo wa Sherry!
“Amna!”
“Ulikua unalia sio? Umelia kwanini?”
“Amna baby nilikua msibani tu!”
“Oooh pole sana mamaa! Umekula??”
“hapana! Baada ya kukuona upo salama nimeshiba kabisa”
Clayton akatabasamu na kufanya dimpoz zitokee kwenye mashavu yake
“aaahm… nina chakula kidogo kwenye kontena! Tule kwanza sawa mama?”
“sawa”
Clayton alitoa kontena alilo lijaza wali maharage! Akatoa kijiko kimoja ambacho wangeshea wote wawili kisha akaanza kumlisha Sherry!
Naaaam, ile sasa ndo furaha ya Sherry. Yeye na Clayton walikuta kitambo sana kipindi Sherry akiwa anaanza chuo. Walipendana na kuamua kuanzisha mahusiano.
Ila kama mnavyo jua Clayton hakua na hela ya kutosha ya kumhudumia Sherry kwa kila kitu! Hiyo ndo sababu ya Sherry kuanzisha mahusiano na Arnold.
Alimkubali tu kwakua alikua na vijisenti ambavyo vingeweza kuyasogeza maisha yake. Na baada ya kupata alicho kipata, Sherry akamtelekeza Arnold kwa namna ambayo ilipelekea Arnold kujiua.
Na hayo yote aliyafanya kwa siri sana bila Clayton kujua. Aliogopa siku ambayo angejua kuwa alimsaliti hapo kabla basi ungekua mwisho wa mahusiano yao na yeye hataki ilo litokee.
Kutokana na kitisho alichopewa na Aliyah, Sherry akawa anachunga sana usalama wa Clayton! Alitaka kujua alikua wapi na alikua akifanya nini. Na hata Clayton hakujali sababu alidhani mpenzi wake ana wivu sana ndo maana alikua akifanya vile.
Basi Sherry akawa anasubiri kama Aliyah angemfanyia Clayton chochote ila haikua ivyo. Mwezi uliishia, ukamalizika mwezi mwingine bado pakawa kimya.
Ndipo hapo akajiridhisha kuwa hakuna kitu ambacho Aliyah angeweza kumfanya mpenzi wake. Lakini kumbe wakati huo Aliyah hakua vizuri kisaikolojia.
Ni kama akili yake ilichanganyikiwa kabisa, akawa anafanya vitu ambavyo sio vya kawaida. Najma akishirikiana na Morris wakampeleka kwa mwanasaikolojia.
Aliyah akaanza kupata matibabu ya afya akili mpaka akakaa sawa kabisa. Ila tangu alipokua sawa Aliyah akaacha kucheka wala kutabasamu. Mda wote alikua serious na ikawa ngumu kwa rafiki zake kujua kama alifurai ama alichukia.
“Una mpango gani?? Si urudi chuo?” Najma alimuuliza Aliyah walipokua wamekaa sebuleni
“ile scholarship ya Canada bado ipo?”
“Ndio! Ikipita miezi mitatu bila kusikia chochote toka kwa mlengwa basi wanaifuta”
“Oooh!”
“unafikiria nini?”
“Nataka niende Canada nikaendelee kusoma”
“Aliyah! Usiende bhana!” Najma alijawa na huzuni
“sina namna! Maana hata nikibaki bado sitakua na uwezo wa kuendelea kujilipia ada mwenyewe! Ila kwakua nimepewa ufadhili wa kusoma bure Canada! Acha niende huko” aliongea kwa sura yake iliyojaa userious
“jamani! Nitabaki na nani sasa?”
“Morris yupo”
“Sijamzoea Morris kama nilivyo kuzoea wewe Aliyah! Alafu ulisema tutamlipizia Sherry”
“kisasi changu kwa Sherry kipo pale pale! Bado sijasahau kuhusu ilo!… Najma unajua raha ya kulipiza kisasi inabidi kwanza uwe na hela, kwa sasa bado sina chochote kwaiyo nikilipiza kisasi sasa ivi nitaonekana kama kichaa”
“Mhhh! Sawa! Sijui ni kitu gani ulicho kipanga kichwani kwako ila jua my dear siku utakapo nihitaji nikusaidie kulipiza kisasi chako nipo tayari”
“Thanks Najma”
“Sasa si utabasamu angalau!”
Aliyah hakutabasamu, alibakia mkavu vile vile na kumfanya Najma azidi kumhurumia.
Basi taratibu za Aliyah kwenda Canada zilianza. Alipata passport na visa na baada ya kila kitu kuwa tayari alijiandaa kwa safari.
Siku hiyo Morris na Najma walimsindikiza Aliyah mpaka airport! Walimuaga vizuri huku Najma akiongoza kwa kutoa machozi.
“Jamani Aliyah”
“Bye Najma!”
Aliyah alivuta begi lake na kuchanganyika na abiria wengine kuelekea panapo ndege.
“Morris! Aliyah kaondoka ujue!”
“Muache aende! Unataka aendelee kubaki hapa aendelee kuchanganyikiwa zaidi?”
“We si unampenda Aliyah? Sasa kwanini umemuacha aende! Alafu ujue Canada kuna mahandsome wa kizungu”
Morris alichukia na kuumia kwa pamoja. Alikua kweli anampenda Aliyah na alishindwa kumuambia sababu ya mikasa na misuko suko iliyokua inamkumba.
“Nani anampenda?? Mimi simpendi Aliyah” alikana
“Mimi naona kabisa machoni mwako! Acha kunifanya mtoto”
“Najma embu jiheshimu basi tupo airport ujue”
“Najua! Ila si useme unampenda Aliyah”
“ndio! Ndio! Ndio nampenda! Nampenda! Aya umefurai” Morris aliondoka kwa hasira akapanda bajaji yake na kuondoka bila hata ya kumsubiria Najma.
“Heee ndo ameniacha?? ila hakuna shida nishapata uhakika anampenda Aliyah wangu!” Najma alitabasamu.
Na icho ndicho kilicho tokea miaka 6 iliyopita. Tumeshajua sababu gani imepelekea kisasi baina ya Aliyah na Sherry.
Basi wapendwa ikawa miaka 6 imepita toka Aliyah alipokwenda Canada. Huku nyuma Najma alimaliza chuo akawa anahangaika kutafuta kazi!
Kwa bahati nzuri alikuja kupata nafasi nzuri kwenye kampuni moja ya mvinyoo (wine) iliyokua imefunguliwa kwa mara ya kwanza Tanzania.
Nae Morris aliajiriwa kwenye kampuni hiyo hiyo aliyo ajiriwa Najma. Na kwanini watu hawa wawili waajiriwe kwenye kampuni moja tena ikiwa Morris hakua na elimu yoyote?
Ni kwasababu kampuni iyo ilimilikiwa na Aliyah. Baada ya Aliyah kumaliza masomo yake nchini Canada, alifanikiwa kupata kazi Italy.
Akiwa huko akajifunza mawili matatu kuhusu mvinyo. Ile biashara ikamvutia sana, akaamua kujaribu na yeye. Niseme Mungu alikua upande wake sababu ile biashara ilimuendea vizuri kuliko alivyo tarajia.
Akaacha kazi yake na kuweka umakini katika utengenezaji na uuzaji wa mvinyo. Biashara ikazidi kukua, akafungua kampuni yake huko huko Italy.
Alipohisi kampuni imekua kubwa kwa kiasi alicho kitaka yeye ndipo akaihamishia Tanzania. Ndipo apo akamuajiri rafiki yake kipenzi Najma pamoja na Morris.
Sasa siku moja mchana Najma alionekana kuwa kwenye pilika pilika nyingi sana. Alimfuata Morris kwenye eneo lake la kazi akamkuta amevunja kabati kuliko maelezo. Najma alicheka kweli na kumuambia
“umesikia Aliyah anakuja basi ukaamua kupiga pamba”
“Fata mambo yako Najma”
“si ukweli!”
“We mbona umependeza? Nimekuuliza kuhusu ilo?”
“Mimi kupendeza ni kawaida yangu ila wewe sasa ni nadra sana! Weeee nilikua sijaona…. Kumbe mpaka ndevu umenyoaa”
“Najma tunaenda airport ama hatuendi??”
“Tunaenda baba yangu! Tunaenda maana wewe ukikasirika unaweza ukaenda mwenyewe ukaniacha”
Morris hakujibu, alipiga hatua ndefu kuelekea kwenye gari huku Najma akimfuata nyuma akiwa anakimbia.
Nakujaaaa……..
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote