Kijakazi Wa Mume Wangu Kipofu

book cover og

Utangulizi

AMA KWELI KUNGURU HAFUGIKI
Sijui kwanini wanawake wengi wazuri hawawezag kutulia kabisa, hata kama wamepata mtu sahihi sana kwenye maisha yao..
Kuna muda mabint wengi wanachezea shilling kwenye tundu la choo kwa upuuzi wao wenyewe, maana unakuta bint anahudumiwa vzr na anapata kila anachotaka ila kutokana na matatizo ambayo mwanaume kapata anataka kuchepuka...
Hapa tunamzungumzia bint natalia, mwanamke mwenye urembo wa kipekee sana, anakuja kukutana na hyden nq kwa mapenzi makubwa hyden anamuhudumia na kumchumbia, hyden anakuja kupata ajali na kupofuka macho kabla ya ndoa, natalia anaamua kumletea hyden mfanyakazi na yeye anaanza kudanga akijua mumewe mtarajiwa haoni, kumbe anamtengenezea njia mfanya kazi wake wa ndani ya kuwa na mumewe badala yake..
Kwa uhondo zaidi usikose simulizi hii ya kusisimua ya kijakazi wa mume wangu kipofu

KIJAKAZI WA MUME WANGU KIPOFU 1
MTUNZI SMILE SHINE

Anaitwa Natalia ni binti wa miaka 23 , Natalia ni binti mrembo sana ana sura nzuri yenye mvuto lakini umbo lilikuwa la kawaida, watu wengi wamekuwa wakimsifia kutokana na uzuri aliokuwa nao pia mwenyewe alijitambua kuwa ni mrembo kuna wakati alijiangalia kwenye kioo na kusema
"Namshukuru Mungu kwa uumbaji wake kwakweli amenibariki na asante kwa mama kwa kunizaa.
Mama yake alikuwa kasimama mlangoni akimuangalia.
" Kweli nimeamini wewe mtoto ni mpumbavu wenzako wako barabarani wa bahasha zao kutafuta kazi wewe kila kukicha unaongea na kioo.
" Jamani mama si nilikuwa namuangalia tu.
" Kuna faida gani unapata kujiangalia, hebu toka katafute kazi huko.
" Mama kusema kweli mimi kuhangaika na bahasha mkononi nimechoka bora nifanye mambo yangu mengine .
" Mambo gani ? Yani kwenda kuzunguka siku mbili umeshakata tamaa.
" Huko kwenye maofisi kuna kera wewe hujui tu.
" Unatakiwa kutanguliza Mungu kwanza mwanangu.
" Sawa acha niende.
Natalia alizunguka sana bila kupata kazi kwani mara nyingi aliishia kulala na maboss lakini mwisho wa siku alikosa kazi. Hapo ndipo alipoamua kuweka vyeti pembeni na kuanza kuzurura mitaani.

Kutokana na uzuri wake wanaume wengi na wakila rika vijana kwa wazee walikuwa wakimfuata na kumtaka kimapenzi, kwa upande mwingine aliona urembo wake ni kama fursa hivyo hakuwa na budi kuutumia urembo wangu kwa kuwa na wanaume tena wale wenye pesa wanaoweza kumgonga pesa ndefu.

Siku moja Natalia alienda kwenye kampuni moja na ya simu kwaajili ya shida zake binafsi , alikutana na muhudumu nakatatua shida zake wakati anaondoka akiwa anashuka kwenye ngazi aliteleza na kutaka kuanguka kwa bahati nzuri kulikuwa na kaka mmoja mtanashati aliwahi kumdaka.
" Vipi haujaumia? Yule kaka alimuuliza huku wakiwa wanaangaliana usoni. Natalia alijinyanyua na yule kaka akamuachia.
" Asante nipo sawa. Alijibu Natalia huku akiwa anajiweka vizuri yule kaka alikuwa bado kasimama anamuangalia usoni Natalia aligundua kuwa yule kaka atakuwa kuvutiwa na uzuri wake hivyo nae akaanza kumkagua kuangalia kama ataweza kukidhi vigezo vya kuwa nae. Akiwa bado anamkagua akasikia kuna dada akamsalimia yule kaka.
" Habari za asubuhi boss.
Yule kaka alimgeukia yule dada na kujibu .
" Salama.
" Samahani boss ratiba yako ya muda huu ni kukutana na wafanyakazi wote na zimebakia dakika tano kikao kianze.
" Ok nakuja.
Yule dada aliondoka na kuwaacha wao wawili wamesimama . Natalia aliachia tabasamu baada ya kujua jamaa ana cheo pale akanyoosha mkono wake na kumpatia.
" Naitwa Natalia.
Yule kaka alitabasamu kisha akampatia mkono wake na kujitambulisha
" Naitwa Hayden.
" Waooo jina zuri sana nakupenda hili jina , mr Hayden nimefurahi kukufahamu pia nashukuru sana kwa kunisaidia maana bila wewe yangekuwa mengi saizi.
" Usijali karibu.
" Asante, mimi nimeshapata huduma nilikuwa naondoka.
Hayden alijipapasa kwenye mifuko yake ya suruali kama vile alikuwa anatafuta kitu , baada ya kukosa alichukua peni iliyokuwa kwenye mfuko wake wa shati kisha akashika kiganja cha mkono wa Natalia kisha akaandika namba zake za simu.
" Naomba unitafute.
" Sawa. Alijibu Natalia kwa sauti ya chini tena huku akitabasamu maana kila kitu lilienda sawa na aliamini Hayden ameshaingia kwenye mitego yake na kutoka mpaka atake yeye.

Siku zilienda Natasha na Hayden walikuwa wanawasiliana pia walianzisha mahusiano ya kimapenzi, Natasha alihakikisha hafanyi kosa alinionyesha mahaba ya kila aina mpaka Hayden akapagawa akawa hasikii wala haoni .
Hayden aliweka wazi mahusiano yake kwa kila mtu ndugu jamaa na marafiki walijua uhusiano wao pia alimfungulia biashara ya vifaa vya umeme pamoja na saloon.
Kwenye duka la umeme aliajiri vijana , saloon alikuwa mwenyewe pamoja na wasaidizi wachache.

Siku moja Natalia na Hayden walitoka wakaenda club wakiwa huko Natalia alikuwa akichanganya na watu na kumuacha Hayden akishangaa shangaa. Alikuja dada mmoja na kukaa pembeni yake .
" Kaka mbona unaniacha mpenzi wako anacheza na watu wengine kwani wewe huna wivu?
Hayden alitia tabasamu lenye madharau flani kisha akasema.
" Kwani ni dhambi kucheza na watu wengine?
" Oooh nilijisahau sio dhambi na je inakuwaje kama una share nao kwenye kumega tunda?
Hayden alikunja uso akasema
" Una maana gani kusema hivyo?
" Au basi ngoja tukacheza kwanza. Alijibu yule dada kisha akanyanyuka na kutaka kuondoka, Hayden alimshika mkono na kumuuliza tena
" Utaniambia au utaendelea kuniacha njia panda?
Yule dada alimuangalia kisha akashusha pumzi alafu akasema
" Kaka sio kila ndege wote wanaliwa mi dege mingine haziliwi inakupa mizoga.
Yule dada alisema kisha akavuta mkono wake na kuondoka huku alimuacha Hayden njia panda hajui aelekee wapi.
[1/28, 4:08 PM] K. Hassan: Hayden aligeuka kumuangalia Natasha akamuona yuko bize anacheza huku maungo yake ya nyuma yakiwa yamegusana na mwanaume aliekuwa anacheza nae. Hayden alishikwa na hasira akamfuata.
" Tuondoke.
Natalia alijifanya hasikii alimshika mkono na kumvuta nje.
" Una nini lakini?
" Muda umeenda tunatakiwa kuondoka.
" Jamani sasa ndio nini unajua ndio kumeanza kuchangamka.
" Ulianza kuchangamka tangia tumekuja sasa umetosheka.
Natasha alikubali kuondoka kwakuwa alikuwa kalazimishwa .

Hayden aliyefikiria sana maneno ya yule dada na kuanza kuyafanyia kazi. Kwanza aliamua kumchumbia Natalia kisha akawa anaishi nae nyumbani kwake kama mke , Pili alianza kumtembelea saloon kwake kwa kushitukiza ili aweze kugundua chochote.
Siku moja Natalia alikuwa chumba cha massage na mwanaume wake wakiwa wanafanya mambo yao mara ghafla akasikia mlango unagongwa kwa fujo . Alikurupuka kutoka kwenye kitanda akawa kasimama na kuvaa nguo zake .
" Kuna nini? Aliuliza yule mwanaume
" Sijui.
Mlango uligongwa tena safari hii ilisikika sauti ikisema
" Dada toka haraka mume wako amekuja.
Natalia alichanganyikiwa alitamani ardhi ipasuke aingie.


KIJAKAZI WA MUME WANGU KIPOFU 2
MTUNZI SMILE SHINE

Yule mwanaume alinyanyuka akauliza
" Kumbe mume wako huwa anakuja huku?
" Ndio lakini leo alitoka nje ya mji hakupaswa kuwa hapa.
" Sasa tunafanya je unajua mimi ni mume wa mtu ?
" Hata mimi uchumba wangu utakuwa matatani na sasa haipaswi tupoteze muda.
Aliongea Natalia huku akifungua mlango.
" Yuko wapi?
" Itakuwa yupo huko maana wakati nakuita alikuwa kashika kwenye gari.
" Sawa ingia huko ndani haraka.
Natalia alimwambia yule mfanyakazi wake (merry) kisha yeye akawa anaenda kumuangalia Hayden.
" Hallow baby!
Alisema na
Natalia huku akitabasamu lakini Hayden hakuonyesha hata tabasamu la uwongo alikuwa kamkazoa macho.
" Vipi hizo nywele mbona zimetimia , zipo ovyo?
Na kweli nywele za Natasha zilikuwa zimevurugika.
" Aaaaa nilikuwa nataka kuosha ikatokea nimeitwa na mteja huko chumba cha massage.
" Ulikuwa na mteja huko chumbani?
" Sikuwa nae mimi yupo na merry ila kulitokea tatizo nikahitajika niende huko.
" Sawa. Hayden alishikwa na maelezo ya Natasha.
" Vipi mpenzi mbona upo hapa na iliniambia kuwa leo utasafiri?
" Ilikuwa hivyo lakini wameenda watu wengine .
" Sawa karibu sisi tupo tunapiga kazi.
" Sawa.

Hayden akiendelea kufanya uchunguzi lakini hakufanikiwa kumfumania ila alikuwa akisikia maneno kutoka kwa watu wa pembeni na baadhi ya ndugu wakimwambia achunguze sana mwanamke wake.
Siku moja Hayden alikuwa kakaa na kaka yake Harry wakawa wanaongea.
" Kaka unajua nampenda sana Natalia lakini sielewi kuna muda nafikiria mpaka naona kichwa changu kinataka kupasuka sielewi nifanye maamuzi gani .
" Kama unaona anakusumbua kwanini usimuache?
" Nikisema namuacha hivihivi itakuwa namuonea natakiwa kumuacha nikiwa na ushahidi natakiwa kumkuta kwenye mambo yake.
" Mmmh sijui nikushauri nini ila endelea kuwa na Subra.
" Au nifunge nae ndoa tu.
" Kumbuka ndoa ni kifungo na sio jambo la mzaha hata kidogo sio unaowa leo unaacha kesho. Ukisikia pingu za maisha ujue hiyo ndoa ni milele unatakiwa uvumilivu kwenye kila kitu ndio maana kwenye kufungisha ndoa wanasema kuvumiliana kwenye shida na raha.

Maneno ya gari ni kama yalimkatisha tamaa Hayden.
" Sasa nafanya nini?
Harry alicheka huku akiwa anamuangalia
" Hilo ndio tatizo la kuwa na mwanamke mzuri inajikuta una washirika kibao.
Hayden aliishia kuguna.
" Nakutania bwana , hutakiwi kukata tamaa endelea kuchunguza na kama umesema kuna mambo mengi kaacha huenda atabadilika .

Natalia alikuwa saloon na mashoga zake wakawa wanapiga story.
" Wewe Natalia unajua za mwizi ni 40 ipo siku Hayden atakukamata.
" Kunikamata mimi anatakiwa kufanya kazi sana .
" Lakini kwanini usitulie mwenzio anakupenda .
"Ni kweli ananipenda na mimi ananipenda ila kuacha mambo yangu ghafla kama mvua za Masika siwezi nimeshakuwa tena mwenzenu natakiwa kupewa muda.
Siku zilizidi kwenda Natalia alikuwa kazini kwake akihudumiwa wateja wake mara simu yake iliita .
" Merry nipe simu yangu.
Merry alienda kuchukua simu mabatini na kumpatia.
" Harry anapiga kuna nini mpaka anipigue ? Aliuliza Natalia kisha akapokea ile simu.
" Vipi shem.
" Safi uko wapi,?
" Nipo saloon.
" Una habari gani kuhusu Hayden?
" Sina habari yoyote .....
" Amepata ajali na sasa yupo hospitali ya st joseph ...
Natalia alishitushwa sana na hizo taarifa
" Mungu wangu imekuwaje mpaka kapata ajali, ameumia?
" Kaumia kidogo anapatiwa matibabu.
" Nakuja sasa hivi.
Natalia alikata simu na kumtaka radhi mteja
" Samahani nimepata matatizo mume wangu kapata ajali merry atakumalizia.
" Jamani pole sana.
Kila mmoja alimpa pole , Natalia alichukua mkoba wake na kwenda moja kwa moja mpaka hospitali ya St Joseph akamkuta Hayden kafungwa bandeji kwenye majereha pia alikuwa Kalala kitandani ndugu zake wakiwa wamemzunguka mama yake mzazi alikuwa analia .
" Jamani Hayden anaendeleaje?
" Kama unavyomuona .
Natalia alianza kulia huku akimshuka
" Hayden wangu ilikuwaje mpaka ukapata ajali...
" Amechinjwa sindano ya usingizi kutokana na maumivu alivyokuwa anasikia hivyo hapo amelala.

Harry alimshika mkono Natalia wakaenda nje kuongea.
" Shem haki ya Hayden imebadilika hata kuwa kama ilivyotokea mwanzo.
" Ki vipi shem?
" Hayden kapoteza uwezo wa kuona.
" Nini? Inamaana Hayden amekuwa kipofu?
" Atadumu kwenye hiyo hali kwa muda tu ila badae atarudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kufanyiwa matibabu .
Habari za upofu wa Hayden zilimshitua sana Natalia akawa kazubaa.
" Shem unampenda Hayden? Harry aliuliza.
" Ndio nampenda sana na nina shukuru kuwa yupo hai .
" Utamvumilia na hali aliyokuwa nayo?
" Shem unanichukuliaje unafikiri mimi sina utu? Hayden ni mwanaume wangu nitakuwa nae kwenye shida na raha matatizo aliyonayo hayawezi kusababisha mimi na yeye kutengana nitampenda Hayden mpaka kufa kwangu na nitamuhudumia kwa hali yoyote. Aliongea Natalia huku machozi yakitiririka mashavuni kwake.
Harry alimkumbatia na kumfuta machozi.
" Basi shem usilie.

Kesho yake Natalia alirudi hospitali akamkuta Hayden kakaa alimsogelea karibu na kumuita
" Hayden...
Hayden aliita jina la Natalia huku akipapasa hapo ndipo Natalia aliamini kweli Hayden haoni
" Natalia sina uwezo wa kukuona tena. Aliongea Hayden kinyonge Natalia alimuinea huruma akamkumbatia na kusema
" Usijali nipo pamoja na wewe.


KIJAKAZI WA MUME WANGU KIPOFU 3
MTUNZI SMILE SHINE

Baada ya siku tatu kupita waliruhusiwa wakarudi nyumbani. Natalia alimuhudumia akampa chakula na kumuonesha alipomaliza alimlaza kitandani kisha yeye akaenda kusimama dirishani na kuangalia nje kwa sekunde kadhaa kisha akageukia kwa Hayden alijikuta anaumia .
" Hiki ni nini kinatokea maishani kwangu mbona najiona nina mkosi yani kabla hata ya ndoa mambo yamebadilika huu ni mtihani mkubwa sana je na huyu mwanaume kipofu. Natalia alijilaumu lakini hakujua itakuwaje huko mbele.
Wazazi wa Natalia waliwatembelea nyumbani kwao kwajili ya kumpa pole mkwe wao.
Natalia na mama yake walikuwa jikoni wanapika.
" Natalia mwanangu umeona hali ya mwenzio unatakiwa kumuangalia, mtunzi mwenzio Hayden ni kijana mzuri sana hana ubaguzi akitoa sana kwenye familia yetu nakuomba mwanangu shikamana na mwenzio.
" Sawa mama nimekuelewa.
Alijibu Natalia lakini moyoni mwake ilikuwa ngumu kukubali.

Siku zilisogea Natalia alikuwa alijikaza mno kumuhudumia kwa kila kitu lakini akitoka hapo alienda kulalamika pembeni.
" Jamani mwenzenu nina mtihani mzito kila nikifikiria njia ya kujitoa kwa Hayden napata ugumu ukizingatia wazazi wangu wananisihi kila siku kuhusu kukaa nae.
" Kwani kuna tatizo gani wewe kumuhudumia kuhudumiwa kwasababu ndio mwanaume ulie mchagua.
"Ni kweli lakini sidhani kama nitaweza.
" Kwa kukuangalia tu huwezi shoga yangu alafu kwanini mtoto mzuri kama wewe uwe mtumwa wa kumuhudumia mtu ambaye hata ndoa hamjafunga achana nae asikuchoshe kwanza huu ndio utakuwa muda mzuri kwako fanya mambo yako kwa uhuru . Daniela alimshauri
" Daniela muogope Mungu hivi lingekufika wewe ungefanya hivyo au unampotisha tu mwenzio? Alisema Neema.
" Nani, mimi na hii roho yangu ningeweza vizuri kwasababu hata ili lingekuwa limemtokea Natasha huyo mwanaume angekubali kuwa nae?
" Daniela rafiki yangu inawaza mbali sana yani kwake na kuweka kwa muda tu baada ya hapo nitakuacha akabiliane na maisha yake siwezi kuendelea kuwa mtumwa.
Daniela na Natalia waliendelea kusapotiana ujinga neema akawa anasikitika na kumuonea huruma Hayden.

Siku moja Hayden akiwa mezani anakunywa chai alisikia Natalia akiongea na mtu kama vile alimueleza kazi za kufanya pale ndani.
" Na huyu ndio mpenzi wangu nikiwa sipo naomba umuhudumie , niangalie kwa kila kitu akitaka chochote mpatie.
" Sawa dada.
" Njoo umuine pia nikutambulishe.
Walisomea mpaka alipokaa Hayden yule msichana akasalimia kwa kunyenyekea
" Shikamoo
" Marahaba.
" Mpenzi huyu ni Balkisi ni dada wa kazi atakuwa alimuhudumia pindi nitakapokuwa nipo kazini.
Hili swala halikumfirahiaha Hayden .
" Natalia nataka tuongee .
" Sawa, Balkisi nenda kaendelee na kazi.
" Sawa
Balkisi aliondoka anaenda kufanya kazi.
" Huyu mtu umeleta wa nini hapa ndani?
" Ni kwaajili ya kukusaidia na kufanya kazi hapa ndani.
" Kwani wewe huwezi?
" Mimi naenda kazini.
" Kwani ukirudi huwezi kufanya hizo kazi?
" Wewe baba hebu kuwa na huruma na mimi yani asubuhi mihangaiko na wewe alafu niende kazini nikahangaike na bado jioni nikirudi Makuwa nimechoka nianze kumuhudumia wewe jaribu kuwa na huruma usinifanye mtumwa bwana.
" Kwahiyo kumuhudumia imekuwa utumwa?
" Sikiliza Hayden wewe ndio unahitaji wa huyu mtu nafanya yote kwaajili yako na huyu binti atakuwa anakuja na kuondoka.
" Kwanini hujunishirikisha tangia mwanzo inajichukulia maamuzi mwenyewe?
" Ndio imeshatokea. Natalia aliachishwa na kelele za Hayden alienda kujiandaa akaenda saloon.
Kuanzia siku hiyo Natalia alikuwa bize na mambo yake na majukumu yote ya pale nyumbani alimuacha Balkisi.
Siku moja jioni Balkisi alimaliza kufanya shuhuri zake zote akamfuata Hayden akamwambia.
" Boss kuna chochote unahitaji nikusaidie?
" Hapana unaweza kwenda hayo mengine atakuja kufanya Natalia.
Balkisi aliendelea kusimama kwa muda kisha akasema
" Lakini alisema leo anaweza kuchelewa kurudi hivyo kama kuna chochote ungeniambia nifanye ili isipate shida badae.
" Asante kwa kujali kwako Balkisi ila wahi tu nyumbani.
" Sawa, kwaheri.

Baada ya Balkisi kuondoka Hayden alikaa mwenyewe kwa muda mrefu sana bila Natalia kutokea, alianza kupata wasiwasi akajikingoja kwa msaada wa fimbo mpaka nje alifika mlangoni na kumuita mlinzi.
" Tizo
" Naam boss
" Njoo.
Tizo alienda kwa kukimbia mpaka aliposimama Hayden.
" Sasa hivi ni saa ngapi?
Tizo alitoa simu yake ya batani akaangalia muda.
" Ni saa saba na nusu.
" Usiku huu atakuwa kaenda wapi? Aliuliza Hayden huku akiwa na wasiwasi.
" Hebu jaribu kumpigia simu .
Mlinzi alitafuta namba za Natalia kwenye simu yake alafu akapiga. Baada ya muda mlinzi akasema
" Simu yake haipatikani.
Hayden alipandwa na hasira na kuwaza kuwa Natalia amefurahia matatizo yake kwani imekuwa nafasi nzuri kufanya mambo yake kwa uhuru.
" Sawa nenda kaendelee na kazi, usiku mwema .
" Asante boss .
Hayden alirudi ndani na kwenda kulala kwenye kochi.
Alipitiwa na usingizi akiwa kajikunyata mpaka ilipofika asubuhi Balkisi alimkuta bado akiwa Kalala.
" Masikini kaka wa watu itakuwa Kalala hapa ona alivyojikunyata kwa baridi yani Natalia hana huruma kabisa. Alijisemea Balkisi kisha akaenda chumbani kuchukua shuka na kwenda kumfunika. Kitendo cha kumfunika Hayden alishituka na kuita Natalia.
" Ni mimi Balkisi.
" Ahaaaa, Natalia yuko wapi?
" Sijui ndio nimefika sasa hivi.
Moja kwa moja Hayden alijua Balkisi hajarudi nyumbani.
" Balkisi naomba uniandalie chai.
" Sawa.
Balkisi alienda dinning akakuta chakula alichokuwa kamuandalia bado kimejaa kwenye hotpot.
" Unamaana tangia alivyokuwa mchana hajala tena? Ngoja nikamuangalie chai haraka.
Alienda jikoni akaandaa chai na vitafunwa haraka kisha akaenda kumtengea.
" Boss chai ipo tayari.
" Sawa asante.
Hayden akipapasa fimbo yake ili aamke lakini haukuwepo alipokuwa jaiegesha ilianguka chini Balkisi alimsaidia kuokota na kumpatia mkononi kwake.
" Asante sana Balkisi.
" Usijali boss.
Wakiongozana pamoja mpaka dinning table Balkisi akamvuta kiti na kumsaidia akae alafu akamnawisha mkono Hayden wakaanza kula na Balkisi akaondoka kwenda kumuangalia nguo za kubadilisha pindi atakapokuwa katoka kaoga.

Mara Natalia aliingia na kwenda pale alipokaa Hayden.
" Vipi hali yako mpenzi?
" Natalia umetoka wapi na ililala wapi?
" Jamani kabla hata ya salamu umeanza na maswali.
" Sina haja na salamu yako nataka kujua ulilala wapi?
" Nililala kazini.
" Umeanza lini kulala kazini?
" Nimeanza jana kwasababu nilikuwa nina kazi nyingi hata hivyo nimerudi kuja kukuona na kujikumbusha kuwa unatakiwa kwenda hospitali kwaajili ya kwenda kuonana na doctor wako.
" Sawa tukitoka hospitali utaniambia sababu za kulala nje .
" Tukitoka na nani? Mimi siwezi kuacha biashara zangu tukaongozana wote hospitali huko utapelekwa na dereva pamoja na Balkisi.

KIJAKAZI WA MUME WANGU KIPOFU 4
MTUNZI SMILE SHINE

Kelele zao zilimfanya Balkisi atoke alikokuwa na kwenda sebleni akamkuta Natalia anampandishia sauti Hayden.
" Ndio nimeshasema kama hutaki kuelewa basi unafikiri tulifuata na kama makondoo Mtakula wapi na ukumbukwe mimi ndio nitakuwa nakuhzdumia au unataka nije kupata lawama kwa ndugu zako kuwa nilikupenda kwasababu ya uzima wako na sasa sijali kuhusu wewe.
" Nani kakwambia nina shida na pesa zako?
" Acha kiburi na jeuri Hayden kumbuka huoni, huna kazi utapata wapi pesa na hivyo vipesa vyako vya akiba vitaisha tu. Uuuuh kwanza sitaki kubishana na mgonjwa huenda hata kichwa chako iliathirika kwenye ajali , Balkisi naomba usinichoke ndugu yangu nisaidie kumpeleka Hayden hospitali kitakachotokea huko naomba unipigie simu.
Kwakuwa ilikuwa ni kazi na Balkisi anataka kulipwa pesa ilibidi akubali japo aliona sio sawa Hayden kufanyiwa kile alichofanyiwa na mpenzi wake .
Natalia aliwaacha akaenda chumbani kwake kuoga kisha akabadili nguo na kuondoka, Hayden alikuwa kakaa kwenye kochi hata chai ulimshinda kumaliza , Balkisi alimfuata pale alipokuwa kakaa akamwambia
" Boss naomba ule hata kidogo .....
" Hapana balkiz unafikiri hicho chakula kina wenza kupita kwenye koo langu na kwenda kutulia tumboni kutokana na hiki kinachofanyika na Natalia mwanamke niliamini ananipenda na mimi nikakutoa kwa moyo mmoja kwaajili yake.
" Pole najua unatumia lakini haipaswi kuendelea kujiumiza isipo kujali wewe yeye hawezi kukujali anza kujijali mwenyewe.
Hayden alishusha pumzi kisha akasema
" Sawa ila nitakula badae kidogo nenda kanihifadhie.
" Sasa ukajiandae twende hospitali.
" Usijali sitaenda leo nitaenda wakati mwingine.

Siku zilizidi kwenda na tabia ya Natalia ilizidi kubadilika kila kulipokucha kile kitendo kilikuwa kinamsumbua sana Balkisi ilifikia hatua alitamani kuacha kazi lakini alipomfikiria Hayden alimuonea huruma alihisi bila uwepo wake Kaka wa watu angepata tabu sana.
Siku moja Natalia alikuwa nyumbani na siku hiyo alimuandalia mume wake chakula na kumuhudumia kwa kila kitu , walikaa pamoja waliongea na kufurahi siku hiyo Hayden alionekana mwenye furaha sana tabasamu hakukukalika usoni kwake. Balkisi aliwaangalua kisha akasema
" Kumbe ana uwezo wa kumuhudumia mume wake na kumuonyesha mapenzi ila jeuri tu. Ilionekana wazi Hayden alikuwa akipenda sana Natalia ndio maana alipokuwa anafanyia mambo ya ajabu alikuwa akionekana kuumia sana.

Hali ya Natalia kumuonyesha upendo Hayden ilikuwa ni maelra moja kwa mwezi na alifanya vile kupooza tu . Mara nyingi alikuwa harudi nyumbani na hata akirudi alirudi muda aliitaka yeye.
Kwakuwa Balkisi aliona wale watu wanapendana na utoto ndio unamsumbua Natalia aliamua kuchukua jukumu la kumsaidia .
Siku moja asubuhi na mapema Balkisi akiwahi kazini akaandaa kifungua kinywa mapema na kuandaa mezani kisha akaendelea kufanya kazi nyingine.
Hayden alipofika mezani akipapasa na kufunua alihisi harufu nzuri .
" Chai ya leo niya tofauti sana ni muda mrefu sijanywa chai ya aina hii ni nani kaandaa?
" Ameandaa dada Natalia kabla hajaenda kazini.
Hayden aliachia tabasamu
" Waooo hii nzuri sana.
" Karibu boss furahia chai yako .
Hayden alikunja ile chai akiwa na furaha akijua ni mpenzi wake ndio kamuandalia kwa mapenzi makubwa .
Baada ya kumaliza kunywa chai alichukuliwa na dereva wakatoka , Balkisi akaona huo ndio muda mzuri wa yeye kuandaa chakula kizuri. Akikumbuka kuja siku Natalia alisema Hayden anapenda sana pilau yenye nyama nyingi tena nyama iwe imenona na sakafu ya kutosha hivyo alitumia huo muda kuandaa hicho chakula tena aliandaa kwa utulivu mkubwa mno harufu ya pilau alipenya mpaka nje.
Alimaliza kupika akapakua chakula chake na cha mlinzi wakala kisha akaandaa chakula cha maboss zake mezani.
Jioni Hayden alirudi akapitiliza moja kwa moja chumbani kwake alivua nguo akaoga alipomaliza alibadili nguo alizokuwa kasandaliwa na Balkisi, alipomaliza alishuka chini kwaajili ya kupata chakula.
Balkisi alimpakulia Hayden wakashindwa kujizuia akasema
" Leo nimeamua kujikinga nyoyo yangu humu ndani sio kwa kuumiza pua zangu namna hii.
Balkisi alicheka na kusema
" Mambo ya dada hayo leo kaamua kukufurahisha.
" Unamaana Natalia amerudi na akaingia jikoni kupika?
" Ndio lakini alitoka tena.
Hayden alivuta sahani akawa anakula taratibu alipomaliza kula alienda kukaa sitting room.
Baada ya muda Natalia alirudi akaungana na Hayden pale sebleni. akiwa na njaa akamuuliza Balkisi
" Hivi kweli kuna chakula humu ndani?
" Ndio kimebaki.
" Hongera mpenzi wangu leo umepokea chakula kitamu sana umenifurahisha sana siku ya leo kuanzia asubuhi, mchana unenionyesha kile ambacho haikuwahi kunionyesha tangia nilipoanza kujuana na wewe.
Natalia alishangaa inakuwaje anapongeza na kupewa sifa kwa kitu ambacho hakujui na hajakifanya
" Natalia wangu mbona unenyamaza wakati na kupongeza? Alisema Hayden na Natalia akaitika
" Asante mpenzi.
" Kila siku ungekuwa unanifanyia hivi basi ningenenepa. Alisema Hayden huku akitabasamu.
" Usijali mpenzi wangu nitafanya kwaajili yako si unajua nakupenda
" Najua asante kwa kunionyesha upendo.
" Usijali baby ni wajibu wangu. Ngoja niende chumbani nakuja sasa hivi.
" Sawa.
Natalia hakwenda chumbani kama alivyokuwa kaaga alienda jikoni kuonana na Balkisi.
" Wewe nini kimetokea leo hapa ndani?
" Mbona hakuna kitu kilichotokea.
" Namaanisha hii furaha ya Hayden inatokana na nini?
Balkisi alitabasamu kisha akasema.
" Dada unajua Hayden anakupenda sana na anatamani umuonyeshe mapenzi kama wanamke wengine wanaoonyesha mapenzi wa wenza wao sasa leo nimeamua kukuandalia kifungua kinywa kizuri na mchana nimempikia chakula kizuri nikamwambia imepikwa wewe kwaajili yake ndio maana amekuwa na furaha hivyo.
Natalia alitabasamu alafu akasema
"Wewe binti una akili sana sijakosea kukuchukua na kukuweka kwenye nyumba yangu ukiendelea kunifanyia mambo mazuri kama haya itafaidi sana.
Alisema Natalia alafu akafungua pochi yake akatoka noti mbili za elfu kumi akampatia.
" Hii ni malipo ya kile alichofanya nimependa unatakiwa kuendelea kuwa mbunifu zaidi.
Natalia aliondoka , Balkisi aliangalia zile hela alafu akafungua kichwa na kusema.
" Sina tamaa na hizi pesa ila nafanya haya kwaajili ya kumfariji Hayden ambae anapitia mazito kwenye hiki kipindi.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote