KAYLA (My STRAWBERRY)

book cover og

Utangulizi

Roho mbaya , chuki na ubinafsi vinaweza kusababisha mambo yako kuharibika na kupoteza kitu fulani na uvumilivu upole na mapenzi kwa watu kunaweza kusababisha ukapata kitu ambacho hujitegemea.
Hii imetokea kwa binti kayla ambae alikuw ananyanyaswa na shangazi yake mpaka kufikia hatua ya kumuuza kwa wanaume bahati anatokea mkombozi Rodney kijana ambae ni mgeni alikuwa anapita kwenda mbugani kutalii. Rodney anashuhudia kile anachopitia kayla na kuahidi kumsaidia.
Rodney anantorosha kayla kwa nia njema na kwenda kuishi nae mjini. Siku ya kwanza tu mzazi mwenzie na Rodney ambae anaitwa Victoria anatokea kumchukua kayla lakinihakuna binti yao Jada anatokea kumpenda sana kayla mpaka anampa jina la strawberry tunda analolipenda sana.
Victoria anampanda kichwani Rodney na kumnyanyasa ndugu zake huku akimnyanyasa kayla kitendo hicho kinamuumiza Rodney na anapojaribu kuongea Victoria anakuja juu kwasababu nyumba wanayoishi ni mali ya baba yake, Rodney anafanya kazi kwenye kampuni ya baba yake hivyo alijua kivyovyote Rodney hawezi kumuacha.
Chuki , na roho mbaya za Victoria kwa kayla zilikuwa zinajenga upendo mkubwa sana kwa kayla mwisho wa siku Rodney anaamua kumpandisha chumba kayla na hapo ndipo penzi linaloenda kuanza na Rodney anapata sehemu ya kutulizwa .
Je nini kitatokea Victoria anaolewa ? Na vipi kayla (strawberry ataendelea kuwa kwenye nafasi ya mchepuo au vipi?

KAYLA MY STRAWBERRY πŸ“1
MTUNZI SMILE SHINE

Ilikuwa Ni siku ya jumapili asubuhi Hali ya hewa ilikuwa ya mvua , mvua ilianza ilinyesha usiku kucha na bado iliiendelea kunyesha mpaka asubuhi , kulikuwa na baridi hivyo ilikuwa ngumu kwa watu kuacha mabrangeti yao .
Kayla ndio kwanza alivuta shuka na kujifunika vizuri ili kuendelea kulala usingizi wake mtamu ghafla alishitukia anapigwa Kofi la mgongoni alikurupuka na kukaa kitandani huku mikono yake ikipapasa mgongo wake.
" Wewe Cha uvivu ndio kwanza unakanyagia shuka utaenda sangapi kutembeza ndizi?ilikuwa Ni sauti ya ukali kutoka kwa shangazi yake.
" Shikamoo shangazi. Alisalimia kayla huku akiendelea kujipapasa sehemu aliyopigwa kibao
" Unaona shikamoo yako Ni Mali Sana? Mimi sifagilii hizo kelele zako ninachotaka pesa nenda kanitafutie pesa , toka hapa punguani wewe unachukua kuendekeza uvivu tu.
Kayla hakujibu alinyanyuka pale kitandani akaenda kupiga mswaki Kisha akachukua beseni lake la ndizi na kutoka kwenda kutembeza mitaani huku manyunyu ya mvua yakimnyeshea. Kila alipokuwa anakanyaga kulikuwa na matope pia utelezi mara nyingi alinusurika kuanguka. Lakini hakuwa na namna alienda hivyo hivyo ili afanye biashara apate pesa ili apate kuunusuru mwili wake kwa kipigo kutoka kwa shangazi yake pamoja na kulazwa njaa.

Kayla alilelewa na shangazi yake tangia akiwa mdogo baada ya wazazi wake kufariki. Kwenye nyumba ya shangazi yake waliishi watu watatu ambao Ni shangazi yake, safia binti wa shangazi yake ambae wamepishana mwaka mmoja hivyo safia alikuwa mkubwa kidogo kwa kayla
Safia alilelewa Kama yai hakuwa anafanya kazi Wala kutumwa sehemu , kayla alifanya kazi zote za nyumbani na kwenda kila sehemu aliyotumwa na shangazi yake.
Kayla alionewa Sana hata na Safia, ilifikia hatua safia aliamuwa kutembea na mwanaume wa Kayla na hatimae kumchukua kabisa akidai kuwa yule mwanaume sio wa hadhi yake anafaa kuwa nae yeye. Kayla alilia mwishoe alimuachia Mungu na kumuomba amuonyeshe njia ya kutoka kwenye hayo matesa.

Siku moja Kayla alikuwa kajilaza chumbani huku akiwa kashika picha ya Mussa ambae alikuwa mpenzi wake . Aliangalia Sana Ike picha huku machozi yakiwa yanamtoka maana Mussa alikuwa tegemeo lake kubwa alikuwa akimliwaza na kumpatia pesa kidogo kwaajili ya kufanya Mambo yake.
Safia aliingia huku akiwa ananyata ili kuona anafanya Nini , alimuona akiwa anaangalia picha ya Mussa alimpiga kibao Cha mgongoni. Kayla alishituka na Ile picha ikadondokea kitandani.
" Wewe mshenzi unajiliza Nini huku unaangalia picha ya mpenzi wangu au ndio umetumwa na mganga wako? Unafikiri mussa atarudi tena kwako, hilo sahau kashafika kwangu hawezi kurudia matapishi.
" Mimi siangalii picha yake.
" Na hiyo Ni Nini?
" Mama, mama hebu njoo uliangalie hili Toto la marehemu Kaka yako . Safia alimuita mama yake na muda huohuo mama safia alifika.
"Kuna Nini?
" Bado anamfuatilia mwanaume wangu angalia alishika picha ya mussa akawa anajiliza.
" Safia mwanangu huyo kashaishiwa Hana chake kwahiyo huna haja ya kupigishana kelele Musa Ni wako muachie huyu mpumbavu nitamtafuta dawa ya kumtibu.
Safia na mama yake walitoka chumbani na kumuacha kayla alilia kwa uchungu.

Kesho yake Kayla alikuwa barabarani anatembeza ndizi jua lilikuwa Kali Sana siku hiyo na biashara ilikuwa ngumu Sana . Alichoshwa na lile jua akaenda kukaa pembeni ya hotel moja. Kwenye hiyo hotel watu wengi Walienda kupata chakula pamoja na huduma ya malazi ilikuwa barabarani Tena kwenye njia inayoelekea mbugani hivyo watalii wengi waliokuwa wanaenda na kutoka mbugani walisimama kwanza hapo kula na wengine walipumzika hapo.
Muhudumu mmoja alienda kukaa karibu nae huku akichukua ndizi akawa anamenya.
" Hivi utaishi maisha haya mpaka lini ? Kwanini usiondike ukaenda mbali kunitafuta maisha yako tena ukiwa huru?
" Nitaenda wapi na unajua nimezaliwa hapa , ndugu zangu wapo hapa na sijawahi kutoka nje ya huu mji.
" Ila maisha yako yanasikitisha Sana shangazi yako amekufanya chuma ulete, ndugu yako nae macho juu asione mwanaume anakupendea anaenda kujipendejeza nasikia hata Musa kamchukua.
" Dada Mai tuachane na hayo unavyoongea ni kama unanitonesha kidonda.
" Pole mwaya.

Pembeni ya walipokuwa wamekaa kulikuwa na wanaume wawili walikuwa wanakula mwanaume mmoja akamuita.
" Dada muuza ndizi hebu njoo.
Kayla alinyanyuka haraka na ungo wake wa ndizi akaenda mpaka walipo na kuwasalimia .
" Karibuni.
" Unauza ndizi shiling ngapi?
" Moja shiling Mia.
" Rodney tunachukua za shiling ngp? Ibra aliuliza.
" Za elfu mbili zinatisha. Alijibu Rodney huku akiwa anamuangalia Kayla usoni . Alishindwa kujizuia akauliza
" Dada mbona Kama unahuzuni Sana, uso wako umekosa nuru unatatizo gani?
Kayla alitoa tabasamu la kulazimisha na vidimpoz zikatokea kwenye mashavu yake kisha kwa sauti ya chini akajibu.
" Nipo sawa.
" Sio kweli kuna kitu nahisi kama hakuna jambo unalopita basi utakuwa mgonjwa.
Kayla alishindwa ajibu nini alinyamaza tu.

Ibra alitoa noti ya shiling elfu kumi akampatia Kayla.
" Ngoja nikatafute chenchi. Kayla aliacha ungo wa ndizi akawa anataka kuondoka lakini Rodney aka msimamisha.
" Usijali kuhusu chenchi hiyo inayobaki utaenda kunywa soda.
Kayla alihisi hajasikia vizuri akauliza
" Umesema.
" Chenchi Ni yako.
" Asante Mungu awazidishie pale mlipo pungukiwa. Kayla aliwaombea Dua Kisha akajitwisha ungo wake wa ndizi akaondoka huku macho ya Rodney yakiwa kwake.
" Vipi Kaka bush girl kakuvutia? Ibra aliuliza
Rodney alitingisha kichwa Kisha akaendelea kula.
" Usijisahau kama wewe ni bwana harusi mtarajiwa unatakiwa kujichunga kwaajili ya Victoria
" Hivi kwanini huwezi kuacha kunitajia huyo kiumbe kila wakati?
" Lakini ni mzazi mwenzio.
"Najua haina haja ya kujikumbusha pia naelewa mipaka yangu. Alijibu Rodney kwa ukali kidogo kisha akaendelea kula.


KAYLA MY STRAWBERRY πŸ“ 2
MTUNZI SMILE SHINE

Majira ya jioni Kayla alienda kumsaidia shangazi yake kwenye biashara yake ya supu na chapati.
" Wewe ndondocha ulikuwa wapi mpaka unakuja saizi na unajua hapa huwa nakuwa na wateja wengi hivyo nazidiwa.
" Nilienda kuchukua ndizi kwaajili ya kutembeza kesho.
" Sasa usinisimamie hapo Nanda kachukue vile viombo ukaoshe.
Kayla alienda haraka kukusanya viombo akatoa nje ya kibanda. Kabla hajaanza kuosha akaitwa.
" Wewe punda fanya haraka uje uhudumie wateja huku.aliingia ndani akiwa anakimbia na kwenda kusikiliza wateja.
Wateja waliokuwa wameingia wakati huo walikuwa Ni zanda na Rodney.
" Karibuni. Aliongea Kayla kwa upole.
" Tunaomba chapati mbili mbili na supu. Aliagiza zanda
" Sawa.
Wakati anaenda kuwachukulia walichoagiza Safia alimuita.
" Wewe njoo utoe hivi viombo na umletee mpenzi wangu maji ya kunywa ya baridi.
Kayla alimuangalia Musa ambae alikuwa Kama hamjui Kisha akajibu
" Sawa.
" Wahudumie kwanza wateja haraka. Akiwa abaenda shangazi take nae alimuita majina ya ajabu ajabu.
Like swala halikumpendeza Rodney alijikuta roho inamuuma sana alitamani kuondoka pale lakini pia alitamani Sana kujua sababu ya Kayla kuishi Yale maisha.
Kayla alichukua chapati na supu akaenda kuwaandalia huku Rodney alimuangalia Sana usoni.
" Masikini binti wa watu anaonekana hana hatia Ila napenda kuongea nae nitamtafuta nafasi ya kuongea nae.

Kesho yake majira ya saa tatu asubuhi Rodney alirudi kwenye kibanda Cha supu akaagiza supu na chapati akawa anakula taratibu , wakati ule hakukuwa na wateja wengi shangazi yake Kayla alikuwa akipiga story na shoga yake.
" Yani yule mtoto Ni damu tu ya Kaka yangu Ila ingekuwa sio hivyo siku nyingi Sana ningefukuza .
" Lakini anakusaidia shoga yangu unatakiwa kumshukuru kwa Hilo.
" Hapa hakuna Cha kumshukuru kwangu kazi atafanya kama punda amechoka atafute njia ya kupita Tena nitashukuru Sana maana Kuna muda nawaza litokee hata janaume kusikojulikana limuowe wakafie mbele ya safari.
Waliendekea na mazungumzo yao Rodney alikuwa anawasikiliza.

Baada ya muda Kayla alienda akiwa na ungo wake wa ndizi.
" Shangazi funguo hii hapa.
" Weka hapo alafu Leo kakae na wake wambea wa hotelini alafu uchekewe kumaliza hizo ndizi utanitambua.
Kayla hakujibu alianza kuondoka.
" Hey wewe hebu njoo.
Kayla alirudi.
" Hebu sogea hapa karibu. Kayla aliweka ungo pembeni akasogea karibu.
" Sikiliza wewe kesho Ni siku ya marejesho na hapa nilipo Sina pesa za kurejesha hivyo Basi Kuna Jambo nataka unisaidie.
" Jambo gani shangazi?
" Mzee kiba so anakutaja wewe Sasa jioni nenda fanya uwezavyo uje na shiling elfu 30 hapa. Kayla alishituka pia yule shiga yake alishituka.
" Mama safia.....
" Shiiiii maisha yangu na wanangu hayakuhusu kama uwezo kuvumilia Nyanyuka uwende.
" Mmmmh.
" Pia ukiishia kuguna itakuwa nafuu. Wewe umenielewa?
Kayla alitingisha kichwa kukubali Kisha akachukua ungo wake akaondoka.

Rodney alisikia yote yaliyozungumzwa aliwaza kitu Kisha akaenda kulipia akaondoka.
Alienda kwenye take maeneo Kayla anatofanyia biashara kwa mbali akamuona akiwa kwenye gari la watalii akiuza ndizi. Alisubiri afanye biashara alipomaliza alimfuata.
" Mambo .
" Safi.
" Nahitaji ndizi za 500.
" Sawa. Kayla alimchagulia Kisha akampatia.
Kilichopelekea pale haikuwa kununua ndizi alikuwa anataka kuongea nae lakini kwa kuogopa watu wasije wakawekwa vibaya akaamua kumfuata kwa njia kama mteja.
" Unaitwa Nani vile.
" Kayla.
" Sasa Kayla Mimi Kuna Jambo nataka kuongea na wewe unaonaje jioni badala ya kwenda kwa mzee kiba ukaja pale hotelini ? Kayla alinywea Kisha akaangalia chini.
" Kayla .
" Abeee.
Aliitikia Kayla huku machozi yakimtoka.
" Aaaaa usilie Basi Mimi sio mtu mbaya kwako Kuna Jambo nataka tuongee baada ya hapo nitakupa hiyo pesa anavyotaka shangazi yako.
Kayla aliingiwa na uwoga hakuamini kile alichosema Rodney.
" Nikweli tutaongea tu hutanifanya chochote ?Mimi sio mwanamke wa aina hiyo ,sijiuzi.
" Najua hata Mimi sitaki kukununua nataka tuongee tu kuna baadhi ya mambo nataka kujua kutoka kwako.
" Sawa nitakuja.
" Utakuja saa ngapi?
" Kigiza kikiingia .
" Basi sawa Mida ya saa moja na nusu utanikuta pale nje nitakuwa nakusubiria.
" Sawa.
Rodney alitoa shiling elfu tano alafu akasema .
" Chenchi utakunywa soda.
" Asante.
Rodney aliondoka huku kayla akawa anamuangalia kwa wasiwasi.
" Mmmh huyu kaka simjui hanijui hivi atakuwa mtu wa kheri kwangu? Mbona maisha yangu yapo mashakani naweza nikamkwepa mzee Kiba nikaangalia kwenye balaa kubwa lakini acha liwalo na liwe nitaenda kukutana nae huyo jioni

Jioni ilikuwa kana walivyopanga Kayla akijiandaa akaenda mpaka pale hotelini akamkuta Rodney kakaa nje anamsubiri.
" Habari za saizi.
" Salama. Sasa hatuwezi kuongelea hapa unaonaje tukaenda kukaa sehemu ya faragha ili watu wasituone?
" Faragha Tena?
" Kayla kuwa na amani Mimi Ni mtu Safi huenda naweza kukusaidia hayo matatizo yako na pesa hii hapa anavyotaka shangazi yako. Rodney alitoa pesa akampa.
" Sawa twende.
Wakuenda mpaka kwenye chumba Cha hotel alipofika Rodney.
Waliingia ndani .
' karibu ukae.
" Asante. Wote walikaa kitandani lakini Kyla alionekana kuwa na wasiwasi Sana hata alipomuona Rodney anataka kunyoosha mkono alishituka.
" Sikiliza Kayla nimeona mengi mabaya unayopitia sijafurahishwa nayo kabisa Kama binadamu hutakiwi kuishi maisha Kama Yale. Hivi unaweza kunipa historia yako ya maisha kwa ufupi?
" Ndio. Alijibu Kayla Kisha akatulia kwa muda. Badae aliendelea kuongea
" Mimi Ni yatima baba na mama yangu walifariki zamani sana. Huyu shangazi yangu alihamia kwetu yeye pamoja na mwanae safia , kwakuwa nilikuwa mdogo alichukua jukumu la kuniowa na kusimamia kila kitu walichoacha wazazi wangu. Katika maisha niliyolekewa na shangazi yangu sijawahi kuishibkwa Raha Wala amani nimekuwa kana mtumwa wao, Sina muda wa kupumzika Kama wengine kulala kwangu Ni saa sita au saba usiku na kuamka Ni saa 11 alfajir. Ilibidi nizowee kwakuwa ndio maisha yangu na Sina sehemu ya kwenda .
" Maamuzi yako Ni Nini kwenye haya maisha?
" Nitakuwa na maamuzi gani? Sina maamuzi Mimi naamuliwa kila kitu. Hilo jibu kilimuumiza zaidi Rodney.
" Acha kujikatia tamaa Kayla unaweza kunitoa kwenye hayo maisha na ukaishi maisha yenye Uhuru.
" najitoaje ikiwa kila mtu anaogopa kunisaidia kutokana na visa vya shangazi yangu?
Rodney alikaa kimnya akifikiria afanye Nini kumtoa Kayla kwenye manyanyaso.
" Inamaana hata viongozi wa Kijiji hawajui jinsi unavyoishi?
" Kwa hapa Kijijini hakuna asiejua ninayopitia.
" Sawa naomba kwa Leo uende Ila keshokutwa jioni tuonane maana kesho naenda mbugani kesho kutwa nageuza.
" Sawa.
Rodney alitoa pesa nyingine akampatia.
" Shika hizi zitakusaidia kwa Mambo yako madogo madogo.
" Lakini Sina shida ya pesa.
" Wewe chukua najua unauhitaji. Kayla alipokea zile pesa na kumshukuru Sana Kisha akaondoka.
Njia nzima Kayla alikuwa aliwaza amekutana na mtu gani wa ajabu mwenye moyo wa huruma.
" Aiseee kumbe kwenye hii dunia Kuna watu Wana roho zao Yani huyu Kaka simjui lakini ameamua kunisaidia, Mungu amlipe zaidi ya hiki alichokionyesha kwangu.







KAYLA MY STRAWBERRY πŸ“ 3

MTUNZI SMILE SHINE

Kayla aliondoka akiwa na furaha huku akimshukuru sana Mungu kwa kumletea mtu mwema wa kumsaidia, alifika nyumbani akamkuta shangazi yake kakaa sebleni akimsubiri.

" Eheeee afadhali umekuja mapema nilikuwa nasinzia kama tena hapa.
Kayla alisogea karibu yake na kumpatia kiasi cha pesa alichotaka. Shangazi yake alitabasamu huku akipokea zile pesa na kuzihesabu
" Haya ndio mambo sasa , yani ukiwa unafanya kama inavyotaka mbona utaishi kwa raha hapa ndani alafu sasa hutakiwi kumwambia mtu yoyote kile unachofanya ni siri yangu mimi na wewe , sijui unamuelewa ninachosema?
Kayla aliitikia kwa kichwa maana ilikuwa ni huzuni kwake shangazi yake hakujali utu wake .
" Basi nenda kaoge vizuri utoe hilo jasho baya alafu kapumzike kesho mapema udamke kwaajili ya majukumu mengine.
" Sawa shangazi.
" Kesho ukipata pesa nzuri nitakupa hela ukanunue hata kigauni na wewe upendeze.

Kayla hakujibu akaingia chumbani kwake akakaa . Akili yake ilienda mbali sana kwa kufikiria.
" Ninavyojua shangazi yangu ataona huu mchezo wa kunifanya kinyago cha ngono kwaajili ya kupata pesa kirahisi sasa sitakiwi kucheka nae kwenye hili kama amekuwa akinifanya mtumwa na mimi nikakubali basi kwenye utumwa wa kingono wala sitathubutu siwezi kuvunja heshima na kutojali utu wangu kwasababu ya tamaa zake.

Kesho yake kulikucha kayla aliendelea na mambo yake kama kawaida alijifanya na kwenda kuchukua ndizi kwaajili ya kwenda kutembeza, kutwa nzima alikuwa akikumbana kutafuta wateja ilimradi ndizi ziweze kuisha apeleke hesabu inayotakiwa.

Ilipofika majira ya saa tatu usiku kayla akiwa kwenye mgahawa wa shangazi yake wakisaidiana kazi shangazi yake alinyanyuka pale alipokuwa amekaa akatoka nje, baada ya kama dakika tano alirudi akamuita kayla
" Kayla hebu njoo mara moja.
Kayla alimfuata wakatoka nje pamoja wakasimama pembeni ya ukuta .
" Kayla umemuona yule mwanaume aliyesimama pale kwenye ule mti wa mwarobaini?
Aliongea shangazi yake kwa sauti ya chini huku alinyoosha kidole kuelekea ulipo mti wa mwarobaini , wakati huo moyo wa kayla ulipasuka kwa mshituko akajua kile alichokuwa amefikiria ndio kinaenda kutokea. Akiwa bado kazubaa alishitukia kibao cha begani.
" Yalaaa...
" Yani mimi hakuelekeza wewe umezubaa kama zezeta.
" Kuna giza shangazi sijui ni nani.
" Huwezi kumjua ni nani lakini si umeona kuna mtu pale?
" Ndio.
" Basi utaenda kulala kwake tutakutana kesho asubuhi .
Kayla alikuwa bado kasimama anashangaa inakuwaje akalale kwa mtu tena hajui ni nani?
" Acha kuzubaa nenda mtu anakusubiri pale na ukumbuke kuamka mapema rudi nyumbani.
Kayla hakujibu alipiga hatua kwenda alipo yule mtu. Alipofika karibu yule mtu akamsemesha
" Oooh kayla vipi?
" Safi. Kayla alijibu kwa sauti ya chini huku akiwa na hofu.
" Nadhani kila kitu umeshaambiwa na shangazi yako twende basi.
" Sawa lakini naomba unisindikize nyumbani kwanza kuna kitu nataka nikachukua.
" Kwani ni muhimu sana hicho kitu?
" Ndio.
" Basi poa twende zetu.
Waliongozana mpaka nyumbani kwao walipofika kayla akamwambia
" Nisubiri hapa nakuja sasa hivi.
" Poa usichelewe basi.

Kayla aliingia ndani akaenda kufungua begi lake na kutoa kitambaa chake kilichokuwa kimefungwa fundo . Kilikuwa na akiba zake za pesa alizokuwa akihifadhi kisha akachukua kikoi cha kimasai akajifunika alafu akatoka mlango wa nyuma na kutokomea gizani huku yule mwanaume aliendelea kumsubiri.

Zilipita kama dakika 10 yule mwanaume alipoona kimnya na hakuna dalili ya kayla kutoka alisogea mpaka mlangoni na kuanza kugonga, aligonga bila kuitikiwa akaamua kumuita kayla bado hakuna mtu alitoka kumsikiliza akaamua kuondoka kwa hasira huku akiwa anafoka, Akiwa njiani alikutana na shangazi yake kayla anarudi kutoka kwenye mgahawa wake
"Mama Safina kwa hiki ulichokifanya na huyo mwanao sijakipenda kabisa kama ilikuwa haiwezekani ungeniambia tu sio kunipotezea muda na pesa yangu umechukua.
" Kwani nini kimetokea jose?
" Kayla kajichimbia huko ndani kwenu namuita hataki kutoka.
" Kwani nilikuja kumalizana huku kwangu na sio kwako?
" Hapana aliniomba nimsindikize huku kuna kitu anakuja kuchukua lakini matokeo yake kakaa ndani hataki kutoka.
" Kumbe huyu mtoto ni mshenzi hivi hebu twende.
" Kama inashindikana nimrudishie hela yangu .
" Kiendacho kwa mganga hakurudi kijana ile hela imeshaingia kwenye bajeti zangu nyingine wewe twende ukamchukue uende nae.

Waliongozana mpaka nyumbani walipofika tu mlangoni mama Safina akaanza kumuita kayla huku akitukana.
" Nasema toka mwenyewe wewe mjinga nikikukuta huko nitakunyuka mpaka mzimu wa wazazi wako uje kukusaidia.

Kuongea kote pamoja na kutoa vitisho vingi lakini kayla hakutokea hapo ndipo alipoamua kwenda kumtafuta chumbani kwake na. Nyumba nzima lakini hakukuwa na mtu akaamua kurudi sebleni huku ameshika kiuno.
" Vipi yuko wapi?
" Hayupo. Una uhakika aliingia ndani?
" Ndio .
" Sasa mbona hayupo humu ndani?
" Aisee mama Safina usiniletee ujanja ujanja wako kama umemficha huko ili mnizurumu mimi sitakubali .
" Sasa nikufiche nini ingia ndani kamuangalie.
" Basi nipe hela yangu.
" Hapo kwenye hela uongo ....
" Basi kama hutaki kunipa hela njoo tumalizane mimi na wewe.
" Unasemaje wewe mwanaharamu?
" Sasa hela yangu hutaki kutoa unataka nini? Nipe basi tumalizane.
Alisema jose huku akinisogelea na kumtaka kumkamata mama Safina akarudi nyuma.
" Jose huoni aibu , huoni kama mimi ni kama mama yako?
" Mama yangu ni yule alienizaa hivyo haina madhara ukinipa.
Jose alionekana kudhamiria kufanya hilo jambo , mama safia alipoona hivyo alipiga kelele za mwizi .
" Sawa leo umeshinda ila kumbuka hela yangu huwa haipotei bure utailipia. Alisema jose huku akiondoka.
Kayla hakuwa na pa kwenda usiku ule na ilikuwa hatari sana kulala nje kwani kuna baadhi ya wanyama huwa wanatembea usiku wakiwemo fisi wakitafuta mizoga pamoja na kuingia kwenye mazizi ya wanyama.
Kwa haraka kayla alifikiria Mai mfanyakazi wa pale hotelini. Alifika nyumbani kwa mai na kugonga dirishani.
" Dada mai naomba unifungulie mlango .
Mai alishituka maana muda ulikuwa umeenda aliangalia saa ilikuwa inakimbilia saa sita.
" Wewe ni nani?
" Kayla naomba unifungulie dada.
" Kayla unafanyanini usiku huu?
" Nifungulie kwanza nitakwambia. Kayla aliongea huku akiwa na wasiwasi kwani alikuwa akisikia sauti za fisi wakilia.

KAYLA MY STRAWBERRY πŸ“ 4

MTUNZI SMILE SHINE

Mai alinyanyuka haraka pale kitandani akaenda kufungua mlango na kayla akaingia haraka wakafunga mlango.
" Wewe mtoto mbona unabalaa ni kitu gani limekufanya utembee usiku kiasi hiki na unajua hili eneo lina wanyama hatari nyakati za usiku? Husikii fisi wanalia huko nje?
" Najua dada na fisi nawasikia wanalia lakini sikuwa na chaguo zaidi ya hili nililofanya.
" Niambie umepatwa na nini?
" Nimechoshwa na mambo inayofanyiwa na shangazi nimeamua kutoroka sitamani tena kuishi na wale viumbe yani ni bora kuliwa na hao wanyama kuliko kujidhalilisha.
" Mmmmh sasa ndio uondoke usiku huu?
" Imebidi dada mai , shangazi ameanza tabia ya kuniuza kwa wanaume ili kujipatia pesa.
Mai alishituka na kusema
" Wewe kumbe yule mama ni shetani kiasi hicho?
" Ndio hapa ninapokwambia nimemtoroka mwanaume ambae alitaka nikalale nae mpaka asubuhi.
Mai alimuangalia kayla alivyokuwa anajieleza akamuona huruma .
" Sasa inakuwaje maana akijua upo kwangu itakuwa balaa.
" Naomba unistiri usiku huu ikifika kesho nitajua kwakwenda.
" Utaenda wapi sasa?
" Sijui ila nataka niondoke hapa kijijini.
" Daaah inasikitisha sana, basi pumzika tutaongea kesho.

Kayla alipanda kitandani akalala lakini hakuweza kupata usingizi alifikiria mambo magumu aliyopitia huko nyuma.

Kulipokucha Mai aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kazini na kayla alikuwa macho amekaa kitandani alijua Mai hawezi kumruhusu abaki pale hivyo akawa ananipangia kuondoka.
Baada ya Mai kumaliza kujiandaa alimwambia.
" Kayla siwezi kuruhusu utoke hapa ndani muda huu kwasababu ya usalama wako na wewe mwenyewe unajua hiki kijiji hakina siri kwahiyo kaa hapa badae nitakuja tujadili cha kufanya.
Kayla aliitikia kwa kichwa.
"Sasa acha mimi niende kazini wewe baki hapa ndani nitarudi badae . Mai alisisitiza
" Sawa.
Mai aliondoka na kumsihi ajifungie ndani asitoke.

Muda ulizidi kwenda pale ndani kayla alikuwa kakaa mwenyewe na mawazo yalizidi kusonga kichwani kwake hakutaka ni kuendelea kukaa pale hakuwa na imani na mtu yoyote alihisi kila mtu anaweza kumgeuka na endapo shangazi yake akimkamata atampa adhabu kubwa na kazi anazotumwa lazima afanye.
" Sipaswi kumuamini mtu huyu Mai anaweza kubadilika na kusema kuwa nipo kwake natakiwa kuondoka .

Wakati huo huko mtaani kila kona habari za kupotea kwa kayla zilizagaa , baadhi ya watu wakiwalaumu shangazi yake na safia kuwa ndio sababu ya kayla kutoroka nyumbani.
Rodney na ibra walikuwa wamefika kutoka porini wanakutana na hizo story. Rodney alionekana kuchoshwa na hizo taarifa kwani matarajio yake alitaka kuonana na kayla ili wapange nini cha kufanya ili kumsaidia.
" Sasa hapa inakuwaje ibra?
" Hapo hakuna jinsi kama kasha jiongeza kaamua kuondoka basi achana nae.
" Hapana ibra unajua yule msichana alikuwa anaishi kwenye mazingira magumu sana nilikuwa natamani kuongea nae zaidi na hata kama itawezekana nimpe msaada.
Rodney alikuwa hana raha alimsikitikia sana kayla aliwaza sijui kwa kipindi hicho atakuwa wapi na atakuwa anapitia nini. Akiwa kajiinamia mara alipita Mai hapo ndipo alikumbuka kuwa siku ya kwanza kumuona kayla alikuwa kakaa na Mai.
Rodney alinyanyuka akamfuata .
" Habari yako dada.
" Salama.
" Samahani nilikuwa naomba kumuuliza kitu.
" Uliza tu.
" Kuna habari nimesikia kuwa yule binti muuza ndizi uliekaanae pale amepotea hivi hizi habari niza kweli?
Mai alimuangalia rodney alafu akasema
" Ndio inasemekana hivyo.
" Daaa hivi atakuwa kaenda wapi?
" Sijui kila mtu hajui alipo maana inasemekana alitoroka usiku na hili eneo lipo karibu na mbuga wanyama wengi huwa wanaingia kijijini nyakati za usiku.
" Unamaanisha nini? Unataka kusema atakuwa Kaluwa na wanyama?
" Hapana ila watu wengi wanahisi hivyo japokuwa hatujaona mabaki ya mwili wala kiashiria chochote.
" Aiseee inamaana alishindwa kunisubiria kwa siku moja , kama ningejua ningeahirisha safari ya kwenda mbugani ningemsaidia kwanza. Hii imeniuma sana najutia sana.
Rodney alionekana kujilaumu sana .
Mai alimuangalia jinsi alivyokuwa anasikitika na kujilaumu akaona huenda anania njema kwa kayla akamuuliza
" Kwani ulitaka kumsaidia?
" Ndio niliwahi kukutana nae akanielezea matatizo yake nikamuomba awe na subira mpaka nitakaporudi nitajua cha kufanya.

Kwakuwa rodney alionyesha nia ya kutaka kumsaidia kayla na mpaka sasa kayla hajui anaelekea wapi Mai aliamua kumwambia ukweli Rodney.
" Kaka mimi najua kayla alipo.aliobgea Mai kwa sauti ya chini
Rodney aliposikia hivyo aliachia tabasamu.
" Unasema kweli? Kayla yuko wapi?
" Shiiiii usiongee kwa sauti hatakiwi mtu mwingine kujua.
" Sawa unaweza kunipeleka alipo?
" Ndio.
" Basi nipeleke sasa hivi.
" Nisubiri hapo nakuja.
Mai alienda kuomba ruhusa baada ya hapo waliondoka wanaelekea nyumbani kwa Mai.
Walipofika walikuta mlango imerudishiwa na kayla hayupo ndani.
" Mbona hayupo?
" Alikuwepo hapa nilimuacha na nikamwambia asiondoke mpaka nitakaporudi.
" Au kuna mtu kamuona akaenda kuwaambia familia yake?
" Sidhani.
" Sasa atakuwa kaenda wapi?
Wakiwa wanafikiria mara. Kayla aliingia na kufunga mlango haraka.
" Wewe kayla ulienda wapi?
Mai aliuliza lakini kayla hakujibu alikuwa anahema kama vile mtu ambaye alikuwa anakimbizwa.
" Kuna nini kayla. Aliuliza Rodney huku akiwa kamshika mabegani.
" Kuna mtu kamuona.
" Kakuona ukiwa unaingia hapa ndani?
" Hapana niliwahi kukimbia.
" Lakini nilimwambia isitokee hapa ndani sasabona unataka kujiletea matatizo, unajua shangazi yako alivyo mshari.
" Nisamehe dada.
" Tuachane na kulaumiana tuongee kitu ambacho kinaweza kumsaidia kayla . Alisema Rodney na wote wakatumia lakini Mai bado alikuwa na wasiwasi alienda dirishani kuchungulia kama kuna mtu alikuwa anamfuatilia kabla.
" Kaka kama unaweza kumsaidia naomba umsaidie huyu binti maana anayopitia ni mazito sana .
" Nina nia ya kumsaidia kama yupo tayari nimuondoe hapa akaanza maisha mapya nitahakikisha anapata kila anachostahili kupata .
" Mimi nipo tayari kaka naomba unisaidie niondokane na haya mateso.
" Basi leo jioni tutaondoka .
" Nahitaji kurudi kazini itakuwaje kama watu watagundua kama yupo hapa ndani? Alisema Mai
" Hilo nalo ni neno tunafanyaje sasa ?
" Kama itawezekana mngeondoka mapema maana hili eneo ni dogo na kila mtu anahofu na maisha ya kayla wakisema wafanye msako wakamkuta hapa ndani itaniletea shida.
" Sawa mimi na wewe tutaondoka pamoja , kayla utabaki hapa baada ya dakika chache nitafika na gari nitakuja kukuchukua.
" Sawa.
Rodney na Mai waliondoka na kufunga mlango kwa nje .

KAYLA MY STRAWBERRY πŸ“ 5

MTUNZI SMILE SHINE

Walipokuwa njiani wanaelekea hotelini walikutana na kundi la vijana waliokuwa wanamtafuta kayla.
" Mai haujamuona kayla huko?
Mai alisita kujibu akamuangalia Rodney, Rodney alimkazia macho usoni akiwa anamaana aseme ukweli.
" Hapana sijamuona kwani ameonekana wapi?
" Inasemekana kukimbilia mitaa ya huku twendeni atakuwa kaingia porini.
Wale vijana waliondoka huku wakiwa wanakimbia. Mai na Rodney wakiendelea kusimama huku wakiwaangalia wanavyoondika kwa kukimbia.
" Uuuuh kaka unaona huu mtihani ulivyo mgumu kwangu kayla anatakiwa kutoka pale ndani haraka sana.
" Usijali nitamuondoa hapa muda sio mrefu kuwa na amani.
Wakati wamesimama wanaendelea kuongea mara mama safia na safia walifika wakiwa wanahema hema .
" Mai mwanangu hivi haujanionea yule ndondocha wangu?
Kitendo cha kayla kuitwa ndondocha kilikuwa kinamkera sana Rodney na kufanya akunje sura yake . kabla Mai hajajibu Rodney alimshika mkono akamvuta waondoke.
" Jamani huyu kijana analaana hajui kuheshimu wakubwa yani mimi naongea na mwenzie yeye akamvuta inamaana ninachokiongea hakina maana au ? Alifoka mama safia lakini Rodney hakujali ndio kwanza walikazana kutembea.
" Huyu mama hana utu kabisa yani mtu anamuita ndondocha au huyu mama ni mchawi?
" Ana roho mbaya tu.
" Huo ndio mwanzo wa uchawi.

Alifika hotelini Rodney akaingia kwenye chumba cha hotel akachukua kila kitu chako kisha akataduta Ibra.
" Ibra tunatakiwa kuondoka sasa hivi.
" Khaa inakuwaje haraka hivi?
" Nimesema niandae tuondoke.
" Lakini haukuwa mpango wetu kuondoka leo.
" Ndio haikuwa hivyo lakini imetokea kama dharula natakiwa kumuondoa kayla kwenye hiki kijiji.
" Unataka kuniambia Umempata?
" Maswali yako yananipotezea muda naomba tuondoke.
" Daaaah yani unavyo nipelekesha kama mtoto mdogo bwana. Ibra alilalamika lakini alifanya alichoambiwa na Rodney .

Walipanda kwenye gari na kuelekea ilipo nyumba ya Mai.
" Ibra mimi mashuka naenda kumchukua kayla wewe toka ufungue mlango wa nyuma na usimame kuangalia kama kuna watu wanakuja.
" Rodney hiki tunachofanya ni hatari hivi wakimuona tunamtorosha huyo binti si ndio utakuwa mwisho wa maisha yetu?
" Ibra acha uwoga wa kijinga unajua kayla anahitaji kusaidiwa na huo msaada tunatakiwa kutoa mimi na wewe.
" Daaah sawa wewe shuka ukamchukue.
" Naomba uwe makini kuangalia sitaki mtu yoyote atuone .
" Sawa nenda kachukue haraka mimi sitaki kuweka maisha yangu rehani.

Rodney alishuka kwenye gari akaenda kufungua mlango wa chumba cha Mai akamkuta kayla kasimama huku jasho likimtoka kwa uwoga.
" Kayla tunatakiwa kuondoka hapa haraka sana maana unatafutiwa kila kona .
" Sawa.
Kayla alichukua lile shuka lake la kimasai alishikilia mkononi.
" Itakuwa vizuri kama ungejifunika. Kayla alikunjua lile shuka huku akitetemeka Rodney alikuwa anaona kama anachelewa akachukua lile shuka na kumfunika kuanzia kichwani alafu akasogea karibu na mlango akachungulia , akamuuliza Ibra.
" Vipi kuko salama?
Ibra aliangalia kila upande alafu akawaita kwa ishara.
" Kayla toka haraka na uende ukapande wenye gari hakikisha unajilaza kwenye kiti watu wasikuone.
" Sawa.
Kayla alitoka haraka na kwenda kupanda kwenye gari bila kuchelewa Ibra alifunga mlango na kwenda kupanda kwenye gari pia Rodney alifunga mlango wa mai na kwenda kupanda kwenye gari na safari ya kuondoka pale kijijini ikaanza.
Walipomaliza kijijini kayla alinyanyuka na kukaa vizuri , alichungulia dirishani huku machozi yakiwa yanatoka. Kadri muda ulivyokuwa unaenda ndivyo alizidi kutoa sauti ya kilio mpaka ibra na Rodney wanageuka kumuangalia.
" Ibra hebu njoo iendeshe gari. Alisema rodney huku akitafuta sehemu nzuri ya kusimamisha gari .
Baada ya kussimamisha gari Rodney alishuka akaenda kukaa nyuma na kayla. Na ibra akakaa sehemu ya dereva na kuanza kuendesha gari.
Rodney aliendelea kumbembeleza kayla .
" Sasa uhakika nini kayla? Nyamaza basi huko tunakoenda utakuwa salama kabisa .
" Kaka niache nilie inaniuma sana hivi kweli leo hii nakimbia sehemu niliyozaliwa na kukulia kama mkimbizi kwa sababu ya chuki za ndugu zangu ambao nilidhani wao ndio kimbilio langu na kila kitu kwangu.
Maneno ya kayla yalimuumiza Rodney akajikuta akamkumbatia huku akipapasa mgongoni.
" Basi kayla sitaki kuona inalia wala unahuzunika kwasababu ya maisha uliyopitia nahitaji usahau kila kitu unaenda kuanza maisha mapya nitakusikamia kwa kila kitu naomba uniamini.
" Sawa kaka nashukuru sana .
Rodney alimfuta machozi na kayla akaacha kulia.

Walifika mjini majira ya saa mbili usiku waliingia Arusha mjini, walifika maeneo ya majengo ibraz alishuka na kuchukua usafiri wa pikipiki kwaajili ya kumpeleka nyumbani kwake maeneo ya bandambili.

Rodney aliendelea kuendesha gari mpaka maeneo ya sakina huko ndiko alipokuwa anaishi Rodney pamoja na familia yake pia alikuwepo mwanamke aliyezaa nae pamoja na mtoto wake Jada. Wakiwa bado wapo nje wanajiandaa kuingia ndani binti wa miaka minne ( Jada) alitoka ndani akiwa anakimbia na kwenda kumkumbatia baba yake. Rodney alimnyanyua binti yake na kumkumbatia kisha akambusu.
" Baba umenileta zawadi? Jada aliuliza
" Mmmm mumy hujanisalimia unadai zawadi.
" Shikamoo baba.
" Marahaba.
" Nimekumiss
" Nimekumiss pia mrembo wangu.
Wakati huo kayla alikuwa anashangaa mazingira Jada akamuuliza baba yake.
" Baba huyu ni nani?
" Huyo ni aunt kayla, msalimie aunt.
" Shikamoo aunt.
Kayla aliachia tabasamu alafu akaitikia
" Marahaba.

Waliingia ndani wakapokelewa na kayla alikaribishwa akakaa huku akiwa kakufunika shuka yake .
" Mama huyu binti anaitwa kayla atakuwa mgeni wetu hapa.
Mama Rodney hakueleza atakuwa mgeni wao kivipi lakini hakuona busara kuuliza maswali mbele ya mgeni.
" Sawa karibu binti.
" Asante.
" Anaitwa kayla. Rodney akimtambulisha kwa kila mtu . Kayla alipokelewa akapelekwa chumbani kwaajili ya kujiandaa kuoga baada ya hapo apate chakula ili apumzike.

" Rodney unajua sijamuelewa kijana wangu. Alisema mama Rodney.
" Najua unataka kujua zaidi kuhusu huyu binti ila naomba nikuelezee kesho mama yangu sasa hivi nimechoka sana.
" Sawa mwanangu.
Rodnz alinyanyuka na kwenda chumbani kwake , alipofika chumbani akawa anavua shati kwaajili ya kwenda kuoga mara akaingia Victoria.
" Wewe huyu msichana ulieleza hapa ndani ni nani?
" Mama Jada ndio kwanza nimefika hata kuoga sijaona unanidaka juu na maswali hii ni sawa kweli?
" Kama ungekuwa hutaki maswali ungenishirikisha kabla haujamleta huyo mwanamke wako hapa ndani.
" Victoria unaongea ujinga gani? Hivi nitakuwa mpumbavu kiasi gani mpaka nianze kuleta mwanamke nyumbani?
" Rodney naona unajisahau sana kumbuka mimi ndio ninafanya uonekane mwanaume mwenye hadhi hapa mjini sasa ile wako ujichanganye nadhani unajua nini kitatokea.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote