JOHAR (Ubavu Wangu Ni Wewe)

book cover og

Utangulizi

Johar binti anaetokea Kijijini na kwenda mjini kusoma kwenye chuo Cha utalii , maisha ya chuo yanaku magumu anashindwa kuomba hela kwa wazazi kutokanana Hali ya nyumbani kwao, huko mjini anapata kazi mgahawani akawa anatenga muda wa kazi na kusoma. Siku moja akitumwa na boss wake kwenda kupeleka chakula kwenye jumba moja la kitajiri huko anakutaja na kijana Ethan, kijana asiepitwa na wasichana. Ethan anambananisha Johar chumbani kwake bahati Bibi yake Ethan anaingia , kwakuwa anamjua mjukuu wake alitoka na yule msichana na kumuonya akae nae mbali.
Ethan anaonekana kuvutiwa na Sana na Johar anaamua kumfuatilia , kwakuwa yeye Ni mfalme wa mapenzi anapambana na kufanikiwa kumpata , wakaanza mahusiano na kumuonyesha mapenzi makubwa Sana lakini alishindwa kabisa kuachana na tabia ya uhuni. Eve rafiki wa johar anajua tabia za Ethan anapojaribu kumkanya wanakuwa maadui. Lichavya Ethan kuwa na Mambo yake lakini anawivu Sana na Johar hataki kumuona akiwa na mwanaume. Wanafanikiwa kuvalishana Pete ya uchumba , Ethan anaenda kumtambulisha Johar kwa Bibi yake akakuta Bibi kanitafutia MKE wa kuowa.
Hapo ndio patamu Sasa Ethan atamchukua maamuzi gani ? Atamchagua Nani Kati ya Hawa warembo wawili mmoja kutoka Kijijini na mwingine mtoto wa kishua?

JOHAR ( UBAVU WANGU NI WEWE)πŸ’“1

MTUNZI SMILE SHINE

Johari Ni binti wa miaka 23 , Ni mtoto wa kwanza Kati ya watoto watatu, anatoka Kijiji Cha mtakuja, familia yake inajishuhurusha na ufugaji wa ng'ombe pamoja na kilimo Cha mkono hivyo uoatikabaji wa mazao haukuwa mkubwa. Johar alitamani Sana kuwatoa wazazi wake kwenye yake maisha hivyo alijitahidi kusoma ili kubadilisha maisha ya nyumbani kwao alitamani siku moja maisha ya nyumbani kwao yawe Kama ya watu wengine wenye maendeleo pale kijijini, alitamani wazazi wake na wadogo zake waishi kwenye nyumba nzuri yenye umeme pia kuwafungulia biashara wazazi wake maana kadri muda unavyoenda wanazidi kuzeeka hivyo hawataweza kufanya kazi za shamba na kuhudumia mifugo.

Baada ya kumaliza kidato Cha sita Johari alichaguliwa kujiunga na chuo Cha Mambo ya utalii.
Wazazi wake waliuza ngombe pamoja na mazao kwaajili ya kumsafirisha binti yao aende chuo pamoja na nahitaji mengine atakapofika huko mjini.

Johari waliwasili chuoni na kuanza masomo huko alikutana na Vanessa binti , Vanessa anavutiwa na uwezo wake kwenye masomo akaamua kuanzisha urafiki. Vanessa alinishawishi ahame hostel wakaishi pamoja kwenye chumba alichopanga. Johar alikubali wakaenda kuishi pamoja huko anakutaja na Eve pia Ni rafiki wa Vanessa. Vanessa anawakutanisha wanakuwa Marafiki watatu wanaosaidia na kwa kila Hali lakini Eve alikuwa tofauti kidogo Mara kwa Mara alikuwa anamkwaza Johar , alikdharau na kumuona mshamba kwasababu ya Mambo yake ya Kijijini na bado alikuwa hajachsngamka lakini badae ilibidi johar amzoee tu.

Vanessa na wanatoka kwenye familia inazojiweza hivyo alipata kilawanacho kutaka kutoka kwenye familia yake na Eve anatoka kwenye maisha ya kawaida Ila alikuwa mtu wa Mambo mengi ,alitoka na wanaume wenye pesa .

Siku moja Vanessa aliwaambia watoke waende kwenye mgahawa mmoja maarufu iliyokuwepo katikati ya mji kwenye huo mgahawa Walienda watu wa aina mbali mbali kutokana na kuwa na sifa ya kuwa na vyakula vizuri pia huduma nzuri.
" Johari mbona unatoa macho haujiandai?
" Vanessa nyie nendeni tu Mimi siwezi kwenda huko.
" Oooh jamani johari najua kwanini unakataa Ni kwamba hauna pesa za kulipia chakula si ndio?
" Ndio Sina pesa.
" Usijali jiandae tutoke.

Johari alikubali hiyo ofa alijiandaa haraka alivalia gauni lake la solo ambalo kila mtoko alilivaa kwakuwa ndio ilikuwa nguo yake nzuri.
" Jamani johari hiyo nguo kila siku hebu leo badilisha bwana unajua watu watatukariri kwasababu yako. Alisema Eve.
" Sina nguo nyingine nzuri.
Vanessa alienda kwenye begi lake akatoa magauni mawili akampatia.
" Shika hizi nguo, kavae moja wapo Kati ya hizo.
"Asante.
Johari aliwaacha akaenda kubadili nguo.
" Yani huyu johari sijui Ni mtu wa aina gani kwani anashindwa kujiongeza mpaka kila kitu apewe? Alisema Eve kana kwamba hakupenda johari kusaidiwa .
" Eve inatosha Sasa usimsimange mwenzio kwani hujui kesho yako.
" Hahahaha unamaanisha Nini unavyosema hivyo?
" Ni kwamba Leo unacho kesho hauna.
" Wewe Mimi Nina akili zangu kwanza sitegemei kwa wazazi Nina Kona nyingi za kusaka pesa.
" Acha kuficha ficha Mambo sema una madanga wengi.
" Ndio si nimejiongeza yeye atachanga mka lini ? Kila siku yupo Kama katoka Kijijini Jana.

Johari alirudi wakanyamaza kuongea.
" Waoooo umependeza shost. Vanessa alimsifia
" Asante.
" Kweli kapendeza lakini Ni nguo za kuvuliwa ingekuwa Bora Kama angenunua kwa pesa yake.
" Eve umezidi Sasa. Vanessa aliongea kwa ukali kwasababu hakupenda na johari alinyamaza kimnya kwasababu kila kilichoongelewa Ni kweli na sio kwamba alikuwa haumii Ila alijilaza tu.
Eve alimuangalia johari usoni akaona Hana furaha.
" Johari rafiki yangu sikusemi kwa ubaya unatakiwa kuchangamka pia kumbuka hapa sio Kijijini hapa Ni mjini watu wanaishi kisasa.
"Sawa nimekuelewa.

Waliondoka walipofika mgahawani waliagiza vyakula na vinywaji. Wakawa wanakula huku wakipiga story . Eve alikuwa macho juu juu alitafuta mwanaume wa kumuweka mjini .
Wakiwa wanaendelea kula Johari alinyanyuka akawa anaenda chooni . Mara alikutana na wafanyakazi wawili wakiongea.
" Hapa kazi zimekuwa nyingi Sana boss amesema wanatakiwa wafanyakazi wawili.
" Itakuwa nafuu tutapata muda wa kupumzika.
Johari aliwasogelea wale wahudumu akawasalimia Kisha akauliza
" Samahani nimesikia mnaongelea swala la kutafuta mfanyakazi hapa mgahawani .
" Ndio.
" Naweza kupata kazi hapa?
" Ndio Kama unaweza kazi utapata na bahati boss yupo hapa unaweza kwenda kuongea nae.
" Nitashukuru Sana Kama mtanisaidia kwenda kuonana na boss wenu.
" Sawa nifuate. Alisema muhudumu mmoja aliondoka na johari alimfuata nyuma. Walifika mpaka kwenye meza moja aliyokuwa kakaa baba mmoja wa makamo alikuwa bize na calculate anapiga mahesabu.
" Samahani boss huyu dada anashida na wewe. Yule baba alinyanyua macho akamuangalia na johari akamsalimia
"Shikamoo.
" Barhabaa binti karibu ukae.
" Asante. Johari alivuta kiti akakaa.
" Samahani Kama nitakuwa nakupotezea muda.
" Usijali
" Samahani nilikuwa na uhitaji wa kazi naweza kupata kazi hapa?
" Mmmh nafasi za kazi zipo na Nina hitaji watu wawili mmoja wa kuingia asubuhi mpaka saa Saba na mwingine kuanzia saa saba mchana mpaka saa moja jioni.

Hii ilikuwanafuu kwa johari maana angeweza kupanga ratiba zake za masomo na kazi.
" Sawa nipo tayari Ila nilikuwa Nina ombi.
" Nakusikiliza
" Nilikuwa naomba niwe shift ya mchana maana Mimi ni mwanachuo.
" Hakuna tatizo kikubwa uwe mchapakazi.
" Hilo kwangu halina shida.
" Mshahara laki mbili Kama upo tayari kesho njoo uanze kazi na usaini mkataba .
" Asante nashukuru Sana baba.
" Karibu.
Johari aliondoka akiwa na furaha pia yule baba alitokea kuvutiwa na johari kwasababu alionekana mstaarabu pia uongeaji wake ulimvutia na kuwa na Imani nae kwenye kazi yake.

Upande wa pili kijana Ethan alikuwa alikuwa chumbani kwake kalala na mwanamke . Ethan aliamka na kujinyoosha alafu skamuamsha ule msichana
" Wewe umelala mpaka saizi unafikiri upo kwenu hapa hebu Nyanyuka haraka uondoke.
" Sabiri kwanza usinisukume.
" Hivi unafikiri Bibi yangu akikuona itakuwaje.
" Hilo Mimi halinihusu kwanza nipe changu.
" Wewe nijibu kwa jeuri nitakupitisha dirishani.
Aliongea Ethan huku akiwa anaenda kufungua droo akatoa kiasi Cha pesa na kumpatia.
" Shika bwana hakuna kuremba hapa.
" Unataka nitoke uchi, ukiendelea kunisumbua nitapiga kelele mpaka Bibi yako ajue kuwa umeleta msichana humu ndani.
" Unanitisha ndani ya kasri langu , hebu twende huko kabla Bibi hajaamka. Ethan alimshika mkono yule msichana na kumvuta nje huku akiwa kashika viatu vyake mkononi.
" Niache nivae viatu.
" Utavalia nje.
Waliburuzana mpaka kwenye lango kuu la kutokea nje ghafla wakasikia sauti ya Bibi yake ikisema .
" Nyie simameni hapo. Ethan na yule msichana walisimama na kumuangalia Bibi yake ambae alikuwa anawafuata waliposimama .




JOHAR (UBAVU WANGU NI WEWE) πŸ’“ 2

MTUNZI SMILE SHINE


Bibi Amanda alifika karibu Yana na kuwaangalia moja mmoja kwa zamu Kisha akauliza
" Ethan hiki Ni Nini?
" Ni rafiki tu.
" Alilala hapa ndani?
"Ndio Ila kila mmoja alilala upande wake.
"Mmmh Ni rafiki na mkalala kwa amani huko chumbani.
"Ndio Bibi huamini?
" Nakujua vizuri mjukuu wangu. Binti ondoka hapa . Yule msichana aliondoka akamuacha Ethan na Bibi yake .
" Wewe nifuate huku. Ethan alimfuata Bibi yake wakaenda kukaa kwenye Kochi.
" Ethan tabia zako zinanishinda Ni Bora utafute mke uowe.
" Mimi swala la kuowa siafikiani nalo kwani Bibi unangangania niowe unataka nigundue Nini?
" Kwani unavyobadilisha hao wanawake huwa unataka kugundua Nini?
" Oooh jamani hapa tutabishana mpaka kesho Hili limeshatokea naomba tusahau. Alisema Ethan huku akiondoka akielekea chumbani kwake.
" Yani miaka 35 nalazimishwa kuowa Yani hapa naongeza miaka mitano mbele ndio niowe.
" Kwahiyo unataka kuowa ukiwa na miaka 40?
" Na nikifikia hapo nitaangalia Kama itafaa.

Siku zilienda Johari aliizowea kazi na alikuwa mfanyakazi mzuri Sana na aliweza kupangilia muda wake vizuri Sana mpaka boss wake akatokea kumpenda .
" Johari upo vizuri Sana nimependa unavyojituma .
" Asante boss .
" Kwakuwa nimefurahishwa na wewe nimeamua kujiongeza mshahara nitakupa laki mbili na nusu.
" Asante Sana boss Mungu akubariki.
" Sawa kaendelee na kazi.
Wakati johar anaondoka simu ya Mr Philip (Boss) iliita alipokea akawa anaongea na mteja aliyekuwa anahitaji chakula.
" Johari , hebu njoo Mara moja. Johari alirudi akaenda kumsikiliza boss wake.
" Kuna mteja wetu anahitaji chakula nenda unatakiwa kupeleka.
" Sawa boss.

Chakula kilichohitajika kiliandaliwa na kupakiwa vizuri Kisha akakabidhiwa johari
" Johari na boss wake walitoka nje mpaka kwa dereva wa pikipiki.
" Ali mpeleke nyumbani kwa Noel.
" Sawa.
Johari alipanda kwenye pikipiki safari ya kupeleka chakula ikaanza.
Johari alifika kwenye jumba la kifahari lakina Ethan alihinyeza kengere mlinzi akafungua.
" Nikusaidie Nini?
" Nimeleta chakula.
Mlinzi alimruhusu aingie . Johari valitekbea hukubakiwa haangalii anakokwenda macho yake yalikuwa yakitazama mazingira mazuri ya Lile jumba alipofika karibu na ngazi za kuelekea kwenye lango kuu la kuingilia ndani alijikwaa na kutaka kuanguka lakini kabla haijafika chini alifikia kwenye mwili wa Ethan na kusababisha kile alichokibeba kuangukia mwilini kwa Ethan na kusababisha achafuke.
" Aaaah Kwani wewe Ni kipofu Yani nimekuona tangia Kule unakuja huku unashangaa shangaa kwani ulikuwa unaangalia Nini Cha ajabu?
" Samahani ilikuwa bahati mbaya.
" Yani watu wengine bwana wanafanya Lisa ukitegemea kuomba msamaha.
Ethan alikuwa mkali , johari alijaribu kuomba msamaha lakini ilishindikana aliamua kukusanya chakula kilichomwagika akaenda kuweka sehemu ya taka alafu akaamua kuondoka maana hakuwa na Cha kupeleka kwa mteja wake bi Amanda
Johari alirudi mgahawani akiwa anaogopa , aliingia ndani ya mgahawa na kutaka kwenda jikoni ghafla alikutana na Mr Philip, johar alisimama na kuinamia chini maana boss wake alikuwa kakunja sura.
" Umefanya Nini ? Mr Philip aliuliza kwa ukali.
" Nisamehe boss ilikuwa Kama ajali.
" Hivi nilikwambia kazi imekushinda na unatakiwa kuondoka hapa nitakuwa nimekuonea?
" Nisamehe boss wangu ninaihitaji Sana hii kazi nitakuwa makini wakati mwingine.
" Hivi unajua unataka kunipotezea mteja muhimu Sana?
Johari hakuwa hajibu lingine zaidi ya kuomba msamaha.
" Kwakuwa ulinieleza shida zako Basi nakupa nafasi nyingine ukiharibu Tena Ni Bora upotekee huko huko usije ukaniletea hiyo pua yako hapa.
" Asante Sana boss. Naahidi kuwa makini.
" Nenda jikoni kaendelee na kazi.
Johari alienda jikoni kuendelea na kazi nyingine , aliandaliwa mtu mwingine wa kupeleka chakula kwenye jumba la bi Amanda.

Baada ya siku mbili kupita Johari akitumwa Tena kupeleka chakula kwenye jumba la bi Amanda .
" Johari unatakiwa kuwa makini na kazi zako bi Amanda huwa hapendi ujinga ulifanya kosa kwa Mara nyingine utanifukuzia mteja wangu Sasa safari hii kuwa makini sawa?
" Sawa boss.
Johar alibeba kile chakula kilichoandaliwa akaondoka na kuelekea kwenye jumba la bi Amanda.
Baada ya muda Johari alifika aliingia ndani ya Lile jumba lakini safari hii alikuwa makini Sana aliangalia Kule anakoelekea. Alikutana na kijana wa kazi .
" Samahani nimeleta mzigo wa bi Amanda.
" Pandisha juu nenda kagonge kwenye chumba Cha pili upande wa kushoto.
" Sawa Asante. Johari alipandisha mpaka ghorofani alipofika kwenye korido iliyogawa vyumba akachanganyikiwa kidogo alikuwa kasahau alikuwa kaambiwa ainginge chumba Cha pili Cha upande gani.
" Mmmh hivi aliniambia kushoto au kulia? Ni Kama alisema upande wa kulia. Johar aliamua kuingia chumba Cha upande wa kulia. Alipoingia akawa anashangaa chumba hakikuonekana Kama kilikuwa chumba Cha mwanamke .
" Mungu wangu nitakuwa nimekosea hiki hakiwezi kuwa chumba Cha bi Amanda. Wakati anataka kutoka alisikia mlango wa chooni unafunguliwa alipogeuka kuangalia alikutana macho kwa macho na Ethan Tena akiwa kavaa boksa na juu alikuwa kifua wazi.
Johar alishituka na kutaka kukimbia .
" Wewe mrembo unaenda wapi?
" Samahani nimekosea sikupaswa kuingia hapa Nina paswa kutoka .
" Unatokaje kirahisi hivyo? Unafikiri msichana aliingia kwenye chumba changu huwa anatoka hivihivi?
" Unamaana gani kuniambia hivyo?
" Hivi haujavutiwa na Mimi hebu niangalie vizuri. Ethan aliniachia bila kuona haya lakini johar alishindwa kumuangalia alienda mlangoni haraka na kutaka fungungua Ethan alimfuata kwa haraka na kumshika .
" Niachie niende tafadhali. Aliongea johar huku akitetemeka na machozi yakitaka kumtoka. Ethan alimuangalia usoni akabaki kaduwaa .
" Usiogope njoo hapa tuongee.
" Wapi?
" Njoo tukae hapa. Ethan alimuonyesha kitandani
" Hapana nataka kupeleka chakula.
" Tutapeleka pamoja. Ethan alimshika mkono na kumvuta mpaka walipofika karibu na kitanda wakakaa.

Huko nje bi Amanda alikuwa anaulizia kwa wafanyakazi.
" Hivi mpaka saizi haijafika mtu wa mgahawani?
" Ni muda kidogo alifika binti mmoja nikamuekeza akuletee chumbani kwako.
" Sasa Kama ulimuelejeza she chumbani kwangu atakuwa kaenda wapi?
" Sijui, labda atakuwa kachanganya vyumba.
" Kwani Mr Philip ananitumia watu wa ajabu nyumbani kwangu kwani wazoefu hakuna?
Alifika bi Amanda alafu akawa anarudi chumbani kwake alipofika karibu na mlango wa chumba Cha Ethan alisikia Kama watu wanavutana.
Alisogea karibu na kusikiliza.
" Niache niende.
" Niambie kwanza unaitwa Nani?
" Johar
" Johar wewe Ni mrembo Sana nimevutiwa na urembo wako. Johar alimuangalia bila kujibu chochote. Muda ule ule mpango ulifunguliwa kwa nguvu na bi Amanda akaingia , johar alisimama haraka haraka lakini Ethan hakuwa na wasiwasi
" Ethan huyu binti Ni Nani?
" Ametoka mgahawani kwa bwana Philip na hapa alileta chakula.
" Kwani wewe ndio ulieagiza chakula?
" Hapana Ila kakosea tu njia akaingia huku.
" Sasa mbona umekaa nae kana ulitambua kuwa kakosea?
" Tulikuwa tunasalimiana.
Bi Amanda alimuangalia mjukuu wake maana anamjua tabia zake.
Wakati huo johar alikuwa akitetemeka kwa hofu.
" Binti beba hicho chakula unifuate. Johar alibeba kile chakula akawa akamfuata. Bi Amanda mpaka chumbani kwake na kuliweka mezani.
" Binti unatakiwa kujifunza vyema mbele ya mjukuu wangu Tena ukae mbali naesitapenda kuona Tena kile nilichokiona.
" Sawa bi Amanda.
" Unaweza kwenda.

Amanda alitoka chumbani wakati anashuka ngazi aliitwa na Ethan.
" Johari.
Johar aligeuka kumuangalia
" Matumaini tutazidi kuonana . Aliongea Ethan akitabasamu huku akishuka ngazi , johar hakumjibu aligeuka na kuendelea kutembea haraka haraka aliogopa asije akambananisha Tena.



JOHAR ( UBAVU WANGU NI WEWE)πŸ’“3

MTUNZI SMILE SHINE

Johar alishituka na kutaka kukimbia .
" Wewe mrembo unaenda wapi?
" Samahani nimekosea sikupaswa kuingia hapa Nina paswa kutoka .
" Unatokaje kirahisi hivyo? Unafikiri msichana aliingia kwenye chumba changu huwa anatoka hivihivi?
" Unamaana gani kuniambia hivyo?
" Hivi haujavutiwa na Mimi hebu niangalie vizuri. Ethan aliniachia bila kuona haya lakini johar alishindwa kumuangalia alienda mlangoni haraka na kutaka fungungua Ethan alimfuata kwa haraka na kumshika .
" Niachie niende tafadhali. Aliongea johar huku akitetemeka na machozi yakitaka kumtoka. Ethan alimuangalia usoni akabaki kaduwaa .
" Usiogope njoo hapa tuongee.
" Wapi?
" Njoo tukae hapa. Ethan alimuonyesha kitandani
" Hapana nataka kupeleka chakula.
" Tutapeleka pamoja. Ethan alimshika mkono na kumvuta mpaka walipofika karibu na kitanda wakakaa.

Huko nje bi Amanda alikuwa anaulizia kwa wafanyakazi.
" Hivi mpaka saizi haijafika mtu wa mgahawani?
" Ni muda kidogo alifika binti mmoja nikamuekeza akuletee chumbani kwako.
" Sasa Kama ulimuelejeza she chumbani kwangu atakuwa kaenda wapi?
" Sijui, labda atakuwa kachanganya vyumba.
" Kwani Mr Philip ananitumia watu wa ajabu nyumbani kwangu kwani wazoefu hakuna?
Alifika bi Amanda alafu akawa anarudi chumbani kwake alipofika karibu na mlango wa chumba Cha Ethan alisikia Kama watu wanavutana.
Alisogea karibu na kusikiliza.
" Niache niende.
" Niambie kwanza unaitwa Nani?
" Johar
" Johar wewe Ni mrembo Sana nimevutiwa na urembo wako. Johar alimuangalia bila kujibu chochote. Muda ule ule mpango ulifunguliwa kwa nguvu na bi Amanda akaingia , johar alisimama haraka haraka lakini Ethan hakuwa na wasiwasi
" Ethan huyu binti Ni Nani?
" Ametoka mgahawani kwa bwana Philip na hapa alileta chakula.
" Kwani wewe ndio ulieagiza chakula?
" Hapana Ila kakosea tu njia akaingia huku.
" Sasa mbona umekaa nae kana ulitambua kuwa kakosea?
" Tulikuwa tunasalimiana.
Bi Amanda alimuangalia mjukuu wake maana anamjua tabia zake.
Wakati huo johar alikuwa akitetemeka kwa hofu.
" Binti beba hicho chakula unifuate. Johar alibeba kile chakula akawa akamfuata. Bi Amanda mpaka chumbani kwake na kuliweka mezani.
" Binti unatakiwa kujifunza vyema mbele ya mjukuu wangu Tena ukae mbali naesitapenda kuona Tena kile nilichokiona.
" Sawa bi Amanda.
" Unaweza kwenda.

Amanda alitoka chumbani wakati anashuka ngazi aliitwa na Ethan.
" Johari.
Johar aligeuka kumuangalia
" Matumaini tutazidi kuonana . Aliongea Ethan huku akitabasamu, johar hakumjibu aligeuka na kuendelea kutembea.
Kuanzia siku Ile Johar alitawala akili ya Ethan. Ethan alitokea Sana kuvutiwa na Johari aliahidi kumtafuta na ikiwezekana awe nae kimapenzi.
Mara kwa Mara Ethan alikuwa akitembelea mgahawani kwa Mr Philip kwaajili ya kupata chakula ilimladi tu amuone Johar. Kwa upande wa Johar hakuwa anafurahia uwepo wa Ethan pale mgahawani kwao kwani alikuwa anamuangalia Sana na Kuna wakati alikulazimisha waongee.

Siku moja Ethan alienda mgahawani akatafuta sehemu akakaa akawa anamsubiri huduma, alienda muhudumu kwaajili ya kumuhudumia.
" Karibu .
Ethan alimuangalia alafu akasema
" Asante.
" Ungependa nikuhudumie Nini boss wangu?
" Mimi huwa napenda kuhudumiwa na muhudumu mmoja tu hapa kwenye mgahawa wenu hivyo nitamsubiri yeye. Yule muhudumu alikuwa kashamuelewa aliondoka na kumfuata Johar.
" Johar boss mtoto anamsubiri ukamuhudumie.
" Kwani wewe huwezi kumuhudumia?
" Hataki anakuhitaji wewe.
" Achana nae Kama hataki kuhudumiwa na muhudumu mwingine.
Johar alimpuuzia akaendelea na kazi zake nyingine.
Ilipita kana nusu saa Ethan alikaa akisubiri huduma kila muhudumu alipoenda kumsikiliza alimrudishia. Mr Philip alienda mpaka alipokaa wakasalimiana .
" Vipi mbona umekaa bila chochote?
" Nipo hapa kwa muda na muhudumu ninaemuhitaji haijafika kunihudumia.
" Ni Nani huyo?
" Binti mmoja hivi mrefu, ana macho flani ya kusinzia ,lips Pana , ana kiumbo flani Cha kuvutia. Ethan alitaja sifa za Johar na kumfanya Mr Philip atabasamu maana abamuelewa vizuri Sana Ethan Ni mtu wa Toto's.
" Sawa anakuja kukuhudumia.
Mr Philip alinyanyuka akaenda jikoni.
" Johar kwanini hutaki kumuhudumia mteja?
" Mteja gani boss?
" Ethan.
" Hataki kuhudumiwa na wahudumu wengine na Mimi nilikuwa Nina kazi .....
" Sikiliza Johar Ile familia kwa kiasi kikubwa wanaifanya biashara yangu kuwa nzuri naomba usije kuniharibia unajua yule alienda kulalamika kwa Bibi yake Mimi naweza kuharibu biashara yangu?
" nisamehe boss naenda kumuhudumia.
Johar alienda alipo Ethan Kisha akasimama pembeni .
" Vipi mrembo wangu mbona unechukua ?
" Nimefika niambie unahitaji Nini nikuhudumie?
" Naweza nisihitaji chochote Ila kukuona wewe tu moyo wangu unaridhika .
" Unajua unanishinda tabia wewe Kaka siku ya kwanza ulinitukana nikanyamaza, Mara ya pili ulinibananisha chumbani kwako nikatulia kwasababu nilikuwa kwenu mbali na hapo umekuwa ukija kula lakini huachi kuongea ujinga wako hivi unaweza kuniambia unachotaka kwangu Ni Nini?
" Swali lako ziri Sana , pia kwa like swala la kukutokea Ile siku ya kwanza hebu lipotezee sababu siku Ile nilikuwa sijamuona uzuri wako na nilikuwa na Mambo mengi kichwani kwangu . Sasa nakuja hapo kwenye swali lako la mwisho.
Johar Mimi mwenzio najikuta nakuwa chizi kwaajili yako ndio maana kila siku nakuja hapa ilimradi nikuone tu, Kuna muda nahisi wewe ndio mapigo yangu ya moyo... Kabla Ethan hajamaliza kuongea Johar alifyonza.
" Unanifyonza?
" Unataka nirudie Tena ndio ujue Kama nimekufyonza? Hebu sema unataka Nini nikuhudumie nimechoshwa na ujinga wako. Johar alikuwa mkari alimfokea mpaka. Mr Philip akasikia.
Mr Philip alinyanyuka alipokuwa kakaa akamfuata
" Hivi wewe binti unataka niongee rugha gani ndio unielewe?
" Lakini boss huyu Kaka Ni msumbufu.
" Johar huwezi kufanya kazi hapa nifuate. Mr Philip alitangulia , johar alimfuata huku akigeuka kumuangalia Ethan wakati huo Ethan alikuwa anatabasamu.



JOHAR (UBAVU WANGU NI WEWE) πŸ’“ 4

MTUNZI SMILE SHINE

Johar alifuatana na boss wake mpaka kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa kana ofisi.
" Johari wewe Ni Kama binti yangu nilikuwa naomba Jambo moja nataka uache kazi.
" Lakini boss yule Kaka ndio msumbufu ....
" Naelewa namjua vizuri Sana Ethan hawezi acha kukusumbua na Nia yake sidhani Kama itakuwa nzuri kwako. Mimi sipendi wewe uharibikiwe Wala sitaki kazi yangu iyumbe kwasababu naitwgemea kwa kuendeshea maisha yangu nikiwa na maana kumsomesha watoto wangu. Mr Philip alifungua drop akatoa kiasi Cha pesa na kumpatia Johan.
" Shika hizi pesa zitaenda kukusaidia najua unaweza kufanya hata biashara ndogo ndogo huko chuo lakini Kama utakuwa na tatizo lolote unaweza kunitafuta .
Kwakuwa Mr Philip alikuwa kashaamka Johari aondoke Johari hakuwa na lakusema alipokea zile pesa na kwenda kubadilisha nguo zake alafu akaondoka.

Alipofika anakoishi na wenzake alijilaza kitandani na kutulia. Eve alikuwa kajilaza kitandani huku headphone zikiwa masikioni alikuwa anasikiliza mziki , Vanessa alikuwa anajisikia kitabu alipomuona Johari karudi mapema Tena akiwa mnyonge alifunika kitabu akauliza.
" Vipi mwenzetu mbona umerudi mapema?
" Acha tu hapa nilipo nimechoka na siku yangu imeharibika vibaya mno.
" Mmm kwanini?
" Sina kazi.
" Unamaanisha umefukuzwa kazi?
" Naweza kusema hivyo.
" Kwani umefanya Nini?
" Kuja Kaka mmoja mpumbavu ndio aliesabanisha.
" Uligombana nae ukiwa kazini?
Kabla Johar hasasimulia ulivyokuwa alisikia Eve akisema.
" Mambo mengine ninkujitakia unajijua unashida na bado unagombana kazini.
" Eve usumlaumu kabla haujasikia anataka kusema nini. Johar ilikuwaje?
" Kuna Kaka mmoja ananisumbua Sana kwanza hataki kuhudumiwa na mtu mwingine zaidi yangu Yani ana Mambo ya ajabu Sana.
Eve alichosikia hivyo aliangua kicheko.
" Yani wewe huwezi kubadilika kila siku nakwambia badilika hapa Ni mjini , Sasa kosa la huyo Kaka Ni lipi hapo Kama kakuelewa kwanini na wewe usikubali kikubwa Skype pesa tu.
" Sio kila mtu anatania ya kujirahidisha Kama wewe ,Mimi Nina jiheshimu.
" Oooh kumbe, Sasa utakula heshima yako.
" Tafadhali Eve unaweza kumuacha mwenzio walau kidogo atulize akili yake? Alisema Vanessa
" Sawa namuacha Ila wakati anapitiliza hiyo akili yake iliuobeba heshima afikilie na maisha anayoishi hata bebwa kila siku.
Johar hakuwa anaweza kubishana alinyamaza na kila siku amekuwa anapuuzia maneno ya Eve.

Ethan aliendelea na tabia yake ya kubadili wanawake lakini mwanamke pekee alieisumbua akili yake alikuwa ni johari.
Ilipita kana wiki moja alikuwa hajaonana na Johar na sababu ya kuto kumuona alikuwa amesafiri. Siku aliyotudi jioni alienda bar wakawa wanakunywa na Marafiki huku pembeni yake alikuwa kakaa msichana ambae alikuwa atoke nae usiku. Wakati anaendelea kunywa ghafla lilinijia wazo la Johar, alitulia kidogo Kisha akasimama na kutoa pesa akaweka mezani alafu akasema
" Chris hiyo pesa utalipa bili Mimi naondoka. Yule msichana alichosikia hivyo nae alisimama kwaajili ya kumfuata.
" Vipi unaenda wapi?
" Tunaenda wote.
" Wapi?
" Si tulipanga kuwa wote usiku wa leo?
" Nimeahirisha sijisikii kulala na mwanamke.
" Sasa mbona umenipotezea muda wangu ?
"Unataka nirudishe muda nyuma au?
Ethan alijibunjwa jeuri wenzake wakaanza kucheka , Ethan aliondoka na kumuacha yule msichana kasimama huku akimuangalia kwa hasira.

Ethan alienda mpaka mgahawani Kama kawaida yake alikaa akisubiri Johar aende kumuhudumia . Kwakuwa wahudumu wanamjua walimpita hawakwenda kumsikiliza. Baada ya kuona kakaa kwa muda bila kumuona johar alimuita muhudumu moja ambae alikuwa anapita karibu na kumuuliza
" Johar Yuko wapi?
" Mbona hayupo hapa kwa muda Sasa?
" Unasemaje?
" Aliacha kazi?
" Kwanini, Mr Philip alimuachusha kazi?
" Inasemekana aliacha mwenyewe. Ethan alikaa kimnya kwa muda akifikiria na yule muhudumu akaamua kuondoka.
" Sasa kwanini kaamua kuacha kazi na nitampataje? Ethan alijiuliza
" Ila kwangu hakitashindikana kitu nitampata tu hata Kama atajificha chini ya handaki.
Alipita muhudumu mwingine akamuita.
" Samahani unaweza kuniambia sehemu anayoishi Johar?
" Mimi simfahamu Ila Davina anaweza akawa anajua alikuwa ni mtu wake wa karibu.
" Niitoe huyo Davina.
" Sawa. Yule muhudumu aliondoka akaenda kumuita Davina.
Davina alipofika Ethan alimuelezea shida yake , Davina alisita kueleza anapoishi Johar. Ethan alitoa pesa akampatia , Davina aliipokea na kuweka mfukoni.
" Johari ni mwanafunzi anasomea Mambo ya utalii
" Nini unanitania wewe? Ethan alishituka kwani hakuwahi kufikiria Hilo.
" Inawezekana vipi asomee na kufanya kazi ya mgahawa anapata wapi muda wa kusoma?
" Ndio alifanya hivyo kwasababu ya Mambo yake binafsi.
" Nitampataje Sasa?
" Ukitaka namba yake ya simu nitakupatia.
" Itakuwa nzuri zaidi. Davina alimpa namba za simu johari na Ethan alimshukuru na kuondoka akiwa na matumaini ya kukutana tena na Johar.
Ethan alipofika nyumbani kwao akiwa chumbani kwake alipiga simu kwa Johar, simu ilianza kuita akawa anamsubiri ipokekewe, baada ya sekunde chache Ilipokelewa na sauti nyororo ilipenya sikuoni kwa Ethan na kumfanya atabasamu.
" Hallow, hallow, mbona huongei? Aliuliza johari baada ya kuona kimnya wakati huo Ethan alikuwa bado akisikilizia sauti.
" Kama huna la kuongea Bora ukate simu.
" Siwezi kukataa ninayo mengi ya kuongea sema sauti yako inanibembeleza unanifanyia nipate usingize.
" Wewe Ni nani?
"Ethan Maxwell..
" Ni wewe tena? Unataka Nini kwangu Yani baada ya kusababisha niondoke mgahawani bado unanisumbua? Johar aliongea kwa ukali Eve na Vanessa wakawa makini kusikiliza. Eve aliona Kama anapitwa alisogea karibu akachukua simu ya johari na kuweka loud speaker ilivaweze kusikia vizuri.

" Unajua siwezi kuwa mbali na wewe nisipokuona kwa siku Ni sawa na mwezi , nimekutafuta Sana bahati nikapata namba yako na imekuwa nafuu kwangu maana sauti yako tu Ni Kama tiba kwangu...
" Unaongea ujinga gani?
" Wewe ndio unaona ujinga lakini kwangu Ni Jambo la maana sana. Johar unaweza kuniambia nitakupatia wapi Nina Jambo nataka kukwambia.
" Sina muda wa kuonana na wewe.
" Alijibu johar na kukata simu.
" Wewe kwanini unakataa ungeniacha tumsikilize , huyu Kaka yupo romantic balaa kwanza ana sauti tamu maneno unaambiwa wewe huku Mimi sijiwezi ....
Eve akiwa bado anaongea iliingia message kutoka kwa Ethan ikisema
" Najua unaniona Kama mtu wa ajabu lakini ukweli Ni kwamba kwako nimejikuta Sina ujanja mbele yako Kama ukomando nauweka pembeni , nanyanyua mikono juu nimesalimu amri nakupenda Johar.



JOHAR ( UBAVU WANGU NI WEWE) πŸ’“ 5

MTUNZI SMILE SHINE

Ule ujumbe walisoma wote watatu ilipofika zamu ya Eve akisoma na kupiga kelele
" Woyooooo hivi huyu Kaka hakuona wakwenda nae sambamba kwenye mapenzi mpaka akaangukia kwako usiejua thamani ya kupendwa Kaja wa watu anajua kumbembeleza hivi lakini wewe Wala mshipa haukushituki, natamani ningepata mwanaume anaejua Nini maana ya mapenzi Kama huyu.
Johar aliguna akasema
" Usilolijua Ni sawa na usiku wa Giza.
" Kwanini unasema hivyo? Vanessa aliuliza.
" Ethan ni kijana mtanashati anatoka kwenye familia inayojiweza Sana tu, ana kila kitu lakini shida yake ni Malaya nasikia anapenda Sana wanawake anaweza kulala na mwanamke yoyote Yule. Yupo Kama abashetani wa ngono
" Hayo yote umeyajulia wapi?
" Nilisikia mgahawani, Watu walikuwa wanasema.
" Kwahiyo unawasikiliza watu? Wengine wanamiwivu yao au chuki binafsi
" Lisemwalo lipo.
" Sikiliza Johar Mimi Ni mtu wa viwanja Sana nakutana na watu wengi kwahiyo nikimuona naweza kumjua , panga siku utukutanishe nae.
" Sitaki kwanza sifikirii mapenzi kwa Sasa .
" Unasubiri imalize kusoma ,upate ajira ndio uwe na mpenzi?
" Ikiwa hivyo itapendeza zaidi.
" sawa bikra wa watu Ila ipo siku utaitamani hiyo nafasi kwa huyo Kaka. Yani unamkataa mtu mwenye kila sifa ya kuitwa mwanaume eti kisa maneno ya watu. Fanya kile moyo wako unataka .
" Moyo wangu umegoma.
" Basi nikutanishe nae nijichukulie hiyo nafasi smaana sisi wengine tunaangalia masrahi.

Siku ziliendelea kwenda Ethan aliendelea kubembeleza kwa Johar japokuwa kuna wakati johar hakupokea simu yake kwa kuepuka usumbufu lakini Ethan alibadili namba akawa anampigia kwa namba mpya na kumtumia message za mapenzi zilizokuwa zinavutia na kusisimua .

Mwanzo ilikuwa kero Sana kwa Johar alikuwa akiona namba mpya akawa hapokei na message alikuwa anasoma bila kujibu. Ilichukua Kama mwezi na nusu bila Ethan kukata tamaa aliendelea kuelezea hisia zake kwa Johar.

Wiki moja badae Ethan alikuwa kimnya hakupiga simu Wala kutuma message. Siku moja johar alikuwa kitandani kwake akisoma message zote za nyuma alizokuwa akitumiwa na Ethan, akisoma huku akitabasamu ilionekana Kama vile zilimvutia au kumkosha.
" Mbona siku hizi yupo kimnya atakuwa kapatwa na Nini au ndio kashakata tamaa ya kunifuatilia? Mmmh lakini atajua mwenyewe.
Johar alisema hivyo kujipa tu moyo lakini kwenye moyo wake na akili yake alikuwa anafiki kitu juu ya Ethan pia taswila yake ilimjia kichwani kwake.

Siku moja nje ya nyumba wanavyoishi ilisimama gari moja ya kifahari na kuanza kumpiga honi mfurulizo.
" Ni Nani Tena huyo anatupigua kelele? Aliuliza johari na Vanessa akasema.
" Bila shaka watakuwa wanaume wa Eve, Eve nenda kamtulize mtu wako huko nje anatusumbua.
" Kwanini unipoint Mimi na usiseme wewe Vanessa huenda akawa mpenzi wako Jofrey .
" Mpenzi wangu yupo nje ya nchi hawezi kuwa hapa saizi.
Eve alienda kuchungulia dirishani.
" Aiseee unaweza ikawa inshu yangu imekuja na gari Kali ngoja niende.
Eve alivaa viatu vyake haraka haraka akatoka nje , alisogea karibu na Lile gari na kujaribu kuangalia kwa makini aliekuwepo ndani lakini hakuweza kuona kwaajili ya vioo vya gari vilikuwa havionyeshi mtu aliekuwepo ndani. Ghafla kioo Cha gari kilifunguliwa Eve alikutana nacho kwa macho na kijana handsome mwenye sura ya kuvutia Ethan.
Taratibu Eve aliachia tabasamu na Ethan alitabasamu pia na kuanza kumkagua kuanzia juu mpaka chini . Alitamani kuanza kumwaga Sera zake Ila akakumbuka kuwa kilichonipeleka sio hicho Bali Ni Johar
" Samahani mrembo unaweza kusogea karibu nataka kukuuliza swali.
Eve alisogea karibu na gari na kusalimia.
" Mambo.
" Safi.
" Samahani nimeelekezwa hapa Kuna dada mmoja anaitwa Johar?
" Johar?
" Ndio
" Wewe Ni Nani yake na ulikuwa unashida nae gani?
" Mbona maswali mengi dada kwani huyo mtu Ni muharifu?
" Hapana nilikuwa nauliza tu.
" Unamfahamu?
" Ndio yupo.
" Naomba uniitie.
" Sawa dakika moja. Eve alienda ndani .
" Johar Ni mgeni wako anataka kuonana na wewe.
Johar alishituka haujawahi tokea yeye kutembelea na mtu Tena mtu mwenyewe Kaja na gari Kali.
" Yupo je huyo mtu?
" Ni handsome mmoja hivi.
" Atakuwa Ethan? Aliuliza Johan
" Inamaana anaweza kuwa yule Mr romantic anaekutumia message nzur za mapenzi?
" Nahisi .
" Nenda kamuangalie kwanza.

Johar aliamua kwenda kumuangalia alipofika alikunja uso wake alipomuona Ethan.
" Kumbe hata ukikasirika bado unakuwa mrembo?
" Nani kakuelekeza hapa?
" Johar siku zote nyoyo zinazopendana huwa hazikai mbali hata siku moja ....
" Unamaanisha Nini unavyosema hivyo?
" Namaanisha kuwa Mimi na wewe tunapendana ......
" Mimi sikupendi. Alisema johar akiwa kamkazia macho , Ethan aliachia tabasamu alafu akasema
" Inawezekana bado haujajijua lakini acha nikupe muda kwanza badae utaelewa ninachomaanisha.

Wote walikaa kimnya wakawa wanaangaliana, zilipita dakika kadhaa johar akamuuliza
" Hicho ndicho kilichokuleta?
" Ndio, pia nilikuwa naomba unipe nafasi ya kuongea na wewe.
Johar alitaka kukataa Mara Eve alijitokeza na kuingilia maongezi yao
" Johar hebu msikilize mtoto wa mwanamke mwenzio hapa duniani watu tunaishi kwa kusikilizana Kama isingekuwa hivyo Basi wazazi wetu wasingeweza kuwa pamoja na sisi tusingezaliwa , mpe nafasi walau kidogo tu.
Ethan alifurahushwa na maneno ya Eve ilimbidi ashuke kwenye gari na kumsogelea Eve.
" Umeongea point ya maana Sana natamani nikupe zawadi.
Eve alibaki anacheka cheka .
" Mrembo unaweza kunisaidia kitu kimoja? Ethan aliuliza
" Bila shaka naweza.
" Naomba umshawishi huyu mrembo tuweze kutoka pamoja?


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote