Jamani Shemejii

book cover og

Utangulizi

Kutana na Binti wa 2002, Binti machachali kabisa wa Kihaya, si mnajua vile wamebarikiwa Mashape ? Walk vizuri jamani maua yao Tuwape.
Kinze Anatoka kijijini kwao bukoba na kwenda Dodoma kwaajili ya masomo.
Kinze anafikia Nyumbani kwa dada yake ambaye ameolewa, Kinze anakuwa na Ukaribi wa hali ya jui na shemeji yake, Mume wa dada wa Kinze, anachukua majukumu
Ya kumsomesha Kinze uku akimdanganya mambo mengi juu ya familia yake.
JE NI MAMBO GANI HAYO ? TUKUTANE KWENYE WEBSITE
JE KINZE NA SHEMEJI YAKE UKARIBU WAO UKOJE? TUKUTANE NDANI NDANI UKO….
💔🥹

JAMANI SHEMEJI
MTUNZI: PATRICIA DAMAS
SEHEMU YA: 01
ANZA NAYO…..

Niite Kinze, binti wa mwaka 2002, nyumbani kwetu Mimi Ndio binti wa Mwisho kabisa kuzaliwa kati ya mabinti wanne, nimekulia kijijini Uko bukoba.
Kwenye makuzi yangu maisha yangu nimekuwa kwa kudekezwa sana, sio mama tu wala baba, Yaani dada zangu wote walinipenda na kunijali sana.
Ndugu zangu walihakikisha kuwa nasoma sana, na nafikia malengo yangu, na katika kusoma sikuweza kuwaangusha kabisa, nilisoma kwa juhudi sana na kufaulu vizuri tu.
Niliweza kumaliza kidato cha tano na nilifahuru vizuri kabisa na kupelekea Mimi kupata nafasi kwenye chuo kikuu cha Dodoma.
Hapo naweza kusema kuwa maisha Ndio Kama yalianza kubadilika hivi, kwaajili ya elimu yangu, nilikalazimika kutoka nje na nyumbani, kwaajili ya elimu yangu nikalazimika kwenda mbali kabisa na mkoa niliozaliwa.
kwa Mara ya kwanza Kinze Mimi nikatoka ndani ya mji wa bukoba na kuingia Dodoma.
Kwanza kabisa nilifikia nyumbani kwa dada yangu wa kwanza ambaye aliolewa Uko Dodoma, dada yangu alikuwa ni mtumishi wa bank na mumewe ni daktari mkubwa tu.
Kwa kifupi wote walikuwa wasomi na wenye kazi za kueleweka sana, hivyo maisha Yao yalikuwa mazuri sana sana.
“Karibu sana Kinze, Yaani nilikaa kila saa najiuliza utafika saa ngapi ??”
Alizungumza dada yangu baada ya Mimi kufika nyumbani kwake.
Aaah nilifika nyumbani kwa dada angu kwa msaada wa Dereva wake, Yaani dereva wa familia yake Ndio alinifata kituo kikuu cha mabasi na kunileta mpaka nyumbani kwa dada.
“Eeeh dada hivi nyumba yako Ndio ya kısasa kiasi hiki ??”
“Kinze umeanza sasa, mdomo juu juu mdogo wangu, ata hivyo ni nyumba ya kawaida kabisa, we Soma sana halafu utakuja kuona na kuelewa “
Nilifika nikiwa Nina njaa sana, na kwenye mambo ya misosi bwana Mimi sio mtu wa kujivunga ata kidogo, pasi na kupoteza muda nikamuuliza dada angu.
“Hamjapika au ??”
Dada aliniangalia Mwisho akaCheka na kuniambia.
“Küpende kula tu, kwanza uoge then utakuja kula binti, ata hivyo umetoka safari ndefu sana acha kwanza mwili upumue”

******

Majila ya saa 3 usiku, shemeji mussa alirudi kutoka kazini kwake, nyiee, lishemeji langu ni lizuri sana, kuna muda nilikuwa Najisemea kimoyo moyo kuwa nataka mwanaume Kama shemeji mussa.
“Aaah Kinze, waooooh kumbe umefika ??”
Shemeji yangu aliniuliza kwa bashasha ya hali ya juu, lakini pia hakuishia tu kuniuliza alinisogelea na kunikumbatia kwa nguvu sana.
KWa upande Wangu ilinishangaza na kunishtua kwa kiasi chake, lakini kwa dada na shemeji ni Kama ilikuwa ni kawaida, dada alibaki akituangalia na kutabasamu tu.
“Shikamoo shemeji “
Nilimsalimia shemeji pale tu alipoacha kunikumbatia.
“Marahaba, eeeh Ndio umekuwa kiasi iki Jamani, urefu sasa ushampita dada Ako “
“Ahahha kawaida tu, Naona ma last born wengi ni warefu “
Nilijibu na kusogea pembeni, kuna Namna nilianza kuona ni Kama nakuwa uncomfortable mbele ya shemeji, ukizingatia nilishakuwa Mdada sasa, hivyo si kuona Sawa kabisa.

*******

Ilipita week moja uku nikisubilia siku ya kuwasili chuoni, Ikiwa ni siku ya jumatano, ilikuwa ni siku ya Mimi kwenda kufanya shopping, maana Nilitakiwa kununua vitu vingi sana vya Mimi kwenda navyo chuoni, Kwani nilikuwa nilienda kuishi hostel.
Kwa siku hiyo dada hakuweza kupata ruhusa kazini kwake , na ukizingatia Mimi ni mgeni sana pale jijini, hivyo nikalazimika kwenda kufanya shopping nikiwa na shemeji mussa, kwa siku hiyo shemeji mussa alikuwa akiingia shift ya usiku.
“Kinze unalionaje jiji ??”
Shemeji Kinze aliniuliza tukiwa ndani ya gari.
“Aaah ni zuri sana, linavutia na Naona kuna utulivu wa hali ya juu”
“Yaah ni kweli, Kinze shemeji yangu, maisha ni magumu sana, hakikisha kuwa unasoma sana, vijana wa mjini ni wajanja wasije wakakulaghai ata kidogo”
Nilitulia sana nikisikiliza maneno ya busara kutoka shemeji yangu.
Siku hiyo tulizunguka sana sana, shemeji alihakikisha kuwa napata kila kitu ninachoitaji, Mwisho kabisa tukamalizia na simu ambapo alininunulia I phone X, aaah shemeji alinibust sana maana nilikuwa nikitumia Itel Tena ya batani.
Baada ya kumaliza manunuzi yote, Mimi na shemeji tukaiingia kwenye restaurant kubwa sana na kwa pamoja tukaagiza chakula.
Nilijikuta nikiinjoy sana, ilifikia hatua nikawa Naona kama nilichelewa sana kuja uku kwa dada maana maisha ni mazuri mno.

********
Siku ya kuwasili chuoni iliwadia, na siku hiyo nilipelekwa chuoni na dada.
Aaah kiukweli safari haikwa ndefu, lakini Sikuinjoy ata kidogo, nilijikuta tu nikizungumza kimoyomoyo.
“Bora ningeletwa na shemeji tu “
Tulifika chuoni na baada ya muda na utaratibu kukamilika dada aliniaga na kuondoka, mwaya first year Mimi, moja kwa moja nikapelekwa kwenye hostel zetu.
Nilifika na kuanza kuweka kitanda changu Sawa maana kilikuwa hovyo hovyo, nikiwa naendelea kuweka mambo Sawa, simu yangu iliita na nilipoangalia ilikuwa ni Namba ya shemeji mussa.
“Abeeh shemeji”
Nilitika baada ya kupokea simu.
“Aaah njoo getini nimekuja kukuaga bwana shemeji yangu “
Aaah Mie tena, kwa haraka nikatoka nje na kukutana na shemeji yangu.
“Aaah nimekuja kukuaga mke mdogo, nasafirii kikazi nitakaa kama mwezi moja hivi “
“Aaah Asante sana shemeji yangu, Mungu akubariki uendelee kuwa na moyo huo huo mzuri “
“Sawa sasa, ukiwa na shida niambie”
“Sawa shemeji “
“Kingine, usimwambie dada Ako kama nimekuja uku, aaaah anaweza akanifokea maana uku nimezunguka mbali sana naweza nikachelewa ndege “
“BAsi Sawa shemeji yangu, wai usafiri wako, Ufike salama “
Nilimkumbatia shemeji Ikiwa ni ishara ya kumuaga, lakini ilikuwa tofauti kwa shemeji ambaye, alitumia mikono yake kutalii kwenye mwili Wangu na kunifanya nipate msisimko…..

ITAENDELEA….
JAMANI SHEMEJI
SEHEMU YA: 02
MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SONGA NAYO.........
Basi shemeji akanipatia kiasi kidogo cha pesa kisha akaondoka na mimi nikarudi zangu hostel, nilifika hostel na kukutana na mwanafunzi mwingine ambaye aliingia baada ya mimi kutoka.

"Mambo "
Alinisalimia msichana huyo mgeni, msichana huyo alikuwa mchangamfu sana na alikuwa na vibe lake la kutosha.
Baada ya salamu tukaamua kutambulishana na hapo ndipo nikajua kuwa msichana huyu alikuwa akiitwa Niffer, muda wa kupata chakula cha usiku, mimi na niffer tukatoka nje na kwendakununua chips bwana, si mnajua ukaribu wa chips na mabinti wa chuo ?.

********
Aaaah muda ulisogea na masomo yalitaladadi bwana, nilianza kuzoea mazingira ya chuo na kuanza kutengeneza marafiki zaidi, lakini rafiki yangu sana ambaye namuita BFF ni Niffer tu.
Kuna kitu nilikuaa sijawaambia, kinze mimi ni muhaya pure, najua mnajua sifa za kihaya, sura za baba ila shape sasa ni kama tumebeba za watanzania wote, kinze mimi nimejaaliwa shape moja matata sana, mguu ndio usiseme, watu wa mjini uwa wnaasema ni mguu wa bia.
Ikiwa ni majila ya saa tatu asubuhi, haikuawa muda wa darasani, hivyo mimi na shoga yangu tulibaki tukizululuka uku na uku, katika tembea tembea tuliweza kupishana na wakaka fulani hivi, ambao waligeuza shingo zao na kuangalia shape yangu vizuri.
"Sister"
Mmoja kati ya wakaka hao alijitosa na kuniita, kwakuwa hakuwa ametaja jina langu nilijifanya kuwa sijaelewa kisha nikaendelea na mate mbuzi mimi na shoga yangu.
Mkaka huyo alishindwa kabisa kuvumilia alichofanya ni kutifuata na alinisimamisha kwa kunishika mkono kabisa.
"Mambo zenu "
Alisalimia mkaka huyo"
"Safi za kwako ??"
Nilijibu uku nikitoa mkono wangu kwenye mkono wa mkaka huyo ambaye hakuonesha dalili ya kuachia mkono wangu.
"Naitwa Rich sijui warembo zangu ni kina nani ??"
Niffer bwana ni mcharuko sana kwa haraka akadakia"
"Naitwa niffer na huyu mwenzangu anaitwa kinze "
"Waooooh, majina yenu ni mazuri sana, aaah samahani kinze naweza nikapata namba yako,nina maongezi na wewe baadae kudogo"
"Mmmh kwanini namba si tunaweza kuongea hapa hapa "
Nilijibu, kiukweli sikuwa comfortable kabisa kwenye kutoa namba yangu ya simu, moyo wangu ulisita kabisa, lakini kabla mkaka huyo ajajibu swali langu nifa akazungumza.
"Nakutajia andika "
Basi rich akapata namba yangu kwa stahili hiyo, naada ya rich kuondoka , nikamgeukia niffer na kumuuliza.
"Kwanini umegawa namba yangu lakini ? "
"Kinze acha utoto wewe, me sijaelewa kabisa, yaani kwanini unaonekana kuyaogopa sana mapenzi sijui mahusiano "
"Ahaaha kilinlamba kikiwa kidato cha sita, naweza kusema kuwa nilikuwa na mihemko ya hali ya juu, nilianzisha mahusiano hayo, na kwakuwa mwili wangu ulinipushi kufanya jambo, nilijikuta nikivunja amri ya sita, achana na hivyo, rudi kwenye maumivu sasa weeh tangu siku hiyo nikasema basi sirudii tena "
Niffer alinicheka sana mpaka akaa chini kicheko cha niffer kilinikela sana aisee na kujikuta nikimuuliza kwa hasira..
"Kinachokuchekesha ni nini ??"
"Mapenzi ujayajua binti, ila siku ukiyajua utaacha kunishangaa kwanini uwa silali bwenini"
Aaah Ila Niffer ni mcharuko Jamani, Yaani yeye kwa weeek hostel anawezamakalala siki moja tu, kwenye Chumba chetu cha hostel typo wasichana wanne na katika wasichana wote hap maweza nikasema kuwa mimi ndio mtulivu.
Siku ziliendelea Kukimbia Jamani na nikawa mzoefu sana, ikiwa ni simu ya jumamosi, Majila ya Saa 4 usiku, roommate Wangu, Wallikuwa wakijiandaa kwaajili ya Mwenda club, walahi kuna Namna Nilianza Kuwatamani, niliwaangalia sana wakijiandaa Mwisho nikalopoka.
“Na Mimi Naenda”
Kwanza walifurahi sana, kila mtu alinichangamkia, bff Wangu Niffer akatoa mavazi yake ya hovyo na kunipatia ili mowers kuvaa.
Aaah walahi nilipendeza sana, nilibaki nikijiangalia tu kila muda, safari ya kutoloka hostel ilikuwa simple sana manna watu Wangu walishakuwa wazoefu kwenye haya mambo.
Tulifika club na kukutana na wanafunzi wenzetu kibao, kitu ambacho kilinivutia zaidi ni Mziki Jamani, nakumbuka ata Shuleni Kwetu bukoba walikuwa wakiniita Chizi mziki.
“Niffer Mbona ukuniambia Kama uku ndio Rahma Kiasi hiki ??”
“Ndo ujionee kwa macho yako “
Nikita naendelea kuongea na Niffer, sijui Rich alitokea wapi, moja kwa moja Alana kunishika mkono na kwa vibe la kutosha tuingia kati na kuanza kucheza mziki.
Nilicheza sana Mpaka koo likakauka, niliacha kucheza na kutoka kwaajili yak kwenda kununua Maji ya Kunywa, Ile Nafika tu kaunta kwaajili ya kununua maji, niliweza kukutana uso kwa uso na shemeji Mussa nika…….
NAKUJA MY ZANGU…..


JAMANI SHEMEJI
SEHEMU YA: 03
MTUNZI: PATRICIA DAMAS

SONGA NAYO.........

Kwanza nilishtuka sana, akili yangu na miguu yangu ikawaza kitu kimoja kabisa nikaona hapa ni kukimbia tu, haraka nikageuka Nyuma na kutaka kukimbia, kwakweli sijui ata shemeji alipiga hatua muda gani maana gafla tu akadaka Mkono Wangu.
Ukisikia za Mwizi ni 40 basi ndio hizi, Yaani zangu zimewai Kufika, Yaani ndio kwanza siku ya kwanza mimi kuja club halafu Nafumwa na shemeji kweli jamani.
Shemeji alionesha kuchukia sana, kwa ukali na Mwendo wa haraka akanikukusa moja kwa moja mpaka kwenye Chumba cha lodge ya eneo ilo na kunisukuma na kunifanya nianguke Kama Mzigo.
“Usiku huu unafanya nini uku kinze ??”
Shemeji aliniuliza uku akionesha kuchukia sana, nilibaki Nikiwa nimetoa macho na machozi yalikuwa yakinitililika tu.
“Kinze unajua ni Pesa Kiasi gani nimetoa mpaka wewe kufika hapa ?, unajua kwanini hautumii Mkopo lakini Ada yako yote ya Mwaka imeshalipwa ?”
Kwa haraka nikapiga goti Mbele ya shemeji na Kuanza kuomba Msamaha.
“Nisamehe sana shemeji, sitakuja kurudia tena, Nisamehe sitakuja kufanya ilo Jambo kwa Mara nyingine, shemeji Mimi sio Mzoefu, Leo ndio siku yangu ya kwanza Nisamehe Mimi “
Nilijikuta Nikianza kulia kama Mtoto Mdogo hivi.
“Nafikili natakiwa kumwambia dada Ako juu ya Hili suala, nafikili kwa kuwa ninyi ni wanawake, mtaelewana zaidi”
Hapo ndio nilizidi kiogopa kabisa, nyie dada zangu ni wakali, na sio dada zangu tu mpaka wazazi Wangu, Nililia sana uku Nikiomba shemeji anisamehe na kunifichia Siri yangu.
Baada ya kulia kwa muda Mrefu, shemeji alinisogelea na kuniinua pale nilipokuwa nimepiga goti.
“Usije ukarudia tena Sawa ??”
Shemeji aliniambia.
Aaah nilifurahi sana, niliona kweli shemeji yangu ni Mzungu Bwana, basi shemeji yangu akanikumbatia kwa Nguvu ili kuniweka Sawa maana nililia sana hivyo nilipatwa na kwikwi.
Katika kukumbatiana na kutulizana, shemeji akaaanza kunipapasa kama siku ile ambayo alikuja Chuoni kuniaga, kwa Wakati huo, niliona uwenda ndio stahili
Ya shemeji ya kukumbatiana.
Nilitulia tu uku nikiwa na Imani Kubwa sana juu ya shemeji yangu.
Mpapaso wa safari hii Bwana ni Kama ulianza kupitiliza hivi, Mwili ulinisisimka sana, kuna muda niliona ni Kama miguu yangu inaanza kukosa nguvu, niliona kabisa nimeanza kuwa dhaifu.
Muda mfupi tu, shemeji Aliweza. Kunisoma vizuri na kwa haraka akahakikisha Mimi na yeye tuna kiss, naweza Kusema kuwa hisia za haraka haraka ni Mbaya sana.
Akili yangu ilikosa kabisa ufahamu, nilijikuta nikiitaji sana Mchezo ambao shemeji ameuanzisha.
“Kinze huyo ni mume wa dada yako “
Nilijikuta tu nikizungumza Kimoyo Moyo na haraka nikamsukuma shemeji maana daaah nilichokuwa naenda kukifanya akikuwa powa kabisa.
“Oooon , am sorry kinze, woiiiih , sijui nini kimenipata Ila Nisamehe sana shemeji yangu “

Shemeji allionekana kujutia sana kwa kile ambacho kimetokea, Moyo Wangu ulijawa wasiwasi wasiwasi wa hali ya juu na kwa haraka nikataka Kutoka nje lakini shemeji akazungumza.
“Naomba ili lililotokea Liwe baina yetu tu, na nakuaidi haitakuja kutokea tena, nakuheshimu sana shemeji yangu kinze “
“Hakuna shida shemeji “
Nilijibu na kwa haraka nikatoka nje, nilitembea kwa Mwendo wa haraka sana, safari yangu ilikuwa ni kurudi kwenye ukumbi wa club ili niweze kuonana na wenzangu, na ikiwezekana tuondoke kabisa.
Kabla sijafika kwenye ukumbi wa club, nilishanga kusikia Kelele za watu, kwa muda huo ata Mziki haukuwa ukisiikika na hiyo ilinipa wasiwasi zaidi.
Nikiwa naendelea kushangaa Shangaa, gafla Nilivutwa mkono na baada ya muda Nilijikuta Nikiwa kwenye Chumba kile kile ambacho Nilikuwa na shemeji.
“Unataka kukamatwa na police au ? Wenzio wanawakimbia mapolice, halafu kuna wewe hapo umeganda kama upo kwenye shirika la utalii”
Alizungumza shemeji kwa kunifokea sana, nilishia Kimshukuru tu shemeji, maana Kama ningekamatwa na police sijui ningejitetea kwa njia gani kinze Mimi.
Kwakuwa muda ilienda sana, na nilikuwa sijui ni kwa njia ipi naweza kufika chuoni, niliamua tu kumuomba shemeji anisaidie kunifikisha chuoni.
“Kinze hii ni Saa 9 Kasoro, nafikili ungelala hapa then asubuhi nitakudrop chuoni Kabla sijaenda kazini “
“Mmmmh “ niliguna.
“Aaah kuhusu kulala, Mimi nitalala kwenye kochi usijali kabisa shemeji yangu, Kikubwa ni usalama wako “

*********

Basi kwa Mara ya kwanza nikalala Chumba kimoja na shemeji yangu, ambapo shemeji Alilala kwenye kochi nami nikalala kitandani.
Niliamka Nikiwa nimechoka sana, Niliangalia Saa na kuona kuwa ni Saa 4 kasoro asubuhi, kwanza nilishtuka sana, nilijilaumu sana maana nilikuwa na kipindi cha Saa 2 asubuhi na kwa ujinga Wangu kipindi kikanipita.
Kwenye kochi ambapo alilala shemeji, kulikiwa na Nguo nyingine ambapo ni Mpya, nilikuwa kabisa kuwa shemeji ndio amenunua maana nisingeweza kurudi chuoni na Nguo ya club .
Nilikoga na kuvaa mavazi yangu mapya, baada ya muda safari ya kurudi chuoni ikaanza.
“Usije ukamwambia dada yako kuwa Mimi na wewe tumeonana Sawa ? Maana akijua, utanifosi Mimi kusema ukweli wa mambo “
“Sawa shemeji “
Tulifika chuoni, shemeji akanikabizi kiasi cha Pesa na cha ajabu, akashika mkono Wangu na kuubusu nika…….

ITAENDELEA….


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote