DESMOND (LINI UTANIPENDA?)

book cover og

Utangulizi

DESMOND Ni mkasa unamuhusu salma baada ya kukutana na familia ya kitajiri ya Desmond
Mama wa Desmond amamuomba Salma kuolewa na mwanae ambae anatabia mbaya za ajabu ajabu akiamini mwanae baada ya kuoa atatulia na salma ni mdada mwenye maadili..
Desmond anakubali kuoa kwa sababu ya kumlidhisha mama yake lakini hakumpenda hata kidogo salma ili amlidhishe mama yake akaamua kumuoa kama Zegelesha , Maishanya ndoa ya salma yanakuwa kichomi kwa sababu Desmond ndo kama alipata Uhuru wa kufanya starehe zake huku akisingizia anatoka na mkewe kumbe anafanya yake hata hakuwa na mkewe ...
Mama aliamini salma ni mdada mwenye maadili sana akiolewa na mwanae atambadilisha lakini mambo yakawa nyuma mbele na salma hakuwahi kusema mateso anayopata kwenye ndoa yake

DESMOND (LINI UTANIPENDA?)❤❤01

Naitwa salma , Nimezaliwa Tabora ,kiloleni nimesoma huko shule ya msingi na Secondary ..
Nilipo maliza elimu ya Secondary majibu yalitoka nimezungusha nilipata Zero , kwahiyo sikuambulia hata cheti tu
Baba yangu aliongea kama atoke na ulimi mwenyewe , shangazi yangu yeye anaishi Dar es salaam akamwambia baba anichukue kwani yeye alisome et mie nisome nifauli akili nimetoa wapi wakati sio upande wa baba wala huo wa mama wote ni La Saba Felia ,At least mie nimefika hicho kidato cha nne ...
Niliondoka Tabora , kwenda Dar es salaam , Haikuwa mara ya kwanza kufika Dar tushakuja mara kibao likizo kwa shangaziii
Alikuja kunipokea mtoto wake mkubwa wa kwanza kumzaa.
Shangazi yangu anafanya kazi za ndani mbali kidogo na mitaa ya nyumbani kwake huwa anakaa huko mpaka w/end ndio anarudi kwake
Ana watoto wawili mmoja wa lika langu mwingine bado mdogo huo wa lika langu yeye aliacha shule Form two kabisa
Ndo mana hata baba alipo kuwa ananinyima raha kisa ku feli yeye alikuwa upande wangu mana mtoto wake mwenyewe zero kabisa
Ana mtoto mwingine mdogo ambae yupo darasa la tano , huwa anamuacha na dada yake kwa kipindi chote ambacho yeye anakuwa yupo kazini mpaka mwisho wa wiki ndio anarudi nyumbani ..
Wakati mie nimefika sikumkuta Shangazi alikuwa yupo kazini mana mie nimefika Ilikuwa Jumatano ..

Mtoto wa shangazi anaitwa leah yeye alikuwa anauza mahidi ya kuchoma sio mbali sana na nyumbani

Ijumaa shangazi alikuja jioni kabisa akanipokea Vizuri sana , Alinipa hela ya mtaji wa mahindi niwe nauza na Leah

Jumamosi na mie nilianza kuuza mahidi ila sio pale kwa Leah mie nilienda kwenye kituo cha dala dala cha tatu kutoka anapo uzia leah ,Lakini nikiwahi kumaliza nampitia kwake ndio tunaenda nyumbani ama yeye akimaliza ananipitia mimi ...

Maisha ya pale mazuri niliyapenda mana kuna amani tunapendana walinipokea Vizuri mno hatuli vitu vizuriiii lakini hatushindi wala kulala njaa , Shangazi akirudi W/end hiyo anatuletea ma pocho pocho kama yotee , kwahiyo raha kama zote leah nae alikuwa ananikubali sana

Kingine nilichompendea shangazi yangu hakuwa na tamaa et umeuza hela umpe !! Hapanaa!!

Unachouza unatoa kidogo mchango wa kununua chakula nyumbani , tunachanga na Da leah na yeye alikuwa anatuachia hela ya kula wiki nzima sio et kwakua tunakazi ndio Hatujali akhaa!!

Helaa anaacha kama kawaida , na wakati mwingine pesa za shule za Rose yaan yule mtoto wa mwisho wa Shangazi tulikuwa tunampa maisha yanaenda

Nilikiwa na nunua viwaloo karibu kila siku mana pesa zangu sikuwa naza kufanya nilikuwa namtumia na mama mara kwa maraa , nilikuwa nanunua nguo ili siku nikienda nyumbani wasinambie nimepauka

Si mnajua ile ukirudi mkoa cha kwanza wanaanza kukukagua kwanza umepauka au vipi!!
Basi mie nilikuwa najaza nguo hatari ..

Ulipita mwezi tayari nilikuwa nishakuwa mwenyeji mzigo natafuta mwenyewe kona zote nazijua hapo nilikuw na miaka kama kumi na saba tu lakini nina mwili mkubwa kidogo unaweza sema hata nina ishirini naa huko
Lakini sio ule mwili wa kuboa usije sema tipwa tipwa buree

Kuna siku shangazi alikuwa nyumbani ilikuwa jumamos hapo alikuja ijumaa nyumbani , na siku hiyo mie sikutoka
Mida ya jioni akapigiwa simu na boss wake akamwambia kuwa kuna wageni wanakuja gafla kutokea SOUTH AFRICA

Hao ma boss zake shangazi ni watu wa SOUTH AFRICA wapo Tanzania kikazi
Walivyokata simu shangazi akaanza kulalamika
Wanamfanyisha kazi nje ya majukuku yake lakini hapo walimwambia watamlipa malipo ya ziada mbali na mshahara wake

Nikamwambia shangazi si wanakupa hela nje na mshahara , akanambia hela sio kila kitu Salma , we unajiua mwili wenzio wanabaki wazima unakufa naa pesa zenyewe unaziacha mie nimechoka sanaa

Nikamwambia mie nngekuwa napajua nngeenda mie mwenzenu vile napenda hela shangazi acha tu
Akanambia enhee we ndio umesema twende wote tukasaidizane halafu utachukua hela

Hao wakiwa na wageni kuna kuwa na kazi kibao kwa wahindi vile aah

Nikasema sawa tu mie nipo tayari , basi tukajiandaa fasta fasta Akampigia simu leah mana leo alikuwa kibaruani kwake akamwambua tunaondoka mimi na yeye akasema sawa

Tukaondoka ni mbali kidogo lazima upande dala dala , ukishuka unatembea kidogo sio mbali na bara bara

Tukafika nje kuna geti kubwa nje ya Geti kuna Camera nyumba nzurii ya Ghorofa nje tu ilikuwa nzuri kweli

Kuna sehem akabonyeza shangazi geti ikafunguliwa na mlinzi ,nikakutaana na yale wanaita ma swimming pool
Ndio mara yangu ya kwanza kuliona Live
Kulikuwa na vitanda pembeni
Basi hata sikujivunga et nisiwe mshamba mwenzangu nilishangaa vizuri tu

Kulikuwa na bembea mbili kubwa mmh nikasema moyoni wanaushi kitajilii hawa nao

Tukaingia sebleni , ilikuwa seble ndogo lakini mamaaa !! Ipo Quality hatari

Sofa za bei kalii bonge wa mtiviiii , halafu ukutani wameweka Wallpaper nzuriii subule imepoaa haijachachuka mbele ya seble kuna Dinning room Halafu pembn ndio kuna ngazi za kwenda juu yaan pale chini hakuna chumba vyumba vipo Juu huko ..

Sebleni pale tulimkuta mmama mmoja na mwanaume wamekaa , shangazi akanitambulisha kwa yule mama ni mtu mzimaa flan hivi lakini kutokana na hela anaonekana bado mdadaa ..

Walinichangamkia kweli tofauti na nilivyokuwa nafikiria , yula mama akawa ananiuliza uliza ile unaitwa nani baba hajambo sijui ninii
Na mie nikawa najibu kwa utiii mana nilijua ndio ma boss wa shangazi na hapo walikuwa mtu na mume wake

Yule mama akamwambia shangazi , wageni wanafika hapa hivi punde naomba unisaide kuweka mazingira sawa
Shangazi akasema haina shida nimekuja na jeshi hapa kutakuwa sawa


DESMOND (LINI UTANIPENDA?)❤❤02

Mwandishi::Malkia Osam

Tukaanza heka heka ingilia hapa kutokea pale pita huku pita kulee,Li saa moja tu vyakula vyote vilikuwa tayari

My dear hapo tunaongelea vyakula kama nane hivii tofauti tofauti , nilikuwa Hoi lakini sio sanaa

Wageni walifika Sa tano usiku , shangazi Tumbo likamshika hata kusogeza mguu hawezi nikamwambia shangazi we pumzika mie nitafanya akasema hapana bwana ngoja nijitahidi

Nikamkazia apumizike mie nikatoka kuhudumia chakula ,walikuwa Familia ,Baba na mama na watoto wao wanne,
Walipo maliza kula nikatoa vyombo nikasafisha meza nikaweka mazingura safi hao watoto wanne kulikuwa na watoto wadogo wawili mapacha miaka minne nikawachukua nikaenda kuwaogesha nikamuuliza mama mwenye nyumba chumba cha kulala watoto

Mana wao walikuwa bize kupiga story kuongea habari za safari kuulizana hakuishi akanielekeza nikaenda kuwaandalia nikawalaza

Ndani ya masaa mawili kila kitu kilikuwa safiii kabisa jikoni palikuwa kama hapajapikwa kitu nishasafisha achaa

Mama mwenye nyumba akaja jikoni akakuta pako safii akanambia jamani ungeachaa tukasafisha Asubuhi nenda kapumzike salma jamanii
Nikamwambia mama yangu hata usijali usijali kabisa nachofanya nakijua na nimetaka mwenyewe

Akacheka akanambia haya bado nini hapa tusaidizane nikamwambia kila kitu tayari hapa bado kulala tu akacheka kweli akasema basi nenda kapumzike

Nikaenda chumbani kwa Shangazi akanambia pole jamani nikawambia hata usijali bwana hakuna hata kazi za kuchosha ..

Sie kwetu tumezoea kazi kazi kwahiyo sikuona shida sanaaa mana nimetoka kwenye familia ya heka heka

Asubuhi niliwahi kuamka shangazi alikuwa bado hajisikii Vizuri , nikamwambia hakuna kazi nyingi kwahiyo yeye akae mie nimalizie tuondoke nyumbani

Nilikuwa wa kwanza kuamka bado giza lile giza la Alfajir lipo, nikatoka chumbani wakati nashuka ngazi kwenda jikoni nashangaa namuona mtu mkaka yupo kifua wazi anaingia ndani kwa kunyataa viatu kashika mkononi

Nikishtukaa nikasema labda mwizi we mtu anatembelea vidole vya miguu ili hatua zake zisiskikee

Uvumilivu ulinishinda nikajikuta napiga kelele mamaaa!!! Aliniwahi mbio akaniziba mdomooo akasema we mpuuzi ninii kwa sauti ya chinii nikasikia mama mwenye nyumba akauliza kuna niniii huku mlango unafungulia

Yule kaka akanambia we Falaa Hakikisha hujaniona ole wako mama ajue hili ....
Hee!! Makubwa nikabaki mdomo wazi akaingia chap kuna chumba kilikuwa karibu hapo

Mama nae akawa ametoka akaniuliza ni nini Salmaa , nikasoma Mungu wangu naombeni mnisamehe ni mende tu nimeshindwa kujizuia

Baba mwenye nyumba akatoka anauliza mendee?? Kwani hamkupuliza dawa ya wadudu mna muda gani humu ndani
Akaja na dawa akaanza kupuliza mpaka jikoni huko mie kimyaa
Lile neno falaa bado linajirudia kichwani nilijisikia vibaya mtu anawezaje kumtukana mti ambae hata hamjui ndio kwanza kamuona leo afu anamtukana Alinitoa mood ya kuwa hapo ....

nilikosha vyombo vyote, nikaandaa kifungua kinywa nikaweka mezani , nikafanya usafi nje na ndani wanaamka watu tayari nishamaliza kila kitu

Tena mana ng'aa sio poa , Yule mama mgeni akanambia jamani we bint kiboko Hongera nikacheka

Watu wote wakawa mezani pale na shangazi na mimi wote wanakula pamoja hapo mezani baba mwenye nyumba , walinambie niwaite baba na mama
Basi niseme baba akauliza Kwani DESMOND yupo wapii , mama akajibu bado amelala baba akasema amelala nyumbani mama akasema ndio alikuwepo chumbani kwake tu

Muda huo akaja mkaka mmoja akashuka kutoka juu , jana yake sikumuona baba alipo muona akasema Hee Derick upo hapa na wewe akasema ndio nilifika jana usiku nikakuta mmelala sikutaka kuwa sumbua

Alikuwa anaongea huku anasogea kwenye meza kukaa nae , baba akanambie Bint yangu samahani naomba ukaniitie kuna kijana chumba hichi mwambie chakula tayari nikaenda mlangoni nikagonga akasema nanii
Nikasema nimeambiwa nije kukuita chai tayari akasema Poa!!

Daah nikajua ni lilee jinga lilee , mie nikarudi zangu zikapita kama dakika Tatu akatoka yule yule kaka ambae aliniziba mdomo

Akaketi kiti cha pembeni yangu ndio kilikuwa wazi...

Yule Derick yeye alikuwa anaonekana mkubwa lakini amefanana kila kitu na Huyo ambae alinitukana

Huyo Derick akasema naona tunamgeni mungine hapaa mama akauliza nani Derick akanioneshea mimi kwa ishara
Mama yake akamwambia aaah huyu ni Mtoto wake na mama leah amekuja kumsaidia tu mara mojaa
Shangazi akaongezea ni mtoto wa kaka yangu ,Derick akajibu ni mzuri mashaallah mama akasema Sanaa halafu ni mchapakazi mpaka rahaa amenifurahisha sanaa

Mie nikawa nacheka cheka tu sasa nitasema niniii?? Yule mama mgeni akasema jamani kumbe huyu sio mschana wenu ooh yaan amenifurahisha tangu jana jamani una miaka mingap

Nijibu kumi na saba mama akasema kumbe mdogo bado mie nilijua hata kwenye 20 huko nikachekaa
Basi story ikawa mimi hapo na baba akawa anachangia wote kasoro yule kaka tu yeye anakula kimyaa

Mpaka baba yake akamuuliza Desmond Vipi kazi jana ,ulichelewa kurudi kulikuwa na kazi nyingi??

Alikuwa anakunywa chai akapaliwa akawa anakohoa huku ananitazama mie kwa jicho la chini sasa na mie nilimtazana huku kichwani najiuliza maswali yangu
Akasema ndio nilirudi mda umeenda kazi zilinitinga sanaaa
Wakati karudi Asubuhi mie namuona
Mama akasema Hongera sana mwanangu akasema Asante mama akanitazama tena mimi

Mie nikatabasam tu,, kama kuna kitu flani nilielewa
Baada ya chakula ,nilitoa nikasafisha nikaosha vyombo nikapaweka sawa ,

Mama akanipa elfu50 akanambia nimekupenda sana Salma uwe unakuja kutusalimia mara kwa mara tafadhalii nikasema sawa nimefurahi kuwajua na mimi

Tukaondoka na shangazi kurudi kwetu , Jiani nikamwadithia heka heka ile ya Asubuhi mana nilipo itaa kwa kelele na yeye alitoka
Akanambia ndo mana nilishangaa huyo mende wakati tangu nianze kufanya kazi humo ndani hakuna mdudu anae ruka wala anaetambaa anakatisha humo


DESMOND (LINI UTANIPENDA?)❤❤03

Mwandishi::Malkia Osam

Nikamwambia shangazi mie sijapenda kwanini anitukane vilee mtu hata hanijui
Shangazi akanambia yaan huyo mtoto ni kichaa cha familia unawajua wale vichaa wa ukoo huyo ndio kachaguliwa kubeba ukichaa wa ukoo wao sasa ni mwehu mpaka wazazi wanamchoka

Ila ndio kipenzi cha mama wazazi wake kuliko hata Derick kaka yake , akanambia huyo Derick ni mtu mmoja safi sana hana shida na mtu ana heshima anampenda kila mtu uwe nacho uwe huna , uwe mdogo au mkubwa hana ubaguzi

Lakini Desmond ohoo lile ni balaa lilee hapendi kazi ,Kiburii pale kwake starehe na yeye , Yeye na starehe analazimishwa kufanya kazi na mama yake huwa anasikiliza kila anachosema mama yake na huwa anafata maamuzi ya mama yake huwa hayapingi wala hana hiyo sauti anamuogopa mama yake kuliko hata baba yake

We achana nae mi namuonaga mjinga tu muhuni huyo kazi yake ni kubadilisha tu wanawake wa Bar .....

Shangazi alinipa maelezo mengiii sifa mbaya mbaya tuuu hakuna sifa hata moja nzuri nikajikuta na mimi limenitoka moyoniii hilo kaka silipendi kama ninii ......


Mie nikaendelea na mishe mishe zangu sikuwa na mpango wa kurudi kule tenaa nina kihela changu hakaa!!
Nikaendeleze kukimbiza maindi yangu
Shangazi kwakua alikuwa anaumwa walimpa wiki moja la kukaa nyumbani ilivyoisha akaendelea kwenda

Akanipigia simu akanambia salma unaitwa na dada huku unaweza kuja leo ??
. Yaan naitwa kulee anapo fanya kazi yeye Boss wake anamuita dadaa
Mmh nikamwambia shangazi kuna nini?? Akanambia we njoo utajua huku nikasema sawa

Nilikuwa ndio nimetoka kutafuta Biashara yangu nikaiweka Vizuri yaan nikaandaa kabisa kwamba nikirudi tu naenda eneo la biashara

Nikapanda dala dala mpaka huko nikawakuta na wale wageni bado wapo kumbe hawajaondoka tu ,

Wakanikaribisha Vizuri mama akanambia Samahani tumekusumbua sana salma lakini mdogo wangu ana shida hapaa
Mmh nikawaza shida gani sijui mie naweza kuwasaidia nini hawa !!

Nikasema ipi mamaa!!?
Akanambia Salma mdogo wangu amekupenda kweli anaomba uende nae ukamsaidie saidie kazi atakulipa Vizuri utakuwa kama mtoto wa nyumbani pale
Mmh nikasema mamaa!! Shangazi amesemaje??
Akanambia ndio amenambia niongee na wewe mwenyewe nikasema ni wapii akanambia ni south Africa ,

Nikasema mmh huko mbalii baba yangu hawezi kukubali akasema kama umeridhia mie nitaongea nae nikasema sawa jaribu
Nilichokuwa namba ya baba nikampa akampigia akamuelezea wee baba akasema hapana hapana hapana huko mbalii siwezi kumpeleka huko mtoto wangu hakuna kwenda

Walimbembeleza na kumbembeleza baba mkalii alifokaa tena shangazi akachukua simu kumuelezea we alimpa yake akamwmbia kwani leah si yupo hapo haya mpeleke huyo mwanangu sitaki kama umemchoka naomba unirudishie mwananguu ..

Yakamshukaa akakata simu akawaambia jamani mie sina kauli lwa huyo mtoto ,
Moyoni mie nilishukuru Dar nilivyo izoea hivyo afu unitoe mbalio akhaa nilishindwa tu kuwakatalia

Basi hawakua na lakusema wakanambia sawa , mama akanisisitiza tena niwe naenda kuwatembelea nikasema sawa nikaaga kuondoka

Wakati natoka na Desmond alikuwa ndio anaingia yeye mbele nyuma yake alikuwa Derick kaka yake wote ndio walikuwa wanaingia

Huyo Desmond alinipita kimyaa hata salamuu
.Derick akasema Ohoo nani huyuuuu ??
Mie nikacheka nikamwamkia akaitikia akanambia Salma eeh?? Nikasema ndio akasema safiii ka jina kazurii sana

Nikacheka huku natoka akanambia mmh usinambie ndio unaenda hivyo nikasema ndio akanambia embu ngoja nikuombee lift hapaa

Akamuita Desmond alikuwa ashapita chumbani kwake akamuita tena baada ya kuwa kimya ile ya kwanza , Ndio akatoka

Akamwambia Dogo si unaelekea juu ,akasema ndio akamwambia embu mpe lift huyu Bibie
Desmond akanitazama yaan juu mpaka chini halafu akaniuliza unaenda wapi nikamtajia
Akasema mie siendi huko akarudi chumbani kwake
Mama yake akamwambia mpeleke halafu nenda na shuhuri zako

Nikasema hapana mama hata hivyo kuna sehem napitia hata msimsumbue jamani huku natoka Derick akanishika mkono nisitoke ,, mama yake akamwambia Desmond mpeleke anapo pita halafu mpeleke kwao mana sie ndio tumemuita hapaa ...

Akatoka kanunaaa hata mie sikupenda aisee ila ndio nitafanyaje
Derick hakuniachia mkono akanivuta mpaka parking akafungua mlango wa mbele akanambia haya keti hapo mie nikaingia

Desmond nae akawa amefika kavaa pensi na Vest na mguu mzuri ana vinyweleo mpaka raha sina tu ndio Linajishaua sana mfyuu

Halafu hata hamzidi uzuri kaka yake , Derick anaongea Vizuri aisee anatembea vizuri mpaka kucheka anacheka vizuri sio mtu wa kukurupuka hizi siku mbili nimemzoea nikampenda ....

Tulienda njiani kimyaaa hakuna hata kupiga story mie nilikuwa bize na simu nipo nachat na leah hapo namwadisia habari za kazi huko SOUTH ,

Tupo tunachati nikasikia kwahiyo utanielekeza unapo ishi au utaendelea kuchati na huyo mpuuzi wako si angekufata kama anakupenda kweli wapuuzi nyiee "

Hiii!!!! Kwanza nikagunaa afu huyu ananichukuliaje mimii halafu nikacheka nikamtazamaa nilitaka nimjibu jibu moja walai angelia ila nikajizuia moyoni nikasema kumbe ukiacha Ukibuli na akili vizuri hana huyu kaka maskini ....

Kwahiyo ana hisi mimi nachati na bwana angu auu?? Mjinga kweli huyu kaka


Nilimtazama kwa kumuonea huruma nikamuelekeza nyumbani akanipeleka mpaka nje ya nyumba ...


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote