Hamima ni muajiriwa wa kampuni moja Kama secretary. Ni binti anafanya kazi zake kwa kujituma Sana Ila alikuwa na tatizo moja alitokea kuvutiwa Sana na boss wake (Nurdin). Nurdin alikuwa Ni kijana mtanashati Sana lakini hakupenda kujihusisha na maswala ya mapenzi. Siku moja kulikuwa na sherehe ya kiofisi hamima alikunywa pombe na ulevi ulipomzidia alienda kusimama mbele ya watu wote na kusema hisia zake juu ya Nurdin , kile kitendo Ni Kama kilimuudhi Nurdin akaondoka kwa hasira. kesho yake hamima alivyoambiwa kile alichokifanya Jana usiku alipata mshituko na wasiwasi alihofia kupoteza kazi yake na kila mtu alijua hamima Hana kazi maana boss alikuwa hapendi ujinga.
Hamima alifika kazini akiwa na barua ya kuacha kazi lakini Nurdin anaichana Ile barua na kumwambia aendelee na kazi. Siku moja Nurdin alitoka lunch na Hamima alafu akaniomba waigize kuwa wapenzi maana wazazi wake wanakuja kwaajili ya kumuona mchumba wake. Hamima alishituka lakini alikubali ombi la boss wake, hamima anahamia nyumbani kwa nurdin wazazi wa Nurdin wanatokea kuvutiwa Sana na Hamima na kuona anasifa zote za kuwa mkwe wao wanamsisitiza mtoto wao afunge ndoa mapema, Lakini baada ya muda wanagundua kuwa hamima na Nurdin hawana uhusiano Bali wanaigiza, mama Nurdin anafanya Jambo ili hamima na Nurdin waweze kutengeneza upendo wa kweli.
Mana Nurdin atatumia njia gani kuwaunganisha na je Nurdin atakubali kuanzisha mahusiano na Hamima ambae ni secretary wake?
CEO'S SECRETARY..🌹. 1
MTUNZI SMILE SHINE
Hamima ni binti wa miaka 25, anafanya kazi katika kampuni ya MC COMPANY. Ni assistant secretary wa CEO,yaani ni msaidizi wa boss ambae yeye ni mwanaume anaejulikana kwa jina la Nurdni. Nurdn ni kijana kijana wa miaka 30 mtanashati na mwenye kuvutia hakuna mwanamke anaemuona asivutiwe nae. Lakini alikuwa ni mkali sana wafanyakazi wengi wanamuogopa hasa wa kike sababu hapendi mazoea kabisa na wanawake. Alikuwa hataki mazoea kwa sababu wasichana wengi walikuwa wakinipitisha na kujipendekeza Ila aliishia kuwaangalia Kama nyanya mbovu au kuwaambia kuwa havutiwi na kile wanachokifanya hivyo ikaonekana anaringa .
Kila inapofika mwisho wa mwaka kampuni ya MC huwa unafanya sherehe za kujipongeza kwa mafanikio ya mwaka mzima. Siku ya sherehe ilifika na sherehe ilikuwa kwenye hotel moja ya kifahari Watu walikunywa na kusaza.
Kwa upande wa Hamima ilikuwa Ni Mara yake ya kwanza kuhudhulia hiyo sherehe maana alikuwa na miezi minne tangu apate ajirakwenye hiyo kampuni.
Hamima alikuwa anashangaa shangaa mazingira ya pale hotelini huku akisifia uzuri wa sherehe. Mara alikuja kushikwa mkono na mfanyakazi mwenzie.
" Hamima unaitwa na boss.
Waliongozana mpaka kwenye meza aliyokuwa kakaa Nurdin, Hamima akasimama pembeni.
" Nimefika boss.
" Vita kiti ukae.
Hamima alifanya Kama alivyoambiwa alivuta kiti akakaa.
" Unataka nikiwa na shida nianze kukutafuta? Unatakiwa kukaa hapa .
" Sawa . Alijibu hamima lakini moyoni alikuwa anasononeka
" Yani huyu sijui yupoje Hadi kwenye sherehe anataka kuleta uboss.
Hamima alitulia huku akiwa anaangalia wenzake wanavyojiachia kwa kusheherekea.
" Mmmh hivi zile file ulinipelekea ofisini kwangu?
" Ndio
" Muhasibu alisaini zile karatasi?
" Ndio alisaini na nimezirudisha ofisini kwako. Mazungumzo ya Nurdin yalikuwa yanamkera Hamima Ila hakuwa na uwezo wa kumwambia bado alikuwa anahitaji kibarua chake.
Wakati wanaendelea na maongezi ya kazi alikuja Mzee mmoja akakaa kwenye meza yao na kusalimiana na Nurdin, walipomaliza kusalimiana hamima alimsalimia yule mzee.
" Nurdin mbona p
Meza yenu imepoa hivi sioni Yale mambo yetu?
" Aaaah si unajua Mimi situmii kilevi.
Baada ya kujibiwa hivyo Yule mzee alimuangalia Hamima usoni, Hamima akasema .
"Vipi binti na wewe Ni Kama boss wako?
" Hapana Mimi natumia
"Hahahaha Safi Sana afadhali nimepata kampani. Nurdni una secretary mrembo sana na anaijua kazi yake naona hata kwenye sherehe hachezi mbali na boss wake.
Alipita muhudumu wakaagizia mvinyo, baada ya dakika chache waliletewa
Yule mzee alipokea akamimina kwenye Alimpa glass na kumpatia grass moja hamima.
Hamima alipokea na kunywa yote kwa mkupuo...
"Wow sio urembo tu pia ni mywaji mzuri sogeza glass nikuongezee.. Hamima alitaka kujibu lakini akaogopa boss atakasirika taratibu alisogeza glass na kuwekewa Tena. Alikunywa mvinyo Kama anakunywa maji akalewa kabisa na kuhisi katosheka lakni yule baba alitaka waendekee kunywa.
" Unaniangusha mrembo acha nikuongezee kidogo. Yule mzee alimimina Tena kwenye grass Hamima alichukua alipotaka kupeleka grass mdomoni
Nurdni alipokonya glass na kuiweka mezani.
"Mh boss wewe ni bonge la gentleman lakini upunguze kuwa serious bwana unajua unatutisha wenzio mpaka tunakosa ujasiri wa kuongea na wewe ... Hamima niliongea kwa sauti ya kilevi huku akinyanyuka
" Unaenda wapi huwezi hata kutembea?
" Nurdin aliuliza
" Naenda chooni
" Kwa Hali hiyo utafika kweli?
" Muache atafika bado Yuko imara. Alisema Yule mzee.
Hamima aliondoka huku akiyumbayumba alipofika chooni alimaliza haja zake Kisha alirudi huku akiyumba yumba akapitiliza moja kwa moja mpaka wa dj alafu akamwambia
" Zima mziki alafu nipeni mic Kuna Jambo langu nataka kuliweka wazi siku ya leo.
" Hamima umelewa nenda kakae kwanza.
" Jamani nope nafasi kidogo. Dj alimuita mshereshaji wa sherehe akamwambia kuhusu ombi la Hamima.
" Anataka kuongea Nini?
" Sijui labda ungemuuliza.
" Hamima unataka kuongea Nini? Hamima hakujibu alikwapua mic kutoka na kuanza kuongea.
" Jamani watu wote naomba mnisikilize Leo Nina Jambo langu muhimu nataka kuwaeleza wote mjue. Kila mtu alitulia na kumgeukia Hamima.
" Leo nataka niseme kile kilichopp moyoni mwangu maana nimeshindwa kuvumilia, mwenzenu Leo nataka kuwaambia kuwa nimependa Kuna mtu nampenda Sana ,kila ninapokuwa karibu nae huwa moyo wangu unakuwa na amani nafarijika na kusahau machungu yote niliyopitia. Ila ndio Sina ujasili wa kumueleza Ila leo nasema liwalo na liwe, Nurdin boss wangu nakupenda sanaaa.
Kila mtu alibaki kusema aaaaaaaaa. Nurdin alimuangalia kwa hasira huku akiwa kakunja uso wake aliona Kama kadhalilishwa lakini yule mzee aliachia tabasamu usoni kwake na kusema "huyu binti Ni jasiri Sana hakuwa tayari kuumizwa na hisia kaamua kutua mzigo kazi kwako Nurdin.
Nurdin aliona maneno ya yule mzee hayana maana zaidi ya kumzidishia hasira.
Hamima aliendelea kuongea
"Uwapo na Mimi pembeni yangu au mbele yangu huwa najiona Nina kila kitu na kusahau kuwa Sina ndugu wa kunishika mkono , nasahau machungu ya kuwapoteza wazazi wangu wawili. Najua Sina hadhi Wala haiwezekani kuwa na wewe Ila angalau nimesema yaliyo moyoni mwangu, nimetua mzigo nilioubeba kwa muda mrefu.
CEO'S SECRETARY🌹2
MTUNZI SMILE SHINE
Kila mtu alibaki mdomo wazi waligeuka kumuangalia boss wao Nurdin, wakati huo Nurdin alikuwa akiangalia moja kwa moja Kule alikosimama Hamima. Alimuangalia kwa muda Kisha akageuka macho kuwaangalia watu waliokuwepo pale alipoona kila mtu anamuangalia aliamua kunyanyuka kimnya kimnya na kutoka nje ya ukumbi. Alivyotoka minongono ikaanza pale ndani kila mtu alitoa maoni yake juu ya kile kilichotokea .
" Hamima kalikoroga , hivi kawaza Nini mpaka kaamua kufanya vile?
" Ameamua kutua mzigo alioubeba kwa muda mrefu lakini itamgharimu. Watu wakiongea mengi Sana mpaka
Katrina rafiki wa Hamima akaamya kwenda kumchukua watoke nje.
" Mbona unanivuta? Hamima aliuliza kwa sauti ya kilevi
" Hebu twende nje.
" Niache bwana. Katrina hakumsikiliza aliendelea kumvuta .
" Hamima naomba usijisumbue nitakupigia mingumi utapike hiyo mipombe yako uliyokunywa. Katrina aliongea kwa hasira maana aliona Kama anazidi kujidhalilisha na kila mtu alikuwa anawaangalia
Hamima alikuwa mbishi kutoka lakini Katrina alimvuta kwa nguvu mpaka nje, walipofika nje walichukua tax na kwenda nyumbani kwake.
" Hivi umeanza lini kunywa pombe kiasi hiki?
" Mmmmm
" Usijifanye kuitika itika hujui umeshajiharibia sijui Kama una kazi. Katrina aliongea na Hamima alikuwa kapitiwa na usingizi .
" Ona Mimi naongea yeye kalala. Alisema Katrina Kisha akaenda kuchukua shuka akamfunika. Nae akapanda kitandani akalala.
Kulipokucha asubuhi hamima aliamka na kuanza kupapasa pembeni ya kitanda alishituka baada ya kushika mtu pembeni yake, alinyanyuka haraka haraka alipomuona Katrina kalala alianza kuangalia mazingira ya chumba.
" Imekuwaje mpaka nimekuja kulala nyumbani kwa Katrina? Alijiuliza maana kwa akili yake alijua yupo nyumbani kwake.
Hakutaka kumuamsha mwenzie alinyanyuka pale kitandani na kwenda jikoni kuangalia kiti chochote kwaajili ya kula maana njaa ilikuwa inamuuma Sana . Alifunua masifuria hakukuta kitu, alifungua friji alikuta vinywaji tu.
" Khaaaa sasa huyu mtu anaishije ikiwa ndani Hamna kiti chochote Cha kula?
Katrina aliamka na kumkuta kasimama jikoni analalamika.
" Sasa Ni njaa inakusumbua baada ya kufakamia mipombe ya bure.
" Katrina siwezi kuongea kwasababu Sina nguvu hivyo naomba tufanye utaratibu wa chakula kwanza alafu ndio uendelee kunipa huo mzigo wa lawama.
" Ila wewe sijui hata nikufanyaje.
Katrina alichukua simu na kupiga sehemu akaagizia supu na chapati.
" Duuu umefanya Jambo la maana Sana.
Katrina alimuangalia hamima huku akiwa kakunja sura.
" Mbona unaniangalia hivyo?
" Ukiona hivyo ujue Nina mengi moyoni mwangu Ila kabla sijayatoa nenda kwanza kaoge na usafishe hicho kinywa chako maana unanuka pombe.
Hamima alijinusa ilikuwa kweli hivyo hakuwa na lakusema alienda bafuni kujifanyia usafi mwili wake.
Alipomaliza alitoka akiwa kavalia gauni ya katrina.
Katrina nae aliingia bafuni akaoga alipomaliza alikuta supu na chapati zimeshaletwa na Hamima alishaanza kula nae akaungana nae wakala walipomaliza ndipo Katrina akaanza kumsimulia kile alichokifanya usiku kwenye sherehe. Hamima aliona ajabu akahisi Katrina anansingizia.
" Hapana Katrina Mimi siwezi kufanya hivyo mbele za watu..
" Lakini kwanini ulikunywa pombe ?" sijui ilikuwaje jamani nijikukuta nakumywa tu.
" Sasa ndio zimekufanya umefanya madudu
"Mungu wangu Sasa itakuwaje? Na kula mtu anajua kilichotokea? Boss pia alisikia na akasemaje? Hamima aliuliza maswali mfurulizo.
" Hayo maswali yako yote jibu lake ni "NDIO" Tena kwa msisitizo na Kama kuandika ningeandika kwa herufi kubwa.
Hamima alihisi kuchanganyikiwa alisimama na kuanza kutembea hovyo Kama mtu anaetafuta kitu.
" Katrina nitafanya Nini mwenzio na sura yangu nitakuweka wapi Mimi?
" Sio kuweka wapi sura yako jiulize je kibarua chako kipo salama?
Hilo swali alilouliza Katrina lilimfanya hamima achanganyikiwe zaidi ukizingatia maisha yake yote anaendesha kwa kutegemea kazi na akifukuzwa itakuwa ngumu kidogo kupata kazi nyingine.
" Sasa nitafanyaje rafiki yangu? Aliuliza hamima kwa upole.
" Sijui tunafanyaje Ila tusubiri litakalotokea siku ya jumatatu.
Kwa upande wa Nurdin alikuwa kasimama juu ya ghorofa akiangalia madhari ya nje huku akinya kinywaji kilichokuwa kwenye grass . Mara alikumbuka tukio lililotokea usiku Kisha akaguna .
" Mmmmh inamaana Ni pombe ndio zimemfanya aongee ujinga ule mbele ya hadhara au alikuwa anamaanisha? Sikuwa najua Kama yule msichana Ni kichaa namna Ile , nitashurikia hili itakapofika jumatatu maana itakuwa gumzo kila mfanyakazi atalizungumzia anavyojua yeye na kila mmoja atakuwa kalichukulia kivyake. Ila sikutegemea Kama hamima angekuwa mpuuzi kiasi kile. Nurdin aliongea vile kana kwamba kachukizwa lakini usoni kwake alionyesha akitoa tabasamu kwa mbali.
Je tabasamu la Nurdin Lina maanisha kuvutiwa na kitendo Cha Hamima au lile tabasamu lina maana nyingine?
CEO'S SECRETARY 🌹 3
MTUNZI SMILE SHINE
Weekend yote ilikuwa chungu kwa Hamima kwani hakutamani Kurudi kwake alibaki kwa Katrina na alikuwa Hana raha ikabidi Katrina apate kibarua Cha kuanza kumbembeleza na kuniliwaza .
" Katrina nimelikoroga kila ninapowaza jinsi la kujitetea nakosa majibu. Unafikiri nikifukuzwa kazi nitaishi vipi hapa mjini mwana yatima Mimi?
" Hutakiwi kuwaza Sana tusubiri neno kutoka kwa boss na Kama ikitokea ukafukuzwa kazi nitakusaidia kutafuta kazi sehemu nyingine.
" Unavyonipa moyo Basi.
" Lazima nikupe moyo Mimi na wewe tumetoka mbali Sana, kumbuka Sina ndugu, ndugu yangu Ni wewe hata Kama nikifa Sasa hivi wewe ndio utakuwa mrithi wangu.
Hamima na Katrina waliangaliana huku machozi yakitaka kuwatoka maana wote walikuwa yatima walikutana wakiwa wadogo na kulelewa pamoja kituo Cha watoto yatima, walikuwa pamoja na kupendana Sana, waliishi kituoni mpaka walipopata mdhamini waliondoka kituoni na kwenda kusoma kwenye mashule ya bweni hatimae walimaliza shule wakaenda chuo na kanza kujitegemea.
Usiku wa siku ya jumapili hamima alikosa usingizi , alisongwa na mawazo alikata tamaa ya Kurudi kazini maana hakuna aliewahi kufanya ujinga akaachwa salama zaidi alifukuzwa kazi. Alichofanya alichukua karatasi na kuandika barua ya kuacha kazi Kisha akaikunja vizuri na kuiweka ndani ya pochi yake hakutaka Katrina ajue kuhusu swala la kuacha kazi maana alijua atampa moyo wakati anajua kitakachoenda kutokea.
Kulipokucha asubuhi waliamka pamoja wakajiandaa wakati wa kuondoka Hamima alikaa kitandani.
" Khaaa Sasa mbona unakaa?
" Katrina nisije nikakuchelewesha tangulia....
" Acha ujinga natanguliaje kwa mfano, kwani unataka kufanya Nini?
" Hakina kitu kibaya ninachotaka kufanya sitaki kiwahi kazini nitakuja kwa kuchelewa.
" Wewe unataka kufanya kosa juu ya kosa?
" Acha iwe hivyo .
" Jamani Hamima mbona tulishaongea hili na tukakubaliana kuwa tusikilize kauli ya mwisho ya boss au unaogopa macho na midomo ya watu?
" Inawezekana ikawa hivyo lakini sijali Sana kuhusu watu watasema Nini ninachoogopa Ni kukutana na Nurdin na ukumbuke Mimi Ni secretary wake nikifika ni lazima nikutane nae.
" Kwahiyo ukichelewa hutakutana nae?
" Katrina utachelewa wewe nenda Mimi nitakuja. Katrina aliamua kuondoka akamuacha akiwa anatafakari jinsi ya kufika kazini na kukabiliana na macho ya watu pamoja na boss.
Ilipofika majira ya saa mbili Hamima aliamua kutoka na kuelekea kazini , alichukua usafiri lakini alishuka mbali kidogo na ofisi zao zilipo akaanza kutembea kwa miguu Tena kwa mwendo mdogo mdogo.
Akiwa barabarani anatembea Mara gari ya boss wake ilimpita , alimuona Nurdin akiwa kamkazia macho. Hii ilimpa hofu zaidi akajikuta anasimama na Nurdin hakusimamisha gari aliendelea na safari yake.
" Mmmh hapa hakuna wema hata kidogo , lakini hakuna namna zaidi ya kupeleka hii barua ya kuacha kazi.
Hamima alilipitisha Hilo kichwani kwake akatembea haraka haraka kuwahi . Alipofika kila mtu alimuangalia na wengine walimcheka. Alijisikia vibaya lakini alijilaza aliwapita na kwenda moja kwa moja ofisini kwake . Muda huo huo alifika prim.
" Habari za asubuhi Hamima!
" Salama.
" Boss anakuita ofisini kwake.
Hamima alishituka .
" Kwani anajua Kama nimefika?
" Ndio alikuwa kasimama kwenye dirisha la ofisi yake akakuona ulivyokuwa unaingia. Katrina aliingia akawakuta wanaongea
" Vipi upo sawa?
" Nipo sawa , naenda kuonana na boss. Wote wawili waliangaliana usoni , Katrina alimshika begani kumtia moyo.
" Usijal kila kitu kitaenda sawa. Hamima hakumjibu alifungua pochi yake akatoa Ile barua aliyoandika na kwenda nayo ofisini kwa Nurdin.
Alibisha hodi akakaribishwa, alifungua mlango akaingia ,wakati huo kijasho chembamba kilimtoka mpaka kwenye viganja vya mikono.
Nurdin alimpokea kwa macho alimuangalia kwa kila hatua aliyopiga mpaka alipofika mbele ya meza yake.
Hamima alikosa hata ujasiri wa kusalimia alijiinamia na Nurdin aliendelea kumuangalia Kama mtu ambae alikuwa anatafakari Jambo la kuongea. Hamima alipoona kimnya ilimbidi aongee
" Samahani kwa kile kilichotokea , Naacha kazi.
Nurdin alizidi kumkazia macho hakutegemea kama Hamima angeweza kujihukumu mwenyewe alichofikiria ni kuwa angeomba msamaha Kama wanachofanya wengine.
" Unajua madhara ya kuacha kazi ?
" Najua Kuna haki zangu nitapoteza. Alijibu Hamima huku akiikabidhi barua kwa Nurdin. Nurdin aliipokea akaifungia na kusoma kilichoandikwa alipomaliza aliichana Ile barua vipande vidogo vidogo na kuweka juu ya meza yake.
Hamima alishangaa na kujiuliza
"kwanini kachana, inamaana hataki niache kazi , Sasa anataka kufanya Nini?
" Safisha ofisi alafu uende ukaendelee na kazi. Alisema Nurdin huku akinyanyuka kwenye kiti chake na kutoka ofisini . Hamima hakuamini alichokisikia kutoka kwa Nurdin ilikuwa Kama ndoto kwake.
" Jamani. Mbona sielewi, eti kasema safisha ofisi yangu alafu nenda kaendelee na kazi hivi Ni kweli au naota? Hamima alisogea mpaka kwenye zile karatasi zilizochanwa na kuzishika.
" Hivi Ni kweli kachana inamaanisha kwamba Mimi bado Ni mfanyakazi wa hapa.
Hamima aliongea huku akiwa na furaha . Alianza kufanya usafi haraka haraka huku aliomba kwa furaha.
CEO'S SECRETARY 🌹 4
MTUNZI SMILE SHINE
Nurdin alitoka na Nurdin wakaenda kupata kifungua kinywa kwenye mgahawa uliokuwa karibu na ofisi zao.
" Nini kinaendelea hapo kazini? Nurdin aliuliza
" Mambo yako sawa.
" Nataka kujua watu wanalichukuliaje swala la juzi?
" Kuhusu yake aliyoongea Hamima kwenye sherehe?
" Ndio.
" Kuna minongono ya chini chini.
" Tulitoka hapa kawatangazie wafanyakazi wote kuwa ilifika Sasa nane nitakuwa na kikao nao.
" Sawa.
Waliendekea kupata kifungua kinywa walipomaliza walirudi kazini na Hamima alikuwa kamaliza kusafisha ofisi ya boss na kupanga vizuri akawa yupo ofisini kwake anaendelea na kazi zake. Nurdin alimpita akaingia ofisini kwake.
Ilipofika muda wa lunch Katrina alimfuata hamima ili kujua kinachoendelea.
" Vipi boss kakwbia Nini?
" Niajabu amechana barua yangu ya kuacha kazi....
" Nini? Inamaana ukiandika barua ya kutaka kuacha kazi?
" Ndio maana nilijua kivyovyote lazima ningefukuzwa.
" Ehee mikawaje Sasa, Yani kakwambiaje kuhusu kilichotokea?
" Hajaongea kitu zaidi ya kuniambia niendelee na kazi.
Wakiwa katikati ya maongezi prim aliingia
" Samahani kwa kuwaingilia .
" Bila samahani.
" Jamani jiandaeni. Baada ya lunch kutakuwa na kikao na boss hivyo wote tukutane chumba Cha mkutano.
" Sawa. Aliitikia Katrina huku akimuangalia Hamima usoni.
" Prim samahani , kwani mkutano inahusu Nini?
" Sijui nimepewa agizo na boss niwatangazie wafanyakazi wote.
Prim aliwaacha wajabaki wanaangaliana
" Bila Shaka utakuwa kuhusu swala la juzi. Hamima aliongea kinyonge.
" Aaaa usijal bwana twende tukale.
" Sijisikii kula unaweza kwenda.
" Hamima acha kujipa presha hakuna baya litakalotokea .
" Hapa nilipo Sina amani ungeniacha kwanza.
Ilifika muda wa kikao watu wote waliwasili kwenye chumba Cha mkutano walikaa na kumsubiri boss Nurdin afike.
Baada ya muda kidogo Nurdin alifika na kwenda kukaa kwenye kiti chake.
Huku akiwa kaegemea na kumuangalia kila mtu, watu wote walikaa kimnya kumsikiliza , hamima alikuwa kajiinamia kwa aibu.
" Jamani nimewaita hapa ili tuwekane sawa kwabkile kilichotokea ule usiku wa sherehe. Alisema Nurdin na kufanya Hamima azidi kuwa na hofu huku mapigo yake ya moyo yakienda mbio.
" Mungu wangu naomba unisaidie nilijua hili swala limeisha kumbe nilikuwa najidanganya.
Nurdin aliendelea kuongea
" Najua minongono bado inaendelea hapa kazini , Sasa nasema hivi hapa kazini nimeajiri watu wenye akili timamu na wanaojitambua hivyo nataka watu wafanye kile kilichowaleta na kuachana na upumbavu mwingine . Siku Ile akili ya hamima haikuwa sawa ilikuwa akili ya pombe. Hakuna ukweli wowote juu ya kile alicho kiongea. Kwa leo yangu yalikuwa Ni hayo tu nadhani tumeelewana.
" Ndio . Walijibu wafanyakazi wote.
" Nawatakia kazi njema . Nurdin Alimalizia kusemakusha akanyanyuka na kuondoka ,alipofika sehemu aliyokaa Hamima alisimama na kusema .
" Hamima namuhitaji ofisini kwangu.
" Sawa. Alijibu hamima huku akinyanyuka haraka kumfuata. Waliongozana mpaka ofisini kwake Nurdin akakaa kwenye kiti na Hamima akasimama mbele ya meza yake.
" Hamima natumai hautafanya ujinga mwingine Tena ndio maana nimeamua kukupa nafasi nyingine .
" Ndio boss siwezi kurudia sitakunywa Tena pombe.
" Itakuwa vizuri maana hautakunywa maana itaishia kudhalilika tu.
Hamima aliangalia chini kwa aibu kwa ni kweli alidhalilika.
" Sitarudia Tena boss.
" Nenda kaendelee na kazi zako.
" Asante boss. Alisema hamima Kisha akatoka ofisini kwa Nurdin akiwa haamini Kama hili Jambo limeisha kirahisi hivyo , haikuwa kwa Hamima tu wafanyakazi wote walishangaa.
" Hamima ana Mungu jamani hakuba alietegemea Kama boss angeweza kulipotezea kirahisi hivyo.
" Kweli nimeamini kila mti na bahati yake.
" Endeleeni kuongea mkisikiwa mtafukuzwa nyie .
" Na kweli tumeshapewa onyo .
Muda wa kutoka kazini ilifika hamima alimfuata Katrina ofisini kwake.
" Bado haujamalizia kazi?
" Nimeshanaliza naweka vitu vyangu vizuri.
" Basi twende zetu. Katrina alibeba pochi yake wakaondoka.
" Katrina nataka kwenda super market kwenda kununua vitu .
" Kwani Leo unarudi nyumbani kwako?
" Hapana nitakuwa kwako nataka tusheherekee kwa hili unajua siamini Kama Boss kakusamehe kirahisi hivi.
" Hata Mimi siamini Ila unatakiwa kuwa makini zaidi Jaribu kuficha hisia zako.
" Mmmh Sina hisia zozote kwake.
" Hilo Ni jibu la akili zako tumamu ni wazi unajitetea Ila kwa utafiti inasemekana mlevi huwa anaongea ukweli mtupu. Hapo hamima hakuwa na lakupinga aliishia kuguna tu.
Walifika supermarket wakanunua vitu walivyohitaji alafu wakarudi nyumbani kwa Katrina.
Siku hiyo walifurahi kwa kunywa na kula huku wakiwa wanasikiloza na kucheza muziki kwa madai wanasheherekea.
" Hamima hebu kuwa mkweli hivi unampenda Boss? Katrina aliuliza
" Katrina hakuna mwanamke ambae hajawahi kuvutiwa na yule Kaka ndio maana wanawake wengi wanajigonga kwake na kuishika kupewa into Kali na wale walioshindwa kumdhibiti hisia zaowameishia kufukuzwa kazi.
" Sasa shoga yangu wewe utaweza kujizuia maana kila sehemu upo nae? Hamima alishusha pumzi alafu akasema .
" Ni kweli Kuna wakati ninapokuwa karibu nae huwa napata shida Sana Kuna Hali flani huwa najisikia Ila kwa Sasa acha niseme na moyo wangu kwakuwa bado Nina hitaji.
" Kwahiyo Kama ingekuwa huna uhitaji ungefanya Nini?
" Ningefanya juu chini ili nijue kwanini boss hataki kuwa na mpenzi na Kama anashida pia ningependa kujua maana haiwezekani mkaka mzuri Kama yule akose mwanamke alafu wadada wazuri wazuri wanamtaka yeye analeta maringo.
" Huenda ana matatizo .
" Itakuwa ha....
Kabla hamima haujamalizia kuongea kuongea simu yake iliita na aliyekuwa anapiga alikuwa Ni boss Nurdin.
CEO'S SECRETARY 🌹 5
Kabla ya kupokea hamima alimuangalia Katrina
" Boss anapiga.
" Sasa si upokee.
" Haujawahi kutokea kunipigua simu muda bao sio wa kazi alafu unajua tangia limetokea hili nashituka hata niliona simu yangu naogopa hata kuonana nae.
" Acha ujinga hayo yameshapita angalia yajayo pokea simu haraka.
Hamima alishusha pumzi Kisha akapokea
" Habari boss.
" Salama
" Nataka kukuuliza swali.
" Uliza tu boss.
" Hivi kesho Nina ratiba gani?
" Mmmmh nadhani mida ya saa mbili asubuhi una ratiba ya kukutana na mkurugenzi wa Femi Transportation na..... Kabla hajamaliza kueleza Nurdin alimkatisha
" Naomba uhairishe kila ratiba yangu ya kesho .
" Sawa boss nitawapigia watu wote uliokuwa una ahadi nao.
" itakuwa vizuri Kama utafanya hivyo mapema.
" Sawa boss.
Siku zilienda waliendelea kufanya kazi Ila hamima bado alikuwa muoga kwa boss wake maana Kuna wakati Nurdin alikuwa anamuangalia Sana Kama vile anamtafakari. Na kweli Nurdin alikuwa ana Jambo lake kichwani kwake kwa kiasi fulani alivutiwa Sana na ujasiri wake .
" Bila Shaka huyu anaweza kufaa kwenye kazi yangu maana anajiamini Sana Ila nitaanzia wapi kuongea nae? Mmmh lakijinga bado siku zipo. Nitaongea nae tu.
Siku moja hamima akiwa ofisini kwake. Prim alimfuata na kukaa pembeni ya meza yake
" Miss Hamima !
" Niambie prim
" Umependeza.
" Kupendeza kawaida yangu.
" Na nikweli.
" Vipi leo tunaweza kwenda lunch pamoja?
" Sawa lakini unajua Mimi huwa naenda kwa mama ntilie huko kwenye vyakula vyenu vya Bei Wala siwezi.
" Sasa upo na Mimi unawasiwasi gani mrembo.
" Mmmh nyie mna maana Basi naweza nikaenda kumbe unajambo lako tusipoelewa na unaniacha Mimi kuisha masifuria siwezi.
" Hahaha Hamima unavituko wewe, huwa unanikosha tu ucheshi wako.
" Prim tupo kazini hebu nenda sitaki majanga na Boss.
" Poa Basi ukifika huo muda tutaonana .
" Usijali.
Mara Nurdin aliingia ofisini kwa Hamima akamwambia
" Hamima muda wa lunch Kuna sehemu nataka twende.
" Sawa boss. Alijibu Hamima huku akimuangalia prim usoni.
" Prim umeona na muhasibu na kuweka Mambo sawa?
" Tumeshamaliza kila kitu.
" Sawa hebu njoo ofisini kwangu. Nurdin na prim waliongozana wakaenda ofisini kwa kwake.
" Haya Sasa sijui prim habari yake imeishia hapo boss kamzidi kete.
Ilipofika majira ya saasaba kasoro Nurdin alimwambia hamima waondoke.
Hamima alichukua pochi yake na kutoka nje haraka akijua wanatoka na boss wake wanaenda kwenye Mambo ya kazi Kama siku zote lakini siku hiyo ilikuwa tofauti Walienda kwenye hotel moja nzuri,. Hamima alikuwa anashangaa tu maana hakuwahi kuingia kwenye hotel kubwa Kama Ile zaidi ya kuona kwenye TV, majarida au kupita tu kwa mbali.
Walienda kukaa sehemu muhudumu alifika kwaajili ya kuwahuumia aliwapstia menu kila mmoja alichagua chakula anachohitaji pamoja na vinywaji.
" Boss kwani leo kuna watu unakutana nao? Hamima aliuliza kwa sauti ya chini na Nurdin aliachia tabasamu kwa mbali Kisha akanyanyua grass ya kinywaji chake akanywa kidogo.
" Unaishi kwa kukariri?
" Hapana nilitaka kujua maana hii haikuwa kwenye ratiba .
" Siku moja moja sio mbaya Boss na secretary wake tukatoka Kama hivi kwaajili ya kufurahi.
Hamima alishangaa maana haujawahi kutokea siku hiyo ndio mara ya kwanza.
" Hivi kesho ratiba yako unasemaje? Nurdin alimuuliza hamima
" Ratiba yangu au yako? Hamima aliuliza kana kwamba hakuelewa swali.
" Ratiba yako wewe.
" Baada ya kutoka kazini Sina ratiba yoyote.
" Hiyo ya kazini niachie Mimi nilihitaji kujua baada ya kazi.
" Nitakuwa free.
" Ahaaa wazazi wangu wanakuja siku mbili zijazo ,wanakuja kunitembelea.
" Waooo hongera Sana. Mlio na wazazi mna Raha Sana huwa natamani wazazi wangu wangekuwepo huenda na Mimi ningedeka.
" Hivi Ni kweli huna wazazi?
" Ndio walifariki kwa kupigwa na radio na kuniacha nikiwa mdogo Sana.
" Ooooh pole Sana.
" Nimeshapoa Ni mipango ya Mungu.
" Kwahiyo baba na mama walifariki siku moja?
" Ndio niliwapoteza siku moja walikufa mbele yangu na Mimi nikalewa kituo Cha kulelekea watoto yatima huko nikapata ndugu na rafiki ambae nipo nae kwenye shida na Raha Katrina.
" Kumbe Katrina nae Ni yatima?
" Ndio.
" Daaah poleni Sana. Nurdin alisikitishwa Sana na hizo taarifa.
" Tumeshapoa, tumezoea .
" Kesho utanisindikiza kuwapokea wazazi wangu?
" Bila Shaka nitakwenda.
" Nitafurahi. Unajua Mimi Ni mtoto pekee kwa wazazi wangu.
" Ndio maana unadeka.
" Wananidekeza kila siku wananichukulia Kama mtoto Hilo swala sikupendi.
Pia ujio wao wanataka kuja kumuona mchumba wangu. Nurdin alivyosema hivyo hamima alikuwa makini kusikiliza.
" Kwahiyo tutaenda kuwapokea na mchumba wako?
" Hapana.
" Ooh atakuwa nyumbani anawaangalia wakwe zake.
" Hapana. Nilikuwa nahitaji mtu wa kuigiza Kama mpenzi wangu mpaka pale wazazi wangu watakapo ondoka.
" Kwahiyo unataka niongee na msichana gani boss?
" Hapana sitaki uongee na mtu yoyote ningependa uwe wewe Hamima maana nahisi unaweza wewe Ni jasiri hautaniangusha.
Hamima alishangaa hakujua amjibu vipi.
" Nilijua utashituka utajaposikia hili lakini una haki ya ya kukubali au kukataa.
Je hamima atakubali ombi la boss wake?
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote