BOSI WANGU (Mpenzi Wangu wa Siri)

book cover og

Utangulizi

Ni story inayomuhusu bint Samara, ambae alikutana na kaka mtandaoni anaitwa salmin, wakaanza kupendana bila KUONANA, kila Samara akitaka picha salmin anasema watakuja KUONANA..

Samara anakuja kupata kazi kwenye kampuni ambayo anafanya kazi salmin ila vyeti vyake alikuwa anatumia jina la nzoya badala ya Tamara, na salmin anatumia murtadhwa ambalo n jina lake la tatu badala ya salmin, ila salmin alikuwa ni kijana mwenye majivuno sana, so hata Samara wlipoenda kufanya kazi akamtolea maneno ya kashfa sana mpaka Samara akamchukia bila kujua ndio yule mpenzi wake wa mtandaoni, siku zinaenda salmin anakuja kugundua kuwa nzoya ndio Samara wake, ila ubaya ni kwamba Samara alikuwa anamchukia na kila siku alikuwa anamlalamikia kuhusu BOSI wake kumbe BOSI mwenyewe ni YEYE....

BOSS WANGU (MPENZI WANGU WA SIRI) 1

MTUNZI SMILE SHINE

Samara binti wa miaka 23 anatokea katika familia ya kawaida Sana, amehitimu mafunzo ya uhasibu lakini hakubahatika kupata kazi mapema lakini hakupata tamaa aliendelea kutafuta ujuzi mwingine ili kuweza kuendesha maisha yake. Alijifunza maswala ya ubunifu wa mitindo ya nguo alikuwa anapenda Sana hiyo kazi na kumpelekea kujifunza kwa bidii na kuelewa mapema Sana. Mwalimu wake aliempenda Sana hata ilipotokea kapata tenda ya kuandaa nguo alimtafuta Samara amsaidie na kumlipa pesa .
Samara alikuwa bize Sana na kazi zake muda mwingi alikutumia kuchora michoro ya nguo na kumfuatilia wanamitindo pamoja na wabunifu mbalimbali wa nguo.

Siku moja Marafiki zake walimfuata kwenda kumtembelea pamoja na kumualika harusi ya dada yake Cecilia ( cecy)
" Mbona mmenishitukiza sijajiandaa kwa chochote .
" Unataka kujiandaa vipi? Cecy aliuliza
" Kwenye sherehe natakiwa kupendeza pia natakiwa kuwa na zawadi kwaajili ya kuwatunza maharusi hasa Tayana Ni Kama dada yangu.
"Usinilaumu siku zote upo bize ,simu hupokei na ukipokea unakuwa bize mno Mara naandaa nguo .
" Kwahiyo umepata kisingizio?
" Sio kisingizio ndio Hali halisi.
" Basi sawa tatizo lipo kwangu nitafika kwenye harusi ya dada Tayana.
" Safi, Sasa ningependa tuvae share na wewe ndio utaandaa vazi langu na lako bila kumsahau happy.
" Msijali nitafanya hivyo.

Siku ya harusi ilifika watu walisheherekea na ilipofika muda wa kwenda ukumbini watu walijaa wakaendelea kusheherekea. Ulifika muda wa kucheza muziki
Happy na Cecy walinyanyuka na kwenda kucheza na wapenzi wao Samara alikuwa kakaa anawaangalia huku akitabasamu, alitamani nae awe na mwanaume wa kucheza nae sema ndio hivyo hakuwahi kupata mwanaume mwenye mapenzi ya kweli wote waliishia kumuumiza kwahiyo akaamua apumzike kidogo kwenye swala zima la mapenzi.
Akiwa anashangaa shangaa alifika Kaka mmoja na kumsalimia .
"Mambo.
" Safi.
" Samahani tunaweza kwenda kucheza?
" Mmmm hapana.
" Tafadhali naomba hii Ni sherehe ya wapendwa wetu hivyo tunatakiwa kuungana nao kwaajili ya kusheherekea . Samara alikubali akanyanyuka na kwenda kucheza na huyo kijana . Wakiwa wanaendelea kucheza yule kijana alijitambulisha
" Naitwa Derick.
" Samara.
" Nimefurahi kukufahamu mrembo Samara.

Waliendelea kucheza huku Derick akiwa anamuangalia Sana Samara mpaka Samara akawa anaona aibu.
" Samahani tunaweza kuwa Marafiki?
" Urafiki wa aina gani?
" Urafiki wa kujuana kwanza huenda badae Mambo mengine yakajitokeza.
" Mmmm hapana .
" Kwanini unakataa kwani una mpenzi?
" hayo Ni Mambo yangu binafsi siwezi kumueleza kila mtu.
" Hata swala la kuwa na mpenzi ni jambo la kuficha?
" Kaka hapa tupo kwenye sherehe acha tufurahie na tufanye kilichotuleta.

Derick alitulia wakaendelea kucheza lakini bado alikuwa anapanga Cha kuongea ili Samara aweze kumuelewa.
" Samara unajua wewe Ni mrembo Sana naona unafaa kabisa kuwa na Mimi .....
Samara alichukizwa na maneno ya Derick aliacha kucheza akasogea nyuma Kisha akaenda kukaa.
Cecy alimfuata Derick akamuuliza
" Vipi mmekubaliana?
" Bado anaonekana mgumu Sana kuelewa.
" Nilikwambia Ila usikate tamaa ipo siku ataelewa na atakupa nafasi yakiwa nae tumpe muda kwanza.
" Sawa Ila naomba na wewe uongee nae huenda akakuelewa Kama rafiki yake.
" Poa usijali.

Kabla ya sherehe haijaisha Samara aliondoka akarudi nyumbani.
Kesho yake asubuhi akiwa bado hajaamka simu take ilianza kuita , Cecy alikuwa anapiga.
" Vipi Cecy mbona unapiga simu mapema hivi?
" Wewe , saizi mapema? Hebu angalia saa.
Samara aliangalia saa ilikuwa saa nne kasoro ya asubuhi.
" Mungu wangu kumbe nimelala Sana afadhali umeniamsha.
" Samara Kuna Jambo nataka tuongee.
" Ongea tu mpenzi.
" Ni kuhusu Derick.
" Derick yupi? Aliuliza Samara kana vile hamjui .
" Yule handsome uliekuwa unacheza nae Jana usiku.
" Mmmh kafanya Nini?
" Derick ametokea kukupenda anahitaji Sana muanzishe mahusiano na Kama itawezekana mje kuishi pamoja Kama mke na mume.
" Kwasasa bado sijafikiria kuingia kwenye mahusiano Nina Mambo mengi Sana ya kufanya kwa hiki kipindi.
" Samara hivi una matatizo gani ,unaishi hivyo mpaka lini?
" Cecy wewe mwenyewe shahidi unajua nilichopitia kwenye mahusiano sitaki kusikia kitu kuwa na mpenzi.
Cecy alijaribu kuongea nae na kumuelewesha kuwa Derick Ni mwanaume ambae yupo tofauti lakini hakumuelewa ikafikia hatua mpaka ya kumkatia simu. Cecy alijaribu kupiga Mara mbili lakini simu haikupokelewa. Alijaribu kutumia namba nyingine Samara akapokea
"Hivi wewe unakichaa Sasa unenikatia simu kwa Nini?
" Kwasababu nachoshwa na maongezi yako.
" Acha ujinga unatakiwa kuwa ..... Kabla hajamaliza kuongea Samara akakata simu na kuitupoa kitandani.
Zilipita dakika kumi simu ikaita Tena ilikuwa
Namba mpya .
" Hivi Cecy ananitafuta Nini Sasa ngoja nimtolee uvivu. Alipokea simu na kusema.
" Kwani unataka niongee rugha gani ili unielewe, nimesema sitaki kusikia kitu kinachoitwa mapenzi, kwanza siamini mapenzi, mapenzi yameniumiza Sana nimeteseka Sana na kujiona Sina thamani Ila kwa Sasa acha niseme mapenzi kwangu Basi.
" Kumbe tupo wengi tunaopitia changamoto za mapenzi.....


BOSS WANGU ( MPENZI WANGU WA SIRI) 2

MTUNZI SMILE SHINE

Sauti iliyotoka upande wa Pili ilikuwa Ni sauti nzito ya kiume iliyopenya vyema kwenye ngoma za masikio ya Samara. Samara alishituka na kukaa kimnya kwa muda kidogo akasikia hiyo mtu alisema.
"Pole Sana inaonekana moyo wako umevunjika vipande vipande..... Kabla huyo mwanaume hajamaliza kuongea samara alimkatisha kwa kusema
" Kwani wewe Ni Nani?
" Naitwa Salmin.
" Salmin wa wapi, na ulikuwa unashida na Nani?
Upande wa pili kulikuwa kimnya kwa muda na samara alikuwa akisikiliza jibu la swali alilokuwa kauliza.
" Oooh! Simu yangu imeingia kwako kimakosa nahisi nimekosea namba maana mtu niliemkusudia kumpigia sio wewe.
" Sawa uwe na siku njema.
" Hapana usikate simu bado natamani kuongea na wewe.
" Unataka kusema nini? Aliuliza samara kwa ukali maana anajua wanaume walivyo wasumbufu.
" Kwani mimi na wewe tu kufahamiana na kuongea mawili matatu kuna ubaya?
" Nawajua sana wanaume hamnaga uvumilivu, hamuwezi kujizuia tukiendelea kusikilizana hapa unaweza kuanzaambo yako ya ajabu acha nikwambie ukweli ni kwamba mimi huwa sidanganyiki na kama nia yako ya kutaka kuongea na mimi ili unitongize basi umekwama baba.
Maneno ya samara yalimfanya Salmin acheke sana alafu akasema.
" Mimi sio mtu wa aina hiyo Ila ningependa kukushauri kitu kimoja kuwa usiishi kwa kukariri kuwa watu wote wanafanana sio wote wanaakili na mawazo sawa. Alafu hutakiwi kujikatia tamaa kiasi hicho Wewe Ni binti itafikia wakati itakubidi upate mwenza hivyo jaribu kutoa kinyongo jipe muda wa kuangalia Nani utaendana nae na Nani atakufaa kuanzisha nae safari ya mapenzi. Maneno ya salmin yalikuwa machache lakini yalimuingia Samara lakini nae alikuwa na swali la kuniuliza
" Nakumbuka hapo mwanzo ulisema umeumizwa kwenye mapenzi Sasa inakuwaje unanipa ushauri Kama huu ikiwa na wewe Ni muhanga Kama Mimi?
" Ni kweli nimepitia maumivu na kuachana na mahusiano kadhaa lakini Ni kwa muda tu siwezi kusema nitaacha kabisa kupenda, hapo mbele nitahitaji kuwa na mweza wangu lakini nitakuwa makini Sana kuchagua kwasababu nimeshajifunza huko nilikopitia mwanzo. Samara alishusha pumzi na kusema
" Nimekuelewa muhanga mwenzangu pia nashukuru kwa kukosea namba ukanipata Mimi maana nimepata tumaini jipya kabisa ambalo lilikuwa halipo moyoni mwangu na akilini mwangu.
" Nafurahia kusikia hivyo, kamwe usikubali kukatishwa tamaa na usihukumu wengine kwasababu ya makosa ya wengine.
" Nimekuelewa sana . Ok uwe na siku njema.
" Nawe pia mrembo.
Kabla Samara hajakata simu salmin akasema.
" Samahani nilisahau kuuliza jina lako,unaitwa Nani?
" Samara.
" Samara, Nice name.
" Thanks.
" Ulale salama samara.
Alisema Salmin kisha akakata simu.

Baada ya siku tatu kupita salmin alimpigia simu Samara, Samara alikuwa anafanya kazi lakini aliacha Ile kazi na kupokea simu kwani alijikuta anashauku ya kuongea na salmin, labda alikuwa hivyo kutokana na Yale maneno aliyoongea siku Ile ya kwanza.
" Hallow
" Niambie Samara.
" Safi
" Nimekumbuka nikaona sio mbaya nikujulie Hali.
" Haujafanya vibaya pia nashukuru Mimi Ni mzima wa afya tele hofu yangu Ni kwako.
" Pia namshukuru Mungu nipo vizuri.
" Nijambo la kumshukuru Sana.
" Sawa nimejisikia furaha kusikia sauti yako kwa badae tunaweza kuongea ama kuchat?
" Ndio inawezekana.
" Basi nitakutafuta badae uwe na mchana mwema.
" Asante na wewe pia. Samara alikata simu akiwa na tabasamu usoni mwake.

Siku zilizidi kwenda Mara kwa Mara walikuwa wakiwasiliana kwa kupigiana simu au kwa kutumiana message walipiga story nyingi na kuongea mambo mengi , kila muda asubuhi waliamshana kwa msg , mchana waliulizana Kama wamekula usiku ndio kabisa waliongea na simu mpaka masikio yalipata Moto.
kila mmoja alionekana kuvutiwa na ukaribu wao wanajikuta wamezoea hiyo Hali hawakuweza kupitisha hata siku moja bila kuwasiliana.

Siku moja ilikuwa majira ya saa mbili usiku Samara akiwa anachora michoro ya nguo kwenye kitabu chake Mara simu iliita kuangalia ilikuwa namba ya salmin.
" Hallow Mr salmin.
" Hallow Mrs salmin. Samara alivyosikia hivyo alicheka Sana
" Vipi mbona unacheka?
" Acha kunifurahisha bwana hayo Mambo ya kuniita Mrs yameanza lini?
" Si ndio tumeanza Leo au haupendi?
" imekuwa ghafla Sana .
" Pole Ila taratibu utaziwea.
" Sawa niambie.
" Nina Jambo langu hapa
" Jambo gani?
" Unaonaje Kama tukafanya kitu kwaajili ya kumridhisha nafsi zetu.
" Jambo gani?
" Tuanzishe uhusiano wa kuongea kwenye simu Yani namaanisha tuwe wapenzi huenda badae Mambo yakawa mazuri na Jambo letu likakalamilika.
" Ila salmini unamasihara Sana Jambo Kama Hilo litawezekana vipi?
" Litawezekana mumy hebu tufanye kubali kuwa mpenzi wangu.
Samara alikuwa anacheka tu.
" Usicheke unajua Kuna wakati na wish kuwa wewe Ni mpenzi wangu Sasa kwanini tusifanye iwe hivyo?
" Sawa nimekubali.
" Safi Sana mpenzi kuanzia leo nitakuwa nakuita majina Matamu Matamu ya kimahaba na wewe utafanya hivyo si ndio.
" Hahaha sawa nimekubali kuwa Eva wako na wewe Ni Adam wangu. Alisema samara kisha akaendelea kucheka maana walichopanga ilikuwa kama utoto inawezekanaje watu kuitana wapenzi na hawajawahi kujuana wala kuonana.

BOSS WANGU MPENZI WANGU WA SIRI 3
MTUNZI SMILE SHINE

Samara alikubali tu ili kudumisha huo urafiki pia alikuwa anafurahia sana kuongea na Salmin lakini hakuamini kama inawezekana watu wasio fahamiana wanaweza kuwa na uhusiano.

Siku zilizidi kwenda mawasiliano Yao yakadumu pia kila mmoja alijitoa na kuonyesha mapenzi na upendo wa dhati kwa mwenzake , waliambiana kila wanachotaka kufanya, Samara alipoenda kukutana na marafiki zake alimwambia Salmin hata kwa Salmin ilikuwa hivyo hivyo kila mmoja alikuwa anajua ratima ya mwenzake.

Siku moja Samara aliona tangazo la kazi Kuna kampuni moja ya mavazi ilitangaza tangazo la kazi. Samara alipoliona alijaribu kutuma barua ya maombi Kisha akampa taarifa salmin.
" Baby nimetuma maombi ya kazi kwenye kampuni moja hivi sijui kama nitafanikiwa.
" Kwanini ukate tamaa mpenzi , utapata kwa uwezo wa Mungu nitakuombea pia Dua zangu zitakuwa na wewe.
" Asante mpenzi, ndio maana nakupenda huwa upo na Mimi kwa kila Jambo langu na haujawahi kunikatisha tamaa.
" Hata wewe haujawahi kunikatisha tamaa, Nafanya hivyo kwasababu nakupenda Mrs Salmin.
" Asante sana mfalme wangu. Samara alijibu kwa hisia sana yani kuna muda walikuwa wakiongea anakuwa na hisia kama vile wapo pamoja hata kwa upande wa Salmin ilikuwa hivyo na hiyo hali ilizidi kufanya upendo uzidi kati yao lakini hakuna hata mmoja aliyetaka kuona picha ya mwenzie wala kuomba waonane.

Siku moja Samara akiwa amekaa sehemu na Marafiki zake wakiwa wanaongea simu yake iliita nae akapokea .
" Habari
" Salama
" Samahani naongea na miss Zoya Ibrahim.(Zoya ni jina alilotumia shule pia ndio lipo kwenye Cheti chake Cha kuzaliwa , Samara Ni jina analotumua mtaani na ndio jina lililozoeleka Sana.)
" Ndio.
" Ok,unaongea na Clinton muajiri wa kampuni ya Muntazar fashion, ulitumamaombi kwenye kampuni yetu?
" Ndio.
" Sawa umechaguliwa hivyo unatakiwa kufika ofisini kwetu kwaajili ya interview.
" Asante Sana.
"Karibu Sana na uwe na siku njema.
" Asante, nawe pia.

Samara alifurahi Sana akawashirikisha Marafiki zake Cecy na Happy walifu Sana
" Hongera Sana kipenzi.
" Kweli wakati wa Mungu ndio wakati sahihi .
" Lakini bado sijafanya interview.
" Usijal dear Kama mwanzo Ni mzuri Basi hata mwisho utakuwa mzuri.
" Asanteni Sana marafiki kwa kunitia moyo.
Samara hakuona vibaya kumjulisha mpenzi wake wa mtandaoni Mr salmin.
Alipiiga simu na dakika chache simu Ilipokelewa
" Hallow my sweetheart
" Hallow baby
" Mpenzi nina habari njema nataka kukishirikisha
" Nishirikishe na mimi nifurahi asali wangu.
" Kesho naenda kwenye usaili....
" Waooo safi sana kweli hizi ni habari za kufurahisha nimefurahi sana mpenzi wangu natumai kila kitu kinaenda sawa na nakuomba upite kwenye usahili.
" Asante sana mpenzi nashukuru sana kwa kunitia moyo .
" Hata wewe huwa unafanya hivyo kwangu , na mimi jukumu langu kuwa hivi kwako.
" Asante. Samara alijibu kwa hisia
" Mmmh uko wapi sasa?
" Nipo sehemu na marafiki.
" Marafiki hao wakike wa kiume?
"Wakike usiniambie unanionea wivu.
" Ni kweli kabisa mimi nina wivu haswa ungeniambia wa kiume ungeniweka kwenye wakati mgumu sana.
" Basi kuwa na amani mpenzi.
" Sawa nakuamini.
" Ok bye.
Samara alikata simu Cecy akamuuliza.
" Huyo ndio mwanaume wako wa online?
" Ndio ni yeye Salmin.
" Ni kweli hajawahi kuonana na hamjuani ?
" Ndio.
" Mbona kama ni watu wenye mapenzi mazito inawezekana vipi ikawa hivi?
" Ndio hivyo imewezekana mnajua kuna wakati natamani hata kumuona lakini haikuwa makubaliano yetu mahusiano yetu ni ya kwenye simu tu .
" Mmmh kwahiyo nini hatma ya hayo mahusiano yenu?
" Sijui kwakweli ila nafurahia kuongea nae maana amenionyesha ulimwengu wa mahusiano ulivyo hata kama atatokea wa kuwa nae serious basi nitaangalia mwenye vigezo kama vyake.
" Usijali kipenzi huyo ndio mwanaume wako. Alisema Happy.
" Unanitia moyo?
" Nahisi hivyo .
" Ni kweli kila kitu huja kwa sababu kikubwa kuwa na Subra kipenzi, hata sisi tunatamani upate mwanaume uwe kama sisi. Alisema Cecy
" Jamani mkaniliza hebu njooni hapa. Walisomea pamoja na kukumbatiana.

Kesho yake mapema Salmin alinuamsha kwa kumpigia simu .
" Hallow baby , umeamkaje?
" Salama vipi wewe umeamka salama?
" Ndio nimeamka salama, nijekupigia ijiandae sitaki uchelewe kwenye usaili.
Samara alitabasamu alafu akasema
" Asante mpenzi , najivunia wewe , unajali sana.
" Kwako ni kawaida kufanya hivyo , amka ukajiandae.
" Sawa asante.
" Ukiwa unaenda usisahau kumuomba sana Mungu .
" Sawa honey.

Samara alienda kujiandaa alipomaliza aliondoka na kwenda kwenye kampuni ya Muntazar . Majira ya saa mbili alikuwa kashafika akapokelewa na secretary akitambulisha.
" Naitwa Toya nipo hapa kwaajili ya usahili.
" Sawa nenda ghorofa ya tatu utakutana na wenzako , utakaa kwenye foleni mpaka zamu yako ikifika itaingia.
" Sawa asante. Samara alienda mpaka alikoelekezwa akakutana na wenzake watatu walioenda kufanya usaili nae akaunga foleni akisubiri zamu yake.

Watu wote walifanyiwa usaili mwisho kabisa akaingia samara na kusalimiana na boss kisha akawasilisha cv zake.
Bissz alipokea cv akaagalia pamoja na kitabu chake cha ubunifu .
" Hiki nini sasa mbona huna ubunifu wa kutisha. Haijanivutia kabisa kwenye kampuni yangu sihitaji mtu wa aina hii kwenye kampuni yangu.
Samara aliumia sana kwani alionekana kumkatisha tamaa .
" Unaweza kuniambia kazi hakuna na sio kunikatisha tamaa kiasi hicho nipatie vitu vyangu.
Yule boss alimwuka mezani na kumsogezea , samara alichukua na kurudisha kwenye bahasha kisha akatoka. Alipofika nje ya jengo akamfunika messege Salmin.
" Mpenzi mambo yamekuwa mabaya nimekuta kuja kwenye huu usahili huyu boss sio muungwana kabisa.
" Kakufanya nini?
" Sio muelewa, sio mtaarabu ni wa ajabu sana kaniharibua siku yangu.
" Kwani uko wapi baby moja nikuchukie twende tukakae sehemu huenda ukawa sawa.
Samara alifurahi kwani alitamani sana kumuona .
" Sawa ngoja nikitumia location.
" Sawa.
Baada ya dakika chache samara alimtumia location.
Salmin alishituka sana kwani alikuwa nje ya jengo lao moja kwa moja akajua yule binti wa mwisho kumfanyia usahili alikuwa ni samara.


BOSS WANGU (MPENZI WANGU WA SIRI) 4

MTUNZI SMILE SHINE

" Unamaana yeye ndio aliekuwa hapa?
Kwa uhakika zaidi aliuliza
" Umevalia nguo gani?
" Nimevaa gauni la pink.
Aliposoma messege kutoka kwa samara akasema
" Ni yeye nafanya nini sasa? Akiwa bado anafikiria iliingia messege nyingine kutoka kwa samara.
" Mr Salmin fanya haraka nina hamu sana ya kukuona, endapo nitamuona nitapata nafuu na kusahau kero zote nilizofanya na huyu boss jeuri.
Salmin alishindwa ajibu nini alichofanya alimpigia simu steve mfanyakazi wake na kumuomba akamuangalia samara pale nje.
"Steve umemuona dada mmoja kati ya wale waliokuja kufanya usahili alikuwa kavalia gauni ya pink ?
" Ndio nimemuona.
" Hebu mcheki hapo chini ukimkuta hebu njoo nae.
" Sawa.

Steve alitoka nje akamkuta samara kasimama.
" Habari yako dada
" Salama
" Boss Muntazar anakuhitaji ofisini kwake.
" Huyu boss wako ananihitaji mimi niende ofisini kwako? Aliuliza samara kama kwamba hajasikia au hajaelewa
" Ndio .
Samara alisimama kwanza akiwa anajishauri amjuze Salmin au aende kuonana na boss.
" Dada vipi mbona umezibaa twende.
Samara aliamua kurudi ofisini kwa boss.
" Karibu ukae. Safari hii boss alimkaribisha kwa upole huku akimuangalia usoni.
Samara alivuta kiti akakaa.
" Kazi umepata. Alisema boss
Samara alishangaa mtu aliyemponda sasa ameamua kumpatia kazi kirahisi vile kwakuwa alikuwa na uhitaji wa kazi alikubali .
" Sawa asante.
"Steve mpeleke kwenye eneo lake la kazi , zoya unatakiwa kuanza kazi mara moja na unatakiwa kuwa makini na kazi yako.
" Sawa boss.
Samara alinyanyuka akangozana na steve mpaka kwenye ofisi yake mpya.
" Miss...
"Zoya . Samara alijitambulisha hivyo na kazini walimtambua kwa Jina la zoya.

Salmin akawa anajiuliza kwanini awe zoya na yeye anamfahamu kwa jina la samara?

Samara akiwa anafanya maandalizi ya ofisi yake uliingia ujumbe kutoka kwa Salmin.
" Samahani mpenzi kwa kuchelewa kujibu messege yako , bado utakuwepo hapo nije sasa hivi?
"Hapana mpenzi usije mambo yamebadilika yule boss jeuri amenipatia kazi.
" Ni jambo la kushukuru maombi yetu yamejibiwa.
" Ni kweli ila anaonekana mtata sana.
" Kwani yupoje yupoje?
"Kumuangalia ni mwanaume mtanashati sana lakini tabia yake sijaipenda anaonekana jeuri sana.
" Umesema mtanashati inamaana imevutiwa nae?
" Hapana mpenzi siwezi kuvutiwa na mwanaume wa aina yake wewe tu unanitisha.
Salmin alisoma akatabasamu kisha akauliza
" Anaitwa nani?
" Muntazar.
"Oooh sawa mpenzi mvumilie tu. Hii messege ya mwisho Salmin alituma huku akiwa anamchungulia. Samara alipotaka kujibu Salmin akajitokeza
" Hey miss hauna muda tena wa kuchezea simu unatakiwa kuanza kufanya kazi andaa mazingira alafu uanze kazi ya kubuni mitindo.
" Sawa boss.
Alijibu samara kisha akasogea kwenye kompyuta na kuanza kufanya kazi. Wakati huo Salmin alikuwa kasimama na kumuangalia kwa
Makini.
Kwa mbali Salmin alikuwa anatabasamu kwani samara alikuwa muoga. Kila alichomwambia alikuwa akisema sawa boss

Muda wa kazi ilipoishia samara alirudi nyumbani , wakati anapata chakula simu yake iliita alikuwa Salmin anapiga.
" Vipi baby uneshafika nyumbani?
" Ndio mpenzi nipo mezani nakula.
" Oooh basi acha nikuachie ule kwanza.
" Hapana naweza kuongea na wewe huku nikiwa naendelea kula.
" Lakini sio salama kula huku unaongea itakuwaje kama ukipaliwa.
" Nitakuwa makini nisipaliwe.
" Unajua ikitokea hivyo nitajilaumu sana maana sipendi upate tatizo.
" Usijali nipo makini sana.
" Ok , vipi siku ya kwanza kazini ilikuwaje?
" Uuuuh ilienda vizuri ila yule boss anajifanya nione kazi ngumu sana.
" Kwanini. Kwani anakusumbua?
" Hapana hanisumbui ila sijavutiwa nae ni mtu anaejisikia sana ,anaonekana jeuri ana dharau.
Salmin alishusha pumzi kisha akauliza
" Anaitwa nani huyo boss wako?
"Muntazar.
Samara alivyotaja hilo jina Salmin alishusha pumzi na tabasamu kwa mbali kwani alijua samara hajagundua wala hajahisi chochote kuwa yeye ndio boss wake anaemponda.
" Vipi muonekano wake yupoje?
" Ni mtanashati sana anavutia mbele za watu ila tabia yake ya ujeuri haimpendezi kabisa.
"Basi achana nae mpenzi wangu wewe piga kazi.
" Hicho ndicho ninachojali.
" Basi acha nikuachie ule ushibe, upumzike kidogo baada ya hapo tutaongeza tena .
" Sawa mpenzi.

Kesho yake mapema sana samara aliamka na kumtumia Salmin ujumbe wa kumuamsha na kumtakia asubuhi njema. Muda sio mrefu Salmin alirudisha majibu.
" Nimeamka mpenzi nashukuru kwa kuniamsha ,siku hizi kila mtu ananisikia kwa kuamka mapema na hizi zote ni juhudi zako malkia wangu, bila shaka utakuja kuwa mama mwema kwa watoto wangu hapo badae.
Salmin valimwagua sifa nyingi na samara alijibu huku akiwa anatabasamu.
Samara alijikuta anachat na kujisahau kama anatakiwa kuwahi kazini . Alikuja kushtuka muda umeenda na hajafanya chochote .
" Mungu wangu hii ni akili gani yani mpaka jua linachomoza nipo kitandani na chat hata kuoga sijaoga.
Aliweka simu pembeni na kukimbilia bafuni. Salmin aliendelea kutuma messege lakini hakujibiwa.

Samara alijiandaa haraka haraka hakupata hata muda wa kupata kikombe cha chai alitoka haraka na kupelekea kazini. Akiwa njiani simu yake iliita alikuwa ni steve anapiga.
" Habari steve!
" Salama , uko wapi ?
" Nipo njiani nakuja .
" Boss alikuwa anakuhitaji.
" Mungu wangu amefika saa nyingi?
" Ni kama dakika 40 yupo hapa .
" Sawa nafika hapo sasa hivi.
Baada ya muda samara alikuwa kashafika kazini akaenda moja kwa moja ofisini kwake alikaa kwenye kiti akatoa simu akakutana na messege kama tano za Salmin, ilimbidi anajibu kwanza ndipo aende kuonana na boss wake.
" Samahani mpenzi nimechelewa kukujibu sababu nilikuwa nimechelewa kazini hata hivyo huyu kisirani ameniulizia naenda kuonana nae kwanza.

Messege ilimfikia Salmin, alinyanyua simu yake na kuusoma ule ujumbe ghafla alisimama na kwenda ofisini kwa samara, alimkuta samara kasimama anajiangalia kwenye kioo chake kidogo kama uso wake upo sawa ili aende ofisini kwa boss maana alitoka nyumbani haraka hakupata muda wa kujiangalia uso wake.
" Hiki nini kinaendelea hapa hujatosheka na kujiangalia na kioo huko nyumbani kwenu mpaka uje kujiangalia ukiwa kazini? Aliuliza Salmin huku akiwa
Kashika meza na akiwa kamkazoa macho usoni kwake .


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote