Ni simulizi inayomuhusu bint husqer ambae alikuwa anaishi na mama yake na mdogo wake mwenye MATATIZO ya moyo, husqer alipofika kidato Cha tatu akajiingiza kwenye mahusiano na Stanley ambae kwa wakat huo alikuwa kidato Cha sita kwenye shule hio hio, Stanley anampenda sana husqer na kutokana na tabia zake na utulivu wake Stanley anamuahidi kuwa hatakaa amguse mpaka ndoa, na ingawa hakuwa na maisha magumu ila siku zote za weekend alikuwa anaenda kutafuta vibarua kwaajili ya kumsaidia baadhi ya majukum maana husqer alikuwa na maisha magumu sana...
Ila siku ya siku mdogo wake husqer anaitwa anarld anakuja kuuguwa na inahutajika million mbili kwaajili ya matibabu, husqer hakuwa na cha kufanya na kwenda kujiunga na kundi la wadada wanaojiuza, siku hio anatoka kwenye shughuli zake anakutana na Stanley na kwa namna alivyo kuwa amevaa ni dhahiri kuwa alikuwa changudoa, stanley anaumia sana ila alishindwa kumsahau na hisia zake bado zikawa kwa husqer mpaka siku aliolazimisha kulala nae akashangaa kumkuta bado bikra na wakat alikuwa na uhakika kuwa alishawah kujiuza
BIKRA TATA 1
HUSQER BALTAZAR
Kuna muda unaweza kufanya jambo ambalo haukuwah kulifikiria kwa sababu ya kuwasaidia uwapendao, ila ikaleta hukmu tofauti kabisa kwa watu ambao wanakuamin sana, naitwa husqer baltazar, baba yangu alifariki kipindi ambacho nilikuwa na miaka mitano, na alimuacha mama akiwa mjamzito wa mdogo wangu wapili, ambae alizaliwa mara baada ya baba kufariki, alikuwa anaitwa anorld, maisha yetu hayakuwa mazuri sana maana mama hakuwa na kipato cha kueleweka, hivyo kazi zake kubwa zilikuwa ni kulea watoto wa watu wanaoenda kazin, maana pale nyumban kwetu kuligeuka day care, maana kila siku asubuh watu walikuwa wanaleta watoto wao, na mama ndio alikuwa anawalea, na kila siku anaachiwa elfu moja kwa mtoto mmoja, na siku za mapumziko kama jumamos na jumapili, mama alikuwa anapita kwenye majumba ya watu na kuwafulia, hapo sisi tulikuwa wadogo, ila tulipoanza kukuwa, nikawa napika karanga nyumban naenda kuuza shule, na kidogo hata nikawa naweza kujitimizia mahitaji yangu
Maisha yalienda na nilikuwa nachunga sana utu wangu, maana nilikuwa naogopa mno kuja kumuongezea mama yangu pressure ya kuwa na tabia mbaya, maana maisha yetu ni stress tosha…
Mdogo wangu anorld yeye alikuwa ni mgonjwa mgonjwa sana kuanzia anazaliwa, walisema alikuwa na tatizo la moyo, hivyo alikuwa hata hawez kuhudhuria masomo vizuri kutokana na afya yake namna ilivyo, na kupelekea mimi na mama tuwe tunafanya kazi kwa juhudi sana, ili kuhakikisha tunampa mahitaji yake hata kidogo, na asiweze kukosa hospital kila anapohitajika kwenda….
Kama mnavyojua mimi ni binaadamu, nilipofika kidato cha nne, kuna kijana nilimpenda, na sio siri na yeye alikuwa anaonekana kunipenda sana, alikuwa yupo kidato cha sita kwenye shule ambayo nilikuwa nasoma, alikuwa anaitwa Stanley….
Alikuwa ananipenda sana mpaka nikawa naogopa, yaan kuna muda alikuwa anataka kunisaidia kuuza bidhaa ambazo nilikuwa naenda nazo shule, ila sikutaka kumuingiza kwenye matatizo yangu, ila alikuwa anaenda kufanya kazi za vibarua kipindi cha jumamosi na jumapili ili aniletee pesa mimi, na kunisaidia kutatua baadhi ya shida zangu….
Nilikuwa nampenda sana, na hata familia yangu ilijua namna ambavyo Stanley alikuwa ananipenda sana, na mama yangu siku zote alikuwa anatuombea sana tuje kuwa pamoja siku moja, dua ambayo mimi na stanley wote tulikuwa tunataman ifikie, maana tulishaambizana kuwa hatutakaa tufanye mapenzi mpaka tutakapofunga ndoa, na stanley alionekana kunielewa kabisa…..
Maisha yakawa yanaendelea na Stanley hakuwah kuatoka nupande wangu, ingawa nyumban kwao hakukuwa na shida sana, ila alikuwa anapambana sana kwaajili yangu, ila siku moja mdogo wangu anorld akazidiwa, ilikuwa ni usiku, tukampeleka hospital, tukaambiwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji maana hali yake sio nzuri kabisa, na pesa inayohitajika ilikuwa ni kama million mbili….
Mimi na mama tulihisi kuchanganyikiwa, mama alikaa chini na kuanza kulia, nilimsogelea na kumuambia mama usijal tutapata tu pesa mama usijali…
“ husqer mwanangu tunaipata wapi hio hela, na maisha yetu ndio haya ya kuunga unga, embu nambie tunapata wapi, mama yangu aliongea kwa sauti ya kukata tamaaa, na hata mimi nilikuwa nampa moyo tu, ila sikuwa na uhakika kama naweza kupata kiasi chote cha pesa, na nilijua ningemuambia stanley angeweza hata kuchukua kitu nyumban kwao kwaajili yangu, maana ameshafanya mara kadhaa, sasa sikytaka achafuke kwa sifa mbaya……
Nilimchukua mama na kurudi nae nyumban, ila wakat wote ambao tulikuwa kwenye daladala nilikuwa nawaza namna ya kupata hizo pesa zote, tumefika nyumbnan sikuwa na raha kabisa, maana nilikuwa naona kama maisha ya mdogo wangu yanaelekea kuisha, nilikaa nikatafakari sana bila kupata majibu yoyote yale, mama yangu hakuwa sawa kabisa hivyo alishinda amejikunyata, kama mtoto mchanga ambae ametelekezwa na mama yake, sio siri nilimuonea huruma sana, maana nilikuwa nayahisi maumivu yake….
Nilitoka nje ilikupata hewa, maana nilikuwa naona kama pale ndani kuna hewa nzito sana, nikiwa nimekaa palem kuna dada alishuka kwenye gari, kila mtu alikuwa anamjua kuwa ni mdangaji, ila ni wale wadada wanaodanga na watu wa maana, na sio hawa wa elfu kumi kumi, alikuwa anaongea na simu akisema “ Yule mzee wa hovyo anataka demu si unajua namna anavyomwaga mahela ila shoo zero, akawa anasema Yule dada….
Nilijikuta navutiwa na mazungumzo yake, yaan niliposikia kuwa kuna mtu ana mwaga hela na mimi nina shida ya hela niliona kama ndio fursa yangu sasa, Yule dada akawa anasema “ amesema atatoa kitita kinene kwa mwanamke ambae hawajui wanaume, unajua akikutana na kabikra katakuwa hakaelewi kama kamepewa shoo au kamechafuliwa, maana sisi wengine hata kama tunapenda pesa ila na shoo za kueleweka ni lazima, akawa anasema Yule dada…
Kwa uwoga na wasiwasi mkubwa nikamfata Yule mwanamke na kumsalimia, hakuwa amenizidi sana, ila alikuwa mkubwa kwangu kidogo, nikamuambia shikamoo, akageuka na kuniangalia kisha akasema “ una shida gani?....
‘ mimi ni bikra, nikajikuta nimeropoka, akaniangalia kisha akacheka na kusema “ shoga subiri nimepata bingo haraka san hata sikutegemea…
Aliniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akanambia kuwa “ nina uhakika umeyasikia maongezi yangu, na najua wewe sio mgeni kwneye huu mtaa na unajua biashara zangu, sasa basi kwa kusema hivyo unajua kabisa sehemu ambayo nitakupeleka si ndioa…
‘ hakuna shida dada nina shida ya hela sana, nipo tayar kufanya lolote lile, akaniangalia kisha akaniuliza una simu?...
‘ hapana dada sina, nikamjibu…
‘ usiniite dada bana, acha kunizeesha, sasa tofauti yangu mimi na wewe ni nini, wewe niite jina langu naitwa paula, akasema Yule dada, kisha akanambia kuwa kesho asubuh niende nyumban kwake akanikague vizuri kama nafaa au laa….
Nikakubali ila nilikuwa na hofu kubwa sana, maana kwanza nilimuahidi Stanley kuwa nitajitunza kwaajili yake, ila shida sasa mimi nifanya je na wakat namuona kabisa mdogo wangu anataka kufa, siku hio sikulala kabisa, nilikuwa nafikiria namna ambavyo naenda kutolewa bikra bila kutegemea, nilikuwa nawaza kuvaa kikahaba na wakat mavazi ya heshima ndio mavazi pekee ambayo naweza kuvaa, nilitaman nisiende ila sikuwa na namna…
Asubuhi ilipofika nikafanya usafi, maana siku hio ilikuwa ni jumamos sio siku za shule, na baada ya hapo nikaenda kwa Yule dada, nilipofika nikapokelewa na harufu kali ya pombe, ila akanikaribisha ndani…
“ mambo akaniambia…
“ poa dada , nikamjibu….
“ nilishakuambia mimi naitwa paula na sio dada bana usinizeeshe, akasema Yule bint kisha akaanza kunikagua na kusema ‘ kumbe wewe ni mrembo, jana usiku sikuwa nimekuona vizur, hakika unafaa sana, akaingia kwenye kabati lake na kunitolea vinguo vya kikahaba, ili nianze kujaribisha…
Ilikuwa shida sana kwangu, maana sijawah kuvaa nguo fupi kiasi kile ila sikuwa na namna nyingine yoyote ile zaidi ya kukubali, nilikuwa nataka kumsaidia mdogo wangu, nilikuwa nataka kumpa amani ya moyo mama yangu….
Basi siku hio nikamuaga mama yangu kuwa naenda kulala kwa shoga yangu flani hivi, na kwakuwa mama alikuwa ananiamin sana akakubali…
Nikaenda kwa Yule dada, akanichukua na tukaenda kwenye hotel moja kubwa sana, na humo ndani kila unaemuona anapesa, nilikuwa nimerembwa mno, na wanaume wengi ambao walikuwa wananiona walikuwa wananitaman sana, ila Yule dada akanambia nisimchekee mwanaume yoyote, maana wengine hawatafika bei maana nay eye anataka cha juu….
Nikiwa na wasiwasi mkubwa sana, maana nilikuwa nimezoea kushinda kanisani na nyumban kwetu, ila siku hio nilikuwa nimeshinda kwenye hotel moja ambapo kila unaemuona unamjua yuko kikazi, maana wanawake wengi walivaa nguo za kuficha tu sehemu zao za siri, na wengine mpaka kivuli cha sehemu za siri ulikuwa unaweza kuina vyema….
Kwenye majira ya kama saa nne usiku, aliingia baba mmoja, ambae alikuwa na kitambi, alivaalia kama hawa wanaijeria, akiwa ameshika fimbo aina ya mkongojo, aliingia na vijana wawili ambao wote walikuwa wamevalia suti nyeusi, akaja mpaka pale tulipo , na macho yake yalikuwa kwangu, na alipofika akatabasamu kisha akasema ‘ mrembo ndio huyu hapa eee…
Yule dada niliekuwa nae, akatabasamu kisha akasema “ kama umemuelewa nilipe change nisepe….
Nilishangaa sana maana Yule baba alitoa elfu kumi nyingi kidogo na kumpatia Yule bint, hata hakuhesabu ametoa kiasi gani, kisha Yule bint akacheka na kuondoka akaniacha nae……
Nilikuwa natetemeka sana, akanambia nimfate, nikakubali, nikafika chumban kwake, akaanza kunishika shika, nilikuwa na hofu kubwa sana, na ni kama ile hofu yangu ndio ilikuwa inampa ujasiri, akanambia nimuwekee kinywaji, nikamuwekea akawa anakunywa mpaka akalewa, nikakaa pemben yake, akawa anacheka cheka , nikashangaa amelala fofofo, amekuja kuamka kama saa mbili nilikuwa pemben yake, akaanza kujisearch akajikuta na kila kitu, aisee akacheka na kusema “ kweli nimeletwa bint bikra, nilijua nitakuta umeniibia, ila wewe ni muaminifu sana, leo sina hela nyingi ila kesho hakikisha unakuja na nitakupa pesa, na wewe utakuwa ndio mwanamke wangu, ila naomba uwe unanifichia aibu yangu, maana watu wananijua kama mzee wa tembeza fimbo, yaan nikimshika demu ataimba, ila sasa siwez kutokana na maradhi, na siwez kukubali kushusha heshima yangu, naomba usikje kumuambia mtu yoyote Yule kwamba hakuna kitu tunafanya, na ikiwezekana kesho ujifunze na namna ya kutoa miguno, ili watu wajue kuwa nakukuna haswa…...
Nikakubali na nikaona ni bora, maana angalau sitolala nae….
Kwa mawasiliano zaidi tutafute kwa 0764872249
NAKUJA…………………………..
BIKRA TATA 2
HUSQER BALTAZAR
Basi nikaubaliana nae pale, na kweli alinipa hela, na yeye alikuwa anasema kuwa sio pesa nyingi ila nilipotulia na kuzihesabu ilikuwa karibu laki nane na sabini, nilishangaa sana, maana nimepata pesa nyingi tena kwa muda mchache mno…
Aliniaga na kunisisitiza kuwa nisimtangaze….
Sasa jumatatu nilikuwa natakiwa kwenda shule maana sikuwa nimemaliza kidato cha nne, na shule ambayo nilikuwa nasoma ndio hapoo hapo stenley alikuwa anasoma, nilipomuona nilikuwa namuonea aibu mno, maana nilikuwa naona kama nilikuwa nimemsaliti ingawa sikuwa nimelala na yule mwanaume, kila nilipokuwa najitahidi kujichangamsha nilishindwa, huzun na hisia za usaliti zilinitawala, maana kila mtu alikuwa anajua ni kiasi ganin Stanley alikuwa anapambana sana na kujitoa mno kwaajili yangu, hivyo sikuwa napaswa kabisa kumlipa ubaya hata kidogo, ila sasa ningefanya nn, na wakat hana uwezo wa kunipa pesa za kumtibu mdogo wangu….
Muda ulienda na muda wa Stanley kumaliza kidato cha sita ukafika, na huwa wanamaliza mwezi wa tano, na mwaka huo huo mwezi wa kumi na moja ndio namaliza kidato cha nne, alifanya mitihani yake na kila wakat alikuwa anaomba nimuombee, maana aliniahidi kuwa mafanikio yake ni mafanikio yangu, na natakiwa kusali sana na kuomba sana kwaajili yake………..
Na kweli nilikuwa nasali sana na kumuombea mno, maana nilikuwa nampenda sana …..
siku moja Yule dada ambae alikuwa anakawaida ya kuja kunichukua na kunipeleka kwa kile kizee alikuja, na sikuwa naweza kabisa kumkatalia anachokitaka, tulienda, na kama kawaida huwa silali nae, nammiminia kinywaji tu, na kumpeti peti, kuna siku huwa ananiambia nigune gune, basi nitaguna hapo kisha nitaondoka, na siku hio ilikuwa hivyo, ila hakuna mytu hata mmoja ambae anajua kuwa sikuwah kulala na hicho kizee zaidi yangu mimi, na nafsi yangu……
siku hio alinambia anataka kwenda kulala nyumban kwake maana anaugeni, hivyo kwenye majira ya kama saa nne usiku nikawa narudi kwetum na yuke dada ambae alikuwa ananipeleka, nae siku hio hakuwa sawa, hivyo tukawa tunarudi wote nyumban, ile tunashuka kwenye gari namuona Stanley huyu hapa……….
Sio siri nilishtuka sana, maana kwanza ilikuwa ni usiku sana, na sio kawaida yake kuja kunitembelea usiku kiasi chote kile, aliponiona ni kama alipigwa na butwaa, hivyo akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasema “ husqer ni wewe…
Nilikosa hata jibu la kumpa, maana kwanza nilikuwa nimevalia kikahaba sana, na pili wakat ule ulikuwa ni usiku sana, sijui ningemuambia nini, akanisogelea na alikuwa amebeba ka cake kadogo, nolipokaona ndio nikakumbuka siku hio ilikuwa ni birthday yangu, maana hata mimi mwenyewe nilikuwa nimesahau, na siku zote styanley huwa anapambana sana kuhakikisha nakuwa na furaha hata kwa chochote kidogo anachonipa, na kweli nilikuwa na rizika sana na kila anachonifanyia, ila ndio hivyo kaka yangu alikuwa anahitaji pesa, na kwa msaada wake najua huwenda kwa wakat ule tungekuwa tunataarifa za msiba, sasa mimi ningefanya je zaidi ya kwenda kwa Yule baba, na Stanley mwenyewe hakujua kuwa mdogo wangu alikuwa anaumwa sana na zilikuwa zinahitajika pesa nyingi…………..
“ umetoka wapi sasa hivi na kwanini umevaa hivyo? Aliniuliza kwa sauti ya ukali kidogo, na sio siri nilijisikia vibaya sana, maana sikuwa nataman kumpoteza kabisa Stanley na sikujua hata jibu zuri ambalo nilikuwa natakiwa kumpa……
Nikiwa natetemeka kwa wasiwasi na woga mkuu, Yule dada akjacheka kwa dharau kisha akasema kwa sauti ya kilevi kuwa “ maswali gani hayo unamuuliza na wewe mwanamke mrembo kama huyu, najua kama umeshawah kupita pita huu mtaa basi utakuwa unajua kazi ambayo mimi huwa nafanya, na kikawaida siwez kuongozana na bint mrembo ambae hawez kufanya kazi kama yangu, sasa ni hivi acha kuuliza maswali ya kipuuzi, akasema Yule dada huku akiwa anayumba yumba na kuanza kuondoka zake kwa tabu huku anacheka cheka na anayumba yu,mba…
Stanley alinisogelea na kusema “ husqer mamaaa mbona sielewi jambo lolote lile linaloendelea, siamin kama na wewe unajiuza licha ya kuniahidi kuwa iutajitunza siku zote kwaajili yangu, ulinambia kuwa unanipenda mimi pekee yangu, na mwili wako ni mali yangu mimi tu, nambie kwanini umeenda kujiuza husqerm ni kitu gani unakosa kutoka kwangu, mbona napambana sana kwaajili yako, mbona najitahidi kuhakikisha kuwa unafuraha na hauna mawazo, au kwakuwa sikuwa nakupa haki ya ndoa ndio maana ukaamua kwenda kuitafuta kwa watu ambao wanapesa, ila kumbuka kuwa uliniahidi kuwa hakuna mwanaume ambae utampa tunda lako zaidi yangu tena kwenye ndoa yangu, akaanza kulalamika Stanley….
“ sio hivyo Stanley, mambo hayako kama unavyofikiria, nikaanza kujitetea…
“ eheeee yapoje, akasema Stanley akiwa ananisogelea, kisha akanikwapua pochi akakutana na simu kali, ambapo kwa kipindi hicho yeye alikuwa anamiliki simu ya button tena ya bei rahisi sana, na pesa karibu laki nane, akazimwaga pale chini, akawa anataman kuzichana chana, ila akajizuia na kuanza zake kuondoka, ila akanambia “ usije ukathubutu kunisogelea tena wewe mwanamke, nakuchukia sana, na siku moja utalipia kila kitu ulicho nifanyia, kisha akaondoka zake….
Sikuwa na cha kufanya zaidi ya kulia, ni kweli nilikuwa naigiza kama naenda kujiuza ila sijawah kulala na mwanaume yoyote Yule, ila sikujua naweza kumuelezea vipi Stanley wangu mpaka anielewe…..
Basi kesho yake asubuh kwenye majira ya kama saa nne kasoro nilienda nyumban kwa akina Stanley, maana kila mtu nyumban kwao alikuwa ananijua, wakanipokea vizuri, maana nilikuwa nasifika kuwa na tabia nzuri sana mtaan, hivyo hata niliopofika wakanipokea vizuri, na nikawa na uhakika Stanley hajawaambia familia yake chochote kile kuhusu mimi…..
Nikaulizia Stanley yuko wapi, wakanambia amesafiri asubuh ya siku hio na kwenda kigoma, na hatorudi mpaka matokeo ya kidato cha sita yatakapotoka, ila walishangaa sana, inawezekana vipi Stanley aon doke bila kuniaga na wakat kila mtu alikuwa anajua namna ambavyo alikuwa ananipenda sana….
Kwa unyonmge nikarudi nyumban, kisha nikakaa zangu mwenyewe ndani na kuanza kulia, maana kumpoteza Stanley kwenye maisha yangu ni pigo moja kubwa sana, maana najiona kabisa kuwa siwez kuishi bila yeye, nililia sana mwisho nikaona niache maisha mengine yaendelee….
Muda ulienda na hatimae nikamaliza kidato cha nne, na wakat wote huo sikuwah kukutana kabisa na stanley….
Matokeo ya kidato cha nne yakatoka, na bahat haikuwa upande wangu kwani nilifeli, ila hata sikuumia maana akili za shule sikuwa nazo kabisa…
Niliacha kabisa kwenda kwa Yule mzee, ila alikuwa bado ananitumia tumia pesa, akisema kuwa nimemuheshimisha sana, hivyo akawa bado ananisupport…
Nilikuja kusikia Stanley alipomaliza form six akaamua kwenda kusoma india, hata sikuwa najua alikuwa ameenda kusomea nini, na baada ya hapo sikuwah kupata taarifa zake tena……………
NAKUJA……………….
BIKRA TATA 3
HUSQER BALTAZAR
Miaka ilienda, na hatimae ikapita miaka mitano sasa, nilikuwa muoga sana wa kuingia kwenye mahusiano husqer mimi, maana niliamin kuwa natakiwa kuwa na Stanley pekee yake, nilikuwa natongozwa ila kila nikitaman kumkubali mtu roho yangu ilikuwa inanisuta sana, nilikuwa nahisi kama namkosea sana Stanley na wakat sikuwa najua kabisa kama huko alipo anamtu au laa, na sikuwa na uhakika hata kama atanipenda akiniona au ndio chuki zake kwangu zitazidi kuwa kubwa zaidi ya mwanzo….
Maisha yalienda na yule mzee sijui hata aliendaga wapi, maana hakuwa anapatikana tena, maisha yangu yakarudi, yalikuwa maisha ya tabu sana, maana sikuwa nimesoma, ila kipindi hichi angalau mdogo wangu anorld alikuwa sawa, hakuwa anaumwa hovyo……
Basi maisha yakawa yanaendelea kama kawaida, na mimi na mama yangu kazi zetu zikawa zile zile, yaan tunapita kwenye majumba ya watu, tunafua na kufanya kazi za ndani, ila siku moja dada yake Stanley alinifata na kunambia kuwa Stanley anakaribia kurudi na alikuwa anataka kutafutiwa mke, akawa ananiuliza kuhusu mimi, maana walikuwa hawajui kama nilikuwa nimegombana na stanley, na walihisi sijui bado tunawasiliana au vipi, maana sikuwa nawaelewa kabisa….
“ husqer kwani mmeachana, au ndio Stanley ameshajua kuwa kwa kipindi chote hichi utakuwa umeshaolewa, maana sisi tunaona kama anakufaa sana, akasema dada yake Stanley…..
“ hamna tupo vizuri tu, nadhan anataka mniandae mimi kwaajili yake maana huenda anashindwa kusema mwenyewe moja kwa moja, nikasema na dada yake akatabasamu kisha akasema “ sawa jiandae, ila tuahidi kuwa haujawah kufanya mambo yetu yale, maana anataka kitu sild….
“ wifi kwani hunijui jaman, mimi mwanaume wangu pekee ni Stanley na sijawah kuwa na mwanaume mwingine yoyote Yule, na kama unavyomjua kaka yako, hajawah hata mara moja kunigusa, na zile sharia zake za kila siku, kuwa hataki kumchezea mtoto wa mtu, na kweli hakuwah kunichezea, nikasema na dada yake stanley akacheka kisha akaondoka zake….
Nilikuwa na shauku sana ya kumuona Stanley, nilikuwa nataman sana hata anioe, au hata mimi ndio niwe mwanamke wa maisha yake, nilikuwa nataman hii bikra yangu iwe zawad yake, sijui kama ataamin kuwa sijawah kufanya au ndio ataona kama nimemtengenezea tu…..
Basi bana kabla Stanley hajaja nikapata kazi kwenye shirika moja linalohusiana na kutengeneza website kisha wanaziuza kwa watu mbali mbali nchini, nikapata kazi pale kama mfanya usafi, ingawa kulikuwa kuna kazi nyingi ila sikuwa nimesoma hivyo sikuwa na kazi itakayonifaa zaidi ya kufanya usafi tu……
Nikaanza kazi, na wafanya usafi tulikuwa watatu tu kwenye jengo zima, mimi nilikuwa nafanya kwenye maofisi yote ya jengo hilo, na kuna mwingine anafanya kwenye kordo zote za jengo, na mwingine alikuwa anafanya nje, huyu anaefanya kwenye kordo anasagfisha mpaka ngazi, ila mimi ni kwenye maofisi tu….
Nilifanya kazi kwa takriban miezi miwili, na mshahara ulikuwa ni laki na nusu, ilikuwa ni pesa nyingi sana kwangu, maana kwanza hatukuwa tunafanya kazi siku nzima, yaan saa sita tumeshamaliza, maana jion kuna wafanyakazi wengine walikuwa wanakuja, siku moja nilipomaliza majukum yangu nikiwa najiandaa kuondoka, boss wetu wa maswala ya mazingira alitufata na kutuambia kuwa, kesho yake kuna mkurugenzi mpya anakuja, na moja ya sifa yake ni kuwah sana kazin, hivyo ule muda ambao huwa tunaanza kusafisha tujitahidi kuwah zaidi, maana pia tutaondoka mapema zaidi…..
Tulikubali,maana huwa tunafika kazin saa moja kamili, na saa mbili kamili ndio kazi zinaanza, basi siku hio nilipofika nyumban hata sikutaka kusema na mtu na nikapitiliza moja kwa moja kulala, lengo ni kuwa kesho yake niwah kwenda kazin, na kweli niliamka saa kumi na moja na nikaanza kujiandaa, mpaka saa kumi na mbili kasoro nilishafika kazin, nadhan mimi ndio nilikuwa mfanyakazi wa kwanza siku hio, yaan nilimkuta mlinzi tu, na nilipofika nikapitiliza moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya huyo boss, lengo ni kuwa nifanye usafi kabla hajaja, kwlei nilifanya usafi, nilipomaliza nikawa natoka kwenye hio ofisi, mpaka wakat huo nilikuwa na uhakika kuwa wafanyakazi bado hawajafika….
Ila wakat nafungua mlango nikapamiana na mtu, alikuwa amevaa kiatu cheusi kinachong’aa mfano wa mbalamwezi change, alikuwa amevaa suruali iliyonyooshwa vizuri na alikuwa anaonekana kama ni mrefu, alikuwa ananukia vizuri mno, sasa lile wenge langu nikajikuta nimeachia ndoo ya maji ya kudekia na maji yakamwagikia miguuni, nilishtuka sana maana nilijua lazima ndio atakuwa mkurugenzi mpya, ila niliponyanyua macho yangu, nikakutana na Stanley…..
Nilishtuka sana, nani kama hata yeye hakuamin kama anaeniona mbele yake ni mimi, akabaki kanishangaa kwa dakika kadhaa kisha akasema “husqer ……
“ Stanley!, na mimi nikamuita kwa sauti ya mshangao …
“ unafanya nini hapa? Akaniuliza….
“ nafanya usafi kwenye hii kampuni, na wewe unafanya nini hapa? Nikamuuliza…..
Akacheka kwa dharau kisha akasema “ mbona sasa maisha yako hayajabadilika, na kujiuza kote kule ulipokuwa unajiuza bado unaishi maisha magumu kuliko kawaida, mbona kujiuza kwako hakujakubadilishia maisha, sasa kulikuwa na haja gani ya kujiuza alafu bado ubaki maskin….
“ haikuhusu, haya ni maisha yangu, na sidhan kama yanamuhusu mtu yoyote Yule, nikajibu nikiwa nataka kuondoka…
Akacheka kwa dharau kisha akasema “ unajua kwanza unaongea na nani, yaan umenimwagia maji machafu, na badala ya kuniomba msamaha unanijibu kwa nyodo, mimi ndio mkurugenzi mpya wa kampuni, hivyo nasikitika kusema kuwa umefukuzwa kazi….
Nikama sikuwa nimemuelewa anachokisema, nafukuzwaje kazi kirahisi hivyo, nikamuangalia kisha nikasema ‘ hauwezi kunifukuza kazi, kwa sababu sio wewe ulioniajiri…
“ ni kweli sijakuajiri, ila hata huyo aliekuajiri mshahara wake unapitia kwangu, mwambie aje kukuombea msamaha nay eye akose kazi, maana naamin uliutumia mwili wako ili upate hii kazi, maana mwanamke haujiheshimu kabisa wewe, akawa analalamika Stanley…
Niliitafuta sana hii kazi, sikutaka anifukuze, basi nikapiga magoti kisha nikaanza kuomba msamaha na kusema “ naomba usinifukuze kazi, sina kazi nyingine ya kufanya zaidi yah ii, ila hata hakunisikiliza, na badala yake akamuita msaidizi wake ambae ndio kwanza alikuwa anaingia wakat huo, kuwa anatakiwa kuhakikisha kuwa sirudi kazin, na kama nikikataa kutoka wanitoe kwa nguvu………
Nikaona sitaki shida, nikawa natoka zangu nje tu, maana sikuwa na namna, nilishangaa ni kwanini ananifanyia vile, kwanini ananifukuza kama mnyama, ila nikawa najiambia kuwa mambo mengine nimejitakia mwenyewe, basi sitakiwi kumlaumu Stanley, maana huenda hata ningekuwa kwenye nafasi yake huenda hata ningekuwa zaidi ya alivyo yeye……
Basi nikaenda nyumban kinyonge, ila wakat nafika tu nyumban nakutana na dada yake Stanley, akaniita pemben maana nilikuwa na mama na kunambia kuwa hio siku ya kwenda kukutana na Stanley ndio siku hio, hivyo nijiandae, na kama tumepishana kauli atahakikisha kuwa Stanley ananisamehe na nakuwa wake milele…
Nilijisikia vizur sana, maana angalau hata dada yake bado analipigania penzi langu na Stanley…………….
NAKUJA………………
BIKRA TATA 4
HUSQER BALTAZAR
Siku moja dda yake stanley alinifata na kutaka niende kwenye hotel moja ambayo ndio ilikuwa imepangwa Stanley akakutane na mwanamke wake, ambae ametafutiwa, ila Stanley alienda hio sehemu akawa anakunywa tu pombe, alikunywa sana, kiasi kwamba mpaka mimi nafika namkuta hajitambui, akawa anataja jina langu tu, yaan husqer, ohhhhh husqer….
Nilijisikia vizur kiasi kwa maana hata kama ananionesha chuki kwenye macho yake ila angalau bado moyoni mwake sijatoka kabisa, nikampeleka chumban, akataka kulala na mimi, mila sikutaka, akawa kama ananiangalia vizur, kisha akasema “ nilijua tu kuwa na leo utakuja kuniuzia, mimi sina cha kununua, kwanza mimi sinunuagi Malaya, nilimuambia dada yangu anitafutie mwanamke bikra ananiletea wewe Malaya, sijui hata anafikiria nini huyu……
“ naomba upumzike Stanley maana umelewa sana, nikasema kwa sauti ya upole, akaniangalia kisha akaanza kucheka na kusema “ kuanzia lini umeanza kujali kuhusu mimi, embu nambie kuanzia lini umeanza kunijali wewe, yaan nilikuwa naenda kubeba zege alafu pesa zote nakupa wewe, nachimba mitaro, alafu pesa zote nakupa wewe, niakiamin wewe ndio mwanamke wangu, ila mwisho wa siku unakuja kwenda kuuza mwili ambao mimi nilikuwa nauthamini, unakuja kujiuza, ama kwelin mfadhili mbuzi, akawa analalamika ……………..
Alikuwa kalewa hivyo hata sikuona haja ya kubishana nae, maana nilikuwa na uhakika kuwa hatutaweza kuelewana…
Basi nilikaa pemben yake mpaka asubuh, nikawa nimepitiwa na usingizi, maana sio rahisi kukesha macho mpaka kunapopambazuka, nikiwa usingizin nikawa nahisi kama kuna mtu amenifunika shuka, ila nilikuwa na usingizi mkali hivyo hata sikushtuka……….
Nimekuja kushtuka muda umeshaenda sana, nilipofumbua macho nikamkuta Stanley ananiangalia, alipoona nimeamka ni kama akashtuka na kusema “ uliambiwa kuwa mimi nanunua Malaya?....
“ samahan jana ulikuwa umelewa sana, nikapigiwa simu ndio maana nikakuleta hapa, nikasema kwa kujitetea…
“ husqer …husqer, nilewe nisilewe wewe inakuhusu nini, embu nambie umeanza lini kujali, maana sijawah kujua kama umeshawah kuwaza kuhusu mimi hata siku moja za maisha yako, sasa inakuwaje leo ujifanye unajali sanaaa, naomba nisema tu hata kama ningekutwa mtaroni, sidhan kama nilitakiwa kushikwa na mikono michafu ya kahaba kama wewe, akasema Stanley kisha akataka kuondoka, ila kabla hajaondoka akasema “ unatakiwa kwanza wewe ndio uondoke maana chumba ni mimi ndio nimekilipia na sio wewe…
Sio siri nilijisikia vibaya sana, na kwa unyonge mno nikaanza kuondoka zangu maana sikuwa na namna, ila nilipogeuza macho yangu kumtazama stanley alikuwa ananiangalia kwa macho ya maumivu sana, kana kwamba anachokifanya kilikuwa kinamuumiza mno, ila ndio hivyo hakuwa na namna, nikaondoka zangu kinyonge na kwenda nyumban kwetu….
Maisha yangu yakazidi kuwa magumu, maana kazi ambayo ndio kidogo nilikuwa naitegemea imeshaharibika, nilikuwa ni mtu wa kulia, na kutaman sana walau Stanley angenisikiliza hata kidogo, maana huenda angenielewa ila ndio hivyo hata hataki kunisikiliza…..
Basi nilishakata tama kabisa na kuwa na Stanley, maana niliamin kuwa ananichukia mno, na kuamua kuanza kuendesha maisha yangu mimi mwenyewe tu, na nikajiambia kuwa sitakiwi kumuwaza tena, na wala kumfikiria, na kuhusu mahusiano basi nimpe nafasi mtu mwingine na sio yeye…..
Siku moja nilikuwa nipo nyumban, ghafla mama yangu akaanza kulegea, sijakaa sawa akapoteza fahamuy, nilishtuka maana namjua mama yangu kuwa ni mtu strong sana, ile hali ilinitisha sana, nikampeleka hospital, ila sikuwa na hata mia, so hata sikujua nikiambiwa pesa za matibabu nitatoa nini, nikaja kuambiwa mama yangu pressure na sukari yake ipo juu sana, so anatakiwa kulazwa na kwa siku kitanda ni elfu 20, nilihisi kuchanganyikiwa, maana kwa nwakat huo hata nauli ya kurudi nyumban sikuwa nayo, nikatoka nje ya iole hospital na kutafuta sehemu nikaanza kulia, nililia sana, maana sikujua kwanini kila siku maisha yangu ni magumu sana, kila siku maisha yangu ni yakuokoteza okoteza…
Nikiwa nimekaa mara akaja bint akanishika began a kuniuliza “ wewe ndio husqer, nikanyanyua uso wangu na kumtazama, kiukweli sikuwah kumuona kabla, na alinipokea kwa tabasamu mpaka kidogo nikahisi faraja kwenye moyo wangu na kujibu “ ndio ni mimi…
“ umeshalipiwa gharama zote za hospital, na kingine nimeambiwa nikupe hii pesa, akasema na kutoa kama elfu 50, nilishangaa maana sikuwa namjua kabisa, ila ukweli nilikuwa na shida mno, hivyo niliona kama malaika wa bahat amenishukia upande wangu…..
Basi mama alilazwa pale na kila kitu kilienda sawa, yaan kuanzia huduma za mama za hospital mpaka maisha yetu, maana Yule dada alikuwa anatimiza kila kitu ambacho tulikuwa tunahitaji wakat mama anaumwa, na nilipotaka kumuuliza yeye ni nani, alikuwa ananiambia kuwa aliguswa tu na matatzio yangu ndio maana alikuwa ananisaidia na mimi nikamuamin kabisa….
Basi maisha yakawa yanaenda na hatimae mama akapona kabisa, ila issue ikaja kuwa ni kutafuta kazi, yaan ni kama nilikuwa na gundu, maana kila nilipokuwa natafuta kazi sikuwa Napata, ila kilichokuwa kinanishangaza, wakat natoka kwenda kwenye mihangaiko Yule dada alikuwa anakuja nyumban kwetu na kuhakikisha kila kitu kinaenda vizuri…
Hakuwa anakuja kila wakat ila alikuwa anakuja mara nyingi sana, na maisha yetu hayakuwa magumu hata kama mimi na mama hatukuwa na kazi ya kufanya….
Basi bana siku moja dada yake Stanley alikuja nyumban kisha akataka kuzungumza na mimi, basi tukatoka nje na kwenda kwenye gari lake kwaajili ya kuzungumza, akaanza kunambia “ husqer mamaa wewe ndio wifi yangu ninae kutambua, naomba unambie mnashida gani na Stanley maana amekuwa mtu asie na raha, amekuwa na hasira kila wakat, na kila siku analalamika kuwa anataka mwanamke bikra na anataka sisi tumtafutie, na wakat kila mtu anajua kuwa yuko na wewe, nina uhakika kitu ambacho kimesababisha mkosane kitakuwa kinamuumiza sana kila siku, naomba unambie ni kitu gani….
“ samahan sana shanely, najua unampenda sana kaka yako na unataman sana kumsaidia, ila naomba umuulize mwenyewe maana hata mimi mwenyewe sijui sababu, nikajibu na wakat nilikuwa najua kila kila kitu, ila sasa ningemuambia je mpaka anielewe….
Basi akaniahidi kuwa atafanya kila kitu ili kuhakikisha mimi na na kaka yake tunakuwa na maelewano mazuri kama mwanzo, nikakubali, ila nilishakata tamaa na kuamin kuwa haiwezekan kabisa….
Basi siku moja shanel alinifata akanambia anataka niende kwao, akanipeleka saloon, nikapodolewa kisha akanitafutia nguo hizo, na baada ya hapo akanichukua mpaka nyumban kwao, maisha yapo yalikuwa yameshjabadilika maana Stanley alikuwa amejipata, akaniacha kwenye garden, nikawa nashangaa shangaa tu sina hili wala lile, nikawa natembea tembea, mara nikajikwaa wakat nikiwa nadondoka nikashangaa nimedakwa na niliposema niangalie, ndio nikakutana uso kwa uso na stanley….
NAKUJA…………….
BIKRA TATA 5
HUSQER BALTAZAR
Kwa namna ambavyo alikuwa ilikuwa ni wazi bado alikuwa anahisia na mimi, tukabaki tunaangaliana kwa muda kidogo, mpka tuliposikia sauti ya shannel akikohoa, na Stanley alivyo na makususi akaniachia nidondoke chini…..
“ kwanini unamfanyia mwenzio hivyo, shannel akaanza kulalamika, ila hata Stanley hakumjibu na akawa anaondoka zake tu, nilijisikia vibaya sana, maana ni kama Stanley alikuwa ananichukia sana, shannel aiona huzun machon kwangu, akaanza kunitia moyo, na nikawa natakiwa kuingia ndani, ila sikutaka nikawa naona kama nitazidi kupishana kauli na Stanley…
Shannel alipambana sana na kunishawashi niende ndani maana kuna jambo anataka nilishuhudie, basi nikaingia ndani watu wote, wakawa wananiangalia wakat nimeingia, ndio nikaja kugundua kuwa shannel alinivalisha vile makusudi, maana Stanley huwa anapenda sana rangi nyekundu na nyeupe, sasa wakat naingia nikiwa nimevaa hivyo, ni kama uzalendo ukamshinda Stanley maan kule nje hakunioa vizuri kutokana na rangi ya nguo nilovaa…
Alikuwa ananiangalia sana, akawa kama kaduwaa mpaka nikashangaa, basi niliingia na kutafuta sehemu na kukaa, na wakat wote macho ya Stanley yalikuwa kwnagu, sio siri macho yake yalikuwa yanaonesha kabisa hisia zake kwangu, alikuwa anaonekana ni kiasi gani alikuwa ananipenda sana ila ni kwamba alikuwa na hasira na mimi tu, na hakuwa anaweza kuzihimili hasira zake…
Basi siku hio ilikuwa ni birthday ya baba yake, wakafanya party pale ila mwisho wazaz wa Stanley wakaniita kwenye meza ya familia, maana kila mtu alikuwa anaziona juhudi za Stanley dhidi yangu kipindi chote tulichokuwa tunasoma, na sikuwa na sifa mbaya mtaa kabisa, maana kila mtu alikuwa anajua namna ambavyo nilikuwa nimetulia na sijawah kuonekana na mwanaume hata kwa bahat mbaya, na nilikuwa bint mwenye adabu sana kiasi kwamba wazaz wengi walikuwa wanataman vijana wao wanioe….
“ mwanagu Stanley, kila wakat unatuambia tukutafutie mwanamke, tunataman sana kukuona unaoa na sisi ni wazaz wako tunajua mtu sahihi zaidi kwako, na mwanamke ambae ulimchagua alikuwa ni mwanamke sahihi sana kwenye maisha yako, leo sisi kama wazaz wako tunaomba tuondoe tofauti zenu na kama kuoa basi umuoe huyu husqer maana anamaadili sana, akasema bababyake na Stanley kwa sauti ya utulivu na wakat huo wote nilikuwa naangalia chini, maana sikuwa najua kama hio familia ilikuwa inanikubali kwa kiasi chote hicho……
“ kama atakuwa bikra nitamuoa, akajibu Stanley kisha akanyanyuka na kuanza kuondoka….
“ umeanza lini kutokuwa na adabu, na kwanini unaongea maneno kama hayo mbele ya wazaz wako, ni lini umekosa heshima Stanley, akawa analalamika mamayake Stanley ila baba yake akamsogelea mkewe, alafu akamnong’oneza jambo kisha akataka kila aliekuwa pale aondoke na wakatuacha mimi na mama yake Stanley pekee yake…
Sasa watu wote walipoondoka Yule mama akanisogelea kisha akanambia “ wewe ni sawa na shannel wangu, embu naomba tuongee maongezi ya mama na bint yake, wewe na kijana wangu Stanley mna tatizo gani, nambie mimi na mimi kama mtu mzima nitatafuta namna ya kusuluhisha tatizo lenu, maana kijana wangu anaonekana ana hasira sana na wewe, ila kila mtu anajua ni kiasi gani anakupenda, na kweli tungeweza kumshawishi hata awe na mwanamke mwingine, ila hawez maana bado mawazo yake yapo kwako……..
“ mama hata mimi sijui, kama hautajal naomba umuite Stanley hapa tuzungumze nijue nimemkosea nini, nikaanza kujitetea…
Mama yake Stanley akanambia kuwa anataka niende nae chumban kwa Stanley, na mimi sikuwa na hiyana nikakubali, hao tukaenda….
NAKUJA….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote