SIKUTEGEMEA KAMA INGEKUWA HIVI 🥹🥹🥹
Nilikuwa ni binti wa kiislam ambae nililelewa kwenye maadili na zinaa kwangu ilikuwa kosa kubwa sana..
Rafiki yangu kipenzi soso anaumwa sana baada ya kutoa ujauzito, na kuanza kubadilika rangi, ili apone inatakiwa laki tano na mfukoni nilikiwa na pesa ya ada ikabidi nimlipie maana niliamin afya ya soso ni muhimu zaidi ila bahati haikuwa upande wangu soso alifariki 😭😭😭
Nilihisi kuchanganyikiwa maana kafariki na pesa yangu ya ada nimeitoa, nilikiwa na uchungu mara mbili, nikiwa natafuta msaada nikashangaa mtu ananipa pesa kisha akanambia kama nitahitaji nyingine nimtafute, sikutegemea na kidogo nikapata auheni, baada ya kulipa ada napigiwa simu baba yangu kapata ajali na mama akawa anaomba kama sijalipa ada nimtumie pesa baba yangu atibiwe...
Nilichoka na kuamua kumtafuta yule alienipa namba, na kinambia kazi natakiwa kulala na boss wake...
Sikuwa na namna nikalala nae, hapo jamii nzima inajua mm ni bikra kutokana na tabia zangu na sijawah kuonekana na mwanaume, na mwisho wa siku najigundua nimjamzito...
Yule mwnauame baada ya kujua kuwa nina ujauzito akaamua kuishi na mimi, ila upole na ukarimu wangu akanipenda hali ya kuwa mimi nilijua kuwa nipo kwake kwa sababu ya mtoto tu na sio kingine
Usikose simulizi hii ya kusisimua ya bikra mjamzito
BIKRA MJAMZITO 1
HUSQER BALTAZAR
Siku moja nilikuwa nimetoka chuo, nilikuwa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Dodoma ambapo nilikuwa nachukua shahada ya sheria katika college ya humaties, nilikuwa mjini siku hio nilienda kwa rafiki yangu mmoja alikuwa anaishi area d dodoma, alikuwa anaumwa hivyo hakuja chuo kwa siku kadhaa nikaona nikamsalimie, alikuwa dhaifu sana, kwa maana alikuwa ametoa ujauzito na huwaga ni yatima, hivyo aliitoa kiholela na ikawa inamletea madhara makubwa sana maana alikuwa anapoteza damu nyingi sana, na hadi mwili wake ukaanza kubadilika rangi….
Niliogopa sana maana nilijua kwa hali aliokuwa nayo ni lazima angekufa, nikamchukua na kumpeleka hospital, walikataa kumpokea, ikabidi nionge, maana nilikuwa na elfu thelathin kwenye pochi kwaajili ya kununua begi la kuwekea laptop yangu…
Ingawa ni kwa tabu sana ila walimpokea na kuanza kumsafisha, na bill ikaja laki tano na nusu…
Nilihisi kupagawa, nikawa nawaza pakupata hizo pesa maana sikuwa na kazi zaidi ya kutegemea boom, na boom lenyewe hata sikuwa napewa asilimia mia, kwa maana serikali ilikuwa inanipa mkopo wa kujikimu na kunilipia asilimia 30 tu, hizo sabini nilikuwa napambana na familia yangu………
Nikiwa natafakari pa kupata hizo hela, mwisho nikapata wazo la kuchukua pesa yangu ya ada, bila kuchelewa nilienda kwenye atm nikaitoa ile pesa na kupeleka kwaajili ya matibabu ya shoga yangu, maana ndio alikuwa rafiki yangu wa damu kabisa, na hali halisi ya maisha ya nyumban kwao nilikuwa naijua vizuri sana…..
Basi nikamlipia pesa yote ambayo ilikuwa ni laki tano na elfu tisini na mbili, na kweli alipatiwa matibabu na nikaambiwa niondoke nitarudi kesho yake kuangalia hali yake, kweli nikaondoka zangu, nikijua shoga yangu anaendelea vizuri, ila siku hio sikuwa na amani kabisa yaan…
Asubuh naenda hospital nikakuta shoga yangu ameshafariki, yaan nimetoa pesa yangu ya ada nikijua akipona tutahangaika wote kuipata alafu mwisho wa siku amefariki…
Nilihisi kuchanganyikiwa, sikujua la kufanya, nilikuwa naongea mwenyewe kama mwehu, na sijui hata nitawaambia nini wazaz wangu wakijua kuwa sijalipa ada na pesa sina, na maisha ya nyumban kwetu sio mazuri kabisa, kwa maana mama yangu anauza sokoni lile soko la kilombero arusha na anauza matango tu, na baba yangu ni winga tu wa kawaida, na najua ugumu walioupata kupata hio pesa yangu ya ada…
Nilipagawa mno, na sikuwa namjua ndugu hata mmoja wa rafiki yangu soso hivyo akazikwa na manispaa…
Nilihisi kama maisha yangu yamesimama vile, siku moja nikiwa natembea hapo najaribu kutafiuta ata mtu wa kumkopa ili angalau anisaidie kulipa pesa nitamrudishia taratibu, mara likapita gari moja kali pemben yangu…
Sikulijali, na nikasimama pemben ya hilo gari na kuanza kusema “ nilishakuambia kila kitu wewe, maana nilitoa pesa yangu n yote kwaajili ya matibabu ya soso, sasa unafikiria pesa nyingine naitoa wapi? Na wazaz wangu unayajua maisha yao vizuri, naomba nisaidie walau laki mbili na nusu nitakulipa chochote unachokitaka tafadhali….
Huyo niliekuwa naongea nae alikuwa ni binamu yangu wa kiume, nimeshamsaidia mambo mengi, na alikuwa ameshapata kazi, hivyo niliamin hawez kushindwa kunisaidia, ila akanambia mpaka anikule maana amenipenda kwa muda mrefu sana, na kwa shida hizi nikakubali kisha nikakaa chini na kuanza kulia, kisha nikawa nasema “ siamin kama nautoa usichana wangu kwaajili ya laki mbili mwasity mimi, siamin kabisa…
Nikiwa nalia mara nikahisi mtu mbele yangu, maana nilikuwa nimechuchumaa huku nimeweka uso wangu kwenye mapaja yangu, ikabidi niinue macho kumtazama mtu ambae amesimama mbele yangu, alikuwa ni kijana mrefu na aliekuwa amevalia nguo nyeusi zote, akatoa kibunda cha hela kisha akanikabidhi, na baada ya hapo akanipa business card na kusema “ ukitaka pesa nyingine nyingi zaidi unaweza kutupigia kwa namba ambazo zipo kwenye hio card kisha akaondoka zake….
Kiukweli sikuamin kama nimepata pesa, nilioshindwa kuzikataa maana siwez kukataa pesa na wakatri nilkuwa na mahitaji makubwa mno ya pesa, nilitafuta sehemu nikakaa na kuanza kuzihesabu…
Ilikuwa ni laki tano kamili, nilishangaa sana ni binaadamu gani ambae anaweza kumpa mwanamke asiemjua kiasi chote cha pesa kama hicho kisha aondoke zake, ila nikajiambia huenda mungu anataka kunirahisishia maisha na huenda amesikia kilio changu….
Bila kupoteza muda nikaenda kulipa ada, maana ndio kitu cha msingi kilichokuwa kinanifanya niombe ombe hela kama omba omba…
Basi hpo nikawa na amani na masomo yangu yakawa yanaendelea kama kawaida, siku moja nikiwa chumban kwangu najisomea, mara simu yangu ikaanza kuita, na nilipopokea alikuwa ni mama yangu akiwa analia…
“ mama kuna shida gani? Ikabidi niulize…
“ baba yako kapata ajali ya pikipiki, na anatakiwa laki nne na nusu ili afanyiwe upasuaji, mwanangu kama haujatumia ile pesa yako ya ada naomba tumsaidie baba yako, maana tutatafuta pamoja, nilihisi kuchoka, na mama kweli alinitumia picha za baba yangu alikuwa na hali mbaya, nikaanza kulia sana, mwisho ndio nikakumbuka kuwa nina namba za Yule mtu siku ile ambae alinipa pesa za ada, nikawa najiambia kuwa huenda akanisaidia tena, hivyo nikatafuta ile busness kadi kisha nikapiga….
Smu iliita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa, na aliepokea sikuwa namfahamu maana sauti yake ilikuwa ni ngeni sana maskion mwangu, kwa sauti ya kilevi akasema “ haloo unataka nini…
“ samahan, mimi ni yule dada ambae unilisaidia ukanipa pesa za ada, nilikuwa nina shida ya pesa kidogo nikasema kwa sauti ya kujiamini kidogo maana hakikuwa kitu kirahisi kabisa kwangu….
Akacheka kisha akasema “wewe binti bikra, embu njoo apa elite club nikupe hela mimi napendaga ukiniomba, ilikuwa bado ni sauti ya kilevi…
Sikuwa na namna nikaanza kujiandaa wakati huo huo na kwenda hio sehemu ambayo alitaka niende, nilifika nkakuta ni zile club za matajiri, maana licha ya kuwa ni club ilan kulikuwa na utulivu wa hali ya juu, na nyimbo ambazo zilikuwa zikipigwa ni zile nyimbon za pole pole….
Nilipofika nikaanza kushangaa, nikashangaa nakuja kupokelewa na yule kijana ambae alinipa pesa ile siku, kisha akasema “ boss yuko huku, na kuanza kuongozana nae…..
Nikashangaa napelekwa chumban, ambapo nikapimwa afya na baada ya hapo kwanza nikapewa pesa, siku hio nilipewa pesa nyingi sana, kisha Yule boss ambae wakati huo alikuwa amelewa akaja nay eye chumban…
Aliponiona akaanza kucheka kisha akasema “ bikra huyo amekuja, ohhh maskin mimi siweza hata kukapa mimba katoto kazuri kama haka, yaan mimi ni useless…..
Nikashangaa anaenda bafuni kuoga, sikujua kuwa mtu akijimwagia maji pombe zinaisha,maana baada ya kuingia bafuni sauti yake ilibadilikan kabisa, akaniita niende kuoga nae, na kwa uoga mkubwa sana nikaenda huku nikiwa natetemeka mno…
Nilifika bafuni hapo nina wasiwasi sio utani, nikamkuta akiwa hana nguo yoyoteb ile na akaniuliza, ‘ unaitwa nani..
“ mwacity nikamjibu kwa uoga…
Ata sikuoga nae, akanibeba akiwa hana nguo na kwenda kunitupa kitandani kisha akaanza harakati za kulala na mimi….
Na aliponikuta bikra akasema kuwa hatonitoa ila nilikuwa nimeshaanza kusikia maumivu akamwaga na mavit
u yake ndani, nilikuwa nasikia kinyaa mno, ila akaniangalia na kusema “ usijali kwanza sijakutoa bikra yako na kingine mimi sina uwezo wa kumbebesha mimba mwanamke……
NAKUJA……..
BIKRA MJAMZITO 2
HUSQER BALTAZAR
“ kama utakuwa na shida yoyote ile naomba usisite kunambia, maana una adabu sana binti, akasema Yule mwanaume kisha akaniambia yeye anaitwa ashraf, na kuvaa kisha akaondoka zake…
Nikaaanza kusikia maumivu, nikajua labda ni kwa sababu ya uoga wangu, ni kweli sikutoka damu na ninavyojua bikra huwa wanatroka damu nikajua labda ni kawaida, nikaingia bafuni nikaoga kisha nikalala hapo apo, maana sikuwa naweza kurudi chuo na wakati ilikuwa ni usiku sana…
Nikalala na asubuh nikavaa zangu na kwenda chuo, mashoga zangu na roommate wangu walishangaa sana kuniona sijalala chuoni, kila mtu alikuwa anajua kuwa mimi sijawah kuwa na mwanaume hivyo kitendo cha kutokulala chuo kilimshtua kila mtu, ila hawakuhoji sana maana niliwaambia kuna ndugu yangu nilienda kukutana nae, ni dada yangu hivyo nililala nae kwenye lodge aliolala maana huku Dodoma alikuwa mgeni….
Basi wakanielewa na maisha yangu yakawa yanaendelea kama kawaida, na nikatuma pesa ya matibabu nyumban,na kumuambia mama kuwa mkopo wangu umeongezwa na nimeshalipiwa ada na serikali hivyo asiwe na wasiwasi sana, mama alinielewa na kuniombea dua kuwa nifaulu mitiani yangu na niishi vizuri….
Basi bana maisha yakawa yanaendelea na yule ashrafu ambae nililala nae sijawah kumtafuta na wala yeye hajawah kunitafuta hata kwa bahati mbaya, ila mwezi wa kwanza ukapita sijaona siku zangu…
Niliona ni kawaida maana mara kadhaa huwa unapita mwezi mmoja au miwili bila sijaona siku zangu, hivyo sikuwa na mashaka, maana niliamin kuwa sijatolewa bikra na niliamin kuwa Yule mwanaume hawez kuzalisha….
Basi maisha yakawa yanaendelea ila nikashangaa sipendi kusikia harufu za manukato yoyote yale, yaan kila manukato ninayoyasikia nilikua nahisi yananuka vibaya sana, ila sikuwa nasema maana kikawaida mimi sio muongeaji sana, ila nilikuwa najitenga na mtu yoyote anaetumia manukato yoyote yale, mwezi wa pili ukapita sjaona siku zangu, bado sikuwa na wasiwasi kabisa, ila nikaanza kuwa na usingizi sio mchezo…
Yaan nilikuwa naweza nikalala mpaka ukanishangaa, yaan na nikilala sisikii hata kama mtu akiniita vip, na wakati mwanzo hata mtu akitembea kwa kunyata nilikuwa nasikia sauti ya nayo zake, ila ghafla ikawa hata mtu afungulie disko pemben yangu basi sisikii chote kile…
Bado niliona ni hali ya kawaida sana maana sikuwa mzoefu na mimba, sasa siku moja tulienda kule ngo’ng’ona, tulienda kula chakula na shoga zangu, sasa Yule mama ambae alikuwa anatuhudumia akasema “ ila mabnt wa chuo sijui ni kwanini huwa wanawah kubeba mimba na wakati hawajamaliza masomo yao, ila mabint wa chuo kwa tamaa sio mchezo…
Wote tuliokuwa pale tulisikia hayo maneno, tukajua wale wa mama wanaongea zao tu, maana hata mimi mwenyewe sikuwa najua kuwa nina mimba, Simulizi hii inapatikana kwenye link ya tupo hapa pekee, epuka matapeli, maana haiuzwi kawaida,basi wakati natoka mama mmoja akanifata na kunambia “ usijal mwanangu, hio mimba yako isikusababishe ukate ndoto zako, soma kwa bidiii kwaajilib yako na mwanao, ila wakati anaongea alikuwa anaongea na mimi pekee yangu, sio siri nilishtuka sana, maana kama ni mimba mimba ipi sasa, maana niliamin kuwa sina mimba…
Nilihisi kuchanganyikiwa, pale pale ng’ong’ona nikatafuta duka la dawa kisha nikanunua kipimo ca mimba na nilipofika chuoni kitu cha kwanza ni kupima mimba, nikakuta imo…
Nilihisi kucanganyikiwa, nilitaman kupiga kelele, nikaanza kuwaza halinyetu nyumban, yaan kwa namna ambavyo wazaz wangu wananiamin na kwa namna ambavyo wanajua kuwa nimetulia, na sio wazaz wangu tu hata ndugu jamaa na marafiki na mtu yoyote Yule ambae ananijua ukimwambia kuwa mimi n muhuni atakushangaa mpaka mwisho.….
Nilikuwa naogopa kumtafuta asharafu maana nilihisi ameshanilipa hivyo sina cha kumlipa, nikawa nawaza kuhusu kutoa mimba maana bado ilikuwa ndogo ila nilikuwa naogopa sana kutoa mimba, nikawa naogopa mno hata mtu akijua kuwa nina mimba itakuwaje….
Basi bidii yangu ya masomo ikazidi, nikaanza kutafuta biashara ya kufanya kwaajili yangu na mwanangu, maana nilijua sina wa kumlea, basi nikaanza kuunza manukato na viatu chuoni, na kwakuwa nilikuwan navaa sana nguo za stara hivyo haikuwa rahisi kugundulika, kama ni mjamzito….
Maisha yangu yalikuwa yabidii kubwa na kutokukata tamaa, niliamin kuwa nikiwa na pesa basi mwanangu ataishi vizuri nja huenda hata akakubalika na jamii yangu, nilikuwa naenda clinic kwa siri maana nikajikuta nampenda tu mwanangu bila kujua hata nitaishije nae…
Siku moja nlikuwa nimenda kuchukua mzigo, huwa kuna mtu ambae ananitumia kutoka dar, sasa nikaingia kwenye mgahawa mmoja na kuagiza kinywaji, sasa wakati nakunywa taratibu nikamuona mtu kama mlinz wa ashraf, nikataka kwenda kumfata, ila kabla sijamfikia nikajikuta napatwa na kizungu zungu kama mnavyojua mimba na nikadondoka chini…
Nimekuja kushtuka nipo hospital nilishangaa kidogo, nikajua labda wasamaria wema wamenisaidia kufika pale, ila nakuja kuona kuwa nipo kwenye hospital ya gharama sana, ila sikutaka kuhoji sana, mara akaja nurse na kuniuliza naendelea je…
‘ nipo salama , nikajibu kwa sauti ya utii na unyenyekevu mkubwa sana, kisha nikasema ‘ nani kanileta hapa…
‘ usijali utamjua tu ila kikubwa ni usalama wako wewe na mtoto, akasema hivyo ikabidi nitulie, si ndio nikaja kuona simu yangu nimepigiwa mara kadhaa na kondakta, nikampigia akaniambia ameacha mzigo wangu ofisin kwao, nikataka kuondoka, ila nikazuiliwa, sikutaka kulala tena nje ya chuo, ila wakati natoka nikamkuta Yule kaka mwenye suti nyeusi, aliponiona akasema ‘ tulia ulale boss yupo kwenye ndege anakuja kukuona….
Nilishangaa sana anakuja kuniona kwa sababu gani, akaniambia kuwa nisitoke na wala nisiwaze kutoka, maana popote nitakapoenda watanipata…
Nikaanza kuogopa sana, ila nikasema nitulie, siku hio nililala hospital, ila walikuwa wananiangalia vizuri sana utasema tajiri flani hivi, basi asubuh na mapema ashrafu alifika pale hospital….
“ nimesikia una mimba, siamin kama ni mimba yangu, maana nyie watoto wa chuo huwa mnamambo mengi sana, akasema asarafu tena hata kunisalimia hakunisalimia…
‘ sawa kama sio wako, sasa mliniweka hapan hospital kwaajili gani naomba niondoke zangu, nikasema kwa sauti ya upole…
“ unataka kuondoka kwa sababu nakuambia ukweli, mimi siku ile sikukutoa bikra na wanawake wote ambao nimeshawah kutembea nao awajawah kubeba mimba hata kwa bahati mbaya, akasema asharafu…
“ labda nikuambie tu ukweli, na maamuzi yatabaki kwako, kuanzia nimezaliwa sijawah kuwa na mahusiano hata mara moja, na wewe ndio mwanaume wa kwanza kunifanyie vile na wa mwisho, sasa nimeshakuambia ukweli naomba niende zangu chuo, akaniangalia kisha akasema subiri naomba usiondoke…
Kumbe akaenda kupima kama anauwezo wa kubebesha mwanamke mimba au laa, na baada kama ya masaa mawili akarudi kisha akanipiga busu kwenye paji la uso na kusema “ asante sana kwa kuniheshimisha mwasity mamaa, nakuahidi nitakutunza wewe pamoja na mwanangu,maana huyu ni mtoto wangu, nataka nikupeleke chuo….
‘ hapana nataka kwanza nifate mzigo wangu kwenye magari ya shabibi, nikasema, akashika simu yake na kupiga simu kwa mtu kisha akaniuliza kuhusu taarifa za mzigo kisha akasema nitaukuta chuo, kisha akanipeleka kwenye gari lake na safari ya kurudi chuo ikaanza….
Nilikuwa naona aibu sana, maana nilijua lazima mtu yoyote Yule anaenijua atajiuliza ni kwanini nimetoka kwenye gari, na sio gari la kawaida, lilikuwa ni gari kali mno, ila ni kama alijua hivyo akaanza kunitoa hofu…
Tumefika chuo akashuka na kunifungulia mlango nishuke, kwa aibu nikashuka kisha akanambia “ nikupeleke mpaka chumban kwako au niishie hapa hapa…
‘ nashkuru sana kwa kila kitu, unaweza kwenda sasa, nikasema na ashrafu akasema “ sitaki tena ufanye hizo biashara zako maana unamtesa mwanangu, kisha akatoa kadi ya nmb na kunambia namba ya siri ni 2324, unaweza kutoa kiasi chochote cha pesa unachokitaka, kisha akapanda kwenye gari na kuondoka zake….
NAKUJA…..
BIKRA MJAMZITO 3
HUSQER BALTAZAR
Nilikuw najisikian vizuri sana, nikaona angalau kilio change mungu kakisikia, na kama ataniangalia mimi na mwanangu huwenda nisipate shida sana ata kwenye masomo yangu, basi kumbe wambea wameniona nashuka kwenye range, ile nafika room nakutana na watu wananisubiri kwa hamu…
“ eheee tuambie mbona jana haujaja chuo, alafu tunashangaa anakuja mtu kama jambazi analeta mzigo wako badala yako, hatujakaa sawa tunashangaa unaletwa na gari kali kwema kweli, au ndio umepata mwanaume mwenye hela shoga yetu ndio maana haukuwa unamtaka haji kwa sababu kapuku, akasema mmoja wa mashoga zangu…
“ amna ni boss wangu kuna kazi nafanya, nikasema kama vile nataka kujitetea flani hivi…
“ ni kazi gani hio utupe na sisi michongo, maana huenda na sisi tukaletwa chuoni na magari makali, akasema shoga yangu mwingine…
“ amna mambo hayapo kama mnavyofikiria kabisa, hivyo achana na hizo hadithi maana nimechoka, nikasema kisha nikapitiliza zangu kitandani kulala…
Kila mtu akawa ananishangaa na minong’ono ikaanza, kuna ambao wakawa wanasema kuwa hawa watu wapole ni wabaya unaweza shangaa ana mimba tu na wakati haujawah kumuona na mtu, kuna ambao walikuwa wananiamin hivyo walikuwa wananitetea kwa sababu wananijua hivyo wanaamin kuwa nilikuwa bado ni bikra na wakati nilikuwa na mimba ya miezi sita wakati huo, ila mungu alinijalia sikuwa na tumbo kubwa, kwa maana hata nikivaa nguo ya kawaida, ni ngumu sana kugundua kuwa nina mimba…
Basi maisha yakawa yanaendelea, na asharafu akawa anakuja chuoni kunijulia hali, kuna muda nilikua naona aibu, nikawa namuomba avae kawaida na asiwe anakuja na gari lake, ikiwezekana atumie daladala kwaajili ya mwanae, maana nilichoka kuona watu wananiongelea…
Siku moja nikiwa zangu darasan, nilikuwa najisomea, maana ndio kwanza nilikuwa mwaka wa kwanza, hvyo nilikua na safari ndefu bado, wakati nasoma wakaja wadada watatu, kila mtu pale chuoni alikuwa anajua ni wadagaji, maana hata kusoma hawasomi, wala hutakaa utawaona darasani, yaan kila siku unawaona viwanja tu, siku hio wakanifata na mmoja akawa kama anaangalia simu yake kisha akasema “ ni yeye bana wala haukumfananisha, haya sasa maustadhati wanaingia club…
Nilishangaa maana sikuelewa walikuwa wanaongea nini, mmoja aknifata kisha akanambia “ kama unataka siri yako ibaki kuwa siri hakikisha unamuacha boss, maana siku hizi hatuhongi tena kwa sababu yako, hivyo kizuri kula na nduguyo bana…
Kiukweli sikumuelewa na wala sikuwa najua alikuwa anamzungumzia boss yupi, ndio mmoja akanionesha simu yake, ilikuwa ndio ile siku ya kwanza naenda kuonana na ashrafu, nilikuwa muoga sana, maana nilikuwa ni mtu ambae naheshimika sana pale chuoni hasa hasa kwa mavazi yangu na namna ambavyo nilikuwa na tabia njema, sasa katika kuparangana ndio mmoja akashtuka kisha akasema “ kumbe kana mimba ndio maana…
Nilistuka sana baada ya kusikia hivyo,maana sikuwa najua kama kuna mtu ambae anaweza kunitazama tu na akagundua kuwa nilikuwa ni mjamzito, akaanza kucheka sana kisha akasema njoeni mumuone bikra wenu mjamzito…
NAKUJA….
BIKRA MJAMZITO 4
HUSQER BALTAZAR
Zile kelele zao zilianza kukusanya umakin wa watu uliokuwa pale, watu wakaanza kusogea ili kujua kuna nini kinaendelea, ndio mwingine akaropoka na kusema “ kumbe ni mjamzito, hatimae bikra yaw a chuo kabeba mimba sisi makurubembe hatujawah kushika hata kwa bahati mbaya…
Ndio watu wakaanza kushangaa, watu wengine wakawa hawaamin, wakaja wakanishika kwa nguvu na kuanza kuniangalia tumbo langu, wakabana nguo yangu ili kuthibitishia watu kuwa nilikuwa ni mjamzito, na mungu sio athumani mtoto akacheza watu wakaanza kushangaa, wengine wakaanza kucheka na wengine wakaanza kunong’ona, mara akaja roommate wangu akanishika mkono kisha akasema “ yaan naona kuna watu wananong’ona na kuna watu wanajifanya kushangaa ila asilimia kubwa ya sisi tuna wanaume wetu na tunalala nao kila siku, na kuna wengi tu wametoa mimba, mnashangaa sijui kitu gani, hakikisha kama unamuhukumu mwasit akikisha hauna dhambi hata moja, kuna watu walevi, asilimia kubwa ni wazinzi, kuna ambao ni wasengenyaji, wengine hata ni wauwaji au hata hawana adabu, sasa kazi kuhukumu makosa ya wenzenu na wakati una makosa kibao, mwasity twende, na nione mtu anakusema vibaya nitaakikisha napambana nae, akanishika mkono kisha tukaanza kuondoka….
Nilikuwa najizuia kulia, ila tulipotoka tu nikaanza kulia, nililia sana na yule roommate akawa pemben yangu ananisikilia, alikuwa anaitwa camila, akaanza kuniuliza ilikuwaje mpaka nikalala na yule mwanaume, msikuona haja ya kumfich, nikamsimulia kila kitu kuanzia kufa kwa jojo ambapo nilitumia ada yangu, kuumwa kwa baba yangu na namna ambavyo nilikutana na ashrafu…
Alinionea huruma sana na kusema “ najua wewe ni mwanamke mwenye heshima sana, najua wewe ni mwanamke mwenye nguvu sana, najua hili sio jaribu kwako ila ni njia ya mafanikio yako, najua mama yako akijua kuwa umetumia mwili wako kwaajili ya afya ya baba yako, atajisikia vibaya sana, ila usijali kama mwanaume anakujali basi hauna haja ya kukata tamaa na kuwa mnyonge na uwe na nguvu ya kupambana na kila ambae anapambana na wewe…
Kidogo nilijisikia vizuri, ila maneno yakaanza, kuna ambao walikuwa wanataka kujua ilikuwaje mpaka nika beba ujauzito ila sikutaka kuongea tena, na maisha yangu yakawa yanaendelea…
Unyonge wangu ulizidi sana, mpaka siku moja ashrafu alikuja shule, siku hio alikuja na gari lake la kawaida tu, nikashangaa wale wadada watatu wameenda mpaka kwenye gari lake na kuanza kujisebedua, sasa nilivyoona vile nikawa nataka kuondoka zangu, sasa ile nageuka tu nyuma nikashangaa napamiana na kijana na wakati huo huo alinikiss bila mimi kutegemea, kisha akasema “ ohhh mwasity mtoto wangu anaendelea je, nikabaki nimetoa macho maana sikuwa najua hata anaongea nini…
Ashrafu alikuja na kunishika mkono kisha kwa hasira akaniuliza “ uyu kijana ni nani..
Wale dada wakadakia kuwa “ ndio babydady wake huyo sasa wewe pumbazwa na wakati kamwanamke kenyewe kanajiufanya bikra kumbe kanagawa mpaka basi…
Ashrafu hakutaka hata kumsikiliza akanipandisha kwenye gari, apo kanuna balaa, nikashangaa kwa mara ya kwanza ananipeleka mpaka nyumban kwake ilikuwa huku area A, NAJUA NI MTAA wa kawaida ila kulikuwa na nyumba moja kali sana…
Tukangia ndani na kitendo cha kufika ndani akaniambia kuwa “ kuanzia leo utaanza kuishi hapa ndani na sio kule chuo naona unataka kuniharibia mwanangu, au kama sio mwanangu niambie mapema niache kugharamika ….
“ usitake kunambia umeyaamini maneno ya Yule kijana ambae hata mimi sikuwa namfahamu? Nikamuuliza..
Akaniangalia kwa sekunde kadhaa kisha akasem ‘ kuwa makin na mwanangu usije ukamuharibu kwa ujinga wako kisha akaondoka zake….
NAKUJA………….
BIKRA MJAMZITO 5
HUSQER BALTAZAR
Sasa nikawa nimekaa pale ukumbin sijui hata nielekee wapi, mara akaja binti wa kama miakan 25 akaniambia “ samahan sana madam naomba nikupeleke chumban kwako…
Sikuwa namuelewa akiseme neon madam, maana najuaga madam anaitwaga mtu mwenye mamlaka flan, sasa huko chumban kwangu ndio wapi, nikawa najiuliza , kwa maana sijawah kufika hapo, ila nikahisi ni maagizo amepewa labda na boss wake, basi nikaanza kuongozana nae….
Alinipeleka kwenye chumba kimoja kizuri kama hoteli, yaan hata mimi sikutegemea kabisa kama anaweza kuna nyumba nzuri vile na watu wanaishi…
“ bafuni kuna maji ya moto nay a baridi, utataka nikuandalie supu au mtori, au nikuletee juice, akasema huyo dada kwa heshima mpaka nikawa nashangaa…
“ juice inatosha, nikajibu kisha Yule dada akaondoka zake…
Kwa kweli nilikuwa nasikia joto mno, nikaingia bafuni sasa sikuwa najua ni sehemu gani ndio ya maji ya moto na nisehemu gani ndio ya maji ya baridi, nikaingia zangu bafuni ile nawasha tu kumbe nimewasha maji ya moto, nyie niliungua mpaka nikaanza kupiga kelele, niliungua sana mgongoni, sasa sijui kuna mtu aliweka maji ya moto, au mimi ndio sielewi nyumba za watu…
Nikashangaa asharafu amekuja hapo nimevaa gauni ila naugulia maumivu…
“ vipi wewe ? akaniuliza…
“ yaan matajiri mnamakusudi sana yaan mnamuwekea mgeni maji ya moto, ona sasa yameniunguza mgongo, nikasema kwa sauti ya kulalamika…
Ashrafu aaagizwa yaletwe mafuta na baada ya muda mfupi yakaletwa, nilidhani labda nitajipaka mwenyerwe ila nikashangaa anataka kunipaka..
‘ boss vipi mbona unataka kunipaka mafuta tena…
“ umeungua mgongoni, siwez kukuacha ukajipaka mwenyewe na wakati najua hautaweza, na nafanya hivi kwa ajili ya mtoto, hivyo akanitaka nilale ubavu…
Kiukweli nilikuwan namuonea aibu sana, ila akawa ananiambia kuwa sitakiwi kuwa na aibu tena, kwa maana hakuna sehemu ya mwili wangu asiyo ifahamu, ikabidi nitulie, nikafungua gauni la nguo yangu kisha akaanza kunipaka mafuta mgongoni taratibu..
Kwa namna ambayo alikuwa anapitisha mikono yake kwenye mwili wangu, nikajikuta Napata msisimko wa ajabu ila nikajikaza, akanipa mwisho nikashangaa ananikiss kwenye uti wa mgongo, sio siri nilishtuka sana, ila nikajizuia na kujiambia kuwa anafanya hivi kwaajili ya mwanae, na huenda hata lile busu alilonibusu ni kwaajili ya mwanae na sio mimi hivyo nisiwe na mawazo ya kijinga…
Alipomaliza akaniinua kisha akasema “ nimefanya hivyo kwaajili ya mtoto na sio wewe kisha akaondoka zake…
Nilijisikia vizuri sana kwa huduma ambayo alikuwa ananifanyia, ila aliponiambia kuwa alikuwa anafaya kila kitu kwajili ya mwanae na sio kwaajili yangu nikajisikia vibaya, sijui ni kwanini nilipatwa na wivu, na vile sijawah kupenda hata sikuwa najua wivu ni nini, siku hio nililala hapo…
Kesho yake nikahisi nashikwa mkono nilishtuka sana, nilipofungua macho nikakutana na sura ya ashrafu ikiwa na tabasamu mwanana sana…
“ umemkaje wewe pamoja na mwanangu…
“ salama boss nikasema ..
“ nimekuletea sup8u, hii supu nimeiandaa mwenyewe kwaajili ya mtoto, akasema kisha akawa anataka kuanza kuninywesha…
Yaan aliponiwekea ijiko kimoja mdomoni nikaanza kusikia kicefu chefu vibaya sana, nikakimbilia bafuni, aiseee nilitapika mpaka nikaishiwa nguvu…
“ samahan mwasity sikuwa najua kama haupendi supu, akasema kwa sauti ya upole, kisha akasema ‘ mtoto wetu anataka kula nini sasa….
Nakuja…
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote