(ARIANNA) I WILL NEVER LOSE YOU

book cover og

Utangulizi

Ford noble ni kijana anaetokea kwenye familia ya kitajiri baba yake ni mmiliki wa makampuni mbalimbali na mama yake ni daktari huko nchini marekani , kutokana na malezi aliyopewa na baba yake ford alikuwa ni mtu wa starehe sana na kusababisha kufeli kwenye mitihani yake , baada ya mama yake kurudi Tanzania aliamua kurekebisha tabia ya kijana wake kwa kumpeleka shule ya kijijini huko alikutana na msichana Ariana aliyekuwa akijua yupo shule kutafuta elimu na sio kucheza ,nyota ya ford na Ariana ni kama hazikuendana ford alikuwa anapenda sana kumchokoza Ariana haikupita siku bila hao wawili kugombana Ariana alianza kumchukia ford. Hatimae chuki ikazaa upendo kwa Ford taratibu alianza kumpenda Ariana na kuanza kumjali flani lakini Ariana hakutaka mazoea. walifanikiwa kumaliza kidato Cha nne bila ya ford kuweka wazi hisia zake kwa Ariana ,baada ya miaka nane kipita Ariana na ford walikutana Tena lakini Ariana aliishia kumdhalilisha ford mbele za watu , baada ya kutafuta kazi kwa muda mrefu Ariana alipata kazi kwenye kampuni ambaya CEO wa kampuni alikuwa ni ford noble , kwakuwa Ariana alikuwa na uhitaji aliamua kufanya kazi, ford anatumia ukubwa wake kumtesa Ariana kwa kumfanyisha kazi nyingi kama adhabu , usoni ford alionyesha kumkasirikia ariana lakini moyoni alikuwa Bado anampenda sana ariana. Uzalendo unamshinda Ford anaonyesha hisia zake waziwazi kwa Ariana . Je Ariana atakubali kuwa na Ford kirahisi kwakuwa ni boss wake au bado atasimamia msimamo wake? Na Ford atashawishi vipi mpaka akubali kuwa nae?

I WILL NEVER LOSE YOU { ARIANNA }
MTUNZI : SMILE SHINE
SEHEMU 1 :

Kwa mbaliii ilionekana nyumba kubwa ya kifahari, ikiwa ina pigwa miziki mkubwa sana na watu walikua wengi sana wakicheza wengine walikuwa wakiogelea na wengine walikuwa wanakunywa vinywaji vikali na wengine walpiga story na wengine walikuwa wamekaa wawili wawili Kwa kujitenga mwanamke na mwanaume Kwa kuyaona haya yote unaweza ukasema ni club ama nyumba yoyote ya starehe.

Ila hiyo ilikuwa ni nyumba ya Mr noble tajiri mkubwa sana nchini .
Jumba lake zuri liligeuzwa kama club ama dangulo kabisa mana wadada walikua wamevaa nusu utupu ,na aliefanya haya yote si mwingine ni mtoto wake kipenzi wa mwisho ford .

Ford noble ni kijana wa miaka Kumi na nane na kipindi hicho alikuwa elimu ya secondary yani form 3.
Ila hakuna club ambayo hajawahi kuingia na Kila aina ya pombe kashatumia na kubadilisha wanawake haikuwa ajabu kwake.

Ford kwao wamezaliwa wawili tu yeyé akiwa wa mwisho na kaka yake anayeitwa Liam noble lakini yeyé amelelewa na mama yake huko nchini marekani.
bi Adeline alipata kazi ya ukufunzi kwenye chuo kikubwa Cha udactari huko nchini marekani , ilimbidi bi Adeline aliondoka na Liam na kumuacha ford kwani ford ndo alikuwa kipenzi Cha baba yake.
Baada ya sherehe kuisha kunaonekana kumepambazuka ford alikuwa amelala nje pembeni ya swimming pool akiwa kalewa chakali.
Ford alihisi kama anaota anasikia sauti ya baba yake na mama yake wakimuita na kumtikisa ila hakuamka kichwani alisema ngoja niendelee kulala nizidi kuota ndoto nzuri ..
Ghafra ford alishtukia akiwa yupo ndani ya swimming pool ,alikurupuka kuangalia aliemuingiza kwenye maji ni nani ,macho Kwa macho na baba yake na mama yake , Ford alipata mshtuko na furaha Kwa pamoja kuwaona wazazi wake mana hakumuona mama yake siku nyingi.

"Mom , dad "
aliita ford huku anatoka kwenye maji ford alimkumbatia mama yake akiwa vile vile na maji .

"My son "
mama yake pia alikuwa amemmiss sana mwanae hakujali kuwa alikuwa ameloana nae alimkumbatia hivyo hivyo .

"Zimekuwa siku nyingi sana mom nikajua umenitelekeza na hunipendi tena unampenda tu liam." alisema Ford huku kashika Mikono ya mama yake .

"No son ,unajua kabisa siwezi kufanya hivyo nawapenda wote wewe pamoja na Liam ,nyie wote ni watoto wangu wazuri"
alisema bi Adeline Wakati huo Mr noble amesimama pembeni anawaangalia .

"Ford panda chumbani kwako ukajisafishe ubadilishe na hizo nguo tuna mengi ya kuongea ", alisema Mr noble.

"Sawa Dad ....mom usinikimbie tena narudi Sasa ivi"
Ford alitoka mbio kuelekea chumbani kwake kubadili nguo zake zilizo loana.

"Mke wangu nimekubali kuwa mimi nimeshindwa Sina malezi bora nimeshindwa kumlea Ford vizuri Kwa kipindi ambacho haukuwepo karibu yetu nilihisi kwamba mtoto anahitaji pesa na Kila kitu kukuwa vizuri lakini nimegundua Sio kweli mtoto anahitaji muongozo Bora kwenye maisha ona liam alivyokua smart ana adabu na kafaulu vizuri na Sasa Yuko chuo kikuu Cha udaktari lakini huyu aliekuwa kipenzi changu anaangamia Kwa kukosa malezi bora nikuombe mke wangu embu mrekebishe na Ford awe kama Liam."

"Mmmh Usijali mume wangu , Kila kitu kitakuwa sawa fuata tu nitakacho kwambia na usinipinge na utaona matokeo yake " alisema bi Adeline

"Sawa mke wangu , Mimi nakusikiliza wewe unamipango gani.

"Cha kwanza fungía kadi zote za benki za ford , Cha Pili mnyanganye magari anayotumia na piki piki yake pia , vingine niachie Mimi nitamalizana nae" alisema bi Adeline

"Sawa nimekuelewa"
Mr noble alichukua simu yake na kumpigia secretary wake

" Hallo ! Jack naomba uzifungie kadi zote ambazo zipo chini ya jina la Ford"

. "Sawa Mr noble nitalifanyia kazi "
Alijibu secretary wake .

"Nimeshamaliza Bado kumnyanganya magari "
alisema Mr noble na mke wake alimuonyesha Dole gumba .

"Mr noble na madam Adeline chakula kipo tayari"
aliwataarifu mfanyakazi wa pale nyumbani

"Sawa asante sana mage" alijibu bi Adeline ...

Mr noble na bi Adeline walishikana Mikono na kuelekea meza ya chakula. Kabla hawajaanza kupata chakula alikuja Ford Kwa speed akiwa kashika simu yake mkononi .

"What the heck is going on Dad??"
alisema ford Kwa hasira huku anaweka Simu yake Kwa nguvu kwenye meza

"As you can see , I freeze all your bank accounts " alijibu Mr Noble

"Hatukukubaliana hivi Kwanini all of a sudden umeamua kuzizuia bank accounts zangu"
aliuliza ford Kwa kufoka bila kujali anaongea na nani

"His is your Dad, inakuwaje unajibizana nae kama mtoto mwenzio? "
alifoka bi Adeline

"Sorry mom"
Ford aliomba msamaha Huku anaangalia chini

"Hiyo Samahani yako muombe baba Yako , yani anakupa Kila kitu Bado hujajifunza kumuheshimu ,kwani hizo pesa unazitafuta wewe mpaka unafoka unajua baba Yako kazipataje hizo pesa ? Si nakuuliza wewe?" bi Adeline alikasirika sana Mpaka mume wake akamtuliza basi

"mke wangu inatosha"

. "Haya kaa na ule kimya kimya kabla hujanikasirisha nikaondoka tena na kurudi marekani. "

" Sorry Dad....mom sorry , sitorudia tena kupandisha sauti "
Ford aliomuomba baba yake msamaha

"It's okay son ,endelea kula"
Mr noble , bi Adeline na ford waliendelea kula kimya kimya bila kufanya mazungumzo ya aina yoyote .

"Enhee nimekumbuka mume wangu Liam alinipa zawadi zenu niwaletee anasema amewamiss sana sema yupo busy na mambo ya chuo na wapo kwenye mitihani Kwa Sasa "

Oh kumbe hakutusahau nitampigia badaee nimpe Asante "
alisema Mr noble na wakati huo Ford alikuwa kimya tu.

"Ford"
aliita mama yake bi Adeline

"Yes mom"

"Kuna shule nataka ukamalizie huko muhula uliobaki wa kidato Cha 3 na 4"
alisema bi Adeline

"Really!?"
alisema ford Kwa furaha Huku akiweka kijiko kwenye sahani na kumuangalia mama yake .

"Ni shule gani ni marekani Kwa bro Liam?"
aliukiza ford Kwa shauku kubwa ya kutaka kujua

"Nope , ni shule ambayo imenifunza Mimi mama Yako vyema mpaka saizi kufikia kuwa dactari mzuri wa mambo ya moyo "
alisema bi Adeline huku anaendele kula, Mr noble alishtuka akamuangalia mkewe usoni, bi Adeline alimkonyeza Mr noble na kumpa ishara asiseme kitu anyamaze kimyaaa.

"Mom hujawahi kuniambia hapo kabla kuhusu maisha Yako ya zamani na shule ulizosoma kwahiyo Bado sijaijua ni shule Gani may be unitajie jina ni Google".
Alisema ford huku anashika simu yake

"Hamna haja son ni surprise Yako hutakiwi kuiona Kwa Sasa Hadi tutakapofika huko"

"Dad niambie basi inaitwaje au na wewe huijui kama Mimi?"
Aliukiza ford

"Yeah siijui "
alijibu Mr noble Kwa kifupi Huku akiendelea kunywa juice yake.

"Come-on Dad you can't be serious , kweli hujui mke wako kasoma shule gani" alisema ford Kwa mshangao .

"Ndo hivyo baba Yako haijui ukitaka kuijua kesho asubuhi na mapema tutatoka hapa ili ukaione hiyo shule, naimani utaipenda sana .Iko vizuri Hata kuizidi winners"

.........................................................

Maisha mara zote huwa hayafanani kabisa wakati Ford anafurahia maisha na familia yake ,upande wa pili tunakutana na Binti Ariana.
Ariana ni Binti ambaye anajitumaa sana kwenye masomo yake , jina lake kamili ni Ariana Joshua kwao wamezaliwa wawili tu Kwa Mr Joshua masawe na bi Ester.
Arianna yeyé akiwa ni wa kwanza na mdogo wake wa kiume anaeitwa Aaron Kwa wakati huo Ariana alikuwa na Miaka 17 na alikuwa kidato Cha tatu na mdogo wake Aaron alikuwa na Miaka 14 akiwa kidato Cha kwanza, miezi michache iliyopita walimpoteza baba Yao Kwa ajari ya gari.
kwanzia hapo visa vya ndugu wa upande wa Kwa baba yao havikuisha na wakati huo nyumban kwao kulikuwa na mgogoro mkubwa sana shangazi zake walitaka kuwafukuza kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi .
Wakati ugomvi unaendelea Ariana alikuwa kimya akiendelea kufanya maswali yake ya math baada ya kumaliza KAZI zake za darasani ndiyo aliingilia ugomvi wa mama yake na shangazi zake wawili mmoja alieenda Kwa jina la sifa na mwingine Eva .

"Hapana mmezidi sasa kiwanda cha baba mmeshakichukua na Sasa hivi mnataka na hii nyumba , mwisho mtataka na roho zetu kabisa" alisema Ariana Kwa kufoka.

"Chunga sana Binti usilete hicho kidomo domo chako nitakuvuruga Sasa hivi "
alisema sifa shangazi yake na Ariana

"Jaribu kumgusa mwanangu uone kama sitoenda kuwashtaki"
alisema bi Ester
" huu ugomvi ni Mimi na nyie wanangu hauwahusu hata kidogo".

"Ndo umwambie huyó Binti Yako aliekosa adabu afunge bakuli lake alisema Eva" .

"Mtu aliekosa adabu ana rangi gani ? Kama rangi Yako uliyojichubua"
alisema Ariana

"Wee mtoto koma naona unataka kupandisha mashetani yangu "
bi Eva alifunga mtandio wake vizuri kiunoni , walianza kupigana bahati alifika mjomba ake na Ariana akawafukuza shangazi zake.

"Afadhali umekuja Kwa wakati "
alisama bi Ester Huku anahema juu juu.

"Anko Kwanini tusiwaachie Kila wanachokitaka twende tukaishi na wewe mama atakuwa anakusaidia kuuza mgahawani unaona hali ya mama Sio nzuri watakuja kumuua Kwa presha."

"Umeongea point nzuri Ariana Bora muwaachie hivyo vitu ,mtaenda kuisha kwangu vitu vinatafutwa lakini uhai haurudi mara ya pili"
alisema Venus anko yake na Ariana mdogo wa mama yao bi Ester

"Umeskia mama hakuna kukata maana nakujua wewe utataka kubaki hapa , hata Mimi natamani kubaki hapa kwani kuna kumbukumbu nyingi sana za baba yangu ila hatuna jinsi kupaacha yeyé ataendelea kuishi kwenye mioyo yetu milele "
alisema Ariana huku anamfuata machozi mama yake na kamkumbatia.

I WILL NEVER LOSE YOU { ARIANNA }
MTUNZI : SMILE SHINE
SEHEMU 2

"Umesikia mama hakuna kukata maana nakujua wewe utataka kubaki hapa , hata Mimi natamani kubaki hapa kwani kuna kumbukumbu nyingi sana za baba yangu ila hatuna jinsi kupaacha yeyé ataendelea kuishi kwenye mioyo yetu milele "
alisema Ariana huku anamfuta machozi mama yake na kamkumbatia.

"Ester umekuza Hadi mtoto anajua jinsi ya kubembeleza na kukufariji" alisema Venus huku anawakumbatia pia .

"Kwahiyo na Mimi mmenitoa nje ya familia si ndio"
alisema Aaron huku anatupa pegi la shule chini aliwakimbilia na yeyé anawakumbatia Kwa juu .

Walijikuta wanacheka ,na kupanga kuondoka pale na kuuanza mwanzo wao mpya . Walifanikiwa kupanga baadhi ya vitu vyao na kuondoka jioni ile ile Wala hawakusubiri pakuche .

Kwa upande wa Kwa kina ford usiku mama yake alienda chumbani Kwa Ford .

"Kipenzi changu Bado hujalala unafanya Nini?"
Aliuliza bi Adeline

"Ndiyo sijalala Bado "
Ford alimjibu mama yake huku akiwa busy kuchati Mama yake hakufurahishwa na kile kitendo alimsogelea ford na kumnyanaganya simu yake .

"Mom please 🙏 usiangalie nipatie hiyo simu" .

"Sikupi , unataka kunipiga au"
aliuliza bi Adeline huku anaigeuza ile simu na kuangalia

"Ford ndo umekuwa kiasi hichi si ndio? yani unachati na wasichana tofauti tofauti namna hii? mbona umeharibikiwa hivyo wewe sio ford wangu ninae mjua , ford wangu ninae mjua Yuko wapi?"
Alisema bi Adeline huku machozi yanamlenga lenga

"Please mom usilie basi , that's why nilikwambia usiangalie ona Sasa " alisema ford huku anamshika mama yake mikono.

"Don't touch me , na vipi kuhusu Kara una mipango Gani kuhusu yeye? baba Yako anasema alishawahi kukufuma umemuingiza mtoto WA watu humu ndani na alilala hapa kama mtu mzima naelewa kilichotokea kati yenu "
alisema bi Adeline huku anamkazia macho ford

"Come-on mom , we were just killing time mpaka Sasa Sina mpango na Binti wa mtu yoyote .

"Killing time ? Kwa hiyo unawachezea tu mabint wa watu?"

"Si wanajileta wenyewe me nifanyaje?"
alijibu Ford akiwa mkavuu..

Bi Adeline alimnasa ford vibao viwili vya nguvu .
"unanijibu Mimi unavyojiskia kama ulikaa tumboni kwangu miezi tisa nakwambia utanyooka tu mwaka huu ,hii Simu huipati ndo nimeshaichukua na hizi funguo za gari nachukua na kila nitakacho kwambia lazima utekeleze nadhani unanielewa vizuri"
alisema bi adeline na kutoka chumbani kwa ford akiwa na hasira..
Ford alibaki ameshika shavu lake .

Asubuhi kulipopambazuka bi Adeline alijiandaa na kumuamsha mume wake .

"Baba Liam umesahau Leo tunamiadi ya kwenda wapi mbona unalala sana" alisema bi Adeline akimuamsha mumewe.

"Oh nilisahau kabisa vipi Ford kashajindaa pia ?"
Itakuwa kashajiandaa tangia saa 11 alfajiri taa ya chumbani kwake ilikuwa inawaka.
Walijiandaa wakapanda kwenye gari na Safari ikaanza walipiga story za kukumbushana mambo Yao ya zamani lakini muda wote Ford alikuwa kimya .

Hatimae walifika wakashuka kwenye gari

"Ford umeona hiyo shule mbele Yako ?"
Aliuliza bi Adeline

"Ndiyo nimeiona"
alijibu Ford Kwa sauti ya chini.

"Hii shule inaitwa mtakuja secondary school ndio shule niliyosomea Mimi elimu yangu ya secondary "

" Nini ?"
aliuliza ford Kwa mshangao maana ilikua ni shule ya pembeni ya mji kama kijijini japo mazingira ya shule yalikuwa ni mazuri lakini hayaifikii hata robo shule ya winners high school aliyokuwa akisoma Ford

"Mom me siwezi kusoma kweny mazingira kama haya"

"Utasoma tu utake usitake na ukitaka nikusamehe kwa ulichokifanya Jana ubadilike , hizo tabia zako za kijinga uziache na kingine matokeo Yako yanatakiwa kuwa mazuri last semester nimesikia umepata wastani wa chini sana lisijirudie hilo."

"Sasa mom me ntakuwa nakuja kusoma mbali kote huku"
Alilalamika Ford

"Usijali utaenda kukaa kwa Yaya flora si unamkumbuka?"
alisema bi Adeline

"Yeah nampata Yaya flora"
Walienda Hadi Kwa bi flora na kumkabidhisha ford kisha wao wakaaga na kuondoka .

"Yaya flora sijui kama nitaweza kuishi huku" alisema ford Kwa kudeka huku anamlalia bi flora kweny miguu yake

"Utaweza tu wewe ni jembe Langu nakuaminia"

alisema bi flora huku anamshika ford kichwani....
Bi flora yeyé aliwalea Ford na Liam tangia wakiwa hawajui hata kusema neno ndio maana walimzoea sana kama bibi Yao.
Kesho yake asubuhi Ford aliwasili shuleni akiwa kavalia nguo za shule lakini alipendeza sana ukiachilia mbali raba Kali alizovaa na saa ya bei mbaya alikua ni handsome na wadada walianza kumkodolea macho na vile waliskia mfadhili mkubwa wa mtakuja secondary school ni mazazi wa ford na ford aliletwa pale kama kufunzwa adabu tu .
Ford alipelekwa hadi Kwenye darasa atakalokuwa anasoma

"Wanafunzi Leo nimekuja na mwanafunzi mpya mnatakiwa kuishi nae vizuri muda wote atakaokuwepo hapa"
alisema Mr Daniel ambae ni mkuu wa shule.

"Kijana jitambulishe"

"Hi guys ,ford noble hilo ndo jina langu, I hope tutaishi vizur Kwa muda nitakaotumia hapa"
Wanafunzi wote walimpigia makofi na wadada walikuwa wakijichekesha ila jicho la Ford lilitua Kwa msichana mmoja tu aliekuwa kanuna hatari Kila wakati anaangalia saa yake na hana mpango hata wa kumuangalia ford na msichana huyó ailikuwa ni Ariana.

"Ford utakaa kiti kile palé pembeni ya Zeno yeyé ni kijana mtulivu unaweza kumfanya rafiki pia"
alisema head master na kutoka darasani.

"Ariana muone huyu mkaka alivyo handsome "
.alisema rosena huku anamtingisha Arianna Kwa nguvu

"Wewe endelea kushangaa uumbaji wa mungu acha mimi nisome wameshanipotezea dakika zangu Saba za kusovu maswali"
aliongea Ariana Kwa sauti huku anafungua vitabu vyake.
Ford alimsikia akabaki kumuangalia tu haikuwahi kutokea msichana yoyote akampuuzia kama aliyofanya Ariana.
Ford hakuchukua muda kuizoea shule alipata na rafiki alieitwa zeno ..
Zeno ni kijana mtanashati pia ila yeyé alikuwa mpole na anafanya vizuri darasani kulinganisha na ford aliyeendeleza michezo yake ya kubadilisha wasichana na kuvuta sigara.
Wasichana wengi walikuwa wanamshobokea sana akiwemo luna na kundi lake la watu watatu Luna , zarina na zawadi.
Kuna siku Ford alimuona Ariana anatembea huku ameshika notebook anasoma

"Oya bro yule Binti hivi ana marafiki kweli namuona Yuko peke yake peke yake tu


I WILL NEVER LOSE YOU { ARIANNA }
MTUNZI : SMILE SHINE
SEHEMU 3

"Oya bro yule Binti hivi ana marafiki kweli namuona Yuko peke yake peke yake tu na muda wote macho yapo kwenye Notebook"
aliuliza ford

"Hana marafiki wengi kiivyo anaongea na Kila mtu ila ukiangalia Kwa ukaribu ana rafiki mmoja tu wa kudumu ambaye ni rosena , muda wote Ariana anasoma tu Hana muda wa kupiga soga kama Sisi"
alisema zeno.

Siku hiyo mida ya jioni wanafunzi walikuwa wamesharudi makwao Ariana alikuwa Bado yupo darasani anajisomea Ariana alianza kuvuta harufu ya sigara .

"Mpuuzi gani huyu anavuta sigara maeneo ya shule tena karibu na darasa Langu pendwa la kusomea ananipotezea umakini wa kusoma ngoja nimfate huko huko."
Alisimama Ariana na kuelekea nyuma ya madarasa alimkuta Ford anavuta sigara .

"Oya ,oya wewe kuku wa kisasa." ...
aliita Ariana huku kaziba púa zake

"Ndo unafanya Nini apo haujui kama wanafunzi hawaruhusiwi kuvuta sigara ni kosa kubwa sana unaweza hata kusimamishwa shule " alisema Ariana huku anamsogelea Ford .

"Mimi hata sijali wakinisimamisha shule itakuwa ni vizuri"
alisema Ford huku anaendelea kavuta sigara hakuwa na wasiwasi Hata kidogo

"Haya tufanye wewe ndo hujali ,ila Mimi najali taaluma yangu so ondoka kavutie sehemu nyingine"
Kabla Ford hajamjibu chochote alimuona mlinzi anakuja Kwa nyuma ya Ariana

"Okay usijali Mimi naondoka "
Alisema Ford akashika mkono wa Ariana na kumpa kitu Ariana hakukiangalia ni kitu Gani

"Kila la kheri kwenye masomo Yako"
alisema ford huku anacheka harafu akakimbia.

"Huyu kumbe chizi ee" alisema Ariana huku anatingisha kichwa alishtuliwa na sauti ya mlinzi

"unafanya Nini apo.?"

"Shkamoo kaka Abdul" alisalimia Ariana huku anatabasamu .

"Ariana kumbe na wewe unavuta sigara ?"
Aliuliza mlinzi huku anaangalia vizuri kitu alichokishika Ariana mkononi

"Hapana Mimi sijawahi kavuta sigara"

"Na hicho kipakti Cha sigara mkononi kwako kimefikaje "
Ariana alijiangalia mkononi akashtuka kuona kweli alishika kipakti Cha sigara

"Kaka Abdul hiki sio changu ni Cha yule ford alikuwepo hapa Sasa hivi"

"Mbona sikumkuta nimekuta peke yako?umeanza kuwa muongo muongo siku hizi ?"

" Nisamehe kaka Abdul sitorudia tena 😭 "
ilibidi Ariana aombe msamaha Kwa kosa ambalo sio lake.

"Haya lete hizo sigara na uondoke haraka kabla Mr Daniel hajakukuta huku nyuma. "
Ariana alimpa mlinzi zile sigara akaondoka hata hamu ya kusoma iliishia alichukua begi lake na kuanza safari ya kurudi nyumbani Kwao

"Wewe mwandawazimu sito kusamehe umefanya Mimi nionekane mvutaji sigara"
Ariana aliondoka akiwa na hasira sana .

"Vipi kipenzi changu mbona umenuna sana Leo Nani kakukera huko shuleni?" aliuliza mama Ariana.

"Yani mama Kuna mpuuzi mmoja kahamia shuleni kwetu hata miezi haijapita ila ana tabia za ajabu ajabu tu."

"Sasa kama atakukera Au kukuchokoza usisite kumwambia mwalimu akusaidie."

"Wala usijali mama nitamfunza adabu Mimi mwenyewe" .
Kesho yake Ariana alichelewa kidogo kuamaka
"Mungu wangu nimechelewa Leo imekuwaje"

"Basi jiandae haraka unywe chai kabisa"

"Hapana mama Leo sitokunywa chai ,badaee mama"
Ariana alitoka kwa kasi mpaka barabara kuu alikutana na ford wakaanza kuongozana ila Ariana alikuwa kimya muda wotee.

"Mambo cute"
Alisalimia ford lakini Ariana alikuwa kimya .

"Umenuna basi nisamehe Kwa nilicho kifanya Jana haikuwa akili yangu ".
Bado Ariana alikuwa kimya.

"Oh kumbe umegoma kuongea ee basi nitakufanya uongee Kwa lazima"
ford alimnyanganya Ariana bagi lake na kaanza kukimbia nalo .

"Wee ford umechanganyikiwa nipe begi Langu ,sasa ivi milango ya madarasa itafungwa bhana na Mimi sitaki kupewa adhabu" .
Ford na Ariana walikimbizana sana

"Niambie umenisamehe ?"
Ford alimuuliza Arianna huku anahema Juu Juu

"Ndiyo nimekusamehe" . Ford alimpa Ariana begi lake lakini Ariana hakukubali kushindwa alimpiga ford ngumi ya mgongoni akakimbia kuelekea darasani .

"Ariana na wewe umeanza kuwa mchelewaji siku hizi aliuliza madam Tessa .

"Hapana madam ni bahati mbaya tu "
Alijibu Arianna huku anamkata jicho ford, Ford yeye alibaki kutabasamu tu

"Kwa sasa ingia darasani ila badae wewe na ford mkasafishe uwanja wa nyuma ya madarasa,"
Ariana alinywea sana siku hiyo ,darasani hakutaka hata kujibu maswali ya madam Tessa, Madam Tessa alipotoka darasani akamuita Ariana

"Ariana najua umechelewa Kwa bahati mbaya ila waliochelewa wote Leo nimewapa kazi nisingekupangia kazi basi ningeonekana nina upendeleo kasafisha harafu ukajisomee sawa eee. "

" Sawa madam nimekuelewa".
Ford na Ariana walienda kasafisha uwanja lakini ford hakuacha kumchokoza Arianna

"wewe Ford hivyo ndo unafagia au unacheza"?Aliuliza Ariana kwa hasira

" Kwani wewe unaona Mimi nafanya Nini hapa au nikakuletee miwani umeshakuwa bibi huoni vizuri "
Ford alianza Tena kumtania Ariana

" Wewe kuku wa kisasa wewe nakwambia maji yanachemka jikoni nitakunyoosha nakwambia mwaka huu "
Ariana aliacha kufagia akaanza kumkimbiza Ford walikimbuzana sana wakajikuta wameangusha pipi la takataka

" Ona Sasa umeangusha pipa la takataka "
alisema Ford kumwambia Ariana

" Sio Mimi ni wewe "
Ariana nae hakukubali alikuwa mbishi walibishana sana mpaka wakakunjana mashati, Zeno na Rosena walienda kuamulia ugomvi

" Kuzozana hakutosaidia kitu tushirikiane tu kwa pamoja tumalize kusafisha hili eneo "
alisema Zeno

" Mimi siwezi kukaa eneo Moja na huyu kuku wa kisasa "
aliongea Ariana kwa hasira

" Kwani Mimi nimekwambia nataka kukaa karibu na wewe bibi "
Ford nae alizidi kumtamia Ariana

" Inabidi iwe hivyo mkae pamoja tusaidiane kengere ya kwenda majumbani itapigwa sio muda mrefu tukizubaa hapa watu wote wataondoka "
alisema rosen....

rosena , Ariana na Ford walisaidiana kusafisha eneo wakafanikiwa kumaliza mapema na kurudi nyumbani na wanafunzi wengine

I WILL NEVER LOSE YOU { ARIANNA }
MTUNZI : SMILE SHINE
SEHEMU 4

Zeno ,rosena , Ariana na Ford walisaidiana kusafisha eneo wakafanikiwa kumaliza mapema .
Kesho yake Ariana aliwahi sana kwenda shuleni akaingia darasani kujisomea kidogo kabla ya kengere ya kuwahi Namba za asubuhi lakini kama kawaida alisikia harufu ya sigara alichungulia dirishani nyuma ya madarasa akamuona Ford anavuta sigara akatabasamu ,alitoka akaenda kuchukua ndoo ya maji na kumsogelea Ford kwa kunyata kufumba na kufumbua Ariana alimmwagia maji Ford ndoo nzima

" Unafanya nini wewe?" Ford alishtuka akasimama akiwa kaloana nguo zake zote

"Oo mungu wangu kumbe ni mtu Mimi niliona kama madarasa yanataka kuwaka moto mana wanasema panapofuka Moshi moto utawaka tu nikaamua kuchukua tahadhari mapema , masikini sukari ya warembo sijui itayeyuka "
aliongea Ariana huku anatabasamu..
Ford alingata lips yake ya chini mpaka damu zikaanza kutoka niwazi alikuwa na hasira sana hakutaka kubishana na Ariana alimpiga kikumbo akaondoka

" Kwisha habari yake akirudi nyumbani kubadilisha nguo ni lazima atachelewa darasani na adhabu itamuhusu Tena na Leo "
aliongea Ariana kwa furaha akarudi darasani kujisomea.
Ford alirudi nyumbani kwa bi flora akiwa kanuna

" Vipi Tena mbona umerudi mapema Leo na umeloa hivyo na hakuna mvua ? Aliuliza bi flora

" Bibi Naomba nibadilishe nguo niwahi kurudi shule nitakwambia nikirudi kilichonisibu"

Ford alibadilisha nguo haraka akatoka alichukua bodaboda Ili awahi kufika shule ila bahati haikuwa kwake alichelewa milango ilikuwa imefungwa alipewa adhabu ya kusafisha choo

" Ford itabidi uzoee tu kuishi haya maisha yetu mama yako amesema tusikuheshimu kwakuwa mama yako ni mfadhili wetu tukuchukulie kama wanafunzi wengine ikiwemo kupewa adhabu ukikosea " alisema mwalimu Daniel

" Ni sawa mkuu naelewa " Ford alimaliza kusafisha vyoo akaingia darasani Ariana muda wote alikuwa anatabasamu Kila akikumbuka sura ya Ford alivyokuwa anasafisha vyoo

" Inaonekana Umefurahi sana Leo ?"
aliuliza rosena

" Sana Yani nimefurahi sana mpaka natamani kupiga kelele za furaha "

" Kimetokea Nini ?"
aliuliza rosena kwa sauti ya chini

" Njoo nikunon'goneze " Ariana alimnon'goneza rosena wakaanza kucheka Ford limuangalia Ariana kwa hasira muda wa kwenda nyumbani Ariana alikuja kuitwa na mwanafunzi wa kidato cha kwanza.

" Dada Ariana , unaitwa na mwalimu zakayo kule nyuma ya uwanja "

" Sawa Asante "
Ariana alienda kwenye uwanja ulioko nje na nyuma ya shule cha ajabu hakumkuta mwalimu yoyote Bali alimkuta Ford kasimama anamchekea Ariana alitaka kukimbia Ford akamdaka na kumbeba begani Ariana alijaribu kumpigia lakini alishidwa Ford alienda mpaka mtoni akamtupa Ariana kwenye maji

" Wow , hii imekaa poa Sasa unayaonaje maji yalivyo matamu "
aliongea Ford huku anacheka

" Ford Mimi si ...sijui kuogelea "
Ariana 😭 aliongea kwa tabu na maji yalianza kumpeleka

" Wewe acha utani ,kweli huwezi kuogelea "
Ford aliuliza kwa wasiwasi japo mwanzo alihisi Ariana anamfanyia utani Ford alivyoona hali imekuwa mbaya alizama mtoni akamtoa Ariana

" Ariana upo sawa"
Ford alimuuliza Ariana aliyekuwa analia kwa kwikwi.
Ariana hakujibu kitu alizidi kulia na kutetemeka Ford alichukua koti lake chini akamfunika Ariana Kisha akamkumbatia

" Ariana nisamehe sitorudia Tena kufanya huu ujinga naomba yaishe"
Ford alimuomba msamaha Ariana Alimbembeleza akanyamaza Kisha akampeleka nyumbani kwao Kwanzia siku hiyo Ford hakutaka kumchokoza Tena Ariana na Ariana aliogopa kumchokoza Ford akihisi ataenda kutupiwa Tena mtoni .
Siku ya ijumaa ilikuwa ni siku ya michezo mtakuja secondary school , wanafunzi walikusanyika kucheza michezo mbali mbali.

"Ariana najua hupendi siku ya michezo ila njoo basi tucheze apo kwa kina Martha mchezo wa Truth or dare "
Rosena alimbembeleza ariana akakubali. Walikaa kwenye duara na kaanza kuzungusha chupa na chupa iliposimama ilikuwa imeelekea Kwa Ariana watu walifurahia na kuanza kumuuliza maswali .
Nafasi ya kuuliza swali alipata baraka mkaka ambae alikuwa akimfukuzia Ariana siku nyingi ila bahati haikuwa kwake Kila mara Ariana alimtolea nje. "Ariana unawaza kutwambia kama upo kwenye mahusiano au laa ? Na kama haupo kwenye mahusiano ni mwanaume wa namna gani anaweza kutoka na wewe?"

" Woyooooo"
wanafunzi walpiga kelele kama kawaida yao na kumuangalia Ariana atatoa jibu gani.

"Mimi kwanza Sina mpenzi na sijafikilia kuwa nae Kwa Sasa kipaombele changu ni masomo na familia yangu, na kuhusu sifaa za huyó mwanaume napenda awe Msomi ,mtulivu ,havuti sigara Wala hatumii kilevi, jicho lake mara zote liwe kwangu tu namaanisha asiwe kicheche."
Ariana aliongea haya yote huku anamkata jicho Ford .

Watu walishangilia
"vipi kuhusu muonekano wake?"
aliuliza rosena

"Kwanza kingine napenda mwanaume awe mrefu kuwa handsome hakunisaidii chochote upendo tu ndo unaotakiwa".
Apo kwenye urefu Ariana alisema makusudi kumkomesha baraka ,maana baraka alianza kufurahi na kuhisi anaweza akampata ariana . Ford alibaki anatabasamu tu huku anamuangalia sana ariana ,Ariana nae hakuona aibu alimkazia macho Ford mchezo ukaendelea . .
Ford alijikuta taratibu anaanza kumpenda Ariana bila kujua aliacha kuvuta sigara ,pombe na kubadilisha wanawake pia , akaanza kusoma Kwa bidii sio Ili kumfurahisha baba yake na mama yake Bali ni kuwa mwanaume anaemuhitaji Ariana.
Ford na Zeno walikuwa wanabaki shule Kila siku jion kujisomea .

"Mmh bro ila umebadilika ghafla kweli mapenzi shkamoo yake "
alisema zeno huku anasahihisha maswali aliyokuwa akiyafanya ford na alikuwa kafanya sahihi yote .

"Ulihisi mimi ni kilaza au? sikuamua tu kuwa serious na masomo "
alisema ford huku anacheka .
Mitihani ya kufunga shule ilifika kama kawaida kweny matokeo Ariana alikuwa wa kwanza haikuwa ajabu ila Kila mtu alibaki mdomo wazi kuona nafasi ya pili ni ford tena wamepishana alama chache sana na Ariana na wa tatú ni Zeno akiwa ameshuka daraja lakini alifurahi sana kuona Ford amefanya vizuri kwenye mitihani yake

"Broo umetisha hadi Mimi umenipita "
alisema zeno huku anamrukia ford .


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote