MSIMU WA PILI
ANNASTAZIA (am just a maid) 20
HUSQER BALTAZAR
Basi madam alichukuliwa na kupelekwa ndani, na kwa aina ya kesi yake, kwa maana alikutwa na mashtaka mengi sana hivyo akahukumiwa miaka 30 jela, nikajua mpaka akija kutoka atakutana na dunia mpya ambayo huenda isimpe nafasi ya kuendelea kufanya ujinga na uchafu wake….
Na mimi nikauza mali zangu zote, kwa sababu sikutaka kuendelea kushikilia vitu ambavyo nilikuwa nahisi kama vina roho chafu ndani yake, na kwenda kununua sehemu nyingine…
Nilikuwa NA Pesa ambazo zingeniwezesha kuishi miaka hata ishirini bila kufanya kazi yoyote, kwa sababu kulikuwa na mashamba na baadhi ya biashara za mazao ambazo zilikuwa zinajiendesha zenyewe, ila nilikuwa bint mdogo hivyo sikuona kama ni bisara kukaa ndani tu bila kazi yoyote ile, na nilihisi kukaa tu huenda watu wakaanza kunihisi vibaya, kwa maana nakula vizuri, nina gari zuri alafu sina kazi, kwa sababu hata nje sikuwa natoka na kazi na baishatra ya mazao kulikuwa na msimamizi kwa sababu sikuwa najua chovchote kile kuhusu hio bishara na yule mwana sharia alikuwa anasimamia kila kitu yeye, ingawa alikuwa anapata asimilia flani za mauzo, na hilo halikuwa tatizo kwangu, kwa sababu angalau naweza kula na kulala sehemu inayoeleweka tofaut na mwanzo….
Nilikaa mwaka mzima bila kazi yoyote, na nikahama kabisa na eneo, nikatoka Morogoro na kuamua kuamia zangu Zanzibar, mimi pamoja na mama yangu, kwa sababu nilihisi kama ni sehemu mpya kwangu, na hakuna anaenijua, na huko nilinunua nyumba, na nikamfungulia mama yangu biashara ili asiwe anakaa tu, na kila mwisho wa mwezi nilikuwa naenda morogoro kuangalia mashamba na mauzo yanaenda je…
Siku moja nikaona tangazo la kazi, na nilikuwa nataman sana kufanya kazi, na kuachana na usimamizi wa mali za wazaz wangu, nilijisomesha mwenyewe secretario caurse, na hilo tangazo lilikuwa linahusiana na kutafuta secretary, nikaona bora nikajaribu bahat yangu huenda nikapata kazi, maana ndio kitu ambacho nilikuwa nakitaman mno….
Basi bana nikaenda hio siku ya usaili, lakin jana yake nilienda na kuandika jina langu, na kulikuwa na watu kama watano ambao na wao walikuwa wanataka kufanya kazi kama yangu, hivyo kulikuwa na mchujo, kuwa kati yetu nani ambae atawania kinyang’anyiro cha kuwa secretary kwenye hio kampuni…
Mimi nilikuwa wa mwisho kabisa kuitwa, na nilikuwa naogopa pia kuingia, kwa sababu sikuwah kufanya kazi kabla, na sijawah kufanya usaili kwenye kazi yoyote ile kuanzia nazaliwa…
Basi kama ilivyo ada kuwa hata inyeshe kiasi gani ni lazima itakatika tu, na mimi muda wangu wa kuitwa kwaajili ya kufanyiwa usaili ukafika, nikaingia ndani na kukuta huyo ambae ananifanyia usaili amenipa mgongo, nikasalimia na kuanza kujielezea, ila wakat wote alikuwa yuko kimya, kitu ambacho kilikuwa kinanishangaza sana, ila nikajua labda ndio namna ambavyo anasaili watu, hivyo nikawa najiondolea pressure…
Lakin cha kushangaza hata maswali hakuwa ananiuliza kabisa, mpaka nikawa nashangaa ni usaili gani huu, ambao hata boss wako hawez kukuuliza maswali………
“ umepata kazi annastazia, mara nikashangaa anajibu Yule boss kisha akazunguka na kiti chake kisha akanitazama…
Alikuwa ni Clinton, sio siri nilishtuka mno mara baada ya kumuona, nikawa nataka kuondoka, akakimbnilia mlango na kuuwah kisha akajufunga, akaanza kuniangalia kwa sekunde kadhaa, kisha akasema “ ulipata mali nyingi sana mwaka mmoja uliopita, embu nambie kilichokufanya uje uombe kazi tena ni nini, maisha yamekupiga eee, unashida ya pesa si ndio, sasa usijal, wewe ndio nutakuwa sectetary wangu…
“ samahan Clinton sitaki kufanya kazi na wewe, naomba niondoke , nikasema…..
Akacheka kwa dharau kisha akasema “ ulichokifanya kilinifanya niwe mwanaume na kuacha kutegemea nguvu za mama yangu, nimejitafutia maisha yangu, na sasa nimejipata mamaa, sasa ni hjivi, ukiacha hii kazi hakuna mtu hata mmoja Zanzibar nzima ambae ataweza kukuajiri…
“ hivi Clinton unataka nini kwenye maisha yangu, naomba niende, nitaenda hata kuuza nyanya kuliko kufanya kazi na wewe, nikawa nasema huku nikiwa nataka kuondoka, nikashangaa navutwa kisha akaanza kunikiss…
Ni dhahiri Clinton alikuwa amenimiss sana, ila bado alikiwa na hasira na mimi, na lile busu ambalo alinipa ndio lilikuwa na maana hio, hata mimi nilikuwa nimemiss ila nilikuwa naona kama ni mapema sana, na sitakiwi kujirahisisha, kwa maana niliona kama atanipelekesha, nikamsukuma Clinton kisha nikasema “ unataka kufanya nini, au ndio namna kampuni yenu ilivyo kuwa, mfanyakazi mpya mpaka aanze kazi ni lazima alale na boss…
Clinton aliniangalia kisha akacheka na kusema “ fikiria unavyotaka, ila kesho mapema uje kazin, kwa maana nataman kukuona ukiteseka na ole wako usije, nitakutafutaq popote, kwa maana nilikutafuta sana na sikujua kama huko huku, na hii sehemu ni ndogo sana, hivyo nina uhakika kuwa lazima nitakupata, sasa usipange kukosa kazi kesho asubuh, kwa maana nikianza kukutafuta utaniongelezea hasira zaidi na nitazidi kukutesa, na baafda ya kusema hivyo akaondoka zake……..
Sio siri lile busu la Clinton lilikuwa limenisisimua sana, nilikuwa nataman hata angefanya zaidi ya pale, nikawa najitafakari kuwa nije kazin au niachane na kazi yenyewe, ila nikajiambia kuwa Clinton ananipenda, na namna ya kumrudisha kwenye milki yangu nikufanya kazi nae, najua kidogo kidogo naweza kubadilisha chuki zake kuwa upendo, na anatakiwa kunipenda kuliko alivyokuwa ananipenda mwanzo…
Basi nikatoka pale ofisin kwake, ila wakat natoka, nikamuona ameshikwa mkono na mwanamke mrembo alafu alikuwa anasema “ my love najua umechoka sana twende ukapate break fast kidogo…
Sijui kwanini nilijisikia vibaya sana, nikawa naondoka huku machozi yakiwa yananilenga lenga, sijui ndio nilikuwa mjinga kwa maana inawezekana vipi kwa mwanaume rijal kama Clinton kukaa single kwa mwaka mzima, nikawa najiambia kuwa sina change tena, na siwez kupambana kwaajili ya kumpata mwanaume wa mtu, nilijilaumu sana, na nilikuwa najisikia vibaya sana, sasa sijui ni Clinton aliona namna ambavyo sikuwa najisikia vizuri , nikashangaa ameniita , kwa maana bado sikuwa nimetoka kwenye jengo la hio kampuni, hivyuo nikasimama, na akaja na mwanamke wake mpaka pale nilipo kisha akasema “ Ryen huyu alikuwa classmate wangu, nimeona nimpe kazi maana tulishawah kuwa marafiki wakubwa sana, na amenisaidia mengi sana wakat ambao nilikuwa na shida…
Wakat ambao walikuwa wanaongea nilikuwa nimewapa mgongo, nikafuta yale machozi kisha nikawageukia na kusema “ nafrah sana kukufahamu ryen na asante sana mr Clinton kwa utambulisho kama hautajal naomba niende…
“ ohhh lakin annastazia sijakuambia kuwa huyu ni nani, akasema Clinton na nikaona nisikilize tu, ingawa nilikuwa najua ni nani…
“ annastazia huyu ni mke wangu mtarajiwa, mwanamke ambae anaweza kuficha aibu zangu na za familia yangu, mwanamke ambae kanipenda mwenywe na sijamlazimisha, na amepambana sana klunipata, mwanamke ambae yupo tayar kufanya chochogte kile kwaajili ya kuniweka upande wangu na sio kunipoteza, akasema Clinton na mimi nikawa natabasamu tu kisha nikasema “ hongeren na Mungu awajali mfunge ndoa mapema, nikawa nataka kuondoka na Clinton akamkiss ryne mbele ya macho yangu kisha akasema “ nakupenda sana mamaa, kisha wakaondoka zao…
Sio siri roho iliniuma, nilipotoka nje ya lile jengo nikakaa sehemu na kuanza kulia, nililia sana, mwisho nikawa najiambia kuwa natakiwa nisimpende mwanaume wa mtu, nikawa nasimama kutaka kuondoka, wakat nasimama nikaona kama kulikuwa na gari nyuma yangu ambalo lilikuwa limesimama, na nilipoangalia vzr nikamuona clinton alikuwa ananiangalia, na alikuwa ananiangalia kwa maumivu sana, kana kwamba mtu ambae hataman kuniona nikiwa kwenye majonzi, mpaka nikapata amani na kujiambia kuwa, Clinton anafanya makusudi ili kuniumiza kwa sababu ananipenda, kisha nikaondoka nyumban nikiwa na tumain kuwa Clinton ananipenda ila bado anahasira na mimi, na kwakuwa bado hajaoa, basi naweza nikabadilisha msimamo wake na kuwa na mimi…..
NAKUJA ……….
SOMA MAELEKEZO
Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote