ANASTASIA (Am Just A Maid)

book cover og

Utangulizi

ANNASTAZIA ( am just a maid) 1
HUSQER BALTAZAR

Naitwa anastessia, mama yangu anapenda kuniita Ana, mama yangu alikuwa na rafiki yake mmoja ambae alikuwa wana mtoto wa kiume na alikuwa anarika kama langu…
Mama yangu na huyo rafiki yake walikuwa wanaonekana kupendana sana, na kila wakat walikuwa wansema mimi na huyo kijana wa rafiki yake ambae alikuwa anaitwa Clinton kuwa tutakuja kuoana…
Tulikuwa tunapendana sana, na mara zote wakat ambao nilikuwa natoka shule nilikuwa nacheza na yule clinton kwa maana walikuwa wanakaa kwetu, mara baada ya clinton na mama yake kufukuzwa na baba yake clinton na kwakuwa mama yangu na mama yake clinton walikuwa na urafiki mkubwa sana, basi mama akaamua kumchukua na tukawa tunaishi nae pamoja….
Mara nyingi sana nilikuwa namkuta mama yake Clinton akiwa anavaa nguo za mama yangu, ila sikuwa naweza kuhoji kwa maana walikuwa ni marafiki sana,na hata mimi nilikuwa namchukulia kama mama yangu, kwa maana mama siku zote alikuwa ananisisitiza sana nimuheshimu…
Ila tatizo lilikuwa kwa baba yangu, kila wakat alikuwa anataka mama amfukuze rafiki yake ila mama hakuwa anataka, na mimi pia sikuwa naona kabisa tatizo kwa baba kutaka kumfukuza mama yake na clinton kwa maana alikuwa anaonekana kunipenda sana na mimi nilikuwa nampenda sana Clinton kwa maana ndio mtu pekee ambae nilikuwa nacheza nae nikitoka shule…
Ila sikuwa naelewa kwanini baba hakuwa anamtaka Yule mwanamke, nimekuja kuelewa baadae sana baada ya kukuwa na kujitambua, kuwa baba alikuwa anataka kusave ndoa yake ila mama yangu alikuwa anauendekeza urafiki kuliko ndoa yake….
Siku moja nilikuwa natoka shule, nikamkuta mama yangu analia, alikuwa analia sana, na nikasikia sautin ya mama yake Clinton nyuma yangu alikuja na kunambia kuwa mama yangu hanipendi na yeye ndio atakuwa mama yangu mpya, nilishangaa, kwa maana nilikuwa bint wa miaka tisa, na katika miaka yote hio mama yangu ndio alikuwa kila kitu kwangu, kwa maana alikuwa ndio furaha yangu, na kila siku alikuwa anapenda kuniimbia nyimbo kabla sijalala na kunipigai story, alafu mtu anakuja na kusema kuwa mama yangu hanipendi, kiukweli sikuwa namuelewa kabisa alikuwa anataka nini…..
“ naomba uondoke, mwanaume ameshasema hakutaki na hatakaa akutake kwenye maisha yake yote, kwa maana licha ya mwanaume wako kuwa ni tajiri, ila hajawah hata mara moja kukupenda kwa maana wewe ni mchafu sana, mwanamke hujui kuchamba, mwanamke hujui hata mapenz mwanamke gani wewe, mama yake Clinton alikuwa anamuambia mama yangu, mpaka nikawa najikuta nashangaa, kwa maana mama ndio alikuwa anamkingia kifua kuwa asifukuzwe na mumewe, alafu yeye ndio anakuja kumfukuza rafiki yake kwenye nyumba yake mwenyewe….

Mara nikashangaa baba yangu anakuja kisha akasema “ ondoka na hicho kimalay* chako kwa maana nyie ndio mnafanya maisha yangu yazidi kuwa magumu, na nashkuru sana mke wangu kipenzi kwa kuniletea mwanamke mjanja anaejua mapenzi, na amenionesha nilikuwa naishi na mwanamke wa bush…
Hakuna kitu ambacho nilikuwa naelewa, mama yangu alikuwa analia kwa maana alikuwa ametupiwa nguo zake chini, nikajikuta nalia na mimi, kwa maana kuanzia nazaliwa sijawah kumuona mama yangu akilia, mara akaja Clinton na kuanza kunibembeleza akanambia “ naomba usilie annastiazia tukiwa wakubwa nitakuoa na nitamjengea mama yako nyumba kubwa, kisha akamgeukia mama yake na kusema “ nakuchukia wewe ni shetani…..
Sikuwa najua ni kwasababu gani Clinton alikuwa ananitetea mimi na mama yangu badala ya mama yake, na wakat mama yake akiwa anapambana kutufukuza na Clinton nae alikuwa anataka kuondoka na sisi, ila mama yake akawa anamzuia, ila hakuwa anataka kubaki nae na kila wakat akawa anasema “ mama wewe ni shetani, nakuchukia sana, nakuchukia mno, mama wewe una roho mbaya sana, akawa analalamika Clinton na mama yake akawa anamuangalia kwa hasira kisha akaja kumchukua pale ambapo yupo na kuingia nae ndani, na wakat huo baba yangu alikuwa nay eye ameingia ndani na wakafunga mlango, mimi na mama yangu tukabaki nje….
Mama alikuwa analia kwa uchungu sana, kisha akanambia kuwa “ usije ukamuamin mtu mwanangu kwa maana binaadamu ni wabaya sana…
Basi nikaondoka na mama na kwenda nyumban kwao, ila mama hakuwa sawa, akawa anataka kwenda na mimi mbali kabisa ya ile sehemu ambayo tupo, kwa maana mkoa ambao aliolewa ndio ,mkoa ambao alikuwa anaishi na wazaz wake kabla…
Basi tukaondoka na kuamia mkoan arusha na wakat mwanzo tulikuwa tunaishi morogoro, na tulikuwa na maisha mazuri sana wakat tulipokuwa tunaishi na baba yangu, ila tukaenda kupangisha sehemu moja inaitwa soko mjinga, karibia na shule ya sinoni…
Nyumba tuliokuwa tunakaa kipindi hicho ilikuwa ni nyumba ya udongo na kodi ilikuwa ni kama elfu kumi na tano tu, na yalikuwa maisha mapya kwangu, kwa maana nilikuwa nimezoea kuishi kama mtoto wa mfalme, kwa maana nilikuwa nasoma shule nzuri na nilikuwa Napata kila ninachokitaka, alafu ghafla nakuja kuishi pamoja na mama yangu kwenye chumba cha udongo tena kisichokuwa hata na sakafu, na tukaanza kulala na mama chini…..
Kipindi kile hakukuwa na shida sana kwenye uhamisho, kwa maana nikahamishiwa shule ya msingi ya sinoni, kwa maana nilikuwa naingia darasa la tano, na ilikuwa ngumu sana kwangu kipindiu cha mwanzo kwa maana nimesoma shule za private kuanzia nikiwa na miaka mitatu, alafu nakuja kuanza kusoma shule zinazotumia mitaala ya kiswahil, ilikuwa ni kazi sana kwangu….
Mama yangu akaanza kufua na kufanya kazi za ndani kwenye majumba ya watu, kitu ambacho kilikuwa kinaniumiza sana, kwa maana tulikuwa na wafanya kazi wawili nyumban kwetu, alafu ,mama leo anakuja kuwa yeye ndio mfanyakazi, ni huzun sana kwa kweli….
Nilisoma kwa tabu sana, ingawa mama yangu alikuwa anapambana kuhakikisha maisha ambayo nilikuwa naishi tukiwa kama familia nayaishi yale yale kwa maana alikuwa anapambana kunipa kila ninachokitaka, bila kujua kuwa hawez tena kunipa maisha yale ambayo nilikuwa naishi kwenye utoto wangu….
Nilipomaliza darasa la saba tukapata taarifa kuwa baba yangu amefariki, na tulipofuatilia tukaja kugundua mali zote amemuandikia Yule mwanamke, kuna muda mama yangu alikuwa analia na kusema kuwa “ joyce umemuuwa mume wangu, mungu akuangamize wewe mwanamke, najua mume wangu hujampata kwa njia za kawaida, alikuwa ananipenda sana baba anastazia, ukaona haitoshi kunitenganisha nae, ukaona bora umuuwe…
Mama yangu akaanza kuumwa magonjwa yasioleweka, ikabidi niache shule na nianze kuishi maisha ambayo alikuwa anaishi yeye, kwa maana zile oda zake za kufua na kufanya kazi za ndani nikawa nafanya mimi, ili tuweze kuishi mimi na mama yangu….
Hali ya mama yangu haikuwa nzuri kabisa, siku moja tukiwa kanisan pale kanisa la moyo safi Arusha. Alikuja mzungu mmoja akawa anamuangalia sana mama akasema kuwa atakuwa anamsaidia…
Na kweli kila mwaka akawa anatutumia million tatu, ambazo kidogo zikaanza kubadilisha maisha yetu, kwa maana nilienda kumpeleka mama hospital na hakuonekana na tatizo lolote lile zaidi ya msongo wa mawazo, hali ya mama yangu ikaniumiza sana na kuapa kuwa Yule mwanamke ambae alifanya kila kitu kwenye familia yangu anatakiwa alipie kila kitu….
Miaka ikapita, tukaondoka Arusha na nikarudi na mama morogoro, nilikuwa nimeshakuwa bint mkubwa na wakat huo nilikuwa na miaka 20, na watu wengi walikuwa wananisifia na wengine wakawa wananiita mrembo fukara, kwa maana walikuwa wanadai kwa namna ambavyo nilivyo mzuri nilitakiwa kuishi maisha mazuri sana….
Siku moja nilienda kwenye nyumba ambayo nilikuwa naishi na wazaz wangu, nikakuta tangazo kuwa wanatafuta hause girl wawili, kwa maana ile nyumba ilipanuliwa sana na ikawa kama kasri, yaan tulikuwa tunaishi ghorofa moja ila kuna vyumba vya nje vikaongezwa, na yule mama alikuwa anawafanyakazi wake wa mpunga ambapo alikuwa anamashamba ya mpunga kilosa, ila alikuwa anaishi nao wote, kwa maan wafanyakazi wake wengi walikuwa ni vijana ambao bado wanajitafuta, sasa akawa anataka hause girl ambae atakuwa anasaidia kupika na kusafisha vyumba vyao, kwa maana walikuwa wanaenda kilosa kwa kupokezana, so hawakuwa na muda kabisa wa kufanya usafi kwenye vyumba vyao…..
Niligonga mlango na kumkuta mlinzi, Yule mlinzi ndio alikuwa mlinzi wetu, na nilipomuona nilidhan labda anaweza kunikumbuka na kusahau kuwa niliondoka nikiwa mtoto na nimeshakuwa bint sasa na Yule mlinzi alikuwa ameshazeeka, maana hata kipindi ambacho tulikuwa tunaishi pale alikuwa tayar ni mtu mzima…
“ unataka nn bint? Akauliza…
“ nimeona tangazo la kutafuta bint wa kazi, nikajibu…

“ ohhh pita pita dada madam yuko ndani na anataka kuondoka, ingia haraka haraka akuone kwa maana umekuja kwenye muda sahihi sana, akasema Yule mlinzi na kuniingiza ndani, na nikamkuta Yule shoga yake na mama yangu, nilipomuona nilishikwa na hasira sana, ila nikajikaza na kumsalimia kwa adabu….
“ unaitwa nani? Akaniuliza…
“ sikuwa nimejipanga kwa jina hivyo nikasema Joyce…
“ owww wow unaonekana una adabu sana na una jina kama langu, karibu bint kazi umepata na nitakuwa nakulipa laki moja na nusu kwa mwezi, “suzan, akaita Yule mwanamama kisha akaendelea kusema kuwa “ nimekuletea msaidizi huyu hapa njoo umpe majukum yake, akasema Yule mwanamama kisha akasimama na kuondoka zake, na kama utani nikajikuta nimeshapata kazi za ndani bila kutegemea….
NAKUJA….


ANNASTAZIA ( am just a maid) 2
HUSQER BALTAZAR

Sijui ni pesa au nini, kwa maana alikuwa anaonekana bint sana kulinganisha na mama yangu, ambae alikuwa anaonekana mzee sana, basi Yule suzan akanichukua kisha akaanza kunipa majukum pale, nikaanza kazi sasa…
Nikampigia simu mama yangu na kumuambia kuwa nimepata kazi, kwa maana nilimuacha nyumban kwao, kwa maana wazaz wake bado walikuwa hai, so walikuwa wanamuangalia, na rasmi nikaanza kazi kwenye jumba kubwa la kifahari ambalo lilikuwa ni jumba ambalo walijenga wazaz wangu…
Nilikuwa nina hamu sana ya kumuona Clinton, ila kuna mawazo yakanijia kuwa sitakiwi kumuwaza Clinton kwa maana yeye ndio anatakiwa kuwa target yangu, kwa maana naweza kumtumia kwaajili ya kulipiza kisasi kwenye ile nyumba…
Basi majira ya kama saa tatu usiku Yule mama alikuja, alikuwa pamoja na mwanaume ambae anaonekana kama anamiaka 28 mpaka 30, kwa umri wa Yule mama Yule kijana ni karibu sawa na kijana wake wa kumzaa, ila akawa anamuita mume wangu na majina mengi ya mahaba, ambapo nilikuja kugundua baadae kuwa baada ya baba yangu kufariki basi huyo kijana ndio akaamua kumuoa, kwa umri alionao huyo kijana ni lazima alikuwa na uoga wa kulima tu, na ni lazima kuwa atakuwa analelewa na Yule mwanamama…
Nikaambiwa niwatengee chakula, nikatenga, ila nikashangaa kuwa Yule mwanaume ananiangalia sana, ila sikumjali kabisa kwa maana sio kazi ambayo ilikuwa imenipeleka pale….
Ila Yule mwanamke hakuwa na adabu kabisa kwa mume wake, alikuwa anamgombeza hovyo, na kila wakat alikuwa anamuita kuwa hana akili, nilijisikia vibaya sana, maana niliamin kama sio umaskin basi huenda Yule mwanaume angekuwa na mwanamke wa ndoto zake, na sio Yule mama mtu mzima mwenye rika karibia na mama yake…..
Basi nikatenga pale, na baada ya kutenga nikaambiwa kuwa natakiwa kwenda kusafisha chumba cha madam, lakin nilipofika chumban kwake, nikakuta nguo zake za ndani zenye damu ya hedhi alikuwa ameziloweka, sikuzigusa nikatandika kitanda na baada ya hapo Yule suzana akanifata na kunambia kuwa nichukue na zile nguo za ndani tukazifue…
“ tunamfulia mpaka hizi? Nikauliza kwa mshangao..
“ ni kawaida , maana madam anajua tu kuoga na kula mwenyewe vitu vingine vyote hawez kuvifanya, nilishangaa sana, kwa maana kipindi ambapo alikuwa anaishi na sisi, alikuwa mchapa kazi sana, na alikuwa anapiga kazi kuliko hata mama yangu, na alikuwa mshapu mno, sasa inawezekana vipi awe hawez hata kujifulia nguo za ndani au ndio jeuri ya pesa nini, nikawa nawaza…..
Basi nikawa naogopa hata kuzishika, ila nikashangaa Yule mwanamama anavaa gloves, kisha akaziingiza kwneye washing mashine, nikaona nafuu, maana kufua madamu ya watu sio kazi rahisi…
Basi maisha yakaanza, ila kuanzia nafika pale sijawah kumuona Clinton hata kwa bahat mbaya, na sikuwa naweza hata kumuulizia, kwa maana watu wangenishangaa na wangeuliza nimejuaje, kwa maana hata muhusika mwenyewe bado hajajua kama mimi ndio Yule anasstazia bint ambae amemkosesha haki zake za msingi….
Basi siku moja yule mwanamama alikuwa ametuaga kuwa anaenda mkoani kikazi, kwa maana alikuwa anathamini sana pesa kuliko kitu chochote kile, kwenye majira ya kama saa nne kasoro Yule mume wake wa mchongo akaniita kisha akanambia kuwa nikamtandikie kitanda, na kiukweli sikukataa, nikaenda chumban na kuanza kutandika, mara nikahisi nakumbatiwa kwa nyuma…
Nilipotaka kujitoa, nikashangaa mtu analia, ikabidi nigeuke nimkumbatie vzr, kisha nikaanza kumpiga piga nyuma ya mgongo wake, ndio akazidi kulia, alilia sana kwa takriban dakika kumi nzima, nikaona maumivu ambayo alikuwa anayapitia, akaanza kusema “ sijui kama ni sawa kukuamin au laa, ila kukosa kwa wazaz wangu pesa za kunisomesha kumesababisha nimekuwa mtumwa, kuna watu wanaamin nina maisha , kwa sababu naendesha magari ya kifahari na nina ishi maisha mazuri, ila naishi kwenye hii nyumba, kana kwamba mimi sio mwanaume, nataman faraja na mimi, na taman kupendwa na kupenda kama binaadamu wengine, ila sijui kama naweza kutoka kwenye huu mtego ambao nimejitengenezea mimi mwenyewe, akawa analalamika Yule mwanaum…
Nilijisikia vibaya sana, ila sikutaka kujiingiza kwake, kwa maana hakuwa target yangu, basi nikaw namfariji pale, mpaka mwisho akatulia na kunambia, “ unaitwa nani?..
“ an, nikataka kutaja jina langu ila nikakumbuka kuwa sikujitambulisha kama anastassia kwenye hii nyumba bali nilijitambulisha kama joyce, hivyo nikajibu joyce….
“ unajina kama la huyu malay, ila una moyo mzuri sana, kama hautajal naweza kukuamin, kwa maana nahisi upweke sana kwenye hii nyumba, nan ataman kupata mtu hata mmoja wa kuyasikiliza maumivu yangu, akasema Yule mwanaume…
“ bila shaka, nikajibu, akanikumbatia tena kisha akaniambia “ asante sana joyce kwa kuwa upande wangu….
Alikuwa kama ana mzigo mzito sana moyon mwake, alikuwa anatafuta sehemu kwa kuutuwa, sasa mimi nikaanza kuogopa kwa maana tupo wafanya kazi wawili kwenye ile nyumba, mimi na huyo suzan, sasa niliogopa asije akanitafuta, nikamuomba mume wa madam kuwa niende nikamuangalie Yule mama, kwa maana alikuwa mtu mzima kidogo kisha nitarudi, nikamkuta jikon amesinzia, na sio siri anafanya kazi sana, na kabla mimi sijafika pale alikuwa anafanya kazi zote mwenyewe, so huwa anachoka mno…
Nikamgusa na kutaka aende kulala ndani, kwa tabu akiwa ana yumba yumba kutokana na usingizi aliokuwa nao akaingia chumban, na huku ndani tulikuwa tunaishi wanne tu, basi nikarudi kwa Yule mwanaume…
Aliponiona akanikumbatia tena kisha akanambia “ asante kwa kuja….
Akaanza kunielezea maisha yake mpaka akamuoa joyce, nilimuonea huruma sana, na ndio maana nilikuwa namshangaa kwa kijana mdogo kama yeye kuoa mwanamke mtu mzima kama madam joyce, basi tukawa tunapiga story pale, na siku hio hatukulala, na alikuwa anaonekana kuwa anataman kujua mambo mengi kuhusu mimi, ila sikutaka kumuambia jambo lolote lile, kwa maana sikuwa najua hata naanzia wapi kumsimulia na licha ya yote sijui kama ni ametumwa, au ni yeye mwenyewe ambae anataka kuwa karibu na mimi, maana sikuwa namuamin mtu kabisa…
Tulipiga story mpaka saa kumi alfajir, nikamuomba niondoke, kwa maana muda sio mrefu Yule suzana ataamka, na akikuta sipo huenda ikaleta shida..
Nikashangaa anamka na kuanza kunisaidia kufanya usafi, akasafisha nyumba yote na mimi nikaosha vyombo vyote, hapo nidhahiri niliona kuwa anataman sana kampan yangu, suzana anakuja kuamka saa kumi na mbili kasoro kila kitu kimefanywa, akauliza nimefanya saa ngapi, nikamuambia kuwa sikuwa nimelala so nilitaka nimalize kila kitu kabla sijalala…
“ ohhh mwanangu, haya kunyw chai uende ukapumzike, na kazi ambazo zimebaki nitazimalizia mimi, akasema suzana na hakuwa amemuona Yule mume wa boss, alikuwa anaitwa Octavian….
Basi Octavian alikuwa amesimama kwenye ngazi anatabasamu na nilipomuangalia akanikonyeza, nikatabasamu tu, kisha akaondoka zake….
Kweli nikaenda kunywa chai, kisha nikaenda kulala, kwa maana sio siri nilikuwa na usingizi sana, na mama hakuwa amerudi kwa maana alikuwa amesema kuwa atakuwa na safar ya kikazi kwa siku tano, na ndio kwanza alikuwa ameshamaliza siku moja kati ya siku tano…

Nikiwa nimelala nikashangaa nakuja kuamshwa, na niliposhtuka nikakuta ni suzana, akanambia kuwa anaenda sokoni, hivyo mimi niende nikamtengee baba, maana huwa anamuita Octavian baba licha ya kuwa anaweza kumzaa, kwa sababu ni mume wa madam…
Basi nikaamka, na kwenda jikon na ni kama Octavian alikuwa ananisubiri kwa hamu, na mara baada ya suzana kuondoka akaja jikon na kuanza kuandaa matunda na mimi, tukawa tunapiga story tu, na mimi ni muongeaji sana, so akawa anacheka mno, mwisho tukasaidiana kutenga vitu mezan, na akataka na mimi nikae mezan tule….
Sikukataa, ila wakat tunakula akawa ananiangalia sana, ikabidi nimuulize “mbona unaniangalia hivyo boss
“ sikuwah kukuangalia vizuri, ila sasa naweza kusema kuwa your soo pretty joyce”…
Haya sasa kazin kwangu kuna kazi, mume wa mchongo wa madam anaanza kunisifia unafikiri madam akijua kazi tunayo hatuna…..
ITAENDELEA ………

ANNASTAZIA ( am just a maid ) 3
HUSQER BALTAZAR

Nikatabasamu tu, kisha nikamuambia kuwa “ akumbuke yeye ni mume wa mtu so asinisifie sana…
Akatabasamu kisha akasema “ hauna haja ya kunikumbusha joyce, nakumbuka kila kitu, ila ndio kizuri nisikisifie, akasema octavian …..
Basi nikatabasamu, kisha tukawa tunaendelea kula, na muda wote akawa ananiangalia sana, tena alikuwa ananiangalia kwa jicho la matamanio kabisa, sikuwa nataman mambo yaende hivyo, kwa maana huyu mwanaume hakuwah kuwa lengo langu, ila kwanamna ambavyo alikuwa ananitizama, nikapata wazo, la kumfanya joyce alipie kwa kumsaliti mama yangu, na kutembea na baba yangu, nikajiambia kuwa, “ mume wako ameingia mwenyewe kwenye mpango wangu joyce, ni lazima usikie maumivu ya kuchukuliwa mume….
“ usiniangalie hivyo bwana boss, unanifanya nisikie aibu, nikasema
“ naomba usiniite boss bwana, naitwa octavian, akasema octavian …
“ naogopa kukuita hivyo, kwa maana madam akijua anaweza kunifukuza kazi, na licha ya yote bado wewe ni mume wa madam, na natakiwa kukuheshimu kama boss wangu…
“ ohhh joyce, naomba usinifanye nijisikie vibaya sana, nadhan jina Octavian likitoka kwenye kinywa chako, linaweza kunipa msisimko wa ajabu sana, akasema octavian ..

Nikatabasamu kisha nikasema “ sawa octavian , nikashangaa nay eye anatabsamu, niliona ananirahisishia sana kazi yangu, kwa maana kumpata mtu mmoja ambae yupo upande wangu na ni mtu wa karibu sana kwa joyce, ilikuwa ni hatuwa kubwa sana kwangu, kwa maana niliamin kw klupitia octavian naweza kujua mambo mengi ya siri ya joyce ….
“ your soo cute joyce, akasema octavian nikatabasamu kisha nikasema “ for you handsome …
Aisee octavian akaachia tabasamu lile kutoka moyoni kabisa, kisha akanambia “ nataman hizi shida zisingekuja upande wangu, alafu nikakutana na wewe, huenda sasa hivi ungekuwa mke wangu, na sio huyu shetani…..
“ una maanisha umenipenda kwa maana sikuelewi? Nikauliza…
“ mbona una shangaa sasa, kwani kuna ubaya gani kwa mimi kukupenda, kwa maana kwani haujawah kusikia love at the first sight, yaan huwez kuamin kuanzia siku ya kwanza kukuona nilijiambia kuwa “ wewe ni wangu, akasema octavian na mimi nikajikuta natabasamu……
“ umenipenda haraka sana, mpaka nimeshanga , sidhan kama unanifahamu vzr, mpaka uanze kunipenda ghafla hivyo, nikasema …
‘ kwani mapenzi yanawakat, au mapenzi yana muda maalum, yaan akishatokea mtu tu, moyo wenyewe na kihere here chake unaanza kuhangaika, joyce naomba usinishangae sasa, kwa maana wewe ni zaidi ya mwanamke, nimekaa na wewe kwa muda mfupi lakin nahisi kabisa wewe pekee ndio unaweza kuniondolea upweke, akasema octavian ….
Nikatabasamu kisha nikasema “ naomba iwe siri, na naomba usije ukafanya jambo lolote lile la ajabu mbele ya mtu yoyote kutokana na hisia zako kwangu, kwa maana sitaman kupoteza kazi yangu…
Octavian akatabasamu kisha akasema “ usijal na nitafanya kila unalolitaka na na nitahakikisha sikupi wakat mgumu…
Basi akanisaidia kuondoa vyombo na kuviosha, kisha nikamuomba akakae chumban kwake, kwa maana suzana alikuwa anakaribua kurudi na sikuwa nataka kabisa, ahisi jambo lolote lile kati yangu mimi na Octavian……..
Suzana akarudi na akanipa majukum pale, ila ni kama octavian alikuwa ameshanogewa, maana kila dakika alikuwa anakuja kunichungulia jikon, na kila saa anajifanya anasikia kiu, lengo ni anione, nilikuwa namshangaa sana, mpaka nikahisi huenda ananipima, kwa maana sina hata mwezi kwenye ile nyumba, na sijawah kulala nae hata mara moja, sasa mbona kama amechanganyikiwa sana juu yangu? Ni swali ambalo nilikuwa najiuliza , nikijua ni mpango , kumbe ni kweli octavian wa watu alikuwa ni mpweke sana na anataka faraja kutoka kwangu……
Siku zilienda, na kila ambapo octavian alikuwa anapata nafasi, basi alikuwa anatumia muda wake pamoja na mimi, kwa maana alikuwa ananiona kama faraja yake ya pekee,,

Basi siku tano ziliisha na madam akarudi, yaan siku ambayo alikuwa anarudi octavion alikuwa analaan siku nzima, kwa maana ni kama alikuwa anataman hata angefia huko huko, alipofika tu akamfata octavian kisha akamkumbatia na kusema, “ leo nataka unifanyie massage baby, nilikumiss sana, na wakat huo mimi na suzan tupo ukumbin tunatenga tenga, ila wakat wote macho ya octavian yalikuwa kwangu……
Basi tukatenga na baada ya kutenga pale, wakaanza kula, ila octavian hakuwa na raha kabisa, alikuwa anatafuta sababu ya kunituma tuma ili nipite pite anione, ila nilijua lengo lake na kama ningetii anachokitaka basi huenda madam joyce angehisi kitu, na huenda ingesababisha kuharibika kwa mipango yangu….
Sasa nikawa namsukumizia suzana, na hakuwa anashida, akawa anaenda yeye kutenga na kupeleka kila ambacho octavian alikuwa anakitaka…
Basi mida ikaenda kama kawaida, na madam akamkokota octavian na wakaanza kwenda chumban, ila wakat wote octavian alikuwa anaangalia nyuma kuniangalia mimi….
Basi na sisi tunaenda kuendelea na majukum yetu, kwa maana mama akiamka huwa sisi tunaamka saa kumi na moja kasoro, kwa sababu huwa anataka saa kumi na moja kamili, maziwa yake na cake viwe tayar amepelekewa chumban kwake na nahisi octavian ndio alikuwa analisha, kwa kifupi octavian alikuwa kama s*x toy wa madam….
Basi mimi nikaamka mapema kwenye saa kumi kasoro, kwa maana suzana hakuwa anajisikia vzr kabisa, ila ni kama octavian alikuwa ananisubiria nitoke chumban kwangu, kwa maana alikuja na kunikumbatia kwa nguvu kisha akasema “ haujui ni kiasi gani ulikuwa unanitesa wakat ambapo nilikuwa nataka kukuona alafu unanikwepa….
“ samahan sana octavian, ila hii ni kazi yangu, na nikifukuzwa hapa nitaenda kuishi wapi? Nikasema …
“ utaenda kuishi na mimi, akajibu octavian, nikaona eheee hapa kazi ninayo……
“joyce Napata faraja sana nikikuona, na naomba unisamehe sana kuhusu huu usiku, kwa maana sikuwa na chakufanya zaidi ya alichotaka madam, ila nakuahidi kuwa hichi kitu hakitadumu, na nitahakikisha nakuwa na wewe muda sio mrefu, akasema octavian …
Nikakubaliana nae pale, kwa maana sikuwa nataka mambo yawe mengi, kisha nikamkiss kwenye shavu na kusema “ naoba nikaendelee na kazi octavian tutaongea baadae, kisha nikaondoka zangu, na nilipogeuka kumuangalia nikashangaa namuona ameshika shavu lake kisha akawa anatabasamu, mpaka nikajiskia vibaya kwa maana mimi nilikuwa nataka kumtumia na maskin ya mungu kijana wa watu amenipenda kweli….
Basi nikaandaa hayo maziwa na keki ya madam, yaan sikuwa naamin, yaan mtu alio saidiwa na mama yangu, leo hii namtukuza na kumuita madam, kwenye nyumba ya wazaz wangu mwenyewe, eee mungu nisaidie…..

Basi kulivyopambazuka madam alikuja na kutuambia kuwa siku hio saa saba mchana kutakuwa kuna ugeni so tuandae mazingira, ila hakuwa ametuambia ni ugeni gani…..
Kweli madam aliondoka na mume wake octavian, na mimi pamoja na suzana tukabaki kuandaa mazingira ya chakula cha mchana cha hao wageni…
Kweli kabla ya saa saba madam alirudi pekee yake bila mumewe, na kweli kwenye majira ya saa saba kama na robo tukashangaa gari linakuja na akashuka kijana mweusi amepanda hewan, anakifua cha mazoezi, madam akamkimbialia kisha akamkumbatia na kusema “ karibu nyumban mwanangu…
Ndio nikagundua kuwa Yule aliekuja alikuwa ni Clinton……..
Basi baada ya mama na mwana kukumbatiana Yule Clinton akawa anaingia ndani, akampita suzana, ila alipofika kwangu alishtuka sana kisha akasema “ annastasia …..
NAKUJA……..


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote