AMARA (Binti Wa Mvuvi)

book cover og

Utangulizi

LAANA ILIYOVUNJWA KWA UPENDO
maisha ni kama fumbo, muda mwingine unaweza kuwa mwema lakin ukaonekana muovu mbele ya jamii ambayo haujawah kuikosea kabisa...
Sijui kwanini mtoto alielelewa na mzaz mmoja anaonekana kama hana maadili na kuzuliwa mambo yote mabaya katika jamii yake...
Bint amara, bint mwenye maadili sana anataka kubakwa na mmoja wa kijana kwenye kijiji chao, amara anajaribu kujitetea ila hakuna atakae muamin kwa sababu amelelewa bila mama, na kuonekana kama yeye ndio alijipeleka kwa mwanaume...
Amara anaonekana bint malaya asie na maadili, na watu wite kijijin wanamnyooshea kidole mpaka pale alipokutana na kijana wa kitajiri ambae aliijua thaman ya amara na akasimama nae kuwaonesha watu kuwa amara ni mwanamke bora sana, binti wa mvuvi amara anakuwa ni bint anaeheshimika sana baada ya kukutana na huyu kijana wa kitajiri ambae alibadilisha hatma yake na kutengeneza heshima yake kijijin...
Hapa kuna love story moja tamu sana, hakikisha haukosi mkasa huu kwenye link ya tupo hapa pekee

AMARA BINTI WA MVUVI 1
MTUNZI SMILE SHINE

Kwa majina naitwa Amara karimu ni binti wa miaka 18,kwenye familia yangu naishi na baba yangu na mtoto pekee kwenye familia yetu, sijawahi kupata malezi ya mama wala upendo wa mama kama ilivyo kwa watoto wengine, simfahamu mama yangu ila namuona tu kwenye picha na wala sijui alipo ila nilishawahi kupewa story ya mama na baba yangu, wawili hawa hawakuwahi kufunga ndoa wala kuishi pamoja. Kuzaliwa kwangu ilikuwa ni bahati mbaya baba alimpatia mimba mama yangu wakiwa bado na umri wa harehe waliishi kwa wazazi wao. Wazazi wa mama yangu yani babu na bibi walikuwa wa kali sana kwa baba . kwakuwa walikuwa na pesa waliiandama sana familia ya baba kwa kumtishia kumfunga baba yangu kwa madai ya kumuharibia maisha binti yao ambae alikuwa bado anasoma. Ilimbidi baba yangu aondoke na kwenda mbali ili kunusuru maisha yake.

Baada ya mimi kuzaliwa nililelewa kwenye familia ya mama yangu baada ya kufikisha miaka minne nilipelekwa kwa wazazi wa baba ambae alikuwa ni bibi tu. Kwani mama yangu alienda mji mwingine kuendelea na masomo na pale nyumbani kila mtu alikuwa bize na mambo yake hakuna ambae angeniangalia
" Mama karimu nimekuletea mzigo wenu hapo tulipowalelea yanatosha sana na nyie pambaneni kwanza huyo mwanao hana hata mpango wa kumlea huyu mtoto hatumii hata hela ya sabuni au unafikiri pesa tulizokuwa nazo ni kwaajili ya watoto wanaokuja kwa bahati mbaya?
Aliongea bibi mzaa mama kwa kero na dharau kisha akanitelekeza na kuondoka.
Bibi yangu mama karimu alichukua jukumu la kunilea huku baba yangu akiwa kisiwa cha Manga akiendelea na kazi zake za uvuvi .

Alipopata riziki kidogo alikuwa akitumia pesa kwaajili ya kujikimu na maisha yetu yakasonga. Bibi alinilea vizuri na kujifunza maadili mema. Pia alinionyesha upendo mkubwa mno.

Nilipofika umri wa kuanza shule nilipelekwa shule na bibi yangu kipenzi.
Nilipofika darasa la tano bibi yangu aliniacha aliaga dunia. Hapo ndipo baba yangu alikuja tulipo maliza mazishi tuliondoka na kwenda kisiwani Manga.
Huko niliendelea na masomo yangu mpaka nilipomaliza darasa la saba. Matokeo yakatoka nilikuwa nimefanya vizuri nikaendelea na masomo ya sekondari nilipofika kidato cha tatu nilipata mtihani ambao ilivuruga ndoto zangu zote na kunifanya niishie kwa tabu pale kisiwani.

Siku moja baba yangu alikuwa anaumwa hivyo hakuweza kufika kwenye shuhuri zake za uvuvi .
Ilipofika usiku aliniambia.
" Amara mwanangu unaona hali yangu haipo sawa na hapa ndani hakuna pesa wala kitoweo sasa nilikuwa naomba kesho mapema uende pwani ukamsubiri Nassibu akipatiwa pesa kidogo kwaajili ya kwenda kulipia mitihani yako huko shule na nyingine kwaajili ya matumizi ya hapa nyumbani pia akupatie samaki kwaajili ya mboga.
" Sawa baba .

Usiku ule tulilala hatimae kulikucha mapema sana Mida ya saa kumi na moja alfajiri niliamka nikatoka kuelekea pwani kumsubiri Nassari anipe hiyo pesa ili niwahi kurudi nijiandae kwenda shule.
Nilitembea njiani nikiwa sina hofu lakini ikawa ghafla sana mtu akatoka mbele yangu. Nilishtuka na kumuuliza
" Wewe nani?
Yule mtu hakujibu zaidi aliniambia na kunivutia sehemu yenye miti na majani. Nilijaribu kujitetea lakini yule mtu alikuwa na nguvu sana , niliamua kupiga kelele akataka kuniziba mdomo nikamngata kidole. Kelele zangu ziliamsha watu . Walitoka kwenye nyumba zangu na kuja kunisaidia. Yule mtu alivyoona watu wanakuja akataka kukimbia lakini ilikuwa bahati walimdaka. Tulimmulika usoni na tochi tukagundua ni Yona kijana wa pale pale kijijini.
" Yona ulikuwa inamfanya nini mtoto wa watu?
" Alikuwa ananivutuga kwenye majani . Nilijibu nikiwa nalia huku nikihema.
" Kwahiyo ulitaka kumbaka ?
" Hapana jamani ngoja niwaambie ukweli.
" Sema haraka kabla hatuja chukua maamuzi magumu.
Baada ya kuzushiwa Yona akaanza kujitetea yani daaah, eti alisema
" Amara mimi ni mwanamke wangu na usiku alilala kwangu.....
Yani nilitoa macho huku nikiwa nashangazwa na maneno ya Yona.
" Yona acha kunisingiuia mimi sijui hata ndani ya chumba chako kuna nini.
" Acha Yona aendelee kuongea.
" Ndio alilala kwangu na sio mara moja leo imejulikana kwasababu kakutana na nyoka ndio akawa anapita kelele.

Nilijaribu kujitetea na kusema ukweli lakini Watu walimuamini Yona kuliko mimi. Nilichukuliwa na watu wa zima wa pale nikarudishwa nyumba na baba akaelezwa ilivyokuwa.
" Hiyo ndio tabia ya mtoto wako analala kwa wanaume kwanza tabia mbaya mapema sana na hii yote ni kwasababu hajapata malezi ya mama.
" Jamani sio kweli Amara nilimtuma na wakati anaondoka nimemsikia anafungua mlango. Masikini baba yangu alijitetea sana lakini hakuna aliyeweza kutuamini walizidi kumlaumu kuwa eti kanidekeza , sina malezi bora nipo huru sana ndio maana nimeharibikiwa mapema.

Baada ya watu kuondoka waliniacha na baba nilijikunyata nikawa nalia.
" Amara ni kweli umefanya, huwa unafanya hayo niliyoambiwa?
" Hapana baba sijawahi kufanya ujinga wowote wananisingizia.
Baba alimuangalia kwa huruma kisha akasema
" Basi binti yangu futa machozi mimi baba yako nakuamini sana tu.
Nilipata faraja kwa kuaminiwa na baba yangu lakini huko mitaani na shule hali ilikuwa mbaya sana, nilisema vibaya na kutukanwa shule karibia walimu wote walinichukia, marafiki walikimbia . Wazazi wao waliwakamata kuwa karibu na mimi wakidai nitawafundisha tabia mbaya.
Kutokana na maneno kulikosa amani hata shule nikawa sielewi kitu niliamua kuchukua maamuzi ya kuacha shule . Baba alikuwa akimuomba sana niende shule nimalize masomo yangu lakini sikuweza nilimjibu.
" Baba kama nasoma ili nipate kazi, nipate pesa ya kuendesha maisha yangu basi nakuhakikishia sita pata shida kwenye haya maisha na kama nilikuwa nasoma ili kuondoa ujinga basi mwanao sio mjinga tena najua kusoma na kuandika hata kingereza cha kuombea maji si haba nakijua mimi shule tena basi. Niliongea kwa kujiamini mno mbele ya baba yangu kipenzi ambae nilimsikiliza kwa kila alichoniambia ila kwa hili aligonga mwamba.

AMARA BINTI WA MVUVI 2
MTUNZI SMILE SHINE

Amara aliamua kufumba Macha na masikio hakutaka kuona wala kusikiliza nini walimwengu wanasema juu yake maana aliamini maneno yao yatamrudusha nyuma nae anataka kupambana ili atoboe na kuweka heshima .
Amara alianza kwenda baharini alichukua samamaki aliibua baba yake na kuwasafisha , alimsaidia kuuza na nyingine alikaanga na kuuza. Mwanzo watu hawakutaka kununua kwake wakidai mchafu lakini hakukata tamaa aliendelea kupambana na wateja wake wakubwa walikuwa ni watu kutoka nje ya kisiwa . Mungu wangu alimfungulia njia nikawa nauza na kumaliza mapema sana baada ya kumaliza nilirudi nyumbani kufanya shughuli zangu.

Siku moja nikiwa naelekea pwani kumsaidia baba kuandaa samaki nilikutana na Yona njiani, nilimpata pembeni kama kirusi hatari.
" Amara umepita mwaka sasa bado unakinyongo na mimi?
" Kwani wewe shetani bado una hamu ya kutimiza kile alichotaka kunifanyia au unataka kuja na mpango gani dhidi yangu?
" Sikiliza Amara.... Aliongea Yona huku akinisogelea na mimi nilirudi nyuma.
" Sasa ndio nini unanikimbia? Aliuliza na mimi nikaona mbona kama hakuwa mpumbavu kuendelea kusimama nae anaweza kujiletea matatizo mengine niliamua kuondoka.
" Sasa unaenda wapi ? Tunatakiwa kuongea ili mambo yawe sawa alafu ujue mimi ndio mume wako . Hilo neno la mwisho lilinifanya nisimame na kugeuka kumuangalia.
" Unaongea ujinga gani wewe hayawani?
" Amara kwa kile kilichotokea unafikiri unaweza kuolewa na nani hapa kisiwani?
" Mmmmh yani hata ikitokea kukawa na wewe Yona na pembeni yako akawa jini nikaambiwa nataka kuolewa na nani nipo radhi kuolewa na jini kuliko wewe. Tena kuanzia leo naomba usome kunifuata fuata.
Niliongea kwa hasira kisha nikaondoka . Nikifika pwani nikamkuta baba na nasibu wameshafika baba anahesabu samaki na kumpatia Nassibu alipeleke kwenye soko la jumla.
" Baba nenda kapumzike hiyo kazi iliyobakia nitaifanya mimi.
" Acha nikusaidie binti yangu.
" Hapana ni kazi ndogo sana kwangu , wewe umekwisha ukiwa baharini na usiku unatakiwa kwenda kuvua huu ndio muda wako wa kurudi nyumbani na kwenda kupumzika.
Baba alimuangalia na kuachia tabasamu la mbali.
" Afadhali hata nina binti wa kumuonea huruma, asante sana mwanangu.
"Nakupenda baba.
Ni kama machozi yalianza kulenga machoni kwa baba aliamua kuondoka, alipiga hatua chache akageuka kumuangalia wakati huo nilikuwa nimevaa chini na kuvuta beseni la samaki ili nianze kazi.
" AMARA! Baba aliingiza nikanyanyua kichwa kumuangalia .
" Nakupenda sana binti yangu.
Nilitabasamu nae akageuka na kuendelea na safari.

Siku hiyo nilifanya kazi kwa juhudi kubwa sana , huwa inatokea hivyo pindi ninapokuwa na hasira.
Nili maliza kuandaa samaki watu walioweka oda walikuja kuchukua na waliobakia nilienda kukaanga kwaajili ya wateja wangu . Siku hiyo nikaanza na kumaliza samaki mapema sana . Sikurudi nyumbani niliamua kwenda kwenye fukwe ya bahari , nilikuwa natembea tembea fukweni huku nikishuhudia jua likizama .
Nikiwa naendelea kutembea huku nikikanyaga maji yaliyokuwa yanaletwa na mawimbi mara nikasikia sauti kama ya mtu aliyeumia nilipofika kumuangalia niliwaona wanaume wawili mmoja alikuwa kunyanyua mguu wake juu kama vile kanyaga mwiba na mwingine alikuwa anamkagua mguu wake. Mara walienda kukaa kwenye mchanga wakawa wanakagua ule mguu.
" Ni kijiwe chenye ncha kali kimekuchoma tunatakiwa kwenda zahanati ukapatwa matibabu. Yule mwenzie alimwambia na kumfanya awe na wasiwasi.
" Basi tafuta usafiri unipeleke.
Nilihisi kuna tatizo nikaenda mpaka waliokaa bila hata ya salamu nilishika ule mguu na kuvuta kile kitu kilichomchona yule kaka aling'ata meno kwa maumivu.
" Pole ni kitu kidogo sana na hakina madhara haina haja ya wewe kwenda hospitali.
" Lakini panavuja damu. Alisema yule mwenzie
" Nenda kalete maji ya bahari tummwagie.
" Sasa hayo maji nitachota kwenye nini? Yule mwenzie aliuliza nikamuangalie na kumwambia
" Nenda kachote na mdomo wako.
Yule kaka mgonjwa alijikuta anacheka kwa jibu nililompa mwenzie.
"Sasa ni jibu gani hilo , na nawezaje kuweka maji ya bahari mdomoni kwangu? Yule kaka alipaniki nikaona isiwe shida nilisimama nikaenda kuchukua jumba la konokono nitachota maji nikaenda kumsafisha yule kaka kisha nikachana kitambaa changu na kumfunga vizuri.
" Usijali utakuwa sawa japo utapata maumivu kidogo.
" Asante nashukuru kwa misaada wako.
Alisema yule kaka na mimi niliondoka na kuwaacha wananiangalia.

Kila siku nilikuwa na kuendelea na biashara zangu baadhi ya watu pale kisiwani walianza kujirudia na kuja kuniambia jinsi walivyokuwa wakisema huko pembeni.
" Yani yule mama nasma alikuwa akisema sana utafikiri hana watoto wa kike na angejua sasa huyo nasma wake anavyogaragazwa kwenye Mitumbwi wala asingekuwa na nguvu ya kuongelea vibaya watoto wa wenzake. Nilikuwa nawasikiliza na jibu langu lilikuwa moja tu
"Nafsi yangu imekataa sijali nini wanasema juu yangu kikubwa Mungu wangu anajua kutenda haki basi atanitendea . Nilipomaliza kuongea hivyo niligeuka macho yangu kuangalia mteja aliekuwa kasimama mbele yangu.
" Nilikutana uso kwa uso na wale wakala nilipokutana nao ufukweni, niliacha tabasamu na kuwakaribisha.
" Karibu wateja wangu.
" Asante tunahitaji hao samaki wakubwa wawili . Alisema yule kaka ambae hakuwa kaumua na yule aliekuwa kaumia alikuwa kanikazia macho.
Siku kali sana nilichukua gazeti na kutaka kuwafungia lakini wakasema watakula hapohapo. Nilichukua sahani nikawe.
" Tuweke na ndizi mbili mbili usisahau pilipili kwa wingi.
Niliwahurumia kama walivyotaka kisha nikawaambia.
" Tangulieni kwenye benchi nawaletea.
Walitangulia na mimi nikawafuata nyuma nikawazengea na kuwanawashi mikono.
Yule mgonjwa alikuwa wa kwanza kunawa , alinawa huku akiniambia.
" Mbona huulizii hali ya mgonjwa wako?

AMARA BINTI WA MVUVI 3
MTUNZI SMILE SHINE

Niliacha tabasamu kisha nikasema.
" Nilikumbuka kuuliza ila mpaka umefika hapa upo sawa.
Mara nikasikia naitwa
" Amara njoo basi utuuzie huku.
" Nakuja.
" Amara jina zuri sana, naitwa Yazid.
" Pia unajiona zuri. Nilimjibu na kumuangalia mwenzie
" Naitwa Hizir.
" Nimefurahi kuwafahamu na karibuni sana.
Walionekana kutamani kuendelea kuongea na mimi lakini wateja walikuwa wananiita sana ilinibidi niende kuhudumia.
Kiliendelea kufanya kazi zangu mara kwa mara nilijikuta nageuka kuwaangalia nao walikuwa wananiangalia .
Walimaliza kula wakaja kunilipa pesa yangu
" Asante kwa huduma yako nzuri.
" Sawa na nyie karibuni sana.
" Asante Mungu akipenda kesho zitakuja tena hakikisha unatuwekea samaki wakubwa wenye Minofu. Alisema Hizir kisha wakaondoka.
Kesho yake mapema walifika sehemu ya nguo ya biashara tukasalimiana kisha Hizir akasema
" Fanya kama jana.
" Sawa.
Nilijisikia wateja waliotangulia kisha nikawahudumia na wao.
Kwakuwa siku hiyo sikuwa na wateja wengi na mzigo ulikuwa wa kumalizia nilikaa pembeni yao tukawa tunaongea mawili matatu. Yazid alionekana kuhangaika kumla yule samaki nilikuwa namuangalia kwa jicho la kuibia huku nikitabasamu yani alikuwa kama mtoto , alijifanya nikumbuke nilipokuwa mdogo bibi yangu alipokuwa ananitolea Minofu ya samaki akihofia nitajivhoma au kukabwa . Nikiwa nakumbuka nikimuona Yazid kashituka na kujiangalia kidole chake, alikuwa akichomwa na mwiba. Nilinyanyuka na kusogea alipo nikachukua ile sahani na kuanza kumchambulia Minofu huku mimba nikisema pembeni. Yazid alikuwa akiniangalia sana usoni niliponyanyua uso kumuangalia akasema.
" Nilijichoma bahati mbaya.
" Najua ila nimeona nikusaidie chukua endelea kula.
Yazid alishindwa kuchukua alimgeukia Hizir wakati huo Hizir alikuwa anakula huku akituangalia.
" Boss wangu kula bwana acha kuniangalia. Samaki mtamu huyu ila nahisi samaki wa Yazid atakuwa mtamu zaidi .....
" Hizir unavuka mipaka sasa.
" Samahani.

Nili maliza kutoa mimba nikakupatia sahani yake , alipokea na kusema kwa sauti ya chini
" Asante.
Walipomaliza kula waliondoka na mimi nilikuwa ya vitu vyangu nikaondoka

Siku zilizidi kwenda wakawa wateja wangu wakubwa sana pia tulizoea na sana . Siku moja tukiwa tumekaa walipita wasichana waliponiona nimekaa na wakina Yazid walicheka na kusema
" Sasa umehamia kwa watu wa mjini laiti wangejuwa tabia yako wala wasingeweza kukukaribia.
Kila mtu alijua naambiwa mimi ila nilivunga kama sijasikia.
" Hivi hawa wasichana wanashida gani mara kwa mara wanapita na mafumbo kwani una tatizo nao? Hizir aliuliza nikajikuta navuta pumzi na kushusha alafu nikamjubu
" Katika hii dunia sio kila mtu atakupenda hivyo sishangai kwa wao kuwa maadui kwangu.
" Nimeipenda hiyo wewe ni mtu mwenye akili sana.
" Ni kweli yupo tofauti sana.
Siku ya jumapili ilikuwa ni siku yangu ya mapumziko, majira ya jioni nilienda ufukweni kupunga upepo kwa mbali nikimuona Hizir akiwa kakaa nilimfuata na kukaa pembeni yake.
" Mbona upo pekee yako hapa mwenzio yuko wapi?
" Wewe yule sio mwenzangu ni boss wangu .
" Boss wako kivipi?
" Mimi ni bodyguard wake.
Nilicheka huku nikimuangalia alafu nikauliza
" Nini? Mbona haonekani kama unafanya hiyo kazi upo kama rafiki kwake.
" Ndio ni marafiki ila kazi yangu ni kumlinda.
" Kwanini umlinde, anashinda gani kwani?
Hizir alisita kusema na mimi nilimkatania nilitaka kujua sababu ya Yazid kulindwa au ana wadhifa gani mpaka alindwe.
" tuachane na hayo maongezi. Hizir alisema baada ya kumuona Yazid akija tulipokaa.
ikabidi nitulie japo nilikuwa na shauku ya kutaka kujua .
" Amara na wewe upo hapa?
" Ndio nimekuja kupunga upepo wa pwani bahati nikamuona Hizir nikaona sio vibaya kuja kumsalimia.
" Sawa umefanya vizuri. Yazid alikaa kisha akamwambia .
" Hizir kaletee madafu.
" Sawa.
Hizir alitaka kunyanyuka lakini nikawahi kuwaambia
" Acha niende nikawachukulie.
" Angeachia aende Hizir.
" Mitumbwi mimi hakuna tatizo.
" Sawa. Hizir alitoa pesa akanipatia nikaenda kununua madafu matatu alafu nikawapelekea.
" Naweza kuwaacha sasa....
" Wewe binti acha kichaa chako hebu kaa hapo unywe dafu lako.
" Mimi huwa nakunywa kila siku nyie kunyweni maana sidhani kama huko mjini yanapatikana kirahisi.
" Basi sawa tunaomba ukae na sisi. Alisema Yazid kwa sauti ya utaratibu na mimi nikaamua kukaa nao.
Yazid alikuwa akiniangalia sana kuna muda alizubaa akiniangalia na mawazo yake kuwa mbali.ilinibidi na mimi nimeshangaa tukawa tunaangalia na , Hizir alimshika begani na kutingisha, Yazid alishituka akageuka kumuangalia.
" Vipi kaka mbona sielewi au.... Yazid alimkatisha kwa kuuliza.
" Nini? Na tangulia hotelini.
" Siwezi kukuacha uende mwenyewe.
" Nipo sawa nako na Amara.
Yazid aliondoka Hizir akimsindikiza kwa macho alipofika mbali akageukia kwangu.
" Ana tatizo gani?
" Huenda ajisikii vizuri.
" Sasa mbona ametaka kwenda mwenyewe ungependa kumsaidia.
" Usijali atakuwa sawa.
" Haogopi kibarua chako kuota nyasi?
Hizir aliachia tabasamu alafu akasema
" Nilikuwa nakutania mimi na Yazid ni marafiki na tupo hapa kwaajili ya kufurahia maisha si unajua sehemu kama hizi zinafanya akili kuwa sawa na kizuri zaidi nikiwa nimekaa na mtoto mzuri kama wewe.
Niliingia kutabasamu tu kwasababu Hizir alikuwa ni mtu wa mambo mengi sana.
Tulikaa pale mpaka kuigiza kilipoanza kuingia nilimuacha ili nirudi nyumbani.
" Hizir muda umeenda narudi nyumbani.
" Naweza kukusindikiza?
Nikifikiria kwanza kabla sijatoa jibu maana naweza kukubali nikawapa cha kusema watu wa Manga.
" Nitakwenda mwenyewe.
" Amara naomba unipe nafasi ya kukusindikiza kwani nafurahia kuwa karibu na wewe.
Nilishangaa na kumuuliza
" Kwanini ufurahie kuwa karibu na mimi?
" Sababu wewe ni waridi kila anaejipenda na anayetaka kumuoa basi lazima atamani kuwa karibu na wewe.

AMARA BINTI WA MVUVI 4
MTUNZI SMILE SHINE

Nilimkazia macho Hizir ni wazi maongezi yake yalikuwa yana maanisha kitu fulani hata macho yake yalienda sambamba na kile alichokiongea. Niligeuka taratibu na kuanza kupiga hatua ndogo nikiondoka, kumbe Hizir anifuata na kumshika mkono wangu.
" Amara umekasirika kwa kile nilichokiongea?
" Hapana, ila siwezi kuongozana na mwanaume ambae sina unasaba nae kwasababu sina ujasiri wa kuvumilia tena matatizo.
Hizir hakueleza ninachokiongea wala ninacho maanisha ilimbidi aulize.
" Unamaanisha nini kusema hivyo? Ni matatizo gani unaongelea?
" Ni story ndefu sana na huwa sipendi kusimulia kwasababu huwa naumia sana ninapokumbuka.
" Labda ungeniambia ningeweza kukusaidia .
" Usijali wewe rudi hotelini, uwe na usiku mwema. Niliongea kwa upole kisha nikaondoka nilipofika mbele kidogo nikageuka kumuangalia alikuwa bado kasimama ananiangalia jinsi ninavyotokomea.

Zilipita siku mbili nikawa sijaenda kwenye biashara zangu kwasababu baba yangu alikuwa mgonjwa nikawa namuhidumia pale nyumbani.
Ilikuwa majira ya jioni nilikuwa natoka dukani kununua mafuta ya kupikia , wakati narudi nyumbani nilikutana na wanaume wawili ambao walinisimamia mbele yangu nilipojaribu kusogea pembeni walikaa tena mbele yangu.
" Unaogopa nini Amara? Alikuwa ni kijana mmoja anaitwa Azan.
" Unataka nini Azan?
" Mimi na rafiki yangu tunakutana wewe ukatupe burudani maana hapa tulipo tuna ugwadu na kuhusu pesa tunazo za kutosha tutakupatia kiasi anachotaka.
Hiyo kauli iliniumiza sana ilikuwa ni dharau kubwa sana kwangu sijui kwanini walinichukulia mimi ni malaya kiasi kile yani kila mwenye shida zake za kingono aje kumalizia kwangu nilimsukuma Azan kwa hasira mpaka akaanguka yule mwenzie akanishika kwa nguvu na kuniburuza sikujua alitaka kunipeleka wapi
" Hebu niachie huko.
" Hebu tulia huko unajifanya mtulivu kumbe jamvi la wageni, hapa manga kila mtu anajua wewe ni cha wote inakuwaje kwetu uwe mgumu sasa leo unaenda kutoa show kwa sisi wawili.
Nilijaribu kupambana na baadhi ya watu walikuwa wanapita lakini hakuna aliyeweza kutoa msaada waliangalia na kupita lakini ikawa ghafla alitokea mtu na kutoa msaada kwangu. Sio mwingine alikuwa ni Yazid , hata mimi nilishangaa kumuona pale muda ule.
" Nyie vijana mnjaribu kufanya nini?
" Kaka pita kama wenzako wanavyopata hili halimuhusu.
" Siwezi kukubali kuona mwanamke anaonewa.
Yazid aligombana na wale wapumbavu. Yule mwenzie alikimbia na Azan alikuwa mikononi mwa Yazid.
" Amara ongozana na mimi.
Yazid alishikilia suruali ya Azan kwa nyuma huku akimsukuma na mimi nilimfuata nyuma huku nimeshika kichupa changu cha energy kilichokuwa na mafuta ya buku. Tulielekea kituo cha polisi Yazid alimsukuma Azani mpaka akataka kuanguka.
" Jamani vipi?
" Nimemleta huyu Kibaka alitaka kumbaka huyu binti.
" Sio kweli tulikuwa tumekubaliana.
Nilivyosikia hivyo nilihisi akili yangu inaruka nikajua lile tukio lililonitokea mwanzo linataka kujirudia na kashfa itarudi upya masikini Amara mimi nina mkosi gani na hawa vijana wa Manga.
" Amara ni kweli?
Yazid aliuliza
" Hapana sijakubaliana nae walinivamia na kutaka kunivutia kichakani huku wakijitolea maneno ya kunidhalilisha
" Afande naomba uchukue maelezo ya Amara hawa vijana wa aina hii wanatakiwa kufunzwa adabu ili siku nyingine waweze kuheshimu mabinti pamoja na wanawake wote .
" Sawa binti njoo utoe maelezo. Nilienda nikaeleza kila kitu na Yazid alikuwa amesomea pembeni na askari mwingine sikujua walikuwa wanaongea nini lakini waliporudi nikasikia yule askari anasema.
" Usijali hili jamaa litakaa ndani .
" Sawa, Amara tunawezakwenda.
Niliongozana na Yazid mpaka nyumbani nilimkuta baba akiwa nje tena alionekana kuwa na wasiwasi sana
" Amara binti yangu nini kimekupata?
" Hakuna baba nipo sawa. Baba alimuangalia kisha akamuangalia Yazid.
" Nimeambiwa kila kilichotokea huko .
" Ni kweli alipata shida kidogo lakini kila kitu kipo sawa.
" Na wewe ni nani?
" Anaitwa Yazid ni mgeni hapa nimefahamiana nae kwenye biashara zangu ni mteja wangu mkubwa na leo amekuwa mkombozi wangu .
" Asante sana kijana karibu ndani.
" Asante mzee wangu ila acha mimi niende muda imetupa mkono.
" Ungesubiri hata ule kidogo.
" Usijali nitakula wakati mwingine.
Yazid aliaga akaondoka.

Kesho yake majira ya saa nne asubuhi walikuja ndugu wa Azan.
" Amara kwahiyo kwaajili ya ujinga wako umeamua kwenda kumuweka ndani ndugu yetu?
" Kwahiyo mnanilaumu badala ya kutaka kujua sababu ni nini?
" Hakuna cha sababu hapa kwani nani hakujui kuwa wewe ni mgawanyo kwenye hiki kijiji.
" Acheni kumvunjia heshima binti yangu kijana wenu ndio mshenzi na kama mtaleta ujinga wenu tutaacha sheria usimame.
" Sawa tutaona na ukumbukwe sisi tunapesa sijui nyie mnanini cha kuhonga , leo hii Azan atatoka utamuona anatamba hapa mtaani .
Mara ikisikika sauti kutoka nyuma ikisema
" Ka
Na nyie mtamwaga shilingi basi mimi nitamwaga dola kuhakikisha kijana wenu anapotea . Wote zikigeuka kumuangalia Yazid ambae alikuwa kaongozana na Hizir.
" Na kama kurumbana rumbaneni na mimi maana mimi ndio niliwapeleka mtu wenu polisi.
" Kwa hiyo wewe ndio unaingilia yasiyokuhusu, kumbuka hapa sio mjini hapa ni kisiwa cha Manga watu tunakutana wenyewe.
Yazid alitaka kuongea kitu lakini akakatishwa na mlio wa simu yake. Alitoa simu mfukoni akaangaoia aliekuwa akampigia kisha akasogea pembeni kwenda kuongea. Ndugu wa Azan walizidi kuongea kwa kujiamini. Hizir aliwaangalia kisha akasema
" Laiti ningejua yeye ni nani mngenyamaza tu.
" Kwani yeye ni nani hatuwezi kunyamaza.
" Acha nitoe maelezo yake kwa ufupi, yeye ni Yazid bin Suleiman bin Kambona ni kijana wa wabarozi wa nchi yetu huko India licha ya hivyo anatoka kwenye familia yenye kujieleza sana pia nae anawadhifa serikali sasa mkitaka kushindana nae mtajikuta mnajua mpaka viwanja vya makaburi mlivyowazika nyanya zenu. Kila mtu alitulia kimnya maana hata mimi sikuwahi kufikiria kama Yazid anatoka kwenye familia maarufu inayojiweza.


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote