ALIYAH

book cover og

Utangulizi

NAKUPENDA DADA
Kuna mambo yanashangaza sana ukiyasikia kuwa kaka anampenda dada yake wa kuzaliwa...
Ipo hivi aliyah alipotea akiwa na miaka miwili na kuokotwa na mama mmoja na kuamua kulea ila akawa anamlea kwa mateso makubwa sana, na alipokuwa bint alikatazwa kutoka nje na akawa kama house girl wa hio nyumba kwa maana yeye ndio alikuwa anafanya kazi zote za hapo ndani...
Ingawa kulikuwa na bint wa rika lake aitwae nuru..
Nyumba aliokuwa anaishi aliyah ilikuwa na urafiki na familia nyingine ambayo kwa miaka zaidi ya kumi na tano ilikuwa inaishi nje..
Familia ile ilikuwa na vijana wawili abdul na luckman...
Familia hii yenye vijana inarudi nchin na kuamua kufikia kwa akina nuru na aliyah akiwa kama house girl...
Luckman alipofika akaja kukutana na aliyah kwenye garden na kujikuta anampenda sana aliyah, kutokana na uzuri wake, upole na ukarimu wake..
Baada ya ule ukaribishi kuisha luckman akawa anakuja kwa siri kuonana na aliyah ili amshawishi awe nae ..
Aliyah anamkubali na wakaanzaa mahusiano ila baadae inakuja kujulika kuwa familia ya aliyah ndio familia ya abdul na luckman na wakati wameshalala pamoja...
Luckman alikuwa anampenda sana aliyah kiasi kwamba anashindwa kukubaliana na ukweli, na aliyah anaamua kumkwepa kitu kilichokuwa kinamuumiza sana luckman na kumuharibia kwa kila mwanaume atakae jaribu kuwa karibu na aliyah...
Unadhan ni ipi hatma ya aliyah na luckman kwenye penzi lao...
Usikose mkasa huu wa kusisimua wa ALIYAH ( am not your brother i love you)

ALIYAH (am not your brother I love you) 1
HUSQER BALTAZAR
Katika jumba moja la kifahari sana anaonekana bint wa kama miaka kumi na nane akiwa anapika chakula, na kwa mavazi yake na namna alivyo ni dhahiri kuwa alikuwa ni dada wa kazi kwenye ile nyumba…

Alikuwa ni bint mrembo sana ila kwa kipindi chote hicho hakuwah hata kutoka nje ya hiyo nyumba na shughuli zake zote alikuwa anazifanyia hapo, na bint huyo anaitwa aliyah, ile familia ambayo alikuwa anafanya kazi za ndani walikuwa wanamchukia sana, kwa maana walikuwa wanamtumikisha kama mtumwa, ila cha kushangaza hawatakagi kumfukuza, na kuna siku walikuwa wanataka kumfukuza wakashangaa mambo yao hayaendi sawa hasa hasa ya kiuchumi….

Katika familia hio hio kuna bnt mwingine ambae yeye kitu pekee ambacho alikuwa anaweza kufanya ni kuagiza tu vitu na hakuwa anaweza kufanya jambo lolote lile hata kujifulia nguo zake au hata kujitandikia kitanda, na binti huyo alikuwa anaitwa Nuru…..

Aliyah hakuwa anajua kama yeye ni mwanafamilia hio, kuna muda alikuwa anahisi labda ni mtoto wa je, maana kuanzia anapata akili alikuwa anaishi pale, na hakuwah kujua taarifa za moja kwa moja za familia yake, na mara zote alikuwa anaamin ile ndio familia yake ingawa walikuwa wanamtesa sana, yaan kuna muda alikuwa hata anaweza kukesha anapika ila hata hicho chakula chenyewe asipate wasaa wa kukila…

Alishazoea hayo maisha hivyo hayakuwa maisha mageni sana kwake, alishazoea maisha ya kufanya mambo mema sana kwenye hio familia na kuambulia lawama badala ya shukurani, ameshazoea kuona watu wanafukuzwa kazi nay eye anabeba majukum yote, kuna muda anakuwa kama housegirl na mlinzi kwa wakati mmoja, alikuwa anafanya kazi kama mwanamke aliepata kazi omani, ila tofaut ni kwamba yeye hakuwa analipwa, kwa maana hakuwa analipwa chochote kile hata shukuran….

Alishayazoea hayo maisha na kuona ni maisha yake, japo kuwa yalikuwa yamateso sana…
Siku moja akiwa zake nyumban mama wa ile nyumba akamfata na kusema kuwa kutakuwa na ugeni siku hio, na ugeni wenyewe ni wa rafiki wa mwanae ambae ilikuwa inaishi London kwa karibu miaka kumi na tano, na familia hio ilikuwa ina watoto wakiume wawili, wa kwanza alikuwa anaitwa Abdul na mwingine alikuwa anaitwa lukman….

Hivyo aliiyah akawa anatakiwa kuandaa vyakula na vinywaji kwa sababu ya ukaribisho wa hio familia tena pekee yake bila msaada wa mtu, na wakawa wanasema hawawez wakaajiri watu wa kupika na wakati aliiyah alikuwa mpishi bora sana, ila wataajiri watu wa kutenga tu, ili aliyah asije akawatia aibu mbele ya wageni kwa maana hakuwah kuwa na ustaarabu hata kidogo….

Aliayah alishazoea hayo maisha hivyo hata hakuwa na umuhimu wa kupinga maagizo yoyote yale ambayo alikuwa anapewa…siku hio nzima aliiyah alishinda jikon akiandaa vyakula mbali mbali na vinjwaji mbali mbali kwaajili ya ugeni…

Alifanya kazi mno, na mpaka saa moja usiku alikuwa ameshamaliza kila kitu, na akapeewa taarifa kuwa ugeni utafika hapo muda sio mrefu, nay eye akawa hatakiwi kuonekana maeneo ya ukumbini, wakidai kuwa atawatia aibu, aliayah hata hakuwa anataka kubishana nao, akaenda zake kukaa bustanini…

Kweli ugeni ulikuja kwenye kama saa mbili kasoro, aliyah aliona magari yakiwa yanaingia, aliona pia watu waliokuwa wanashuka, walishuka vijana wawili ambao kwa muonekano tu walikuwa wanaonekana kama ni wanaume wenye muonekano mzuri sana na wakipekee mno, walikuwa wanaonekana kama wanapesa sana, aliayh aliwatazama kisha akaenda zake kuendelea na majukum yake ya kila siku, maana hakuwa anataka kuzua ugomvi baina yake na maboss wake…..

Basi akawa anaskia mapokezi yanaendelea, sasa kuna muda akawa amepigiwa simu na kuambiwa alete juice mlango wa nyuma na kuna mtu atapokea maana yeye hakuwa anaruhusiwa kuingia kwenye huo ukaribisho, sasa wakati ametoka zake jikon, maana kulikuwa na jiko la nje na jiko la ndani, na siku hio aliandaa kila kitu kwenye jiko la nje, akaichukua ile juice na kuanza kuipeleka, ila kabla hata hajafika akashangaa amempamia mtu, na ile juice ikamwagika na ikamwagikia kijana mmoja mtanashat mno, na lile jug likavunjika….

“ samahan sana kaka yangu sijakusudia kufanya hivi, akasema aliiayah kwa sauti ya kujitetea….
Ila akashangaa Yule mwanaume anakuwa kimya tu, akiwa anamuangalia huku anatabasamu tu, ikabidi aliayah aseme tena kwa sauti kuwa “ samahan kaka yangu sikukusudia….

Yule mwanaume ni kama hakuwa amezingatia sana kuhusu kumwagiwa juice ila uzuri wa aliiyah ni kama ulimshtua akajikuta anashindwa kusogeza macho yake pemben, akawa anajikuta anataman kuendelea kumtazama tu, akajikuta anamuuliza ‘ unaitwa nani akauliza Yule kijana akiwa anatabasamu….

“ naitwa aliyah, akajibu aliyah akiwa anaangalia chini kwa aibu…
Yule kijana akamuinua uso wake kwa kumshika kidevu kisha akawa anamuangalia kana kwamba alikuwa anamkagua kisha akasema ‘ unajua kuwa wewe ni mrembo sana aliyah, kuna mtu ameshawah kukuambia hilo? Akauliza Yule kijana….

Aliyah akatikisa kichwa kwa ishara ya kuwa hakuwah kuambiwa hivyo kabla, Yule kijana akasema “ mimi naitwa luckman, ila unaweza kuniita jina lolote zuri ambalo unalipenda, sasa ndio nakuambia kuwa wewe ni mzuri mno, yaan katika maisha yangu, sijawah kukutana na mwanamke mrembo kama wewe, akasema luckman na aliyah akawa anaangalia chini tu, mwisho akasema “ samahan sana kaka yangu, natakiwa kwenda kutengeneza juice nyingine maana muda sio mrefu mama atakuja na kunigombeza….

“kwani hio juice ni juice ya nini? Akauliza lucman…
“ ya maembe boss, akasema aliayah…

“ aaaa mimi sio boss wako mrembo bana, niite tu luckman, akajibu luckman kisha akachukua simu yake na kumpigia mtu akawa anamuambia kuwa alete juice ya embe, akawa anamuelekeza sehemu ilipo, na kumtaka aweke kwenye jag na sio kwenye maboksi….
Basi kweli baada ya dakika chache mleta juice akafika, na aliayah akaenda kuikabidhisha, akawa anataka kuondoka zake, akashangaa anashikwa mkono kisha luckman akamsogeza karibu yake na kumuambia “ una enda wapi mrembo, mbona kama unanikimbia sasa…

“ samahan sana kaka yangu, mama au mt yoyote Yule wa hii familia akija kuniona nimekaa na wewe maisha yangu yatakuwa magumu sana hapa, naomba uende zako ndani na mimi niendelee na shughuli zangu, akasema aliayah kwa saut ya wasiwasi…

“ unatkiwa kunifulia nguo zangu ambazo umezichafua, hivyo hauwez kunifukuza, akasema luckman na aliyah akawa mpole, akamtaka luckman avue hizo nguo wakazifue, na kweli akavua na kwenda kukaa kwenye chumba cha aliiyah akiwa na boksa na singlend tu, na aliyah akaenda kuzisafisha…

Ila kila ambapo luckman akiwa anamuangalia aliayh akawa anajikuta anazidi kumpenda, akawa anajikuta anataman sana kuwa nae siku zote za maisha yake, akawa anataman sana aliyah siku moja ndio awe mke wake, ni kweli wamekutana siku moja tu, ila mapenzi yake kwa aliyah yalikuwa makubwa sana na alijikuta anasisimka kwa namna ya kipekee sana akiwa karibu yake….

Luckman alikiwa anafurahia kumtazama aliyah mara simu yake ikaanza kuita na alikuwa anapiga kaka yake aki9muuliza yuko wapi…
“ nakuja, akasema luckman kisha akapiga simu mtu amletee nguo, maana hakukuwa na uwezekano zile nguo ambazo amezifua aliyah kukauka, kisha akavaa na kumfata aliayah kisha akamuambia “ naomba usikubali mwanaume yoyote Yule kukuambia wewe ni mrembo, hakikisha unakuwa mkali sana umesikia…

Aliyah kwa sura ya tabasamu akasema “ sawa kaka luckman, kiukweli luckman hakupenda kuitwa kaka ila ndio hivyo hana namna, akatabasamu kisha akaingia ndani huko ambapo ameitwa……
NAKUJA……………



ALIYAH (am not your brother I love you) 2
HUSQER BALTAZAR
“ oyaaa ulikuwa wapi? Akauliza abduli mara baada ya luckman kuingia ndani…
“ mungu ni wa ajabu sana unajua, kuna watu ni wazuri sana ila wanafichwa, aisee kuna bint kwenye hii nyumba ambae ni mzuri sana, yaan ni mzuri kuliko hata hilo neon uzuri nimemuona, akasema luckman…

“ kumbe kuna bint humu tofauti na nuru , sasa kwanini hakujumuika na sisi? Akauliza abdul…
‘ hawez kujumuika na sisi maana ni mfanyakazi tu hapa, akasema luckman, akashangaa abdul anaanza kucheka kish akasema “ usinambie kuwa umevutiwa na house girl, are you crazy bro….

‘ ukweli ni kwamba nimempenda na nampenda, yaan nampenda sana Yule binti, nimejikuta namuona kwa mara ya kwanza ila moyo wangu na hisia zangu zote zipo kwake, moyo wangu na mawazo yangu yapok wake, siwez kuficha hili bro, I really love aliyah, akasema luckman kwa sauti ya kujiamin kabisa yaan….

“ hauwez kumpenda mfanyakazi, nuru anakupenda na unalijua hilo siku zote, na hata sababu ya sisi kuja hapa ni kwa sababu ya upendo wake kwako, usinambie kuwa unataka kumpotezea nuru kwa sababu ya mfanyakazi wa ndani kweli, nahisi haupo sawa wewe, akasema abdul…

“ nuru hajawah kuwa mwanamke wangu, na siku zote huwa namchukulia kama rafiki tu, nay eye mwenyewe anajua kua sijawah kuwa na hisia za kimapenzi juu yake, sasa kama ndio nimependa ni kwamba siruhusiwi kwa sababu nimempenda mfanyakazi wa ndani, huu utakuwa ni upuuzi, na kama kumpenda aliayah ni upumbavu nimekubali kuwa kichaa, akasema luckman kwa sauti ya kujiamin sana…

Sijui hata alikuwa anajiamin nini na ndio kwanza amemuona aliuyah kwa mara ya kwanza, basi luckman akawa anataka aliyah aje ndani ili abduli amuone ajue kwamba hata yeye kumpenda aliyah basi hatakiwi kulaumiwa maana uzuri wa aliyah haupingiki kwa kila binaadamu mwenye macho na anaeweza kutazama vizuri…..

Basi ni kama abduli hakuwa anaamin kama huyo mwanamke ni mzuri kwa kiasi cha kumchanganya ndugu yake, akajikuta nay eye anataman sana kumuona…

Basi wakawa wanatafuta namna kwa aliyah kuingia ndani ila haikuwa rahisi, kwa maana hakukuwa na sababu ya aliyah kuingia ndani kabisa…
Ikabidi lukman amtake ndugu yake waende kwenye bustani kumuangalia huyo mrembo ambae amemchanganya lukman, kweli wakatoka na kwenda kwenye chumba kimoja ambacho kilikuwa njje ya lile jumba kubwa, ni dhahiri kwamba chumba hicho ndio alikuwa anakaa aliyah au mfanyakazi yoyote wa hio nyumba , wakamkuta aliyah yuko nje, anafuma kitambaa, vile vya kufuma kwa uzi, aliyah hakujua kama kuna watu ambao wamekuja kumshangaa akawa zake busy na ushonaji wake, maana ndio kitu pekee ambacho huwa anakifanya kujipoteza muda endapo akiwa amemaliza kazi zake za kila siku…

‘ umemuona namna alivyo mrembo lakin? Akauliza lukman …
“ ni kweli ni mrembo sana, ila laity kama angekuwa ametoka kwenye familia nzuri basi ningeamin huenda ndio Yule dada yetu aliyepotea maana amefanana na mama sana alipokuwa msichana, akasema abdul ….
Unadhan ni kwanini abduli alipomuona aliyah alisema anafanana na mama yake, au aliyah ndio mtoto aliepotea nini
NAKUJA….


ALIYAH (am not your brother I love you) 3
HUSQER BALTAZAR

“ sikuelewi unajua, yaan una maanisha aliyah amefanana na mama yetu alipokuwa msichana, huenda ndio Yule bint wa mama ambae kapotea, akasema luckman, ila alikuwa analaani maneno yake, kwa maana hakuwa anataka kabisa aliyah awe ndugu yake maana alihisi kungemkosesha haki ya kummiliki na wakati alikuwa tayar ameshampenda sana….

“ haiwez kuwa bana. Hata nuru angeshawah kukuambia kuwa wana binti ambae wamemuokota miaka yote hii, maana amekuwa rafiki yako kwa muda mefu sana, mimi naamin ni mfanyakazi wa kawaida tu, na mama ameshaacha kufuatilia kabisa kuhusu kumtafuta Nurath, akasema abdul…

Wakiwa pale mara simu ya lukman ikawa inapigwa na aliekuwa anapiga alikuwa ni nuru alikuwa anauliza wako wapi, ndio akajibu wapo bustanini ila wanakuja muda sio mrefu…

Basi wakangia ndani na abduli alikuwa anamshangaa sana ndugu yake kuangukia kwa mwanamke maskin ambae hana cheo chochote kile zaidi ya kuwa mfanyakazi wa ndani tu, hata kama alikuwa mzuri kiasi gani ila aliamin kuwa failia yake hakutakiwi kuingizwa damu ya kimaskin kabisa, hivyo abdul aliona kama sio sahihi kwa lukman kumuona mara moja tu aliyah na kumpenda….

“mlikuwa wapi? Akauliza tena nuru mara baada ya abduli na lukman kuingia ndani…
“ si rafiki yako nae ameshindwa kuushikilia moyo wake, akasema abduli kitu ambacho ni kama lukman hakukipenda hata kidogo na abduli alifanya makusudi tu kusema vile…

‘ una maanisha nini? Akauliza nuru…
“ yaan unafikiri ni sawa kwa mwanaume msomi, na tajiri na mwenye muonekano mzuri kama mdogo wangu lukman, kuacha wanawake wote wa marekani, kuacha wanawake wote wa London, hata wale wa hapa Tanzania ambao walikuwa wametoka kwenye familia nzuri na kuja kumpenda mfanyakazi wenu wa ndani kweli, akasema abdul makusudi mpaka lukman akajutraka mno kuchukua maamuzi ya kwenda kumuonesha abduli aliyah au kumpa taarifa zozote zile za aliyah…..

“ usinambie kuwa umempenda Yule house girl mchafu lukman, ila kweli wanaume hawajawah kujua wanataka nini, akasema nuru, ila alikuwa anasema hivyo kwa sauti ya wivu maana ni dhahiri alikuwa anamuonea wvu sana aliyah, maana yeye amekaa na lukman kwa zaidi ya miaka mitano ila hakuwah kumpenda ila anakuja kumuona aliyah kwa dakika chache nja kujikuta anampenda, akajiambia kuwa ni lazma amkomeshe so akaanza kujichekesha kisha akasema “ ngoja nikakuletee mwanamke wako ukae nae hapa, maana hata kama nikikushangaa tatizo sio wewe bali ni moyo wako, na maamuzi ta mtu ni lazima yaheshimiwe….

Nuru hakusema hivyo kwa mapenzi, ila alisema hivyo kwa chuki, akiwa na lengo la kumuabisha aliyah, maana anajua kuwa hajawah kunywa kilevi chochote na hanaga uzoefu wa kukaa na watu wengi…

Basi akaenda kumuita aliyah na kumuambia kuwa anaitwa ndani, akiwa na nguo zake kuu kuu, akaanza kuongozana na nuru bla kujua dhamira yake, ila alipoingia tu ndani, lukman alikuwa anamuona kama malkia ambae kavaa nguo za thaman sana, alikuwa anamuona mrembo zaidi maana walipokuwa nje hakukuwa na mwanga wa kueleweka kama pale ndani akajikuta anatabasamu, mara akasikia watu wengine ambao wapo pale wakisema kuwa “ ni nani huyu bint mrembo hivi, na minong’ono ya hapa na pale ikawa inaendelea, na nuru akamfikisha moja kwa moja kwenye meza ya vilevi lukman akamfata na kumnyang’anya kisha akasema “ usile wala kunywa kitu chochote kile ambacho amekupa mtu tofauti na mimi, tena aliongea hivyo mbele ya nuru, akimaanisha kuwa nuru sio mtu mzuri kwake, kisha akasogea nae pemben, ila sehemu ambayo walisogea, mama yake abdul na lukman akasema “ mwanangu … nimempata mwanangu, huku akiwa anamuangalia aliyah….

NAKUJA……..


ALIYAH (am not your brother I love you) 4
HUSQER BALTAZAR
Abdul na lukman wakaangaliana, lukman akaanza kupata mashaka, maana ameshaanza kumpenda sasa inakuwaje mama yake aseme kuwa aliyah ni mwanae…
“ mama umemaanisha nini? Akauliza abdul kwa sauti ya tahadhari…
“ nilipomuona huyu bint nikahisi kama nimemuona mwanangu, bnt yangu kipenzi nurath akasema Yule mama…

Haya maneno yakamsogeza mama yake na nuru karibu yao, kisha akamuambia nuru na aliyah waondoke kisha akaanza kuongea na Yule mama na kumuuliza, “ nilisikia umempoteza bint yako, nuru alishawah kunambia kuhusu hili, kwani kuna alama gani ambayo ilikuwa inakutambulisha, au ni kitambulisho pekee kwa bint yako, akasema mama yake nuru….
“ bint yangu ana alama ya kuunga ambayo ni kama birthmark tumboni, akasema mama yake abdul na lukman, bibie aisha, kauli hii ilimshtua sana mama yake na nuru, akamuambia bi aisha kuwa “ tunaweza kuna bint ambae nimemuona ana alama kama hio, ngoja nikakuletee umuangalie, akasema mama yake nuru kisha akamfata mwanae, hapo mwanae hana kitu chochote kile anachokielewa juu ya hilo…

“mama kuna nini mbona sikuelewi? Akauliza nur mara baada ya kufika chumban na mama yake…
“ najua lukman hakupendi, hio sio tatizo, maana hata kama hautakuwa mwanamke wake, unaweza kuwa ndugu wa lukman na abdul na hio itasaidia sana kwenye familia yetu, maana si unajua namna baba yako alivyo na madeni, ni lazima uolewe na mwanaume ambae anajiweza ili uweze kutusaidia, akasema mama yake nuru na wakati huo alikuwa anaongea kwa umakin mkubwa sana….

“ una maanisha nini mama?, akauliza nuru…
“ huyo bint yao ambae amepotea ni aiyah, unaweza ukawa ndio wewe maana ana hio alama ya kuzaliwa tumboni, na pia nilimuokota si nilishakuambia kuwa nilimuokota akiwa na miaka mitatu, akasema mama yake nuru…

“ ni kweli nuru alikuwa anampenda sana lukman, la wazo la mama yake kuwa mwanafamilia wa lukman na abdul likuwa wazo bora sana, maana aliamin kuwa anaweza kuwakimbiza wanawake wote ambao waikuwa karibu na lukman, nan hata ukweli ambapo utagundulika atahakikisha kuwa lukman ameshampenda, maana anamjua lukman ni mtu wa maamuzi, na atakapompenda hakuna mtu ambae ataweza kumpinga hata iweje……

Basi wakati huo huo wakamuita mchora tatuu, na kumuambia aliyah atulie na afungue tumbo lake, kweli akatulia na ile lama akachorwa nuru, na kwakuwa haikuwa alama kubwa sana hivyo haikuchukuwa muda mrefu sana kuwa tayar, kisha nuru na mama yake wakatoka kule chumban kisha wakamfata bi aisha na kusema kuwa wanataka kumuonesha jambo…

Kweli wakaingia nae kwenye chumba kimoja, ambapo mama yake nuru akaanza kusema kuwa “ nilimuokota nuru mwaka 2000 alikuwa ana miaka mitatu tu, nilimuokota kwenye bustan ambayo ilikuwa karibu na mgahawa mmoja hivi, nilienda kumpeleka mpaka polisi kureport kuhusu kumuokota ila hakukutokea ndugu yake wala mtu anaemfahamu hivyo nikaamua kumlea, akamsema mama yake nuru kwa sauti ya kujiamin kabisa…

Bi aisha akanyanyua shati la nuru kweli akaona ilea lama ya kuzaliwa, akashindwa kujizuia akamkumbatia, ila akashanga ile hisia ya mama na mtoto hakuipaa kabisa, maana siku zote tunajua kuwa mama ni mama tu,l hivyo lazima kutakuwa na muingiliano flanin hivi wa kihisia kati ya mama na mtoto na bi aisha hakuipata kabisa, akawa anajiaminisha labda ni kwa sababu ni miaka mingi imepita hivyo huenda ni mwanae…
Nakuja……

ALIYAH (am not your brother I love you) 5
HUSQER BALTAZAR

Basi kwa furaha na bashasha kuwa akawafata vjana wake kisha akawaambiwa kuwa “ nimempata dada yenu ambae nimempoteza nimelia kwa kipindi kirefu sana kwaajili ya huyu mtoto, na hatimae nimempata, nakushkuru sana kwa kunilelea mwanangu kwa upendo mkubwa, na hata kupoteza pesa zako kumsomesha shule za gharama sana, hakika wewe ni mwanamke wa mfano kabisa kwenye jamii yetu, akasema bi aisha maneno ya kumpongeza mama yake nuru bila kujua ukweli unaendaje, na Yule mama alivyo mnafki akawa anajichekesha chekesha kisha akasema “ sinaga rpho ya kumchukia mtu bila sababu, moyo wangu ni msafi sana wewe mwenyewe umeona….

Basi shangwe ikawa mara mbili, na abdul alifurah sana ila moyo wa lukman ulikataa kabisa, maana anamjua nuru ni mtu wa drama na huenda kuna kitu kimefichwa hapo, hivyo hakufurahia kabisa zile taarifa……

Basi bi asiha hakutaka kabisa kupoteza muda akataka nuru aondoke siku hio hio na waende nae kwao, kitu ambacho kilikuwa furaha kwa nuru na mama yake ila baba yake hakuwa anaelewa kabisa mambo ambayo yanaendelea….

Kaba ya nuru na ile familia yake ya mchongo kuondoka, lukman akamfata aliyah kisha akamuuliza “ una simu?...
“ hapana kaka sina, akajibu aliyah kwa sauti ya unyenyekevu mkubwa sana…
Lukman akatoa simu yake na kumpa, ila aliyah akakataa na kusema mama yake akiona atamnyang’anya…
“ najua wewe ni mtu mzika bana, embu tafuta namna ya kuificha umesikia, akasema lukman kisha akasema “ muda gani ambao una maliza kufanya kazi zako?....

“ yaan mpaka saa tatu usiku, akajibu aliyah…
Lukman akamshika mikono yake kisha akambusu na kusema “ uwe makin na uniamin nitahakikisha nakutoa kwenye haya mateso mrembo, kisha akamkonyeza na kuondoka zake…

Kuanzia amekuwa aliyah hakuwah kusikia mtu akimuita mrembo, hakuwah kubusiwa wala kushikwa na mwanaume yoyote Yule, na vile ambavyo lukman amemkonyenza kukamfanya aliyah awe anacheka pekee yake kila anapomkumbuka lukman….

Basi nuru bla aibu akaenda kwenye familia ambayo sio yake, na akaambiwa akifkisha miaka 25 atapewa asilimia hamsini ya mali zote, kwa maana amekaa muda mrefu bila mapenzi ya familia yake, na hawana cha kumlipa zaidi ya hicho, nuru hapo muda wote meno yalikuwa nje kama kaona bia za offer…

La kuanzia nuru ameingia kwenye ile nyumba, ni abdul pekee ambae alikuwa anampenda na kumchukulia kama ndugu, ila mama yao pamoja na lukman hawakuwa wanahisi bondi yoyote ile, ila mama akawa anajilazimisha na kujiambia anajihisi hivyo anavyojihisi kwa sababu muda umepita mrefu sana huenda atakuja kupata ule muungano wa kiroho na kihisia muda ukienda, na akamzoea vizur ila lukman akaanza kuhisi kama kuna kitu ambacho hakiko sawa…..

Lukman hakutaka kuingilia hayo mambo, yeye kichwani kwake alikuwa aliyah tu, hivyo akaenda zake chumban kwake kisha akajifungia, alikuwa na simu nyingine akaichukua na kuweka line kisha akampigia aliyah….
Kweli simu iliita kwa sekunde kadhaa na sauti nyororo ya aliyah ikapokea simu,na alikuwa anaonekana kama alikuwa amelala hivyo sautin yake ikazid kuwa tamu zaidi yaan, mpaka lukman akajikuta anapata msisimko wa le utamu wa hio sauti, na kushusha pumzi kisha akajikuta anasema “ nenda taratibu mamaa utaniua….
NAKUJA…..


Soma Kitabu

SOMA MAELEKEZO

Bonyeza hi "Soma Kitabu" kisha itakupeleka kwenye fomu yaku login, hakikisha ume login na namba uliyojiunga nayo ndipo utaendelea sasa kusoma kitabu chote